Pope Francis reveals top 10 secrets to happiness

Slowing down, being generous and fighting for peace are part of Pope Francis' secret recipe for happiness.

In an interview published in part in the Argentine weekly "Viva" July 27, the pope listed his Top 10 tips for bringing greater joy to one's life:

1. "Live and let live." 

Everyone should be guided by this principle, he said, which has a similar expression in Rome with the saying, "Move forward and let others do the same."

2. "Be giving of yourself to others." 

People need to be open and generous toward others, he said, because "if you withdraw into yourself, you run the risk of becoming egocentric. And stagnant water becomes putrid."

Ngoma Africa Band seeks sponsors and promoters worldwide


The German based Ngoma Africa Band would like to go on a “World Tour” to spread its brand of African band music. 

The band is seeking sponsors and promoters worldwide for flight tickets, transportation and accommodation to fulfill its World Tour dream.

Please keep in touch: [email protected]
Listen to our music at http://www.ngoma-africa.com

Mahakama yazuia uongozi wa muda NICOL

Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam imeweka zuio la muda kwa uongozi wa muda wa Kampuni ya Uwekezaji ya Taifa (NICOL) kwa kuitaka kutojihusisha na biashara au shughuli yoyote ya kampuni hiyo hadi kesi ya msingi itakapokwisha.

Kesi ya msingi namba 91 ya mwaka 2014, iliyofunguliwa na wanahisa waanzilishi dhidi ya uongozi wa muda wa Kampuni ya NICOL).

Uamuzi huo ulitolewa na Jaji wa Mahakama hiyo, John Utamwa, Julai 10, mwaka huu, baada ya kusikiliza maombi yenye namba 297 ya mwaka 2014 yaliyofunguliwa na waombaji; Philemon Mgaya, Thabita Siwale, Ibrahim Kaduma, Balozi Anthony Nyaki na Sylvester Barongo.

Uongozi wa muda wa NICOL) uliopo madarakani, ambao katika maombi hayo ni wajibu maombi, ni

Niko tayari kugombea Jimbo la Mrema mwaka 2015 - Mbatia

Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia, ametangaza rasmi nia yake ya kuwania ubunge katika Jimbo la Vunjo, lililopo Wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro.

Mbatia, ambaye pia kwa sasa ni Mbunge wa Kuteuliwa na Rais, alitangaza azma hiyo, jana ikiwa ni siku moja baada ya wafuasi wa vyama vya CCM, Chadema, NCCR-Mageuzi na TLP kumwita jimboni humo, wakimtaka achukue maamuzi magumu ya kurejea nyumbani kugombea ubunge.
“Ni kweli kabisa kuna wananchi wameniandikia barua, wengine walikuja Dodoma wakati wa Bunge la Bajeti na wengine wamenifuata Dar es Salaam hivi karibuni kuniomba nikubali kugombea ubunge. Kimsingi, nimewaelewa. Na siyo dhambi nikitamka kwamba, niko tayari kugombea Vunjo mwaka 2015,” 
alisema Mbatia.

Alisema kwa nafasi aliyonayo hivi sasa kama mbunge wa kuteuliwa na Rais kwa mujibu wa katiba na

Wanafunzi 10 wa Uuguzi Tanzania kupelekwa kujifua Marekani

CHAMA cha Wauguzi Tanzania (TANA), kimesaini mkataba wa makubaliano na Shirika la Colom Foundation Inc kuendesha mafunzo ya uuguzi yatakayofanyika nchini Marekani.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Rais wa chama hicho, Paulo Magesa, alisema wauguzi wanahitaji kutoa huduma kwa ufanisi na kwa wakati, hivyo kwa kulitambua hilo, chama chake kimejitahidi kutafuta fursa ya mafunzo ambayo yatawasaidia kujifunza zaidi namna ya utoaji huduma.

Magesa, alisema wamepata nafasi ya kupeleka wauguzi kumi, ambao watachaguliwa Oktoba na watakwenda mwakani katika Chuo cha Dixie State nchini Marekani.

Mkuu wa Colom Foundation Inc, Wilbur Colom, alisema hiyo ni fursa muhimu kwa wauguzi wa Tanzania kwenda kujifunza mambo mengi zaidi yanayohusu taaluma yao na anaamini mafunzo hayo yataweza kutatua kero mbalimbali zilizopo.

via Tanzania Daima

Shirika la Colom Faundation Inc (CFI) la Marekani limetoa ufadhili wa mafunzo ya muda mfupi kwa wauguzi 20 nchini, watakaokwenda nchini humo kujifunza zaidi masuala ya afya ya uzazi na mtoto kwa lengo la kuboresha huduma hiyo nchini.

Hayo yalibainishwa jana jijini Dar es Salaam na Rais wa Chama cha Taifa cha Wauguzi nchini (TANNA), Paulo Magesa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Magesa alisema makubaliano hayo, yamefanywa baina yao na CFI. Alisema katika mpango huo wa mafunzo, awamu ya kwanza wauguzi 10, kati ya 20 watakwenda nchini Marekani majira ya joto katika Chuo Kikuu cha Dixie kwa ajili ya mafunzo ya wiki nane.

Alifafanua jinsi ya kuwapata wauguzi hao, kwamba watatangaza nafasi hizo za mafunzo kwenye vyombo vya habari ili kutoa fursa kwa wauguzi nchini, kuomba na kwamba wenye sifa watafanyiwa usaili na watakaoshinda ndio watakaokwenda.

Magesa alisema gharama zote za mafunzo hayo, zitagharamiwa na shirika hilo na kwamba kwa wale watakaopata nafasi za mafunzo, watakaporudi watatakiwa kutoa mafunzo kwa wengine ambao hawakupata fursa hiyo.

Alisema lengo la mafunzo hayo ni kuboresha huduma za afya nchini, hasa kwa afya ya mama na mtoto.

Alisema kwamba fursa hiyo, itakuwa endelevu ili kutoa nafasi zaidi kwa wengine kushiriki na kurudi kusaidia huduma za afya ya uzazi kwa wananchi.

Kwa upande wake, Mkuu wa CFI ambaye pia ni mwekezaji nchini wa Hoteli za Nashera, Wilbur Colom alisema wameingia kwenye mkataba huo, ikiwa ni sehemu ya kusaidia jamii ya Tanzania kutokana na wao kuwekeza hapa nchini.

“Tumeamua kuwa na makubaliano ya ushirikiano na TANNA, tumewekeza nchini, na tuna wajibu wa kusaidia jamii tuliyomo, ili tuendeleza undugu na kusaidiana ili afya ya mama na mtoto iboreke,” alisema Colom.

TANNA ilianzishwa nchini mwaka 1979, ikiwa ni chama cha wauguzi wenye taaluma ambao wamesajiliwa katika baraza ya wauguzi na ina matawi 29 nchini, yenye zaidi ya wanachama 3,500 ambao wanafanya kazi kwenye taasisi mbalimbali nchini.

via HabariLeo

Baraza la Vyama vya Siasa laamua mazungumzo ya pande zinazokizana Bunge la Katiba yaendelee kupitia kamati zitakazoundwa

Na Magreth Kinabo - MAELEZO

Baraza la Vyama vya Siasa nchini limeamua mazungumzo ya maridhiano kati ya pande zinazokizana kuhusu kuendelea kwa Bunge Maalum la Katiba kutokana na mvutano wa kutaka serikali mbili au tatu yaendelee kupitia kamati zitakazoundwa.

Aidha baraza hilo,limeamua kufanyike kongamano Agosti 9 na 10 mwaka huu mjini Dodoma kwa ajili ya kuangalia maslahi mapana ya taifa.

Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa baraza hilo, Peter Kuga Mziray, wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa kikao kati ya baraza hilo, na baadhi ya viongozi

Tanzania yalabuliwa 4 kwa nunge na Amajimbos

TIMU ya Taifa ya Tanzania ya vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys imebugizwa mabao 4-0 dhidi ya timu ya Taifa ya vijana wa umri huo ya Afrika kusini maarufu kama Amajimbos katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za vijana za mataifa ya Afrika.

Mechi hiyo rahisi kwa Afrika kusini imepigwa jioni ya leo katika uwanja wa Dobsonville uliopo Soweto na kushuhudia wenyeji wakitoka na furaha.

Taarifa kutoka nchini Afrika kusini zineeleza kuwa vijana wa Serengeti walizidiwa kila idara na wangepigwa hata mabao 7 kwasababu Amajimbos walikosa nafasi nyingi za wazi.

Serengeti ambao hawakuandaliwa tangu siku nyingi, wiki mbili zilizopita walitoka suluhu ya

Saa 10 zamajadiliano kati ya UKAWA na CCM

Licha ya agizo la Rais Jakaya Kikwete la kuwataka viongozi wa vyama vya siasa na wafuasi wao, wanaounda kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), kuacha kususa na kurejea katika vikao vya Bunge Maalumu la Katiba ili kuendelea na mchakato huo, kufikia jana hakukuwa na mwelekeo wa kulegeza msimamo wao.

Hali hiyo inajitokeza, licha ya jana kuwapo kwa kikao kirefu cha maridhiano baina ya pande zinazovutana, UKAWA na wale wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika mchakato huo, unaotarajiwa kuendelea tena kwa siku 60 kuanzia Jumanne ijayo mjini Dodoma.

Katika nasaha zake kwa UKAWA juzi, wakati akihutubia taifa kupitia utaratibu aliojiwekea wa kuzungumza na wananchi kila mwisho wa mwezi, Rais Kikwete aliahidi kuwa tayari kusaidia kwa

Taarifa ya Serikali ya Tanzania kuhusu Watanzania wanaosoma Ukraine

Mkutano ukiendelea (Picha na Reginald Philip)

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

SERIKALI HAIJAWATELEKEZA WATANZANIA WANAOSOMA UKRAINE


Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa inapenda kukanusha vikali taarifa iliyotangazwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), tarehe 30 Julai, 2014, iliyodaikuwa Serikali ya Tanzania imetelekeza wananchi wake wanaosoma Ukraine Mashariki, ambako kunarindima vita ya wenyewe kwa wenyewe.

Taarifa hiyo ya upande mmoja, iliyomnukuu mtu anayeitwa Shamila, aliyedai ni mmoja wa wanafunzi Watanzania nchini Ukraine, ilisema eti wananchi hao wameachwa bila msaada wowote.

Wizara imesikitishwa na taarifa hiyo iliyotolewa bila kufanyiwa uchunguzi wa kutosha. Ukweli ni kwamba Ubalozi wa Tanzania nchini Urusi, ambao unatuwakilisha pia Ukraine, umechukua hatua za

Maelezo ya Serikali kuhusu habari ya “Ex-soldiers want $3m for covert Congo operation”


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA


IDARA YA HABARI (MAELEZO)
S.L.P.9142, Dar es Salaam, Simu:2110585, 2122771/3, Fax: 2113814, e-mail: [email protected]

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Gazeti la Kiingereza la The East African, Toleo Na. 1030 lililochapishwa mwishoni mwa wiki, Jumamosi, Julai 26, 2014, limeandika habari yenye kichwa cha habari “Ex-soldiers want $3m for covert Congo operation”, ikiwa na maana kuwa wanajeshi wastaafu wanadai kulipwa dola za Marekani milioni tatu kwa kushiriki operesheni ya siri katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Inadaiwa katika habari hiyo kwa zaidi ya wanajeshi 400 wastaafu wa Tanzania, wametishia kuishitaki mahakamani Serikali ya Tanzania, wakidai posho ya zaidi ya dola za Marekani milioni tatu (sawa na karibu sh. Bilioni sita) kwa kushiriki operesheni ya kivita ya siri katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kati ya 2000 na 2003.

Inadaiwa na gazeti hilo kuwa askari hao wastaafu walipelekwa Congo ili kutoa mafunzo kwa Jeshi la

Taarifa ya tahadhari kutoa Wizarani kuhusu ugonjwa wa Ebola

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA UGONJWA WA EBOLA


Mnamo mwezi wa Machi 2014 Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ilipokea taarifa kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) kuhusu ugonjwa wa Ebola katika nchi za Afrika Magharibi ambao ulianzia katika ya Guinea na kusambaa katika nchi za Siera Leone, Liberia na Nigeria. Hadi tarehe 31 Julai, 2014 idadi ya wagonjwa ilikuwa 1323 na vifo 729.

Ugonjwa wa Ebola husababishwa na virusi vya Ebola. Dalili zake ni homa kali ya ghafla, kulegea mwili, maumivu ya misuli, kuuma kichwa, na vidonda kooni. Mara nyingi dalili hizo hufuatiwa na kutapika, kuharisha, vipele vya ngozi, figo na ini kushindwa kufanya kazi na kwa baadhi ya wagonjwa kutokwa damu ndani na nje mwilini. Kipindi cha kuonekana kwa dalili za ugonjwa ni kati ya siku 2 hadi 21 baada ya kupata maambukizi.

Ugonjwa wa Ebola unaambukiza kwa kasi na unaenea kati ya mtu na mtu kwa:-

Polisi Zanzibar yamshikilia Mansour Himid kwa kumiliki silahaJeshi la Polisi visiwani Zanzibar linamshikilia aliekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Kiembe Samaki kupitia tiketi ya CCM Bwana Mansour Yussuf Himid.

Akieleza sababu za kukamatwa kwake Naibu mkurugenzi wa makosa ya jinai Zanzibar wakati akizungumza na Mazrui media, Bwana Salum Msangi amesema wamemshikilia Mansour baada ya kupata taarifa za raia wema kuwa anamiliki silaha.

Alieleza kuwa mara baada ya kupata taarifa hio jeshi hilo liliamua kufanya msako maalumu nyumbani kwa aliekuwa Mheshimiwa huyo mnamo majira ya 2:30 asubuhi huko Chukwani nje kidogo ya mji wa

Taarifa ya mabadiliko ya muda wa saa za kazi katika ofisi za NHIF

MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA (NHIF)

TAARIFA KWA UMMA


MABADILIKO YA MUDA WA SAA ZA KAZI KATIKA OFISI ZA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA


Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) unapenda kuwatangazia wadau wake na wananchi wote kwa ujumla kuwa umebadili muda wa saa za kazi kwa ofisi zake kote nchini. Mabadiliko haya yanatokana na ukweli kwamba wadau wa Mfuko wanawahi sana kufika ofisi za Mfuko kupata huduma. (Uzoefu wa Mfuko unaonyesha wadau hufika kabla ya saa 2 asubuhi kupata huduma).

Hivyo, kuanzia tarehe 1 Agosti 2014 ofisi za NHIF zitakuwa wazi kuanzia saa moja na nusu (1.30) asubuhi hadi saa kumi kamili (10:00) jioni kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa.

Huduma zote zinazotolewa na Mfuko zitaendela kutolewa kama kawaida muda huo na wote mnakaribishwa kuendelea kupata huduma za Mfuko kama kawaida.

NHIF: "Huduma bora za matiabau ni haki yako na ni dhamana yetu"

Kwa maelezo zaidi wasiliana na:

Kaimu Mkurugenzi Mkuu,

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya,

S.L.P.11360, Dar es Salaam; Simu: 022 2133969/964;

Barua pepe: [email protected]; Tovuti: www.nhif.or.tz

Injili kutikisa Taifa katika Tamasha la Matumaini 2014; Azam FC, Mtibwa Sugara lazima kieleleweke 08.08.2014


UPAKO! Zikiwa zimesalia siku chache kuelekea katika Tamasha la Matumaini litakalofanyika katika Uwanja wa Taifa, Agosti 8, mwaka huu, pamoja na burudani mbalimbali, waimbaji wa muziki wa Injili watakuwepo kulipamba tamasha hilo.

Akizungumza na Mikito Nusunusu, mratibu wa tamasha hilo, Luqman Maloto alisema kila kitu kimekwenda kwenye mstari na kinachosubiriwa ni muda ufike, Watanzania wajumuike kwa pamoja uwanjani kushuhudia burudani zisizo na mfano.

Kwenye muziki wa Injili, Maloto alisema mkongwe wa nyimbo za Injili, Upendo Nkone ataliongoza