Huduma za NMB katika maonesho ya Nane Nane nchi nzima

Meneja wa huduma wa Benki ya NMB tawi la Mwanjelwa Jijini Mbeya, Happnes Pima (kulia) akimwelekeza jambo Mkuu wa Wilaya ya wangi'ombe Mkoa wa Njombe, Estelina Kilasi (kushoto) wakati alipotembelea banda ya benki hiyo kwenye maonyesho ya wakulima ya nanenane yanayoendelea  kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya, ambapo kwa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini yanafanyikia Mkoa wa Mbeya.
Meneja wa huduma wa Benki ya NMB tawi la Mwanjelwa Jijini Mbeya, Happnes Pima (kulia) akimwelekeza jambo Mkuu wa Wilaya ya wangi'ombe Mkoa wa Njombe, Estelina Kilasi (kushoto) wakati alipotembelea banda ya benki hiyo kwenye maonyesho ya wakulima ya nanenane yanayoendelea kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya, ambapo kwa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini yanafanyikia Mkoa wa Mbeya.

NMB inashiriki maonyesho ya wakulima ya nane nane katika mikoa saba huku huduma zote za kibenki zikiwa zinafanya kazi katika mabanda yake kama kuweka na kutoa fedha, kupata taarifa za mikopo hasa ya kilimo.

NMB inashiriki maonesho ya Nane Nane katika mikoa ifuatayo; Lindi ambako yanafanyika kitaifa, Morogoro, Dodoma, Tabora, Mbeya, Arusha na Kagera.

Wakulima pia wanaotembelea mabanda ya NMB kote nchini watapata fursa ya kukutana na wataalam wa kilimo na pembejeo, vyama vya ushirika na hivyo kuwa na fursa nzuri za wao kupata taarifa sahihi na ushauri wa jinsi ya kutumia benki kunufaisha shughuli zao za kilimo.

Kwa kuwa moja ya malengo ya NMB ni kuhakikisha inasaidia ukuaji wa kilimo na kukifanya kuwa cha kibiashara, yenye malengo la kumkwamua mkulima. Hii ni fursa nzuri kwa wakulima, wafanyakazi wa serikali na wajasiriamali kuweza kufika kwenye mabanda ya NMB ili kujionea huduma ambazo benki inatoa.

Kilimo ni uti wa mgongo kutokana na ukweli kwamba karibia 80% ya watanzania wanajishughulisha na kilimo. Kwa kutambua hilo, NMB ipo karibu yao zaidi katika kipindi hiki cha Nane Nane kwa kuleta huduma za kuwanufaisha.

Kauli mbiu ya ‘Kilimo na Mifungo ni biashara’ kwa mwaka huuimeifanya NMB kushirikiana na serikali katika kufanikisha maonyesho ya nane nane katika mikoa yote saba.

Benki ya NMB inatoa huduma mbali mbali za kilimo ikiwa ni pamoja na akaunti maalumu ya Kilimo yaani ‘Kilimo Account’ ambayo inamruhusu mkulima kuweza kujipatia mikopo mbali mbali ili kuweza kuinua uchumi wa Nchi.

Meneja wa huduma wa Benki ya NMB tawi la Mwanjelwa Jijini Mbeya, Happnes Pima (katikati) akimwelekeza jambo Mkuu wa Wilaya ya wangi'ombe Mkoa wa Njombe, Estelina Kilasi (kushoto) wakati alipotembelea banda ya benki hiyo kwenye maonyesho ya wakulima ya nanenane yanayoendelea kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya, ambapo kwa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini yanafanyikia Mkoa wa MbeyaWafanyakazi wa Benki ya NMB wakiwajibika katika banda lao kwenye maonesho ya wakulima maarufu kama Nane nane ambayo kwa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini yanafanyikia Mkoa wa Mbeya, katika Viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya.

Askari wakiwa wameimarisha ulinzi kwenye banda ya benki ya NMB katika maonyesho ya wakulima ya nanenane yanayoendelea kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya, ambapo kwa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini yanafanyikia Mkoa wa Mbeya.

Kauli ya CCM kuhusu yatokanayo na mdahalo wa Katiba Mpya ulioandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Katika Mdahalo ulioandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere, uliofanyika tarehe 04/08/2014 mjini Dar es salaam, aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mzee Joseph Sinde Warioba na baadhi ya wajumbe wenzake pamoja na mambo mengine, walikitupia lawama nyingi Chama Cha Mapinduzi na Mwenyekiti wake Rais Jakaya Kikwete kwa hisia nyepesi, dhaifu na za kutunga. Mara kadhaa na hata katika mdahalo uliopita, baadhi ya waliokuwa wajumbe wa Tume ya Warioba wamekuwa wakitumia muda mwingi kujaribu kupotosha umma na kuwashambulia wote wenye mitazamo tofauti na ya kwao. Inaelekea baadhi ya wajumbe wa Tume ya Warioba wameufanya mchakato wa Katiba kuwa mali yao na kufanya kila juhudi za kujitengenezea hati miliki ya Katiba. Katika mazungumzo yake Mzee Warioba na wenzake wamekuwa wakitumia takwimu kutetea hoja ya serikali tatu.

Lakini hivi sasa wanahama na kusisitiza kuwa ni busara zao ndizo zilizopelekea kupendekeza muundo wa serikali tatu. Kimetokea nini? La kusikitisha zaidi ni kuwa; wamekuwa na msimamo mkali usiokubali kusikiliza na kutoa nafasi kwa mawazo yoyote yanayotofautiana na ya kwao. Badala yake

Taarifa ya Ofisi ya Katibu: Bunge la Katiba lipewe nafasi kufanya kazi yake

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

BUNGE MAALUM

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

BUNGE MAALUM LA KATIBA LIPEWE NAFASI YA KUFANYA KAZI ZAKE


Ofisi ya Bunge Maalum, imeshangazwa na kusikitishwa na baadhi ya vyombo vya habari na makundi ya jamii yanayoeneza upotoshwaji mkubwa ambao umedakwa katika mitandao ya kijamii kuhusu kauli aliyoitoa Mwenyekiti wa Bunge Maalum Mhe. Samuel Sitta (Mb) wakati wa mjadala wa kupitisha Kanuni tarehe 5 Agosti, 2014 kuhusu midahalo ya Katiba inayoendelea katika baadhi ya televisheni hapa Nchini.

Mwenyekiti wa Bunge Maalum, Mhe. Sitta hapo tarehe 5 Agosti 2014 alitahadharisha kuhusu baadhi ya midahalo hiyo inayoendeshwa ikiwa na mapungufu makubwa. Wanapangwa washiriki wenye mawazo na malengo ya upande mmoja na kutumia fursa hiyo kushambulia kwa lugha chafu makundi yenye mawazo tofauti ambayo kimsingi yalitakiwa yashirikishwe kwenye midahalo hiyo. Tumeshuhudia upotoshwaji mkubwa kuhusu kauli ya Mwenyekiti. Hali hii inadhihirisha jinsi maadili

Ratiba ya Mkutano wa Bunge la Katiba: Agosti - Oktoba, 2014

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

BUNGE MAALUM

RATIBA YA MKUTANO WA BUNGE MAALUM KUANZIA TAREHE 05 AGOSTI, 2014 HADI 31 OKTOBA, 2014


IMEANDALIWA NA: 

OFISI YA KATIBU WA BUNGE MAALUM 

AGOSTI, 2014
__________________


TAREHE
SHUGHULI
MUDA
05 Agosti, 2014
Kujadili na kupitisha marekebisho ya Kanuni za Bunge Maalum
Siku 1
06 - 27 Agosti, 2014
Kamati kujadili Sura zote za Rasimu ya Katiba
Siku 15
28 Agosti - 01 Septemba, 2014
Kamati kuandaa taarifa za Sura zote za Rasimu ya Katiba
Siku 3
02 – 08 Septemba,2014
Kamati zote kuwasilisha taarifa zake ndani ya Bunge Maalum
Siku 5
09 - 29 Septemba, 2014
Majadiliano ya taarifa za Kamati ndani ya Bunge Maalum
Siku 15
30 Septemba - 06 Oktoba, 2014
Kamati ya Uandishi kuandika upya ibara za Sura zote za Rasimu ya Katiba
Siku 5
09 Oktoba, 2014
Kamati ya Uandishi kuwasilisha taarifa yake katika Bunge Maalum
Siku 1
10 – 21 Oktoba, 2014
Kupitisha ibara za Rasimu ya Katiba kwa kupiga Kura
Siku 7
22 - 28 Oktoba, 2014
Kujadili na kupitisha masharti ya mpito
Siku 5
10.
29 - 30 Oktoba, 2014
Katibu kukamilisha Katiba inayopendekezwa kwa ajili ya kuwasilisha kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano na Rais wa Zanzibar
Siku 2
11.
31 Oktoba, 2014
Mwenyekiti wa Bunge Maalum kuwasilisha Katiba inayopendekezwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano na Rais wa Zanzibar
Siku 1

NB: Siku za JUMAMOSI, JUMAPILI na SIKU KUU ni mapumziko hivyo hazijajumuishwa katika Ratiba hii.

Kauli ya CHADEMA kuhusu taarifa za Wabunge wake 'kuonekana Dodoma'

Kumekuwepo na madai yanayosambazwa kupitia njia mbalimbali za upashanaji habari kuhusu baadhi ya wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuonekana mjini Dodoma au kujisajili kwa ajili ya kuhudhuria vikao vya Bunge Maalum la Katiba vinavyoendelea mjini humo.
Chama kupitia Idara ya Habari kingependa kutoa ufafanuzi kama ifuatavyo;

1. Uamuzi wa kuwataka wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wanaotokana na CHADEMA kushirikiana na wenzao wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), kutoshiriki vikao vya bunge hilo ili kuepuka kunajisi mchakato wa Katiba Mpya, ulitokana na maazimio ya kikao cha Kamati Kuu iliyoketi Julai 18-19 na kuazimia kwamba;
  • Wajumbe wa Bunge Maalum wanaotokana na CHADEMA, kama sehemu ya UKAWA, watarudi kwenye vikao vya Bunge Maalum endapo tu mamlaka ya Bunge hilo yatafafanuliwa kuwa ni ya kuboresha, na sio kuibomoa au kuifuta, misingi mikuu (basic features) ya Rasimu ya

Tunakwamishwa na uzalishaji na matumizi madogo mno ya umeme - Kikwete

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898

Fax: 255-22-2113425


PRESIDENT’S OFFICE,
STATE HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa moja ya sababu kubwa zinazokwamisha maendeleo makubwa zaidi na ya haraka zaidi ya Afrika ni uzalishaji mdogo na matumizi ya chini mno ya umeme.

Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa hali hiyo inaeleza jinsi ongezeko la uzalishaji na matumizi ya umeme linavyoweza kuharakisha maendeleo ya Afrika na kuleta manufaa ya dhahiri kwa kila familia na kwa kila Mwafrika.

Rais Kikwete ameyasema hayo jana, Jumatano, Agosti 6, 2014, wakati alipozungumza kwenye

Mahojiano na mtaalamu wa uchumaji asumin: Bustani ya mapenzi yenye mauwa madogo yenye harufu nzuri, huwekwa kitandani ili bwana asitoke...

Mtaalamu wa uchumaji asumin Alwatan Kijakazi Hassan Mustafa akiwa katika harakati za uchumaji wa mauwa ya yenye harufu nzuri asumin
Blog ya Swahilivilla siku ya Jumamosi, Julai 19 2014 ilifafanya mahojiano na mtaalamu wa uchumaji wa mauwa ya asumin, Alwatan Kijakazi Hassan Mustafa, a.k.a (Kijakazi) ambaye alielezeaa mengi kuhusu umuhimu wa asumin pamoja na utunzani wake.

Katika mahojiano haya na mtaalamu wa utunzaji wa miasumini, Kijakazi Hassan Mustafa, mkaazi wa Mwembetanga Zanzibar anatuelezea mambo mbalimbali kuhusu umuhimu wa mauwa ya asumin yakiwemo kusingwa kwenye sherehe za harusi na hata kutengezea uturi pamoja na vikuba vyenye

Tamasha la Matumaini 2014 kesho, Taifa


Ally Kiba.

SIKU iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa burudani mbalimbali imewadia ambapo kesho Agosti 8, katika Uwanja wa Taifa patakuwa hapatoshi wakati Tamasha la Usiku wa Matumaini litakapokuwa likichukua nafasi.

Akizungumza na Centre Spread, mratibu wa tamasha hilo, Luqman Maloto alisema kuwa maandalizi yote yameshafanyika na tayari mkali wa muziki kutoka Nigeria anayetamba na ngoma ya Johnny, Yemi Alade ameshatua nchini, kinachosubiriwa ni burudani mwanzo mwisho.

“Kila kona ya burudani imeshakamilika hivyo kama wewe ni mpenzi wa ndondi kuna ngumi kati ya

Rais KIkwete, Rais Mutharika, Waziri Membe wateta jijini Washington DC, Marekani

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Malawi Profesa Peter Mutharika wakimsikiliza Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe kwenye hoteli ya Ritz Carlton katika kitongoji cha George Town jijini Washington DC, Marekani, ambamo marais hao walikuwa wamefikia. Rais Kikwete na Rais Mutrharika, ambao walikuwa miongoni mwa viongozi wa Afrika walioalikwa kuhudhuria Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika chini ya uenyekiti wa Rais Barack Obama wa Marekani, walifanya maongezi mafupi yasiyo rasmi, ambapo pamoja na mambo mengine walizungumzia kudumisha mahusiano mazuri na ya muda mrefu baina ya nchi hizo mbili.

Picha za Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Afrika huko Washington DC

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akijadiliana jambo na Rais Barak Obama wa Marekani kwenye ukumbi wa Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika uliofanyika jijini Washington DC chini ya uenyekiti wa Rais Obama wa Marekani Agosti 6, 2014

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akijadiliana jambo na Rais Barak Obama wa Marekani kwenye ukumbi wa Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika uliofanyika jijini Washington DC chini ya uenyekiti wa Rais Obama wa Marekani Agosti 6, 2014

Kongamano la wazi TGNP lajadili mchakato wa Katiba Mpya

Mwanaharakati na aliyekuwa Mjumbe wa Kamati iliyokusanya maoni ya wananchi katika mchakato wa katiba mpya, Humphrey Polepole akichangia mada katika kongamano hilo.
Mambo muhimu yaliojadiliwa katika kongamano hilo ni pamoja na ilani ya wanawake katika katiba mpya kuangalia suala la usawa wa kijinsia, wanawake wanapataje haki zao za msingi hasa katika suala la matibabu, uzazi salama, elimu, maji salama, ushiriki wa kutosha katika nafasi za ajira ngazi zote. 

Mengine ni pamoja na ushiriki sawa katika nafasi za maamuzi na ulinzi wa kutosha kutokana na kukithiri kwa ukatili wa Kijinsia. 

Kongamano hilo lilifanyika Agosti 6, 2014 kwenye viwanja vya TGNP jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wanaharakati pamoja na wana jamii wakiwa kwenye Kongamano la kujadili mchakato wa kutengeneza katiba mpya kwenye viwanja vya TGNP, Mabibo Dar es Salaam.

Kaimu Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia Tanzani TGNP, Lilian Liundi (katikati), akitoa hotuba yake wakati wa kongamano la wazi la jamii kujadili mchakato wa kutengeneza katiba mpya. (kushoto), Mdau wa Maendeleo Humphrey Polepole, na kulia Mwanaharakati wa Masuala ya Kijamii na Haki za Binaadamu, Gemma Akimali.

Baadhi ya wanaharakati pamoja na wana jamii wakiwa kwenye Kongamano la kujadili mchakato wa kutengeneza katiba mpya kwenye viwanja vya TGNP, Mabibo Dar es Salaam.

Mazishi ya ANDREA DUMA, baba wa mwandishi wa MOblogJeneza lililobeba mwili wa mchungaji mstaafu wa kanisa la Free Pentekoste (FPCT) Ihanja wilaya ya Ikungi, Andrew Duma (92).Katibu mkuu wa makanisa ya Free Pentekoste nchini,Elias Shija, akihubiri kwenye ibada ya mazishi ya mchungaji mstaafu wa Free Pentekoste Ihanja wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida, Andrea Duma.

[audio] Hotuba ya Rais Kenyatta kwa Wakenya akiwa Washington DC

Mhe. Rais Uhuru Kenyatta akihutubia waKenya jijini Washington Aug 6, 2014

Karibu kusikiliza hotuba (imepachikwa kwenye pleya hapo chini) ya Mhe. Uhuru Kenyatta alipozungumza na Wakenya usiku wa Agosti 6, 2014 kwenye hotel ya Marriott Wardman Park Hotel, jijini Washington DC nchini Marekani.Shukurani: Mubelwa Bandio

MO awashtaki CCM Singida kwa Kinana

Katibu wa CCM Mkoa wa Singida Naomi Kapambala aaizungumza na waanndishi wa habari juu ya ufafanuzi wa maendeleo ya ujenzi wa uwanja huo.

Hillary Shoo, Singida - Mbunge wa Jimbo la Singida mjini (CCM), Mohammed Dewji ameulalamikia uongozi wa Chama chake Mkoa wa Singida kwa kitendo cha kuchelewesha mchakato wa kumalizia ujenzi wa Uwanja wa michezo Namfua ikiwa ni moja ya ahadi zake alizotoa kwa wananchi wakati wa Uchaguzi Mkuu mwaka 2010.

Kuchelewa huko kuanza kwa mchakato wa ukarabati na uwekaji wa nyasi za bandia kwenye uwanja huo imeelezwa ni kutokana na urasimu na maslahi binafsi miongozi mwa viongozi wa CCM Mkoa wa

NMB YASHIRIKI NANE NANE NCHI NZIMA

NMB inashiriki maonyesho ya wakulima ya nane nane katika mikoa saba huku huduma zote za kibenki zikiwa zinafanya kazi katika mabanda yake kama kuweka na kutoa fedha, kupata taarifa za mikopo hasa ya kilimo.

NMB inashiriki maonyesho ya nane nane katika mikoa ifuatayo; Lindi ambako yanafanyika kitaifa, Morogoro, Dodoma, Tabora, Mbeya,Arusha na Kagera.
Wakulima pia wanaotembelea mabanda ya NMB kote nchini watapata fulsa ya kukutana na wataalam wa kilimo na pembejeo, vyama vya ushirika na hivyo kuwa na fulsa nzuri za wao kupata taarifa sahihi na ushauri wa jinsi ya kutumia benki kunufaisha shughuli zao za kilimo.
Kwa kuwa moja ya malengo ya NMB ni kuhakikisha inasaidia ukuaji wa kilimo na kukifanya kuwa cha kibiashara, yenye malengo la kumkwamua mkulima. Hii ni fursa nzuri kwa wakulima, wafanyakazi wa serikali na wajasiriamali kuweza kufika kwenye mabanda ya NMB ili kujionea huduma ambazo benki inatoa.

Kilimo ni uti wa mgongo kutokana na ukweli kwamba karibia 80% ya watanzania wanajishughulisha na kilimo.Kwa kutambua hilo, NMB ipo karibu yao zaidi katika kipindi hiki cha Nane Nane kwa kuleta huduma za kuwanufaisha.

Kauli mbiu ya ‘Kilimo na Mifungo ni biashara’ kwa mwaka huuimeifanya NMB kushirikiana na serikali katika kufanikisha maonyesho ya nane nane katika mikoa yote saba.
Benki ya NMB inatoa huduma mbali mbali za kilimo ikiwa ni pamoja na akaunti maalumu ya Kilimo yaani ‘Kilimo Account’ ambayo inamruhusu mkulima kuweza kujipatia mikopo mbali mbali ili kuweza kuinua uchumi wa Nchi.


Meneja wa huduma wa Benki ya NMB tawi la Mwanjelwa Jijini Mbeya, Happnes Pima (katikati) akimwelekeza jambo Mkuu wa Wilaya ya wangi'ombe Mkoa wa Njombe, Estelina Kilasi (kushoto) wakati alipotembelea banda ya benki hiyo kwenye maonyesho ya wakulima ya nanenane yanayoendelea  kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya, ambapo kwa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini yanafanyikia Mkoa wa MbeyaNane Nane Njiro Arusha: Baadhi ya askari polisi wakipewa maelezo ya namna ya kuchukua mikopo kutoka Benki ya NMB na Ofisa Mikopo Shekha Diwani, askari hao walitembelea kwenye banda la NMB jana lililomo Viwanja vya Maonyesho ya Nane Nane yanayoendelea jijini Arusha eneo la Njiro.


Wafanyakazi wa Benki ya NMB wakiwajibika katika banda lao kwenye maonesho ya wakulima maarufu kama Nane nane ambayo kwa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini yanafanyikia Mkoa wa Mbeya, katika Viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya.Askari wakiwa wameimarisha ulinzi kwenye banda ya benki ya NMB katika maonyesho ya wakulima ya nanenane yanayoendelea  kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya, ambapo kwa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini yanafanyikia Mkoa wa Mbeya


Meneja wa huduma wa Benki ya NMB tawi la Mwanjelwa Jijini Mbeya, Happnes Pima (kulia) akimwelekeza jambo Mkuu wa Wilaya ya wangi'ombe Mkoa wa Njombe, Estelina Kilasi (kushoto) wakati alipotembelea banda ya benki hiyo kwenye maonyesho ya wakulima ya nanenane yanayoendelea  kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya, ambapo kwa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini yanafanyikia Mkoa wa Mbeya.