Hatari ya unga wa lishe ya watotoMchanganyiko usiozingatia makundi matano ya vyakula, unaotengenezwa na wajasiriamali au nyumbani kwa ajili ya unga wa watoto maarufu ‘Lishe’, una athari za kiafya kwa watoto wachanga na walio chini ya miaka mitano.

Daktari Bingwa wa Watoto katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Augustine Massawe, amesema unga huo ni hatari kwa sababu mchanganyiko wake si muafaka kwa watoto.

Dk Massawe alikuwa akitoa mada kwenye semina ya waandishi wa habari kuhusu Maadhimisho ya Siku ya Unyonyeshaji Maziwa ya Mama.

Alisema kwanza utengenezaji wa unga huo hauzingatii vipimo maalumu, wala makundi ya virutubisho anavyopaswa kupata mtoto katika mlo mmoja, ambavyo ni wanga, protini, vitamini, mafuta na madini.

Massawe alikosoa utengenezwaji wa unga unaochanganywa mahindi, mchele, ulezi, soya, mtama,

Aeleza walivyotapeliwa milioni 29/= na 'mganga Manyaunyau'

Shahidi wa pili katika kesi ya kujipatia Sh29.6 milioni kwa njia ya udanganyifu inayomkabili mganga wa jadi, Dunia Salumu (37) ‘Manyaunyau’ amedai kuwa walilazimika kuuza kiwanja na nyumba ya urithi kutafuta fedha za kununua mabeberu saba na mafuta ya ngamia ili kumpa mganga huyo kama masharti ya kumfufua ndugu yao aliyefariki dunia.

Manyaunyau alifikishwa kwa mara ya kwanza katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Desemba mwaka 2013 akikabiliwa na shtaka la kujipatia fedha hizo kutoka kwa Tecla Modest.

Akiongozwa na Mwendesha Mashtaka, Nassoro Katuda shahidi huyo, Diana Steven (26) alidai kuwa baada ya kumaliza matanga ya mjomba wake, Saimon Modest aliyefariki mwaka 2008, wakiwa

Tamko rasmi la Matokeo ya Uchaguzi DMV kutoka Kamati ya Uchaguzi

Kwa WanaDMV,

Inaelekea kumebakia suitafahamu au tafsiri fulani kuhusu matokeo ya uchaguzi wa DMV 2014 kufuatia takwimu za kura tulizotoa na kuwasilisha kwa bodi ya DMV. 

Tamko hili linaweka wazi mshindi katika kila nafasi iliyogombaniwa. Hivyo kwa mujibu wa matokeo ya kura na wa katiba, wafuatao ndiyo viongozi wapya wa jumuia yetu kwa miaka miwili ijayo:-

RAIS- Iddy Sandaly
RAIS- Iddy Sandaly
MAKAMU WA RAIS - Harriet Shangarai
MAKAMU WA RAIS - Harriette Shangarai

KATIBU- Saidi Mwamende
KATIBU- Saidi Mwamende
MAKAMU WA KATIBU- Bernadetta Kaiza
MAKAMU WA KATIBU- Bernadetta Kaiza
MWEKA HAZINA- Jasmine Rubama
MWEKA HAZINA- Jasmine Rubama

Tamko hili pia limefikisha Kamati ya Uchaguzi wa 2014 kwenye tamati yake.

Mungu ibariki DMV, na adumishe mshikamano imara wa Watanzania.”

Safari Ohumay
Mwenyekiti

Q&A about an unproven drug for Ebola

WASHINGTON (AP) -- A Spanish missionary priest is the third Westerner with Ebola to be treated with an experimental drug that's never been tested in people and is said to be in very limited supply.

Spanish authorities' disclosure on Monday raised further ethical questions about why no Africans have received the drug and how to decide who gets access to an unproven drug in an emergency. The first two recipients were Americans.

The World Health Organization debated the issue Monday, even as Ebola experts have warned that scarce doses of experimental drugs aren't going to stop an outbreak that has now spread to four African countries.

Some questions and answers about the Ebola drug:

Q: What is this drug?

A: Called ZMapp, it is a cocktail of specially engineered antibodies designed to target and inactivate the Ebola virus.

Q: What do we know about whether it works?

Robin Williams aaga dunia

Robin WIlliams enzi za uhai wake mwaka 2013 (picha: soulculture.com)

Aliyekuwa akiigiza vichekeso na kucheza sinema na filamu, Robin Williams ameaga dunia Jumatatu asubuhi akiwa na umri wa miaka 63 kwa kifo kinachoelezwa kuwa kilitokana na kujiziba pumzi na kujinyima hewa (asphyxiation). Imeelezwa kuwa kwa siku za hivi karibuni alikuwa akipambana na sonona (depression). Kwa taarifa zaidi bofya hapa.

Mcolombia akamatwa JNIA na cocaine alizozivaa nguoni

Suruali ya mtuhumiwa huyo ikiwa imezungushiwa Cocaine. (picha: Francis Dande)
Baadhi ya dawa alizokuwa amemeza mtuhumiwa huyo.

DAR ES SALAAM, Tanzania - KIKOSI cha Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini kinamshikilia Andres Filipe Ballesteros Uribe (28) raia wa Colombia kwa tuhuma za kuingiza dawa hizo nchini kinyume cha sheria.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam leo, Mkuu wa kikosi hicho, Kamanda Godfrey Nzowa alisema mtuhumiwa huyo aliingia nchini saa nane usiku kwa ndege ya shirika la Ethiopian akitokea Adisi Ababa.

Alisema mtuhumiwa huyo alikutwa na cocaine iliyofungwa kwenye pakiti sita tofauti na kuiweka

Viongozi wapya wa CHADEMA Kigoma

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mkoa wa Kigoma kimepata viongozi wapya wa muda katika ngazi ya Mkoa na Wilaya katika uchaguzi uliyofanyika jana kama ifuatayo:-
 1. Ally Kisala ambaye ni Diwani wa Mwandiga, alichaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa CHADEMA Mkoa wa Kigoma
 2. Katibu Mkuu ni Shabaan Madede 
 3. Mratibu wa Baraza la Wanawake Mkoa (BAWACHA) ni Vestina James Luhihi 
 4. Omary Gindi ni Mratibu wa Baraza la Vijana (BAVICHA)
 5. Jeremia Misigaro ni Mratibu wa Baraza la Wazee.
Viongozi wa Jimbo 
 1. Mwenyekiti ni Khalfani Bona
 2. Katibu ni Frank Luhasha
 3. Katibu Mwenezi ni Idd Ngesha
 4. Mratibu wa Baraza la Wazee ni Yassin Mapigosaba 
 5. Mratibu BAVICHA ni Amfua Athumani
Mkurugenzi Mkuu wa Oganaizesheni na Usimamizi CHADEMA Taifa, Benson Kigaila, ambaye ndiye alikuwa msimamizi mkuu katika uchaguzi huo, alisema chama kimefanya uchaguzi huo kutokana na mapengo yaliyoachwa wazi na viongozi waliyohama hivi karibuni, na watashika madaraka hayo hadi uchaguzi utakapofanyika tena kwa mujibu wa katiba Agosti 30 mwaka huu.

Msimamo ACT-Tanzania kuhusu Katiba Mpya

Alliance for Change and Transparency-Tanzania Maoni ya ACT-Tanzania kuhusu namna ya kutoka katika mkwamo uliopo katika mchakato wa Katiba Mpya.

1. Nchi yetu iliingia katika mchakato wa Katiba kwa kushirikisha wananchi wote ili kupata Katiba bora yenye kuakisi matakwa ya nchi kwa sasa na baadaye. Ili kupata Katiba bora na inayokubalika na wananchi wengi iwezekanavyo, ni lazima mchakato wa kutunga Katiba uwe wazi, shirikishi na wenye kuzaa mwafaka na maridhiano miongoni mwa makundi mbalimbali ya wananchi

2. Chama cha ACT-Tanzania kinaipongeza sana Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyofanya kazi yake kwa bidii, umakini na weledi mkubwa kwa kuwashirikisha wananchi kwa upana wake na kwa

South Africa honours Mwalimu Julius K. Nyerere

Pretoria - The National Heritage Council of South Africa (NHC) will on Monday hold an honorary ceremony in Tanzania for the late President of that country, Dr Nwalimu Julius Nyerere.

The ceremony will be held at the University of Dar es Salaam in Tanzania, where Maria Nyerere, the President’s widow, will receive the Ubuntu Honour of 2014 on behalf of her late husband.

Arts and Culture Deputy Minister, Rejoice Mabudafhasi, is travelling to Tanzania to bestow the Ubuntu Honour on Nyerere, her department said on Monday.

Dr Nyerere joins other citizens of the world, who received the honour for their living evidence of the

Mjumbe wa Bunge la Katiba adai kupigwa na vijana wa CHADEMA

Mh. Edward Lowassa akimjulia hali Mgoli hospitalini, wote wako kamati namba 12. (picha: Fikra Pevu)

Mjumbe wa bunge maalum la katiba kutoka kundi la 201,Thomas Magnus Mgoli amelazwa katika hospital ya mkoa Dodoma baada ya kudai kupigwa na wanaodaiwa kuwa 'vijana ambao mashabiki wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)'.

Kwa mujibu wa FikraPevu akiwa kitandani hospitalini, Mgoli amesema alishambuliwa na vijana hao jana usiku majira ya saa moja eneo la area D anakoishi.

Amedai kuwa hukutana na vijana hao mara kwa mara anapokwenda dukani na huzungumzia masuala ya bunge hilo, lakini hiyo jana walimshambulia kwa kumuambia kuwa yeye ni CCM.
Mwenyekiti wa Bunge Maalum Mhe. Samuel Sitta akimjulia hali mjumbe wa Bunge Maalum kutoka kundi la 201 Mhe. Thomas Mgoli aliyelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma baada ya kujeruhiwa na watu wasiojikana wakati akipata huduma katika duka moja lililopo karibu na mahali anapoishi Mjini Dodoma. (picha: Owen Mwandumbya)

Taarifa ya usaili wa Jeshi la Polisi Tanzania kwa wakazi wa Mbeya

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, BARAKAEL .N. MASAKI – ACP anawatangazia Wananchi wote ya kuwa orodha ya majina ya vijana waliomaliza Kidato cha Nne mwaka 2013 na cha Sita mwaka 2014 na kuchaguliwa kufanya usalii wa kujiunga na Jeshi la Polisi inapatikana kwenye tovuti ya Polisi: www.policeforce.go.tz au wafike ofisi ya kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya iliyopo Forest jirani na Mahakama kuangalia majina yao.

Muhimu:
 • Mwombaji anaruhusiwa kufanya usaili kwenye kituo chochote cha usaili kilicho karibu naye kulingana na tarehe zinavyoonesha kwenye jedwali hapo juu ili mradi tu awe amejiridhisha kuwa

Invitation for admission into various program at the Centre for Foreign Relation in 2014/2015


CENTRE FOR FOREIGN RELATIONS
DAR ES SALAAM
(FULL ACCREDITED BY NACTE)

(Established by the 1978 Tanzania/Mozambique Agreement, Incorporated in the
Consular and Diplomatic Immunities and Privileges Act. No. 5, 1986)


INVITATION FOR ADMISSION INTO CERTIFICATE (NTA LEVEL 4), ORDINARY DIPLOMA (NTA LEVEL 5 & 6), DEGREE (NTA LEVEL 7 & 8) AND POSTGRADUATE DIPLOMA PROGRAMMES FOR THE ACADEMIC YEAR 2014/2015

A: IMPORTANT INFORMATION FOR ALL APPLICANTS

i)            THE CENTRE HAS INTRODUCED A BACHELORS DEGREE IN INTERNATIONAL RELATIONS AND DIPLOMACY (BDIRD) BEGINNING IN THE 2014/15 ACADEMIC YEAR.

ii)            Applicants aspiring to pursue Bachelors Degree in International Relations and

Shibuda, Arfi, Leticia watakwenda na maji CHADEMA? Arfi ahoji: "Hivi Lissu ni nani?" Aeleza sababu ya kurudi Bungeni

Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Said Arfi akitia saini kitabu cha mahudhurio mara baada ya kurejea katika Bunge hilo wiki iliyopita pembeni ni Lweli Lupondo akitoa maelezo jinsi ya kutia saini. (picha via Tz Gov blog)

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimesema kuwa kitawafukuza wabunge wake, John Shibuda (Maswa Magharibi), Said Arfi (Mpanda Mjini) na Leticia Nyerere (Viti Maalum) baada ya kujiridhisha kwamba wameshiriki vikao vya Bunge Maalum.

Hatua hiyo inakuja baada ya wabunge hao kuripotiwa kujisajili na kushiriki vikao vya Bunge hilo kinyume na msimamo wa CHADEMA kupitia kundi lao la Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) ambalo wamesusia wakidiai CCM imechakachua rasimu yenye mapendekezo ya wananchi.

Msimamo wa CHADEMA ulitolewa jana na Mwanasheria wake, Tundu Lissu akisema kuwa

Orodha ya wahitimu Kidato cha Sita na Nne walioitwa kwenye usaili Jeshi la Polisi

Jeshi la Polisi Tanzania linawaita kwenye usaili vijana waliomaliza kidato cha nne mwaka 2013 na kidato cha sita mwaka 2014 ambao wamechaguliwa kufanya usaili kabla ya kujiunga na Jeshi la Polisi.

Usaili utafanyika katika miji ya makao makuu ya mikoa Tanzania Bara Kwa tarehe zilizooneshwa kwenye jedwali hapa chini:-

Wakulima almanusra wamtandike Naibu Waziri

Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Godfrey Zambi amenusurika kupata kipigo kutoka kwa wakulima wa zao la pamba katika kijiji cha Marekano wilaya ya Maswa mkoa wa Simiyu kwa madai ya kutoridhishwa na majibu aliyoyatoa juu ya mbegu za pamba zisizo na manyoya (za Quton) kutoota katika musimu uliopita wa kilimo.

Tukio hilo limetokea kijijini hapo wakati Naibu Waziri huyo alipofanya ziara ya kushitukiza ya kutembelea vituo vinavyonunua zao hilo katika wilaya hiyo ili kukagua mizani zinayotumika kupimia zao hilo kutoka kwa wakulima.

Wakati akitoa majibu kwa wakulima ambao walikusanyika ghafla wakati akikagua mizani hiyo katika moja ya kituo kilichopo kijijini hapo ambao walihoji ni kwa nini serikali iliwalazimisha kununua mbegu hizo ambazo hazikuota pamoja bei ya kununulia zao hilo.

Taarifa ya Samweli Mwanga-Simiyu via Malunde1 blog

Proin Promotions Ltd., Mzee Yusuph wasaini mkataba wa kusambaza fiamu

Mzee Yusuph (Katikati) akiwa katika picha ya Pamoja na Meneja Wake Said Mwangushi (kulia) na Meneja Masoko wa Proin Promotions Limited, Evans Stephen (Kushoto) mara baada ya kumaliza kuongea na waandishi wa Habari leo katika ofisi za Kampuni ya Proin Promotions Limited zilizopo Mtaa wa Ursino MikocheniNa Josephat Lukaza - Proin Promotions Limited

Hatimaye Mzee Yusuph ametambulisha rasmi ujio wake katika tasnia ya filamu leo mara baada ya kuitambulisha filamu yake mpya na ya Kwanza iitwayo NITADUMU NAE ambapo filamu hiyo ni moja ya filamu ambazo zimetoka katika nyimbo zake.

Akiongea na Waandishi wa Habari, Mzee Yusuph alisema "Filamu hii nimeitengeneza muda mrefu sana na imetoka katika nyimbo zangu lakini nilishindwa kuisambaza kutokana na kukosa Msambazaji ambaye anaweza kukubaliana na vigezo vyangu lakini kwa bahati nzuri Proin Promotions

UNESCO, Read International watoa vitabu vya Sayansi, ArumeruNa Mwandishi wetu, Arumeru

Wanafunzi wa shule ya Mwedo sekondari iliyopo wilayani Arumeru wamelishukuru Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kupitia Read International la nchini Uingereza kwa kuweza kuwapatia vitabu vya kiada vya masomo ya Sayansi hali itakayowafanya kupiga hatua katika masomo hayo.

Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi hao Kaimu mkuu wa shule hiyo Clara Meijo alisema kuwa