Fidia ya bilioni 2.3 kwa wakazi wa Mloganzila yakabidhiwa

SERIKALI imetoa kiasi cha shilingi bilioni 2.3 ya fidia kwa wakazi wa eneo la Mloganzila lililopo katika Kijiji cha Kwembe Manispaa ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam ambao waliathiriwa kutokana na ujenzi wa barabara kutoka Kibamba- Kisokwa hadi barabara ya Morogoro.

Akizungumza jana (juzi) wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya barabara katika Manispaa hiyo, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli alisema kwa mujibu wa vifungu vya sheria ya ardhi na barabara inasema iwapo barabara ikimfuata mtu eneo alipo lazima mtu huyo apewe fidia, na mtu atakayeifuata barabara hataweza kupewa fidia yoyote.

Kwa mujibu wa Dkt. Magufuli, baadhi ya wananchi waliokuwa wakiidai serikali tayari

Not ready to use Ebola drug in Africa

A Canadian drugmaker working on an experimental drug for Ebola said Wednesday that it is not ready to make the treatment available in Africa, despite assurances by international health officials that it is ethical to use untested treatments to fight the deadly outbreak.

Tekmira Pharmaceuticals Corp. said that the "regulatory framework" for giving its drug to patients in Africa is not clear, given that the drug's safety and effectiveness has not been established.

"There can be no assurance that an appropriate framework for the use of this product will be found," said CEO Mark Murray on a call with investors and analysts. "Given the severity of the situation, we are carefully evaluating options for use of our investigational drug within accepted clinical and regulatory protocols."

Murray said the company is continuing discussions with governments and international agencies trying to contain the outbreak, including the World Health Organization. 

--- The AP

[audio] Mama aeleza alivyoshuhudia mbwa wakimla mtoto Ibrahim

Marehemu Ibrahim enzi za uhai wake
Marehemu Ibrahim enzi za uhai wake
Audio iliyopachikwa hapo chini ni ya mahojiano baina ya BEST FM radio na wananchi wa wilaya ya Ludewa kuhusiana na mbwa ambao walimla mtoto Ibrahim Faraja Chipungahelo akiwa hai na kufariki dunia.

Mama mmoja anaelezea hali halisi ilivyokuwa aliposhuhudia mnyama huyo akimla marehemu/

Mwananchi mwingine anazugumzia kushangazwa na ujasiri wa mwenye mbwa kwa majibu yake ya kejeli kwa wafiwa.

Ikulu yalaumiwa kuwa pango la mbwa waliokula watu, mifugo


Na Nickson Mahundi, Ludewa.

Utata umeendelea kugubika kwa wananchi wa wilaya ya Ludewa kuhusiana na mmiliki wa mbwa ambao walimuua mtoto Ibrahim Faraja Chipungahelo, Bw. Bosco Thobias Lingalangala uhalali wa kuyanunua baadhi ya majengo ya Ikulu ndogo ya wilaya ya Ludewa na kugeuza sehemu ya kufugia mbwa ambao ni hatari kwa maisha ya binadamu.

Hali hiyo ya sintofahamu imeendelea kuwashangaza wananchi hao wenye shauku ya kuhoji kwa

Njoo ushuhudie Perfect 6 National Finals 2014


BMK: Wajumbe waridhia madaraka ya Rais kupunguzwa

BAADHI ya wajumbe wa kamati namba 12, wamekubaliana kupunguza majukumu ya Rais na kutengwa kwa orodha ya viongozi ambao Rais anaweza kuwateua endapo atafanya uteuzi.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Paul Kimiti, alisema kamati yake pia imeridhia utaratibu wa uraia pacha.

Kimiti alisema wajumbe wa kamati yake wameona wapunguze majukumu ya Rais, ikiwa ni pamoja na

“Serikali imelisikia suala la uraia pacha, lakini ni la kikatiba sio la Rais." - Rais Kikwete akifungua Mkutano wa Kwanza wa diaspora, Dar es Salaam

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua mkutano wa kwanza wa Diaspora katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo Agosti 14, 2014
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua mkutano wa kwanza wa Diaspora katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo Agosti 14, 2014. (picha: Ikulu)

Na Joseph Ishengoma, MAELEZO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete amesema hana mamlaka ya amri kuzungumzia uraia pacha kwasababu ni la katiba.

Rais Kikwete amesema hayo leo katika Kongamano la Kwanza la diaspora lililofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Diaspora ni lugha inayotumika kuwatambulisha Watanzania walioko nje ya nchi wanaojiendeleza kwa njia mbalimbali ikiwemo elimu.

Kongamano hilo la siku mbili lenye lengo la kuelimishana, kubadilishana mawazo na kujadili fursa za uwekezaji, linaudhuriwa na wajumbe kutoka nchi 17 duniani.

“Serikali imelisikia suala la uraia pacha, lakini ni la kikatiba sio la Rais. Katiba ndio sheria mama sisi hatuna mamlaka ya amri kulizungumzia.”

Kwa mujibu wa Rais, watanzania waliowengi uraia pacha hauwakeleketi, hivyo diaspora wanaoishi nje ndio wanaostahili kulisukuma, lakini kwa sasa sauti yao bado haijasikika sana, badala ya kulizungumzia kwa nguvu, wanatumia muda mwingi kuzungumzia siasa za mitaani kwenye mitandao ya kijamii pindi wanapopata nafasi.

“Sauti yenu haijasikika sana, badala yake mnatumia muda mwingi kuzungumzia siasa za mitaani. Suala la uraia pacha liko mikononi mwa Bunge Maalum la Katiba. Kama katiba haijasema nyinyi ni rais, sheria ikitungwa haiwezi kuwapa uraia,” amesema.

Kwa mujibu wa Rais, rasmu ya Katiba iliyopo inazungumzia hadhi ya Watanzania walioko nje sio uraia. “Mnachoweza kufanya ni kushawishi wabunge wa Bunge Maalum la Katiba kukubali uraia pacha kuwa ndani ya katiba na hili sio jambo haramu, zungumzeni nao serikali haina tatizo nalo iwapo Katiba itawatambua.”

Pamoja na uraia pacha, Rais amewaomba wanadiaspora kuzingatia uwekezaji ndani ya nchi ili kuleta maendeleo ya kiuchumi, kutafuta masoko ya bidhaa ya bidhaa za Tanzania nje ya nchi, kuunda umoja utakaowaunganisha na kutumia teknolojia na maalifa wanayopata nje kuendeleza taifa lao.

Kauli mbiu ya kongamano hilo ni, “Nyumbani ni Nyumbani.”

Awali Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Mizengo kayanza Pinda ametaka mkutano huo kusaidia kukata kiu ya Watanzania kupata majibu ya mambo ambayo wamekuwa wakiulizia pindi wanapokutana na viongozi mbalimbali wa nchi nje ya Tanzania.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua mkutano wa kwanza wa Diaspora katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo Agosti 14, 2014. (picha: Ikulu)

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akibonyeza kitufe kuzindua tovuti rasmi ya Diaspora wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kwanza wa Diaspora katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo Agosti 14, 2014. Pamoja naye ni Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda, Mwenyekiti wa Taasisi ya Diaspora Bw. Emmanuel Mwachullah (wa pili kulia), Mwana-Diaspora Dennis Londa (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa Diaspora Bi. Rose Jairo
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akibonyeza kitufe kuzindua tovuti rasmi ya Diaspora wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kwanza wa Diaspora katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo Agosti 14, 2014.
Pamoja naye ni Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda, Mwenyekiti wa Taasisi ya Diaspora Bw. Emmanuel Mwachullah (wa pili kulia), Mwana-Diaspora Dennis Londa (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa Diaspora Bi. Rose Jairo. (picha: Ikulu)

Taarifa ya JWTZ ya kuzindua huduma ya Tiba bure kwa jamii

Jeshi la Ulinzi la Wananchiwa Tanzania (JWTZ), linatarajia kuzindua huduma ya Tiba kwa jamii kuanzia tarehe 15 Agosti 2014 hadi 19 Agosti 2014 kuanzia saa 12:00 asubuhi hadi 12:00 jioni katika viwanja vya Mnazi mmoja. Huduma hizi zinakwenda sambamba na maadhimisho ya miaka 50 ya JWTZ.

Huduma zitakazotolewa ni pamoja na vipimo vya magonjwa ya Homa ya Ini (Hepatitis B& C), Presha, Kisukari, Huduma za Ushauri nasaha na kupima VVU, Huduma za uchangia damu salama, Macho,

Gazeti la SANI laonywa kuhusu habari linazochapisha

Mkurugenzi wa Idara ya Habari Assah Mwambene (kulia) akiwaonyesha waandishi wa habari gazeti la Sani leo mjini Dar es Salaam lililochapisha habari ya upotoshaji inayoweza kujenga hofu kwa wananchi. es Salaam.Kushoto ni Afisa Habari anayeshughulika na Usajili wa magazeti Jovina Bujulu. (picha: MAELEZO)

SERIKALI imelionya gazeti la SANI kwa kuchapisha habari na picha zisizokuwa za kweli na kuzua hofu kwa wananchi.

Hatua hiyo inafuatia na gazeti hilo kuchapisha habari zilizokuwa na kichwa kisemacho ''EBOLA YATUA na kuonyesha picha za maiti bila kueleza kuwa sio za tukio lililotokea nchini.

Onyo hilo limetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Assah Mwambene wakati akiongea na waandishi wa habari.

“Sio vizuri na kuleta mizaha katika habari makini na zinazogusa maisha ya wananchi kama

"UKAWA ni kikundi kidogo cha watu waliojipanga kuvuruga AMANI ya nchi" - Makonda

Katibu wa Hamasa na Chipukizi wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi, Ndugu Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa sekretarieti uliopo Ofisi za makao makuu ya Chama Cha Mapinduzi maarufu "White House", mjini Dodoma, leo

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Demokrasia bila mipaka ni ukichaa na demokrasia bila nidhamu ni uwendawazimu” Mwl Jk Nyerere

Ndugu zangu Watanzania, naomba mfahamu kuwa miongoni mwa wajumbe wote wa bunge la katiba takriban 600, wajumbe waliofanya maamuzi haramu ya kugomea ni 79 ambao ni pungufu ya asilimia 15% ya wajumbe wote, na sio kweli kuwa wao pekee ndio wenye tafsir sahihi ya rasimu. Wajumbe wa makundi mbalimbali wakiwemo wawakilishi wa vyama vyote vya siasa takriban 18 kati ya 22 bado wamo kwenye bunge, kati ya wajumbe wa kundi la 201 walioasi ni 15 ambapo bara ni 9 na zanzibar 6 lakini pia katika wanaojiita UKAWA wapo wabunge ambao wameendelea kurudi bungeni kwa kuzingatia maslahi mapana ya Taifa.

Takwimu hizi zinatuthibitishia kuwa UKAWA ni kikundi kidogo cha watu waliojipanga kuvuruga

Ethical issues in using experimental Ebola drug

Reflecting unanimous agreement from a panel of experts, the World Health Organization said in a statement today that it is ethical to offer unproven drugs to treat or prevent the spread of the Ebola virus.

The panel, including ethicists, researchers, regulators and patient advocacy experts, met to consider the dilemma brought to the forefront after two American health care workers and one Spanish clergyman, who later died, were treated with experimental drugs in scarce supply. The virus, spreading out of control through West Africa, has already infected more than 1,800 people, killing more than 1,000.

"The WHO did the easy part," says Alta Charo, professor of law and bioethics at the University of Wisconsin, Madison. The moral quandary posed by a rapidly spreading deadly disease that might be helped by as-yet unproven drugs runs much deeper.

What are the bigger ethical concerns?


The biggest is who gets a drug that is in scarce supply. It's a classic rationing problem. In a public

Miss Ilala 2013 Dorice Mollel atembelea Kampuni ya kutengeneza umeme wa gesi na kutunza mazao, Riela, Ujerumani


Bw. Karl Heinz Knoop akielezea historia fupi kuhusu kampuni yake kwa wanafunzi wa Chuo cha kumbukumbu ya Mwl. Nyerere akiwemo Miss Ilala 2013 Dorice Mollel wanaoshiriki program ya mwezi mmoja nchini Ujerumani.

Miss Ilala 2013 Dorice Mollel (kushoto pichani) akiwa kwenye program ya mwezi mmoja, na wenzake 8 kutoka Chuo cha kumbukumbu ya Mwl. Nyerere ambapo wamepata nafasi ya kwenda kutembelea Kiwanda cha Kilimo kilichoanzishwa mwaka 1972 ambacho kinamilikiwa na Bw. Karl Heinz Knoop, mwenye uzoefu wa miaka 50 ambaye anatarajia kujenga kiwanda hiki pia nchini Tanzania mkoani

Serikali itimize ahadi ya ujenzi wa zahanati za kataGari la wagonjwa lilitolewa na serikali likiwa limeharibika kutoka na miundo mbinu ya barabara na kushindwa kufanyiwa matengezo kwa muda mrefu hali inayomfanya daktari wa Zahanati hiyo kuwafuata majumbani wagonjwa mahututi kwenda kuwapatia huduma za afya.
Ngorongoro

Wakazi wa vijiji vya Ololosokwan, Soit-Sambu, Njoroi na Loipir kata za Ololosokwana na Soit-Sambu wilayani Ngorongoro wanakabiliwa na changamoto kubwa ya huduma ya Afya kwa kutembea umbali mrefu kufuata huduma hizo kwenye kijiji cha Sero huku waathirika wakubwa ni kinamama na watoto.

Umbali wa zahanati hizo imekuwa sababu kubwa ya vifo hususani kwa akina mama wajawazito wanaotaka kwenda kujifungua na watoto halikadhalika wanapozidiwa hufia njiani kutokana na umbali wa zahanati kutoka kijiji kimoja kwenda kingine wanapotakiwa kuwahishwa hospitalini hali

[audio] Mkurugenzi Mtendaji Azania Bank aihutubia Diaspora ya Tanzania

Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Charles Singili alipokuwa akizungumzia huduma za benki yake kwa waTanzania jijini Washington DC (picha zote kwa hisani ya Ikulu)


Hotuba fupi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank, Charles Singili alipokutana na Watanzania waishio nchini Marekani usiku wa Agosti 2, 2014.

Hotuba hii ilitolewa kwenye mkutano kati ya Watanzania wanaoishi Marekani na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk Jakaya Kikwete

Karibu umsikilize


Daktari bandia akamatwa baada ya kusababisha kifo cha mgonjwa

.

Polisi mkoani Singida inamshikilia mtu anayedaiwa kuwa daktari ‘feki’ kwa tuhuma ya kusababisha kifo cha mgonjwa, mkazi wa kijiji cha Iyumbu, Wilaya ya Ikungi mkoani hapa.

Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Dk Philip Kitundu alimtaja Prosper Samson anayetuhumiwa kusababisha kifo cha Jubulu Mahende ambaye alikuwa mgonjwa. 

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida, Geofrey Kamwela amekiri kuwepo tukio hilo na kuongeza kuwa Polisi wanaendelea na uchunguzi zaidi wakati mtuhumiwa akishikiliwa. 

Kwa mujibu wa Dk Kitundu, mtuhumiwa alikiri kutokuwa na cheti kutoka chuo chochote cha afya na

NMB Yazindua tawi la Nanyumbu

NMB katika kuongeza idadi ya matawi yake na kuhakikisha inawafikia watanzania wengi na kila kona nchini, jana imezindua tawi jipya la wilaya mpya ya Nanyumbu katika mkoa wa Mtwara.

Kwa sasa NMB imefikisha matawi Zaidi ya 150 na wateja Zaidi ya milioni 2 huku ikijivunia ATM mashine Zaidi ya 500 nchi nzima. Hiyo ni idadi kubwa kuliko benki yoyote Tanzania.

Ufunguzi wa tawi hili ni Faraja kubwa kwa wakazi wa Nanyumbu ambao wamekuwa wakipata tabu kufuata huduma za kibenki wilayani Masasi. Uwepo wa NMB pia utarahisisha biashara kwa wakazi wa Nanyumbu kwani wengi wao wanafanya biashara na wananchi wa Msumbiji. Ubadirishaji wa fedha za kigeni pia ni mojawapo ya huduma itakayosaidia wakazi wa Nanyumbu nan chi ya Msumbiji.NMB pia ili kusogeza huduma Zaidi kwa watanzania, measisi ubunifu mkubwa katika soko la Tanzania ikiwa ni pamoja na huduma za benki kwa njia ya simu yaani NMB mobile , Pesa Fasta na malipo kwa kutumia mashine za ATM. NMB inaendelea kujikita katika kutoa huduma kwa makampuni makubwa, masoko ya kifedha pamoja na huduma za kusaidia makusanyo ya kifedha na biashara. Lakini Pia  imekuwa mstari wa mbele katika maendeleo ya kilimo na imeanzisha mfumo wa stakabadhi ghalani kupitia vyama vya ushirika nchini.


Kaimu mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu, Kristofer Maga (katikati) akikata utepe kufungua tawi la NMB Nanyumbu

Meneja wa NMB kanda akitoa maelezo mafupi baada ya uzinduziMmoja wa wafanyabiashara wa Wilaya ya Nanyumbu akizungumza