Taarifa ya uteuzi wa Dkt Msonde kuwa Katibu Mtendaji NECTA


THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898

Fax: 255-22-2113425


PRESIDENT’S OFFICE,
STATE HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Dkt. Charles Msonde kuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Mitihani Tanzania (NECTA).

Taarifa iliyotolewa Ikulu, Dar es Salaam jioni ya jana, Alhamisi, Agosti 14, 2014, na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue inasema kuwa uteuzi huo ulianza juzi, Jumatano, Agosti 13, 2014.

Kabla ya uteuzi wake, Dkt. Msonde alikuwa Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza hilo la mitihani.

Dkt. Msonde anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Joyce Ndalichako, ambaye amerudi kuendelea na kazi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam baada ya kumaliza likizo yake ya kujinoa (Sabbatical Leave).

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.

15 Agosti, 2014
Lives of 3 Tanzanian peacekeepers lost in Goma

On 13 August 2014 in Goma, North Kivu, MONUSCO carried out the repatriation of the mortal remains of three Tanzanian peacekeepers who lost their lives on a road accident in Masisi territory. (Photo MONUSCO/MPIO)

Kwa nini Diaspora ya Tanzania tunaitaka ijenge vihenge nyumbani, lakini hatutaki iwe na haki tuliyonayo?

Ndugu zangu,

Leo alfajiri niliongoza mjadala kwenye redio za Kwanza Jamii na Nuru FM kuhusiana na kongamano linaloendelea Dar la Watanzania wa Diaspora wanaokutana nyumbani, Tanzania.

Ni kwa nini tuna hofu na Watanzania wenzetu walio ughaibuni? Hofu hii ni ya kihistoria. 

Kwanini kongamano hili la kwanza kufanyika lisiwe la mwisho kufanyika katika sura yake hii, kwamba maudhui ya kongamano yenyewe kuwa ni ; connect, engage, inform and ivest nako kunakosekana dhana integration kwa maana ya kujumuisha.

Hoja kubwa kwa sasa ni kwa namna gani tunawajumuisha wenzetu walio ughaibuni kupitia uraia pacha. Kwamba wakati umefika wa kubadilika na kuona kuwa uraia pacha una maanufaa makubwa kwetu kama taifa. Haipaswi kuendelea kuwachukulia wenzetu walio diaspora kama ' Ng'ombe wa Maziwa'- Fuatilia mjadala huu... kwa kubofya hapa (mjengwablog.com)

8 Wakamatwa JNIA na pasi bandia za Ulaya


Idara ya Uhamiaji Nchini, imewakamata Raia wa nane (8) wa kigeni wakati wakiingia nchini kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. Nyerere, wakiwa na pasipoti bandia za kusafiria za Mataifa tofauti ya Ulaya. Wageni hao walikuwa wakijaribu kuingia nchini leo tarehe 15.08.2014 majira ya saa nane na nusu usiku kwa ndege ya shirika la Ndege la Uturuki yenye Namba TK 603, wakitokea Uturuki na kujitambulisha kuwa Raia wa Sweden na Belgium.

Maofisa Uhamiaji katika kituo hicho baada ya kuwatilia mashaka na kuwafanyia ukaguzi wa kina, waligundua kuwa wageni hao ni Raia wa Iraq wakijaribu kuingia nchini Tanzania na pasipoti za bandia.

kukamatwa kwa wageni hao ni jitihada za Idara ya Uhamiaji kupambana na Uhamiaji haramu nchini ambapo suala la Udhibiti wa Mipaka linapewa kipaumbele. akizungumzia tukio hilo, Kaimu Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Tatu Burhan, anasema, kwa kutumia ujuzi na weledi walionao Maofisa Uhamiaji wanaendelea kufanyakazi usiku na mchana kuhakikisha Sheria na Taratibu za Uhamiaji zinafuatwa. "Idara ya Uhamiaji, iko macho hatulali kuhakikisha Ulinzi na Usalama wa nchi ikiwa ndio jukumu letu namba moja unaimarika. kwahivyo, kila mtu awe Raia wa kigeni na Watanzania wanapaswa kufuata Sheria na Taratibu zilizopo za kuingia na kutoka nchini."

Hadi sasa, Wageni hao wamezuiliwa kuingia nchini na wanaendelea kushikiliwa na Maofisa wa Idara ya Uhamiaji kituoni hapo huku wakisubiri kurudishwa walikotoka. Hili ni wimbi lililoibuka hivi karibuni kwa baadhi ya Raia wa nchi za Iraq, Iran, Syria kujaribu kuingia nchini isivyo halali huku ikisemekana lengo lao kubwa ni kuingia Tanzania na baadae kutoka kuelekea Mataifa ya Ulaya.

Majina ya Wageni hao na Pasipoti bandia walizokuwa wakitumia pamoja na Majina halisi na Pasipoti zao za Iraq zilizogunduliwa baada ya upekuzi kwenye mabano ni kama ifuatavyo;

  1. ADEL SHAALAN MOHAN - SWEDISH, PPT. NO. EI282207 ( ADEL SHAALAN MOHAN Pasipoti Nam. G1489664)
  2. SAMER HELMI KAMIT - SWEDISH, PPT. NO. 87187804 ( LAZIM MOSA HITEET, PPT. Namba, A 13466001)
  3. MOHAMMED JAFAR AL MOSAWI - SWEDISH, PPT.NO. 87168871 (ALI HUSSEIN OLEIWI, PPT. NO. G 1111623)
  4. 4. DAVID GABRIEL POBLETE - SWEDISH PPT.NO. 86867751 (AYAD SAMI MAKTTOOF, PPT NO. A 4910203)
  5. SADDAM ALKHAMERI AREF - SWEDISH, PPT NO. 81640513 (SAIF ALDAN FALIH HASAN, PPT. NO. G 1489664)
  6. ALI MOHAMMED ABDULLAH - IRAQ, PPT. NO. A 5931725
  7. OSAMAH ZAID GHAEB AL-OBAIDI - IRAQ, PPT. NO. A 6175951
  8. ALI HUSSEIN OLEIWI - IRAQ, PPT. NO. G 1111623
Kesho kuna Mkutano wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Wanahabari

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Jaji Fredrick Werema atazungumza na Wanahabari kesho, Jumamosi, Agosti 16, 2014 kuanzia saa 4:30 asubuhi katika Ukumbi wa Mikutano (Ground Floor) wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora uliopo katika Jengo la Haki (Haki House), mtaa wa Luthuli -- mkabala na jengo la Ofisi ya Makamu wa Rais na mita chache kutoka Makao Makuu ya Wizara ya Fedha.

Katika mkutano huo, Mhe. Jaji Werema atafafanua masuala kadhaa ya kisheria yanayohusu mchakato wa Katiba.

Nyote mnakaribishwa. Wanahabari mnaombwa kuwa ukumbini ifikapo saa 4:15 asubuhi kesho.

Picha za kuapishwa kwa Majaji wa Mahakama KuuZifuatazo ni picha zikimuonesha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwaapisha Waheshimiwa Majaji wapya wa Mahakama Kuu ya Tanzania leo, 15 Agosti, 2014 huko Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Call for nomination: 2015 UN Public Service Awards

The United Nations Department of Economic and Social Affairs

UN DESA has issued a call for nominations for the 2015 UN Public Service Awards. The Awards are an international contest designed to promote and support innovations in public service delivery worldwide. The awards are open to all public organizations, including governments and public-private
partnerships involved in delivering services to citizens.

Please note, nominations must be submitted online at www.unpan.org/applyunpsa2015 by 31 October 2014.

In Memory of Judge RAPHAEL B. MAGANGA who died 16 August 1986 RAPHAEL B. MAGANGA
 RAPHAEL B. MAGANGA 

Dad, it is now 28 years that you departed from us too sudden without bidding farewell to anyone.

Since that fateful and dreadful Saturday 16th of August 1986 when you answered God’s call peacefully, a dark cloud of grief, sorrow and confusion fell upon us, punched a big hole in our life. It was like a nightmare. To others you are gone forever but in our hearts you shall be remembered forever.

Your sudden death still hurts us Dad. Oasis of wisdom and intelligence and advisor to many. Life has not been the same but with God at hand we are cared up.

Memory is a way of holding onto the things you love, the things you are, the things you never want to loose. They say time is healer, is it really? Or we just burry our sorrow deeper and deeper! We wonder. Death leaves a heartache no one can heal, love leave a memory no one can steal.

Fondly remembered by your loving Children Nelly, Gerald, Louisa, Alice, Susan and Andrew, Son in-laws Pascal, Rikard, Peter and Alvin, Your daughter in-law Aisha (Angel), grand children Jadden, Nelly, Andrew, Simon & Mercy, relatives & friends.

Kuhusu taarifa za kuwepo kwa mgonjwa wa Ebola nchini Tanzania


Mkurugenzi wa Maabara ya Taifa ya Afya na Ubora, Dk.Fausta Mosha (kulia), akitoa ufafanuzi wa kimaabara kuhusu ugonjwa huo.
Mkurugenzi wa Maabara ya Taifa ya Afya na Ubora, Dk.Fausta Mosha (kulia), akitoa ufafanuzi wa kimaabara kuhusu ugonjwa huo.

Baada ya kuenea kwa taarifa kuwa kuna watu wawili, mmoja raia wa nje na mwingine Mtanzania kuwa na dalili za ugonjwa wa Ebola, serikali imethibitisha kuwa hadi sasa hakuna mgonjwa wa Ebola nchini. Imesema wagonjwa waliohisiwa awali, walikuwa na magonjwa tofauti.

Akizungumza leo asubuhi na kipindi cha East Africa Breakfast cha East Africa Radio, Waziri wa Afya, Dk. Seif Rashid amesema wagonjwa hao waliohisiwa kupata maambukizi kutokana na dalili za awali, ni wa kutoka Benin na Mtanzania.

“Kuna wagonjwa ambao tumewalaza lakini kwa mujibu wa dalili walizokuwa nazo na

Akutwa na saa, simu ya marehemu mfanyabiashara wa Uganda aliyeuawa Tanzania

Police have started investigations into the death of Dr. Asadu Bakka Musujja who was allegedly murdered in Tanzania.

Bakka 48, a business man and brother to a renowned city businessman, Godfrey Kirumira, was buried Wednesday, in Goloola village, Gomba district.

He was reportedly killed on August 2, 2014, by unknown people as he travelled back to Uganda abode a bus from South Africa.

Deputy police spokesperson, Polly Namaye said they want to ascertain the real cause of his death as a

[audio, video, picha] Rais Kikwete akihutubia Mkutano wa Kwanza wa Tanzanian Diaspora

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizendo Pinda akimueleza jambo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mkrisho Kikwete wakati wa kongamano la Watanzania waishio ughaibuni lililofanyika kwa mara ya kwanza nchini, leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizendo Pinda akimueleza jambo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mkrisho Kikwete wakati wa kongamano la Watanzania waishio ughaibuni lililofanyika kwa mara ya kwanza nchini, leo Jijini Dar es Salaam.

Picha zaidi zimepachikwa hapo chini pamoja na audio na video...

"...katiba ipatikane, isipatikane sisi wengine tutaendelea..."

Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, Fahmi Dovutwa (pichani), ameunga mkono msimamo wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na amewataka wajumbe hao kutolegeza msimamo wao.

Akizungumza na NIPASHE akiwa mjini Dodoma, ambako vikao vya Bunge hilo vinaendelea, Dovutwa alisema wajumbe hao wana haki na uhuru wa mawazo kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aliwashauri wasichoke wala kupumzika na badala yake waendelee kushikilia msimamo wao wa kushinikiza Bunge lisitishwe kwa nguvu zao zote hadi mwisho ili kuona wanapata kile wanachotarajia.

“Nawashauri wasitetereke, wasiogope, wasimame hapo hapo walipo maana wana haki ya

Mtoa kibanzi kwenye jicho la mwenziye kabla ya kutoa boriti jichoni mwake...

Ikulu yazungumzia taarifa kuwa Rais Kikwete alihoiwa na Obama kuhusu IPTL

MKURUGENZI wa Mawasiliano Ikulu, Salva Rweyemamu amekanusha madai yaliyotangazwa hivi karibuni kwamba, Rais Jakaya Kikwete amehojiwa na Rais wa Marekani, Barack Obama, kuhusu fedha za kampuni ya kufua umeme ya IPTL.

Akizungumza na waandishi wa habari Ikulu Dar es Salaam jana kukanusha taarifa hizo zilizotolewa na moja ya gazeti la kila siku nchini, Rweyemamu alisema katika ziara ya Rais nchini Marekani hivi karibuni, hakukutana kwa mazungumzo ya ana kwa ana na Rais Obama.

“Rais pia alikutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID) na katika mikutano yote hiyo hakuna jambo lolote linalohusu IPTL lililojadiliwa wala kuulizwa.
“Huu ni uongo na ni habari ya kutungwa na habari kama hizi huandikwa kwa ajenda, sasa sijui hawa wenzetu waliandika kwa ajenda zipi” 

Alisema masuala yote yanayohusu kilichojiri katika mkutano huo na namna Tanzania ilivyonufaika katika sekta mbalimbali, yatabainishwa hivi karibuni na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.