Athari za vikwazo Urusi vs Marekani na Ulaya, sasa Estonia wanaomba Tanzania iinunuze maziwa yao

Estonia seeks urgent export to Asia, Africa

TALLINN (Xinhua) -- Estonian government has called on authorities of Indonesia, Kenya and Tanzania to import its superfluous dairy products as part of the country’s efforts to tackle Russia’s import ban.

Ago Pyartel, Estonian Chief Veterinary Inspector has sent letters to authorities of Indonesia, Kenya and
Tanzania to seek instant possibilities to address the difficult situation faced by Estonia’s producers due to

Safari ya Rais Kikwete katika gari-moshi mkoani Mogorogo

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa ndani ya behewa maalum la VIP la treni la TAZARA wakati wa safari ya Rais Kikwete kuelekea Kisaki katika ziara yake ya mkoa wa Morogoro.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, leo, Alhamisi, Agosti 21, 2014, ameweka historia nyingine katika ziara yake ya Mkoa wa Morogoro wakati aliposafiri kwa treni ya Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA), ikiwa ni mara yake ya kwanza kutumia usafiri huo katika kipindi chake cha Urais.
Rais Kikwete, akifuatana na Mama Salma Kikwete, amesafiri kilomita 143 ndani ya Behewa la Kirais (Presidential Coach) la T-One kwa kiasi cha saa tatu na dakika 25 akitokea stesheni ya Ifakara katika Wilaya ya Kilombero kwenda Stesheni ya Kisaki, Wilaya ya Morogoro.
Rais Kikwete akiandamana na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mheshimiwa Joel Bendera na Waziri wa

Barua ya wazi ya Ally Saleh kwa Rais Kikwete

KUHUSU: MADAI YA KUTESWA MAHABUSU WANAOTUHUMIWA KWA MAKOSA YA UGAIDI


Ndugu Rais,

Nisamehe sana nakuandikia barua ya wazi, lakini mimi raia wako sijui njia nyepesi ya kuweza kukufikishia waraka huu, maana sizijui taratibu zilizotandikwa na za wazi za kufanya hivyo.

Mheshimiwa Rais, waraka huu unahusu madai ambayo wiki mbili hizi yamekuwa yakiandikwa katika vyombo vya habari kuhusiana na watu kadhaa ambao wako mahabusu kukabili makosa ya ugaidi.

Mimi ni katika raia wako wanaopenda mfumo wa sheria ufanye kazi, na ndio maana barua hii si kulalamikia

Tanzania Youth Olympic team 2014, Nanjing, China


Rais Kikwete aahidi ufumbuzi wa kudumu baina ya wakulima, wafugaji

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  • Asisitiza kuwa tatizo ni wafugaji kulisha ng’ombe mashambani
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameahidi kuwa Serikali yake italipatia ufumbuzi wa kudumu tatizo sugu la ugomvi kati ya wakulima na wafugaji katika Mkoa wa Morogoro ambalo kimsingi linasababishwa na wachungaji kuingiza mifugo yao katika mashamba ya wakulima.
 
Aidha, Rais Kikwete amewataka wachungaji kuacha mara moja tabia yao ya kuingiza na kulisha ng’ombe wao katika mashamba ya wakulima akisisitiza kuwa hicho ndicho chanzo cha ugomvi kati ya makundi hayo

Huu ni upendo usiopimika!

South Africa too, bans travelers from Ebola-hit countries

South Africa said on Thursday that due to fears over the spread of the Ebola virus it was banning travelers from Guinea, Liberia and Sierra Leone from entering the country, apart from its own citizens.

Travelers from Nigeria, where there is a much smaller outbreak, will be allowed entry.

South Africans returning home from these areas will be permitted entry but undergo a strict screening process, a health ministry statement said.

“For citizens of South Africa who wish to travel to these countries, they will be requested to delay their travels unless it is also absolutely essential for them to travel to these countries,” Health Minister Aaron Motsoaledi said.
VOA News - South Africa Bans Travelers From Ebola-stricken Countries

Bunge Maalum la Katiba: Prof. Shivji aitwa

.

Bunge Maalumu la Katiba, limemwalika Mhadhiri mashuhuri wa masuala ya Katiba, Profesa Issa Shivji, kuwasaidia aina ya Muungano na namna mambo yake yatakavyoingizwa kwenye Katiba.

Pia Bunge hilo limepokea mapendekezo ya nyongeza ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, yaliyokuwa yamehifadhiwa, ili yatumike wakati wa kuunda katiba ya Tanganyika, yajadiliwe na kamati hizo.

Uamuzi huo ulifikiwa jana kwenye Kamati ya Uongozi, iliyokaa ambapo Mwenyekiti wa Bunge, Samuel Sitta, aliunda Kamati Ndogo ya Kamati ya Uongozi, kufanyia kazi kwa undani mambo ambayo kamati nyingi zimeshindwa kufikia muafaka.

Mambo hayo ni pamoja na Mahakama ya Kadhi, Muundo wa Bunge na kuangalia Mambo ya Muungano,

Rais Kikwete azindua TeleMedicine; Aahidi kutafuta soko la mazao ya chakula nje ya nchi

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa  kituo cha Afya cha Kibaoni Morogoro vijijini Agosti 22, 2014
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa kituo cha Afya cha Kibaoni Morogoro vijijini Agosti 22, 2014Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa  kituo cha Afya cha Kibaoni Morogoro vijijini Agosti 22, 2014

Rais Jakaya Kikwete amezindua mradi mpya wa huduma ya afya kwa njia ya mtandao (TeleMedicine) katika kituo cha afya cha Mwaya, wilayani Ulanga, mradi ambao ni moja ya utekelezaji wa sera ya afya ya mwaka 2007 wenye lengo la kuboresha huduma za afya vijijini ili kupunguza vifo vya watoto wenye umri chini ya imaka mitano na wajawazito.

Rais alisema huduma hizo zitasaidia kutatua matatizo yaliyoshindikana katika zahanati na kwamba watahakikisha huduma zote muhimu kama ya upasuaji, zitakuwepo.

Rais pia aliaidi kushughulikia tatizo la soko la mpunga katika wilaya hiyo. Alisema serikali itatafuta masoko ya mazao ya chakula nje ya nchi ili kusaidia wakulima kuuza kwa tija.
“Nitahakikisha tunatafuta soko la mazao ya chakula nje ya nchi ambapo nilikwishawaagiza mawaziri nchi ya Sudan Kusini kuyatafuta, jambo litakalowezesha wakulima kuuza kwa faida,”
Taarifa ya maanishi via gazeti la UHURU
Taaifa kwa picha ni kutoka Ikulu.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuashiria kufungua kituo cha Afya cha Kibaoni Morogoro vijijini Agosti 22, 2014

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Mama Salma Kikwete pamoja na Wabunge Mhe Abdul Mketeme (kushoto) na Mhe Getrude Rwakatale (kulia) wakifunua pazia kwa pamoja kuashiria kufungua kituo cha Afya cha Kibaoni Morogoro vijijini Agosti 22, 2014

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitembelea akikagua wodi mpya ya kituo cha Afya cha Kibaoni Morogoro vijijini Agosti 22, 2014

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitembezwa maeneo mbali mbali ya kituo cha Afya cha Kibaoni Morogoro vijijini baada ya kukifungua Agosti 22, 2014

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wazazi baada ya kufungua kituo cha Afya cha Kibaoni Morogoro vijijini Agosti 22, 2014


US bans diplomats from ALS Ice Bucket ChallengeLawyers at the United States State Department have banned high-profile U.S. diplomats from participating in the fundraising phenomenon that has swept social media in recent weeks - The ALS "Ice Bucket Challenge".

In an unclassified cable issued earlier this week, the department lauded the unique effort to raise money and awareness for amyotrophic lateral sclerosis, also known as Lou Gehrig's disease, but said it violates internal policy.

"There are firmly established rules preventing the use of public office, such as our Ambassadors, for private gain, no matter how worthy the cause. Thus, high-ranking State Department officials are

Katiba inayotafutwa ni ya CCM na siyo ya Tanzania - Prof. Baregu

Akizungumza na NIPASHE jana, aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba,  Prof. Baregu, aliliomba radhi taifa yeye binafsi na kwa niaba ya wenzake 30 waliokuwa kwenye Tume hiyo, ambao kati yao hiyo 15 kutoka Tanzania Bara na 15 Zanzibar, kwa kutekeleza mchakato wakiamini ni wenye lengo la kupatia Taifa Katiba mpya, kumbe walilaghaiwa wakatumika kuitumikia CCM kutafuta Katiba yake.
“Niligoma kujitoa kwenye Tume nilipotakiwa kufanya hivyo na chama changu (CHADEMA), nikiamini mchakato ulikuwa kwa maslahi ya taifa, kumbe tulilaghaiwa na sasa binafsi nimeamini Katiba inayotafutwa ni ya CCM na siyo ya Tanzania”
Prof. Baregu alisema uamuzi wa CCM wa kubariki Bunge Maalum la Katiba liendelee siyo wa busara wala hekima bali umegubikwa na mihemko ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwakani.

Kwa mujibu wa Prof. Baregu, kinachoelezwa na chama tawala kuwa kuna maendeleo mazuri katika mchakato wa Katiba, ni kuondoa mambo yote yaliyo kwenye Rasimu ya pili, ambayo yalilenga kudhibiti nidhamu, uwajibikaji na utumishi bora kwa umma.
“Mgawanyo wa majimbo, ukomo wa mtu kugombea ubunge, miiko na maadili ya watumishi wa umma na mawaziri kutotokana na wabunge, vyote hivyo wanaviondoa kwenye rasimu wanataka kuunda utumishi au uongozi wa aina gani kama siyo unafiki?” “Hatunabudi kuomba radhi Watanzania tuliowaahidi kuwaletea Katiba Mpya.”
amenukuliwa Prof. Baregu akisema hayo.

NIPASHE - Baregu:Najuta

Ajira zilizolalamikiwa kutolewa kiupendeleo zimefutwa

Hatimaye zile lawama kuhusu upendeleo wa ajira katika Idara ya Uhamiaji kwenye Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, zimefutwa baada ya Kamati ndogo iliyoundwa kuchunguza tuhuma hizo kubaini kuwa ni kweli nafasi hizo ziligawiwa kwa upendeleo bila ya kufuata taratibu, kanuni na sheria za ajira.

Ajira hizo zilitangazwa Februari 17, mwaka huu na watu 15,707 walijitokeza kuwania nafasi hizo 200, miongoni mwao, waombaji 1,005 waliitwa kwenye usaili na waliothibitishwa waliitwa kazini.

Katibu Mkuu wa Wizara hiyo ambaye ndiye aliyeiongoza Kamati hiyo, Mbarak Abdulwakil amesema nafasi hizo zitatangazwa upya na kusimamiwa na Wizara hiyo badala ya Idara husika.
“Kamati hiyo iliyoanza kazi yake Agosti Mosi, mwaka huu ilibaini kwamba hata kigezo cha umri, ambacho ni miaka 25 kwa konstebo na miaka 30 kwa koplo hakikuzingatiwa kwani wenye umri zaidi ya huo waliitwa kazini... “Lakini zaidi, baadhi ya wasailiwa walioitwa kazini ni ndugu na jamaa wa watumishi wa Idara ya Uhamiaji.”
Aidha, ajira hizo zilizofutwa zinahusisha pia nafasi 28 zilizokuwa zimetangazwa kupitia Idara ya Uhamiaji Zanzibar.

Ilitanabahishwa kuwa si kosa kwa ndugu na jamaa wa watumishi kuajiriwa iwapo wanakidhi vigezo vyote, lakini inapotokea kwamba hakuna msimamizi huru ni wazi kwamba kunakuwa na upendeleo kama ilivyotokea.

Hali halisi katika Shule ya Msingi Medeli

Wanafunzi wa shule ya msingi Medeli iliyopo kata ya Tambukaleli manispaa ya Dodoma wakiwa wamekaa kwenye mifuko ya salfeti iliyotandikwa chini kutokana na shule hiyo kukosa madawati tangu mwaka 2007 ilipojengwa.
 Hali halisi katiak Shule ya Msingi Medeli: Wanafunzi hukaa chini na matundu ya vyoo ni 6 kwa ajili ya wanafunzi 789.

Wanafunzi wa Shule ya msingi Medeli kata ya Tambukaleli wakicheza mpira uliotengenezwa na vitambaa kutokana na shule hiyo kukosa vifaa vya michezo kama ilivyo kwa shule nyingine hali inayochangia kwa kiasi kikubwa michezo kushuka shuleni hapo.


Picha zote: John Banda

Christian Bella kuburudisha kwenye fainali za TMT @ Mlimani City

Christian Bella

Na Josephat Lukaza - Msanii wa Muziki wa Dansi anayejulikana kama Christian Bella anayetamba na kibao chake cha Nani Kama Mama ni mmoja wa Wasanii watakaotoa burudani katika ukumbi wa Mlimani City siku ya Jumamosi, tarehe 30 mwezi huu katika fainali kubwa za Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT).

Bella amehaidi kutoa burudani ya uhakika ambapo wapenzi wa muziki wake watafurahi na kufurahishwa na show atakayoitoa siku hiyo katika fainali ya kumkabidhi mshindi wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) kitita cha shilingi milioni 50 za Kitanzania.

Viingilio ni V.I.P shilingi 50,000 na kawaida 30,000. Fainali itaoneshwa moja kwa moja (live) kupitia kituo cha runinga cha ITV na milango itakuwa wazi kuanzia saa 7.30 usiku.

Tanzania Movie Talents (TMT) ni shindano la kwanza kufanyika Afrika Mashariki na Kati ambalo limeanzishwa na Kampuni ya Proin Promotions Ltd likiwa na lengo la kuibua na kusaka vipaji vya kuigiza kwa watanzania ambao wana vipaji lakini walikosa fursa ya kuonekana. TMT ilianza rasmi tarehe 1 Aprili 2014 katika mkoa wa Mwanza, Kanda ya Ziwa ambapo baadaye shindano likaendelea katika Kanda nyingine tano huku katika kila Kanda washindi walikuwa ni watatu huku kanda ya Pwani washindi walikuwa ni 5 ambapo jumla ya Washindi 20 walipatikana na kuletwa Dar es Salaam katika kambi na hatimaye mchujo kuanza na kubakiwa na washiriki 10 ambao leo hii wameingia fainali ya kuzisaka zile milioni 50 za Kitanzania.

Katika Fainali hiyo kubwa kutakuwa na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali.

Sikiliza moja ya nyimbo atakazoimba LIVE stejini siku hiyo...

Survey: Elephant population increase in Tanzania- Kenya ecosystem

DAR ES SALAAM, Aug 22 (Bernama) -- The number of elephants in the Serengeti-Maasai Mara ecosystem has increased from 258 in 1986 to 7,535, a latest survey has found.

The census was conducted by a scientists' community from Tanzania and Kenya which are sharing the ecosystem, Xinhua news agency reported.

The eco system covers 32,000 sq km of the Ngorongoro Conservation Area, Serengeti National Park, Maswa District, Ikongoro and Grumeti Wildlife Management areas and Kijereshi Game Reserve on the Tanzanian side and Masai Mara National Park and adjacent areas in Kenya's Narok County.

Tanzanian Minister for Natural Resources and Tourism Lazaro Nyalandu said an aerial survey

Mapendekezo ya Kamati za BMK kuhusu mgawanyo wa madaraka, Mahakama ya Kadhi, Uraia, Haki za Wanaume

Kamati namba 1 na 11 za Bunge Maalumu la Katiba zimetaka Rais wa Zanzibar kuwa makamu wa kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano na Waziri Mkuu kuwa Makamu wa pili.

“Makamu wa kwanza awe ni Rais wa Zanzibar na wa pili awe ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ili kumpa mamlaka Rais wa Zanzibar…kwenye kamati yetu tumeondoa neno nchi washirika na Waziri Mwandamizi,” amenukuliwa akisema Mwenyekiti wa kamati namba moja, Ummy Mwalimu.

Makamu Mwenyekiti wa kamati namba 11, Hamad Yusuph Masauni, alisema kamati yake imependekeza kuwa na Makamu wa Rais ambaye ni Rais wa Zanzibar ili kumwezesha kutambulika nje ya nchi kama