Kauli ya CUF kuhusu kunyanyaswa na kulawitiwa viongozi wa Uamsho

Bila ya shaka kila mmoja wetu ndani ya Tanzania na nje ya Tanzania ameshtushwa kwa kiasi kikubwa baada ya kupata taarifa ya kunyanyaswa vikali pamoja na kufanyiwa matendo ya kulawitiwa viongozi wa Jumuia ya Uamsho Zanzibar.

Matendo haya katika hali ya kiubinadamu hayafai kabisa na nidhahir kwa kila mmoja wetu kuyapiga vita ili jamii na mataifa kwa ujumla wazisikie sauti zetu juu ya viongozi hawa wakubwa wa Dini ya Kiislamu.

Tukiwa kama taasisi kubwa ya hapa Tanzania Chama cha Wananchi CUF tunalaani vikali ukatili na ushenzi uliofanywa na jeshi la polisi dhidi ya viongozi wa Jumuiya ya Uamsho na wenzao 19.

Kwa mujibu wa walivyoeleza watuhumiwa hao wakiwa Mahakama ya kisutu Shekh Farid Had

Kubenea afika Mahakama Kuu kusimamisha Bunge Maalumu la Katiba

Mwandishi wa Habari Said Kubenea amewasilisha ombi katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam akiiomba mahakama itoe amri ya kusimamisha Bunge Maalumu la Katiba linaloendelea Dodoma.

Kubenea aliwasilisha ombi hilo juzi dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) kupitia kwa wakili wake Peter Kibatala, akiomba Bunge hilo lisimamishwe hadi mahakama itakapotoa tafsiri sahihi ya bunge hilo kuhusu mamlaka iliyonayo na kama ni sahihi kwenda kinyume na rasimu.

Katika ombi hilo, Kubenea anaiomba mahakama itoe amri hiyo wakati wakisubiri uamuzi wa

Uaumuzi wa Kamati ya TCRA dhidi ya Clouds FM Radio

Wawakilishi kutoka Clouds Entertainment FM Radio wakiwa kwenye mkuatno huo. (picha: jamii.com | simu namba 0712-727062)

SHAURI LA UKIUKAJI WA KANUNI ZA UTANGAZAJI NAMBA 4/2014 DHIDI YA CLOUDS ENTERTAINMENT FM RADIO


Tarehe 15/06/2014, kituo cha Clouds Entertainment FM Radio cha Dar es Salaam kilikiuka Kanuni za Utangazaji (Maudhui) za mwaka 2005, kupitia kipindi chake cha Njia Panda kilichorushwa hewani kati ya saa 8.00 mchana na saa 10.00 jioni. Kipindi hiki kilikuwa na mada iliyohusu Safari ya Kuzimu. Maudhui ya kipindi hiki yalijaa simulizi za kufikirika, za kishirikina na kichawi.

Bofya hapa kupakua na kusoma shauri hilo.

Serikali yampiga marufuku raia wa Iraq kuingia nchini

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Idara ya Uhamiaji

Raia wa Uholanzi mwenye asili ya Iraq, Shirwan Naseh aliyezuliwa kuingia nchini na Idara ya Uhamiaji

Idara ya Uhamiaji nchini ni moja ya Taasisi za Ulinzi na UsalamA iliyo ndani ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ikiwa na jukumu kuu la kudhibiti na kuwezesha uingiaji, ukaazi na utokaji nchini wa raia na wageni.

Katika taarifa hii kwa vyombo vya habari, Idara inakusudia kuelezea umma kuhusu kuzuiliwa kuingia nchini kwa Bw. SHIRWAN NASEH ISMAIL, RAIA WA NETHERLAND, mwenye PASIPOTI NA. BRR40RK68 iliyotolewa tarehe 15 Julai, 2014.

Raia huyu wa Uholanzi mwenye asili ya Iraq, amekamatwa jana tarehe 21.08.2014 majira ya saa

Uaumuzi wa Kamati ya TCRA dhidi ya Clouds Television


Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Margaret Munyagi (wa pili kulia), akiwa na wajumbe wenzake wakati wa mkutano huo. Kutoka kushoto ni Abdul Ngarawa, Joseph Mapunda, Walter Bgoya na Mkurugenzi wa Utangazaji (TCRA), Habby Gunze. (picha: jamii.com | simu namba 0712-727062)

SHAURI LA UKIUKAJI WA KANUNI ZA UTANGAZAJI NAMBA 5/2014 DHIDI YA CLOUDS TELEVISION


Tarehe 16/05/2014 na 06/06/2014 kati ya sa 3.00 na 4.00 usiku, kituo cha Clouds Television cha Dar es Salaam kilirusha kipindi cha Bibi Bomba ambacho kilikiuka Kanuni za Utangazaji (Maudhui) za mwaka 2005, Kipindi hicho katika tarehe tofauti kilitangaza shindano la kumtafuta mshindi wa bibi bora nchini ambaye angezawadiwa shilingi Milioni kumi. Maudhui ya kipindi hiki yalidhalilisha mabibi hao washiriki kutokana na maswali ya aibu waliyokuwa wakiulizwa na Waamuzi wa shindano hilo ambayo ni kinyume na Kanuni za Huduma ya Utangazaji(Maudhui),2005.

Bofya hapa kupakua na kusoma shauri hilo.

Uhusiano wa Tanzania na IsraelILIWAHI kutokea Tanzania ikavunja uhusiano wake wa kibalozi na Israel katika mazingira ya kiutu, mazingira yaliyoonyesha kwamba Israel iliusahau sana utu na kufanya ma bo yaliyoonyesha unyama zaidi. Lakini nchi hiyo ilipojirudi mambo yakabadilika, uhusiano baina ya mataifa haya mawili ukarudi kwenye hali yake ya kawaida.

Nimeshawishika kulijadili hilo kufuatia maandamano yaliyofanywa hivi majuzi na kundi la wau Jijini Dar es salaam, wakiitaka serikali ya Tanzania ivunje tena uhusiano wake na Israel, shinikizo linalofuatia hali mbaya inayoendelea kwa sasa kati ya Israel na Palestina.

Machafuko hayo yamesababisha roho za mamia ya watu kupotea bila sababu yoyote ya lazima.

Ninaposema roho za watu simaanishi za upande mmoja tu, kama baadhi ya watu

Acheni ulegevu, acheni woga - Rais Kikwete


Jengo la  mradi mkubwa wa maji ambao  umegharimiwa na Serikali ya Marekani kupitia MCA-Tanzania Agosti 22, 2014

 
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
Website : www.ikulu.go.tz   
Fax: 255-22-2113425

PRESIDENT’S OFFICE,
STATE HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

JK: Acheni woga na udhaifu wa kusimamia sheria

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewataka viongozi nchini kuacha woga na ulegevu katika kusimamia sheria za kulinda mazingira na vyanzo vya maji ambavyo ni namna ya uhakika ya kuwawezesha wananchi kuendelea kupata maji ya uhakika, safi na salama.

Aidha, Rais Kikwete amewataka watu wanaokopa fedha katika vyama vya ushirika vya akiba na mikopo kuhakikisha kuwa wanarudisha fedha hizo kwa wakati kwa sababu kushindwa kurudisha mikopo hiyo kwa wakati kunawarudisha nyuma wengine ambao pia wanahitaji mikopo hiyo.

Rais Kikwete amesema hayo jana, Ijumaa, Agosti 22, 2014 kwenye siku yake ya tatu ya ziara yake ya

Muhongo ni Mhanga wa propaganda ya udini

Kumekuwepo na habari ambazo zimeendelea kushamiri kila uchao katika mitandao ya kijamii na pia habari hizo kuripotiwa na magazeti kadhaa, ambapo kwa mara ya kwanza gazeti la mtanzania la Jumanne ya tarehe 19th Aug 2014, kisha gazeti la Jambo leo la Alhamis ya tarehe 21st Aug 2014 na baadaye gazeti la An nuur la Ijumaa ya tarehe 22nd Aug 2014, kwa mfululizo, kwa mfanano wa dhamira na maandishi magazeti hayo yote yameandika habari ya upotoshaji, uchonganishi na kukuza chuki ya kidini hapa nchini. Habari katika magazeti hayo zimebeba hoja kuu UDINI wa PROF MUHONGO ambae ni Waziri wa Nishati na Madini wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambapo vyombo hivyo vya habari vimeripoti “unbalanced story” kuwa miongoni mwa wanafunzi 10 waliopewa scholarship na Serikali ya China hivi karibuni wote ni wakristo, na kwamba jambo hilo limefanywa kimkakati hili kuwatenga, kuwabagua na kuwakandamiza waislamu wa Nchi HII.

Ukweli halisi ni kuwa jumla ya Scholarship za Msc Oil/Gas ambazo zimetolewa katika chuo cha Petroleum nchini china ni 15 ambapo katika hizo 10 zinalipiwa na Serikali ya China na 5 zinalipiwa na Serikali ya

Rais Kikwete azindua jengo jipya la SACCO Kinole


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifunua pazia kuzindua jengo jipya la Chama cha Kuweka na Kukopa (SACCOS) cha kijiji cha Kinole, Morogoro vijijini Agosti 22, 2014.Rais Kikwete akiongea na mtoto Rebecca Mbena ambaye ni mwanafunzi wa darasa la kwanza katika shule ya msingi ya Kinole wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa shule ya msingi ya Kinole Agosti 22, 2014

Tanzania 11 vs Real Madrid Legends

screen-shot iliyochukuliwa pnde tu goli la tatu lilipofungwa. (picha: wavuti.com) Ilionekana kupitia: tanzaniabox.com

Beki wa timu ya Tanzania 11, Shadrack Nsajigwa akichuana na mshambuliaji wa Real Madriad Legends, Luis Figo wakati wa mchezo wa Kimatifa wa Kirafiki uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Picha hi na inazofuatia hapo chini ni kutoka kwa F. Dande


Kiungo wa timu ya Real Madrid Legends, Christian Karembeu akimwonesha Rais Jakaya Kikwete picha ya kumbukumbu aliyopiga kwa kutumia iPad tablet yake.

Baada ya miaka 5 rumande Mahakama yaamuru Wachina 'wa Samaki wa Magufuli’ warudishiwe mali, meli, samaki na waachwe huruBaada ya kusota rumande kwa miaka mitano hatimaye raia wawili wa China waliokuwa wanakabiliwa na kesi ya kuvua samaki katika Ukanda wa Kiuchumi wa Bahari ya Tanzania bila kibali wameachiwa huru katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Aidha, mahakama imeamuru washitakiwa warudishiwe mali zao, ikiwemo meli iliyotumika kufanya uvuvi huo ikiwezekana na samaki walikutwa nao pamoja na hati zao za kusafiria.

Kwa mara ya kwanza, walishitakiwa watu 35 kutoka mataifa tofauti ya Bara la Asia, kama vile China, Ufilipino, Vietnam na wawili raia wa Kenya, walikamatwa Machi 8, mwaka 2009 wakivua na walikutwa na

International Higher Education Fair in Ethiopia, Kenya, Tanzania, Uganda, Rwanda

Africa Student Fairs Series, 2015

International Higher Education Fair in Ethiopia, Kenya, Tanzania, Uganda, Rwanda

Dates and Venues:
- Addis Student Fair - 2nd and 3rd March, 2015 (Radisson Blu Hotel, Addis Ababa)
- EdExpo Kenya - 6th and 7th March, 2015 (Hilton Hotel, Nairobi)
- EdExpo Tanzania - 9th & 10th March, 2015 (Serena Hotel, Dar es Salaam)
- Uganda International Education Fair - 13th and 14th March, 2015 (Hotel Africana, Kampala)
- Rwanda International Education Fair - 16th March, 2015 (Hotel des Mille Colline, Kigali)

For more information visit - www.edexpo.catalystexpo.com

Rais Kikwete sasa ni Chifu Chidukila baada ya kutawazwa na Chifu Kingalu wa WaluguruCHIFU wa Waluguru Kingalu Mwanabanzi wa 14, akijiandaa kumtawaza Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuwa Chifu Msaidizi wa kabila hilo katika sherehe za aina yake zilizofanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi ya Kinole, kata ya Makuyuni, Morogoro vijijini Agosti 22, 2014. Rais Kikwete pia alipewa jina la CHIDUKILA, lenye kumaanisha "muibukaji", kwa maana ya kwamba Rais Kikwete ana uhuru wa kuibuka kijijini Kinole bila taarifa wala kusubiri kualikwa.

Tangazo la Wizara la Mkutano na Watanzania wanaosoma Ukraine

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI

TANGAZO KWA UMMA


MKUTANO KATI YA WIZARA NA WANAFUNZI WANAOSOMA MASHARIKI MWA UKRAINE HUSUSANI ENEO LA LUGANSK


Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inawatangazia wanafunzi wote wa Tanzania wanaosoma katika vyuo vya Lugansk, Ukraine na maeneo mengine Chini ya Ufadhili wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ambao hivi sasa wako likizo hapa nchini kuwa kutakuwepo na mkutano kujadili, pamoja na mambo mengine, hali ya usalama na hatua za kuchukua kabla ya kurudi Lugansk kuendelea na masomo, mwezi Septembea, 2014.

Mkutano huo utafanyika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, siku ya Jumatano, tarehe 3 Septemba, 2014 saa nane mchana. Aidha, wanafunzi wengine wanaosoma Lugansk kwa udhamini binafsi wanaombwa kuhudhuria ili kushiriki katika mkutano huo.

Imetolewa na:

Katibu Mkuu
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
7 Mtaa wa Magogoni,
Post Code 11479,
S.L.P. 9121,
DAR ES SALAAM.

Wakamatwa kwa kutengeneza noti za fedha bandia USD10,640


Kamishna wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam akionesha fedha bandia zilizokamatwa

SABA WAKAMATWA KWA KUJIHUSISHA NA UTENGENEZAJI WA NOTI BANDIA ZA DOLA ZA KIMAREKANI WAKAMATWA


Jeshi la Polisi katika Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kukamata kundi la watu saba wanaotengeneza noti bandia za dola ya Kimarekani huko maeneo ya Sinza katika Hotel iitwayo Mombasa Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

Watuhumiwa hao walikamatwa mnamo tarehe 04/8/2014 wakiwa na noti bandia zipatazo 10,640 za dola mia (100) ambazo ni sawa na dola 1,064,000 ambazo ni zaidi ya shilingi za Kitanzania bilioni moja katika

Albino 20 wapewa simu na Kamanda Kova na SAPNA Electronics

Kamishna wa Polisi wa Kanda maalumu ya Dar es Salaam, Suleman Kova akimkabidhi Mwenyekiti wa chama cha albino Dar es Salaam, simu kwa ajili ya albino waishio jijini Dar es salaam

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewashauri albino wanaoishi jijini humo kuwa karibu sana na jeshi hilo ili kurahisisha mawasiliano kati yao na Wakuu wa vituo vya Polisi vilivyo karibu na makazi yao au wanapofanyia usalama wao jijini Dar es Salaam.

Kamishna wa Polisi wa Kanda hiyo Maalum ya Polisi, Suleman Kova amewataka kwa sasa waongeze mawasiliano na jeshi la Polisi kutokana na taarifa za uhalifu dhidi ya albino katika baadhi ya mikoa hapa nchini.
 
Kova ameongea na albino hao ofisini kwake kuwataarifu kwa ujumla kuhusu jitihada kubwa sana za

HESLB call to loan applicants for missing information

CALL FOR LOANS APPLICANTS TO CORRECT THEIR LOAN APPLICATIONS

 

During the verification exercise of the 2014/2015 loan application forms, the Board has come across loan applications which are incomplete or are missing some vital information for further loans processing. For that reason, the Board would like to inform concerned Loan applicants that such incomplete applications will not be processed until the missing information is provided.

Therefore, loan applicants and/or guarantors who have not signed their documents are required to come physically at HESLB offices on Plot No. 8, Block No. 46 Sam Nujoma Road, Mwenge- Dar es Salaam for correction of their loan applications.

Applicants who have not attached (to their application forms) birth certificates, guarantor’s particulars such

Vifaa vya kupimia wenye dalili za ugonjwa Ebola

Mkurugenzi wa Ugavi wa Bohari ya Dawa Tanzania (MSD), Heri Mchunga (kushoto) akimpima Mkurugenzi wa Afya na Usafi wa Mazingira wa Wizara ya Afya na Ustawi Dkt. Elias Chinamo (kulia) kuonyesha namna moja ya kifaa cha kupimia joto la mwili wa Binadamu kinavyofanya kazi kwa kubaini dalili za Ugonjwa wa Ebola eneo la uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Sehemu ya vifaa vya kubaini hatua za awali za ugonjwa wa Ebola kwa kupima hali ya joto la mwili kwa wasafiri kutoka nje nchi wanaotumia viwanja vya ndege vilivyokuwa vimeagizwa na Serikali vimewasili jijini Dar es salaam.

Vifaa hivyo vinavyohusisha kamera 4 zenye uwezo wa kubaini joto la mwili wa msafiri kwa umbali wa mita 100 bila kumgusa muhusika vimewasili leo katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam kutoka nchini Afrika ya Kusini vilikonunuliwa.

Akikabidhi vifaa hivyo kwa wataalam wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Kebwe Steven Kebwe amesema kuwa kuwasili kwa vifaa hivyo ni moja ya juhudi za Serikali za kuhakikisha kuwa wananchi wanakuwa salama kwa kuuzuia ugonjwa huo kuingia nchini.

Amesema vifaa hivyo vitapelekwa katika maeneo ya viwanja vya ndege na maeneo yanayotumiwa na