Man gets Ebola after stealing a phone from patient

Security and medical officials in Kibaale District have registered a case in which a man allegedly went in an isolation ward at Kagadi Hospital and stole a cellular phone from one of the Ebola patients.

The 40-year-old resident of Kyakabugahya LCI in Kagadi Town Council travelled about three kilometers to the hospital to apparently obtain a phone estimated to be valued at Ugandan Shs 60,000 weeks ago.

The suspect allegedly broke into the isolation ward on the night of Tuesday August 14, undetected by hospital guards. The patient, who has since succumbed to the deadly hemorrhagic fever, then reported the theft to the hospital security that then embarked on tracing the alleged thief.

Police detectives began tracking him after he apparently began communicating to his friends using the phone. But as police zeroed in on him, he developed symptoms similar to those of Ebola and sought medication at the hospital.

While at hospital he reportedly confessed stealing the phone and has handed it to Kagadi police.

--

Washiriki wa Dance 100%chini ya Vodacom waendelea kujifua kwa nusu fainali


Mshiriki wa shindano la Dance 100% wa kundi la”Tatanisha Dancers” la Mabibo jijini Dar es Salaam Mstafa Yahaya akionesha umahiri wake wa kudansi wakati wa mazoezi yao ya kujindaa na nusu fainali ya shindano hilo litakalofanyika Septemba 13 mwaka huu kwenye viwanja vya Don Bosco Oysterbay. Shindano hilo limeandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.

Midwifery Services Gap Analysis 5 Days Workshop in Dar e Salaam


ICM/TAMA – Midwifery Services Gap Analysis 5 Days Workshop in Dar e Salaam from 8th to 12th September 2014 at White Sands Hotel.


The International Confederation of Midwives (ICM) from The Hague Netherlands will be visiting Tanzania Midwives Association (TAMA) from 8th 2014. This is the first time for ICM to visit Tanzania.

ICM works to strengthening midwifery globally including in low-resource countries for the achievement of Millennium Development Goals (MDGs) especially MDG 4, 5 and 6. Similarly, TAMA works to strengthening midwifery nationally and foster the development of midwifery care in Tanzania.

During their visit TAMA in collaboration with ICM have arranged to hold a Gap Analysis workshop for 5 African country teams including Tanzania from 8thSeptember 2014. One of the strategies that

Promota aliyemvuruga Diamond nchini Ujerumani matatani

Msanii Diamond akiondolewa chupu chupu katika mikono ya wenye hasira
Msanii Diamond akiondolewa chupu chupu katika mikono ya wenye hasira

Promota Awin Williams Akpomiemie
Promota Awin Williams Akpomiemie

Fujo za Agosti 30, 2014 katika show ya Diamond zasababisha hasara ya euro 300,000

Stuttgart, Ujerumani - Anayejiita promota Biritts Event - inayomilikiwa na Awin Williams Akpomiemie raia wa Nigeria amejikuta katika mashaka baada ya ripoti ya polisi kuthibitsiha jumla ya hasara ya Euro 300,000 (Tsh.600 million) zilizo sababishwa na fujo ya siku ya Jumamosi 30 Agosti 2014 baada ya msanii wa Nasib Abdul aka Diamond Platnumz kuchelewa kufika ukumbini mjini Stuttgart, Ujerumani.

Baada ya uchunguzi wa polisi kufuatia fujo hizo imegundulika kuwa muandaaji wa onyesho hilo Mr. Awin Williams Akpomiemie aliudanganya utawala wa ukumbi wa Sindfingen kwa kukodisha

Taarifa ya TFF kuhusu mgogoro wa kimkataba baina ya Okwi, Yanga, Simba

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Septemba 7, 2014

MKATABA WA YANGA, OKWI HAUPO


"Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imekutana leo (Septemba 7 mwaka huu) na kupitia masuala mbalimbali ikiwemo mgogoro wa kimkataba kati ya klabu ya Yanga na mchezaji Emmanuel Okwi.

Mkataba huo ulipitiwa na Kamati ikiwemo kumsikiliza mchezaji mwenyewe pamoja na upande wa Yanga, na kuridhika kuwa mkataba kati ya pande hizo umevunjika.

Ukiwa ni mkataba wa pande mbili, Yanga ilikiuka kipengele namba 8 kuhusu malipo ya ada ya usajili.

Yanga ikiwa mwajiri, haikutekeleza kipengele hicho cha kimkataba hadi kufikia Juni 27 mwaka huu ilipoandika barua TFF kuomba mkataba huo uvunjwe. Kwa maana hiyo Okwi ni mchezaji huru, hivyo yuko huru kujiunga na timu yoyote.

Mkataba ni uhusiano kati ya mwajiri (Yanga) na mwajiriwa (Okwi), ambapo Kamati imebaini kuwa

Taarifa ya Benki Kuu kuhusu toleo la sarafu ya Shilingi Mia Tano

Mkurugenzi Huduma za Kibenki kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Bw. Emmanuel Boaz (kulia) na Mshauri wa Fedha kutoka ofisi hiyo Bw. Hassan Jarufu wakiwaonesha waandishi wa Habari(Hawapo Pichani) Toleo jipya la sarafu ya Shilingi 500 inayotarajiwa kuingizwa kwenye mzunguko kuanzia mwezi Oktoba 2014.
(picha: Hassan Silayo/Maelezo)Benki Kuu ya Tanzania ndiyo chombo chenye jukumu la kutoa sarafu na noti halali (legal tender) zinazotumika nchini. Katika kutekeleza jukumu hili Benki Kuu hutengeneza noti na sarafu zenye uwiano mzuri wa thamani (denominations) unaozingatia uwezekano wa zile zenye thamani kubwa kuweza kugawika katika zile zenye thamani ndogo ndogo.

Hii hulenga kurahisisha upatikanaji wa chenji na uwezekano wa wahitaji wa viwango mbalimbali vya bidhaa na huduma kupata katika mafungu yatakayokidhi mahitaji yao.
Katika kutekeleza jukumu hili, Benki Kuu imetoa toleo jipya la Sarafu ya Shilingi 500. Hatua hii imezingatia yafuatayo:
  • Kwamba noti ya shilingi mia tano (500), ndiyo inayotumika zaidi kwenye manunuzi ya kawaida ya kila

Mmoja wa wanaohisiwa kuvamia na kuua polisi Geita akamatwa juu ya mti na bomu

Silaha ziliroporwa kituo cha olisi Ushirombo, wilaya ya Bukombe na kukamatwa leo

Habari kutoka Geita zinasema kuwa, msako uliofanywa jana na jeshi la polisi mkoani Geita huko Ushirombo umefanikisha kumkamata mtu mmoja (waliyekuwa wakimhisi kuwa ni jambazi) akiwa ameketi mtini huku ameshikilia bomu.

Msako huo pia umepata mabomu 3 na bunduki 7 aina ya SMG vikiwa vimewekwa kwenye tanuru la kuchomea matofali.

Jeshi hilo pia imemkamata pia mwalimu mmoja katika shule ya sekondari Ushirombo na watu wengine watatu wanaohitsiwa kushiriki katika tukio la jana.

Mjapani aweka historia katika mchezo wa tenisi

Kei Nishikori (photo: Julian Finney/Getty Image)
 Raia wa Japan, Kei Nishikori ameweka rekodi mpya katika historia ya mchezo wa tenisi kwenye US Open jijini New York nchini Marekani baada ya kumshinda mchezaji anayeshikilia nambari moja katika mchezo huo, raia wa Serbia, Novak Djokovic siku ya Jumamosi, Septemba 6, 2014.

Nishikori amekuwa raia wa kwanza kutoka barani Asia kufikia nusu fainali za mashindano ya mchezo huo.

Bingwa huyo wa French Open 1989 anatarajiwa kuambana na Marin Cilic wa Croatia ambaye naye alimshinda bingwa mwingine wa dunia Roger Federer katika nusu fainali nyingine.

Fainali hizo zitashindaniwa sikuya Jumatatu.

Nishikori alimshinda Djokovic kwa seti 6-4 1-6 7-6(4) 6-3.

Hata hiyo, hii ni mara ya pili kwa Nishikori kumshinda Djokovic baada ya kufanikiwa kufanya hivyo mwaka 2011. Wawili hao walishapambana mara tatu.

Dk Kigwangalla atangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania 2015

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya serikali za Mitaa na Mbunge wa jimbo la Nzega Dk. Hamisi Kigwangallah akiwasili katika hoteli ya Hyyat Kilimanjaro kwenye mkutano na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali ambapo leo ametangaza nia ya kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania unaotarajiwa kufanyika mwaka ujao. Dk. Khamis Kigwangallah ameongozana na mke wake Dk. Bayoum Awadh na watoto wake Sheila ambaye ni mkubwa Hawa na HK Junior aliyembeba.

Hotuba Aliyoitoa Dkt. Hamisi Kigwangalla, MB (Nzega), Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya TAMISEMI, kwa Waandishi wa Habari Kutangaza Nia ya Kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mwaka 2015 Kwenye Ukumbi wa Zanzibar, Hyatt Regency, The Kilimanjaro Hotel, Dar es salaam, Siku ya Tarehe 7 Septemba 2014.

Utangulizi

Ndugu viongozi mlioko hapa, wazazi wangu, wageni waalikwa, wanahabari, marafiki zangu, mke wangu na watoto wangu,

Nianze kwa kuwashukuru viongozi wa dini kwa dua za utangulizi.

Pia nitume salamu zangu za rambirambi kwa Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mara, Eng. Evarist Ndikilo na ndugu, jamaa na marafiki wa watu waliopoteza maisha kutokana na ajali mbaya ya gari iliyotokea juzi. Pia nitumie fursa hii kutuma salamu zangu za rambi rambi kwa Inspekta Mkuu wa Jeshi la polisi, IGP Ernest Mangu, ndugu wa marehemu na askari wote wa jeshi la polisi kutokana na uvamizi wa kituo cha polisi kule Bukombe. Na pia naomba nitumie fursa hii kumpa pole Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi, CUF, Maalim Seif Sharif Hamad kwa kupata ajali eneo la Misungwi, Mwanza.

Ndugu zangu mlioko hapa, ni heshima na furaha kubwa sana kwangu kupata fursa hii. Awali ya yote nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia uhai na kutukutanisha hapa siku ya leo. Pili niwashukuru nyote mliofika hapa kuja kunisikiliza. Niwashukuru zaidi waandaaji wa Mkutano huu kwa

Al-Shabab wamtangaza kiongozi mpya baada kifo cha Godane

Kundi la al-Shabab la nchini Somalia limemchagua Ahmed Umar (Ahmad Omar au Abu Ubaidah) kuwa mridhi wa Ahmed Abdi Godane (Abu Zubeyr) aliyeuawa katika mashambulizi yaliyoongozwa na Marekani siku ya Jumatatu kuamkia Jumanne ya wiki iliyopita.

Katika taarifa yake iliyonukuliwa na kituo cha habari cha Al Jazeera, kundi hilo limeapa kulipiza kisasi kwa mauaji ya mmoja wa waasisi wao likisema kuwa kifo cha mwanazuoni na kiongozi wao kinawalazimu kujitwika mabegani jukumu la malipo ambalo hawataliangusha wala kulisahau bila kujali muda wa

Salamu za Rais Mkapa kwa Rais Moi za miaka 90 ya kuzaliwa


Ninafurahi na kushukuru kwa kupata fursa hii ya kutoa salamu na pongezi zangu za dhati kwa Rais mstaafu Daniel Toroitich arap Moi wakati akitimiza umri wa miaka 90. Hakika Moi ni nembo, mtu mashuhuri na kizazi adimu cha viongozi wa Afrika.

Kwa karibu miaka minane, tulifanya kazi kwa karibu na kwa amani kama viongozi wa nchi zetu; Kenya na Tanzania, na katika muktadha wa Ukanda wa Maziwa Makuu, kukuza maendeleo na kuimarisha amani na utulivu.

Tangu mwanzo kabisa, Rais Moi alionekana akiibukia kuwa mmoja wa viongozi wakubwa wa Afrika

[video] Mugabe's tribute to Nyerere "We will do something"

Zimbabwean President Robert Mugabe showered praise on the Late Mwalimu Julius Nyerere, Tanzania's first President for his role in the the liberation struggle of Southern African States saying that little has been done to recognize Nyerere's contribution.

Watch the video below...

Kwa mara ya kwanza wanaotaka Scotland ijitenge na Uingereza waongoza kwa kura

.
 Evarist Chahali, Uskochi — Zikiwa zimebaki siku 11 tu kabla ya wakazi wa hapa Uskochi kupiga kura ya kuamua iwapo taifa hili liwe huru au liendelee kubaki katika 'Muungano wa Uingereza', kwa mara ya kwanza kabisa, kura ya maoni kuhusu 'uhuru' huo inaonyesha wanaotaka 'uhuru' huo wanaongoza kwa asilimia 51.

Japo kitakwimu, hiyo ni sawa na sare, ukweli kwamba haijawahi kutokea kwa wanaotaka uhuru kuongoza katika kura yoyote ile ya maoni unaleta uwezekano japo kidogo wa kura ya 'Ndiyo' kwa wanaotaka uhuru kufanikiwa.

Kura mpya ya maoni iliyofanywa na taasisi ya kura za maoni inayoheshimika sana hapa

Utafiti wa UNICEF unaopingana na maandiko ya Mungu


Nimesoma utafiti wa UNICEF (United Nations Children's Fund) au Mfuko wa Kimataifa wa Watoto ambalo ni shirika la Umoja wa Mataifa kwa shabaha ya kuwasaidia watoto duniani, limekuja na utafiti ulioniacha nitafakari mengi kuhusu wanangu Fariss na Fridausi. Na wewe pia kama u-mzazi tafakari kuhusu utafiti huo kisha vuta subra na hekima, durusu maandiko kwenye vitabu vitukufu.

Nianze na sehemu ya utafiti huo kabla sijagusa mafundisho ya dini na muono wa mitume kwenye dini ambazo wengi wetu tu waumini, hapa naangazia Uislamu na Ukristo ambazo ni dini kuu mbili zenye waumini
wengi hapa nchini.

Sehemu ya utafiti huo inasema “…six (6) in ten (10) children ages two to 14 are regularly beaten by parents and caregivers..” yaani watoto sita kati ya kumi wenye umri kati ya miaka 2 hadi 14 hupigwa mara kwa
mara na walezi wao na wazazi wao. Yaani watoto wa umri huo (miaka 2 hadi 14) wamekuwa wanakula mkong’oto kutoka kwa walezi (Walimu/wadada/wakaka wa kazi nk) wazazi wanapokuwa hawapo nao

Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif ahutubia Mwanza

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar na Katibu Mkuu wa CUF, Seif Sharif Hamad akiwasili mjini Mwanza, Jumamosi, Septemba 6, 2014.

Khamis Haji, MWANZA — Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amewahimiza wananchi wa mkoa wa Mwanza kujiweka tayari kukipa talaka Chama Cha Mapinduzi (CCM) na waunge mkono Umoja wa vyama unaotetea Katiba ya Wananchi (UKAWA) katika uchaguzi wa 2015 uwaletee mabadiliko ya kimaisha.

Maalim Seif ameyasema hayo alipokuwa akihutubia katika mikutano ya hadhara katika vijiji vya Ngudu na Hungumalwa Wilaya ya Kwimba, akiwa katika zaiara ya siku nne, ambapo pia amefuatana na viongozi waandamizi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wa mkoa wa Mwanza.

Maalim Seif alisema katika kipindi cha miaka 53 tangu nchi ilipopata uhuru kila siku zinavyokwenda mbele hali za maisha ya wananchi zinazidi kuwa mbaya, kutokana na nchi kukosa uongozi bora chini Chama cha