Hoteli ya Blue Pearl yafungwa

Fanicha za hoteli ya Blue Pearl viitolewa nje. (picha: The Citizen)

Huduma za hoteli ya Blue Pear ya Ubungo jijini Dar es Salaam imefungwa baada ya mmiliki kuripotiwa kushindwa kulipa fedha ya pango inayokadiriwa kufikia shilingi bilioni sita ($3,800,000).

Gazeti la The CITIZEN linaripoti kuwa juzi mchana maafisa wa kampuni ya Majembe Auction Mart walifika katika eneo la hoteli hiyo na kuanza kutoa fanicha nje kisha kuzipakia kwenye lori.

Wateja waliambiwa wahame kutoka kwenye eneo la hoteli hiyo kwa kuwa ilikuwa imefungwa na huduma kusitishwa.

Mr Seth Motto wa Majembe Auction Mart alisema kampuni yake ilipewa jukumu hilo na menejimenti ya Ubungo Plaza Ltd, ambao ni wamiliki wa jengo hilo.

Pres. Kikwete addreses The 69th UN General Assembly in New York

President Jakaya Mrisho Kikwete speaks during the "Every Woman, Every Child High Level Event" at the Trusteeship Council Chamber of the United Nations in New York. To his left is the UN Secretary General Mr. Ban ki Moon.

[audio] Chahali azungumza na Makutano Show kuhusu Uhuru wa Uskochi na somo kwa Muungano wa Tanzania

Mahojiano na Fina Mango katika kipindi cha Makutano Show kinachosikika katika kituo cha redio cha Magic FM, Dar es Salaam.

Masahihisho:

Katika mhojiano hayo nimeeleza kwa makosa kuwa Great Britain inaundwa na England yenye mji mkuu London, Wales yenye mji mkuu Cardiff, na GLASGOW yenye mji mkuu Edinburgh. Niliitaja Galsgow kimakosa badala ya Scotland.

Kadhalika, katika mahojiano hayo kuna sehemu nimesema kimakosa kwamba moja ya ugumu ulioikabili kambi ya NO ni jinsi ya kuitetea hoja ya mafuta. Nililenga kusema 'kambi ya YES na sio NO.

Naomba samahani sana kwa makosa hayo yaliyotokana na kile Waingereza wanaita 'heat of the moment.'

Evarist Chahali

Land Rover Discovery inauzwa


Landrover Discovery 2002 td5, 2500 cc, Diesel engine, Manual transmission, at 167,000 km inauzwa shilingi milioni 18/=

Tafadhali wasiliana na Chaote kupitia namba ya simu 0755 696 855 au [email protected]

SmartCodes ‘PATIKANA’ platform to help SME’s Get Online

Smart Codes Tanzania Chief Executive Officer, Edwin Bruno (L) addressing a news conference in Dar es Salaam yesterday. With him is the company’s Customer Support Manager, Emmanuel Jackson.

Smartcodes, a leading Tanzanian company in IT has launched an affordable service & platform called ‘PATIKANA’ where small business owners in Tanzania can now get online for an affordable price.

Sitting with journalists at their offices, CEO of SmartCodes, Edwin Bruno takes them through the service and explains how this innovative platform works.

Mr Bruno explains, “We see that many small businesses have been losing customers to larger competitors because they can’t be found online. Complicated procedures and minimal budgets prevent them from creating a company website. Our PATIKANA platform will now give a chance to small

Mtandao wa Wanawake na Katiba Wawapongeza Wajumbe wa Bunge la Katiba

Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanawake na Katiba Tanzania, Prof. Ruth Meena (wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Lilian Liundi na wajumbe wengine wa mtandao wa wanawake na Katiba. 

MTANDAO wa Wanawake na Katiba Tanzania umewapongeza wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba na hasa wajumbe waliokuwa mstari wa mbele kupigania masuala mbalimbali yaliyokuwa yanapendekezwa na mtandao huo juu ya uwepo wa Katiba inayopendekezwa yenye mtazamo wa kijinsia.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanawake na Katiba Tanzania, Prof. Ruth Meena akizungumza na waandishi wa habari ikiwa ni siku moja baada ya Rasimu ya Katiba inayopendekezwa kuwasilishwa kwenye Bunge Maalum la Katiba Mjini Dodoma tayari kwa zoezi la kuanza kupigiwa kura kifungu kwa kifungu na wajumbe wa bunge hilo.

Prof. Meena alisema Mtandao wa Wanawake na Katiba Tanzania haunabudi kuwapongeza wajumbe wote wa bunge maalum na hasa wale waliowaunga mkono kupaza sauti juu ya madai ambayo

Waraka wa Mlimandago akimfyatua Dialo kwa kumlipua LowasaNAIBU Waziri wa zamani wa Maji, Anthony Diallo, amesema dhana inayojengwa kwamba Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria ulifanikishwa kwa nguvu ya aliyekuwa Waziri, Edward Lowassa, ni potofu na afadhali angetajwa yeye.

Katika mazungumzo na Raia Mwema yaliyofanyika mjini Mwanza wiki hii na ambayo yatachapishwa katika gazeti dada la hili la Raia Tanzania kesho, Diallo ambaye sasa ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza, ameweka wazi kwa kila hatua kuhusu mradi huo.

Kimsingi, Diallo ameeleza kwamba mradi huo wa maji ulitokana na ahadi iliyotolewa na Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, kwa wananchi wa Kanda ya Ziwa mwaka 2000 na kama ingekuwa sifa ni bora zingeenda kwake.
“Kwanza kuna vitu viwili. Cha kwanza miradi yote inayolipiwa na kodi za wananchi ni jukumu la serikali iliyoko madarakani, sidhani anaweza kutokea mtu mmoja kudai kwamba nilifanikisha hiki.
Ukienda kwa staili hiyo ndiyo watu wanasema ile dhana ya wabunge kuwa mawaziri inaleta haya matatizo kwamba mtu anavutia kwake akiwa na nia fulani, sasa hao wanaodai kwamba walifanya hivi definitely lazima ujue kwamba wana nia fulani, wanataka kuwavutia wapiga kura kwamba wao wanawajali sana.

Sitakueleza mambo ambayo ni siri ya Baraza la Mawaziri, siwezi kuitoa, lakini moja ni kwamba mradi huo ulikuwa ahadi ya Rais Mkapa, mwaka 2000 wakati anaomba kura kipindi cha pili, alipopita Shinyanga na Kahama alisema lazima tufanye chini juu tutajenga mradi wa maji kuelekea huko kutoka Ziwa Victoria.

Sasa ngoma ilikuwa ni pesa zitapatikana wapi, mwaka 2002 tukaanza mazungumzo makali sana na nchi hizi zilizo kwenye Bonde la Nile, na bahati nzuri mimi ndiye nilihudhuria vikao vyote, mpaka tukafika mahali tukauvunja ule mkataba wa Misri na Uingereza, kwa sababu walikuwa wanatuzuia tusitumie maji ya Ziwa Victoria na hiyo mikutano yote nimehudhuria mimi, Addis Ababa. Na nimshukuru sana waziri mwingine aliyenisaidia, maana nilikuwa vocal sana, Martha Karua wa Kenya, aliyekuwa Waziri wa Maji wakati huo,”

alisema Diallo.

Kauli hii ya Diallo ni ya kwanza kutamkwa hadharani kuhusiana na mradi huo ambao mara nyingi

Vipeperushi vyenye vitisho vyasambazwa Dodoma

Jengo la CCM Dodoma. (picha: Lukwangule blog)
WanaCCM walifika katika jengo lao leo Alhamisi, Septemba 25, 2014, Dodoma na kukuta limeandikwa maneno kwa rangi nyekundu "NO KATIBA UFISADI " na kama hilo halitoshi kukawepo vipepersuhi vinasambazwa. (picha: Lukwangule blog)
Kaimu Katibu wa CCM Mkoa wa Dodoma, Dunga Omary akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani) moja ya ujumbe wa vitisho kwa wajumbe wa bubnge la katiba vilivyosambazwa jana Mjini Dodoma. (picha: Lukwangule blog)

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME - SACP amesema tarehe 25/09/2014 alfajiri vimeokotwa vipeperushi maeneo mbalimbali mjini Dodoma vyenye ujumbe ufuatao: ONYO – DODOMA SI MAHALI PA KUFUGA WEZI WA FEDHA ZA UMMA. UTAKAYEINGIA BUNGENI KUANZIA KESHO, YATAKAYOKUPATA UTAJUTA.

Kamanda MISIME amesema tumeendelea kupokea taarifa za watu wanaodaiwa kuandaa vipeperushi hivyo na tunafanyia kazi ili tuweze kuwakamata ili washtakiwe kulingana na kosa walilolitenda hasa la kutoa vitisho na kuhamasisha uvunjifu wa amani.

Aidha Kamanda MISIME ameongeza ametoa wito kwa wananchi na wageni wanaofika Dodoma watii sheria bila shuruti. Kila mmoja ajiepushe kujiingiza kwenye kuhamasisha uvunjifu wa amani, kujiingiza katika mikusanyiko isiyo halali na maandamano ambayo yameshapigwa marufuku na Jeshi la Polisi.

Atakayekiuka na kujiingiza katika vitendo hivyo vya kiuhalifu atashurutishwa kwa nguvu zote kwa mujibu wa sheria za Nchi na kwa mamlaka iliyopewa Jeshi la Polisi.

Kamanda MISIME ameongeza kuwa wananchi na wageni wapenda amani waendelee na shughuli zao kama kawaida kwani Jeshi la Polisi limejiimarisha ipasavyo kukabiliana na yeyote yule atakayekiuka sheria na maelekezo yaliyotolewa.

  • Taarifa ya Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi, Dodoma.

Waraka wa Jaji Joseph Warioba wa ufafanuzi kuhusu aliyoyasema Stephen Wasira

Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba ameandika waraka kumjibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Stephen Wasira kwa kauli yake kuwa ndiye aliyemkimbiza CCM kwenda upinzani mwaka 1995 (bofya hapa kurejea).

Katika waraka wa maandishi alioutuma kwa gazeti hili, Jaji Warioba alisema maelezo ya Wasira dhidi yake katika mahojiano maalumu na gazeti hili hayakuwa sahihi na hivyo akamtaka ajifunze kusema ukweli kwa kuwa mambo anayosema yanaweza kumrudia baadaye.

Waraka wenyewe
Tarehe 22 Septemba 2014, Gazeti la Mwananchi lilitoa taarifa ya mahojiano kati yake na Mheshimiwa Steven Wasira. Katika mahojiano hayo, Mheshimiwa Wasira alisema mimi ndiye niliyemkimbiza CCM.

Tangu mchakato wa Katiba Mpya kuanza nilikuwa napata taarifa kwamba Mheshimiwa Wasira alikuwa amenifanya mtaji wake katika kutetea msimamo wake. Wakati mmoja kuna kiongozi mwenzake aliniuliza kama nina ugomvi binafsi na Mheshimiwa Wasira kwa sababu kila akipata nafasi kwenye vikao vyao ananishambulia. Wakati wa mabaraza ya Katiba nilipata taarifa za aina hiyo. Nilichofanya ni kuwaarifu viongozi wake wa CCM.

Mengi aliyosema Mheshimiwa Wasira siyo ya kweli. Napenda nitoe ufafanuzi kwa machache yafuatayo:-

Viongozi wa CHADEMA Mwanza wakamatwa baada ya maandamano

Picha zote kutoka blogi ya GSengo

Vyuo vya Afya vyakabidhiwa mabasi na Wizara ya AfyaKatibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Charles Pallangyo akikagua mabasi hayo yaliyonunuliwa kwa ufadhili wa Mfuko wa Dunia mzunguko wa 9 ambayo yamekabidhiwa kwa wakuu wa vyuo 6 vya afya leo jijini Dar es Salaam.

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imekabidhi mabasi 6 kwa vyuo vya elimu ya Afya kwa lengo la kurahisisha huduma ya usafiri kwa wanafunzi na wakufunzi wanaokwenda kwenye mafunzo kwa vitendo katika maeneo mbalimbali nchini.

Vyuo vilivyokabidhiwa mabasi hayo ni Chuo Kikuu cha Hurbert Kairuki Memorial (HKMU) kilichopo jijini Dar es salaam, Chuo cha Uuuguzi Bagamoyo,Chuo cha Uuguzi Mirembe mkoani Dodoma, Chuo cha Uuguzi Tanga na Chuo cha Tabibu kilichopo mkoani Mtwara.

Akikabidhi mabasi hayo kwa wakuu wa vyuo hivyo leo jijini Dar es salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Charles Pallangyo amesema mabasi hayo yatasaidia kuondoa

UPDATE: Muuguzi atuhumiwa uzembe uliosababisha vifo vya mapacha

UPDATE/TAARIFA MPYA, Septemba 26, 2014:

Mganga mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga, Dkt Fredrick Mlekwa akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kwa niaba ya mganga mkuu wa mkoa wa Dkt Ntuli Kapologwe kuhusu tuhuma hizi amesema wamebaini kuwa mimba ilikuwa na miezi 6 na ilikuwa imeharibika. 

Pia amesema mama anayedaiwa kujifungua ana umri wa miaka 15 na ni mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari ya Mwasele. 

Dkt Mlekwa ameongeza kuwa watoto waliozaliwa mmoja alikuwa na uzito wa gramu 500, wa pili gramu 700 ambapo kimsingi ni vigumu kuishi.

Ameema muuguzi aliyetupiwa lawama alikuwa ameshawapa taarifa ndugu wa binti kuwa mimba imeharibika lakini hawakuelewa.

Binti aliyejifungua amekiri kujifungua watoto wadogo sana tofauti na watoto wengine wanaozaliwa. Amesema alijifungua mtoto wa kwanza mdogo sana akiwa amekufa na wa pili akiwa hai lakini alifariki baadaye.
Huko mkoani Shinyanga nje ya wodi namba 8 ya wazazi, jioni ya siku ya Alhamisi, Septemba 25, 2014 inaripotiwa kuwa muuguzi mmoja anatuhumiwa kusababisha vifo vya watoto wawili mapacha kutokana na kutumia muda mwingi kwenye simu.

Imedaiwa kuwa mama mjamzito alifikishwa hospitalini hapo kwa ajili ya kujifungua lakini muuguzi aliyekuwepo hakukumjali wala kumpatia huduma yoyote, wachilia mbali kuombwa na ndugu wa mama mjamzito huyo kwa kuwa tayari mjamzito alikuwa ameanza kusukuma.

Bi Mwanaisha Juma mkazi wa Mshikamano mjini Shinyanga, Mama mzazi wa mjamzito huyo akizungumza na waandishi wa habari alisema alimfikisha mwanaye kujifungua tangu saa 6 na nusu mchana leo na dalili za kujifungua zilikuwa zimeanza saa 7 na ilipofika saa 10 wakiwa hospitalini hapo wodi namba 8 alianza kupush, wakaomba msaada kwa wauguzi waliokuwa zamu lakini hakuna aliyejali matokeo yake watoto wakafariki dunia saa 10 u nusu.

Gari lililotumika kumtorosha mtuhumiwa aliyektti katia kiti cha nyuma akiwa amejifunika nguo

Taarifa via Malunde1 blog, bofya kuona picha zaidi.

BAWACHA yapinga Rasimu ya Katiba Mpya kutoka Bunge Maalum la Katiba

Baraza la Wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAWACHA) limekuwa la kwanza kuipinga Rasimu ya Tatu ya Katiba Mpya kutoka Bunge Maalum la Katiba iliyowasilishwa jana katika Bunge hilo.

Pia, BAWACHA imetangaza kuwa itaandamana wiki ijayo hadi Ikulu ya jijini Dar es Salaam kwa lengo la kupeleka kilio chao kwa kile walichoita kushindwa kuwapa wanawake nafasi stahiki katika rasimu hiyo.

Mwenyekiti wa BAWACHA ambaye pia ni Mbunge wa Kawe, Mhe. Halima Mdee akizungumza na wanahabari amesema kuwa kuwapa wanawake nafasi za uongozi za hamsini kwa hamsini kama rasimu hiyo ilivyoelekeza bado siyo kipaumbele cha wanawake wa Tanzania bali kuendelea kuwalaghai wanawake wa Tanzania.

Aidha amesema kuwa rasimu hiyo bado haimjali Mtanzania kwani kuna mambo mengi ambayo yameondolewa kwenye rasimu ambayo aliiwasilisha Jaji Warioba.

[video] Amazing! Russian cyclist survives in a scary car crash

Bwaya: Kushinda vikwazo vya jitihada za kumpa mwenzi wako anachostahili


KUYAELEWA mahitaji ya kihisia ya mwanamke ni suala moja, lakini kutekeleza ni jambo jingine kabisa. Yapo mambo mengi sana ambayo tunayafahamu lakini hatuyatekelezi. Tunatenda tusiyoyajua, wakati tunayoyajua inakuwa vigumu mno kuyatenda.

Mwaka mmoja kabla ya kuoa, nilipata bahati ya kupata pre-marital counselling, nasaha za maisha ya ndoa kabla ya ndoa. Namshukuru sana mzee Kisinza na mkewe mama Kisinza kwa muda mwingi walioutumia kunipa elimu muhimu ya mahusiano. Kadhalika wenzi wengine niliobahatika kukutana nao miaka hiyo na kuchota mengi ya kuniandaa. Baade nilioa. Miaka kadhaa imepita sasa.

Ingawa niliingia kwenye ndoa nikifahamu mengi yaliyonipasa kuyafanya  katika mahusiano shauri ya

Alitarajiwa kufa ndani ya saa 24, ni miaka 37 sasa...

Anasema wazazi wake waliambiwa mtoto wao asingeishi zaidi ya saa 24 tokea alipozaliwa, lakini sasa ana umri wa miaka 37 na anasema anaishi bila maumivu yoyote.

Tizama video iliyopachikwa hapo chini...

Internet Top Ten Languages in 2013
Internet Top Ten Languages

Continuing with the new statistics and information from the Internet World Stats, today we report about the top 10 languages in the web. This is original and exclusive research of interest to everyone involved with the globalized world we live in today.

Originally the official languages used at the United Nations (UN) were English and French. Later, Arabic, Chinese, Russian and Spanish were added. At present, these six languages are the official working languages at the United Nations for the General Assembly, the Economic and Social Council as well as the Security Council.

A delegate may speak in any of the six official languages, and his or her speech is interpreted

Dereva taxi, Mwandishi habari watajwa kuzuia mapinduzi ya Serikali Tanzania

SIRI ya mashujaa waliozima jaribio la kutaka kupindua Serikali ya Tanzania chini ya Mwalimu Julius Nyerere mwaka 1982, imewekwa hadharani kwamba mashujaa hao walikuwa vijana wawili; mmoja dereva wa teksi na mwingine mwandishi wa habari wa gazeti la Serikali la Daily News.

Akitoboa siri hiyo katika Maadhimisho ya Siku ya Amani Duniani, aliyekuwa Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Balozi Augustine Mahiga, alisema kama si vijana hao, huenda mapinduzi yangefanyika na yangefanikiwa, amani ya Tanzania leo isingekuwepo.

Akisimulia ilivyokuwa, Balozi Mahiga ambaye alikuwa Naibu Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa akiwa kijana wa miaka 30, alisema kuna kijana wa miaka 23 aliyekuwa dereva wa teksi (bila kumtaja jina), ambaye alipata taarifa hizo ambazo Serikali haikuwa nazo.

Baada ya kupata taarifa hizo, Balozi Mahiga alisema kijana huyo alimweleza mwandishi wa

Polisi! Mbona kwingine 'hamkomai' kama huku?

(picha kutoka mtandaoni)


Ulinzi tulioupata leo wa kuzungukwa na gari za Polisi na Polisi wenye mbwa na mabomu tukiwa ofisini (Makao Makuu) ili tu kuzuia maandamano ya amani ambayo mwisho wake yalifanywa na kundi lingine na ofisi za mkoa wa Ilala kufungwa siku nzima ya leo, ni ushahidi tosha kuwa kuuwawa na kunyofolewa viungo kwa ndugu zetu Albino ni kwa kuwa serikali haijaamua kuwalinda kwa dhati kama wanavyokomaa na CHADEMA ili wasiandamane.

Ulinzi wa leo umedhihirisha kuwa CCM wako radhi iwawatumie Polisi kuithibiti CHADEMA wasiandamane lakini wanyama kama twiga na tembo, ambao ni wakubwa kuliko mwili na uzito wa binadamu, waachwe wakiibwa kwenda Arabuni huku Polisi yenye silaha kama za leo ikiwa kimya na wao wakiwa baa wakigongeana mivinyo na mapaja ya kuku.

Mkwara na mbwembwe zilizooneshwa leo na jeshi la Polisi na bado maandamano yakafanywa

Yaliyojifichua katika mchakato wa kupata Katiba Mpya

Kisomo cha halalbadri au halbadiri kama wengi wanavyo fahamu ni kisomo cha majina wa mashujaa walioshiriki katika vita maarufu vya Badri. Lengo la kisomo hiki ni kushitaki mbele ya Mwenyezi Mungu kushitakia jambo fulani, iwe ni wizi au idhilali yoyote ile au mateso aliyoyapata au aliyofanyiwa ili ibainike na kutegemea malipo kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa alietenda haya yanayolalamikiwa. Wengi huamini kwamba ombi hilo kuwa linatakabaliwa au linakubaliwa.

Hii inatokana na hadithi maarufu katika uislamu kwamba dua ya mwenye kudhulumiwa basi hairudi na inajibiwa. Hiyo kutokana na imani hii watu kusoma halalbadri au halbadiri kumshatikia Mwenyezi Mungu. Mara nyingi hubainika na hubainishwa yule aliefanya yale maovu.

Kama inavyojulikana katika lugha ya kisasa utaratibu wa ukusanyaji maoni kuhusu kupatikana kwa Katiba mpya “Mchakato” umeibua hisia na kubainisha mambo mbali mabali na kutoa taswira halisi na ya undani na kufichua yale yaliyokuwa yamejificha ndani ya nyoyo za Wazanzibari.

Zoezi hili limewapa Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla fursa adhim ya kujiamulia mustakbali wao

Ads vs Reality: This is how the art of deception in advertising works

Maoni ya CCM na CHADEMA kuhusu kupiga kura kielektroniki

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema Mfumo wa Uandikishaji na Uhakiki wa Wapiga kura (BVR) ambao Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inataka kuutumia kwenye kuandikisha upya majina ya wapiga kura ni matumizi mabaya ya fedha za umma.

Kadhalika, kimesema ni mfumo ambao umeundwa na watu wachache ili kujitengenezea ulaji na siyo kurahisisha zoezi la upigaji kura na njia mbadala ni kushirikiana na Mamlaka ya Vitambulisho Vya Taifa (NIDA) ili kupunguza gharama za uandikishaji.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Chalinze, mkoani Pwani jana, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, alisema mfumo huo wa Biometric hautarahisisha uchaguzi kama ilivyoelezwa na tume, bali unaongeza gharama na siyo wa uhakika kwa uchaguzi.
“Mfumo huu umeshaleta matatizo katika chaguzi za nchi mbalimbali zilizowahi kuutumia ikiwamo, Kenya, Ghana na Malawi, hivyo hauwezi kusaidia kwenye uchaguzi, kinachoonekana hapa kuna ulaji na watu wachache ndio watakaofadika nao na kuongeza gharama zisizokuwa na msingi” 
Nape alisema mfumo wa BVR lazima utaleta matatizo kwenye uchaguzi mkuu ujao na itaonekana ni njama ambayo CCM wameipanga ili washinde katika chaguzi hizo hivyo ni bora kuukataa sasa kabla haujaanza kufanya kazi kwa kuwa wameshajua ni mbovu na kwamba CCM inataka