CDC, Texas Health Department confirm first Ebola case in U.S.A

The Centers for Disease Control and Prevention (CDC) confirmed today, through laboratory tests, the first case of Ebola to be diagnosed in the United States in a person who had traveled to Dallas, Texas from Liberia. The patient did not have symptoms when leaving West Africa, but developed symptoms approximately four days after arriving in the U.S. on Sept. 20.

The person fell ill on Sept. 24 and sought medical care at Texas Health Presbyterian Hospital of Dallas on Sept. 26. After developing symptoms consistent with Ebola, he was admitted to hospital on Sept. 28. Based on the person's travel history and symptoms, CDC recommended testing for Ebola. The medical facility isolated the patient and sent specimens for testing at CDC and at a

Kwanza Production audio: Mahojiano na mgombea Urais DICOTA, Dk NhigulaKaribu katika mahojiano kati ya Mubelwa Bandio wa Kwanza Production na Dr Patrick Nhighula, mgombea wa nafasi ya uRais wa DICOTA 2014. Mbali na kuielezea DICOTA yenyewe, pia ameeleza nia yake kugombea nafasi hiyo Karibu umsikilize.


Jack Zoka ateuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Canada

Jack Mugendi Zoka

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Bw. Jack Mugendi Zoka kuwa Balozi mpya wa Tanzania nchini Canada.

Bw. Zoka anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Alex Masinda, ambaye amestaafu kwa mujibu wa sheria. Kabla ya uteuzi huu, Bw. Zoka alikuwa Ofisa Mwandamizi Ofisi ya Rais Ikulu.

IMETOLEWA NA
KATIBU MKUU
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
Dar es Salaam,
Septemba 30, 2014

Kizimkazi wakiri Zanzibar bado ni kivutio kikubwa kwa Watalii

Kizimkazi imekuwa kivutio kikubwa cha Watalii kutoka sehemu mbali mbali Ulimwenguni kuja kuangalia Dolphine katika Bahari Hindi ya Zanzibar, Afrika Mashariki.

Kwao ni kivutio cha kuwatia hamasa hasa kwa kuwaona vile wanavyoshuhulika katika maeneo yao na kupata fursa ya kuwapiga picha na video.

Wavuvi wa Kizimkazi hufaidika na shughuli hiyo ya kuwapeleka Watalii kuona umashuhuri wa Dolphin wa Bahari hiyo walisema wakati nilipofanya mahojiano nao katika ziara yangu huko Zenj.Tumeshirikishwa na Abou Shatry, Chifu wa blogu ya SwahiliVilla

Rais Kikwete arejea nyumbani

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali Samuel Ndomba mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo Septemba 30, 2014 akitokea Marekani alikohudhuria Mkutano wa 69 wa Umoja wa Mataifa. (picha hii na zote zinazofuzta ni kutoka
Ikulu)

Ommy Dimpoz kutumbuiza Redd's Miss Tanzania Talent Show 2014

.


Azam yadhamini maonesho makubwa ya keki 'Azam World of Cakes Exhibition'

Mkurugenzi wa Kampuni ya Insights Productions Limited, Marion Elias (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya maonesho makubwa ya keki yanayotarajia kufanyika jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mratibu wa Matangazo na Uhusiano wa Umma wa kampuni ya SSB, Mohammed Ramadhan wazamini wa maonesho hayo na kulia ni Meneja Bidhaa za Azam, Abubakar Suleiman.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Insights Productions Limited, Marion Elias (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya maonesho makubwa ya keki yanayotarajia kufanyika jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mratibu wa Matangazo na Uhusiano wa Umma wa kampuni ya SSB, Mohammed Ramadhan wazamini wa maonesho hayo na kulia ni Meneja Bidhaa za Azam, Abubakar Suleiman.

Dar es Salaam

KAMPUNI ya Insights Productions Limited kwa udhamini wa Kampuni ya Azam Tanzania imeandaa maonesho makubwa ya keki yanayotarajia kufanyika jijini Dar es Salaam na kuwakutanisha wadau mbalimbali wa uandaaji na utayarishaji wa keki. Maonesho hayo yatajulikana kama 'Azam World of Cakes Exhibition'.

Akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kampuni ya Insights Productions Limited, Marion Elias alisema maonesho hayo yanatarajiwa kuwakutanisha wadau mbalimbali binafsi, makampuni na taasisi waandaaji wa keki nchini Tanzania ikiwa

Taswira mbalimbali toka party ya Castle Lite Just Got Paid
Mwishoni mwa wiki iliyopita katika ufukwe wa Azura ilifanyika party ya Just Got Paid iliyowakutanisha wakazi mbalimbali wa Dar es Salaam kusherehekea kuumalizia mwezi salama.

Party hiyo iliyodhaminiwa na bia ya Castle Lite na kufana ilitawaliwa na burudani ya

Mafanikio bila kutumia uchawi

Kwa nini watu huamini uchawi huleta mafanikio?


Wiki zilizopita tuliona uhusiano kati ya uchawi na mafanikio na pia kwa nini waganga wanaweza kuwasaidia wengine kuwa matajiri wakati wao ni masikini. Katika makala hizi tuliona ni jinsi gani hata wewe unaweza kutumia mbinu hizo za kisaikolojia bila hata ya kuwa mchawi na ukaweza kufikia mafanikio makubwa. Kama hukupata nafasi ya kusoma makala hizo bonyeza hizo link kuzisoma.

Leo tutajadili kwa nini watanzania wengi wanaamini uchawi unaleta mafanikio. Kwa nini tunashuhudia mauaji ya vikongwe na albino yakiendelea? Kwa nini kila siku tunaona mabango ya waganga wakijinadi kuweza kuwapatia watu utajiri na bahati? Na kwa nini kwenye jamii kila anayeonekana kuwa na mafanikio makubwa anaambiwa ni freemason?

Kuna sababu kubwa tano zinazosababisha watu wengi kuamini kwenye uchawi na ushirikina.

1. Mila na desturi.

Katika makabila mengi ya kitanzania kwa muda mrefu kumekuwa na mila ambazo watu hufanya ibada tambiko. Pia makabila mengine yana asili ya imani hizi za uchawi hivyo mtu

Differences between American and British English

Differences between American and British English

Infographic by Kaplan

Polisi aliyepata ajali atuhumiwa alikuwa akitoka kufanya ngono na mwanafunzi

TAARIFA kutoka mkoani Kilimanjaro, zinapasha kuwa askari mmoja wa jeshi la polisi katika kituo kimoja cha polisi kilichopo wilaya ya Moshi Vijijini, anatuhumiwa kumtorosha mwanafunzi wa Kidato cha Tatu wa shule ya Sekondari Okaoni na kwenda kumtumikisha kwenye kitendo cha ngono.

Tukio hilo limetokea Septemba 21 mwaka huu ambako mwanafunzi huyo alimdanganya mama yake mzazi kuwa anakwenda Umbwe Sekondari na marafiki zake na angerejea si muda mrefu.

Habari zinadai kuwa, tofauti na matarajio yake, mama mzazi wa mwanafunzi huyo

Mtanzania aripotiwa kuteswa Dubai na kutakiwa kusafirisha dawa za kulevyaUSALAMA wa Watanzania wanaopelekwa nchini Dubai falme za kiarabu kujaribu fursa za ajira upo shakani kutokana na baadhi ya waajiri nchini humo kuwafanyia vitendo visivyokuwa vya kibinadamu ikiwamo kupokwa pasi zao za kusafiria na wengine kujikuta wakiswekwa jela bila hatia.

Uchunguzi uliofanywana mtandao wa Kalulunga kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa, umebaini kuwa mbali na hilo,watanzania hao wamejikuta wakifanya kazi kwa mali kauli pasipo kulipwa mishahara yao kama ambavyo mikataba ya ajira inavyoonesha.

Mmoja wa wahanga hao ni Mwanaisha Athuman Pinde (36), Mwanaisha mzaliwa wa mkoa wa Morogoro, Novemba 25, 1978 kama pasi yake ya kusafiria inavyoonyesha.

Kwa mujibu wa nyaraka tulizonazo, Mwanaisha aliondoka Jijini Dar e s salaam, kwenda Dubai Februari 17 mwaka huu, na ndege ya shirika la ndege la Qatar yenye namba QR1350.

Uchunguzi umebaini kwamba alisafiri kwa msaada wa kampuni ya Bravo Job Centre Agency Ltd ya Jijijini Dar es salaam, inayojihusisha na kuwatafutia fursa za ajira Watanzania katika

Ahukumiwa kwa kutengeneza app ya kufumania mpenzi 'mchepukaji'

Kwa mara ya kwanza hukumu ambayo haikuwahi kutolewa awali imeandikwa katika vitabu vya historia duniani baada ya Wizara ya Sheria nchini Marekani kumtia hatiani na kumhukumu raia wa Pakistani kwa kuuza app inayotumiwa kwenye simu kufuatilia miito ya simu, maongezi, sms, kudukua jumbe fupi za maandishi kwa simu, video, eneo na njia nyingine za mawasiliano baina ya mtu na watu wengine pasina wao kufahamu.

Mpakistani huyo, Hammad Akbar (31) wa jijini Lahore, Pakistan ambaye ni mmiliki wa kampuni hio ya StealthGenie, alikamatwa jijini Los Angeles nchini Marekani siku ya Jumamosi iliyopita.

Wanaharakati wanaopinga ukatili majumbani wamehimiza maafisa kuchukua hatua zaidi kwa apps nyingine zinazofanana na hizi kwani zinaingilia uhuru binafsi wa mtu, zinatumika kunyanyasa na zinaweza kutumiwa kuingilia simu ya mtu bila ridhaa yake.

Tovuti hiyo ina ujumbe unaohamasisha wazazi kununua app hiyo ili kufuatilia nyendo za watoto wao lakini pia ina mstari unaosema, "kwa ajili ya wale wanaohisi wapenzi au wenza wao wana mahusiano ya kimapenzi na watu wengine."

Hukumu iliyotolewa na kuchapishwa kwenye tovuti ya FBI na inasomeka ifuatavyo:-

Pakistani Man Indicted for Selling StealthGenie Spyware App

U.S. Department of JusticeSeptember 29, 2014
  • Office of Public Affairs(202) 514-2007/ (202) 514-1888
WASHINGTON—A Pakistani man has been indicted in the Eastern District of Virginia for allegedly conspiring to advertise and sell StealthGenie, a spyware application (app) that could monitor calls, texts, videos and other communications on mobile phones without detection. This marks the first-ever criminal case concerning the advertisement and sale of a mobile device spyware app.
Assistant Attorney General Leslie R. Caldwell of the Justice Department’s Criminal Division, U.S. Attorney Dana J. Boente of the Eastern District of

Baada ya Dengue Fever na tishio la Ebola sasa ni Chikungunya

(image: pasteur.fr)

Zipo taarifa ambazo hazijatolewa rasmi kuhusu kuwepo kwa wagonjwa wa Chikungunya nchini.

Ugonjwa wa Chikungunya unasababishwa na virusi wa Chikungunya (CHIKV) ambao husababisha ugonjwa huu kwa binadamu na wanyama kutoka kwa mbu aina ya Aedes Eegypti kama ilivyo kwa homa ya Dengue.

Dalili za ugonjwa wa homa ya Chikungunya hazitoafutiani na zile za homa ya Dengue.

Homa ya Chikungunya humpata mtu kati ya siku 2 hadi 7 baada ya kuambukizwa kwa kudungwa na mbu ni pamoja na ikiambatana na:-

NMB yawafikia Wanakongwa: Yafungua tawi jipya Kibaigwa, Kongwa, Dodoma


Naibu Spika akisaini kitabu cha wageni
NMB leo imefungua tawi jipya katika mji maarufu wa Kibaigwa –Dodoma. Tawi hilo litakuwa na huduma zote za kibenki kama yalivyo matawi mengine ya NMB nchini kote.

Tawi la Kibaigwa limefunguliwa na Naibu spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni mbunge wa Kongwa, Mh Job Ndugai.

Kufunguliwa kwa tawi la Kibaigwa kunafuatia mahitaji ya muda mrefu ya wateja wa

Amuua Mwinjilisti aliyekuwa akimwombea

Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la AMBUMBULWISYE MWASOMOLA (35), ambaye ni Muinjilisti na mkazi wa Kijiji cha Lukasi, ameuawa kwa kupigwa kichwani na mchi wa kutwangia.

Aliyefanya mauaji hayo amefahamika kwa jina la SWALAPO MWAISANILA (56), mkazi wa Kijiji cha Lwangwa ambaye ni mgonjwa wa akili.

Tukio hilo lilitokea juzi TAREHE 27.09.2014Majira ya SAA 23:30 usiku, huko katika kijiji cha Luka, Kata ya Lwangwa, tarafa ya Busokelo, wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya.

Mauaji hayo yalitokea baada ya Muinjilisti huyo wa kanisa la Baptist kutaka kumfanyia maombi mtuhumiwa huyo kutokana na ugonjwa wa akili alio nao mtuhumiwa, ndipo mtuhumiwa alichukua mchi na kumpiga nao marehemu kichwani na kupelekea kifo chake.

Mtuhumiwa amekamatwa na Polisi.