Tanzania to ban public officials from holding private sector jobs

By Kizito Makoye

DAR ES SALAAM (Thomson Reuters Foundation) - In response to a growing outcry over corruption and abuse of office, Tanzania is working on a new law to ban elected leaders and civil servants from using their position to build business empires and enrich themselves.

The law is intended to end numerous scandals that have arisen in the absence of a clear definition of conflict of interest.

Gertrude Cyriacus, the Ethics Secretariat’s Assistant Secretary, told the Thomson Reuters Foundation the conflict of interest law would prohibit public officials from transacting private business while in office and ban them from holding positions in private companies.

It would include penalties of up to two years in prison if public servants, their families or companies strike business deals with public institutions they manage. She expects it will be enacted before the October 2015 presidential election.

“Conflict of interest is still a big challenge in our country. We hope that this law will bring a lasting solution to the problem by ensuring that leaders make decisions in the interest of the public,” Cyriacus said in an interview.

Reuters  via Yahoo! News

Kauli ya Mnyika baada ya BMK kupitisha Rasimu ya Katiba Mpya

MAHARAMIA WAMEPITISHA KATIBA HARAMU; WAMEANZISHA MGOGORO CHANYA NA MWANYA WA MABADILIKO

Dira ni kuwa na katiba bora itakayojenga Tanzania yenye demokrasia ya kweli, uhuru wa kweli na maendeleo endelevu kwa watu wake wote. Lakini uharamia katika mchakato wa katiba mpya umelipasua taifa. Mpasuko huu unaweza kuwa mgogoro hasi wenye madhara kwa wananchi au mgogoro chanya utakaoleta mabadiliko nchini.

Maharamia wanashangilia kilevi katika Bunge Maalum baada ya kukamilisha uharamia dhidi ya rasimu ya katiba ya wananchi kwa kupata theluthi mbili kwa njia za kiharamia. Katiba iliyopendekezwa kiharamia na kudharau maoni ya wananchi ni katiba haramu iliyokosa maridhiano na muafaka wa kitaifa.

Katiba haramu, katiba ya maharamia, katiba ya mafisadi, katiba ya CCM wahafidhiana na mawakala wake inapaswa kupingwa mtaani na mahakamani kwa mbinu mbalimbali.

Iwe ni kwa mikutano, migomo, maandamano, mashtaka au katika sanduku la

Bunge Maalum la Katiba laahirishwa baada ya kupitisha Rasimu ya Katiba

Wajumbe wa BMK ndani ya Bunge hilo siku ya Alhamisi, Oktoba 2, 2014 (picha: Benedict Liwenga, Dodoma)

Hatimaye Bunge Maalum la Katiba (BMK) limehitimisha kazi yake baada ya kupitisha Rasimu ya Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano inayopendekezwa Bungeni humo baada ya kuipitisha kwa idadi inayohitajika kwa Sura zote 19 na Ibara zote 289.

Akitangaza matokeo hayo, Naibu Katibu wa BMK, Dkt Thomas Kashilillah, amesema pande zote mbili za Muungano zimeridhia kwa theluthi mbili (2/3) kwa mujibu wa kanuni za upatikanaji wa Katiba hiyo.
Idadi ya Wajumbe wote wa Tanzania Bara walipaswa wawe 411, Wajumbe wote waliopiga kura walikuwa 335. Wajumbe ambao hawakupiga kura walikuwa 76. Kura za ndiyo zilikuwa kati ya kura 331 na kura 334. Kura za hapana zilikuwa ni kati ya kura 1 na kura 3. Kura ya ushindi kwa kila ibara ilipaswa iwe kura 274.

Dkt. Kashililah alisema kuwa kwa upande wa wajumbe 154 kutoka Zanzibar waliopiga kura, wajumbe zaidi 146 walipiga kura ya 'ndiyo' kuunga mkono Rasimu ya Katiba inayopendekezwa na wajumbe 7 hadi 8 wakitaa kwa kupiga kura ya 'hapana' katika baadhi ya Sura na Ibara.

Jumla ya wajumbe wote wa BMK ni 629, ambapp 419 wanatoka Tanzania bara huku 210 wakitoka Zanzibar.

Mwenyekiti wa Bunge hilo, Mhe. Samuel Sitta akasema yafuatayo:
Waheshimiwa kwa mujibu wa Kanuni ya 38, kanuni ndogo ya 8, ninao wajibu wa kuwatangazia rasmi, tulichokipitisha. Baada ya Katibu kunisaidia kusoma matokeo, mimi Samuel Sitta, Mwenyekiti wa Bunge Maalum, sasa nathibitisha leo tarehe 2.10.2014 hapa Dodoma, Bunge Maalum kwa kura zinazostahili limepitisha Rasimu ya Katiba inayopendekezwa.

Zoezi hilo la upigaji kura ambalo lilianza Septemba 29 mpaka Oktoba 2, siku matokeo yalipotangazwa, lilisusiwa na wabunge wengi wa upinzani, kwa madai kuwa baadhi ya vipengele vya awali vilivyopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyopewa kazi ya kukusanya maoni kutoka kwa mwananchi, vilikuwa vimeondolewa.

Kabla ya kupitishwa kwa rasimu hiyo, bunge hilo maalum la katiba lilikaa kama kamati kujadili mapendekezo katika Rasimu ya Katiba iliyoandaliwa na tume hiyo ya Mabadiliko ya Katiba iliyokuwa chini ya uongozi wa Jaji Joseph Warioba.

Baada ya kamati hizo za bunge hilo kutoa mapendekezo yao, kamati ya uandishi ilikuwa na jukumu la kuandika upya Ibara za Sura za Rasimu ya Katiba zilizojadiliwa na Bunge Maalum na hatimaye kutoa taarifa kwa Mwenyekiti baada ya kukamilisha kazi hiyo.

Hivyo, Kamati ya Uandishi ilikuwa na jukumu la kuhakikisha kuwa mapendekezo ya marekebisho, maboresho au mabadiliko katika Rasimu ya Katiba yanakidhi matakwa na masharti ya Kanuni za Bunge Maalum za Mwaka 2014.

Hatma ya katiba hiyo itahitimishwa kwa kura ya maoni inayotarajiwa kupigwa na wananchi.
Mhe. Sitta pia alilivunja rasmi Bunge hilo na kusema kuwa Rasimu inayopendekezwa itakabidhiwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein hapo tarehe 8 ya mwezi huu.

Ufafanuzi wa Rais wa TFF, Jamal Malinzi kuhusu taarifa za mgongano wa Kamati ya Utendaji TFF na Bodi ya Ligi Kuu

Vyombo kadhaa vya habari vimeripoti kuhusu hali ya mgongano kati ya Kamati ya Utendaji ya TFF na Bodi ya ligi Tanzania (Tanzania Premier League Board).

Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania linapenda kutoa ufafanuzi ufuatao:
  1. Bodi ya ligi imeundwa kwa mujibu wa Katiba ya TFF kifungu 40(11). Hivyo Bodi ya ligi ni zao la Mkutano Mkuu wa TFF.
  2. Katiba ya TFF imeipa mamlaka kamati ya utendaji ya TFF kutunga kanuni za uendeshaji wa Bodi ya ligi,kanuni hizi ndiyo nguzo kuu ya uendeshaji wa shughuli za Bodi ya ligi na ndizo zinaipa Bodi uhalali wake wa kuendesha shughuli zake za kila siku.
  3. Bodi ya ligi ni chombo cha TFF kama vilivyo vyombo vingine vikiwemo kamati mbali mbali za TFF. Kisheria Bodi ya ligi sio chombo huru (its not a legal entity) hivyo Bodi pamoja na mambo mengine haina mamlaka ya kuingia mikataba ya aina yoyote ya kisheria.

Tanzania mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Umoja wa Vyuo vya Usafiri wa Anga Afrika

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi , Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania, Mbwana . J. Mbwana akisalimiana na Rais wa Umoja wa Vyuo vya Usafiri wa Anga Barani Afrika(AATO) Tchagbele Sadamba wakati wa mkutano mkuu wa kwanza wa AATO unaofanyika Zanzibar kwa ajili ya kujadili mbinu za kuboresha mafunzo ya usafiri wa anga barani Afrika. Katikati ni Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti Uchumi Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Dkt. James Diu.

Tanzania itakuwa mwenyeji wa mkutano mkuu wa kwanza wa Umoja wa Vyuo vya Mafunzo ya Usafiri wa Anga Barani Afrika (AATO) utakaofanyika Zanzibar.

Mkutano huo wa siku tatu, kuanzia Oktoba 1-3, utakutanisha vyuo vya mafunzo ya usafiri wa anga, wataalamu wa sekta na taasisi nyingine zinazohusiana na masuala ya usafiri wa anga. Kauli mbiu ya Mkutano ni “Uhuishwaji na Viwango vya Mafunzo ya Usafiri wa Anga kwa Usalama wa Usafiri wa Anga Barani Afrika na Kwingineko”.

Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe atafungua mkutano huo wakati,

Waraka wa Wakereketwa kuhusu "Ubaya wa Ubalozi wetu wa Italy"

UBAYA WA UBALOZI WETU WA ITALY

Tunaomba uitangaze habari hii bila kuificha na wala usipunguze hata herufi moja!!!

Kila aliyewahi kuomba huduma toka ubalozi wetu wa Rome ana malalamiko yake. Ima atakuwa amecheleweshwa mno kupatiwa huduma hiyo au hakupatiwa kabisa.Muda mrefu tumenyamaza kimya tukitegemea kuwa hali ingebadilika, lakini kila siku zinavyokwenda mambo ndivyo yanavyozidi kuwa magumu na kuharibika hasa katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.

Kutozingatiwa matatizo yetu limekuwa ni jambo la kawaida mno kiasi cha kutufanya tujiulize mara mbili.. Sisi kweli ni raia wa Tanzania wenye haki ya kupatiwa msaada toka ubalozini kwetu?

Mara zote msaada tunaokuwa tukiuhitaji SI PESA, kiasi cha kwamba Mh. Balozi aseme kuwa nchi yetu haina uwezo wa kipesa kusaidia raia wake. Msaada tunaoomba ni KUPATIWA VYETI HUSIKA ILI NASI TUWEZE KUKAMILISHA HATI ZA UHALALI WA UKAAZI WETU.

Matatizo yetu yana sehemu tatu kuu zifuatazo:

Rais Kikwete ahutubia Kikao cha Kazi kwa Viongozi wa Mikoa, Wilaya na Halmashauri


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubuia Kikao cha Kazi kwa Viongozi wa Mikoa, Wilaya na Halmashauri katika ukumbi wa Chimwaga Chuo Kikuu cha Dodoma leo Oktoba 2, 2014.

Polisi aliyefanya ngono na mwanafunzi ashitakiwa

TAARIFA tulizozipata mchana huu kutoka mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, zinasema jeshi la polisi nchini limemkamata na kumfikisha katika mahakama ya kijeshi askari wake Pc.Godlisen anayetuhumiwa kumtumikisha katika vitendo vya ngono mwanafunzi wa kidato cha tatu wa shule ya sekondari Okaoni iliyopo wilaya ya Moshi.

Habari zinasema kuwa, askari huyo ambaye Septemba 21 mwaka huu alimfungia kwenye nyumba ya kulala wageni mjini moshi mwanafunzi huyo na baadaye wawili hao kupata ajali mbaya ya pikipiki, aliumia kwenye moja ya bega lake na hivyo kushindwa kupelekwa kwenye mahakama ya kijeshi.

Kaimu kamanda wa liposi mkoa wa Kilimanjaro, Koka Moita, pamoja na

Rais Kikwete afungua maonesho ya Kimataifa ya Utalii, S!TE


Rais Jakaa Kikwete akishirikiana na viongozi mbali mbali kukata utepe ikiwa ni ishara ya Ufunguzi wa Maonyesho ya Kimataifa ya Utalii "Swahili International Tourism Expo (SITE)" kwenye Ukumbi wa Mlimani City,Jijini Dar es Salaam leo Oktoba 2, 2014.

Finals for Dance100% now scheduled for October 4th


voda

By Staff reporter

THE finals for Dance 100% competition is now scheduled for 4th of October at Don Bosco grounds located in Oyster bay Dar es Salaam.

Sponsored by Vodacom Tanzania and coordinated by East Africa Television ltd, the finals will see five groups competing for top position.

The competition coordinator Happy Shame, said the tournament started in 19th July this year by searching for participants followed by quarter and semi finals.

She said, the five groups to compete in the finals have been working hard in their

Mnada wa hadhara wa vifaa vya UNICEF na balozi za Canada, Norway, SwedenNdovu Special Malt inakuletea Golden ExperienceJishindie safari ya watu wawili kwenda mbuga ya selous kupitia Ndovu Golden Experience. Kufahamu namna ya kushiriki bofya: http://bit.ly/1oylw95