Picha za baadhi ya vitakavyouzwa katika mnada wa vifaa vya UNICEF, balozi za Canada, Norway, SwedenTaarifa ya Polisi: Kusitisha maandamano ya BAWACHA; Usalama katika sikukuu ya Idd el Haji

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA


PRESS RELEASE
03/10/2014

KUSITISHA KUFANYA MAANDAMANO YA AMANI TAREHE 04/10/2014 BARAZA LA WANAWAKE WA CHADEMA (BAWACHA) KWENDA IKULU


Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limepokea taarifa kwa maandishi toka Baraza la Wanawake la CHADEMA (BAWACHA) yenye kusudio la kufanya maandamano ya amani kuelekea IKULU kwa nia ya kumwomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete asipokee RASIMU YA KATIBA.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum limefanya utafiti wa kina juu ya jambo hili na kugundua mambo yafuatayo:

 1. Kwa vile kusudio la kufanya maandamano ya Amani kwenda Ikulu ni kupeleka ujumbe wao wa kumwomba Mhe. Rais asipokee Rasimu ya Katiba, hawakutoa sababu za msingi za kisheria kwa nini asipokee Rasimu hiyo.
 2. Kutokana na sheria ya mabadiliko ya Katiba Sura ya 83, hakuna mtu; chombo; au taasisi yeyote yenye uwezo kisheria kuzuia mchakato wa kupatikana Katiba.
 3. Mnamo tarehe 01/10/2014 katika Sherehe za ufunguzi wa Barabaara ya Bagamoyo-Tegeta ambayo ilihudhuriwa na Mbunge wa Kawe Mh Halima Mdee ambaye pia ni Mwenyekiti BAWACHA – Taifa, alipewa fursa na Mhe. Rais aende akamwone Ikulu juu ya masuala mbali mbali yanayohusiana na Katiba au BAWACHA.  Anashauriwa atumie fursa hiyo ya kumwona Mhe. Rais kumweleza masuala ya Katiba pamoja na BAWACHA na siyo maandamano.
 4. Suala la Maandamano katika kipindi hiki cha mchakato wa kupatikana Katiba, halina nafasi na litaleta uvunjifu wa Amani kwa vile linagusa watanzania wote bila kujali itikadi zao.  Aidha, katika barua yao waliomba maandamano hayo yaanzie ofisi za CHADEMA Makao Makuu kinondoni kupitia barabara za Kinondoni, Ally Hassani Mwinyi, Sea View, Ocean Road hadi Ikulu. Maandamano ya aina hiyo yatasababisha usumbufu kutokana na msongamano wa magari na watu.
Kutokana na sababu zilizotajwa hapo juu, Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Polisi D’Salaam amezuia maandamano haya chini ya Kifungu 43 (1-6) cha sheria za Polisi na Polisi Wasaidizi sura 322 kama ilivyorekebishwa mwaka 2002.  Hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakayekiuka amri hii.

Kama hawajaridhika na maamuzi hayo wanashauriwa kukata rufaa kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi chini ya Kifungu 34 (6) cha sheria niliyotaja hapo juu.

POLISI WAIMARISHA USALAMA WAKATI WA SIKUKUU YA IDD EL HAJI - 2014.


Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limeweka mikakati ya mpango kazi kama ifuatavyo:-

 • Limepanga kushirikiana na vyombo mbalimbali vya ulinzi na usalama ikiwa ni pamoja na Kikosi cha Zimamoto na uokoaji, Kampuni binafsi za ulinzi, Vikosi vya uokoaji wakati wa majanga, na vikundi vya Ulinzi Shirikishi ili kuhakikisha kuna udhibiti wa matukio ya uhalifu au fujo zinazoweza kujitokeza.
 • Tumejipanga kutumia Kikosi cha FFU kikijumuisha askari na magari ya washawasha, Askari wa Mbwa na Farasi. Kikosi cha Polisi Wanamaji nacho kitakuwepo. Pia Vikosi vya Kuzuia Dawa za Kulevya, askari wa kawaida (GD), askari wa Usalama Barabarani, na askari Makachero. Wote hawa wamepewa maagizo maalum ya kuchukua hatua kabla matukio ya uhalifu hayajajitokeza na sio kungoja tukio lifanyike. Kwa mantiki hiyo, dalili zozote za uvunjifu wa amani litashughulikiwa bila kuchelewa.
 • Zitakuwepo doria za Miguu na doria za pikipiki  katika barabara zote muhimu.
 • Sambamba na hatua hizo, vikosi vyote vya Polisi vikihusisha askari wa vyeo vyote vitakuwa barabarani.
 • Wananchi wanashauriwa kusherehekiea siku ya IDD EL HAJ katika ngazi ya familia au kukusanyika katika mitaa wakisherehekea kwa amani  na utulivu.
 • Aidha kutokana na sababu za kiusalama na matishio mbalimbali katika ukanda wa Afrika ya Mashariki, Jeshi la Polisi limepiga marufuku disko toto katika kumbi mbalimbali kutokana na sifa za kumbi hizo kutokidhi viwango vya kiusalama.
 • Wananchi wanapoona dalili zozote au maandalizi ya uvunjifu wa amani watoe taarifa mapema iwezekanavyo katika vituo vya Polisi vya karibu ili hatua zichukuliwe kwa haraka.
 • Aidha, madereva wanatakiwa kuzingatia sheria za usalama barabarani ikiwa ni pamoja na kutoendesha vyombo vya moto kwa mwendo kasi, kutoendesha vyombo hivyo wakiwa wamelewa, magari au pikipiki zenye sauti kali/zenye kuleta mshtuko nazo ni marufuku.
 • Aidha, Kikosi cha Polisi Wanamaji (Marine Police) kitafanya doria kwenye fukwe za Bahari na maeneo yote ya Bahari jijini Dar es Salaam. 
 • Polisi watatoa ulinzi katika fukwe za bahari, kwa kuweka vituo vya Polisi vya muda vinavyohamishika (Mobile Police Station) ili kutoa msaada wa haraka pindi unapohitajika. Pia askari wa kutosha watakuwepo kuhakikisha wananchi wanasherehekea kwa amani.  
 • Aidha, kwa urahisi wa mawasiliano wananchi wasisite kutoa taarifa za uhalifu kwa namba muhimu za simu zifuatazo:
 1. RPC ILALA: MARY NZUKI – SACP           0715 009 980
 2. RPC TEMEKE: KIHENYA – SACP                       0715 009 979
 3. RPC K’NDONI:CAMILLIUS WAMBURA – ACP  0715 009 976
 4. AMIR KONJA - ACP  0764 168 772 (Mkuu wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Kanda Maalum Dar es Salaam).


ZINGATIA: “Utii wa Sheria bila Shuruti”

“NAWATAKIA NYOTE HERI YA IDD EL HAJ - 2014”.

S. H. KOVA
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM

Mtizamo wa Wananchi Ruvuma kuhusu Rasimu ya Katiba inayopendekezwa

SIKU moja baada ya rasimu ya pili ya katiba kupitishwa na wajumbe wa bunge maalumu la katiba baadhi ya wananchi wa mjini Songea mkoani Ruvuma wameipokea kwa hisia na kauli tofauti tofauti huku baadhi wakishangawzwa na kitendo cha wajumbe wa bunge hilo kuipokea kwa nderemo na vifijo kwenye ukumbi huo wa bunge maalumu.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti mjini Songea wamesema kitendo hicho kimeshawashangaza baadhi kwa sababu kinaashiria kuwa kilichokuwa kinatafutwa si muafaka wa kitaifa wa kuandikwa katiba bali ilikuwa ni kutafuta mshindi katika mchakato huo na kinaweza kuamsha hisia hasi kwa baadhi ya wananchi ambao hawaelewi na wanahitaji kueleweshwa zaidi kuhusiana na mchakato huo wa kuandikwa kwa Katiba.

Wakizungumza Wilfred Ngonyani na Hamza Hamis wamesema kitendo hicho hata kama hakikuwa na mrengo wowote zaidi ya kushangilia kuikamilisha kazi hiyo nyeti salama lakini

Matokeo ya Kura za Bunge Maalum kuhusu Rasimu ya Katiba

Unsafe Abortion in Tanzania: A Review of the Evidence

What needs to be done to achieve Millennium Development Goal 5 of reducing maternal mortality and ensuring universal access to reproductive health care by 2015?

This In Brief from the Guttmacher Institute argues that abortion-related deaths and unwanted pregnancies must be prevented by improving access to contraception, scaling up post-abortion care services and making safe abortion services available. It provides an overview of facts and figures around induced abortion in Tanzania and highlights key actions for government and programme planners.

Eastern Africa has the highest regional unsafe abortion rate in Africa - 2.4 million unsafe induced abortions in 2008. Unsafe abortions are one of the leading causes of maternal deaths in Tanzania. 

Action needs to be taken in order to reduce the unmet need for contraception, ensuring family planning becomes more accessible. Health care workers need to be sensitised and trained to be able to provide safe abortion services within legally permitted circumstances. 

More research needs to be conducted, strengthening the evidence base for policymakers to get a better understanding of the extent of the problem of unsafe abortions in Tanzania.

Mkutano wa maafisa mipango wafunguliwa rasmi

Picha ya pamoja wakati wa mkutano wa mwaka wa wachumi namaafisa mipango unaofanyika jijini Dar es Salaam.

Mkutano wa kitaalamu ambao unawakutanisha wataalamu mbalimbali kutoka tasnia za mipango, uchumi, takwimu na maendeleo, wenye wajibu wa kusimamia uchumi na mipango umefunguliwa rasmi na kuwakutanisha kwa pamoja wakurugenzi wa sera na mipango, maafisa mipango kutoka kwenye wizara, Serikali za Mitaa, idara na wakala wa Serikali, pamoja na taasisi za kitaaluma na watafiti wanaojishughulisha na masuala ya maendeleo na uchumi.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, Balozi (Mstaafu) Dkt. Lumbanga alisema kuwa wachumi na maafisa mipango wana wajibu mkubwa katika kuishauri

Rais Kikwete amteua Shelukindo kuwa Balozi na Msaidizi wa Rais

Samwel William Shelukindo
Samwel William Shelukindo

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Bwana Samwel William Shelukindo kuwa Balozi na pia kuwa Msaidizi wa Rais (Diplomasia).

Kabla ya uteuzi huu, Bwana Samwel William Shelukindo alikuwa Mkuu wa Utawala kwenye Ubalozi wa Tanzania Mjini Addis Ababa Ethiopia.

Uteuzi huu unaanza tarehe 01 Oktoba, 2014.

“Mwisho”

Imetolewa na;
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu – Dar es Salaam. 02 Oktoba, 2014

[video] Chereko za Bungeni baada ya kutangazwa matokeo ya kura za Rasimu ya Katiba inayopendekezwa


Vodacom yaendeleza kampeni ya "Wait to Send" ya Wiki ya Usalama Barabarani

Mkuu wa Idara ya Mazingira, Afya na Usalama wa Vodacom Tanzania, Karen Lwakatare akielezea umuhimu wa ziara maalum ya maofisa wa polisi wa usalama barabarani ya ukaguzi wa magari makao makuu ya Vodacom Tanzania yaliyopo Mlimani City jijini Dar es Salaam jana ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani.

Rasimu ya Katiba Mpya "Kura zimechakachuliwa"

Habari kutoka kwa baadhi ya wajumbe wa CCM, zilisema kuwa akidi inayotakiwa kutoka Zanzibar kupitisha Katiba inayopendekezwa, ilikwama lakini ilibidi kura zichakachuliwe kukidhi matakwa ya kisheria.
 
Mchanganuo wa kura halisi uko hivi; Wabunge wote wa Bunge Maalum la Katiba, wako 629 kati yao 419 wanatoka Tanganyika na 210 wanatoka Zanzibar.
 
Wajumbe wanaotoka Zanzibar wako 210 na theluthi mbili yao ni 140. Wajumbe wa UKAWA kutoka Zanzibar waliotoka bungeni, wako 67 na wajumbe kutoka Zanzibar waliopiga kura ya hapana wako wanane.
 
Na ili kuinyima Rasimu ya Katiba iliyopendekezwa isipite, kura 71 ambayo ni

Work and Live in the USA! 2016 Diversity Visa program is now open

October 3, 2014 – The U.S. Embassy in Dar es Salaam announces the opening of the 2016 Diversity Visa program (DV-2016). We invite interested and qualified Tanzanians to apply for this immigration program before November 3, 2014.
 
Please review the full instructions at the Department of State Consular Affairs' website, dvlottery.state.gov. The entry submission period for DV-2016 is open now through 12 p.m. EDT on November 3, 2014. You can only submit one entry during this time period and only online. Entries will NOT be accepted through the mail or via courier.
 
Please note the following important information:
 • There is no fee to submit the online application. Please do not send, pay, or transfer money to any organization or person who offers to assist you or increase your chance of winning the lottery.
 • If you win the lottery, you pay for the visa application only at the U.S. Embassy in

Treni ya Uwanja wa Ndege kuanza ndani ya miezi 3


KATIBU Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Dk Shaaban Mwinjaka, amesema serikali inatarajia kuanzisha usafiri wa treni kutoka katikati ya jiji hadi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere (JKNIA), ndani ya miezi mitatu kuanzia sasa

Dk Mwinjaka aliitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam wakati alipokua akinadi vivutio mbalimbali vya uwekezaji kwa Wawekezaji kutoka nchini Marekani, ambapo wamo wanaohusiana na sekta ya usafiri wa reli.

Alisema kuanzishwa kwa usafiri huo kutasaidia kupunguza hali ya usafiri tata wa kutoka katikati ya jiji hadi uwamja wa ndege na Gongo la Mboto, ambapo majadiliano ya kuanzisha usafiri huo, yako katika hatua za mwisho kati ya wanasheria wa wizara na wale muwekezaji kutoka Marekani.

“Wakezaji hawa wapatao 12 waliokuja ni matunda ya ziara ya Rai Jakaya Kikwete aliyoifanya hivi karibuni, ambapo wako katika maeneo mbalimbali ya Bandari, Reli na yule

"Buriani UKAWA"

Nimepokea kwa furaha kifo Cha Marehemu Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), kilichotokea jana saa nne asubuhi ya Oktoba 2 mwaka huu, jijini Dar es Salaam, kutokana na maradhi ya shinikizo la Damu (BP).

Marehemu Ukawa alikumbwa na umauti Jana wakati akitaka kuingizwa Kwenye Gari akimbizwe hospitalini akatibiwe.

Kwa mujibu wa mashuhuda tukio Hilo, walisema Marehemu Huyo alikuwa ameketi kwenye Televisheni akifuatilia kikao cha Bunge Maalum la Katiba lilokuwa likiitimisha kazi yake mjini Dodoma, na ghafla Ukawa Alipomuona na kumsikia Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.Thomas Kashilila akitangaza matokeo ya kura zilizokuwa zimepigwa na wajumbe wa bunge hilo na kumsikia Dk.Kashilila akisema theluthi mbili ya Zanzibar imepatikana na kwamba Katiba iliyopendekezwa na Bunge imepitishwa kwa kupigiwa kura nyingi za ndiyo.

Ndipo marehemu Ukawa hali yake ya kiafya ikabadilika ghafla na alianza Kulalamika kuwa

Pongezi za BASATA kwa Nasib Abdul aka Diamond

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


PONGEZI KWA MSANII NASSIB ABDUL AKA DIAMOND KWA KUSHINDA TUZO YA MSANII BORA WA MWEZI WA KITUO CHA MTV BASE


Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kama msimamizi na mratibu wa sekta ya Sanaa nchini linapenda kutoa pongezi za dhati kwa Msanii wa muziki wa kizazi kipya Nassib Abdul maarufu kama Diamond kwa kushinda tuzo ya Msanii bora wa mwezi wa kituo cha televisheni cha MTV Base kinachorusha matangazo yake kutoka Afrika Kusini na kuyafikia maeneo mengi duniani.

Aidha, Baraza linampongeza msanii huyu na wenzake Peter Msechu na Vannessa Mdee kwa kuchaguliwa kushindania tuzo mbalimbali katika tuzo za “All Africa Music” (Afrima) ambapo

Paul Francis: Maoni yangu kuhusu Kura ya HAPANA kwa Rasimu ya 3 ya Katiba Mpya

Waraka wa Pili wa Mchochezi Paulo kwa Watanzania

Zingatieni mambo haya mtakapoenda kuipigia kura Rasimu ya Tatu ya Marekebisho ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1)

Na Mchochezi Paulo

NDUGU ZANGU WATANGANYIKA, naam, leo, tarehe 2 Oktoba 2014, kwa matumizi makubwa ya vyombo vya usalama vya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rasimu ya 3 ya Marekebisho ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, maarufu kama Rasimu ya Sitta, imepitishwa rasmi huko Dodoma, kwenye Bunge Maalum la Katiba (BMK), huku mwenyekiti wake, Samuel Sitta, akisema hili ni jambo kubwa la kihistoria ambalo halijawahi kutokea hapa nchini. Aliwapongeza wajumbe wa BMK walopiga kura kuipitisha rasimu hiyo, aidha, aliwapongeza pia wale wote waliochangia katika kuipitisha rasimu hiyo, wakiwamo madereva wa wajumbe, wafanyakazi wa bunge, wasaidizi wa wajumbe walemavu, waandishi wa

Wajumbe wa DICOTA 2014 Convention kwenye cocktail party kufahamiana


Bw. Lunda Asmani akielezea utaratibu utakavyokuwa kwenye DICOTA 2014 Convention itakayoaanza muda si mrefu leo Ijumaa Oktoba 3, 2014, katika hafla ya Cocktail iliyofanyika Alhamisi jioni Oktoba 2, 2014 katika hoteli ya Millennium Durham North Carolina. Bw. Lunda Asmani pia

Tafadhali piga kura kuboresha maisha ya albinoShirika linalojibidisha na kutetea na kulinda watu wenye ulemavu wa ngozi nchini Under the Same Sun, (UTSS) limeteuliwa kushindania Tuzo ya Haki za Binadamu ijulikanayo kama "Tulip" itolewayo nchini Uholanzi. Iwapo UTSS watashinda tuzo hiyo, ni dhahiri kwamba kutakuwa na mapinduzi makubwa katika uboreshaji wa maisha ya watu wenye ulemavu wa ngozi. Shiriki kwa kupiga kura ili UTSS washinde Tuzo hii na kulinda ndugu zetu wenye Ulemavu wa Ngozi Tanzania kwa kupiga kura hapa chini na kusambambaza tarifa hizi kwa taasisi na watu mbalimbali.

Kwa kupiga kura hiyo bofya hapa (humanrightstulip.nl)

Rhapsody's @ Viva Tower, The only place to be this Saturday

rhapsody finalRhapsody's @ Viva Tower, The only place to be this Saturday

Usiku wa Wakali, Dar LIVE siku ya Idd el Haji

.

DICOTA 2014 Convention, Durham, North Carolina


Wadau mbalimbali wakiwasili kwenye hotel ya Millennium Durham tayari kwenye DICOTA 2014 utaonza rasmi Ijumaa Oct 3, 2014 kwenye mji wa Durham jimbo la North Carolina mkutano utamalizika siku ya Jumapili Oct 5, 2014 kwenye picha kushoto ni mpiga picha za kiwango na maarufu kutoka DMV Bi Iska