Tanzia: Katibu Mkuu CPA

Dk William Shija
Dk William Shija

KATIBU Mkuu wa Umoja wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola (CPA), Dk William Shija amefariki dunia jijini London, Uingereza.

Dk Thomas Kashililah ambaye ni Katibu wa Bunge, amethibitisha juu ya kifo hicho. Hata hivyo alisema ofisi yake ilikuwa haijapata taarifa kamili juu ya chanzo cha kifo.

Kifo chake kimetokea wakati mkutano Mkuu wa 60 wa CPA ukiwa umeanza,

Mhe. Mahiza afungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Tume ya Mipango

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Bi. Mwantumu Mahiza akizungumza katika ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango katika Ukumbi  wa Hoteli ya JD Complex – Kibaha, Pwani mwishoni mwa Septemba.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Bi. Mwantumu Mahiza akizungumza katika ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango katika Ukumbi
wa Hoteli ya JD Complex – Kibaha, Pwani mwishoni mwa Septemba.

MKUTANO WA BARAZA LA WAFANYAKAZI WA OFISI YA RAIS, TUME YA MIPANGO KATIKA UKUMBI WA HOTELI YA JD COMPLEX – KIBAHA, PWANI.

HOTUBA YA MKUU WA MKOA WA PWANI MH. MWANTUMU BAKARI MAHIZA KATIKA UFUNGUZI WA MKUTANO WA BARAZA LA WAFANYAKAZI WA OFISI YA RAIS, TUME YA MIPANGO KATIKA UKUMBI WA HOTELI YA JD COMPLEX – KIBAHA, PWANI.


Ndugu Mwenyekiti

Mwakilishi wa TUGHE Taifa

Mwakilishi TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam

Mwenyekiti wa TUGHE ORTM

Ndugu Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi

Mabibi na Mabwana

Awali ya yote napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia kuwepo hapa leo hii tukiwa na afya njema. Pia, nikushukuru wewe binafsi Kaimu Katibu Mtendaji, pamoja na timu yako kwa kunipa heshima hii kubwa ya kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.

Ndugu washiriki,

Nimearifiwa kuwa Baraza hili ni la kwanza katika mwaka 2014/15 na limewakilishwa na Wakuu wote wa Klasta, Idara na Vitengo, wajumbe wa TUGHE Taifa, TUGHE Mkoa – Dar es Salaam, Halmashauri ya Tawi la TUGHE Tume ya Mipango na mjumbe mmoja mmoja kutoka kila Klasta, Idara na Vitengo.

Picha za sikukuu ya Eid al-Adhwa-Haa 2014 Ughaibuni

Nchini Uingereza: Waumini wa wakiwa katika Sala sala ya Eid Al Hajj, iliosaliwa Siku ya Jumamosi, Oktoba 4, 2014,  Coventry nchini Uingereza.


Waumini wa dini ya Kiislam hapa nchini Marekani na baadhi ya nchi za ulaya na uwarabuni leo wameungana pamoja kusali sala ya Eid baada ya kukamilika ibada ya Hija huko Mecca nchini Saudi Arabia.Waumini wa Jumaiya ya Kiislamu, Tanzanian Muslim Community Washington DC wakipata picha ya pamoja baada ya kumaliza sala ya Eid Al-Adhw-haa, iliosaliwa mapema asubuhi ya saa moja na nusu ya siku ya Jumamosi Oktoba 4, 2014 Msikiti wa Islamic Center New Hampshire Maryland USA.

Baadhi ya kina Dada wa Tanzanian Muslim Community Washington DC wakipata picha ya pamoja mara tu baada ya kumaliza sala ya Eid Al Hajj, iliosaliwa siku ya Jumamosi, Oktoba 4, 2014 katika Msikiti wa Islamic Center uliopo New Hampshire Maryland nchini Marekani.Waumini Watanzania nchini India wakipata picha ya pamoja mara tu baada ya kumaliza sala ya Eid Al Hajj, iliosaliwa siku ya Jumamosi, Oktoba 4, 2014Dj Moody akipata picha ya pamoja na Hudhaifa Shatry pamoja na Cheif wa Swahilivilla blog mara tu baada ya kusali sala ya Eid Al-Adhw-haa iliosaliwa Siku ya Jumamosi Oktoba 4, 2014 Msikiti wa Islamic Center New Hampshire Maryland U.S.A.

Muazilishi wa Hilmy Disability Charity Organisation Faria Zam a.k.a (Ferry Butcher) akipata picha ya pamoja na Waumini wa Coventy Way Hansloe, nchini Uingereza mara tu baada ya kumaliza kusali Sala ya Eid Al Hajj.

Picha zote tumeshirikishwa na Abou Shatry/swahilivilla.blogspot.com

DICOTA 2014 Convention Gala Dinner; Vyeti vyatolewaWaliowezesha DICOTA 2014 Convention kupata mafanikio kuanzia uongozi wa juu wa DICOTA mpaka kamati ya maandalizi wakaazi wa North Carolina wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, Katibu Mkuu Wizara ya

Kulikoni? Kuuawa Wahadhiri wa Vyuo Vikuu Tanzania

Mauaji ya Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Athuman Livigha, aliyeuawa kwa kupigwa risasi na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi nyumbani kwake, Bunju B-Kitunda, Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam yamegubikwa na utata.

Utata huo unatokana na maelezo yaliyotolewa na watoto wa marehemu, baba mdogo pamoja na mfanyakazi wake kutofautiana kuhusiana na namna alivyouawa.  Mtoto wa kwanza wa marehemu, Said Athuman, baba yake aliuawa na watu hao usiku wa kuamkia juzi saa 3 usiku wakati anatoka ndani mwake na kwenda kuchukua vinywaji alivyokuwa ameviacha kibarazani.  Said alisema wakati anatoka ndani, watu hao walikuwa nje wakimvizia bila yeye kujua.

Alisema alipofika kwenye kibaraza hicho, watu hao walimpiga risasi moja mgongoni iliyotokea kifuani.Kwa mujibu wa Said, baada ya kupigwa risasi, marehemu alijikongoja na

Shukurani za "Mimi na Tanzania" kwa kuchangia matibabu ya Zuhura

Pichani ni Zuhura Matata mgonjwa mwenye uhitaji wa upasuaji utakaofanyika nchini India.
Kipindi cha “Mimi na Tanzania” kinachoongozwa na mrembo aliyewahi kushika taji Miss Tanzania mwaka 1999 Hoyce Temu, kinatoa shukrani kwa watanzania wote walioguswa na kufanikisha michango ya matibabu ya Zuhura Matata mwenye tatizo la kuvimba mguu ambao unahitaji Oparesheni nchini India.

Kupitia Akaunti yake ya mtandao wa kijamii Facebook muongozaji wa kipindi

Halima Mdee akamatwa na Polisi walipowatawanya BAWACHA

Mdee akiongoza maandamano kabla ya kukamatwa kwake na kupelekwa katika kituo cha Polisi cha Oyster Bay leo.

Jeshi la polisi katika Kanda maalum ya Dar es Salaam limetumia maji ya kuwasha kuwatawanya wafuasi wa Baraza la Wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAWACHA) waliokuwa wamejiandaa kuandamana hadi Ikulu.

Aidha, jeshi hilo limemkamata Mwenyekiti wa BAWACHA, Mhe. Halima Mdee aliyekuwa akiyaongoza maandamano hayo.

Jeshi la Polisi lilizuia maandamano hayo kupitia taarifa yake iliyoitoa hapo jana.

BAWACHA walipanga kuandamana hadi Ikulu ya Dar es Salaam kwa nia ya kuonana na Rais Jakaya Kikwete ili kumsishi asisaini Rasimu ya Katiba inayopendekezwa, ambayo ilipitishwa na Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba siku ya Alhamisi mkoani Dodoma.

Kaimu Kamanda wa Polisi wa Kinondoni, Simon Sirro amesema:
“Walikuja polisi jana kuomba kibali cha kufanya maandamano kwenda ikulu kwa ajili ya kumshinikiza Rais asipitishe Katiba Inayopendekezwa” 
Kamanda Sirro amesema BAWACHA walianzia maandamano yao ofisi za BAWACHA zilizopo Kinondoni wakielekea Ikulu.

Kamanda alisema Mdee alisema aliachiwa baada ya kuhojiwa na kwamba ametakiwa kuripoti polisi keshokutwa kwa mahojiano zaidi.

Polisi wakimpandisha Halima mdee kwenye gari la polisi leo

Mfuasi wa CHADEMA mikononi mwa Polisi akipelekwa katika gari la Polisi

Halima Mdee akiwa ndani ya gari la polisi pamoja na wafuasi wa CHADEMA wakipelekwa katika kituo cha polisi cha Oyster Bay. 


Halima Mdee akizozana na polisi mara baada ya kuingizwa kwenye gari


Wafuasi wa CHADEMA wakimueleza polisi madai yao wakiwa nje ya kituo cha polisi cha Oyster Bay wakidai kwenda kwa wanaohusika kutuoni hapo kwa ajili ya kumtoa mwenyekiti wao Halima MdeeWafuasi wa CHADEMA wakilalamika kwa polisi 


Ulinzi katika kituo cha polisi cha Oyster Bay ambapo hakuruhusiwa mtu yeyote kuingia 


Polisi wa Oyster Bay wakizuia gari kupitia 


Wakina Mama wa CHADEMA wakifika katika eneo la Polisi OsterbayViongozi wa CHADEMA wakiomba kuruhusiwa kupita.


  • Picha hizi ni kutoka kwenye blogu ya Habari24

[video] Jaji Warioba 26.09.2014 akizungumzia mchakato wa Katiba

TBS Invitation for Bids

INVITATION FOR BIDS

BID No. PA/044/2014/2015/NC/01 FOR PROVISION OF PRE-SHIPMENT VERIFICATION OF CONFORMITY TO STANDARDS (PVoC) SERVICES FOR USED MOTOR VEHICLES FOR TANZANIA BUREAU OF STANDARDS


Date: 3rd October, 2014.

  1. This Invitation for Bids follows the General Procurement Notice (revised) for this Project which appeared in The Guardian and Mwananchi newspapers, Issue Nos. 6118 and 5157 respectively dated 5th September, 2014 and The East African, Issue No. 1036 of 8th September 2014.
  2. The Tanzania Bureau of Standards has set aside funds for the operations of the Bureau during the financial year 2014/2015. It is intended that part of the proceeds of the funds will be used to cover eligible payment under the contract for Provision of Pre-Shipment Verification of Conformity to Standards (PVoC) Services for used motor vehicles for Tanzania Bureau of Standards. 
  3. Firms which won PVoC tender No. PA/044/2013/2014/NC/05 for