Maneno ya bango hili la Walimu ndiyo yalisababisha Polisi walirukie

(picha: Gazeti la Mwananchi)

Maandamano ya walimu kuingia katika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba kuadhimisha Siku ya Walimu Duniani, juzi yalipata mtafaruku baada ya polisi kuyaingilia na kuchana bango mojawapo lililohoji posho za wajumbe wa Bunge la Katiba.

Bango hilo la kitambaa cheupe lilikuwa na maandishi yanayohoji posho ya Sh300,000 (Sh230,000 kama posho ya kujikimu na Sh70,000 ambazo ni posho ya vikao) waliyokuwa wanapata wajumbe wa Bunge la Katiba, yakilinganishwa na kazi kubwa wanayofanya walimu.

Ujumbe wenyewe ulisomeka hivi: “Haki iko wapi? Usawa uko wapi? Posho ya Mjumbe Bunge la Katiba Tsh 300,000/= mshahara wa Mwalimu Tsh 370,000/= kwa mwezi. No big results without big salary”.

Hata hivyo bango hilo lilichanwa hatua chache kabla ya walimu hao hawajaingia uwanjani humo, ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

Mwenyekiti wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), mkoani Kagera Dauda Bilikesi, alisema amesikia habari za bango hilo kuharibiwa lakini akasema asingezungumza kwa kina kuhusu suala hilo kwa kuwa hayo yamepita.

Rais Kikwete ateua Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) nchini

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 

Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Biswalo Mganga kuwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) nchini.

Taarifa iliyotolewa Ikulu, Dar es Salaam, leo, Jumatatu, Oktoba 6, 2014, na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi (KMK), Bwana Peter Ilomo imesema kuwa uteuzi huo umeanza Ijumaa iliyopita, Oktoba 3, mwaka huu, 2014.

Kabla ya uteuzi wake, Bwana Mganga alikuwa Mkurugenzi Msaidizi, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka na Wakili wa Serikali Mfawidhi.

Imetolewa na;

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.

6 Oktoba, 2014.

Mbunge aliyejeruhiwa kwa mapanga apelekwa India akipumua kwa taabu

Kiwia baada ya kutekwa na kushambuliwa Aprili Mosi 2012 usiku huko Ibanda, Kirumba
Kiwia baada ya kutekwa na kushambuliwa Aprili Mosi 2012 usiku huko Ibanda, Kirumba

Hali ya afya ya Mbunge wa Ilemela, Highness Kiwia (CHADEMA), imeelezwa kuwa mbaya kutokana na kushindwa kupumua kwa kutumia pua na badala yake anatumia mdomo kitendo ambacho ni hatari.

Taarifa hiyo imetolewa juzi na Kiongozi wa Operesheni Kanda ya Ziwa Magharibi, Tungaraza Njugu, wakati Baraza la Vijana CHADEMA (BAVICHA), wakitoa tamko juu ya Polisi kwa kushirikiana na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuhatarisha amani ya nchi.

Kiwia, alisafirishwa kwenda India usiku wa Septemba 28 mwaka huu, kwa ajili ya uchunguzi zaidi na matibabu ya afya yake kutokana na matatizo ya kichwa. Alikumbwa na tatizo hilo baada ya kushambuliwa kwa mapanga na watu wanaosadikika kuwa ni wafuasi wa CCM katika uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Kirumba.

Katika tukio hilo, Kiwia akiwa na mwenzake Mbunge wa Ukerewe, Salvatori Machemli (CHADEMA), inadaiwa walitekwa na kushambuliwa na wafuasi wa CCM Aprili Mosi 2012 usiku eneo la Ibanda Kirumba.

“Kutokana na nafasi aliyonayo ya ubunge, Serikali inagharamia jukumu hilo na kama chama, kimechangia kufanikisha anapata matibabu na gharama za huko ni zaidi ya dola elfu nane ambazo zitatumika,” alisema.

SAX-Tanzania to launch First Flights in time for Christmas 2014

(image: ultimatetraffic.flight1.net)

Fly-SAX, Kenya’s premier safari and private charter airline, is pleased to announce that its fully-owned subsidiary, SAX-Tanzania, the new airline established in Tanzania, is making final preparations to commence flights in time for Christmas this year, subject to receiving regulatory approvals from the Tanzania Civil Aviation Authority.

“Since we announced our plans to launch the airline earlier this year, we have been working hard to get all the regulatory approvals in place to ensure that during Christmas time, we have an efficient airline servicing Tanzanians as well as international tourists,” said Don Smith, CEO & Founder of Fly-SAX and Fly540 Kenya. “We are in the process of recruiting the crews, sourced locally within the country, and training them to deliver service to international standards, making sure they

Jirani bila kututaja huendi? Eti, "Forget Kilimanjaro: Mount 'naniliu' is Africa's most rewarding peak"


Habari imechapishwa Yahoo!

Why are Ebola patients in the U.S.A sent to Nebraska?

Because the hospital is home to the largest of four high-level biocontainment patient care units in the U.S.A.

"It was designed to provide the first line of treatment for people affected by bio terrorism or extremely infectious naturally occurring diseases," the center's website says.
"isolation unit in Nebraska is isolated from the rest of the general hospital. It runs on its own air circulation system, and the air is passed through a high-efficiency particulate air (HEPA) filter before it is vented outside of the building. That's the same kind of precautions that you would see in a biosafety level 4 lab (the highest) that works with deadly or highly contagious diseases.
"In addition, the biocontainment unit has negative air pressure, which means that air pressure inside the isolation rooms is slightly lower than that outside. Essentially, air is gently sucked into the room, so particles from inside the room can't float out when you open a door. As another line of protection, ultraviolet lights zap any viruses or bacteria in the air or on surfaces."
Gizmodo.

"staff volunteers at Nebraska Medical Center run twice yearly drills with decontamination at their hospital's 10-bed biocontainment unit. It's the country's largest, opened in 2005 with $1 million in federal and state funding. 'It's built like a concrete box,' says Angela Hewlett, the unit's associate medical director."

The three other high-level biocontainment facilities in the U.S.A. are at Rocky Mountain Laboratories (RML) in Hamilton, Mont., the National Institutes of Health in Maryland and at Emory University Hospital in Atlanta, where two infected patients were treated this summer.

Taarifa ya vikao kusikiliza Mashauri ya ukiukwaji Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma

TAARIFA

Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma inatarajia kuendesha vikao vya Baraza la Maadili kwa ajili ya kusikiliza Mashauri yanayohusu ukiukwaji wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma dhidi ya Viongozi wa Umma. Vikao hivyo vitaanza tarehe 9/10/2014 hadi 17/10/2014 katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.

Katika vikao hivyo, Baraza litapata fursa ya kusikiliza Mashauri 19 yanayohusu ukiukwaji wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na. 13 ya 1995 katika vipengele vya matumizi mabaya ya madaraka na kutotoa Tamko la Rasilimali na Madeni.

Kimsingi, Baraza hili linafanyika baada ya kukamilika kwa uchunguzi wa awali uliofanywa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa mujibu wa fungu la

Taarifa ya kuahirishwa kwa Mkutano Mkuu wa CCM-New York

.
WanaCCM,

Mkutano Mkuu wa uchaguzi uliotarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi tarehe 11/10/2-14 umeahirishwa.

Viongozi katika kamati ya Halmashauri Kuu ni 5 na kati ya hao 3 wamepitisha na kukubali kuahirishwa kwa uchaguzi na 2 bado hawajajibu.

Sababu:
  1. Wengi wa wanachama siyo hai kwani ada za wanachama hazijalipwa.
  2. Wapiga kura wengi hawana kadi.
  3. Kila muombaji uanachama ni lazima kamati iliyopo ipitishe ombi lake.
  4. Hadi asa haijajulikana tuna wanachama wangapi na hatuwezi kuweka chama hatarini.
  5. Kila mwanachama anayo haki ya kugombea, mgombea wa nafasi hawezi kujitangaza kabla ya Kamati Kuu haijaidhinisha na kueleza wanachama.
  6. Katiba izingatiwe kwa nguvu zote kuhakikisha wanachama wakereketwa na wagombea wenye maadili yanayokubalika na jamii wamepta nafasi za kugombea.
  7. Kamati Kuu ya uchaguzi ndiyo iwe na mamlaka ya kuidhinisha majina ya wagombea na kutangawa na Mwenyekiti wa kamati hiyo kwa idhini ya Mwenyekiwia wa CCM.
  8. Mwenyekiti wa CCM ndiye anayo mamlaka ya kuongoza vikao vyote vya kujadili na kuidhinisha wagombea baada ya uchunguzi wa maadili ya mgombea ndani ya Kamati ya Uchaguzi.

Hofu ya viongozi waliokubali kuahirishwa ni hizi zifuatazo:
a) Usajili holela wa wanachama unaweza kuweka maisha ya chama chetu hatarini kwa kuingiliwa na mamluki
b) Kuchambua maadili ya wagombea nafasi ndani ya chama ili tusihatarishe usalama wa chama.
c) Katiba kutupiliwa na kufanya maamuzi ya binafsi kwa faida binafsi za wagombea.

Kwa hayo machache, wengi wameamua kusitisha uchaguzi wa viongozi wa CCM - New York na vitongoji vyake.

Viongozi wa Kamati Kuu ya CCM New York ni hawa wafuatao:
Mwenyekiti: Masudi H. Maftah
Katibu: Akina Seif
Katibu Mwenezi: Peter Kiula, Isaac Kibodya na Professor Lwiza Kamazima.

Naomba WanaCCM wote wa New York na vitongoji vyake wavumilie hali iliyopo sasa hivi na Mkutano wa Viongozi utafuatiwa na Mkutano wa Wanachama ili kujadili mustakabali wa Chama na uchaguzi wa viongozi.

Kidumu Chama Cha Mapinduzi.

UONGOZI CCM/ NEW YORK

MWENYEKITI

MASUDI H. MAFTAH

Rais Kikwete aomboleza kifo cha Jenerali Kimario

Muhidin Kimario
Muhidin Kimario

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mheshimiwa Dkt. Hussein Mwinyi, kuomboleza kifo cha Meja Jenerali Muhidin Kimario, Waziri Mwandamizi wa Zamani wa Serikali na Jenerali Mstaafu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (TPDF).

Aidha, Rais Kikwete amewatumia pole nyingi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF), Jenerali Davis Mwamunyange na familia ya Meja Jenerali Kimario kufuatia kifo hicho kilichotokea mchana wa leo, Jumatatu, Oktoba 6, 2014, nchini India, ambako alikuwa anapata matibabu.

Amesema Rais Kikwete katika salamu hizo kwa Waziri Mwinyi: “Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Meja Jenerali Muhidin Kimario, ambaye

Mkenge tena? Serikali na "Mwekezaji" Dk Robert Shumake wa Kampuni ya Ms Shimoja

Yafuatayo ni baadhi ya majibu ambayo bado yamejaa maswali kuhusiana na anayeidaiwa kuwa mwekezaji wa "Treni ya Uwanja wa Ndege" nchini Tanzania, mradi ambao tayari umeshatiliwa saini.

Maswali ya baadhi ya watu wanaojadili suala hili yanauliza ikiwa hii ilikuwa ni bahati mbaya ama ni makusudi kama ilivyofanyika mikataba mingine mibovu na kuigharimu Serikali na Taifa fedha nyingi.

Fuatana na Evarist Chahali katika chapisho hili akitafuta majibu kwa maswali ya mambo 'yale yale' kama vile watu hufanya kwanza ndipo wakafikiri baadaye kana kwamba viongozi wetu wamekuwa ni "sikio la kufa, dawa halisikii."
Rasi Jakaya Kikwete akipokea zawadi ya saa kutoka kwa Robert Shumake, ambaye pia ni mkurugenzi wa kampuni ya M/S Shumoja inayotajwa kuwa itawekeza katika mradi wa usafiri wa treni ya kisasa Dar

Hebu soma kwanza habari ifuatayo kisha tujadili 'sintofahamu' kuhusu mwekezaji wa mradi huo
SERIKALI imetia saini mkataba wa uwekezaji wa pamoja kati yake na kampuni ya Marekani kwa ajili ya kuanza mradi wa usafiri wa treni ya kisasa itakayoanzia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Julius Nyerere (JNIA) hadi katikati ya Jiji la Dar es Salaam.
Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe amesisitiza ni lazima kufanya haraka kwani mwekezaji, Kampuni ya Ms Shimoja ya Marekani, iko

Rais Kikwete awajulia hali Wakuu wa Mikoa na Mjumbe wa BMK waliolazwa MuhimbiliRais Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe Leonidas Gama aliyelazwa kwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam, leo.

Mbunge Dkt Ndugulile afungua Fursat Dhahabiyya, Mji Mwema KigamboniMbunge we jimbo la Kigamboni Dkt Faustine Ndugulile akifungua rasmi (wa pili kulia) kiota kipya Mji Mwema Kigamboni kinachoitwa Fursat Dhahabiyya.

Rais Kikwete akutana na Menejimenti ya NBCRais Jakaya Kikwete (kulia) akizungumza na Mtendaji Mkuu wa Menejimenti ya Barclays Africa, Bi. Mizinga Melu (wa tatu kushoto) alipokwenda kumuaga Ikulu, Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano, Bi Rukia Mtingwa na

Katibu Mkuu Kiongozi ajipatia nakala ya kitabu cha "Nyayo za Obama"Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akipokea nakala ya Kiswahili na Kiingeraza ya kitabu cha nyayo za Obama kutoka mwandishi wa kitabu hicho Mzee Safari Ohumay kwenye siku ya Jumamosi Oktoba 4, 2014 kwenye mkutano wa DICOTA 2014 uliofanyika Durham, North Carolina.


Vodacom yaadhimisha "Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani" kwa kishindo

Vodacom says yes to excellence

Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja wakiinua bango lenye ujumbe wa "We say yes to excellence" ikiwa ni kauli mbiu ya kampuni hiyo katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja duniani.

Unafikiri umechelewa, umekosea maishani?


Mara nyingi katika safari yoyote ya mafanikio kukutana na changamoto ni kitu ambacho kinakuwa hakikwepeki. Wengi wetu mara kwa mara tumekuwa tukikutana na changamoto za aina mbalimbali katika maisha yetu. Unapokutana na changamoto hizi usipokuwa makini na kuwa mtulivu unaweza ukakata tamaa na kuamua kuachana na malengo yako makubwa uliyojiwekea.

Wengi wanapokutana na changamoto za namna hii katika maisha yao, huwa wanajiona hawafai, wamekosea na kuona maisha hayawezekani tena kwao, pasipo kujua wao ni watu muhimu sana na wa pekee katika hii Dunia ambao wanauwezo wa kufanya kitu chochote kile bila ya kuzuiliwa na mtu.

Inawezekana kabisa katika maisha yako umekutana na changamoto nyingi ambazo zimekufanya ukate tamaa, ukose tumaini na kujiona kama vile umekosea sana na umechelewa katika

‘Kukurupuka’ kunavyorudisha nyuma wajasiriamali...!

Na: Meshack Maganga- Iringa.

Kwa muda mrefu sasa, Baadhi yetu tumekuwa tukitamani kufanya ujasirimali, na jamii yetu kwa mapana yake, tumeshaamini kwamba ujasiriamali unalipa, na mtu yeyote kwenye jamii yetu anae fanya ujasiriamali anaonekana kwamba ni mtu mwenye pesa. Hata kama ameenza jana. Tunasahau kuchunguza sababu zilizo msukuma huyo mtu kuanza ujasiriamali, tunasahau shida na changamoto alizozipitia huyo mtu katika safari yake ya ujasiriamali.

Kimsingi, ujasiriamali Tanzania umeshika kasi miaka ya 2000, hasa kutokana na juhudi za Serikali ya Tanzania kuruhusu uwekezaji na ndipo msamiati wa Ujasiriamali uliposhika kasi na kuboreshwa na sera na sheria mbalimbali za uchumi

Kutokana na hali hii, tumeshuhudia watu wengi wakijitoa kimasomaso kuanzisha biashara au kufanya shughuli mbalimbali za ujasiriamali. Niwahi kusoma makala moja siku za nyuma kwamba, David McClelland ambaye ni mwanasaikolojia kutoka chuo kikuu cha Havard nchini Marekani aligundua tabia za kisaikolojia zinazojengeka ndani ya mjasiriamali ambaye