Tanzania yaanza kuzalisha lami ya maji

Tanzania imeanza kuzalisha lami ya maji kupitia mtambo uliozinduliwa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam unaomilikiwa na kampuni ya Starpeco Limited.

Lami hiyo ambayo kwa kitaalamu inajulikana kama Bitumen emulsions inatumika katika ujenzi wa barabara na kuziba viraka vya barabara zilizoharibika.

Kwa mujibu wa wataalamu, lami hiyo ndio yenye unafuu zaidi kulinganisha na lami aina nyingine na pia rafiki kwa mazingira.

Bei ya lami hiyo itakayokuwa na jina la biashara la Colabinder itakuwa na unafuu wa asilimia 20 hadi 30 kulinganisha na gharama katika soko kwa sasa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Starpeco Limited, Mhandisi Gratian Nshekanabo, alisema kuwa upatikanaji rahisi na wa uhakika wa bidhaa hiyo utasaidia kwa kiwango kikubwa sekta ya ujenzi nchini, “Mtambo huu umefuata viwango vya kimataifa,” na kuongeza kuwa una uwezo wa kuzalisha lita 10,000 za lami hiyo kwa saa. Mtambo huo utatengeneza ajira za moja kwa moja 25 na 100 zisizo za moja kwa moja.

Alisema mtambo huo umetengenezwa Ukraine lakini vifaa vyake vingine vimetoka Italia na Ufaransa.

Halima Mdee apelekwa korokoroni Segerea


Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAWACHA) ambaye pia ni Mbunge wa Kawe, Halima Mdee akitoka katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kulekea katika Gereza la Segerea baada ya kukosa dhamana katika kesi inayoamkabili pamoja na wanachama wenzake ya kuandamana bila kibali cha polisi na hivyo kushindwa kutii amri halali ya Jeshi la Polisi la kutofanya maandamano.

Katika audio iliyopachikwa hapo chini, Mwandishi wa BBC jijini

Hotuba ya Dk Kigwangalla alipopokelewa Nzega baada ya kutangaza nia ya kuwania Urais

Kigwangalla akicheza na jeshi la sungusungu

 • Historia fupi: Mimi ni Mtemi wa kurithi kutoka kwa Babu yangu Chief Lumola Bakari Maulid, ambaye alaikuwa Mtemi wa Usaguzi, maeneo ya Mwegelezi, kule Kaliua. Mwaka 2010, mjukuu wa Mtemi Makaranga Ng'wana Ng'washi alinitawaza kuwa Mtemi wa Lusu, ambao ni utemi wake wa asili wa kurithi. Juzi tarehe 4 Oktoba nilipata heshima nyingine mbili: Mtemi wa Sungusungu wote wa wilaya ya Nzega, heshima niliyopewa na viongozi wa Sungusungu wenyewe, na nilitawazwa kuwa Mtemi wa Puge, Ibhambangulu.

Hotuba ya Dkt. Hamisi Kigwangalla, Mbunge wa Jimbo la Nzega na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya TAMISEMI alipopokelewa Jimboni Nzega baada ya kutangaza nia lugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania


Imetolewa mjini Nzega, kwenye viwanja vya parking, siku ya leo, Jumamosi tarehe 4, Oktoba, 2014.

UTANGULIZI: SAFARI YA KUAMINI/A JOURNEY OF BELIEVE!

Ndugu viongozi wa dini,

Ndugu viongozi wa kimila,

Ndugu wazee wangu mliopo hapa,

Ndugu Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya,

Ndugu Katibu wa CCM wa Wilaya,

Ndugu viongozi wa vyama rafiki mliofika hapa,

Waheshimiwa madiwani,

Wananchi wenzangu wa Nzega,

Mabibi na mabwana,

Salaam,

Awali ya yote nianze kwa kumshukuru mwenyezi mungu, mwingi wa rehema na mwenye kurehemu, kwa kutujalia afya njema na kutukutanisha hapa siku hii adhimu ya leo, maana ni kwa utashi wake tu tunaweza kuyafanya haya yote.

Nitumie fursa hii kwa namna ya kipekee kuwashukuru nyote kwa kuacha shughuli zenu kuja kunipokea na kushiriki mkutano huu. Mmenipa heshima kubwa sana na mimi nawajibika tu kusema ‘ahsanteni sana’.

Mimi hapa ni aidha mtoto wenu, mjukuu wenu ama mdogo wenu, mnapoacha shughuli zenu kuja kunisikiliza mimi, mnakuwa mmenitwisha mzigo mzito sana. Ninajiona nawajibika kwenu kutoa utumishi uliotukuka. Ninajipa deni la kuongeza bidii kubuni miradi itakayotatua shida zetu hapa Nzega, kupigana kuondoa umaskini, ujinga na maradhi.

Ulinzi wakati wa makabidhiano ya Rasimu ya Katiba inayopendekezwa

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi David Misime ameeleza kuwa kutokana na tukio la kihistoria ambalo litafanyika tarehe 08.10.2014 ambapo Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mh. Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar watakabidhiwa Rasimu ya Katiba inayopendekezwa ulinzi umeimarishwa katika maeneo yote ya Mkoa wa Dodoma hususani Dodoma Mjini.

Ufuatiliaji wa taarifa mbalimbali na kuzifanyia kazi umeimarishwa zaidi, doria za miguu, magari, pikipiki na mbwa na farasi nazo zimeimarishwa. Pia vyombo vyote vya

Taarifa ya kuondolewa zuio la mikutano ya vyama vya siasa

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI


Serikali imeondoa zuio la mikutano ya Vyama vya Siasa lililokuwa limetangazwa mwezi Mei mwaka juzi kuzuia mikutano hiyo kufanyika katika mikoa ya Lindi na Mtwara.

Zuio hilo limeondolewa leo na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mathias Chikawe.

Mikutano hiyo ilizuiliwa kutokana na vurugu za wananchi waliokuwa wakipinga ujenzi wa mradi wa bomba la gesi kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam hali iliyosababisha kuvunjika kwa amani na utulivu katika mikoa hiyo.

Katika vurugu hizo, watu kadhaa walipoteza maisha na wengine kujeruhiwa huku magari na nyumba zikichomwa moto.

Hatua hii ya sasa imechukuliwa baada ya Serikali kuridhika kuwa hali na

Majina ya Taasisi na Halmashauri zilizofungiwa kushiriki zabuni za Serikali

Mwenyekiti wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Dk. Martern Lumbanga (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kuhusu matokeo ya ukaguzi wa shughuli za ununuzi katika taasisi za umma uliofanywa na PPRA kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 30 mwaka huu. Kulia ni Mjumbe wa Bodi ya PPRA, Jaji mstaafu, Thomas Mihayo.

Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) imeikabidhi Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) majina 10 ya taasisi na halmashauri ambazo zimeonekana kuwa na viashiria vya rushwa katika matumizi ya fedha za Serikali mwaka 2013/14.

Bodi hiyo pia imezifungia kampuni 23 kushiriki zabuni za Serikali, huku ikiagiza menejimenti ya PPRA kufanya uhakiki kwa taasisi 19 ambazo katika ukaguzi, zimeonyesha kufanya ununuzi unaotia shaka wa Sh1.7 bilioni.

Mwenyekiti wa Bodi ya PPRA, Balozi Marten Lumbanga alisema jana kuwa taasisi zilizoonekana kuwa na viashiria vya rushwa katika ununuzi ni:-
 1. Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere
 2. Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam
 3. Halmashauri ya Jiji la Mwanza
 4. Halmashauri ya Kondoa
 5. Halmashauri ya Monduli
 6. Halmashauri ya Kilwa
 7. Halmashauri ya Maswa 
 8. Halmashauri za wilaya ya Kigoma

Mahujaji wetu wote wako salama

Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limesema mahujaji wote wa Tanzania waliokwenda Saudi Arabia kwa ajili ya Hijja wako salama.

Mkurugenzi wa Hijja wa BAKWATA, Yusuf Musunu amenukuliwa na gazeti la MWANANCHI akisema mahujaji wote ni wazima licha ya taarifa za vifo vya watu zaidi ya mia moja, “Naomba niwajulishe Watanzania wote kuwa, mahujaji wetu wote wako salama kwenye hijja,” alisema Musunu.

Mahujaji 130 kutoka katika nchi za Kiarabu walifariki dunia wakati wa ibada hiyo kutokana na umri mkubwa na maradhi mbalimbali.

Kiongozi wa CHADEMA akamatwa 'alivyotabiri' kwenye ujumbe wa bango

Kungu Masanja akiwa ndani ya gari la polisi 

Kungu Masanja akiwa amebeba bango lake kabla ya kukamatwa.

Wakazi wa kijiji cha Chibe kata ya Chibe katika manispaa ya Shinyanga wamepigwa butwaa baada ya mjumbe wa serikali ya kijiji hicho Kungu Masanja kukamatwa na askari polisi akiwa ameshikilia bango katika mbio za Mwenge wa Uhuru katika kijiji cha Chibe.

Kungu Masanja ambaye pia ni katibu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika kijiji cha Chibe alikutwa amebeba bango wakati kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru mwaka huu Rachel Stephen Kassanda akifungua zahanati ya kijiji hicho.

Baadhi ya maneno yaliyokuwa yanasomeka katika bango hilo ni “KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE KITAIFA. 
I. HIVI MAPATO NA MATUMIZI YA ZAHANATI YA KIJIJI HUSOMWA WAPI?

Taarifa ya kuteuliwa na kufutwa kazi Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mweneyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohammed Shein amemteua Mh. Said Hassan Said kuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa leo na Katibu wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia ni Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee, Dkt Shein amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu 55(1) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.

Mheshimiwa Said Hassan anachukua nafasi ya aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mh. Othman Masoud Othman ambaye Uteuzi wake umefutwa kwa mujibu wa Vifungu vya 53, 54 (1) na 55 (3) vya Katiba ya Zanzibar ya 1984 na Kifungu 12(3) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Namba 2 ya 2011.

Kabla ya Uteuzi huo Mheshimiwa Said Hassan Said alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Uteuzi huo umeanza tarehe 07, Oktoba, 2014

IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR 07, Oktoba, 2014

Rais Kikwete awaonya Mabalozi "majanga makubwa" kuhusu dini na siasa

Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika pich ya pamoja na washiriki wa Mkutano wa viongozi wa dini kubwa za Kikristo na Kiislam nchini kwa lengo la kujenga na kuleta amani na maelewano nchini katika hoteli ya White Sands jijini Dar es salaam. Mkutano huo wa siku nne ulioanza jana unajulikana kama Tanzania Christian & Muslim Religious Leaders’ Initiative for Peace and Co-existence.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa kuna ushahidi sasa unaothibitisha kuwa baadhi ya mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini wamekuwa wanachaganya dini na siasa wakitumia dini kuunga mkono baadhi ya vyama vya siasa na shughuli za kisiasa nchini.

Aidha, Rais Kikwete amewaomba mabalozi hao “kuiokoa” Tanzania katika majanga makubwa yanayoweza kuipata kwa kutumia dini kuendeleza siasa, hatua ambayo ameielezea kama “njia ya hatari kweli kweli.”

Tuwapeleke wanetu katika chanjo ya surua na rubella Oktoba 18-24Surua na rubella ni magonjwa hatari yanayoenezwa haraka kwa njia ya hewa, kutoka kwa mtu mwenye vimelea vya ugonjwa huo kwenda kwa mwingine.

Wataalamu wa afya wanaeleza kuwa dalili za magonjwa haya mawili zinafanana, hivyo ni vigumu kutofautisha. Wataalamu hao wanasema dalili kuu ni homa na vipele vidogovidogo.

Chanjo ya surua-rubella hutoa kinga kamili dhidi ya magonjwa haya. Dozi ya kwanza hutolewa kwa mtoto anapofikia umri wa miezi 9 na dozi ya pili akiwa na mwaka mmoja na nusu (miezi 18).

Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, imekutana na wadau wake wa masuala ya chanjo jijini Dar es Salaam jana, kuzungumzia mkakati wa kampeni za chanjo ulio na lengo la kuwafikia walengwa wengi zaidi ili kuongeza idadi ya watu wenye kinga dhidi ya magonjwa ya surua na rubella.

Endelea kusoma zaidi hapa : FATHER KIDEVU BLOG

Tamasha kubwa la Karibu Music Festival kufanyika Bagamoyo


Meneja wa tamasha la Karibu Music Festival, Richard Lupia akizungumza katika mkutano na waandishi wa Habari Dar es Salaam hii leo juu ya maandalizi ya tamasha hilo. Kushoto ni Mratibu wa Tamsha, Issam Ramadhan na Kulia ni Afisa Habari wa Karibu Music Festival, Said Hashim.
Meneja wa tamasha la Karibu Music Festival, Richard Lupia akizungumza katika mkutano na waandishi wa Habari Dar es Salaam hii leo juu ya maandalizi ya tamasha hilo. Kushoto ni Mratibu wa Tamsha, Issam Ramadhan na Kulia ni Afisa Habari wa Karibu Music Festival, Said Hashim.

Na Father Kidevu Blog -- Tamasha kubwa la Karibu International Music Festival, linataraji kufanyika nchini kwa mara ya kwanza katika Pwani ya viwanja vya Taasisi ya Sanaa Bagamoyo (TASUBA).

Waratibu wa Tamasha hilo Karibu Cultural Promotions kupitia kwa Meneja wa Onesho hilo, Richard Lupia, amesema litafanyika kwa siku tatu kuanzia Novemba 7-9 Mwaka huu wa 2014.

Lupia amesema vikundi zaidi ya 30 na wasanii zaidi ya 500 kutoka kila

Citizens overwhelmingly support integration into the East African Community

 • Large majority are in favour of single tourist visa, regional travel with ID card, joint infrastructure and free movement of labour

7 October 2014, Dar es Salaam: Eight out of ten citizens (80%) think Tanzania should remain in the East African Community (EAC). In addition, nine out of ten (85%) approve (or strongly approve) of greater integration with Kenya and Uganda in particular. Six out of ten citizens also support increased integration with Rwanda (62%) and Burundi (59%).

These findings were released by Twaweza and the Society for International Development (SID) in a research brief titled Let’s build one house! What Tanzanians think about the East African Community. The brief is based on data from Sauti za Wananchi, Africa’s first nationally representative high-frequency mobile phone survey that interviews households across

Vodacom launches ‘phone doctor’ service

Vodacom Tanzania's, Kelvin Twissa in a press conference with Doctors, Sulende Kubhoja, MD (seated on his left) and Meshack Shimwela, MD (right).


Staff reporter

THE leading cellular network company in Tanzania Vodacom has launched a new service which will allow Vodacom subscribers to access important information on health for free for 30 days.

Speaking during the service launching ceremony in Dar es Salaam, Dr.Meshack Shimwela noted that, access to health information to the public was very important in creating a disease conscious society.

With ever increasing penetration of mobile phones, Dr Shimwela said the service is expected to be of great benefit to marginalized communities which can hardly access such kind of

American Generations "Baby Boomers, Gen X, Gen Y, Millennials..." explained

(illustration image source: thindifference.com)

American Generations Timeline


GI Generation
Born 1901-1924 (Age 85+)


They were teenagers during the Great Depression and fought in World War II. Sometimes called the greatest generation (following a book by journalist Tom Brokaw) or the swing generation because of their jazz music.

Silent Generation
Born 1925-1942 (Age 67-84)


They were too young to see action in World War II and too old to participate in the fun of the Summer of Love. This label describes their conformist tendencies and belief that following the rules was a sure ticket to success.

Baby Boomers
Born 1943-1964 (Age 48-66)


The boomers were born during an economic and baby boom following World War II. These hippie kids protested against the Vietnam War and participated in the civil rights movement, all with rock 'n' roll music blaring in the background.

Generation X
Born 1965-1979 (Age 32-47)


They were originally called the baby busters because fertility rates fell after the boomers. As teenagers, they experienced the AIDs epidemic and the fall of the Berlin Wall. Sometimes called the MTV Generation, the "X" in their name refers to this generation's desire not to be defined.

Millennials
Born 1980-2000 (Age 14-34)


They experienced the rise of the Internet, Sept. 11 and the wars that followed. Sometimes called Generation Y. Because of their dependence on technology, they are said to be entitled and narcissistic.

Generation Z
Born 2001-2013 (Age 1-13)

These kids were the first born with the Internet and are suspected to be the most individualistic and technology-dependent generation. Sometimes referred to as the iGeneration.

Q: Who names generations, what do these names mean, and how do we avoid stereotyping a group of people that can span decades?

Hand writing psycholoagy: Can the way you write tell your personality?

The Psychology Of Handwriting � You Are What You Write

Watu na viroja kwenye mitandao jamii

Kapata lift kwenye gari anajipiga selfie anatuma Instagram na kusema, ‘Driving to work!’

Kwa mara ya kwanza baada ya miezi kadhaa, anaingia Kanisani, Padre aliposema tufunge macho tuombe, anapost eti, ‘Feeling Blessed.’

Pata vichekesho zaidi kwenye JohnKitime.co.tz

Mchonga nanasi stadi!

Tizama video iliyopachikwa hapo chini kufurahia ustadi wa mchonga nanasi katika kazi yake...

How to choose whether to engage in a fight or not

You've probably heard or being told to “Choose Your Battles.”

But, when is a battle not worth the aftermath? 

How and what exactly does choosing your battle really mean?

Kathleen Kelley Reardon tells us to consider the following guidelines and know it's best not to engage when:
 1. There’s a low probability of winning without doing excessive damage
 2. Upon reflection, winning isn't as important as it originally seemed 
 3. There likely will be a time down the line when you can raise the issue again with a different person or in a different way
 4. The other party's style is provocative whether speaking with you or others, so it’s not worth taking personally
 5. You could win on the immediate issue, but lose big in terms of the relationship

Wachagga na 'sale' linavyotumiwa kuficha maovu na kupalilia unyanyasaji

(image: wikimedia.org)

Imeelezwa kuwa vitendo vya ukatili wa kijinisa vitaendelea iwapo jamii haitaacha kukumbatia tamaduni potofu kama vile watu kuombana wapatane au 'mambo yaishe' kwa kutumia jani maarufu kwa kabila la Wachaggga mkoani Kilimanjaro lijulikanalo kwa jina la 'sale'.

Wananchi, Wanasheria, Dawati la Jinsia na Watoto wakitoa maoni yao kuhusu mila hiyo wamesema kutumia 'sale' kutaendeleza ukatili wa kijinsia miongoni mwa jamii.

Mwananchi mmoja amesema kwa mfano, katika Kata ya Uru Shimbwe katika vitongoji vya Temboni na Shimbwe kuna baba mmoja mnywaji wa pombe haramu ya gongo alimbaka mtoto wa miaka 6 na hakuna kesi iliyofunguliwa baada ya wahusika 'kuyamaliza' kwa

[video] Amcharaza viboko Waziri Mkuu Mstaafu wa Kenya, Raila Odinga

Moshi: Mwalimu mbaroni kwa kufanya ngono na mwanafunzi wake

Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro linamshikilia Mwalimu wa Shule ya Sekondari Muungano baada ya kukutwa wakifanya ngono na mwanafunzi wa Kidato cha Tatu wa shule hiyo.

Akitoa taarifa hiyo kwa wanahabari, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Kilimanjaro amesema tukio hilo limetokea Oktoba 3, 2014 mwendo wa saa tano adhuhuri katika mji mdogo wa Himo.

Amesema Mwalimu huyo na Mwanafunzi wake walikamatwa katika nyumba ya kufikia wageni ya Kilimanjaro Guest House katika mji huo wa Himo.

Awali, mwalimu huyo alionekana akiwa amembeba mwanafunzi wake katika pikipiki na kuelekea katika nyumba hiyo ya kulala wageni. Baada ya wazazi wa binti huyo kung'amua hilo, walifunga safari na ndipo wawili hao walipokamatwa.

Mwalimu huyo anashikiliwa katika kituo cha Polisi katika mji wa Himo akisubiri kufikishwa mahakamani punde Polisi itakapokuwa tayari ili taratibu za kisheria zifuate.

Taaria ya Rehema Goodluck, Radio Sauti ya Injili, Moshi.