Tamko la Wachungaji kuhusu mauaji ndani ya Kanisa Bukoba

TAMKO LA WAKRISTO BUKOBA KUHUSIANA NA MAUAJI PAMOJA NA UCHOMAJI MAKANISA TAREHE 11/10/2014.


Baada ya tukio la kutisha la kushambuliwa kwa washirika na hatimaye kuuawa kwa mshirika na kujeruhiwa vibaya kwa mwingine kanisani Kagemu PAG; Wachungaji na viongozi wa kiroho wa Bukoba tumepokea taarifa hizi kwa mshtuko mkubwa. Tumekutana tarehe 10 Oct 2014 na kutafakari hatima ya wakristo katika eneo hili.

Matukio rejea tuliyojikumbusha ni kama ifuatavyo:

1. Kanisa la Living water pale Buyekera mlimani limechomwa moto mara.

2. Kanisa la Hofan ministries limechomwa moto pale Rugambwa.

3. Kanisa la la International assemblies of God lilipo Magoti lilichomwa moto na kuteketea.

4. Kanisa la TAG Kihwa lilichomwa moto na kuteketea.

Mfanyakazi wa Benki afariki katika ajali ya gari dogo na basi, Hedaru


Wafanyakazi wa Benki moja hapa nchini wamekumbwa na simanzi iliyosababishwa na kifo cha mwajiriwa mwenzao kilichotokana na ajali iliyotokea jana jioni huko Hedaru, Wilayani Same mkoani Kilimanjaro iliyohusisha gari lenye namba za usajili T653 BZR na basi la Happy Nation.

Imeripotiwa kuwa watu wote wanne waliokuwemo ndani ya gari dogo walipoteza uhai papo hapo.

Picha zilizopachikwa hapo chini zinaonesha jinsi gari hilo dogo lilivyoharibika vibaya baada ya ajali.

Rais Kikwete aongoza waombolezaji kutoa heshima kwa mwili wa Dkt ShijaRais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa Marehemu Dkt William Shija alipoongoza shughuli za kuaga leo Jumapili Oktoba 12, 2014 katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

Picha hii na zote zinazofuata ni kutoka IKULU.

Kampuni ya VIP yaomba CAG, TAKUKURU zitoe taarifa dhidi ya madai ya Kafulila kuhusu akaunti ya Escrow ya BoT

Mwanasheria maarufu kutoka Amterdam Holand, Dk. Camilo Schutte (kushoto), akitoa ufafanuzi wa kisheria kuhusu jambo hilo. Kulia ni Mmoja wa wakurugenzi wa kampuni ya VIP na Mabibo Beer Wines and Spirits Limited, Joe Mgaya na Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea, James Rugemalira.

Na Mwandishi wa tovuti ya Habari Za Jamii

KAMPUNI ya VIP Engineering and Marketing Limited imetoa wito kwa Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) kutoa mapema taarifa ya uchunguzi inayohusiana na uchotwaji wa fedha katika akaunti maalumu ya Escrow ya Benki Kuu ya Tanzania.

Mwito huo umetolewa na Mshauri ya Kimataifa wa Kujitegemea James Rugemalira wakati akiongea na waandishi wa habari pamoja na jopo la wanasheria wa kimataifa kutoka Marekani waliopo nchini Dar es Salaam jana kwa ziara maalumu.
“Mimi nashangaa kwa nini taarifa hizi hazitoki. Nilitegemea zitoke hata jana. Mimi nimeshatoa maelezo yangu na niko muwazi kwa jambo hili. Nilitegemea taarifa hizi ziwe zimeshatolewa ili wananchi wajue ukweli wa swala hili,”

Mabingwa wa Dance 100% waunganishwa na mtandao wa Vodacom

Kundi la”WAKALI SISI”ambalo ni mabingwa wa shindano la Dance 100% 2014 wakionesha makali yao ya kucheza dansi katika makao makuu ya Vodacom walipofika katika hafla fupi yakukabidhiwa rasmi ya simu zao aina ya Vodafone Smart Kicka zilizounganishwa na muda wa maongezi wa kiasi cha shilingi laki moja ambazo ni moja ya zawadi walizojishindia katika fainali ya shindano hilo na kuibuka washindi wa kwanza na kujizolea kombe pamoja na kitita cha shilingi milioni5.

Kundi la ”Wakali Sisi” lenye makazi yake Kiwalani jijini Dar es Salaam, ambalo liliibuka na ushindi miongoni mwa makundi matano yaliyoingia fainali za shindano la kucheza muziki maarufu kama Dance 100% na kujishindia kitita cha shilingi milioni 5 wiki iliyopita leo/ jana wasanii wa kikundi hicho walikabidhiwa simu aina ya smart Phone na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom.

Akiongea katika hafla ya kuwakabidhi zawadi ya simu Meneja Uhusiano wa

Texas health care worker tests positive for Ebola

A health care worker at Texas Health Presbyterian Hospital, where an Ebola patient died last week, has tested positive for the virus after a preliminary test, the hospital said early Sunday in a statement.
"We knew a second case could be a reality, and we've been preparing for this possibility," said Dr. David Lakey, commissioner of the Texas Department of State Health Services.
"We are broadening our team in Dallas and working with extreme diligence to prevent further spread."
Confirmatory testing will be conducted by the Centers for Disease Control and Prevention in Atlanta. If confirmed by the CDC, the health care worker's case would mark the second diagnosis of Ebola ever in the United States.

This is a breaking news story.

Dar: Mtoto Darasa la Kwanza abakwa, achinjwa, anyofolewa viungo na kufariki

Mwanafunzi wa shule ya msingi jijini Dar es Salaam mwenye umri wa miaka saba, ameuawa kikatili baada ya kubakwa, kuchinjwa na kunyofolewa sehemu zake za siri.

Mwanafunzi huyo wa darasa la kwanza (jina linahifadhiwa), mwili wake ulikutwa umetupwa kwenye shamba karibu na nyumbani kwao jana maeneo ya Mbezi Temboni, kata ya Saranga.

Akisimulia tukio hilo, mama wa mtoto huyo (jina linahifadhiwa), alisema kuwa juzi baada ya mwanawe kurejea toka shuleni alimuogesha na kumpa chakula majira ya saa 12 ya jioni.

Alisema baada ya kumtayarishia chakula hicho, alitoka kidogo kuelekea