Wanachama TADEA watuhumu Uongozi kutumiwa na Shibuda

Baadhi ya wanachama wa chama cha Democratic Alliance (TADEA), wameutuhumu uongozi wa chama hicho kutumiwa na vyama vya siasa akiwamo Mbunge wa Maswa Magharibi, John Shibuda (Chama Cha Demokrasia na Maendeleo - CHADEMA), kwa maslahi binafsi.

Tuhuma hizo zimetolewa na Joachim Mwingira, Makamu wa Rais Mstafu wa Tadea,Vurugu Luziga; Katibu wa Tadea Meatu na Bavi Mdumrua, mwanachama namba 0026 wa TADEA, walipokuwa wakizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam.

Walidai uongozi huo umekiuka misingi ya chama, kwa kuunga

Tanzania calls for international ban on ivory, rhino trade

By Peter Saramba Ongiri
ARUSHA, Tanzania


Tanzania is calling for an international ban on trading in ivory products in hopes of protecting its endangered species – including rhinos and elephants – from poachers.

"Without putting an end to international trade in these products, the war against poaching will be futile," Natural Resources and Tourism Minister Lazaro Nyalandu told Anadolu Agency in the northern city of Arusha, which is surrounded by some of Africa's most celebrated nature preserves.

"About 10,000 elephants are killed every year by poachers in Tanzania, which currently has less than 70,000 jumbos [large elephants]," he said.

Taarifa ya kuanza kwa vikao vya Kamati ya Bunge ya Bajeti

Kamati ya Bunge ya Bajeti inatarajia kuanza vikao vyake kuanzia tarehe 13 Oktoba hadi 2 Novemba, 2014.

Katika vikao hivyo Kamati inatarajia kushughulikia Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Kodi (Tax Administration Bill, 2014) na Muswada wa Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (Value added Tax Bill, 2014).

Katika kutekeleza azma hiyo, Kamati imepanga kupokea maoni ya wadau kuhusu Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Kodi (Tax Administration Bill, 2014) na Muswada wa Kodi ya Ongezeko la Thamani (Value Added Tax Bill , 2014) siku ya Jumamosi hadi Jumanne ya tarehe 25 – 28 Oktoba, 2014 kuanzia saa 4:00 Asubuhi Ukumbi wa Mkwawa, Ofisi ya Bunge Dar es Salaam. Miswada hiyo itashughulikiwa kwa pamoja kutokana na maudhui yake kushabihiana.

Kwa maelezo zaidi unaombwa kuwasiliana na Ndugu Michael Chikokoto simu Na.0785-570685 au Michael Kadebe kwa simu Na.0713-705463.

15 Oktoba 2014

Vodacom kumzawadia mchezaji bora wa Septemba 2014

Kunduchi waandamana hadi vituo vya polisi
Wakazi wa Kunduchi jijini Dar es Salaam leo wameandamana kuelekea vituo vya Polisi vya Wazo na Mtongani kwa madai kuwa ndugu zao wamekamatwa bila makosa na kupelekwa vituoni.

Wakizungumza na GPL baadhi ya waandamanaji walisema magari matano ya Polisi yalikwenda eneo hilo na kuanza kukamata watu hovyo kwa madai kuwa ni wahuni na wavuta bangi.

Dereva mmoja wa bodaboda alisema kawaida ya Polisi hao hufika na kuwakamata wahuni, wavuta bangi na vijana walio katika makundi ya uhalifu, ila kilichotokea ni wahuni hao kushtuka na kukimbia, ndipo polisi wakaaanza kukamata watu hata wasiohusika.

Habari/Picha na: Gabriel Ng’osha/GPL

Kazi, uadilifu, mafanikio na utata wa Membe kidiplomasia

Bernard K. Membe
makala iliyopita nilianza kumjadili Benard Membe anayetajwa kuwa kati ya wagombea urais wenye nafasi kubwa ya kupitishwa kupeperusha bendera ya chama chake cha CCM katika Uchaguzi Mkuu ujao.

Katika makala haya ninajadili wasifu wa Membe katika maeneo ya kazi, uadilifu na diplomasia.

Kikazi, tunaweza kusema Membe ni mtu aliyekulia katika ushoroba wa madaraka (power corridors). Mara baada ya kumaliza mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa, Membe aliajiriwa kufanya kazi katika ofisi ‘nyeti’ ya Rais. Na hata baada ya kuhitimu masomo yake ya shahada ya kwanza Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alirudi kuendelea na kazi yake ya ukachero na hivyo kushindwa kuchukua kazi aliyokuwa amepewa ya uhadhiri msaidizi katika Chuo hicho.

Membe alipanda ngazi kadhaa na hata kuwa msaidizi wa waliopata kuwa wakurugenzi wakuu wa Idara nyeti ya Usalama wa Taifa, Dk. Hans Kitine na Apson Mwang’onda.

Ni kukua kwa Kiswahili, kuporomoka au uzao wa lugha nyingine?

(image: benjamins.com)

Pamoja na kuwa Kiingereza ndio lugha rasmi ya kufundishia katika shule za sekondari na vyuo vikuu, ni muda mrefu sasa kumekuwa na mijadala ya lugha ipi kati ya hizi mbili ni muafaka katika kufundishia. Mijadala hii inakuja kufuatia kuendelea kudorora kwa ubora wa elimu nchini Tanzania.

Kuhusiana na hili, tafiti nyingi zimeshafanyika. Lengo si kujadili tafiti hizi, wala ni lugha ipi ni muafaka katika kufundishia wanafunzi nchini Tanzania. Hii inaonesha kuwa Tanzania tuna utata katika matumizi ya Kiswahili na Kiingereza. Utata unaohitaji suluhisho.

Wema Sepetu na MC Pilipili Kuizindua Kili Chats

Muigizaji maarufu nchini Wema Sepetu na Mchekeshaji MC Pilipili wanatarajiwa kuwa wa kwanza kukizindua kipindi cha Kili Chat Shows kinachotarajiwa kuanza leo. Kipindi hicho kitakachokuwa kikiendeshwa na Gadner G Habash kitakuwa ni cha nusu saa na kitakuwa kikiwakutanisha mastaa wawili wanaoshabikia timu za Yanga na Simba ambapo watapata nafasi ya kushindana namna wanavyozielewa klabu hizo. Pia mashabiki watapata nafasi ya kuwahoji maswali kuhusu shughuli zao.

Kipindi hicho kitakachokuwa kikirushwa Alhamisi saa tatu usiku katika kituo cha East Africa TV ni muendelezo wa kampeni ya Nani Mtani Jembe ambayo ilianza mwanzoni mwa mwezi huu kwa mashabiki wa Yanga na Simba kushiriki kampeni hiyo ambayo jumla ya Sh 100 zinashindaniwa kwa mashabiki kupiga kura kwa SMS kwa kutuma namba za ndani ya kizibo kila wanapokunywa bia ya Kilimanjaro.

Polisi yawataja 5 waliopoteza uhai wakichota mafuta ya lori lililopata ajali

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova amethibitisha kutokea kwa vifo vya watu watano na wengine 16 kujeruhiwa katika ajali ya moto iliyotokea Oktoba 13 mwaka huu majira ya saa 5:00 usiku huko kwenye mzunguko wa Mbagala Charambe baada ya lori aina ya Scania T347 BXG lilipoanguka likiwa na mafuta aina ya petrol lita 38,000.

Aliwataja waliofariki kuwa ni:
  1. Masoud Masoud mkazi wa Charambe
  2. Hassani Mohamed mkazi wa Mbagala Kibangulile
  3. Mohamed Ismail mkazi wa Mbagala Charambe

Kizazi cha BRN kinavyoandika insha siku hizi

ITV wanadhani nakwenda kujitangaza na si kusaidia watu - Makulilo

Muda mchache uliopita, nimesoma kwa masikitiko ujumbe wa Ernest Makulilo, aliyeko Tanzania kwa sasa baada ya shughuli ya mazishi ya baba yake mzazi kumalizika, ambapo kabla ya kurudi nchini Marekani anakoishi na kufanya kazi, alipanga pamoja na mambo mengine, aendeleze utamaduni wake wa kuzungumza na Watanzania, hasa vijana wanaotafuta nafasi za ufadhili wa masomo, ili awaeleze uzoefu wake na mbinu mbalimbali za kuwasaidia kuweza kunyakua nafasi hizo zenye ushindani mkubwa kote duniani.

Akiwaandikia Wanazuoni (via Yahoo! Groups), Makulilo anasema:
Samahanini WANAZUONI, kipindi Cha kesho kumekucha ITV "kimezuiliwa" sababu Watu wa ITV wanadhani na kuamini lengo langu ni kwenda kujitangaza na si kusaidia Watu. Hivyo inabidi nilipe kama milioni 2 kuwepo hewani.

Bahati mbaya wadau wengi mnakosa fursa hii