Joko WIdodo aapishwa kuwa Rais wa Indonesia

Rais mpya wa Indonesia, Joko Widodo aliyeapishwa, Oktoba 20 mwaka 2014, jijini Jakarta.

Rais mpya wa Indonesia ameapishwa jana Jumatatu Oktoba 20, 2014, miezi mitatu baada ya kuchaguliwa kwenye wadhifa huo.

Widodo ni mfanyabiashara wa zamani wa ambaye ni kiongozi wa kwanza kuchaguliwa kutoka nje ya wanasiasa wasomi na jeshi.

Joko Widodo atajaribu kuleta mabadiliko katika taifa hilo la kwanza kiuchumi katika Asia ya Kusini. Asilimia kubwa ya raia wa Indonesia wana imani kwamba rais huyo ataleta mabadiliko makubwa katika nyanja mbalimbali.

Tangu mwaka 1998 na baada ya kutimuliwa kwa utawala wa kiimla wa dikteka Suharto, aliyeongoza taifa la Indonesia kwa muda wa miaka 32, marais waliyofuta walikuwa ni kutoka katika ukoo wa dikteta huyo.

Indonesia inaundwa na visiwa 13,466 ambavyo vina wakaazi milioni 240. Asilimia 90 ya raia wa Indonesia ni Waislam.

via RFI Kiswahili

Mrema awafukuza madiwani 2 waliomuunga mkono Mbatia

Mbunge wa jimbo la Vunjo na Mwenyekiti wa chama cha TLP,Dk.Augustine Lyatonga Mrema akihutubia mkutano wake wa hadhara jimboni kwake jana kwa ajili ya kuhamasisha uchaguzi wa serikali za mitaa na pia kuelezea utekelezaji wa miradi ya Maendeleo,aidha katika jimbo hilo la Vunjo kumekuwepo na Mvutano mkubwa kwa vyama vya CCM,Innocent Shirima na Mh.James Mbatia wa NCCR-Mageuzi.

MWENYEKITI wa Tanzania Labour Party (TLP), Augustine Mrema, amekunjua upya makucha yake yaliyowahi kurarua viongozi wenzake akiwa katika NCCR-Mageuzi na TLP, na sasa amefukuza hadharani madiwani wawili wa chama chake waliounga mkono nia ya Mbunge wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia, ambaye ametangaza kugombea ubunge wa Vunjo.

Mrema amewavua uanachama wa TLP, Meja Mstaafu Jesse Makundi, aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo hilo kabla ya Mrema; na Yorolanda Lyimo, Diwani wa Kilema Kaskazini.

Jimbo hilo linawakilishwa na Mrema tangu 2010, na amesema mara kadhaa kwamba hataki kusikia mtu akitaka ubunge katika jimbo lake. Tayari amemlalamikia Mbatia kwa rais na katika Bunge Maalumu la Katiba.

Tanzania rescue Tsh 15/= billion at airports from gem smugglers

Tanzania Minerals Audit Agency (TMAA) has succeeded to rescue Tsh15.8 billion ($9.44 million) from minerals and gemstones nabbed at the country’s three largest airports, Julius Nyerere, Kilimanjaro (KIA), and Mwanza International Airports.

This has been revealed by the TMAA’s acting Director for Mineral Production and Exportation Monitoring, Conrad Mtui while briefing the media who visited the agency for a familiarization tour.

Tanzania is the East Africa’s biggest exporter of gemstones. However, there are also smuggling rings that seek to by-pass government scrutiny.

Tanzanian police kill bombing 'mastermind' suspect

Tanzanian police said on Monday that they had shot dead a man suspected of carrying out bomb attacks in the tourist town of Arusha, including targeting a church and restaurant.

Yahaya Omari was described by police as the “mastermind, brain, co-ordinator and the main performer of terrorist bombings and acid attacks in Arusha”.

He was being transferred to the Tanzanian capital Dodoma when he tried to escape, with officers shooting him dead late on Sunday.

UK Trade & Investment London/South East Trade Mission to Tanzania

14 UK companies cutting across various sectors e.g. Education and Training, Security, Consultancy, Healthcare amongst others are hoping to penetrate new trade opportunities within Tanzania by taking part in UKTI London and South East trade mission to Tanzania between October 22nd-24th 2014. This is the first, independent visit by UKTI London and South East to Tanzania and East Africa.

Tanzania is fast emerging as a thriving commercial entity with a GDP growth rate of over 7% year upon year. The major city of Dar es Salaam where we will be staying is the centre of most government activity as well as being the major commercial centre with its own deep water port with trading links to the landlocked countries of Malawi, Zambia, Democratic Republic of Congo, Burundi, Rwanda and Uganda.

Taarifa ya kupotea kwa Rehema Salum Msambya


Rehema Salum Msambya

Bi Rehema Salum Msambya pichani juu amepotea tokea tarehe 16/10/2014 maeneo ya Kigamboni - Kisota karibu na Shule ya Sekondari ya Abdu jumbe.

Siku hiyo alikuwa amevaa dela na skin tight ya rangi ya bluu. Bi Rehema ana Matatizo ya Akili. Yeyote atakayemuona anaombwa kutoa taarifa katika kituo cha Polisi Kigamboni au kilicho karibu au Apige simu namba 0712 22 77 22 au 0753 63 49 67 au 0712 70 77 87 au 0713 23 52 94

Ratiba ya CCM ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa

RATIBA YA MAANDALIZI YA UCHAGUZI WA
SERIKALI ZA MITAA NDANI YA CHAMA


TAREHE
 SHUGHULI
19/10/2014 -  22/10/2014
Mikutano ya Wanachama wote wa CCM Matawini kwa ajili ya kuelimishwa na kuhamasishwa kuhusu Uchaguzi.
23/10/2014 – 25/10/2014
Kuchukua na kurejesha Fomu za kuomba kugombea Uenyekiti wa Mtaa, Kijiji, Kitongoji na Ujumbewa Serikali za Vijiji na Mitaa kwa Makatibu wa Matawi ya CCM.
26/10/2014 – 27/10/2014
Kampeni ya wagombea ndani ya Chama.
28/10/2014 – 29/10/2014
Wanachama wa CCM kupiga kura za Maoni za Wagombea Uenyekiti wa Kitongoji na Wajumbe wa Kamati ya Kitongoji kwenye Mashina yanayohusika.
 30/10/2014 – 31/10/2014
Wanachama wa CCM kupiga kura za Maoni za Wagombea Uenyekiti wa Kijiji na Wajumbe wa  Halmashauri ya Kijiji na vilevile kupiga kura za Maoni kwa Wagombea Uenyekiti wa Mitaa na Wajumbe wa Kamati ya Mtaa kwa Mijini.  Kura zitapigwa na wanachama wote wa CCM kwenye Matawi ya Kijiji au Mtaa husika.
01/11/2014 – 03/11/2014
Kamati za Siasa za Matawi kujadili wagombea na kutoa mapendekezo yake kwa Kamati za Siasa za Kata
04/11/2014 – 06/11/2014
Kamati za Siasa za Kata kujadili wagombea na kutoa mapendekezo yake kwa Halmashauri Kuu za Kata na kwa Kamati za Siasa za Wilaya.
07/11/2014 – 09/11/2014
Halmashauri Kuu za Kata kufanya uteuzi wa mwisho kwa wagombea Uenyekiti wa Vitongoji.
10/11/2014 – 11/11/2014
Kamati za Siasa za Wilaya kujadili wagombea na kutoa mapendekezo yake kwa Halmashauri Kuu za Wilaya.
12/11/2014 – 14/11/2014
Halmashauri Kuu za Wilaya kufanya uteuzi wa mwisho wa Wagombea Uenyekiti wa Mtaa, Uenyekiti wa Vijiji, Wajumbe wa Kamati za Mitaa na Wajumbe wa Halmashauri za Vijiji.
15/11/2014 – 21/11/2014
Kuchukua Fomu na kurudisha kwa Msimamizi wa Uchaguzi.
16/11/2014 – 21/11/2014  
Mafunzo ya wajibu wa Wagombea na Mawakala.
24/11/2014
Siku ya uteuzi wa Wagombea kwa Msimamizi.

Taarifa ya SUMATRA ya utaratibu wa daladala zilizohamishiwa Mawasiliano Towers

KUHAMISHIA DALADALA KITUO CHA SIMU 2000
(NYUMA YA MAWASILIANO TOWERS) KUANZIA ALHAMIS TAREHE 23.10.2014


Baada ya kituo cha Simu 2000 kukamilika SUMATRA kwa kushirikiana na Manispaa ya Kinondoni na Kikosi cha usalama barabarani Mkoa wa Kinondoni tumekubaliana kufungua kituo hiki tarehe 23.10.2014 asubuhi kwa daladala ambazo zilikuwa zinaishia au kuanza safari katika kituo cha daladala Ubungo.

Kila dereva anatakiwa kufuata utaratibu ulioelekezwa hapa chini ili kuondoa usumbufu usio na tija.

1. DALADALA ZINAZOTOKA MASAKI
zikifika barabara ya Shekilango zitaingia kulia kwa kutumia barabara ya TANESCO inayokwenda moja kwa moja kituoni simu 2000 na zitarudi barabara ya Shekilango kwa kutumia njia hiyo hiyo ya TANESCO.

2. DALADALA ZINAZOTOKA KARIAKOO, POSTA na KIVUKONI

Taarifa ya TFF kuhusu mapato ya mechi ya Simba v/s Yanga

Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara kati ya Yanga na Simba iliyochezwa juzi (Oktoba 18 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 427,271,000.

Washabiki 49,542 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo ambapo viingilio vilikuwa sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 20,000 na sh. 30,000. Asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 65,176,932 wakati asilimia 5 ya gharama ya tiketi kwa CRDB ni sh. 21,363,550.

Taarifa ya JWTZ kwa umma kuhusu raia kutumia sare zakeJESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA
KURUGENZI YA HABARI NA UHUSIANO

Simu ya Upepo   : “N G O M E”            Makao Makuu ya Jeshi,
Simu ya Mdomo : DSM  22150463       Sanduku la Posta 9203,
Telex                     : 41051                        DAR ES SALAAM, 20 Octoba, 2014
Tele Fax                : 2153426
Barua pepe       : [email protected]
Tovuti                  : www.tpdf.mil.tz
                  
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linatoa taarifa kwa wananchi wote kuwa ni kosa kisheria kumiliki au kuvaa sare za JWTZ kwa mtu yeyote asiyehusika.
          Aidha,  kumeonekana matukio kadhaa ya baadhi ya vikundi, ama mtu mmoja mmoja kumiliki au kuvaa sare za JWTZ.  Inakumbushwa kuwa kwa yeyote atakayeonekana amevaa ama kumiliki sare hizo sheria itachukua mkondo wake. 

  
Imetolewa  na  Kurugenzi  ya  Habari  na  Mahusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P  9203,   Dar es Salaam,  Tanzania.

Kwa Mawasiliano zaidi: 0783 - 309963

Smart Kicka: Smartphone ya bei rahisi zaidi nchini toka Vodacom

Smart Kicka

Vodacom wameingiza simu zao mpya sokoni zinazokwenda kwa jina la Smart Kicka. Simu hii ni ndogo, lakini ina uwezo mkubwa ambao simu nyingi kubwa zaidi yake hazina. Nimeweza kuipitia na kwa jumla naweza kuipa rating ya 7/10.

Kuhusu Smart Kicka


Smart Kicka Start Screen


Smart Kicka ilizinduliwa tarehe 1/08/2014 ambapo mtengenezaji wa simu hizo ni Alcatel aliyeingia mkataba na Voda. Model yake ni Vodafone VF685. Sim card yake ni ya kawaida haihitaji kukatwa.

Urefu wake ni 112mm na uzito wake ni gram 100 (very light). Betri yake ina uwezo wa kukaa masaa karibu 9 ukiwa unaongea na mtu. Nilichokipenda kuhusu sii simu ni kutokupata joto kurahisi.

Smartphone nyingi imekuwa ni kama kawaida kuona zikiwa za moto baada ya kutumia mfululizo au ukiwa unatumia apps nyingi. Hii imekuwa tofauti kwa Smart Kicka.

Ndovu Yaizindua Golden Experience