Ujumbe kwa wanaochukua taarifa wavuti.com na kutoza malipo

(image: lovefromtheoven.com)

Habari za leo,
Mimi naitwa Makirita Amani mmiliki wa AMKA MTANZANIA blog. Mmekuwa mnachukua makala kwenye blog ya AMKA MTANZANIA na sio kitu kibaya kwa sababu mnaonesha credit. Nashukuru sana kwa hilo kwani napata wasomaji kutoka wavuti.
Naandika ujumbe huu kutaka kupata ufafanuzi kwa sababu nimeona sehemu za makala za amka mtanzania zikitumwa kwenye ujumbe wa simu kwa watu. Ningependa kujua mimi nanufaikaje kwenye hili maana naelewa wanaotumiwa ujumbe hizi wanalipia.
Asante.
Nimesikitishwa na taarifa iliyopo kwenye ujumbe wa Amani Makirita (ulionukuliwa hapo juu), mwenye blogu ya AMKA MTANZANIA ambaye anaandaa makala na kuziweka kwenye blogu yake kwa faida ya kumsaidia Mtanzania. Kwa sababu isiyo ya kiungwana, wapo watu ambao wameziona baadhi ya makala zake kwenye wavuti.com na kuanza kuzitumia kwa faida zao binafsi.

Ujumbe wa Amani ulifahamisha kuwa mtu/watu hao hutuma makala kwenye simu na kuwatoza watu fedha bila yeye kufahamiswa wala kufaidika kwa namna yoyote ile.

Kutokana na hayo:-

Hasheem Thabeet, 3 others waived from Pistons

Hasheem Thabeet
Hasheem Thabeet

On Monday, Detroit Pistons waived the No. 2 pick in the 2009 draft by Memphis, Hasheem Thabeet, forward Brian Cook, and guards Josh Bostic and Lorenzo Brow.

The 7-foot-3 center has never averaged more than 3.1 points per game. He played 23 games for Oklahoma City last season.

With the Pistons' regular season approaching in the next nine days, they began the process of cutting down their roster of training camp invitees.

None had guarantees coming into camp, and with the Pistons already having 16 guaranteed contracts, one over the league limit of 15, it was highly unlikely any of them would be able to crack the roster.

The Pistons still have to decide on whether they'll keep Tony Mitchell, a second-round pick from 2013 who's on the roster bubble.

  Hatari! Risasi zafyatuliwa Bungeni Canada na kuua

  .

  Hali ya wasiwasi imetokea leo Jumatano mchana Oktoba 22 katika mji wa Ottawa, nchini Canada, baada ya milio mingi ya risasi kusikika pembezoni mwa eneo la kibiashara katikati ya mji na ndani jengo la Bunge.

  Mwanajeshi mmoja wa Canada aliyejeruhiwa kwa risasi akiwa mbele ya mnara wa ukumbusho kwa wafu, amefariki.

  Mmoja wa watu waliyofyatua risasi hizo ameuawa kwa kupigwa risasi na vyombo vya usalama. Polisi inawasaka watu wengine waliohusika na kitendo hicho.

  Bodi ya Huduma za Maktaba yaanzisha masomo ya jioni ya Diploma ya ukutubi

  Mkuu wa Kitengo cha Mipango kutoka Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania Bw. Comfort Komba akiwaeleza waandishi wa habari(hawapo pichani) Kuhusu mafanikio yaliyofikiwa na Ofisi hiyo ikiwamo ujenzi wa majengo ya chuo cha ukutubi na uhifadhi wa nyaraka kilichopo Bagamoyo na uzinduzi wa maktaba za wilaya za Kibaha, Chunya, Ruangwa, Ngara, Rulenge, Masasi na Mbulu, wakati wa Mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bi. Georgina Misama.
  Mkuu wa Kitengo cha Mipango kutoka Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania Bw. Comfort Komba akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani) Kuhusu mafanikio yaliyofikiwa na Ofisi hiyo ikiwamo ujenzi wa majengo ya chuo cha ukutubi na uhifadhi wa nyaraka kilichopo Bagamoyo na uzinduzi wa maktaba za wilaya za Kibaha, Chunya, Ruangwa, Ngara, Rulenge, Masasi na Mbulu, wakati wa Mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bi. Georgina Misama.

  Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania imeanzisha masomo ya jioni ya diploma ya ukutubi katika Kampasi ya Dar es Salaam katika mwaka wa masomo 2014/2015.

  Hatua hiyo inatokana na kuongezeka kwa maombi ya wanafunzi wanaohitaji kuendelea na masomo baada ya kuhitimu mafunzo ya cheti.

  Picha za mazoezi ya pamoja ya Wanajeshi wa Tanzania na China

  Askari wa majini wa Tanzania na China, wakiwasubiri maelekezo mwanzoni mwa mazoezi ya pamoja ya kijeshi kwenye komandi kuu ya wanamaji wa JWTZ, Kigamboni jijini Dar es Salaam, Jumanne Oktoba 21, 2014.


  Aliyeunguliwa nyumba yake yote Kigamboni aomba msaada  Familia ya ndugu Aron Sondi inayeishi Kigamboni jijini Dar es Salaam, ambao taarifa zikiambatana na picha za kuungua kwa nyumba na kupoteza mali na vitu vyote jana jioni zimekuwa zikisambaa kwenye mitandao (zimepachikwa hapo chini), wanaomba michango ya hali na mali. 

  Mfano wa fomu ya udhibiti wa Ebola mpaka wa Mutukula

  Kamala ametuma ujumbe ufuatao kupitia Wanazuoni Yahoo! Group:
  Walumuna
  Nimekatiza mpaka wa Mutukula unaotenganisha Tanzania na Uganda na hiyo ndiyo fomu inayopitiwa kuona kama una Ebola au la.
  Ukiishaijaza unaikabidhi kwa bwana mmoja halafu unaruhusiwa kugonga pasipoti.
  Yaani ukiwa na Ebola au Marburg unamwambukiza huyo mkagua fomu, maafisa uhamiaji na jamaa wa TRA maana hamna hata mmoja mwenye kujikinga.
  Fungua ambato kuona fomu yenyewe.

  Waziri Dk Kamani akabidhi ng'ombe wa maziwa 83 kwa wafugaji


  Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dr. Titus Kamani, akikabidhi moja ya Ng’ombe 83 wa Maziwa, kwa Bibi. Robi Chacha ambaye ni miongoni mwa wanakikundi 83 waliokabidhiwa Ng’ombe hao ambao wamenunuliwa kwa Mkopo na Covenant Bank. Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi wa Covenant Bank. Sabetha Mwambenja, (Mwenye miwani katikati) na Mwenyekiti wa Wajasiriamali wasio katika Sekta Rasmi Dauda Salmin.

  Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dk Titus Kamani, amekabidhi mikopo ya Ng’ombe wa maziwa themanini na tatu (83) kwa kikundi cha wafugaji cha Somangira walioko Kigamboni wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam.

  Ng’ombe hao ambao wamenunuliwa kwa mkopo uliotolewa na Covenant Bank wana uwezo wa kuzalisha maziwa zaidi ya Lita 20 kwa siku. Akizungumza na wakazi wa eneo hilo Waziri Kamani ametanabaisha kuwa mikopo ya aina hiyo italeta mapinduzi makubwa katika sekta ya mifugo.

  “Kitendo cha kukabidhiwa Ng’ombe kwa kikundi cha wafugaji wadogo wa Somangira kinafanyika kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu hususan katika sekta ya mifugo, Mikopo ya aina hii imekuwa ikitolewa i kwa Ranchi za taifa lakini haikuwahi kutolewa kwa wafugaji wadogo wadogo” alisema Dk. Kamani na kuongeza kuwa: 

  [video] Ujumbe wa Wizara ya Afya kuhusu ugonjwa wa Ebola

  Matokeo ya usaili wa mchujo TBC

  Wasailiwa waliofanikiwa kuendelea na usali wa mahojiano wanatakiwa kuzingatia mahali na muda wa usaili.

  KADA: PRODUCER II
  MWAJIRI: TANZANIA BROADCASTING CORPORATION (TBC)
  TAREHE: USAILI WA MAHOJIANO 22/10/2014, SAA MOJA KAMILI ASUBUHI
  MAHALI: TBC TAIFA - NYERERE ROAD

  EXAM NUMBERS SCORE REMARKS
  PSRS-TBC-PRD-031 60 SELECTED
  PSRS-TBC-PRD-013 55.5 SELECTED
  PSRS-TBC-PRD-014 55.5 SELECTED
  PSRS-TBC-PRD-027 53 SELECTED
  PSRS-TBC-PRD-011 52.5 SELECTED
  PSRS-TBC-PRD-025 50.5 SELECTED
  PSRS-TBC-PRD-000 49 NOT SELECTED
  PSRS-TBC-PRD-002 49 NOT SELECTED
  PSRS-TBC-PRD-008 49 NOT SELECTED
  PSRS-TBC-PRD-006 48.5 NOT SELECTED

  Kauli rasmi ya Serikali kuhusu taarifa za 'mgonjwa wa Ebola' nchini

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

  WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII


  TAMKO LA SERIKALI KUHUSU TETESI ZA KUWEPO MGONJWA ANAYEHISIWA KUWA NA UGONJWA WA EBOLA WILAYANI SENGEREMA MKOANI MWANZA


  20 Oktoba 2014

  Utangulizi

  Mnamo tarehe 18 Oktoba 2014, Wizara ilipokea taarifa kutoka Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ya kuwepo kwa mgonjwa aliyehisiwa kuwa na ugonjwa wa Ebola. Mgonjwa huyu aliyekuwa na umri wa miaka 17, jinsia ya Kike na mkazi wa kijiji cha Bupandwa Tarafa ya Kahunda Wilaya ya Sengerema, alilazwa akiwa na dalili za homa kali, manjano, kutokwa na damu sehemu mbalimbali za mwili.

  Mgonjwa huyu alilazwa katika Kituo cha Afya Mwangika tarehe 15 hadi 16 Oktoba, 2014 ambapo pia alionekana kuwa vimelea vya ugonjwa wa Malaria kabla ya kuhamishiwa Hospitali Teule ya Wilaya ya Sengerema mnamo tarehe 17 oktoba 2014 na kufariki duniani siku hiyo hiyo muda wa saa 3.30 usiku.

  Hata hivyo, mgonjwa huyu hakuwa na historia ya kusafiri kwenda nchi zilizoathirika na ugonjwa wa Ebola na hakuwahi kupokea mgeni kutoka nchi hizo ndani ya siku ya 21 zilizopita.

  Hatua zilizochukuliwa ni pamoja na;