Yanga warushiana makonde na Stand United kisa uchafu

Wachezaji Yanga wakikabiliana na mashabiki wa Stand United,katikati ya nguzo mbili yupo kocha wa Yanga Maximo. (picha: Kadama Malunde-Malunde1 blog)

Jana jioni wakati wa mchezo wa soka wa ligi Vodacom 2014/2015 kati ya timu ya Yanga na Stand United katika uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga ilitokea vururu kipindi cha mapumziko baada ya wachezaji wa Yanga wakiongozwa na kocha wao Marxio Maximo kupanda Jukwaa Kuu wakidai kuwa vyumba vya kubadilishia nguo vilivyoko uwanjani ni vichafu na hivyo walihitaji kutumia vyumba vilivyoko Jukwaa Kuu, kitendo ambacho kilipingwa na mashabikiwa Stand United.

Hapo ndipo vurugu zikaanza,wachezaji wa Yanga wakirushiana makonde na mashabiki wa Stand United. Hali hiyo ilisababisha Kocha wa Yanga Maximo kuingilia kati huku naye akinusurika kuchapwa makonde na mashabiki, na kulazimika kukabiliana nao huku wakimrushia chupa za maji.Mapendekezo ya Mwalimu wa Madereva kuhusu ajali za barabaraniMimi ni dereva na pia ni Mwalimu wa madereva “Drivers Instructor ”. Napenda kutoa maoni yangu na mapendekezo kuhusu ajali barabarani kama ifuatavyo:-

Nimefanya uchunguzi kwa muda wa miaka mitatu kwa madereva tofauti, wa malori makubwa , mabasi makubwa na madogo (daladala), tax pick up za kukodi, malaori ya mchanga, madereva wa Serikali, madereva wa Waheshimiwa Wabunge na bajaji. Kwa makundi yote haya ukiondoa Madereva wa Serikali kinachowafanya madereva hawa kuendesha magari bila kujijali wao wenyewe, abiria na watembea kwa miguu kwa kuendesha mwendo kasi bila ya kujiwekea tahadhari ya chochote barabarani.

Madereva karibu asilimia 92 hawana ajira ya kudumu wala mikataba inayoainisha malipo na maslahi yao, hivyo malipo yao ni kutokana na safari wanaozifanya na idadi ya tripu, hali hiyo inawalazimu madereva kama wa bus wakimbie ili ajitahidi azipite gari zilizomtangulia bila kujali madhara yanayoweza kumkuta endapo atapata ajali. Unaweza kukuta madereva wengine mfukoni hawana hata shilingi elfu kumi (10,000/=) ambayo inaweza kuwa ya thadhari ya kumuona dokta kwa hatua ya huduma ya kwanza endapo atapata ajali. Hali hii inasikitisha sana kulingana na thamani ya gari analoliendesha , uhakika wa

Kilichotokea katika uchaguzi wa Zanzibar 2010

Baada ya gazeti moja lilichapisha habari kuhusu nafasi ya *Mzee Nassoro Moyo kwenye uchaguzi wa Zanzibar mwaka 2010, Josephat Charo wa DW alizungumza na mwanasiasa huyo, hasa kupata ufafanuzi wa madai kuwa chama tawala, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilikuwa tayari kwa lolote lakini siyo kutangazwa mgombea wa kilichokuwa chama cha upinzani, CUF, kama mshindi wa urais kwenye uchaguzi huo.

Katika mahojiano haya, Mzee Moyo kwanza anaelezea vipi aliweza kumshawishi mgombea wa CUF, Seif Sharif Hamad, akubali ushindi wa mpinzani wake mgombea wa CCM na rais wa sasa wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein.

Kusikiliza mahojiano kamili, tafadhali bonyeza pleya ifuatayo:*Mzee Nassoro Moyo alikuwa mjumbe kwenye Baraza la kwanza la Mapinduzi la Zanzibar chini ya Marehemu Abeid Karume, Waziri wa Sheria wa Muungano, Waziri wa Elimu wa Zanzibar na sasa Mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano.

Mwandishi wa habari wa Mtanzania, Elias Msuya akifanya mahojiano ya Mzee Hassan Nassor Moyo nyumbani kwake Fuoni.
Mwandishi wa habari wa Mtanzania, Elias Msuya akifanya mahojiano ya Muasisi wa Muungano na kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mzee Hassan Nassor Moyo nyumbani kwake Fuoni.

Hivi karibuni Bunge Maalum la Katiba limekabidhi rasimu ya Katiba inayopendekezwa kwa rais Jakaya Kikwete na rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein.

Hata hivyo rasimu hiyo imepokelewa kwa hisia tofauti huku makada wa CCM wakiiunga mkono na wapinzani wakiipinga.

Kwa upande wa Zanzibar, siyo wapinzani tu wanaoipinga, bali hata wana CCM wanaojitaja kuwa na uchungu wa visiwa hivyo.

Akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni mjini Zanzibar, mwanasiasa mkongwe aliyeshiriki Mapinduzi ya Zanzibar ya Januari 12, 1964 Hassan Nassor Moyo anasema Katiba hiyo inapingana na Mapinduzi ya Zanzibar hivyo haikubaliki.

Swali: Katiba inayopendekezwa imepiotishwa na sasa inapigiwa debe kuelekea kwenye kura ya maoni. Nini nafasi ya Zanzibar katika Katiba hiyo?