Eti huyu ni mwekezaji ama kuna utafiti unaendelea?

Nimepokea ujumbe na maelezo kupitia anwani pepe ambao nimeupachika hapo chini bila kubadili hat aiota moja.

Ujumbe huo umenisababisha niulize swali lililo kichwa cha habari hapo juu. Mtoa mada amegusia upande mmoja, nami nimegusia upande mwingine kuwa huenda huyu akawa anachagiza jambo kwa ajili ya kupata mwitikio wa mawazo na hisia tofauti za watu, utakaosaidia utafiti wake.

Inawezekana nawe una mtizamo wa tofauti.WAWEKEZAJI WA KIGENI WATUPIWE JICHO NA SHUGHULI ZAO
Je ! Huu ndio uwekezaji wenyewe ? Idara ya Uhamiaji mpo wapi ?
ah !  "MGENI WA MUNGU HUYU" mwache ajitafutie riziki ! 

Baadhi ya wawekezaji wa kigeni au pengine watumishi raia wa kigeni wamekuwa
wakivunja sheria za nchi kwa kujiingiza au kufanya shughuli zisizo katika miktaba yao
 ya kazi,au nje ya vibali vyao vya kufanyakazi hapa nchini Tanzania,lakini uvunjwaji wa sheria za nchi unaofanywa na wageni hawa unasaidiwa na sisi wenyewe kwa kuzingatia
zile mila zetu na misemo ya ah !  "MGENI WA MUNGU HUYU" mwache ajitafutie riziki.Matokeo yake tumekuwa na wachoma mahindi mtaani kutoka china,wabeba zege pia,
Kumradhi pengine makahaba au changudoa kwenye madangulo ya siri.
tunaweza kuwa na wakaanga samaki, walinzi "Kolokoloni" kutoka Thailand na Bangladesh,
inawekana kabisa tunao hapa nchini wapishi na tour guider kutoka nchi za ulaya !
Kwa mtindo na utamaduni wetu huu wa ah! wache "WAGENI WA MUNGU " wajitafutie ridhiki   tutajikuta tunao akina mama ntilie wakigeni.
Tunajiuliza wale wawekezaji wanajiusha na biashara za mitumba au maduka ya nguo kariakoo hivi vibali aliwapa nani? yaani muuza mtumba na duka la sukari atoke china,Yemen,Bangladesh ulaya ! hii kweli inaingia akilini kwa watanzania?
Sasa wawekezaji hawa kigeni wanafanya shughuli hizi mcha wa jua kali tena kweupe
Mkondo wa sheria ya nchi unavunjwa walinzi wa sheria wako wapi?
Wizara zinazohusika amlioni hili au ndio ah! TUWAACHE WAGENI WA MUNGU wajitafutie ridhiki ?  Watanzania ukarimu ni jadi yetu ! misemo hii haifanani kabisa
na ukiwikaji wa sheria za uhamiaji na ajira za nchi, kwani katu kwame uruma na
haki havikai pamoja.

Ushauri wa Amani kwa Lady Jaydee

Lady Jaydee (picha: Nairobi Wire)

Siku chache zilizopita mwanamziki maarufu wa Tanzania Judith Wambura maarufu kwa jina la Lady Jaydee aliweka ujumbe kwenye mtandao wa facebook kwamba hayuko kwenye kipindi ambacho anaweza kutunga nyimbo. Ujumbe huo ulisomeka kama ifuatavyo;
Hiki ni kipindi ambacho siwezi kutunga/kuandika nyimbo, sina hisia zozote na nikilazimisha hazitakuwa nzuri.

Huwa nakaa hata miaka 3 au 5 pengine mwezi mmoja au miwili au 6 , yaani huwa haitabiriki, pale inapotokea tu ndio huwa. 

Natumaini jibu hili ni muafaka na litawaridhisha walio uliza, Poleni kwa kusubiri, i wish ningeweza
Niliona linaweza kuwa tukio la kawaida kwake na hivyo sikufikiri sana kuhusu hilo mpaka nilipokutana na rafiki yangu siku chache baadae. Rafiki yangu huyu ni mwandishi na nilitaka kujua anaendeleaje kwenye uandishi, nae akanijibu hayupo kwenye wakati mzuri wa kuandika, yaani hajisikii kuandika na hata akijisukuma haoni kama anaandika kitu kizuri. Hapa niliona kuna tatizo na hivyo kuona umuhimu wa kutoa ushauri kwa watu hawa na kwako pia kama unakutana na hali kama hizi kwenye kazi zako.

Tatizo analopitia Jaydee, na huyo rafiki yangu, huenda na wewe pia linaitwa writer’s block. Yaani

Nakala ya makubaliano ya vyama vinavyounda UKAWA

Umati wa watu waliohudhuria mkutano wa CUF uliohudhuriwa na wafuasi wa kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).

Kutoka kushoto ni James Mbatia wa NCCR-MAGEUZI, Prof Ibrahim Li[pumba wa chama cha Wananchi CUF, Freeman Mbowe wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Dk. Emmanuel Makaidi wa NLD wakionesha hati yao ya makubaliano waliyoisaini jana katika viwanja vya Jangwani Dar es Salaam
Kutoka kushoto ni James Mbatia wa NCCR-MAGEUZI, Prof Ibrahim Li[pumba wa chama cha Wananchi CUF, Freeman Mbowe wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Dk. Emmanuel Makaidi wa NLD wakionesha hati yao ya makubaliano waliyoisaini jana katika viwanja vya Jangwani Dar es Salaam

Pichani ni viongozi wa juu wa vyama vinne vya siasa nchini Tanzania vilivyoingia makubaliano ya ushirikiano wa shughuli mbalimbali za siasa Oktoba 26, 2014.

Miongoni mwa mambo hayo ni kusimamisha wagombea wa pamoja katika uchaguzi wa Serikali za Mtaa na Uchaguzi Mkuu wa Wabunge, Madiwani, Wawakilishi na Rais katika uchaguzi ujao.


“Ushindi wa CCM uchaguzi ujao hauepukiki” asema Dk Shein mkutanoni Kibandamaiti

Makamo Mwenyekiti CCM Zanzibar na Rais wa zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed shein akionesha Katiba iliyopendekezwa na bunge maalum la Katiba kwa wananchi na wanachama wa CCM zanzibar katika viwanja vya Kibandamaiti mjini Unguja leo jioni.

Umati mkubwa wa wananchi waliofurika katikauwanja wa Demokrasia kibandamaiti mjini
unguja wakiwa katika mkutano wa hadhara wa CCM uliohutubiwa na Makamo Mwenyekitiwa
CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali mohamed
Shein.
(picha: Ramadhan Othman, Ikulu.)

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amewataka wananchi wa Zanzibar wasikubali kugawiwa kutokana na mchakato wa Katiba unaoendelea

Akihutubia maelfu ya wana CCM na wananchi wa Zanzibar katika Mkutano wa hadhara uliofanyika leo katika viwanja vya Demokrasia Kibandamaiti mjini Unguja, Dk. Shein alisema wananchi wote waliridhia na kushiriki mchakato huo hivyo hakuna sababu ya kugawanyika baada ya Bunge la Katiba kupendekeza Katiba Mpya.

Wito wa kuhudhuria mkutano wa 'kuzika' CCM

Ujumbe niliopokea kupitia anwani pepe unasema:

Umoja wa katiba ya Wananchi (UKAWA) unawatangazia Wananchi wote wazalendo wapenda nchi yao kuhudhuria katika mkutano mkubwa wa aina yake wenye lengo la kuizika CCM siku ya Jumapili katika viwanja vya Jangwani kuanzia saa 8:00 mchana.

Njoo ushuhudie tukio muhimu la kihistoria ambapo Viongozi wa Kitaifa wa Vyama vinavyounda UKAWA watakavyosaini makubaliano ya pamoja ya ushirikiano katika chaguzi zote zijazo kuelekea 2015. Njoo ujionee namna madalali wa nchi hii watakavyoumbuliwa na katiba yao feki kusasambuliwa!

Mkutano utaoneshwa moja kwa moja 'live' na kituo cha ITV.

Mpe taarifa hii na mwenzako.

Kuhusu majibizano ya risasi kati ya Mbunge na mwanaye

Polisi wakiwasili eneo la tukio katika ofisi za Faraja Trust Fund zinazomilikiwa na Mhe. Lucy Nkya ambako imeripotiwa kuwa milio ya risasi ilisikika jana asubuhi. (picha: Dunstan Shekidele)

Utata umeibuka, kufuatia tukio la mlio wa risasi linalodaiwa ni la majibizano kati ya Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki, Dk. Lucy Nkya na mtoto wake Jonas Nkya.

Kauli za kugongana zilizotolewa na pande mbili hizo, zimezua utata baada ya mtoto kusema bastola yake ilijifyatua, huku Mbunge akisema kishindo kilichosikika ni cha mlipuko wa mtungi wa jokofu.

Dk. Nkya ambaye aliwahi kuwa Naibu waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, aliiambia NIPASHE Jumapili kwa njia ya simu jana kuwa, wakati tukio hilo linatokea alikuwa nyumbani.

Alisema alipigiwa simu na Afisa Utawala wake, akimweleza kuhusu kishindo cha mlipuko

Tanzania to regulate mobile money services

Tanzania will establish a law to oversee mobile money and Internet banking transactions now being actively entered into by more than half of the country’s mobile phone subscribers. The number of active users of the services in Tanzania is set to increase from the current 55 per cent to 60 per cent of the population in 2015.

Kenya and Rwanda have recently enacted similar legislation to protect consumers against mobile money fraud, while Uganda is in the process of doing so.

Ministry of Finance sources said the National Payment Act will be tabled in parliament early next year for review to align it with new modes of settlement such as money transfers and mobile banking, which an estimated six million subscribers use to save.

CHADEMA yakamata askari 'wapelelezi' katika mkutano wake

Kadi ya mmoja wa waliokamatwa

CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimewabaini na kuwakamata polisi wawili  wa kituo cha polisi wilaya ya Geita, Ernest Silayo na mwingine ambaye jina lake halikufahamika mara moja waliokuwa kwenye mkutano wao wilayani Geita wakiwa wamevaa sare za chama hicho huku wakiwa na kadi za uanachama wa chama hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari juzi Naibu Katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake CHADEMA, (BAWACHA), Kunti Yusuph alisema, askari hao wa kike na wa kiume walikamatwa na walinzi wa chama hicho (Red Brigedi) ambapo walinyang’anya simu zao za za kiganjani, vinasa sauti na kadi ya CHADEMA.

Yusuph alisema kuwa tukio hilo limeuthibitishia umma namna polisi wanavyotumika kufanya vurugu kwenye mikutano yao ikiwemo tukio la utupaji wa mabomu kwenye mkutano ya chama hicho iliyotokea jijini Arusha Juni mwaka jana na kusababisha vifo vya watu wanne na wengine zaidi ya 70 kujeruhiwa vibaya.

Taarifa ya NHIF kuhusu kupeleka huduma za Madaktari Mabingwa mikoani1.0 UTANGULIZI

Pamoja na kutekeleza mpango wa kusogeza huduma karibu na wanachama na wadau kwa maana ya kufungua ofisi mikoani, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya umeanzisha mpango wa kupeleka huduma za Madaktari Bingwa mikoani.

Mpango huu unawahusisha Madaktari Bingwa ambao ki-ukweli ni wachache kutoka katika hospitali zifuatazo:-

  • Hospitali ya Taifa ya Muhimbili;
  • Taasisi ya Mifupa MOI;
  • Hospitali ya Bugando.
Madaktari Bingwa hao wanafanya kazi katika hospitali za mikoa kwa kushirikiana na madaktari waliopo huko mikoani. Madaktari hao ni mabingwa wa:-

Simba haiachani na sare msimu huu?

Kikosi cha Tanzania Prison kilichohceza na Simba leo jioni.

Kikosi cha Simba kilichochuana vikali na timu ya Tanzania Prison uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jana jioni.
(picha: Rashid Mkwinda)

Timu ya kandanda ya Simba ya Jijini Dar es Salaam jana iliondoka kwa sare ya magoli na maafande wa Magereza Tanzania Prison.

Simba ndiyo ilikuwa ya kwanza kujipatia bao katika dakika ya pili ya mchezo baada ya Emmanuel Okwi kutikisa wavu kwa njia ya adhabu ndogo.Adhabu hiyo ilitokana na mchezaji wa Prison Lugano Mwangama kumfanyia madhambi mlinzi wa Simba Ramadhani Singano.