Taarifa kwa viongozi kuhusu urejeshaji fomu za Tamko la Rasilimali na Madeni


Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, inawataarifu Viongozi wote wa Umma nchini kwamba tarehe ya mwisho ya kurejesha Fomu za kutolea TAMKO LA RASILIMALI NA MADENI ya viongozi kwa Kamishna wa Maadili kwa mwaka huu ni tarehe 31/12/2014. 

Fomu hizo za kutolea tamko zimeanza kutolewa na zinapatikana katika Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma makao makuu Dar es Salaam na katika ofisi za Kanda za Mashariki Kibaha, Arusha, Dodoma, Tabora, Mwanza, Mbeya na Mtwara. Pia Fomu hizo zinapatikana katika Tovuti ya

Ushauri kwa wanaoanza Elimu ya Juu mwaka huu

Mwezi huu wa octoba wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na elimu ya juu hapa Tanzania wameanza kuripoti kwenye vyuo walivyopangiwa. Awali ya yote nichukue nafasi hii kuwapongeza wale wote ambao wamepata nafasi ya kuendelea na elimu hii ya juu. Iwe ni kwa nafasi ya cheti, stashahada au hata shahada kuna kazi kubwa umeifanya huko nyuma na sasa unaingia kwenye ngazi nyingine ya elimu.

Leo naomba nichukue muda wako kidogo kukupa ushauri ambao unaweza kuwa msaada mkubwa sana kwako kama utaufuata. Ushauri nitakaokupa hapa sio namna gani ya kusoma maana naamini kwa miaka zaidi ya kumi uliyokaa kwenye mfumo wa elimu, unajua ni jinsi gani ukisoma utafaulu na jinsi gani ukisoma utafeli. Hivyo endeleza mbinu zilizokusaidia nyuma na ziboreshe zaidi ili uweze kupata ufaulu mzuri.

Ushauri mkubwa nitakaokupa hapa ni kuhusu mafanikio na uchumi.

Mpaka sasa umeshaimbiwa sana wimbo huu kwamba nenda shule, soma kwa bidii, pata ufaulu mzuri,

Statoil scholarship for Master Programme in Energy and Petroleum

Background

Since 2011 the University of Dar es Salaam (UDSM), specifically the Department of Chemical and Mining Engineering, the Norwegian University of Science and Technology (NTNU) of Norway and the Angolan University of Agostinho Netto are collaborating under the ANTHEI project to train professionals for petroleum engineering and geosciences at Masters level. Already three batches of a total of 28 Tanzanian students have been enrolled under the program. In this program the students spend one year in Norway for class work and another year at the University of Dar es salaam and the industry for project work and thesis. While in Tanzania the students are under the responsibility of the Tanzanian project coordinator at the University of Dar es Salaam with the support of local professors, NTNU Professors and Statoil Professionals. Statoil is a Norwegian oil Company already engaged in petroleum activities in Tanzania.

Under the same scheme, another batch of 10 students will be granted scholarship next year (2015) to undertake M.Sc. in Petroleum Engineering and in Petroleum Geosciences.  The scholarship covers subsistence allowance (stipend), travel grant to and fro, tuition, insurance and stationeries. The certificate will be issued by NTNU.

M.Sc. Petroleum Engineering and M.Sc. in Petroleum Geosciences

Rais Kikwete ziarani nchini Vietnam


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Katibu Mkuu wa Chama Cha Kikomunisti cha Vietnam Ndugu Nguyen Phu Trong, katika Makao Makuu ya Kamati Kuu ya Chama hicho tawala cha nchi hiyo Jumatatu Oktoba 27, 2014.

Job opportunity at Sikika for a Head of Finance

SIKIKA is a non-governmental organization that advocates for quality health services for all Tanzanians. The organization works to ensure equitable and affordable quality health care services through social accountability monitoring of health systems at all government levels. For more information about Sikika please visit us at www.sikika.or.tz

Sikika is seeking to recruit a Head of Finance who will be reporting to the Executive Director, with the following responsibilities; For more details, click here to read more…

Title: Head of Finance

Work Station: Dar es Saalam

Reports to: Executive Director

If you are interested and satisfy the above requirements you are encouraged to send your application only by e-mail to: [email protected]

Application Deadline: November 10, 2014

Shiriki na fuatilia masuala ya Katiba via ukurasa Facebook


Taarifa rasmi ya Serikali kuhusu uvumi wa mgonjwa wa Ebola Kilimanjaro

TAMKO LA SERIKALI KUHUSU TETESI ZA KUWEPO MGONJWA ANAYEHISIWA KUWA NA UGONJWA WA EBOLA MKOANI KILIMANJARO

Utangulizi

Mnamo tarehe 22 Oktoba 2014, Wizara ilipokea taarifa kutoka Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ya kuwepo kwa mgonjwa aliyehisiwa kuwa na dalili za ugonjwa wa Ebola. Mgonjwa huyu mwanaume ana umri wa miaka 37, na mkazi wa Dar es salaam (Kimara ) ambaye alikwenda Kilimanjaro tarehe 20 Oktoba 2014 katika kijiji cha Kirua kwa ajili ya kusalimia ndugu. Mgonjwa huyu alikuwa na dalili za homa kali ( 38.2 0c), maumivu ya Misuli, kuchoka na maumivu ya kichwa pamoja na maumivu ya koo na kupoteza hamu ya kula.

Mgonjwa huyu anatibiwa katika Kituo cha Afya Shirimatunda, Kilimanjaro kuanzia tarehe 22.10.2014 ambako yupo hapo hadi sasa. Mgonjwa huyu kikazi ni “Land Surveyor” na hufanya kazi zake nchini na nje ya nchi ikiwemo nchi ya Senegali. Mnamo siku za karibuni alikwenda nchini Senegali kwa kazi za mkataba na kurejea nchini mwanzoni wa Oktoba 2014. Hata hivyo, mgonjwa huyu hakuwa na

Powering Africa - Tanzania's 2014-2025 energy reform roadmap to success

Web1_0.png

Tanzania’s 2014-2025 energy reform roadmap to success

The Ministry of Energy and Minerals has published an Electricity Supply Industry Reform Strategy and Roadmap for 2014 to 2025

DAR ES SALAAM, Tanzania, October 27, 2014/African Press Organization (APO)/ -- In its recent Investment Policy Review the OECD cited energy in Tanzania as a “critical bottleneck” and that the problem of reliable energy was the top barrier to doing business in Tanzania. This view was echoed during the Tanzania panel at the Africa Energy Forum in Istanbul in June at which TANESCO and EWURA specifically addressed this point. (www.energynet.co.uk/fr/event/powering-africa-tanzania)

It’s clear that project developers are keen to participate and that a multitude of funds are available to

Maelezo ya Waziri kuhusu huduma dhoofu hospitalini na deni la Serikali kwa MSD

Kuna taarifa katika vyombo vya habari iliyotolewa na Shirika lisilo la Kiserikali la SIKIKA, kwamba serikali haijalipa kiasi cha shilingi bilioni 90 kwa bohari kuu ya dawa na kusababishia ukosefu dawa katika baadhi ya hospitali.

Ni kweli bohari kuu ya dawa imepungukiwa fedha za kununulia dawa, lakini sio kwa kiasi cha kushindwa kutoa huduma kabisa kama inavyoelezwa. Kiasi cha pesa kinachotajwa si kigeni na serikali imekua ikitoa kiasi cha fedha kidogo kidogo ili kuongeza uwezo wa bohari ya dawa iweze kufanya kazi ya kununua na kusambaza dawa.

Katika kukabiliana na hali hii hospitali zote kupitia waganga wakuu wa mikoa na wilaya zimeagizwa kupeleka asilimia 50 ya mapato yanayotokana na uchangiaji kwenda bohari kuu ya dawa.

Taarifa kwa vyombo habari kuhusu ukosefu wa dawa na vifaa tiba

TAMKO LA SIKIKA KUHUSU UKOSEFU WA DAWA NA VIFAA TIBA KATIKA HOSPITALI, VITUO VYA AFYA NA ZAHANATI ZA UMMA NCHINI.


Sikika imesikitishwa na taarifa za hivi karibuni zinazoeleza kuwa na uhaba wa dawa na vifaa tiba muhimu katika vituo vya kutolea huduma vya umma nchini. Upungufu huu unasemekana kuathiri zaidi wananchi wasio na bima za afya.

Matatizo yanayosababishwa na uhaba wa dawa ni makubwa, kwani sio tu yanatishia uhakika wa huduma kwa mgonjwa anapokuwa katika kituo cha huduma za afya lakini pia yanapunguza ari ya kufanya kazi kwa watoa huduma. Aidha, matatizo haya pia yanaathiri ustawi wa jamii na mfumo wa huduma za afya nchini. Hali hii imeathiri wananchi wengi hasa wale wasio katika mfumo wa bima za afya na wale wenye bima zenye wigo mdogo.

Mfanyabiahara ajiua kwa kujifyatulia risasi

Timoth Mroki
Timoth Mroki
Na Mroki Mroki

MFANYABIASHARA wa Arusha anayemiliki kampuni ya Tanzania Bush Camp yenye kambi za watalii katika hifadhi za Serengeti mkoani Mara na Manyara iliyopo katika mikoa ya Arusha na Manyara, Timoth Mroki (36) amejiua kwa kujipiga risasi tatu kifuani akiwa katika baa maarufu ya Arusha Raha iliyopo la Shams, jijini hapa.

Kisa cha kujiua kwake kimetajwa ni kusababisha ajali, baada ya kuligonga gari jingine katika eneo la Mbauda wakati akitokea katika makazi yake yaliyopo eneo la Kwa Mrombo, jijini hapa.

Mmiliki wa KEAR Computer Training akamatwa kwa kuwatapeli Wanafunzi

MAKACHERO wa Jeshi la Polisi Nchini, wamemtia mbaroni mmiliki wa Kampuni ya KEAR Computer Training, Uttu Kingwande, kwa tuhuma za utapeli.

Kingwande anadaiwa kuwatapeli wanafunzi lukuki waliokuwa wakipata mafunzo ya kompyuta katika kituo chake alichokuwa amekifungua katika Shule ya Sekondari ya Mbeya.

Inadaiwa kuwa kituo hicho hakikuwa kimesajiliwa na hivyo alikuwa akijipatia pesa kiujacha ujanja.

Mtuhumiwa huyo alikuwa akitafutwa kwa zaidi ya miezi mitatu sasa, ambapo taarifa za kiuchunguzi

Siku umechelewa shule halafu "unamtaimu" Mwalimu wa zamu getini... we!

THE pupils (above) at Mgulani Primary School in Temeke, Dar es Salaam, peep from the entrance to the school as they either wait for the opportune moment to get inside after their mid-day recess or looking at another interesting spectacle. (Photo by Mohamed Mambo/DAILY NEWS)

Dawa zitapatikana vipi mahospitalini wakati MSD inaidai Serikali bilioni 90?

UHABA mkubwa wa dawa na vifaa tiba umezikumba hospitali nyingi nchini, zikiwemo za Muhimbili na Ocean Road, kutokana na serikali kudaiwa zaidi ya sh. bilioni 90 na Bohari Kuu ya Dawa, (MSD).
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilo la kiserikali linalofuatilia masuala ya afya nchini la SIKIKA, Irenei Kiria, alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa hali hiyo inahatarisha maisha ya wananchi kwa kukosa matibabu.

Irene alisema kutokana na madeni hayo, MSD imesimamisha usambazaji wa dawa katika hospitali za serikali, zikiwemo za rufani na za wilaya, hasa za Mpwapwa na Kiteto, ambazo zinadaiwa mamilioni ya shilingi.