Haya, PAC yaipa TanTrade saa 48 kuhusu yaliko magari 5, pikipiki 8 za Serikali

MAKUCHA ya Bunge, kupitia Kamati yake ya Hesabu za Serikali (PAC) imeendelea kufichua maovu katika idara za Serikali na Mashirika ya Umma, safari hii ikiwa zamu ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara nchini (TanTrade) iliyopewa saa 48 kuwaanika wahusika wa magari matano na pikipiki nane zilizoyeyuka katika mazingira ya kutatanisha.

Mali hizo za umma, zinatajwa kununuliwa na iliyokuwa Bodi ya Biashara ya Nje (BET, sasa TanTrade) na kusajiliwa kwa namba za Serikali (STK), lakini bila maelezo yoyote, zimegeuzwa na kusajiliwa kwa namba binafsi. Maagizo hayo yalitolewa jijini Dar es Salaam jana na Makamu Mwenyekiti wa PAC, Deo Filikunjombe wakati kamati hiyo ikikagua hesabu za mamlaka hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG), Mamlaka hiyo mwaka 2012, ilipokuwa BET, wakati wa Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Nyerere, maarufu kama Sabasaba,

Ushauri wa biashara unazoweza kufanya Mwanafunzi wa Chuo Kikuu

Habari za leo mpenzi msomaji wa AMKA MTANZANIA, karibu tena kwenye kipengele hiki cha ushauri wa changamoto mbalimbali zinazotuzuia kufikia mafanikio. Kwa wiki chache zilizopita kulikuwa na makala ya ushauri kwa wanafunzi wanaoanza Chuo Kikuu, pia tumewahi kuweka makala za ushauri kwa wahitimu wa vyuo vikuu. Leo tutatoa ushauri mwingine kwa wanafunzi wanaoendelea na masomo yao ya vyuo vikuu na vyuo vingine vya elimu ya juu.

Kabla ya kuingia kwenye ushauri huo kwanza tupate maoni ya msomaji mwenzetu:
Habari za kazi, ninakupongeza kwa makala nzuri na za kuelemisha, ninaombi moja kwako utoe makala ya biashara gani au ujasiriamali gani mwanafunzi wa Chuo Kikuu anaweza kufanya huku anaendelea kusoma?
Hayo ndio yalikuwa maoni ya msomaji mwenzetu aliyetaka kujua ni biashara gani au ujasiriamali gani mwanafunzi wa Chuo anaweza kufanya.

Kuna maswali matatu muhimu ya kujiuliza katika swala hili:-

Swali la kwanza, je inawezekana kufanya biashara au ujasiriamali ukiwa Mwanafunzi wa Chuo?

Gharama za kulala Muhimbili sasa ni 5,000/= kwa siku

(picha: wavuti.weebly.com)

Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), imepandisha gharama za huduma hospitalini hapo na sasa mgonjwa atakayelazwa atalazimika kulipa Sh5,000 kwa siku.

Gharama hizo zitalipwa kwa wagonjwa wote wa rufaa, ilisema taarifa iliyosainiwa na Mkurugenzi mtendaji wa hospitali hiyo, Dk Marina Njelekela na kusambazwa kwenye vyombo vya habari.

Taarifa hiyo ilibainisha kuwa gharama mpya zilianza kutumika Oktoba 17, mwaka huu. Hata hivyo, taarifa hiyo haikufafanua uamuzi wa kupandisha gharama hizo.

Alipofuatwa ili kutolea ufafanuzi mabadiliko hayo, Ofisa Uhusiano wa MNH, Aminiel Algaesha

Kontena laangukia daladala na kulipondaLori la mizigo ambalo limefunga tela limeangukia daladala (aina ya Hiace yenye namba za usajili T769 AFP) lililokuwa katika kituo cha mabasi katika eneo la Jet-Lumo.

Daladala hilo lilikuwa limeegeshwa katika kituo cha Kona, mwisho wa lami likisubiri abiria na mara semi-trailer ilipokuwa ikikunja kona, kontena lililokuwa limepakiwa lililiangukia daladala hiyo.

Haijafahamika ikiwa ajali hiyo ilisababisha majuhi ama vifo.

Juhudi za gari la kunyanyua makontena zilishindwa kuzaa matunda kutokana na kuzidiwa na uzito wa kontena ambalo kila likinyanyuliwa lilizidi kushuka chini na kuiponda bodi ya Hiace.

Taarifa ya DAWASCO ya kukatwa maji Dar es SalaamDawasco inawatangazia wakazi wote wa jiji la Dar es salaam na Mji wa Bagamoyo kuwa mtambo wa kuzalisha Maji wa Ruvu Chini utazimwa kwa wastani wa saa 48 kwa siku za Alhamisi na Iijumaa ya tarehe 30 na 31 Octoba 2014, kuanzia saa kumi na mbili asubuhi, ili kuruhusu mkandarasi (Sino-hydro Corporation ltd) kuunganisha bomba la zamani na bomba jipya (cross-connection) katika mtambo wa Ruvu Chini eneo la Chambezi, Bagamoyo.

Kuzimwa kwa mtambo wa Ruvu Chini kutasababisha maeneo yafuatayo kukosa Maji;
Mji wa Bagamoyo, Mapinga, Bunju, Boko, Tegeta, Kunduchi, Salasala, Jangwani, Mbezi beach na

Rais Kikwete aondoka Vietnam kurejea Tanzania

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisindikizwa na wenyeji wake katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Noi Bai jijini Hanoi tayari kuanza safari ya kurejea nyumbani baada ya kuhitimisha ziara yake ya siku sita nchini China na Vietnam leo Oktoba 28, 2014.

Msanii aliyekamatwa na dawa za kulevya apelekwa Segerea

Msanii wa Hip Hop, Rshid Makwiro ‘Chidi Benzi’ akisindikizwa na askari Polisi wakati akiingia katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam jana kujibu mashtaka matatu likiwemo la kukutwa na dawa za kulevya kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Msanii wa muziki wa Hip Hop, Rashid Makwiro ‘Chidi Benzi’ leo amepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na mashitaka matatu likiwemo la matumizi ya dawa za kulevya.

Chid Benz, alipandishwa kizimbani majira ya saa nane mchana, mbele ya Hakimu Warialwande Lema, ambaye alimtaka msanii huyo atolewe nje kutokana na uvaaji mbaya wa suruali yake kwani alivaa ‘Kata Kei’ ili avae vizuri nguo.

Akisomewa mashitaka yake, na Wakili wa Serikali Mwanaamina Kombakono, alidai kwamba mnamo

Africa Diaspora Marketplace III launched at the Tanzanian Embassy in USA

Jeffrey L. Jackson, Senior Private Sector Advisor, USAID speaking about the launch of ADM III. 

The Embassy of Tanzania in Washington, DC hosted the launch of the African Diaspora Marketplace III (ADMIII), on October 27th 2014. ADM is an opportunity for African diaspora members who are involved in businesses in their home country to acquire a grant from the United States Agency for International Development (USAID), which works together with Western Union and Homestrings to provide grants and technical support to these businesses. The Marketplace was initiated in 2009 in

Taarifa ya Wizara kuhusu habari iliyochapishwa na gazeti la Jamhuri

TAARIFA RASMI

Katika gazeti la Jamhuri la Jumanne Agosti 19 – 25, 2014 ISSN No. 1821-8156 Toleo No. 150, zilichapishwa taarifa potofu zenye kichwa cha habari; 

KASHFA IKULU;
  • Nyalandu atumia Leseni ya Rais kuua wanyamapori 704 bure,
  • Watakaouawa wamo pia tembo 8, chui 8, Simba 8, ndege,
  • Wauaji ni Wamarekani marafiki wa Waziri wa Maliasili.
I. Wizara ya Maliasili na Utalii inapenda kuwafahamisha Umma kuwa, tuhuma hizi si za kweli. Tuhuma hizi zimetolewa na watu wenye nia ovu na zimelenga kuchafua jina la Wizara ya Maliasili na Utalii na kumchafua mheshimiwa Waziri Lazaro Nyalandu, kumshushia Heshima, kumdhalilisha kwa umma ili kumpunguzia dhamira, malengo na kasi ya kupambana na ujangili.

Ukweli ni kwamba Familia ya Freidkin ilipewa Leseni Maalum/Leseni ya Rais (Special

Tanzania: "la kutambua ndoa za jinsia moja, hilo tumekataa"SERIKALI ya Tanzania imekataa rasmi kutambua ndoa za jinsia moja (ushoga) kama moja ya agenda za maendeleo katika malengo ya milenia 2015 mpaka 2030 katika mkutano wa Umoja wa Mataifa.

Akizungumza jijini Dar es Salaam kwenye mkutano wa majadiliano ya malengo ya milenia yanayotazamiwa kumalizika mwakani na kuanza malengo mapya, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy amesema serikali ya Tanzania imekataa kutambua ushoga kama moja ya agenda za maendeleo.

“tunatambua haki za binadamu, usawa wa kijinsia kati ya wanaume na wanawake na hata Katiba yetu

Karibu Festival kupambwa na Jhikoman, Zawose, Maembe, Prof. Jay, Barnaba...

Msemaji wa tamasha la Karibu Music Festival, Muslim Nassor ‘Jazzphaa’ (katikati) akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa utambulisho huo.

Wapo pia Prof. Jay, Barnaba, Shilole

Na Andrew Chale

WASANII kutoka ndani na nje wanatarajiwa kupamba tamasha la Muziki la Kimataifa la ‘Karibu Music Festival’ litakalofanyika kwa siku tatu kwenye mji wa Kihistoria wa Bagamoyo, Novemba 7 hadi 9 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari

Haya, Vigogo wa dawa za kulevya wauza mali na "kutoweka"

SIKU chache baada ya kunaswa kwa watuhumiwa wanaotajwa kuwa ni vinara wa kusafirisha na kuingiza dawa za kulevya nchini, hali imeanza kuwa tete kwa vigogo wengine wa biashara hiyo.
Baadhi ya vigogo wakiwemo wafanyabiashara wakubwa nchini, wameanza kukimbia nje ya nchi kukwepa mkono wa sheria, huku wengine wakisubiri hali itulie ndipo wajitokeze.

Hatua hiyo inatokana na askari wa Kikosi Maalumu cha Kudhibiti Dawa za Kulevya kuendelea kuwasaka vinara wa biashara hiyo kimya kimya, ikiwa ni mkakati wa kusambaratisha mtandao wa biashara hiyo haramu nchini.

Habari za kuaminika kutoka ndani ya kikosi hicho, zinasema kuwa operesheni hiyo imekuwa ikifanyika kwa usiri mkubwa, kiasi cha mamlaka zingine kutofahamu kinachoendelea.

Bomu lategwa TBC na jirani na wanapokaa Polisi; JWTZ yatliegua

Bomu lenyewe kama linavoonekana katika picha.

Jeshi la polisi kwa kushirikiana na Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wamefanikiwa kulipua bomu lililotegwa katika eneo la kituo cha kurushia matangazo kilichopo Mshangano cha Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Songea Mkoani Ruvuma siku ya jana majira ya saa moja jioni.

Bomu hili linalosadikiwa kutengenezwa kienyeji na watu wasiojulikana lilitegwa hatua zinazokadiriwa thelathini kutoka kitika kituo kilipo katika eneo ambalo askari wa usalama barabarani wanakaa kwa ajili kufanya kazi zao za kila siku.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela amesema kwa mujibu wa wataalamu wa

Walipoteza cheti cha NECTA kulipia 100,000/= wapate nakala

BARAZA la Mitihani la Tanzania (NECTA), limeanzisha utaratibu wa kutoa nakala za vyeti kwa watahiniwa waliopoteza vyeti vyao kwa gharama ya sh. 100,000.

Utaratibu huo utawanufaisha watahiniwa waliohitimu kuanzia mwaka 2008, ambao vyeti vyao viliwekwa picha.

Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk. Charles Msonde, akizungumza jijini Dar es Salaam jana, alisema hatua hiyo itapunguza changamoto zilizokuwa zikiwakabili watahiniwa waliopoteza vyeti vyao kwa sababu mbalimbali.