Kagera Aluminum & Welding Metal Fabrication services, East Africa


The Network of Kagera Aluminum & welding Metal fabrication

Kagera Aluminum & welding Metal Fabrication Workshop deals with welding and fabricating different things such as:
  1. Fabricating grills,steel windows,sliding windows,doors,Fences and gates.
  2. Fabricating and joining materials of houses of aluminum windows, doors, office partitions, tables, film rooms etc.
  3. We do shipping and fitting the materials we made for our clients.
We are able to move every where in East Africa (mobile welding workshop) in countries like

Msaada kuhusu TRA na ukaguzi wa mali zangu

Update/Taarifa mpya imeongezwa yenye maoni na ushauri niliopokea kupitia WhatsApp
  • Ndiyo, ni haki yao, yes. But there is a right to refuse them entrance hadi ujiandae.
  • Ndiyo. Ila mnaweza kuwaomba muda wa kujiandaa na kuweka vitabu vya stock sawa.
  • Ndiyo, na TRA wanayo access ya akaunti yako bank.
  • Sina uhakika wa hayo mengineyo ya stoo.
  • Wana uwezo wa kisheria kukagua na ku audite mali yote, ila wanafanya hivyo kwa kutoa notice kwako. Hii ni kwa mujibu wa sheria kwakuwa wewe ni mbia wa serikali kwenye ukusanyaji kodi.
----------------- update ends / mwisho wa taarifa mpya ---------------------

Mdau anaomba ushauri na maelekezo kutokana na uzoefu wako kuhusu maswali haya:
  1. Je, TRA wanayo haki ya kuja kuhesabu mali iliyoko dukani kwangu?
  2. Je, TRA wanaruhusiwa kufuatilia na kujua ninakohifahi mali (yaani stoo au dogown) na kuzihesabu?

Most sub-Saharan USA immigrants among best educated; Tanzanians likely to have 4-yr degree


Immigrants from several Anglophone African countries (Cameroon, Nigeria, Tanzania, Uganda, and Zimbabwe) were more likely to have at least a four-year degree, while those born in Cape Verde, Eritrea, Liberia, and Somalia, though accounting for a small share of the total sub-Saharan population, were disproportionately refugees and less likely to have a college degree.
Most sub-Saharan African immigrants who obtain lawful permanent residence in the United States (also known as receiving a green card) arrive as immediate relatives of U.S. citizens, refugees, or through the Diversity Visa Lottery. Compared to the total foreign-born population, sub-Saharan African immigrants were among the best educated and less likely to be Limited English Proficient (LEP). Sub-Saharan Africans also had a higher rate of health insurance coverage.
Full article: MigrationPolicy.org - Sub-Saharan African Immigrants in the United States

10 Bora ya Wasichana, Wavulana, Shule, Mikoa Wilaya katika Matokeo ya Mtihani STD VII Kitaifa 2014

BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA
                                               
TAARIFA YA MATOKEO YA MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI (PSLE) MWAKA 2014

1.0       UTANGULIZI

Katika Mkutano wake wa 102 uliofanyika tarehe 04/11/2014, Baraza la Mitihani la Tanzania liliidhinisha kutangazwa kwa matokeo ya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi ulifanyika kuanzia tarehe 10 hadi 11 Septemba, 2014.  Watahiniwa walifanya mtihani huo kwa kutumia Karatasi Maalum za Optical Mark Reader- OMR” ambazo zilisahihishwa kwa kutumia Mfumo wa kompyuta.  Matumizi ya teknolojia ya OMR kwenye Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi yalianza mwaka 2012.

2.0       USAJILI WA WATAHINIWA

Jipakulie kitabu chenye elimu ya jinsi ya kuwa mjasiriamali, mawazo mbalimbali ya biashara, kutafuta masoko, usimamizi wa fedha, huduma kwa wateja, nkTafadhali bofya hapa ili kujipakulia pakua faili (pdf) ili kufaidi elimu ya ujasiriamali na biashara.

Imeandaliwa na feminahip.or.tz: Femina HIP, "Jenga maisha yako"

Kauli ya Waziri kuhusu taarifa za Ndege ya Rais na Viongozi wa China kuhusishwa na vipusa vya ndovu kutoka Tanzania


Iliyopachikwa hapo chini ni nukuu ya kauli ya Waziri kuhusiana na habari iliyochapishwa na vyombo mbalimbali vya habari vya Kitaifa na Kimataifa baada ya utafiti uliofanywa na shirika moja (video imepachikwa hapo juu) kusema kuwa viongozi wa China walitumia ndege ya Rais wa nchi yao kujinunulia 'kwa fujo' vipusa vya tembo kutoka Tanzania.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe

KAULI YA WAZIRI WA MAMBO YA NJE NAUSHIRIKIANO WA KIMATAIFA KUHUSU SHUTUMADHIDI YA SERIKALI ZA CHINA NA TANZANIAKUJIHUSISHA NA BIASHARA HARAMU YA PEMBE ZANDOVU INAYOTOLEWA KWA MUJIBU WA KANUNI YA 49(1) YA KANUNI ZA KUDUMU ZA BUNGE TOLEO LA 2013


Mheshimiwa Spika,

Siku ya Jana Vyombo vya Habari mbalimbali vya Ndani na Nje ya Nchi vilitoa habari kwamba ujumbe wa Rais wa China uliokuja nchini Miezi 18 iliyopita ulijihusisha na ununuzi wa pembe za ndovu nchini. Chanzo cha habari hizo ni taarifa ya taasisi isiyo ya kiserikali ya nchini Marekani ijulikanayo kama Environmental Investigation Agency (EIA). Habari hiyo imekwenda mbali zaidi kuituhumu nchi yetu na viongozi wake kutojali, wala kushughulikia tatizo la biashara haramu ya pembe za ndovu.

Mheshimiwa Spika,

Ninapenda kupitia Bunge lako tukufu kuutaarifu umma wa watanzania na dunia kwa ujumla kwamba madai yaliyotolewa na NGO hiyo ya Marekani ya kuihusisha ziara ya kihistoria ya Rais wa China kutembelea Tanzania kama nchi ya kwanza toka aingie madarakani na biashara ya pembe za ndovu hayana ukweli wowote. Vilevile, madai ya kwamba Serikali ya Tanzania

Majina ya waliochaguliwa kwenye usaili wa kazi TBS

Dokta... Niandikie nikacheki afya India

Polisi yamshikilia mwanafunzi aliyetaka kujiua baada ya kunusurika kubakwa na baba'ke mdogo

Polisi mkoani Tanga, inamshikilia mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Old Tanga (16), kwa tuhuma za kutaka kujiua kwa sumu baada ya jaribio la baba yake mdogo kumbaka kushindikana.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Fraisser Kashai alisema mwanafunzi huyo alitaka kujiua juzi sasa tatu usiku katika eneo la Barabara ya 20, Mtaa wa Ngamiani.

Kamanda Kashai alisema binti huyo alikunywa sumu ya panya, ambayo hata hivyo ilishindwa

Ayafanyayo Warioba, aliyafanya Nyerere pia!

(picha: JuliusNyerere.info)

WAVURUMISHAO makombora dhidi ya Jaji Joseph Warioba wamekuwa wakitoa hoja kwamba mzee huyo muda wake wakuzungumzia suala la katiba mpya ulishamalizika kwa minajili kuwa Tume yake ya kukusanya maoni ya Katiba mpya ilishavunjwa.

Kelele zimepigwa katika bunge maalum la katiba, mtaani wanasema “mzee pumzika muda wako umekwisha” hawataki tena atumie uhuru wake wa kikatiba kuzungumzia mambo ambayo yeye anaona hayajaenda sawa, wao wazungumze yeye anyamaze, au sasa hivi kuna sheria inasema ni wakati wa Chama fulani tu peke yake kujimwaya mwaya uwanjani na kuipamba katiba pendekezwa.

Nafurahi wanaomkosoa Mzee Warioba wamekuwa wakijinadi kuwa wao ni wafuasi wazuri sana wa hayati Mwalim Julius Nyerere, wamekuwa wakitusihi kila uchao tuige yale mazuri aliolifanyia taifa

Katiba ya Wananchi - (Shairi)


Katiba ya wananchi, mwafaka wa taifa
Kuna kucha hakukuchi, isije kuwa maafa
Kuandika ya kukidhi,yahitaji maarifa
Katiba ya wananchi, nauliza tutapata?

Iokoe wakulima, wavuvi na walemavu
Uchumi ukue hima, iondoe udumavu
Ilinde raia wema, viongozi wasikivu
Katiba ya wananchi , nauliza tutapata?

Watawala watambue, kilio wakisikie
Ukasuku waambae, waikatae ya kale
Machakato uenee, na demokrasi ikue
Katiba ya wananchi, nauliza tutapata?

Kukaa peke Dodoma,kuichambua rasimu
Kilio cha kina mama, haki zao ni adimu
Ile siku ya kiama, waso haki ni dhalimu
Katiba ya wananchi, nauliza tutapata?

Beti tano nakomea, kalamu naweka chini
Katiba kuongelea,sitachoka ulimini
Tunataka ya kumea, iuondoe uduni
Katiba ya wananchi,nauliza tutapata?

Nova Kambota,

0712 -544237, 
Alhamisi, Novemba 6, 2014

Raia wa kigeni waingiza dawa za kulevya Tanzania kwa meliRAIA 13 wa Iran wamekamatwa wakiingiza nchini dawa za kulevya aina ya heroin zaidi ya kilogramu 41 yenye thamani ya shilingi bilioni mbili.

Wairani hao wamepandishwa kizimbani Jumatano Oktoba 5, 2014 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma ya kuingiza nchini dawa hizo za kulevya aina ya Heroin zenye thamani ya zaidi ya Sh. bilioni 2.

Walisomewa mashitaka na Wakili wa Serikali, Helen Moshi, mbele ya Hakimu Janeth Kaluyenda na kusomewa mashitaka na wakili wa serikali Hellen Moshi.

Washitakiwa hao Mansour Rais, Kheri Mohamed, Rasul Barh, Gulam Rezar, Nawab Bari, Said

Amtuhumu mtoto kuiba 4,500/=; Amchana kwa wembe; Atia vidonda chumviPOLISI wanamshikilia Tausi Omary (30), mkazi wa kata ya Chamwino, Manispaa ya Morogoro kwa tuhuma za kujeruhi mtoto wa dada yake, Jafari Mashaka (11) kwa kumchanachana mguuni kwa wembe na kisha kuweka chumvi kwenye vidonda, kwa madai ya kumwimbia fedha kiasi cha Sh 4,500.

Mashaka, mwanafunzi wa Memkwa wa darasa la tatu katika shule ya msingi Kiwanja cha Ndege, alikutwa na majanga hayo, majira ya saa 12 ya asubuhi ya Novemba mosi mwaka huu, nyumbani kwao wanakoishi mtaa wa Kiwalani, kata ya Chamwino.

UDOM inauarifu umma kuwa wafuatao si waajiriwa wake

TAARIFA KWA UMMA

 BWANA CHRISANTUS LUCAS MILANZI

Bwana Chrisantus Lucas Milanzi, mzaliwa wa Masasi Mtwara, ambaye picha yake inaonekana hapo juu, si mwajiriwa wa Chuo Kikuu cha Dodoma.

Chuo hakihusiki na muamala wowote unaofanywa na mhusika kwa niaba ya Chuo. Wananchi wenye malalamiko kuhusiana na miamala iliyofanywa au inayofanywa na muhusika kwa niaba ya Chuo wayafikishe kwenye vyombo vya dola kwa hatua za kisheria.

Wananchi wanaombwa kuzingatia kwamba Chuo Kikuu cha Dodoma kina taratibu za kuendesha shughuli zake kwa mujibu wa sheria.
Bw. Tito Ivan William

Chuo Kikuu cha Dodoma kinapenda kuutaarifu umma kuwa Bwana Tito Ivan William, mzaliwa wa Kijiji cha Mtumba - Manispaa ya Dodoma, ambaye picha yake inaonekana hapo juu, sio mwajiriwa wa Chuo Kikuu cha Dodoma kuanzia tarehe 31 Januari 2014.

Chuo Kikuu cha Dodoma hakitahusika na makubaliano yoyote yatakayofanywa na mhusika kwa niaba yake. Malalamiko yoyote (kama yatakuwepo) kuhusiana na mhusika, yapelekwe kwenye vyombo vya dola kwa hatua za kisheria.

Tunatanguliza Shukrani kwa Ushirikiano

IMETOLEWA NA OFISI YA UHUSIANO – CHUO KIKUU CHA DODOMA

www.udom.ac.tz