Ni imani tu! Kisayansi supu ya pweza, karanga, muhogo mbichi haviongezi urijali - Daktari

Dk Cuthbert Maendaenda akiwatwanga lekcha wahariri mbalimbali mjini Morogoro

ULAJI wa supu ya pweza, karanga mbichi, muhogo mbichi, mbata kwa dai kwamba vinaongeza urijali kwa wanaume kumeelezwa kuwa ni dhana potofu inayostahili kupigwa vita kwa kuwa haina uhusiano kati ya urijali wa mwanaume na virutubisho vinavyotolewa na vyakula hivyo.

Kauli hiyo imetolewa na Dk Cuthbert Maendaenda wakati akitoa mada yake katika semina ya wahariri iliyofanyika mkoani Morogoro iliyojadili nafasi ya wanaume katika kuleta mabadiliko katika jamii juu ya afya ya uzazi na ujinsia.

Dk Maendaenda ambaye alikuwa akijibu maswali pia kuhusiana na dhana

Lapitishwa Azimio la Arusha la Kukabiliana na Ujangili

Wawakilishi kutoka Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Kenya, Malawi, Uganda, Mozambique, Tanzania, na Zambia wakisaini Azimio la Arusha lenye lengo la kukabiliana na ujangili na kuendeleza wanyama kabla ya Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda (wa tatu kushoto) kufunga rasmi mkutano huo uliomalizika jana jijini Arusha.

JUMUIYA ya kimataifa imepitisha Azimio la Arusha lenye lengo la kukabiliana na ujangili na kuendeleza wanyama.

Azimio hilo limepitishwa baada ya mkutano wa siku mbili ambapo pia imekubalika kwamba hali ya baadae ya wanyama barani Afrika ni suala linalohitaji uwajibikaji wa pamoja.

Aidha nchi za Afrika zimetakiwa kuukomesha ujangili na kufanya juhudi ya kuhakikisha wanyama walio katika hatari ya kutoweka wanalindwa na kuhakikisha kundi hilo linakua.

Wanyamama ambao kwa sasa wapo hatarini kutoweka ni tembo, faru na simba.

Chuo cha Kilimo Nice Dream hakijasajiliwa; Wanafunzi watelekezwa siku 5 bila chakula


Wakipata chakula cha mchana baada ya wananchi wa Ilemi kuwachangia. Wanachama wa CHADEMA walichangishana na kuapata debe 7 za mahindi na fedha taslimu shilingi 20,000/=
Wanachuo 48 wa Chuo cha Kilimo cha Nice Dream kilichopo mtaa wa Mapelele Kata ya Ilemi Jijini Mbeya wanakabiliwa na ukosefu wa chakula baada ya uongozi wa Chuo hicho kuwatelekeza na kutokomea kusikojulikana.

Hayo yamebainishwa na Diwani wa Kata ya Ilemi Mheshiwa Furaha Mwandalima baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wanachuo hao na kufika Chuoni hapo na kujionea hali halisi.

Mwandalima alichukua hatua za haraka za kumtafuta Mstahiki Meya ambaye alimshauri kutoa taarifa kwa Mkuu wa Wiliya ya Mbeya ili kupata mustakabali wa suala hilo.

Hata hivyo lilitolewa agizo la kuorodhesha majina ya wanafunzi na mahali wanakotoka ili kuwarudisha makwao na Chuo kifungwe kutokana na Chuo hicho kutosajiliwa rasmi na kwamba kilikuwa kinaendeshwa kijanja na wanachuo hao wamelipa malipo ya awali zaidi ya shilingi laki tano.

Zaidi ya wanafunzi 40 wanatokea Mkoa wa Kagera na wawili wakitokea

Leo Mkanyia - Mwasisi wa Swahili Blues anayetikisa Kimataifa



Gazeti la The Citizen la Tanzania linamwita 'lulu iliyofichika' hidden gem, kwa kimombo). Huyu ni Leo Mkamia, msanii wa Kitanzania na mwanzilishi wa aina ya muziki ujulikanao kama 'Swahili Blues.'

Siku chache zilizopita, Leo alirekodi wimbo wake mpya uitwao 'Pamoja.' Miongoni mwa yatakayoonekana katika video ya wimbo huo ni performance ya kihistoria ya msanii huyo katika moja ya vyuo vikuu vikubwa hapa Uingereza, Nottingham University, ambapo Leo alifanikiwa kuwaimbisha Kiswahili baadhi ya wahadhiri na wanafunzi wa chuo hicho kikuu. Katika shughuli hiyo, Leo aliimba na kwaya ya Nottingham Academy.

Kinachomfanya Leo kuwa msanii wa kipekee kutoka Tanzania kuwa na

Barabara ya Ukonga Mazizini - Moshi Bar iliyogharimu milioi 90/=



Hii ndiyo ile barabara ya Ukonga Mazizini- Moshi Bar ambayo inadaiwa kugharimu kiasi cha shilingi milioni 90 kuikarabati kwa kiwango cha changarawe kwa umbali wa kilometa tatu. Picha hizi ni madimbwi ya mwanzo tu ya hizo kilometa tatu.

Wimbo aliotungiwa Rais Kikwete na Lokassa ya Mbongo

Meneja TANESCO azungumzia kukatika umeme Ilala

Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wa Ilala, Mhandisi Athanasius Nangali ametoa ufafanuzi kuhusiana na kukosekana kwa huduma ya umeme katika maeneo kadhaa ya Wilaya ya Ilala kuanzia jana usiku.

Nangali ametaja kuwa chanzo kikubwa cha kukosekana kwa huduma hiyo ni kutokana na hitilafu kubwa kwenye moja ya transfoma za kusambaza umeme, licha ya mvua kubwa inayonyesha.

"...ni kwamba kumetokea hitilafu, katika kituo chetu kidogo cha kupoozea umeme pale Gongo la Mboto, kwa hiyo imesababisha maeneo ya Gongo la Mboto pamoja na maeneo yaliyo karibu na hapo kukosa umeme, lakini mafundi tayari wako pale, wanaendelea na kazi tangu usiku, na tunajitahidi ili tuhakikishe leo baadaye umeme uwe umerudi katika maeneo yote yanayoathirika sasa hivi." amekaririwa akizungumza na TBC (katika taarifa iliyosomwa saa saba mchana wa leo).

Maeneeo yaliyoathirika yametajwa kuwa ni Gongo la Mboto, Vingunguti na Kiwalani.


90% ya Wanaume walioshuhudia wenzi wao wakijifungua wameathirika kisaikolojia

“Hatua ya kujifungua inatisha. Ni wanaume wachache ambao wanaweza kushuhudia wenzi wao wakijifungua kisha wakaendelea kuwa katika hali ya kawaida kisaikolojia,” anaanza kuelezea Dk Matilda Ngarina.

“Ni tukio la kuogopesha. Linahitaji ujasiri wa ziada. Wanaume waliojaribu kushuhudia wenzi wao wakijifungua asilimia 90 wameathirika kisaikolojia,” anasema.

Dk Ngarina ni miongoni mwa madaktari bingwa wa magonjwa ya wanawake na uzazi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

Anaeleza baadhi ya athari za kisaikolojia walizopata wanaume hao, zimesababisha wengine kujikuta hawatamani tena kutungisha mimba.

“Wapo wanaume wengine waliochukua uamuzi wa kuomba wake zao

Polisi: Wanawake wawajibike kinyumba kwa waume zao

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Jafari Mohamed amewasihi wanawake walioolewa kuwajibika katika masuala ya unyumba kama maandiko ya dini yanavyoelekeza.

Kamanda huyo alitoa wito huo baada ya kutakiwa kutoa taarifa ya kukatwakatwa na panga kwa mwanamke mmoja kutokana na kukataa kufanya tendo la ndoa na mumewe kwa sababu ya uchovu.

Kamanda Mohamed alisema alikuwa hajapata taarifa za kutokea tukio hilo, lakini akashauri wanawake walioolewa kuwajibika katika masuala ya unyumba ili kupunguza migogoro ya ndoa.

Mwanamke huyo mkazi wa Sigunga wilayani Uvinza, Jasmin Kassim alilazimika

EDCTP and TDR offer first joint Clinical R&D Fellowships

Members of clinical research teams from low- and middle-income countries (LMIC) are now invited to apply for the EDCTP-TDR Clinical Research and Development Fellowship scheme. Successful candidates will be placed with leading product development organisations, including pharmaceutical companies and product development partnerships - the 'host organisations'- for a period of up to 24 months.

A total of 25 fellowships is available for this call; 20 product development organisations have offered to host fellows. The host organisations will train individuals to develop specialist product development skills not readily taught in academic centres or public research institutions. On returning to their home organisations, the fellows are expected to become an important resource for

Sherehe za jando Butiama



Wanamwita "Dokta" wa kijiji cha Ryamisanga wilayani Butiama akiendelea na shughuli yake ya kumtahiri kijana kwa dakika 17 bila ganzi.



Baadhi ya vijana ambao wameshatahiriwa wakimtizama mwenzao ambaye anafanyiwa tohara

Finalist for Emerging Designers Competition