Rais Kikwete aendelea vyema baada ya upasuaji

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na daktari Bingwa Mpasuaji Edward Shaeffer muda mfupi kabla ya kuingia kwenye chumba cha upasuaji uliofanyika katika Hospitali ya Johns Hopkins iliyopo Baltimore Maryland Marekani Jumamosi asubuhi.Upasuaji huo uliochukua muda wa saa moja na nusu ulifanyika salama.

Habari kutoka hospitalini hapo zinasema Rais Kikwete anaendelea vyema na leo asubuhi alianza mazoezi ya kutembea, kuashiria kwamba mambo yote ni mswano. Tutaendelea kwuashirikisha taarifa ya maendeleo yake mara kwa mara. Tuzidi kumuombea apate nafuu haraka ili arejee nyumbani
kulijenga Taifa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alfajiri ya jana, Jumamosi, Novemba 8, 2014, alifanyiwa upasuaji wa tezi dume (prostrate) katika Hospitali ya Johns Hopkins iliyoko Baltimore, Jimbo la Maryland, Marekani.

DJ JD na DJ Fast Eddie warejesha muziki wa disko kileleniDJ JD akiwa kazini katika ukumbi wa Isumba Lounge jijini Dar es salaam usuiku wa kuamkia leo. Yeye na DJ Fast Eddie wameweza kurejesha utamu wa wapenzi wa muziki kwenda disco kwa wingi kama ilivyokuwa enzi hizo. Hapo Isumba ni mambo ya Old Skul na Mayenu kwa

Lowassa azindua helikopta ya Kanisa la Ufufuo na UzimaMbunge wa Jimbo la Monduli, Mhe. Edward Lowassa akiiingia ndani ya helikopta kuashiria kuizindua rasmi kwa safari mbali mbali za kihuduma ya kiroho, itakayotumiwa na Mchungaji Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima.Lowassa akiteta jambo na rubani wa helikopta hiyo muda mfupi baada ya kuizindua.Helikopta iliyozinduliwa ikipaa kuondoka uwanjani hapo na baadae kurudu mara baada ya kuzinduliwa na Mh. Lowassa.

Zitto ajibu mashambulizi dhidi yake, PAC


Nashambuliwa, tunashambuliwa! PAC tunasema “Hatutetereki”

Zikiwa zimebaki siku chache kabla ya Kamati ninayoongoza ya PAC kuwasilisha Bungeni Taarifa Maalumu kuhusu ukaguzi maalumu wa akaunti ya Tegeta Escrow, kumekuwa na kampeni za chini chini zinazoendeshwa kwenye korido za Bunge na kwenye mitandao dhidi yangu binafsi na baadhi ya wabunge waliosimama kidete dhidi ya wizi wa fedha kutoka Benki Kuu ya Tanzania akaunti ya Escrow.

Baadhi ya tuhuma nimezipeleka kwenye vyombo vya dola ili zichunguzwe kwani zina vielelezo vya mahala pa kuanzia (kama leseni ya udereva ya mwanamke anajulikana kama Vivian Emmanuel Sirikwa na muhuri wa kampuni ya uwakili inayomilikiwa na Bwana Joseph Mkandege).

Baadhi ya Tuhuma

Baadhi ya tuhuma nitazijibu moja baada ya moja.

Mchezaji bora wa mwezi "Sure Boy" akabidhiwa tuzo yake

Kaimu Katibu Mtendaji wa Bodi ya Ligi Stephen Mguto (kulia) akimkabidhi tuzo Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa mwezi Oktoba,Abubakar Salum "Sure Boy" katika sherehe iliyofanyika kwenye uwanja wa Azam, Chamazi jijini Dar esSalaam jana.

KIUNGO mkabaji wa Azam FC, Salum Abubakar”Sure Boy”aliyeibuka Mchezaji Bora wa Oktoba juzi alikabidhiwa zawadi ya shilingi milioni 1/= na kombe dogo.

Makabidhiano hayo yalifanyika muda mfupi kabla ya mechi ya raundi ya saba kati ya mabingwa watetezi Azam FC na Costal Union katika mechi ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara iliyochezwa nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam katika uwanja wa Chamazi, ambapo Azam FC waliichapa Coastal Union 2-1. 

Akizungumza na gazeti hili jijini Dar es Salaam juzi,Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa, alisema kampuni yake itakuwa ikitoa zawadi kila mwezi kwa mchezaji anayefanya vizuri.

How to choose the right sunglass according to the shape of your face

​This Chart Helps You Choose the Best Sunglasses for Your Face Shape

via LifeHacker: ​This Chart Helps You Choose the Best Sunglasses for Your Face Shape