Serikali yakifunga kile chuo 'feki' cha Kilimo

Kulia ni Richard Mchomvu mkuu wa Polisi wilaya ya Mbeya akiwa na jalada la uchunguzi kuhusiana na chuo hicho.

Serikal imekifunga Chuo cha Kilimo na Mifugo cha Nice Dream kilichopo mtaa wa Mapelele Kata ya Ilemi Jijini na kuwataka wanachuo wa chuo hicho kuondoka chuoni hapo baada ya siku tatu.

Agizo hilo lilitolewa na Kaimu Katibu Tawala Wilaya ya Mbeya Bi. Quip Mbeyela aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Daktari Norman Sigala na kwamba Serikali itagharamia chakula kwa siku tatu ambapo Serikali ilikabidhi shilingi laki tatu kwa Mtendaji Kata Bi Gladness Sapuka kwa ajili ya

Mazungumzo ya Frank Mtao na Salum Mwalimu kuhusu muungano wa CUF, CHADEMA, NCCR-Mageuzi

Vyama kadhaa nchini Tanzania vimetia saini maafikiano ya ushirikiano kwa ajili ya kukiondoa chama tawala (Chama Cha Mapinduzi -CCM) madarakani.

Mtangazaji wa SBS Radio, Frank Mtao alizungumza na Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Zanzibar, Salum Mwalimu kuhusu muungano huo.Baada ya Mbatia (NCCR-Mageuzi) Makyao (CHADEMA) atangaza kuwania Vunjo ya Mrema (TLP)

Mbunge anayepambana kulichukua Jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro kwa tiketi ya chama cha NCCR-Mageuzi James Mbatia amejikuta katika wakati mgumu sasa kutokana na mgombea Exaud Makyao kutangaza nia ya kugombea jimbo hilo kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Akitangaza nia yake ya kulinyakua Jimbo hilo linalozozaniwa na wababe wawili wenye historia tofauti katika medani ya siasa hapa nchini, katika mkutano wa kampeni kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa katika kijiji cha Holili wilayani Rombo mkoani hapa, Makyao aliweka bayana kuwa ana ubavu wa kupambana na Mbatia.

Makyao aliongeza kusema kwamba ujio wa Mbatia katika Jimbo la Vunjo kumeibua maswali mengi kutokana na kwamba wakazi wa jimbo hilo hupiga kura ya ndio kwa mgombea ambaye wanamfahamu kwa muda mrefu.

“Mbatia haeleweki alikotokea, ndio changamoto kubwa hapo la sivyo licha ya

Discussion on USAID African Diaspora Marketplace III

Discussion with Jeffrey L. Jackson, Senior Private Sector Advisor, USAID, Barbara Span, Vice President, Global Public Affairs, Western Union, Eric-Vincent Guichard, CEO, Homestrings and Zelalem Dagne, ​ CEO, Global Tracking before the launch of the African Diaspora Marketplace III (ADM III), on October 27th 2014 at The Embassy of Tanzania in Washington, DC.
Watch the video embedded below...

Mikataba ya nchi...Walimu wakamatwa wakifanya mtihani wa Kidato cha IV Taifa

Walimu wawili wa Shule ya Sekondari ya Embarway wanashikiliwa na polisi wilayani Ngorongoro wakituhumiwa kufanya mtihani wa kidato cha nne ofisini.

Licha ya walimu hao kukamatwa pia waliokuwa wasimamizi wa ndani wa mitihani kwenye shule hiyo, wameondolewa kutokana na uzembe.

Kaimu ofisa elimu wa Wilaya ya Ngorongoro, Chacha Megewa alidai walimu hao, Jakob Jadie na Reginald Boniface, walikamatwa wakati wakifanya mtihani wa historia.

Alisema walikamatwa Novemba 5 walikamatwa na msimamizi mkuu wa mitihani, Faustine Bura baada ya kuingia ghafla katika ofisi ya mwalimu mkuu.

“Msimamizi alikuwa anafuata moja ya fomu ofisi ya mkuu wa shule, baadaye aliita polisi na kuwakamata,” alisema.

Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas jana hakupatikana kuelezea tukio hili, lakini polisi Kituo kidogo cha Ngorongoro ilithibitisha kukamatwa kwa walimu hao.

Baada ya Mwinyi, Warioba kupigwa, Serikali "kupitia upya mpango wa ulinzi wa viongozi wote waliostaafu"


Serikali inapitia upya ulinzi wa viongozi wastaafu ili kuepuka fedheha iliyotokana na vurugu alizofanyiwa Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba hivi karibuni.

Mpango huo umeelezwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue mwishoni mwa wiki, akisema Serikali imekerwa na kufedheheshwa kutokana na tukio hilo lililotokea wakati wa mdahalo wa Katiba Inayopendekezwa katika Hoteli ya Blue Pearl, Dar es Salaam Novemba 2, mwaka huu.
“Kimsingi tutakachokifanya ni kupitia upya mpango wa ulinzi wa viongozi wote waliostaafu, japokuwa huwa tunafanya hivyo mara kwa mara, lakini kwa hili la Mzee Warioba tunaliangalia kwa umakini wake.
“Tumekerwa sana na tukio lile, halikutufurahisha hata kidogo kama Serikali kwa kuwa limemvunjia heshima Mzee Warioba, yule ni mzee wetu, anahitaji heshima, kwanza heshima yake na ulinzi.”
Kauli hiyo ya Sefue imekuja wakati mdahalo huo uliovunjika baada ya Mzee

Salamu za rambirambi za Rais Kikwete kwa msiba wa "Amigolas"

Khamisi Kayumbu "Amigolas"

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Profesa Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa Dkt. Fenella Mukangara kuomboleza kifo cha Mwanamuziki Muasisi wa Bendi Maarufu ya Twanga Pepeta, na baadaye Kiongozi wa Bendi ya Ruvu Star, Khamisi Kayumbu maarufu kama Amigolas (pichani).

“Nimehuzunishwa na kusikitishwa na taarifa za kifo cha Mwanamuziki

Zaidi ya Wanadiaspora 400 wajitokeza kwenye Career Africa New YorkSophia Yona mwanadiaspora wa New York akiuliza jambo kwa mwakilishi wa Exim Bank Bwn. Dinesh Arora kwenye Career Africa iliyofanyika jiji lisilo lala New York City ndani ya hotel ya Hilton iliyopo mtaa wa 1335 avenue of americas, New York New York 10019 na Wana-diaspora takribani 400 walijitokeza kwenye Careear Africa hiyo iliyokua imeandaliwa na