Hali halisi Mrema alipoketi kitako na 'watu wake' jimboni


Msimamizi mkuu wa (MUWSA) Kituo cha Himo Brucevictor Sangawe akitoa ufafanuzi kwa wananchi mbele ya mbunge wa jimbo la Vunjo, Agustine Mrema juu ya upatikanaji wa maji kwa wakazi wa maeneo ya ukanda wa juu katika mji wa Himo.

DKT International yazindua kondomu mpya za Bull na Trust

Rais wa DKT International Christopher Purdy akizungumza 
Macmillan George to Data Vision International akitoa ripoti ya tabia za kimapenzi kwa wakazi wa Dar es Salaam

Shirika la DKT International limezindua kondomu mpya za Bull na Trust. Akizungumza katika uzinduzi huo, rais wa DKT ndugu Christopher Purdy alisema nia hasa ya kuleta bidhaa za kondomu nchini ni kusaidia katika jitihada za kukabiliana na uzazi wa mpango na pia magonjwa ya zinaa.

Kauli ya FEMACT kuhusiana na vurugu katika mdahalo wa 02.11.2014

TAMKO LA FEMACT KUHUSU VURUGU ZILIZOTOKEA KATIKA MDAHALO KUHUSU KATIBA PENDEKEZWA KATIKA HOTEL YA BLUE PEARL UBUNGO DAR ES SALAAM TAREHE 2 NOVEMBER 2014


Sisi Mashirika yapatayo 50 yanayotetea Usawa wa Kijinsia, Haki za Binadamu, Demokrasia, Utawala bora, Maendeleo na Ukombozi wa Mwanamke Kimapinduzi (FEMACT) tumekuwa tukifuatilia kwa karibu mchakato wa katiba unavyokwenda tangu ulipoanza pamoja na changamoto zinazojitokeza bado kuna fursa ambazo wananchi wameweza kushirikishwa na kutia matumaini ya kupata katiba mpya.

Jambo la kusikitisha ni kwamba wakati mchakato ukikaribia mwisho kumeanza kujitokeza matukio ya aibu naya kusikitisha ambayo yanaweza kuuchafua kabisa au kuharibu kazi nzuri ambayo ilikuwa imeanza kufanyika.

FemAct imesikitishwa na vurugu za hivi karibuni zilizosababisha kukatishwa kwa mdahalo wa kujadili mchakato wa katiba mpya ya Tanzania huku baadhi ya watu wakipigwa na kujeruhiwa akiwemo mwandishi wa habari wa BBC aliyeumizwa, mwanamke moja aliyepigwa na kuangushwa pamoja na kuzingirwa kwa mlemavu wa macho aliyekuwa akishiriki katika mjadala huo.

Mahututi aliyekimbiwa na mwanamke 'guest' afariki

Mtu mmoja amefariki dunia katika hospitali ya rufaa ya Mbeya baada ya kukutwa hali mahututi katika nyumba ya kufikia wageni.

Mtu huyo aliyetambuliwa kwa jina la Kassim Rashid (55) mkazi wa Ghana, Mbeya alifariki dunia wakati akitibiwa katika hospitali hiyo ya rufaa tarehe 10 Novemba 2014 mwendo wa saa kumi alasiri.

Taarifa ya Polisi kutoka mkoa wa Mbeya imesema kuwa awali majira ya saa tatu asubuhi, marehemu alifika kwenye nyumba ya wageni iitwayo Atukuzwe iliyopo eneo la Soko Matola akiwa

Taarifa mpya kuhusu maendeleo ya afya ya Rais Kikwete

Rais Kikwete akiwasiliana na baadhi ya wananchi waliokuwa wakimjulia hali kupitia simu yake ya mkononi kupitia ujumbe mfupi(sms) leo Jumatatu.Rais Kikwete anayepata matibabu katika hospitali ya Johns Hopkins jijini Baltimore Maryland nchini Marekani anaendelea vizuri na anafanya mazoezi mara kwa mara na afya yake inaendelea kuimarika

(picha: Freddy Maro)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete jana, Jumatatu, Novemba 10, 2014, alianza kuwasiliana na mamia kwa mamia ya wananchi mbali mbali nchini kujibu ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) wa kumpa pole, kumtakia heri na nafuu ya haraka ambao amekuwa anatumiwa na wananchi tokea mwishoni mwa wiki.

Tangu alipofanyiwa upasuaji wa tezi dume (prostate Jumamosi iliyopita kwenye Hospitali ya Johns Hopkins, Baltimore, Jimbo la Maryland, Marekani, Rais Kikwete amepokea mamia kwa mamia ya SMS zikimpa pole na kumtakia nafuu ya haraka.

Safu ya uongozi wa Wamiliki wa Blogs Tanzania

Baadhi ya wamiliki wa Blogs nchini wakiwa katika warsha hiyo leo

  1. Mwenyekiti: Joachim Mushi
  2. Makamu Mwenyekiti: Francis Godwin
  3. Katibu: Khadija Kalili
  4. Wajumbe: Shamim Mwasha, Mdimu Henry, William Malecela, Othman Maulid 

MWANDISHI wa gazeti la Jamboleo kutoka mkoani Iringa Bw Francis Godwin ameteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa chama cha Wamiliki Mitandao ya Kijamii (Blogs) nchini Tanzania.

Godwin ambae ni mmiliki wa blog ya "MatukioDaima" na "FrancisGodwin" ameteuliwa katika nafasi hiyo kama mwakilishi wa wamiliki wote wa blogs za mikoani, huku Joachim Mushi akiteuliwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho.

Uteuzi huo umefanyika leo katika ukumbi wa Mlimani City baada ya kumalizaka kwa warsha ya siku moja iliyoandaliwa na mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA).