Patashika Bungeni! Hoja za Wabunge zataka mwenendo wa Serikali ujadiliwe

Nje ya ukumbi wa Bunge, Dodoma wakati wa usiku

HALI si swari tena ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!

Hivyo ndivyo inavyoweza kutafsiriwa kutokana na joto linalolikumba Bunge hilo kutokana na hoja tata ambazo sasa wabunge wameshikilia bango wakitaka Bunge kujitokeza na kuonesha meno yake katika kuisimamia serikali kwa mujibu wa kanuni ya 63 (2).

Kutokana na hali hiyo, jana wabunge walipendekeza Bunge hilo kukubali kujadili mwenendo wa serikali kwa kile walichoeleza kwamba hawaridhishwi na uwajibikaji wake, huku wengine wakiomba
kuundwa kwa Kamati Teule ya Bunge kujadili hoja mbalimbali.

Masuala yaliyosimamiwa na wabunge leo ni suala la fedha za akaunti ya Escrow Tegeta, mauaji ya kutisha wilayani Kiteto mkoani Manyara na uwajibikaji wa serikali katika siku za hivi karibuni.

Waziri wa Afya asema la hospitali kukosa dawa limekuzwa mno

Mgeni rasmi Waziri wa Afya, Dkt. Seif Rashid akizungumza wakati wa kuzindua kongamano la tisa la NHIF na Waandishi wa Habari,lililofanyika leo katika moja ya ukumbi wa Dodoma hotel mkoani humo,ambapo kauli mbiu ya kongamano hilo ni ''Tanzania na Huduma bora za matibabu inawezekana''.

Tatizo la ukosefu wa dawa katika hospitali kadhaa nchini, limekuzwa mno kuliko hali halisi na serikali itatoa taarifa rasmi kesho kuelezea tatizo hilo na hatua ambazo imechukua.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Rashid Seif wakati akijibu hoja za waandishi wa habari baada ya kufungua Kongamano la Wanahabari na NHIF mjini hapa.

Dk Seif alisema deni lililopo kwa sasa asilimia 80 ni kulipia gharama za dawa zilizoletwa kama msaada, lakini ununuzi wa dawa ni asilimia 20 pekee. Dawa hizo ni kama za UKIMWI, kifua kikuu na dawa za malaria.

Rais Kikwete ahamishiwa katika hoteli maalum

Rais Jakaya Kikwete akiagana na Daktari Edward Schaeffer muda mfupi baada ya kuruhusiwa kutoka katika hospitali ya Johns Hopkins huko Baltimore, Maryland nchini Marekani ambapo alifanyiwa upasuaji mwishoni mwa wiki iliyopita.(picha na Freddy Maro)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ambaye anaendelea na matitabu yake nchini Marekani, jana, Jumatano, Novemba 12, 2014, alitoka wodini katika Hospitali ya Johns Hopkins na kuhamishiwa kwenye Hoteli Maalum ambako ataendelea kuwa chini ya uangalizi wa madaktari.

Rais Kikwete amekuwa kwenye Hospitali ya Johns Hopkins tokea Jumamosi iliyopita wakati alipofanyikwa upasuaji wa tezi dume (prostate) na afya yake imekuwa inaimarika kiasi cha kuanza mazoezi ya kutembea.

Kutokana na kuondolewa kwa bandeji kwenye mshono ambao nao umeanza kukauka vizuri, Rais Kikwete baadaye leo atahamishwa kutoka wodini kwenda kwenye Hospitali Maalum yenye uhusiano na Hospitali ya Johns Hopkins iliyoko karibu na hospitali hiyo.

Ziara ya Makamu II wa Rais, Balozi Seif nchini China

Ujumbe wa Zanzibar ukiongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif na Ule mwenjeji wa Hainan ukiongozwa na Gavana wa Jimbo hilo Bwana Jian Dingzhi ukiendelea na mazungumzo yao ya uhusiano hapo katika Hoteli ya Le Meriden Mjini Haikou.

Uongozi wa Kisiwa cha Jimbo la Hainan Nchini Jamuhuri ya Watu wa China iko tayari wataalamu na awekezaji wake kufungua milango ya uwekezaji katika Visiwa vya Zanzibar katika miradi ya Kilimo, Utalii na Mazao ya Baharini kwa lengo la kusaidi maendeleo ya Zanzibar.

Gavana wa Jimbo la Hainan Bwana Jian Dingzhi alitoa kauli hiyo wakati wa mazungumzo yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na ujumbe wake ambao umenza ziara rasmi ya Kiserikali ya Siku Kumi katika Jimbo hilo hapo Hoteli ya Le Meriden Mji Mkuu wa Kisiwa hicho wa Haikou.

Bwana Jiang Dinmgzhi alimueleza Balozi Seif kwamba Jimbo hilo ambalo ni Kisiwa kiliopo ncha ya Kusini mwa China limekuwa na utajiri mkubwa wa wataalamu wa Sekta hizo ambao unaweza kusaidia maendeleo na uchumi wa Zanzibar.

Hotuba ya ufunguzi wa warsha ya udhibiti wa ukatishaji fedha haramu

HOTUBA YA UFUNGUZI WA WARSHA JUU YA UDHIBITI WA UTAKASISHAJI WA FEDHA HARAMU KWA MAAFISA UPELELEZI KUTOKA JESHI LA POLISI NA WAENDESHA MASHTAKA KUTOKA AFISI YA MKURUGENZI WA MASHTAKA ZANZIBAR TAREHE 12 – 13 NOVEMBA, 2014


Imetolewa na Mhe. Said Hassan Said

Mwanasheria Mkuu Zanzibar.

1. Kaimu Kamisha, kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu,
2. Ndugu Washiriki kutoka Afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka na Jeshi la Polisi Zanzibar,
3. Washiriki wa Warsha,
Mabibi na Mabwana,

Assalamu Alaykum.

Kwanza, sina budi kumshukuru Mwenyezi Mungu Muumba wa kila kitu, Mola wa utukufu wote na mwingi wa Rehema kwa kutujaalia uzima na kutuwezesha kukutana hapa siku ya leo kuhudhuria warsha hii muhimu tukiwa na amani, usalama na utulivu.

Natoa shukrani zangu za dhati kwa Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu kwa kuandaa Warsha hii muhimu inayohusu Udhibiti wa Utakasishaji wa Fedha Haramu na kunialika kuwa Mgeni Rasmi katika ufunguzi. Aidha, ninatoa shukrani kwa washiriki wote kwa jumla kwa kuitikia mwaliko na kuhudhuria warsha hii muhimu na kuwa tayari kutoa michango yenu ambayo ninaamini itaifanya nchi yetu iimarishe mfumo wa udhibiti wa utakasishaji wa fedha haramu.

Kajala Entertainment yatozwa 1,000,000/= kwa kukiuka sheria

Mkurugenzi wa Kampuni ya Kajala Entertainment, Kajala Masanja (wa pili upande wa kulia) akijitetea mbele ya Katibu wa Bodi ya Filamu Tanzania wakati aliitikia wito wa Ofisi ya Bodi hiyo leo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuelezwa juu ya Sheria na Kanuni zilizokiukwa katika filamu yake ya "Mbwa Mwitu".

BODI ya Filamu Tanzania imezitaka Kampuni za filamu nchini kufuata Sheria na Kanuni mbalimbali wakati wa kutengeneza filamu ili kuepusha ukiukwaji wa Sheria na Kununi.

Rai hiyo imetolewa leo na Katibu wa Bodi hiyo, Bi Joyce Fissoo wakati alipofanya mkutano na Kampuni ya Kajala Entertainment ambapo mnamo Septemba 22, mwaka huu ilikagua Filamu fupi ya kampuni hiyo iliyopewa jina la Mbwa Mwitu yenye dakika 12 na kubaini baadhi ya makosa.

Akiongea wakati wa mkutano na wadau wa kampuni hiyo, Bi Fissoo alisema kuwa Bodi iliielekeza Kajala Entertainment kuifanyia marekebisho filamu hiyo katika dakika ya 7 ambapo ilionekana wanawake wakidhalilishwa na kubakwa kinyama na pia katika dakika ya 11 ambapo ilionyesha wizi na uvamizi.

Alisema kuwa, wahusika walielekezwa kufanya marekebisho hayo kwa

Aonavyo Wakudata katika "nchi ya matukio"...

Taarifa kuhusu huduma ya 'treni ya Mwakyembe'

Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania -TRL unasikitika kuwatangazia kuwa kuanzia leo jioni saa 10 hakutakuwepo huduma ya usafiri wa treni ya Jiji maarufu kama ' treni ya Mwakyembe' hadi siku Jumatatu Novermba 17, 2014 huduma itakaporejea kama kawaida.

Ufafanuzi wa sababu za kusitishwa huduma umeeleza kuwa kichwa kimojawapo ambacho hutoa huduma kimepelekwa Karakana Kuu ya Morogoro kwa ajili ya ukarabati maalum na kwamba kinatarajiwa kurejeshwa Dar es Salaam jioni ya siku ya Jumapili. Novemba 16, 2014 baada ya kukamilika zoezi hilo la ukarabati.

Huduma zitarejea tena siku ya Jumatatu saa 12:30 asubuhi kuanzia kama kawaida kituo cha Ubungo Maziwa.

Atakayesoma taarifa hii amwarifu mwenzake!
Uongozi wa TRL unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza!

Imetolewa na Afisi ya Uhusiano ya TRL
kwa Niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TRL
Mhandisi Kipallo Amani Kisamfu.
Dar es Salaam,
Novemba 13, 2014

Muhongo: PAC haikufuata utaratibu ilipoiagiza TPDC kuwapatia mikataba

WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amesema mwenye mamlaka ya kutoa mikataba ya wawekezaji kuhusu Wizara hiyo na wawekezaji ni yeye, hivyo Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), chini ya Zitto Kabwe haikufuata utaratibu ilipoagiza Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Michael Mwanda na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo, James Andilile kuwapatia mikataba hiyo.

Profesa Muhongo alitoa kauli hiyo jana (Novemba 13, 2015) wakati akijibu maswali ya waandishi kuhusu TPDC kugoma kuipatia PAC mikataba wakati huo huo akijinadi kuwataka wawekezaji kuzingatia uwazi katika mikataba wanayoingia na Serikaki.

Alisema alipopewa taarifa na TPDC alishauriana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) ambapo walikubaliana kutotoa mikataba hiyo kwa kile alichodai kuwa utaratibu uliotumika haukuwa sahihi na mikataba ni siri kati ya mwekezaji na Serikali.

Kuelekea 2030 serikali nyingi za kusini mwa jangwa la Sahara zitang’olewa

Museveni akiwa kulia mwa Mugabe (photo: nehandaradio.com)

Habari kubwa hivi sasa barani Afrika ni mapinduzi ya umma yaliyofanyika Burkinafaso, makala haya ni mtazamo wangu kuhusu kitakachojiri kusini mwa jangwa la sahara kuelekea 2030, mtazamo huu umejikita katika kutathimini matukio yanayoendelea kusini mwa jangwa la sahara na hali ya kisiasa kwa ujumla, fuatana nami katika maandishi haya ya kusisimua;

Kusini mwa jangwa la Afrika si salama

Dalili za wazi zinaonyesha kuwa nchi nyingi za kusini mwa jangwa la Sahara zipo katika hali mbaya zaidi ya nchi za kiarabu zilizopinduliwa kama Misri na Tunisia , halikadhalika kwenye mataifa hayo ya kusini mwa jangwa la sahara kuna ukosefu mkubwa zaidi wa ajira hivyo kufanya idadi kubwa ya vijana kuwa wazururaji kuliko Burkinafaso ambayo imepinduliwa hivi karibuni. Sasa ikiwa hali iko hivi kwanini viongozi wa mataifa ya kusini mwa jangwa la Sahara hawachukui tahadhari? Kwa nini wanazidi kujisahau?

UNESCO, Samsung kujenga kijiji cha kidijitali Ololosokwan

Pichani ni muonekano wa mchoro wa kijiji hicho utakavyokuwa.

SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limetiliana saini mkataba na kampuni ya elektroniki ya Samsung ya ujenzi wa kijiji cha digitali cha Ololosokwan, Loliondo.

Makubaliano hayo yalitiwa saini hivi karibuni kati ya Mwakilishi mkazi Unesco nchini Bi. Zulmira Rodrigues na Mkurugenzi wa Samsung Electronics nchini Tanzania, Bw. Mike Seo katika hafla iliyofanyika ofisi za UNESCO.

Kijiji hicho kitakuwa na shule yenye Tehama ikiwa na maunganisho ya intaneti, kiliniki ya kisasa ikiwa na kituo cha teknolojia ya mawasiliano yenye kuwezesha utabibu (telemedicine) na jenereta linalotumia nguvu za jua kwa ajili ya kijiji hicho.

[video] Sensei Rumadha Fundi aonesha umahiri wake

Mtaalam wa ngazi ya juu wa mchezo karate na Yoga, Sensei Rumadha Fundi (Mtanzania) mwenye Black Belt, 6 Dan, anayetambulika Kimataifa mwenye makao yake nchini Marekani akifanya vitu vyake katika kupasha pasha mwili. Tazama video hizo mbili.

(ONYO: Tafadhali usiige mchezo huu bila kupata maelekezo ya wataalamu)