Nimekerwa kabisa na kauli ya Sitta na kauli ya Rais - Prof. Mbele
Kati ya mambo yaliyonishtua sana mwaka huu ni kunyanyaswa kwa Jaji Warioba. Kadhia hii imetokana na kazi murua aliyofanya Jaji Warioba na tume yake ya kukusanya mawazo ya wananchi kuhusu Katiba Mpya.

Kumekuwa na mlolongo wa matukio kadhaa ya unyanyasaji huo, ambao, kwa kadiri ninavyofahamu, mwanzilishi wake ni Ikulu. Tukio la kupigwa Jaji Warioba mkutanoni, ambalo limeripotiwa sana, ni kilele cha utovu huu. Wengi tunaamini kuwa Jaji Warioba ananyanyaswa kwa sababu ya uwazi na uwakilishi wa mawazo ya wananchi, jambo ambalo ni mwiba kwa mafisadi.

Nimeshtushwa vile vile na kauli ya Rais Kikwete kuhusu tukio hili la vurugu na kupigwa Jaji Warioba. Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari, Rais Kikwete aliishia tu kusema kuwa anaomba yasimkute yaliyomkuta Jaji Warioba. Sikuona popote kama aliongelea suala hili kwa undani na mapana kama linavyostahili.

Kumbukumbu ya Mama Anna Satweve Mgina

Anna Satweve Mgina
Anna Satweve Mgina

Leo tarehe 15/Nov/2014 ni Miaka 13 kamili tangu ulipofariki Mama yetu mpendwa. Ulizimika kama mshumaa katikati ya upepo. Ulituachia mambo mengi ya kuigwa na kwetu unaendelea kubaki kama SHUJAA ASIYEANDIKWA POPOTE (HERO WITHOUT TITLE).

Utaendelea kukumbukwa kwa ucheshi, busara, uaminifu, Hekima, bidii ya kazi, Miongozo ya kidini na Mwalimu mkuu wa watoto Wako 11 (mmoja wetu akiwa amekufuata). Ulitulea kwa akili ya ajabu na kwa namna isiyoelezeka. Yamkini yapo mengi ya kuandika.

Utaendelea kukumbukwa na Mumeo Mpendwa Rev Stefano Yohana Mgina. Watoto wako Mariam, Anjanushe, Azaria, Cyprian, Rehema, Polikapo, Obed, Furaha, Frank na Joseph. Wakwe zako na Wajukuu pamoja na ndugu na jamaa wote.

Umetangulia lakini Fikra zako zinaendelea kuishi mioyoni Mwetu.

Bwana alitoa na Bwana Ametwaa ; Jina la Bwana lihimidiwe.
Obed Mgina.
Amen.

Mkuu wa Mkoa aliyeachwa ashukuru; Atoa milioni 19/= za maabara

Dk Ishengoma

BAADA ya kuachwa katika uteuzi wa wakuu wa mikoa, alisekuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dk Christine Ishengoma (pichani) amewaaga wakazi wa mkoa wa Iringa kwa kuchangia kiasi cha Tsh milioni 19 kwa ajili ya kutekeleza agizo la Rais Jakaya Kikwete la ujenzi wa maabara katika shule za sekondari.

Akizungumza katika mahojiano maalum na matukiodaima.co.tz leo, Dk Ishengoma ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum, mkoa wa Morogoro (CCM) alisema kuwa pamoja na kutemwa katika nafasi hiyo ya Ukuu wa Mkoa, bado anampongeza sana Rais Profesa Jakaya Kikwete kwa uteuzi wake kama Mkuu wa Mkoa, nafasi iliyoishia mapema mwezi huu baada ya

Official opening of 39th World Congress of Africa Travel Association, Kampala, UgandaUgandan President Yoweri Kaguta Museveni shaking hands with the Tanzanian Minister for Natural Resources and Tourism Hon. Lazaro Nyalandu after the official opening of the 39th World Congress of Africa Travel Association (ATA) in Kampala, Uganda.