Mbowe: "siwezi kumpiga vita Zitto" "nilimwezesha Dk. Kabourou kutoka Uingereza"


Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Kazuramimba mkoani Kigoma, katika mkutano wa hadhara wa Oparesheni Delete CCM juzi.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amesema hana ugomvi na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, kwa kuwa amemlea na amemesaidia vitu vingi zikiwamo fedha, gari, kula na kulala nyumbani kwake.

Mbowe alisema CHADEMA haijamtenga Zitto bali alijitenga mwenyewe na kufafanua kuwa Chama hicho hakiwezi kujengwa na viongozi ambao ni wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Aliyasema hayo jana katika Kata ya Kalinzi, Jimbo la Kigoma Kaskazini katika ziara zake za ‘operesheni delete CCM’ kuelimisha wananchi kuhusiana na uchaguzi wa serikali za mitaa na kuikataa Katiba iliyopendekezwa.

Mbowe alisema hayo baada ya kuruhusu maswali kutoka kwa wananchi ndipo Cheche wa Cheche alipomuuliza kwamba kwa nini Zitto hayumo katika ziara hiyo wala ya

Viongozi wa UKAWA warejea CCM kwa utendaji wa Mgimwa

Wananchi wa Lyamgungwe wakiwa wameongozana na mbunge wake kwenda kutembelea miradi ya maendeleo

VIONGOZI watatu wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kata ya Lyamgungwe jimbo la Kalenga wamempongeza mbunge wa jimbo la hilo Godfrey Mgimwa kwa kutekeleza ahadi mbalimbali zilizoachwa na marehemu mbunge aliyepita Dk Wiliam Mgimwa kwa muda mfupi na kuwa katika kuonesha umoja wao wameamua kuunganisha nguvu zao kwa mbunge huyo kwa kuhama CHADEMA na kujiunga na CCM.

Akizungumza kwa niaba ya wanachama wenzao zaidi ya 20 ambao walikuwa nyuma yao kabla ya kujiengua CHADEMA na kujinga na CCM walisema kuwa sababu ya kujiunga na upinzani ilitokana na makundi ndani ya CCM na upendeleo wa uteuzi wa wagombea mbalimbali pamoja na wabunge waliotangulia kuonesha kutumia ubunge kulea familia zao badala ya kuleta maendeleo katika jimbo hilo jambo ambalo mbunge Mgimwa amekuwa wa tofauti na wabunge wengine kwa kuonesha kuwajali zaidi wapiga kura wake.

Ugomvi wa eneo lamalisho Siha: Wamaasai vs Mwekezaji - Nyumba, magari vyatekekezwa

Mabaki ya nyumba yaliyoteketezwa kwa moto na wafugaji wa kimasaii wakidai eneo la malisho yao.
(picha: Elias Kija, Siha, Kilimanjaro)

Mgogoro mkubwa wa kugombea malisho umeibuka katika kijiji cha Miti Mirefu, wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro, baina ya jamii ya kifugaji ya Kimasai na Mwekezaji katika shamba la Ndarakwai, na kusababisha ugomvi hata kuzua hali ya wasiwasi katika eneo hilo ambapo magari tisa yameteketezwa kwa moto huku nyumba zaidi ya 16 zikichomwa moto.

Vurugu hizo zilizuka hivi karibuni kati ya wafugaji jamii ya wamasai na Mwekezaji katika shamba la Ndarakwai, kijiji cha Miti Mirefu, wilaya ya Siha, mkoani Kilimanjaro na kusababisha uharibifu mkubwa wa mali huku mlinzi mmoja wa mwekezaji huyo akijeruhiwa vibaya kwa risasi.

Mashuhuda wa tukio hilo walisema vurugu hizo zilizuka baada ya mifugo zaidi ya 300 ya wananchi wanaokaa jirani na shamba la Ndarakwai Ranchi, linalomilikiwa na Mwekezaji huyo anayefahamika kwa jina la Peter Jones, kukamatwa na walinzi wa shamba hilo.

Waziri Mkuu Mstaafu: "Viwango vya ufaulu vimerekebishwa ili wanaofeli waonekane wanafaulu”

Hoja kuwa hali ya elimu ya taifa hili ni mbaya imeendelea kuungwa mkono na wadau mbalimbali, safari hii Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye, ameeleza kushangazwa kwake kuwa kwa Tanzania kadri mtu anavyozidi kusoma ndivyo anazidi kuwa tegemezi kwa ajira.

Alisema kipimo cha elimu kuporomoka ni hali iliyopo katika vyuo vikuu ambavyo viongozi wake wanakiri kutopata watu wenye viwango vinavyotarajiwa kuingia vyuo vikuu.
Katika mahojiano maalum na NIPASHE wiki iliyopita, Sumaye alisema ubora wa elimu nchini unazidi kuporomoka.

Kauli ya Sumaye inashabihiana na ile aliyotoa Jaji Mkuu Mstaafu, Augustino Ramadhani, katika mahojiano maalum na NIPASHE akisema kuwa baadhi ya mahakimu wa mahakama nchini hushindwa kuandika hukumu za kesi wanazoziendesha kiasi kwamba zinapofikishwa Mahakama ya Rufaa huwa hazieleweki.

Sumaye naye alisema kuwa tatizo halipo kwa mahakimu tu bali pia kwa wahitimu wengine wa fani mbalimbali wanaoingia katika soko la ajira kwani hushindwa kuonyesha uwezo wao wa kitaaluma kwa sababu wengine hufundishwa kwa mtindo wa bora liende alimrad wanamaliza vyuo vikuu.
“Ukweli ni kwamba siyo jambo linalojificha na wala hatuwezi kulikwepa … elimu imeshuka na ndiyo maana idadi ya wanaofeli ni kubwa na ili waonekane wanafaulu,

Wanyonge mkiungana - Shairi


Tano miongo yapita, taifa ladidimia
Wengi wameshastuka,dawa wajitafutia
Viongozi kadhalika, mali walimbikizia
Wanyonge mkiungana, minyororo mtakata

Tazama kwenye ramani, utaona hiyo nchi
Nchi ya wasio soni, wenye tabu wananchi
Raia wapo kinuni, watwangaji wana mchi
Wanyonge mkiungana, minyororo mtakata

Chama kisicho na dira, kimekamata hatamu
Wanakula kwa papara, hamu ya kula utamu
Roho zao za harara, mikono yao ya damu
Wanyonge mkiungana, minyororo mtakata

Ushauri kuhusu kilimo cha mitiki mkoani Tanga

Miti ya mitiki michanga (picha kutoka ndanda.org)

Ndugu yangu, mimi nipo kijij cha Bwitini wilaya ya Muheza mkoa wa Tanga.

Ninalo shamba na ninahitaji kulpanda miti aina ya mitiki, lakini sina uelewa kuhusu miti hiyo, kwa maana jinsi ya kuotesha mbegu, jinsi ya kupanda na jinsi nitakavyo faidika na zao hilo.

Naomba ushauri wako, maelezo yako ya namna yakuotesha mbegu, kupanda na jinsi nitavyo nufaika na zao hilo.
Jina langu ni Athumani Iddi

email address ni [....]
Namba ya simu ni [...]

Ndugu Athumani,

Nashukuru kwa ujumbe wako ulioutuma kupitia ukurasa wa 'contact'.

Nakupongeza kwa kutumia muda wako vizuri wa kuperuzi mtandaoni kwa kutafuta elimu na maarifa ya kufaa kujiendeleza kimaisha. Umekuwa mfano wa kuigwa.

Kuhusu kilimo cha miti ya mitiki, kwa kuwa mimi sina utaalamu, tafadhali peruzi blogu ya mtaalamu wa kilimo, Chris Bennet kwa kutumia Google.com, ambapo unatakiwa kuandika 

mitiki site:mitiki.blogspot.com

halafu bofya alama ya kutafuta (au gonga "Enter" kwenye kibodi yako) ili kuona majibu ya makala zote zilizochapiswa katiba blogu hiyo kuhusu mitiki.

Pia, katika blogu hiyo utaona anwani ya kuwasiliana na Chris ili umwandikie kumwomba akupe ushauri zaidi kwa sababu kilimo cha zao lolote husitawi kutegemea na aina ya udongo na hali ya hewa. Kutokana na uzoefu wa mtaalamu, atakushauri vyema ikiwa mitiki itasitawi katika udongo na hali ya hewa unayotaka kuipanda.

Yaliyoandikwa na gazeti la Jamhuri kuhusu IPTL

Serikali ya Awamu ya Nne chini ya uongozi wa Rais Jakaya Kikwete, kwa mara nyingine imekutana na mtihani mgumu ambako Waziri Mkuu wake, Mizengo Pinda yupo chini ya shinikizo la kujiuzulu kutokana na malipo ya karibu Sh bilioni 400 kwa Kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL).

Shinikizo la Pinda kujiuzulu limetokana na msukumo mkubwa wa wafadhili kutoka nchi zilizoendelea ambao wamesitisha msaada wa Sh trilioni 1; hali iliyoifanya miradi ya maendeleo kukosa fedha na kuifanya Serikali iwe katika wakati ngumu.

Wachambuzi wa mambo, wameitafsiri safari ya Rais Kikwete kwenda Marekani kufanyiwa uchunguzi wa afya yake ni zaidi ya kufanya hivyo kwani shinikizo la kutikiswa Serikali yake huenda ikawa ni sababu ya ziada.

Taarifa ya Ikulu kwa vyombo vya habari iliyotolewa Ijumaa iliyopita, inasema kuwa Rais Kikwete aliondoka Jumatano ya wiki jana na kwamba kulingana na ratiba ya uchunguzi wa afya yake anatarajiwa kurejea nchini Alhamisi ya wiki hii.

Curious! Mmasai mdadisi...

A Maasai elder looks in amazement at a video camera that had been set on the ground by a visitor at Loiborsoit Village, Simanjiro District in Manyara Region.

(Photo by Mohamed Mambo/DAILY NEWS)


PAC kujadili wazi ripoti ya CAG kuhusu IPTLHATIMAYE Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kuhusu utoaji wa zaidi ya Sh bilioni 200 katika akaunti ya Escrow ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), imekabidhiwa kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Kabwe Zitto.

Juzi usiku, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alikabidhi ripoti hiyo kwa Spika wa Bunge, Anne Makinda, kama alivyoahidi bungeni siku ya Alhamisi Novemba 13, 2014.

Akitoa taarifa ya kukabidhiwa kwa ripoti hiyo kwa Spika, Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azzan Zungu, aliliambia Bunge kwamba tayari Waziri Mkuu Pinda, amekabidhi ripoti ya CAG kwa Spika na wakati wowote itakabidhiwa kwa Kamati ya PAC.

Akizungumza na gazeti hili (HabariLeo) jana, Zitto alikiri kukabidhiwa ripoti hiyo ambayo inatarajiwa kujadiliwa katika ngazi ya kamati, kabla ya Mwenyekiti wa kamati hiyo, kuwasilisha taarifa yake bungeni Novemba 26, mwaka huu.

Padri wa Uganda miongoni mwa wengi waliozikwa kaburi moja Mexico

Wataalamu wa uchunguzi wa kisayansi nchini Mexico wamegundua mwili wa mchungaji wa Kikatoliki kutoka Uganda, ikiwa ni miongoni mwa mabaki ya miili iliyopatikana kwenye kaburi lenye watu wengi mwezi uliopita.

Mchungaji John Ssenyondo alikuwa hajulikani alipo tangu alipotekwa katika jimbo la Guerrero lililopo kusini-magharibi, miezi sita iliyopita.

Kaburi hilo liligunduliwa na polisi waliokuwa wakiwatafuta wanafunzi 43 ambao walitoweka eneo hilo tarehe 26 Septemba.