Rombo yaongoza kwenye pombe za kienyeji; Viwanda 21 vyafungiwa

Halmashauri ya wilaya ya Rombo imevifunga viwanda 21 vinavyotengeneza pombe haramu inayodaiwa kupunguza nguvu za kiume.

Mkuu wa Wilaya ya Rombo, Elinasi Pallangyo aliyasema hayo juzi katika baraza la madiwani.

Alisema viwanda hivyo vilikuwa vikisababisha baadhi ya watu kujihusisha na unywaji wa pombe katika saa za kazi.

Alisema kwa zaidi ya miaka miwili sasa, Wilaya imekuwa ikipambana na tatizo la pombe haramu, lakini uzalishaji huo ulikuwa ukiendelea. Alisema Rombo imekuwa ikiongoza kwa kutengeneza pombe za kienyeji zisizo na viwango.

“Halmashauri imeamua kufunga viwanda 21 vinavyozalisha pombe hizo zinazoharibu afya za vijana, kupunguza uzazi katika Wilaya hii na kukosa wanafunzi kutokana na uzazi kupungua kwa kiasi kikubwa,” alisema Pallangyo.

Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Mohamed Maja alisema wameziomba taasisi za dini kutoa elimu kwa jamii kuhusiana na madhara ya pombe hizo. Alisema kikosi kazi kilichoundwa na mkuu wa wilaya kitasimamia idara ya biashara na kwamba mfanyabishara atakayekiuka agizo na kuuza pombe saa za kazi atatozwa faini.

Wizi wa fedha Stanbic Kinondoni: Wafanyakazi 3; Raia 2 wa Kenya washikiliwa

JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam linawashikilia watu sita wakiwemo raia wawili wa Kenya, baada ya kukiri kuhusika na wizi wa fedha zaidi ya Sh milioni 500 zilizoibwa Oktoba 23 mwaka huu katika Benki ya Stanbic, tawi la Mayfair, Kinondoni.

Mbali na raia hao wa Kenya, pia polisi inawashikilia wafanyakazi watatu wa benki hiyo akiwemo Meneja Msaidizi, Celestine Mkumbo (46), mtunzaji wa funguo, Anastazia Ringo (46) na mpelelezi wa benki hiyo, Tegemea Ayoub (39) kwa tuhuma za kula njama na wezi waliohusika na wizi huo.

Akizungumza jana, Kamanda wa Kanda hiyo, Suleiman Kova alisema kukamatwa kwa watuhumiwa hao kumetokana na upelelezi uliofanywa na jeshi hilo kwa kuhusisha mbinu mbalimbali za kiintelijensia.

Aliwataja raia wa Kenya waliokamatwa kuwa ni Francis Wanjohi (39) mkazi wa Nairobi na Richard Ottieno (37), mkazi wa Kisumu ambao kwa mujibu wa Kova ni majambazi sugu waliowahi kuhusika na matukio mbalimbali ya uhalifu nchini Kenya.

Darasa: Jinsi ya kuendesha nchi vs Darasa la Jinsi ya kuchukua nchi


US State Dept computers hacked, email shut down

WASHINGTON (AP) -- The State Department has taken the unprecedented step of shutting down its entire unclassified email system as technicians repair possible damage from a suspected hacker attack.

A senior department official said Sunday that "activity of concern" was detected in the system around the same time as a previously reported incident that targeted the White House computer network. That incident was made public in late October, but there was no indication then that the State Department had been affected. Since then, a number of agencies, including the U.S. Postal Service and the National Weather Service, have reported attacks.

The official said none of the State Department's classified systems were affected. However, the official said the department shut down its worldwide email late on Friday as part of a scheduled outage of some of its Internet-linked systems to make security improvements to its main unclassified computer network. The official was not authorized to speak about the matter by name and spoke on condition of anonymity.

The official said the department expects that all of its systems will be operating as normal in the near future, but would not discuss who might be responsible for the breach. Earlier attacks have been blamed on Russian or Chinese attackers, although their origin has never been publicly confirmed.

The State Department is expected to address the shutdown once the security improvements have been completed on Monday or Tuesday.

Ni nchi au makaburi ya kuzikia wachawi!?

%^&*()+£€?# ....! Leo nahisi Kichaa changu kimepanda au sijui kimepandishwa, yaani hata sielewi, kinacho endelea vichwani mwa Wabongo wanaoishi ndani ya nchi ya Wachawi Giningi, heri mie Mwendawazimu Kichaa Aliyechanganyikiwa, kwa sababu hakuna anayeweza kuniangalia mara mbili, zaidi ya wale watoto wanaopenda kunitania na wengine wakifikiria kuwa eti nimesoma sana mpaka vitabu vikiniona vinachakaa vyenyewe, ndio akili zikaelewa saaaana mpaka nikawa Mwendawazimu Aliyechanganyikiwa.

Hivi hawa wenye akili sana zilizopitiliza mpaka wakawa Wachawi, huwa wanafikiria nini kwenye vichwa vyao? Hivi hawajui kuwa wale wenye akili robo ndio walio wachaguwa kuwa pale walipo? Eti nasikia kuwa baadhi ya vyama vya Kichawi vimeamua kuungana ili kukichangia na kukigomea chama Kikuu cha Wachawi.

MV Dar es Salaam yawasili bandarini

Kivuko cha MV Dar es Salaam kama kinavyoonekana juu ya meli kabla ya kushushwa majini katika bandari ya Dar es Salaam.

MCHAKATO wa kukabiliana na foleni katika Jiji la Dar es Salaam, jana ulipata msukumo mpya baada ya Serikali kupokea kivuko kipya kinachokwenda kasi zaidi kuliko vyote nchini, ambacho kitakuwa kikifanya safari zake kati ya Dar es Salaam na Bagamoyo, mkoani Pwani.

Mbali ya serikali kuahidi kuleta kivuko hicho pia imekuwa ikiboresha barabara zake kuwezesha magari yaendayo kasi, lakini pia imekuwa ikipanua kwa kiwango cha hali ya juu barabara katika Manispaa zake tatu za Dar es Salaam ambazo ni Ilala, Temeke na Dar es Salaam.

Kivuko hicho kilipokewa jana na Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli ambaye alisema ujio wake ni juhudi za serikali katika kukabiliana na foleni Dar es Salaam.

PAC yakabidhiwa ripoti ya CAG kuhusu "akaunti ya escrow Tegeta"

Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai (kulia), akiwakabidhi Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Deo Filikunjombe ripoti ya Uchunguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu kashfa ya kuchota fedha zaidi ya sh. bilioni 200 katika akaunti ya Tegeta Escrow zilizohifadhiwa katika Benki Kuu ya Tanzania (BOT).

RIPOTI ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuhusu sakata la akaunti ya Tegeta Escrow, imeanza kufanyiwa kazi na Bunge na ndani ya siku nane zijazo, umma utajua ukweli wake. Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai alikabidhi ripoti hiyo kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Kabwe Zitto, jana bungeni, na kamati imeanza kazi mara moja. Kwa mujibu wa Ndugai, taarifa hiyo ya CAG ina maoni kwa kila hadidu za rejea kama chombo hicho kilipoagiza wakati ilipotoa kazi kwa mkaguzi huyo.

Aliiagiza kamati hiyo ya Zitto iichambue zaidi na kutoa ushauri wake kwa Bunge kwa kuzingatia ushauri wa CAG pamoja na ushahidi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), ambayo iliwahoji wahusika wote wa sakata hilo.

Diwani aomba: "Mwenyekiti naomba uniruhusu dakika 10 tu tupigane na huyu jamaa"

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, juzi kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama mkoani Shinyanga, juzi kilisimama kwa muda baada ya kutokea ugomvi wa kurushiana maneno na kejeli kwa baadhi yao, huku wengine wakiomba kikao kisimamishwe angalau kwa dakika kumi ili wapigane.

Hali hiyo ilijitokeza baada ya Diwani wa Kata ya Idahina, Sospeter Bunanda (Chadema) kusimama na kutoa ushauri kwamba wajumbe wa mabaraza ya ardhi ya Kata, wapewe semina ya uendeshaji wa mabaraza hayo kuliko kutumia vipeperushi walivyopewa na Mwanasheria wa halmashauri hiyo ili kuwajengea uwezo mkubwa wa kutatua migogoro ya ardhi katika kata zao.

Kufuatia hali hiyo, Diwani wa Kata ya Sabasabini, Emmanuel Makashi (CCM) alisimama na kumwomba Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Juma Kimisha, kutupilia mbali maombi hayo. Alisema kusema hiyo ni kumfundisha mwanasheria, ambaye tayari ana taaluma yake.

Salam za Rais Kikwete akiwashukuru waliomtakia buheri ya afya

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman aliyemtembelea na kumjulia hali Jumapili Novemba 16, 2014 katika hoteli maalumu jirani na Hospitali ya Johns Hopkins jijini Baltimore, Maryland, Marekani anakoishi baada kutoka katika hospitali hiyo alikofanyiwa upasuaji wa tezi dume. Kushoto ni mke wa Rais Mama Salma Kikwete. Jaji Mkuu yuko Marekani kwa ziara ya kikazi ambapo pamoja na mambo mengine yeye na ujumbe wake watahudhuria mkutano maalumu wa kimataifa wa Mabadiliko ya Sheria ya Ushahidi jijini Washington na pia kukutana na taasisi mbalimbali za fedha na marafiki wa maendeleo katika ili kupata wabia wa ujenzi wa maendeleo ya mahakama


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete jana, Jumapili, Novemba 16, 2014 alikutana na kufanya mazungumzo na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mheshimiwa Mohammed Chande Othman na ujumbe wake.

Aidha, Rais Kikwete amewashukuru Watanzania kwa maelfu ya salamu za upendo kwake zikimtakia heri aweze kupona ambazo Rais amekuwa anapokea.

Rais Kikwete pia huenda akatolewa nyuzi katika siku tatu zijazo ikiwa maendeleo yake yataendelea kuwa ya kasi kama ambavyo imekuwa tokea alipofanyiwa upasuaji wa tezi dume Novemba 8, mwaka huu, katika Hospitali ya Johns Hopkins, Baltimore, Maryland, Marekani.