Jumba la kihistoria Mji Mkongwe laporomoka

Taarifa mpya zinasema hadi sasa hakuna mtu yeyote aliyeripotiwa kufukiwa na kifusi cha jengo lililoanguka (taaria kwa mujibu wa ZanziNews.com)
---------------------------------


Jumba moja kongwe liliopo eneo la Mji Mkongwe limeporomoka leo asubuhi.

Jumba hilo lipo Jaws Corner kama unaendea Kanisa la Minara Miwili, kwenye kona ambapo nje huwa panauzwa vinyago. 

Nyumba hiyo zamani aliishi aliyekuwa Mwenyekiti wa mwanzo wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Mr Zubeir.

Soccer legend Patrick Kluivert visits Zanzibar


Tarehe ya kujiandikisha kwa ajili ya chaguzi za Serikali za Mitaa

Mkurugenzi wa Serikali za Mitaa katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali Mitaa Bwana Kharist Michael Luanda amesema wananchi wanapaswa kujiandikisha katika daftari maalum la kupigia kura kwa ajili ya kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa kuanzia tarehe 23/11/2014 hadi tarehe 29/11/2014.

Mkurugenzi huyo alisema kuwa wananchi wanaotaka kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika ngazi za vijiji, vitongoji na mitaa wanapaswa kuchukua fomu za kugombea kuanzia tarehe 16/11/2014 hadi tarehe 22/11/2014.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma, Bwana Luanda aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika zoezi la kujiandikisha ili waweze kupata fursa ya kushiriki katika kupiga kura ili kuwachagua viongozi wa vijiji, vitongoji na mitaa wanaowataka.

Wakamatwa na Dola bandia zenye thamani ya milioni 20/=

Dola bandia

Elizabeth Kilindi, TANGA

WATU watatu wanaojishughulisha na biashara ya uuzaji wa noti bandia mkoani Tanga wamekamatwa na Jeshi la Polisi mkoani hapa wakiwa na dola za kimarekani zenye thamani ya 11200 ambazo ni sawa na shilingi milioni 20 za Kitanzania.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Fresser Kashai aliwaambia waandishi wahabari jana kuwa watuhumiwa hao walikamatwa Novemba 17 mwaka huu saa saba na nusu eneo la barabara ya kumi na sita Kata ya Ngamiani wilayani Tanga wakati kwenye harakati za kuziingiza kwenye mzunguko.

Usikose! Lady Jaydee's single "Forever" feat. DaboMwanamuziki Lady Jaydee anatarajia kuachia single mpya aliyomshirikisha Dabo inayoitwa "Forever' hapo Jumatatu tarehe 24 Novemba. 

Single hii inakuja baada ya kimya cha muda mrefu kidogo.

Siku ya Ijumaa ndio itakuwa official launch day pale M.O.G Bar & Restaurant ambapo video ya wimbo huu itaonekana kwa mara ya kwanza. 

Wimbo umetayarishwa na mwandaaji mahiri Man Water wa Combination Sounds, na video ya wimbo huo imefanywa na muongozaji mkongwe Adam Juma wa Next Level.

Instragram: @jidejaydee @dabomtanzania
Twitter: @jidejaydee @dabomtanzania

Huduma ya Simu Dokta yanufaisha maelfu ya Watanzania

  • Idadi ya wanaojiunga nayo yazidi kuongezeka

Kulwa Saiduni wa Bombo,mkoani Tanga ni miongoni mwa maelfu ya watanzania wanaoweza kupata taarifa zinazohusu afya katika hali ya utulivu wakiwa majumbani mwao.Hii inatokana na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom kuanzisha huduma ya Simu Dokta ambayo inawawezesha wateja wake waliojiunga na huduma hii kupata taarifa za afya kupitia simu zao za mkononi.

Hii huduma ni ya aina yake kuanzishwa nchini Tanzania ikiwa inatolewa na Vodacom.Inashirikisha madaktari bingwa wa fani mbalimbali ambao wamejitolea kutoa utaalamu wao kuhusiana na masuala ya afya na taarifa hizo zinawafikia watanzania kwa njia ya mtandao wa simu popote walipo nchini.

Viongozi wabovu wametokana na sisi kupiga ama kutokupiga kura


Imefika wakati Watanzania tuache kulalamika juu ya udhahifu wa viongozi wetu, kabla hujalalamika jiulize kwanza, hao viongozi unao walaumu wamewekwa na nani madarakani. Usikurupuke kulalamika wakati unajua ujinga wako ndio uliowaweka madarakani.

Kuna asilimia kadhaa za ukweli kuwa ujinga wa wapiga kura wetu ndio chanzo cha malalamiko mitaani, lakini asilimia kubwa sana ya matokeo ya kura tunayotangaziwa si halisi. Kwa hiyo hata pale ambapo wananchi wamechagua vizuri kiongozi wao,hujuma hutumika.Ukishatengeneza mazingira mabovu ya kupigia kura unategemea nini? 
- KILLANEKELI

Badala ya kuchonga mtumbwi, "tunasubiri"


Tutakuwa nchi ya walalamikaji mpaka lini?

Juzi Naibu Spika, Job Ndugai, aliitaka Serikali kushughulikia suala la mauaji ya Kiteto yanayotokea mara kwa mara kiasi cha kulifananisha eneo hilo na nchi ya Somalia.

Somalia ni miongoni mwa nchi za Afrika zilizodumu kwenye vita ya wenyewe kwa wenyewe kwa kipindi kirefu hali iliyowafanya wananchi wake washindwe kushiriki kikamilifu shughuli za uzalishaji mali.

Kwa mujibu wa Ndugai tangu Februari hadi sasa, watu 30 wameuawa na zaidi ya 200 wamejeruhiwa katika kile kinachoelezwa ni ugomvi kati ya wakulima na wafugaji na serikali imeshindwa kuchukua hatua zinazotakiwa kukomesha hali hiyo.

Uchambuzi kuhusu mtikisiko wa 5: IPTL - Escrow ya TegetaBunge jana lilikabidhi ripoti ya uchunguzi wa IPTL kwa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) ili ipitie na kutoa mapendekezo bungeni, hatua ambayo inatazamiwa kusababisha mtikisiko wa tano katika Serikali ya Rais Jakaya Kikwete.

Ripoti hiyo iliyoandaliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), katika vitabu vitano, ilikabidhiwa na Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai kwa Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe huku akimpa masharti ya kuipitia kwa siri, kinyume na Zitto alivyokuwa ameahidi kuwahoji watuhumiwa katika kikao cha wazi.

Ripoti hiyo inatokana na uchunguzi maalumu wa fedha zilizochotwa katika akaunti ya escrow ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), iliyokuwa inatunza fedha za gharama za uwekezaji (capacity charge) kwa Kampuni ya Kufua Umeme ya IPTL baada ya kutokea mgogoro wa kibiashara baina yake na TANESCO.

50 Mayors, experts from around the World meet in Tanzania to tackle rapid urban expansion

More than 50 mayors, urban planners and technical experts from 25 cities around the world on Monday began their four-day meeting in Dar es Salaam to share experiences on managing rapid urban expansion through metropolitan planning.

As the first such meeting being held in Africa since the initiative was launched in April 2013, the Global Lab on Metropolitan Strategic Planning is jointly organized by the World Bank and the city of Dar es Salaam.

"Dar es Salaam is one of the fastest growing cities in the world," said Philippe Dongier, the World Bank Tanzania country director.