As Malawi owns whole North of Lake, Tanzania has valid claim on same

As Malawi owns the whole North of Lake Malawi, neigbouring communities on the Tanzanian side have valid claim on the same. 

Author: Dr. Antipas Massawe -Mining Engineer –Dar es-Salaam

President Peter Mutharika of Malawi is very right when he says the whole North of Lake Malawi belongs to his country (Mutharika maintains Lake Malawi ownership non-negotiable: 'No war with Tanzania' Nyasa Times‎)

It is due to the fact that the boundaries of Tanganyika (now Tanzania) and Malawi which were established by the Helgoland treaty of 1890 show the whole north of the Lake belongs to Malawi; and these are the boundaries communities within Tanganyika and Malawi inherited collectively when they inherited the independence of self-rule from the colonialists who created the two countries for themselves.

It means, if Tanzania won’t prove otherwise that the map of the Tanganyika which secured the independence of self-rule from colonialists’ shows that half of the North of the Lake Malawi belongs to Tanganyika, Malawi will remain the owner of the whole north of the lake.

But, the communities who share the shores of Lake Malawi on the Tanzanian side have a valid claim on half of the North of Lake Malawi they shared peacefully with their counterparts on the Malawian side throughout generations before the arrival of colonialists who created for themselves Tanganyika and Malawi.

Theirs is a genuine continuation of the African liberation struggle from colonial rule because communities who shared the shores of the lake within Malawi, Tanganyika and Mozambique throughout generations before the arrival of the colonialist who created these countries are the true shareholders of the lake.

Consequently, the most responsible thing Tanzania could do is to help the Tanzanian communities who share the shores of the lake on the Tanzanian side claim their traditional right (through OAU and UN recognized International Court) on their traditional share of the lake they had throughout generations before the arrival of colonialists who created for themselves Tanganyika, Malawi and Mozambique.

The International Court will consider that the granting of self rules to African communities within the colonies Tanganyika and Malawi based on the boundaries created by the Helgoland treaty of 1890 maintained violation of the traditional rights of communities on the Tanzanian side of Lake Malawi as it maintained denying them their share of the lake they had been sharing with their counterparts on the Malawian side throughout generations before the arrival of colonialists who created for themselves Tanganyika, Malawi and Mozambique.

It is only the International court could determine on the claim of communities on the Tanzanian side based on consideration that the granting of self rules to Tanganyika and Malawi should have made correction on the boundaries set by the Helgoland Treaty of 1890 to ensure communities who share shores of the Lake Malawi on the Tanzanian side also get self-rule on their traditional share of the North of the lake they had shared with their counterparts on the Malawian throughout generations before colonialists created for themselves Tanganyika, Malawi and Mozambique.

A Malawi-Tanzania integration founded search for common ownership solution on the lake dispute is the only way a Malawi-Tanzania negotiation could determine on the matter amicably. It is the most sensible approach taking into consideration that neigbouring communities around the lake in the now Malawi and Tanganyika/Tanzania used to share the lake as a common resource without any subdividing boundary in place throughout generations before the arrival of the colonialists who created for themselves Malawi and Tanganyika, and that integration means a lot more opportunities for the smaller population of landlocked Malawians.

Otherwise, the matter is very unlikely going to solve through negotiation due to the fact that communities of Malawi and Tanganyika were not involved in the demarcation of the boundaries of their countries, and the population of Malawians and its future generations are very unlikely going to endorse a solution to surrender half of the North of Lake Malawi which obtains from the ongoing negotiation involving international mediator and the Governments of Malawi and Tanzania.

Kauli ya Prof. Lipumba kuhusu ripoti ya CAG ya IPTL / BoT

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI, 23 Novemba 2014

Katika Kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2000 na 2005 nilitumia muda mwingi kuelezea rushwa inayohusiana na mkataba wa TANESCO na IPTL. Kwa bahati mbaya hoja zangu hazikupewa uzito na vyombo vya habari.

Wakati Tanzania inaelekea kwenye uchaguzi Mkuu, Serikali ya CCM imewawekea fursa wapambe wake kujichotea fedha za umma kupitia fedha zilizowekwa katika akaunti maalum ya Escrow kwenye Benki Kuu ya Tanzania. Akaunti ya Tegeta Escrow ilianzishwa baada ya Shirika la kufua na kusambaza umeme la Tanzania TANESCO kudai kuwa kampuni binafsi ya kufua umeme ya IPTL imekuwa inaitapeli TANESCO kwa kuitoza Capacity Charge kubwa kuliko makubaliano yaliyoko katika mkataba. Toka imeanzishwa kampuni ya IPTL imekuwa mzigo mzito kwa TANESCO na watumiaji umeme wa Tanzania kwa sababu ya kuilipa capacity charge kubwa na mashine zake zinatumia mafuta mazito kufua umeme. Mafuta mazito yana bei kubwa zaidi ya mara mbili ya gharama za gesi.

UKAGUZI WA MDHIBITI NA MKAGUZI WA HESABU ZA SERIKALI (CAG)

Ukaguzi wa CAG wa akaunti Tegeta Escrow umebainisha kuwa TANESCO ililipa capacity charges zaidi ya kiwango kinachotakiwa kulipwa. TANESCO walipaswa kurejeshewa tshs 321 bilioni zilizolipwa ziada kwa IPTL kati ya mwaka 2002 - 2012. Kwa hiyo fedha zote za akaunti ya Escrow jumla ya tshs 306 bilioni ni mali ya Tanesco na bado wanaidai IPTL shilingi bilioni 15.

Kampuni ya Pan-Africa Power Tanzania Ltd (PAP) haikununua kihalali asilimia 70 ya hisa za kampuni ya Mechmar katika IPTL kwani zilizuiwa na mahakama na PAP hawana hati halisi za hisa hizo ( share certificates). Pia PAP ilifanya udanganyifu mkubwa katika malipo ya kodi kwa kutoa nyaraka za uwongo kuwa walinunua hisa kwa tshs 6m badala dola 20m na kuikosesha Serikali Mapato ya tshs 8.7 bilioni. Kosa hili linahusu pia mamlaka ya TRA Ilala ambao walihusika katika kupokea kodi ya mauzo hayo.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali alivunja sheria kwa kuelekeza kuwa kodi ya ongezeko la thamani kwenye capacity charges isilipwe na kupelekea Serikali kupoteza mapato ya tshs 21 bilioni.
Waziri kwa kushirikiana na Katibu mkuu Wizara ya Nishati na Madini hawakufanya uhakiki (due diligence) kuhusu uhalali wa umiliki wa kampuni ya IPTL. Katibu Mkuu alisaini kutoa fedha za escrow bila ya kuhakikisha fedha za TANESCO zinarudi na hivyo kupelekea kulipotezea Shirika zaidi ya tshs 321 bilioni.

Mkurugenzi wa Tanesco na Bodi ya Shirika la TANESCO haikutimiza wajibu wake wa kulinda maslahi ya shirika wanaloliongoza na kugeuza maamuzi yake yenyewe ( ama kwa kushinikizwa na Wizara au kwa rushwa) na kulikosesha Shirika shilingi bilioni 321.

Waziri Mkuu ambaye ndiye Kiongozi wa Serikali Bungeni na Msemaji Mkuu alilipotosha Bunge aliposema bungeni mwezi Mei kuwa fedha hizo sio za umma isipokuwa kodi.

James Rugemalira wa VIP Engineering and Management (VIPEM) na Harbinder Singh Sethi, wa Pan African Power (PAP) kwa kushirikiana na viongozi wa serikali wameitapeli na kuibia serikali fedha zote zilizochukuliwa toka akaunti ya Tegeta Escrow.

HATUA ZA KUCHUKUA

CUF inaitaka serikali kupitia TAKUKURU kuwakamata James Rugemalira na Harbinder Singh Sethi na kuwafungulia mashtaka ya rushwa na wizi wa mali ya TANESCO. TAKUKURU isifanye ajizi kama ilivyokuwa katika kesi ya Rada ambapo walimpeleka Sailesh Vithlani Mahakamani baada ya yeye kutoroka nchini. Hatuna uhakika kama Harbinder Singh Sethi bado yuko nchini.

Akaunti zilizopokea fedha ya Tegeta Escrow zisimamishwe (freeze). Fedha iliyobakia kama bado ipo isichukuliwe.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Werema, Waziri wa Madini na Nishati Prof. Sospeter Muhongo, Katibu Mkuu wa Waziri wa Madini na Nishati E. C. Maswi wajiuzulu au kufukuzwa mara moja.

TAKUKURU iwachunguze kama wamehusika na rushwa katika kuwezesha PAP kuchukua fedha za Akaunti ya Tegeta Escrow.

Ni wazi Benki Kuu ilikuwa na wasiwasi kuwa fedha za Tegeta Escrow zilikuwa zinachukuliwa kinyume cha utaratibu. Bila shaka Gavana alimjulisha Rais Jakaya Kikwete. Je Rais Kikwete alichukua hatua gani? Rais Kikwete aueleze umma kwa nini serikali yake ilishindwa kuzuia fedha za Tegeta Escrow zisiporwe wakati Benki Kuu ilionyesha wazi wasiwasi wake kuhusu uhalalali wa kuhamisha fedha hizo.

Sakata la Tegeta Escrow Account linaonyesha umuhimu wa Bunge kuisimamia serikali na Wabunge kutokuwa Mawaziri kama ilivyopendekezwa katika Rasimu ya Katiba na kuondolewa kwenye Katiba Inayopendekezwa. Waziri Mkuu amekuwa anatafuta kisingizio cha kuzuia mjadala wa taarifa ya CAG ndani ya Bunge.

Rasimu ya Katiba ilipendekeza zawadi za viongozi zirejeshwe serikalini. Taarifa ya vigogo wengi kupewa fedha toka akaunti inayomilikiwa na James Rugemarila inaonesha umuhimu wa kifungu hiki kilichomo katika Rasimu ya Katiba. Katiba Inayopendekezwa iliyoandaliwa chini ya uongozi wa Andrew Chenge imenyofoa kifungu hiki.

Baada ya mjadala ndani ya Bunge kukamilika CUF kwa kushirikiana na wadau wengine tutaandaa maandamano makubwa kulaani vtendo vya kifisadi kuhusiana na akaunti ya Tegeta Escrol na kuwapongeza Wabunge walioibua hoja hii na PAC mpaka kufikia CAG kufanya ukaguzi wa akaunti hii.
Viongozi wa serikali kushiriki kuihujumu TANESCO kunaonesha jinsi CCM kimekuwa Chama Cha Mafisadi kisichokuwa na hata chembe ndogo ya uzalendo. Nchi yetu inahitaji mabadiliko na uongozi thabiti wenye utashi wa kisiasa wa kupambana na rushwa na mafisadi bila woga. Uongozi utakaouhamasisha na kuushirikisha umma katika vita dhidi ya mafisadi. La sivyo Tanzania itakuwa na dola iliyofeli (A Failed State).

HAKI SAWA KWA WOTE

Ibrahim Haruna Lipumba
Mwenyekiti,
Jumapili, 23 Novemba 2014.

Lissu 'amtusua' Werema kuhusu hasara ya BoT escrow account

Lissu akizungumza Bungeni (kulia kwake ni Mhe. John Mnyika)

MNADHIMU wa Kambi Rasmi ya Upinzani, Tundu Lissu, amemvaa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, (AG), Jaji Fedrick Werema kuwa ameliingiza hasara taifa kwa kushindwa kuzuia wizi wa fedha zaidi y ash bilioni 300, zilizohifadhiwa katika Akaunti ya Escrow, Benki Kuu ya Tanzania (BoT) .

Amesema ameshindwa kuchukua hatua zozote dhidi ya mawaziri wa sasa na wa zamani wa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), na majaji wa Mahakama Kuu ambao wametajwa kuwa miongoni mwa watu waliovuna mabilioni ya fedha katika Akaunti ya Escrow.

Lissu alisema hayo juzi bungeni wakati alipokuwa akisoma maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani kuhusu muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali wa mwaka 2014.

Lissu alisema kama Bunge lingepitisha kifungu cha II hadi cha XXVIII ambacho kilikuwa kinampa nguvu Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuingilia kesi yoyote ya taasisi au mashirika ya umma mahakamani ilikuwa ni sawa na kiini macho.

Alisema pamoja na kuwepo kwa kifungu hicho ndani ya Katiba ya nchi lakini bado imekuwa sawa na kiini macho hasa kwa kitendo cha kuwepo kwa nyaraka zinazothibitisha ufisadi serikalini au matumizi mbaya ya madaraka kama ilivyotokea wakati wa kashfa ya Richmond/Dowans au Akaunto ya EPA pamoja na ufisadi wa sasa wa Akauti ya Escrow ya IPTL ambazo zingetolewa mahakamani.

“Mheshimiwa Mwenyekiti haya ni majigambo ya bure kwani, katika matukio mengi na makubwa ambayo yameliingizia Taifa hili hasara ya mabilioni ya fedha na kulichafua Taifa letu mbele ya jumuiya za kimataifa, Mwanasheria Mkuu amekuwa mhusika muhimu kama sio mkuu katika kashfa ya Escrow.

Akitolea mfano alisema katika kashfa inayoendelea sasa ya Akaunti ya Escrow, Mwanasheria Mkuu Mkuu, ameshindwa kuchukua hatua yoyote dhidi ya mawaziri wa sasa na wa zamani wa Serikali ya CCM, Mwanasheria Mkuu wa zamani, majaji wa Mahakama Kuu ambao wametajwa kuwa miongoni mwa waliovuna mabilioni ya fedha za Akaunti hiyo.

Aidha alisema mtangulizi wake katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu pia alishindwa kuchukua hatua yoyote kwa mawaziri na watendaji wa ngazi za juu ‘waliovuna’ mabilioni ya Richmond/Dowans mwaka 2007/08.

Lissu alisema kabla ya hapo Mwansheria Mkuu huyo alishindwa kuchukua hatua dhidi ya Mwanasheria Mkuu mwenzake aliyemtangulia (Chenge), ‘aliyekatiwa’ mgawo wa ‘vijisenti vya rada’ wakati Mwanasheria Mkuu mwenzake wa Uingereza kupitia Serious Fraud Office(SFO), ya nchi hiyo ikiwashughulikia mafisadi wa kiingereza walihusika na kashfa hiyo.

“Kashfa hiyo iliyoliingizia Taifa letu hasara ya mabilioni ya fedha za umma na kutupaka matope ya ufisadi duniani kote. Yote haya ni nje kabisa mikataba mingi ya kifisadi katika sekta mbalimbali za uchumi wa nchi yetu ambayo Serikali imeingia kwa sababu ya ushauri hafifu na usiofaa wa Mwanasheria Mkuu.

“Kama ilivyokuwa imeombwa na Serikali hii ya CCM kungepanua uwanja zaidi kwa Mwanasheria Mkuu kuendeleza hujuma dhidi ya masilahi halisi ya nchi yetu kwa kuyaingiza mashirika na taasisi nyingine za umma katika makucha ya Sheria ya Mashauri ya Serikali,” alisema Lissu.

Lissu ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), alisema Mwanasheria Mkuu alihoji uhalali wa Shirika Hodhi la Serikali (CHC), kuwalipa mawakili wake wa kujitegemea Sh milioni 855 kama malipo ya mawakili katika kesi 338 za shirika hilo zilizokuwa na thamani ya Sh bilioni 373.264 kwa maneno ya Mwanasheria Mkuu mwenyewe.

“Kama taasisi na mashirika hayo yana mawakili wenye uzoefu iweje waajiri mawakili hao wa kijitegemea na kutumia kiasi kama hicho cha fedha. Malipo yaliyolalamikiwa na Mwanasheria Mku ni sawa na asilimia 0.22 ya thamani ya kesi zote.

“Kauli hii pekee inaonyesha kwamba Mwanasheria Mkuu ameteleza vibaya kisheria. Ili isonekane kwamba tunamdhalilisha Mwanasheria Mkuu bila sababu yoyote ya msingi tunaomba kufafanua kauli hii.

“…Utaratibu wa malipo kwa mawakili umewekwa na kanuni za malipo ya mawakili na maamuzi ya gharama za mashauri za miaka ya 1991. Kwa waliogombaniwa ambalo thamani yake ni Shilingi milioni tatu au zaidi, ni asilimia tatu ya thamani ya shauri husika,” alisema

Alisema kutokana na hali hiyo kama mawakili wa keso zote zenye thamani iliyotajwa na Mwanasheria Mkuu, basi malipo yao halali yangekuwa takriban Sh bilioni 11.198 balada ya kulipa mabilioni halali.

Jaji Werema

Awali akiwasilisha Muswada wa mabadiliko hayo ya Sheria mbalimbali bungeni, ambao umelenga kufanya marekebisho katika sheria 32 kwa lengo la kuimarisha matumizi ya sheria hizo ili kuongeza masharti mapya katika sheria.

“Muswada huu ulikuwa umegawanyika katika sehemu kuu Thelathin na tatu, baada ya marekebisho yakiyofanywa sasa Muswada utakuwa na sehemu tano. Baada ya majadiliano ya kamati ya Katiba, Sheria na Utawala Serikali imeridhia.

“Sehemu ya pili ya Muswada ilikuwa ni 29 kabla ya marekebisho yaliyofanywa na inapendekeza marekebisho katika sheria ya mbolea, sura ya 378 na ibara ya 58 ya muswada,” alisema Jaji Werema

Alisema sehemu tano ya muswada ilikuwa ni sehemu ya 33 ya marekebisho na inapendekeza kwenye sheria ya huduma za maji na usafi na mazingira sura ya 272 kwa mujibu wa marekebisho katika sehemu ya kifungu cha 59.

Harusi ya David Kafulila na Jessica Kishoa

 David Kafulila na Jessica Kishoa

MBUNGE wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi), ameaga ukapera baada ya kufunga ndoa na Jessica Kishoa katika Kanisa Katoliki, Parokia ya Uvinza, huku akisindikizwa na Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe (CCM), aliyekuwa mpambe.

Akizungumza katika harusi hiyo jana, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto alimpongeza Kafulila kwa kukamilisha ndoa yake na mwenza wake na kumuomba mke wa Kafulila, kuwa mvumilivu katika kipindi hiki kwani hawatakuwa na fungate na mume wake hadi watakapomaliza kushughulikia suala la Escrow lililoko mbele yao.

Naye Filikunjombe alimpongeza Kafulila kwa kukamilisha mchakato wa ndoa yake, licha ya kuwa katika kipindi kigumu cha kupigania maslahi ya Watanzania.

Naye Kafulila alishukuru watu wote waliojitoa kwa hali na mali kuhakikisha harusi yake inafanikiwa, lakini alisema kuwa analo jukumu kubwa katika kuhakikisha tuhuma za ubadhirifu wa fedha za umma kupitia akaunti ya Escrow, linafikia mwisho na kila mmoja anavuna alichopanda.

Harusi hiyo pia ilihudhuriwa na Mbunge wa Mbozi Magharibi, David Silinde (CHADEMA) ambaye alisema kuwa Kafulila ni kaka yake na wametoka mbali kisiasa na kwamba anamuunga mkono katika ajenda wanayoisimamia kwa maslahi ya Watanzania. (HabariLeo: Kafulila aoa, mpambe Deo Filikunjombe)

Mbunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe akimpongeza Mbunge wa jimbo la Kigoma Kusini David Kafulila (kati kati) huku mke wa Kafulila, Jessica Kishoa (kulia) akishuhudia


Jessica Kishoa (kushoto) , Mbunge wa jimbo la Kigoma Kusini David Kafulila wakibarikiwa katika ibada ya ndoa iliyofanyika kanisa katoliki parokia ya Uvinza mkoani Kigoma.
Zitto Kabwe, mbunge wa Kigoma Kaskazini na David Silinde, mbunge wa Mbozi, wakishuhudia tukio la ndoa ya Kafulila na Bi.Jessica katika Kanisa Katoliki Parokia ya Uvinza.


Wazazi wa maharusi wote wawili walikuwa miongoni mwa mashuhuda wa tukio hilo.


Bwana na Bibi David Kafulila baada ya kula kiapo cha ndoa.


Mpambe wa David Kafulila, Deo Filikunjombe, akimtambulisha mkewe Sarah, ambaye pia alikuwa mpambe wa Bibi harusi.


Wanandoa wakifurahia vyeti vya vya ndoa pamoja na marafiki zao.

Maharusi wakiondoka Kanisani kufunga ndoa tayari kabisa kuelekea kwenye sherehe ya ndoa yao nyumbani kwa mzee Zacharia Kafulila, mjini Uvinza.


Kikwete analazimisha Lowasa awe Rais

Gordon Kalulunga

NCHINI India makabila madogo hayapati uongozi wa juu ya nchi, kutokana na kasumba tu, ya kwamba kama hujasoma shule fulani ambayo ni ya karo kubwa huwezi kushika madaraka.

Maana yake ni kwamba masikini wote kamwe hawataweza kushika madaraka katika nchi hiyo tofauti na hapa nchini Tanzania.

Mfano wa nchi ya India unashabihiana na jirani zetu wa Kenya, ambao kabila moja kubwa la Wakikuyu, ndiyo wanazidi kuwa watawala na wamiliki wakuu wa ardhi ya nchi hiyo kwa asilimia 90, vivyo hivyo ni tofauti sana na hapa nchini Tanzania.

Kwa mfumo huo, mahala pengine wananchi wanaamua kuchagua mtu anayetokana miongozi mwao na hali kama hiyo imejitokeza katika taifa la Indonesia ambako wananchi wamempa fundi seremala kuwa rais.

Baada ya kuona hivyo, serikali ikakatalia fedha kwa ajili ya kuapishwa kwake, lakini wananchi wakiwemo wauza vibama, walichanga fedha kwa ajili ya sherehe.

Mwanzoni mwa wiki hii, nilipata simu ya rafiki yangu mmoja ambaye ni afisa wa Jeshi la Polisi, pamoja na salamu, alisema kuwa kama nipo karibu na baadhi ya viongozi wa CCM niwaambie kuwa muda ukifika hawapaswi kumsimamisha mbunge wa Jimbo la Monduli, Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa katika katika nafasi ya Rais.

Alitoa sababu moja ambayo alisema kuwa ni sababu kubwa sana na itakuwa turufu ya siasa za vyama vya upinzani. Sababu hiyo ni kwamba kabla hajajiuzulu(Lowassa), aliyekuwa mwenyekiti wa tume ya uchunguzi kuhusu Richmond, Dkt. Harrison Mwakyembe, alitoa majibu ya tume yake mbele ya Bunge huku akirekodiwa na waandishi wa habari na baadhi ya mikanda ya siku hiyo ipo mitaani.

“Ile mikanda inamaana itakusanywa? Maana wapinzani watawawekea wananchi ili waangalie na kusikiliza, itakuwa pigo kubwa kwa CCM na wapenzi wa chma hicho, anayefaa ni mtoto wa mkulima, Mizengo Pinda” aliniambia rafiki yangu huyu.

Sikumpuuza bali niliheshimu mawazo yake na uhuru wa kusema mtazamo wake, ambao kimsingi ulinitia shaka kwasababu yeye pia ni mzawa wa mkoa wa Rukwa, ambako anatokea kiongozi aliyemtaja kuwa nikipata nafasi ya kuzungumza na viongozi wa CCM wenye maamuzi, niwaambie kuwa anafaa fulani na fulani hafai.

Ieleweke kwamba, hakuna kitu kizuri kisicho na ubaya na hakuna ubaya usio na uzuri kwa upande mwingine wa shilingi, sawa na picha mnato ingawa haizungumzi lakini anayeona anaweza kuifurahia au kuichukia.

Kuna wakati niliwahi kusema kuwa nawafurahia sana wezi maana wamenifikisha mahala ambapo katika nyumba yangu niliweza kuweka mlango imara ili wezi wasiweze kuingia kwa urahisi ndani mwangu na kuiba vitu, ingawa sifurahii wizi.

Wizi ni jambo baya na kisheria ni kosa ambalo wanaobainika wanafungwa na baadhi wanaohisiwa wanakamatwa na kuhojiwa na vyombo vya kisheria vinavyohusika(sina imani kama Lowassa alihojiwa na akina Dkt. Mwakyembe).

Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimekuwa kikitangazwa na baadhi ya wanasiasa wa vyama pinzani(kwa sasa) kuwa ni chama cha siasa kinachofumbia macho (mafisadi) ambao wamekuwa wakila bila kunawa, lakini sijawahi kuwasikia wakimtaja Lowassa, bali kiongozi huyu anatajwa sana na baadhi ya wapinzani wake wa siasa ndani ya CCM.

Licha ya kuwa ufisadi huo ni jambo baya inapothibitika, lakini nakipongeza sana chama hicho kwa kuwa na kimya kingi ambacho kinaleta mshindo mkubwa kwa vyama vingine vya siasa hapa nchini.

Wanaokitangaza chama hicho kuwa ni chama cha mafisadi hawakosei sana kwasababu kila jambo lina uzuri na ubaya wake kama nilivyosema hapo juu.

Uzuri ninaouona kwa ufisadi wa CCM ni kuruhusu hata baadhi ya makabila ambao kimsingi na kwa historia walikuwa manamba au wapagazi nao sasa ni moja ya wanaotajwa kuwa mafisadi.

CCM imeweka mfumo hata wa wapagazi ambao ni masikini na makabila madogo kama Wakwele, waandali, waha, wanyamanyafu na makabila mengine madogo kuwa viongozi wa nchi hii na baadhi yao kutajwa kwenye ufisadi.

Hofu yangu baada ya kuondoka CCM madarakani ni kwamba taifa linaweza kuwa na mafisadi wa upande mmoja na kabila moja la kusini, kusini magharibi, kaskazini au mashariki.

Leo hii tuna utitiri wa wanaoitwa wagombea wa nafasi za rais kupitia vyama mbalimbali, akiwemo, Edward Lowassa.

Kiongozi huyu tangu mwaka 2008 tuliposikia na kuambiwa kuwa alihusika katika kashfa ya mradi wa kufua umeme wa Richmond, mpaka leo hii hajapelekwa mahakamani na kama amepelekwa basi kwa siri kubwa sana na hata hukumu yake tunashindwa kuelezwa.

Waziri mkuu huyu aliyejiuzuru chini ya uongozi wa Rais Jakaya Kikwete, huku nyikani tunashindwa kuelewa ukweli wake maana miruzi iliyopo huku kwetu ni mingi sana imuhusuyo Lowassa na Rais Kikwete.

Sasa imebaki miezi isiyopungua kumi, ili tuingie katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Ni vema ukweli kuhusu Lowassa dhidi ya tuhuma za ufisadi wa Richmond, ukajulikana ili tumkate kwa nguvu zetu zote au tumkubali kwa vibwebwe na nderemo kuu.

Kama siyo serikali kumpelekea mahakamani kiongozi huyu ili ijulikane ukweli wa miruzi ya ufisadi anaotajwa nao, nimuombe Lowassa mwenyewe, asimame na kueleza ukweli wa tatizo la Richmond na kwanini kama yeye alihusika hajawahi kuomba radhi kwa watanzania kabla hajapiga kipyenga rasmi cha urais.

Kuna maeneo ambayo nimepita hapa nchini, jina la Lowassa limekuwa kama dini, amekaa mioyoni mwa watu hata wasiomfahamu lakini wanaimba Lowassa! Hivyo kabla wengine hawajajawa na imani ya jina Lowassa, ni vema ukweli wa Richmond na Lowassa ukawa peupe kwa mustakabali wa CCM 2015.

Vinginevyo katika jambo hili, Rais Jakaya Kikwete analazimisha Lowassa kuwa mrithi wake na kama siyo hivyo, basi pia analazimisha wananchi wamtafute rais wanayemtaka na wala si yule anayetakiwa na chama fulani cha siasa hapa nchini.

Mkasa wa mtoto aliyenusurika kifo kwa kipigo cha "binti wa kazi"  • ILANI! Habari hii inaambatana na video ya kuhuzunisha iliyopachikwa hapo chini.

Habari kutoka Rukungiri, Uganda zinasema kuwa mtoto mdogo wa miaka miwili aliyekuwa mgonjwa, amenusurika kifo baada ya kupata kipigo kutoka kwa dada wa kazi, Jolly Tumuhiirwe (22), aliyekuwa akimlisha.

Jolly alimpiga mtoto huyo Jumamosi iliyopita wakati akimlisha mtoto huyo aliyekuwa mgonjwa, baada ya kushindwa kula haraka kama alivyotarajiwa na kutapika.

Bila kujua kuwa nyumba hiyo ilikuwa na kamera ya usalama liyokuwa ikichukua matukio yote, Jolly aliyeanza kazi katika nyumba hiyo miezi mitatu iliyopita, aliamua kunywa uji wa mtoto huyo baada ya kuona mtoto mwenyewe hawezi kunywa kwa haraka.

Picha ya sekeseke hiyo ilitembea sana katika mitandao ya kijamii jana watuw akibadilishana kw akasi ya ajabu.

Wakati akinywa uji huo, picha hiyo iliyosambaa katika mitandao ya jamii jana, ilionesha Jolly akimpiga vibao mtoto huyo kabla ya kumtupa chini akiangukia uso, kutoka katika kochi la sofa.
Wakati mtoto huyo akiwa chini amelala kwa tumbo, Jolly akitumia mkono wa tochi, alianza kumpiga mtoto huyo katika makalio yake akiwa hana nguo yoyote.

Kama vile hakuridhika na kipigo hicho, dada huyo wa kazi aliamua kumpiga mtoto huyo mateke na baadae aliamua kumkanyanga kiunoni kwa mguu wake.

Picha hiyo imeeonesha namna dada huyo alivyompiga mtoto huyo kwa teke kwa mara nyingine, kabla ya kumnyanyua kwa mkono mmoja na kumuingiza katika chumba kingine.

Taarifa kutoka katika familia ya mtoto huyo, zilizoripotiwa na mtandao wa The investigator today, imeeleza kuwa baba wa mtoto huyo, Erick Kamanzi, aliporejea nyumbani alibaini kuwepo kwa michubuko katika maeneo ya nyuma ya mwanaye.

Kabla ya kuuliza kilichotokea, Kamanzi alikimbilia chumbani kwake kuputia video na kuona kilichofanyika, ambapo alimvamia Jolly na kuanza kumpiga na baada ya kumaliza hasira zake, alirejea kwa mwanaye ili kumsaidia.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, dada huyo wa kazi aliamua kukimbilia Kituo cha Polisi Kiwatule, ambako aliripoti tukio la kuvamiwa na kupigwa na mwajiri wake na askari Polisi walifika nyumbani na kamkamata Kamanzi.

Akiwa kituo cha Polisi, taarifa za Polisi zinasema Kamanzi alikiri kosa na kuwekwa ndani na baada ya muda, aliwaomba askari hao kuangalia picha za video zilizosababisha ampige msichana huyo wa kazi, hatua iliyosababisha askari Polisi kumuachia mara moja.

Akizungumza na mtandao wa The investigator today, Msemaji wa Jeshi la Polisi la Uganda, Kamishna wa Polisi, Fred Enanga, alikiri kuwa Jolly ameshafunguliwa mashitaka katika Mahakama ya Nakawa juzi kwa kosa kukiuka Sheria ya Kuzuia Mateso.

Hata hivyo, Kamishna Enanga aliongeza kuwa Jeshi la Polisi linajiandaa kubadilisha mashitaka ili yawe ya jaribio la kuua.

Kamishna Enanga alisema Jolly atafikishwa tena mahakamani Desemba 8, 2014. Juhudi za mtandao huo kupata maelezo ya mama wa mtoto huyo, Angella ambaye ni raia wa Rwanda, hazikufanikiwa, kwa kuwa chanzo cha habari kilikataa kuzungumzia hilo.

Hatari hii! Watoto wanaparamia kuta

Kinondoni Primary School pupils in Dar es Salaam precariously scale up a wall to head back to their classrooms after a brief sports break on Saturday. Upon returning, the pupils noticed that the gate to the school had been closed.

photo: Mohamed Mambo/DAILY NEWS


Picha za jezi za Taifa Stars zilizopendekezwa na wabunifu