Wananchi wamng'oa meno kwa kombeo askari wa FFU

Pc Idd Makame (25) aliyejeruhiwa vibaya mdomoni kwa kung’olewa meno sita baada ya kupigwa jiwe kwa kutumia kombeo na watu wanaodaiwa kuwa ni wachimbaji haramu wa madini katika mgodi wa Mwadui akiwa amelazwa katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga

Kumetokea tukio la aina yake katika mgodi wa madini ya almasi wa Mwadui uliopo katika wilaya ya Kishapu mkoani ambapo askari polisi wa kikosi cha kutuliza ghasia wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga Pc Idd Makame(25) amejeruhiwa vibaya mdomoni kwa kung’olewa meno sita baada ya kupigwa jiwe kwa kutumia kombeo (kwa lugha ya kisukuma Nh'ago) na watu wanaodaiwa kuwa ni wachimbaji haramu wa madini katika mgodi wa Mwadui wakati akitimiza wajibu wake wa kuhakikisha usalama wa raia na mali zao

Tukio hilo limetokea Novemba 21,2014saa mb ili na robo usiku katika eneo la Tanex katika mgodi huo wakati askari huyo akiwa na askari wenzake wakiongeza nguvu baada ya askari wa kampuni ya ulinzi ya Zenneth iinayolinda mgodi wa Mwadui kushindwa kuwadhibiti wachimbaji wadogo wa madini maarufu "Wabeshi" waliotaka kuingia kwa nguvu mgodini wakiwa na silaha za jadi.

Mashuhuda wa tukio hilo wameiambia malunde1 blog kuwa kampuni ya ulinzi ya Zenneth Security Services Limited inayolinda mgodi huo ilipata taarifa kuwa kuna wachimbaji haramu maarufu kwa jina la Wabeshi walitaka kuvamia mgodi wakiwa na silaha za jadi ikiwemo mishale,mikuki,virungu,makombeo,mapanga na fimbo.

Kufuatia hali hiyo askari hao wa Zenneth wakifika eneo la tukio kuwadhibiti Wabeshi hao lakini ghafla walianza kushambuliwa kwa silaha za jadi yakiwemo marungu,mishale,mikuki na makombeo.

Baada ya kuona wanazidiwa nguvu,askari wa Zenneth walilazimika kuomba msaada wa askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) cha jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga.

Baada ya askari wa FFU kufika eneo la tukio nao walianza kushambuliwa na Wabeshi hao ,ndipo PC Idd akapigwa jiwe mdomoni kwa kutumia kombeo na kung’oka meno sita mdomoni na kukimbizwa katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya matibabu.

Mkurugenzi wa kampuni ya ulinzi ya Zenneth Security Services Limited Elisha Ndulu amethibitisha uwepo wa tukio hilo.

Naye mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Shinyanga Dkt Mfaume Salum amesema Pc Idd alipigwa na kitu chenye ubapa mdomoni na kusababisha meno sita kung’oka na anaendelea kupatiwa matibabu,hali yake inaendelea vizuri.

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha alikiri kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa tayari wanawashikilia watu wanne kwa mahojiano zaidi na wanaendelea kufanya uchunguzi ili kuwakamata wahusika wengine.

Tweet by Pres. Kikwete on allegations of Govt to evit Maasai

Spika akataa hoja ya kujadiliwa akaunti ya escrow ya BoT

Spika wa Bunge Mhe. Anna Makinda akiliongoza Bunge mjini Dodoma leo, wakati akitoa ufafanuzi kuhusu mtu mmoja kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma kwa kosa la kupatikana akisambaza Ripoti ya (ESCROW) ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali kinyume na Sheria Baada ya Hoja iliyoibuliwa na Mhe. James Mbatia.


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Anne Makinda amezuia hoja za Wabunge kutaka kujadiliwa Bungeni, suala la kuvuja kwa ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) kuhusu wizi wa fedha za Benki Kuu (BoT) kupitia akaunti ya Tegeta escrow, kwa vile suala hilo lipo mikononi mwa polisi tayari.

"Tukipata taarifa ya polisi ndipo tutajadili. Tujadili nini? ...ninasema ofisi yangu imedhalilishwa, kwa hiyo tumeshirikiana na ofisi ya Polisi pamoja na akina Mbatia wenyewe... Tukipata taarifa tutachukua hatua. ...hakuna ubabe. Nasema hivi, nyaraka zilizopewa kamati ya PAC zina alama maalumu. Hizi zilizosambazwa, ndiyo maana polisi tumeruhusu, polisi hawa walipom-identify, Katibu wa Bunge alikwenda kuarifu polisi, ameshikwa, yupo ndani. Sasa hivi wanaendelea kufanya uchunguzi, huyu alipata wapi documents hizo na ataje watu walioempa. Ya pili, kama ni mashine zile, ni mashine gani zilitumika kusudi na zenyewe ziwajibike" 
amenukuliwa akisema Makinda.

Spika amechukua uamuzi huo baada ya James Mbatia (NCCR-Mageuzi, Mbunge wa Kuteuliwa na Rais) kuomba Bunge lisitishe shughuli zake, ili litoe nafasi kujasili suala la kusambaa mitaani kwa nyaraka zinazohusiana na ripoti ya CAG.

Keshokutwa Novemba 26 ndipo inapotarajiwa kuwa ripoti hiyo itawasilishwa Bungeni kwa hatua zaidi.

Mbunge wa Kuteuliwa Mhe.James Mbatia akiwa amekaa na Hasimu wake wa Siasa jimbo la Vunjo Mhe.Agustino Mrema wakimsikiliza kwa makini Spika wa Bunge Mhe.Anna Makinda.
Video ya kikao cha juzi...

Taarifa: Taratibu za Tiba za Rais Kikwete zakamilika

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
Website : www.ikulu.go.tz               

Fax: 255-22-2113425


PRESIDENT’S OFFICE,
     STATE HOUSE,
             1 BARACK OBAMA ROAD,   
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Taratibu za Tiba za Rais zakamilika

Taratibu za matibabu ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, zimekamilika leo, Jumatatu, Novemba 24, 2014.

Taratibu hizo za matibabu za Mheshimiwa Rais Kikwete zimekamilika kiasi cha saa 12 asubuhi ya leo wakati madaktari bingwa katika Hospitali ya Johns Hopkins iliyoko mjini Baltimore, Jimbo la Maryland, Marekani, walipomfanyia hatua ya mwisho ya tiba.

Hata hivyo, Rais Kikwete ataendelea kupumzika na kuangaliwa kwenye Hoteli Maalum inayohusiana na Hospitali ya Johns Hopkins kwa siku mbili hadi tatu kabla ya kuanza safari ya kurejea nyumbani.

Kama kila kitu kitakwenda kama ilivyopangwa na madaktari, Rais Kikwete anatarajiwa kurejea nyumbani Jumamosi, Novemba 29, 2014.

Rais Kikwete aliondoka nchini Alhamisi ya Novemba 6, 2014, kwenda kufanyiwa uchunguzi wa afya yake lakini madaktari katika Hospitali ya Johns Hopkins waliamua kumfanyia upasuaji wa tezi dume Jumamosi ya Novemba 8, 2014.

Rais Kikwete anaendelea kuwashukuru Watanzania kwa sala na maombi yao ya kumtakia heri ya kupona haraka na kurejesha afya njema katika kipindi chote cha ugonjwa wake.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.

24 Novemba,2014

Jebby amerudi na wimbo mpyaMsanii wa siku nyingi wa kundi la TMK UNIT Jebby anatatajia kuachia wimbo wake mpya kuanzia tarehe 25.11 au tarehe 5.12 mwaka huu.

Akizungumza na matukiodaima.com, amesema kuwa alikuwa amekaa kimya muda mrefu bila kuachia wimbo wowote kutokana na changomoto za kimuziki na maisha nje muziki.

Hata hivyo Jebby alisema kuwa wimbo wake ameufanya katika studio Mazuu Record na producer wa wimbo huu ni Mazuu na kuomba Watanzania kumpokea tena kama ambayo walikuwa wakimpokea hapo awali.

Edited by Fredy Mgunda
wavuti.com imeshirikishwa taarifa hii na Francis Godwin/Matukio Dai,a Blog

Mhe. Kabati asema UKAWA inapotosha wananchi kuhusu Katiba pendekezwa

Ritta Kabati

MBUNGE wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati (CCM) amewakata wananchi kutokubali kudanganywa na vyama vya siasa vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) juu ya mchakato wa katiba iliyopenekeshwa na badala yake kuungana na  Watanzania wapenda maendeleo kuikubali katiba hiyo muda utakapofika.

Mbuge Kabati alitoa kauli hiyo kwa nyakati tofauti juzi na jana wakati wa semina zake za ndani na wanawake wanachama wa UWT katika wilaya ya Iringa, Kilolo na Mufindi, semina iliyolega kuwajengea uwezo wa kujiamini kwa wanawake waliojitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi wa serikali za mitaa na vijijini.

"Mimi kama mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa wajibu wangu ni pamoja na kukutana na wananchi wa Iringa na kuwajengea uelewa mpana wa katiba hiyo iliyopendekezwa ila muda ukifika wa serikali kutangaza mchakato wa kupokea maoni ya wananchi juu ya katiba hiyo iliyopendekezwa basi viongozi hao waweze kuelewa zaidi pamoja na wananchi wanaowazunguka... hivyo nitaendelea kutoa elimu kwa viongozi wa chama katika semina mbalimbali."

Kabati alisema kumekuwepo na upotoshwaji mkubwa ambao umeendelea kufanywa na UKAWA kwa kuzunguka huku na kule kujaribu kupotosha ukweli juu ya katiba iliyopendekezwa kwa madai kuwa ni katiba ya CCM jambo ambalo ni upotoshaji mkubwa na kuwa mchakato wa katiba hiyo ulifanywa na vyama vyote na makundi maalum.

Pia alisema kuwa kitendo cha baadhi ya wanasiasa wasilolitakia mema Taifa hili kwa kupotosha juu ya katiba hiyo ni sawa na kutaka kuona nchi haitawaliki na hivyo kuamua kuanza upotoshaji huo.

Alisema kuwa si kweli kama katiba hiyo iliyopendekezwa haina jambo lolote la msingi kama ambavyo UKAWA wamekuwa wakizunguka na kupotosha ila alidai kuwa ndani ya katiba hiyo kuna mambo mengi yamezingatiwa kwa ajili ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

Akielezea kuhusu mchakato wa uchaguzi wa serikali za mitaa ,vijiji na vitongoji unaotaraji kufanyika hivi karibuni alisema kuwa upande wa mkoa wa Iringa wanawake baada ya kuhamasishwa wamepatika kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu za kuwania nafasi mbali mbali za uongozi na kuwa baadhi ya maeneo wamepata kushinda kwa kishindo nafasi walivyoomba ndani ya CCM wakisubiri uchaguzi rasmi wa serikali.

Hivyo aliwataka wananchi wa mkoa wa Iringa kujitokeza kuwapa kura zao wanawake hao waliogombea nafasi mbali mbali na kuwa imani yake kuona kunakuwa na uongozi mchanganyiko.

wavuti.com imeshirikishwa taarifa hii na Francis Godwin/MatukioDaima Blog

Mahojiano na Ernest Napoleon, Muigizaji wa filamu ya 'Going Bongo'

 
Cheif wa swahilivilla blog Abou Shatry na Ernest Napoleon

Blog ya swahilivilla imepata fursa ya kufanya mahojiano na muigizaji, muongozaji na muandishi wa filamu ya kwanza Afrika Mashariki kukubalika kuuzwa kupitia iTunes 'Going Bongo Ernest Napoleon'

Pata filamu hiyo ya kihistoria kwenye iTunes bit.ly/goingbongoitunes ama DVD bit.ly/goingbongodvd. Check trailer hapa bit.ly/goingbongotrailer, share na wenzio.

Jiunge nasi ka kusikiliza.


Angalia Trailer ya Filam Going Bongo 

Msaada kwa ajili ya Suleiman Othuman tafadhaliAssalam Aleikum ndugu zangu mnaotusoma kwenye blog hii kila siku, msaada unahitajika kwa kijana Suleiman Othman Ally mwenye umri wa miaka 19, mkaazi wa Zanzibar, amepatwa na tatizo la uvimbe mkubwa kwenye mgongo wake baada ya kupatwa na ajali kugongwa na Vespa kwa muda wa siku nyingi tu, walimpeleka Hospitali ya Mnazi mmoja ambapo ilishindikana kupata matibabu kutokana na damu nyingi aliotoka wakati wa upasuaji, hivyo kuwalazimu kumshona bila ya kumfanyia operation iliyokuwa wamemkusudia.

Kijana Suleiman Othuman hali yake inazidi kudhoofika na maumivu makali alionayo kwa sasa hawezi kukaa kusimama vizuri na hata kulala inavyostahiki kwa sababu ya ule uvimbe aliokuwa nao kwenye kiuno chake kam picha inavyojionyesha.

Hivi sasa familia yake haina budi kuomba ushirikiano wa msaada wenu kwa ajili ya kumgharamia mtu mmoja wa familia kufuatana nae nchini India kwaajili ya matibabu, kutokana na gharama ni kubwa na uwezo ni mdogo.

Hivi sasa yuko hospitali ya Mnazi Mmoja wodi ya chini upande wa dirisha la dawa kitanda no 12.

Ndugu zangu tujitahidini kuokoa maisha ya ndugu yetu Suleiman Othuman kwa hali na mali.

Kwa mtu yoyote atakayeguswa na habari hii, na mwenye kutaka kuchangia msaada wake anaweza kuwasiliana na Mama yake mkubwa. Bi Salma.

Numba yaze za simu ni-:

255777489015
Tigo: 255655489015

Pia unaweza kuwasiliana na Mdau wa Blog Hii Abou Shatry Number 301-278, 3977,
Email [email protected]

Pichani kiijana Suleiman Othuman akiwa amelazwa hospitali ya Mnazi Mmoja wodi ya chini upande wa dirisha la dawa kitanda no 12.

Katibu Mkuu UVCCM apata mapokezi ya kihistoria Mbinga


Katibu mkuu wa jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa Ndugu Sixtus Mapunda amepata makubwa wilayani Mbinga yaliyoacha gumzo kubwa wilayani hapo. Mapunda ambaye alitoke wilaya ya Nyasa amepokelewa kwa kishindo kikubwa na viongozi wa CCM pamoja na mamia ya wananchi wa wilaya ya Mbinga ambako ndipo alikozaliwa.

Mapunda ameingia Mbinga jana akitokea wilaya ya Nyasa ambapo ni muendelezo wa ziara yake ya siku tano (5) Mkoani Ruvuma. Ziara ambayo inalenga kukagua na kuhamasisha ujenzi na uimara wa jumuiya mkoani humo pamoja na kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha mapinduzi ya mwaka 2010-2015.

Katika hotuba yake Katibu Mkuu amewataka wananchi wa Mbinga kujitokeza kwa wingi na kuwachagua wagombea wanaotokana na Chama Cha Mapinduzi katika uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotegemewa kufanyika mapema mwezi ujao pamoja na uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwishoni mwa mwaka 2015.

Pia Katibu Mkuu, Mapunda amemtembelea Mzee Constantine O. Millinga mmoja wa waasisi kumi na watano (15) walioanzisha Chama Cha Ukombozi cha TANU wakiongozwa na Marehemu Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, mnamo tarehe 7.7 1954. Mzee Millinga ni miongoni mwa wawili kati ya waasisi hao ambao wako hai mpaka hivi sasa.

Mapunda ametoa wito kwaWatanzania, wananchama wa Chama Cha Mapinduzi na hasa Vijana wa Taifa hili, kuwaenzi na kuwatembelea wazee ambao ni waasisi, wazalendo wa kweli na wapigania uhuru wa nchi hii, ambao wametuwekea misingi ya Umoja na Utaifa ambayo imeifanya Tanzania kuwa nchi ya amani na utulivu.

Katibu Mkuu huyo wa UVCCM anaendelea na ziara yake Mkoani Ruvuma ambapo atatembelea wilaya ya Namtumbo na baadae Songea Mjini ambako atahutubia mkutano mkubwa wa hadhara katika wilaya hiyo ambayo ni makao makuu ya Mkoa wa Ruvuma.Pongezi Datius Jovit kwa kuhitimu elimu ya Chuo KikuuKijana Datius akiwa katika Picha ya Pamoja na Baba yake Mzazi (nyuma ya babu yake aliyevaa miwani) Babu zake na dada zake wakati alipotunukiwa nondo yake ya elimu kutoka Chuo Kikuu Kishiriki cha DUCEDatius Akiwa katika picha ya pamoja na Baba yake Mzazi (Kushoto) pamoja na Babu yake mdogo (kulia)Akivishwa taji na Dada yake aitwaye NeemaAkiwa na Dada

wavuti.com imeshirikishwa picha habari hii na Josephat Lukaza wa http://www.josephatlukaza.com
Pongezi Datius kwa kuhitimu masomo yako.

TAWNET yaipongeza Vodacom kuwa mllipa kodi bora


CHAMA cha Waandishi wa Habari za Kodi Tanzania (TAWNET) umeipongeza kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania kwa kuwa moja kati ya walipa kodi bora wakubwa wa pili kwa mwaka 2014.

Sambamba na kampuni ya Vodacom, TAWNET pia imeipongeza kampuni ya bia Tanzania (TBL) na Kampuni ya Sigara Tanzania (TCC) kuweza kushika nafasi katika makampuni matatu bora. Mwaka huu, mchango wa Vodacom katika pato la taifa umeongezeka na kuisukuma kampuni hiyo katika nafasi ya pili kutoka ya tatu waliyoshika mwaka jana.

Mkurugenzi Mtendaji wa TAWNET Judica Tarimo aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuwa, Vodacom imeshika nafasi ya pili bora kwa mara ya kwanza haijawahi kutokea na

Kodi ni chanzo kikuu cha mapata kwa serikali na ndiyo inaiwezesha kutoa huduma kwa wananchi. Kwa niaba ya wana TAWNET napenda kutoa pongezi za dhati kwa Vodacom kwa kulipa kodi kwa uaminifu na pia makampuni mengine yafuate mfano huu, alisema.

Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa, Vodacom imekuwa mdau mzuri wa maendeleo kwa Watanzania na kuongeza kuwa uwekezaji wake umekuwa wa manufaa makubwa kwa nchi kwani pamoja na kuwa mlipa kodi mzuri wa pili, pia kupitia mfuko wake wa jamii kusaidia wa Vodacom Foundation kampuni hiyo imeweza kusaidia watanzania wenye matizo mbali mbali.

Alisisitiza kuwa nchi inaweza kuondokana na utegemezi wa ufadhili endapo kila mtu na makampuni yatalipa kodi kwa uaminifu na kuzitaka mamlaka zinazohusika kuwa macho dhini ya watu na makampuni yanayotumia mbinu mbali mbali kukwepa kulipa kodi ahalali za serikali.

Kuhusu kodi zilizolipwana Vodacom katika kipindi cha miaka miwili na kuifanya kampuni hiyo kuwa miongozi mwa walipa kodi bora Mtendaji wake Mkuu, Mkuu Rene Meza anasema“katika kipindi cha miezi sita cha mwaka wetu wa fedha kuanzia mwezi Aprili mpaka Septemba 2014,tumelipa kodi serikalini shilingi 27.6 bilioni/- kwa Kodi ya mapato,na tulikusanya shilingi bilioni 141.5 kwa kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) na kodi ya zuio kwa niaba ya serikali”.

Pia aliongeza kuwa mwaka jana Vodacom ililipa kodi ya shilingi 47.1 bilioni/-kwa kodi ya mapato pia ilikusanya zaidi ya shilingi bilioni 262.8 za kodi ya Ongezeko la Thamani(VAT) ,kodi ya zuio na kodi nyinginezo zinazolipa serikalini. “Tunatimiza taratibu za kulipa kodi kulingana na sheria za serikali na kuendelea kutimiza matakwa ya serikali.Ushindi huu tulioupata kwa mara ya pili ni uthibitisho wa kutosha”.Alisema.

Kuhusiana na uwekezaji mtendaji huyo Mkuu wa Vodacom anasema kampuni hadi kufikia sasa Vodacom imewekeza nchini zaidi ya shilingi trioni 1.7/- na bado ina dhamira ya kuendelea kuwekeza na kukuza sekta ya mawasiliano nchini.

TAWNET ni asasi isiyokuwa ya Kiserikali inayojitegemea ambayo inaundwa na waandishi wa habari wenye mapenzi ya kuandika habari za kodi ikilenga kuwajengea uwezo waandishi wa habari ili kubobea katika uandishi wa masuala ya kodi.

Tangazo la mdahalo wa Katiba Mpya Novemba 25, 2014


Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF), imeandaa mdahalo maalumu wa Katiba utakaofanyika kesho kwenye Ukumbi wa Mlimani City ambao mzungumzaji mkuu atakuwa Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba.

Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Joseph Butiku alisema jana kwamba mdahalo huo wa amani ni kwa ajili ya Watanzania wenye mapenzi mema na utakuwa wa wazi, ikiwa ni sehemu ya kuziba pengo la mdahalo wa Katiba uliovunjika Novemba 2 ambao ulifanyika kwenye Hoteli ya Blue Pearl.

Ulivunjika baada ya kutokea vurugu zinazodaiwa kuanzishwa na kikundi cha watu kwa lengo la kuvuruga uwasilishwaji wa ujumbe wa Katiba, huku Katibu wa Uhamasishaji wa UVCCM, Paul Makonda akitajwa kinara wa vurugu hizo.

Siku moja baada ya vurugu hizo, Makonda alitumia muda mwingi kujisafisha kuwa alichokifanya ni kumkinga Jaji Warioba asidhurike.

“Tunasema ni mdahalo wa amani na utakuwa wa wazi kwa watu wote wenye mapenzi mema. Tuna mambo mengi ya kujadili, pia tunazungumza kuhusu maadili… Tunaona namna watu wanavyojichukulia fedha za watu bila woga, mdahalo huu unatupa fursa za kujadili kuhusu umuhimu wa Katiba kulinda maadili ya viongozi na vifungu vingine muhimu,” alisema Butiku.

Aliongeza kuwa hiyo ni sehemu tu ya ushiriki wa mijadala na midahalo ya umma kuhusu Katiba Inayopendekezwa, ambayo kwa sasa inaendelea katika maeneo yote ya nchi, ikifanywa na viongozi wa kisiasa, mashirika ya kujamii na hata watu binafsi katika vyombo mbalimbali vya habari.

Alisema japokuwa sasa hivi wamepata ukumbi mdogo unaoweza kuingiza watu 350, watatoa fursa kwa watu kuuliza maswali na kupata majibu kuhusu vifungu na vipengele mbalimbali vyenye utata vinavyoyahusu makundi yote ya kijamii ambayo yamepata uwakilishi katika mapendekezo hayo ya Katiba.

Aliwataja wengine watakaoshiriki kutoa mada kwenye mdahalo huo kuwa ni waliokuwa makamishna wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Butiku mwenyewe, Mohamed Mshamba, Maria Kasonda, Profesa Mwesiga Baregu, Profesa Palamagamba Kabudi na Humphrey Polepole.

Alisema midahalo hiyo ya ndani ni sehemu tu ya mwendelezo wa mijadala inayoendeshwa na taasisi hiyo iliyoanzishwa mwaka 1997 na kuzinduliwa na Rais wa Awamu ya tatu, Benjamin Mkapa mjini Mwanza.

“Hawa vijana waliovuruga mkutano wetu wa awali pale Ubungo Plaza, ambao ni vijana wetu na tunawafahamu, hatutarajii kwamba watarudia tena vitendo vya kihuni kama vile. Kimsingi hawana sababu kwa kuwa hawakunyimwa fursa ya kujadili na kutoa mawazo yao, tulishawaonya,” alisema.

Taarifa via gazeti la MWANANCHI