SADC Essay Writing Competition for Secondary Schools 2015

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

MINISTRY OF EDUCATION AND VOCATIONAL TRAINING

SADC ESSAY WRITING COMPETITION FOR SECONDARY SCHOOLS, 2015

The Southern African Development Community (SADC) Secretariat has organized the SADC students essay writing competition for year 2015. The Essay writing competition is intended to broaden knowledge of the secondary school going population on SADC activities. The competition is open to form 1 to form 6 students. The students are required to begin researching on the topic prior writing and submitting to their Heads of School.

The 34th summit of Heads of State and Governments deliberated that, the topic for year 2015 be “Leveraging the Region`s Diverse Resources for sustainable Economic and Social Development through Beneficiation and Value Addition” Discuss how this would result in Sustainable Economic Development.

The set of questions below are meant to guide students when responding to the question above. Thus, on answering the above question , student should answer all the questions listed below:
 1. Discuss the abundant natural resources versus economic development in the SADC Region as a whole expounding the issues of ownership, monetary values and benefits accrued from them on annual basis over the past five years?
 2. Has the SADC Region ultimately benefited from its abundance of natural resources since the complete democratization with the fall of the Apartheid regime in South Africa in 1994?
 3. Discuss Beneficiation and Value Addition with concrete proposals for SADC Region on ownership and processing of mineral/natural resources and how they benefited SADC Citizens if at all and what can be improved to maximize benefits to the SADC citizenry?
 4. How should the SADC Region go about implementing the 34th Summit Theme in order for it to benefit the whole region including some of its Member States that might not have as much natural resources as the others? 
 5. What role should be played in the operationalisation of the 34th Summit Theme by the non-state actors in the SADC Region, thus, private sector, Nongovernmental Organizations, traditional authorities and local communities?
 6. As a secondary school learner, what do you think should be the education sector`s role in the operationalisation of the 34th Summit Theme to benefit the education sector in the whole region?

Heads of schools are supposed to ensure that the students adhere to the following guidelines:
 • The essay should not be longer than 2000 words and not shorter than 1000 words.
 • Where students have access to computers, they are advised to type their essays and submit both the soft and hard copies.
 • Students who will type their essays will have to sign and initial the hard copies to make sure that they have not been altered.
 • The essay shall be written in English language.
 • The front page or cover page will display the name, sex, class, school address and stamp, Headmistress/Headmaster’s email address, signature and phone no, region, country.
 • The title of the essay should be written in the cover page (students should not paraphrase the title)
 • The handwritten essays will be written on one side of the A4 paper with double margin of two centimeters.
Students are expected to begin writing immediately and submit their essays to their head of school. The Head of School will then be expected to constitute a marking panel which will choose best essays of the school. The panel should go through the essays (Please do not mark the essays) and choose three essays to be submitted to The Permanent Secretary Ministry of Education and Vocational Training not later than 15th April 2015. The national adjudication will take place from 02nd to 11th May 2015 in order to get three entries which will be submitted to the SADC Secretariat in Botswana.

The same Information can be found on the website www.SADC.int, www.foreign.go.tz and www.pmolarg.go.tz

Wishing you and your schools best wishes.

PERMANENT SECRETARY

Faida ya kashfa ya akaunti ya BoT Tegeta Escrow kwa Mzanzibari

Waswahili tuna msemo kuwa “kila jambo lina kheri yake“, tukiamini kuwa hata kutoka kwenye matumbo ya shari, huweza pia kukazaliwa kheri. Ndivyo tulivyo, tumeumbwa kuwa watu wa kuyapa maana machungu na majaaliwa yanayotukumba maishani.

Nami najaribu kuyapa maana machungu yaliyomo kwenye kashfa ya Tegeta Escrow Account, ambayo – kwa sababu ya mfumo – sisi Wazanzibari hatujioni kuguswa nayo. “Baada ya yote, hizo si ni pesa za TANESCO, ambalo ni shirika la umeme la Bara. Linatuhusu nini sisi tunaoelea kwenye visiwa vya Bahari ya Hindi?“ Ndivyo wenzangu wengi wanavyodhani.

Lakini hili linatuhusu, kwa pande na rangi zake zote. Kwanza, na kubwa kuliko yote, ni kwamba bado tunabakia kuwa Watanzania – kwa sheria na kwa kodi tunayolipa. Hata kama tupo ambao utiifu wetu kwa huo Utanzania ni mdogo sana na tunajinasibisha zaidi na utiifu kwa Uzanzibari, ambao hauna jeshi, mizinga wala jela.

Pili, ingawa sijui ni wangapi miongoni mwa wanaoshukiwa kujipatia manoti hayo ya TANESCO ni Wazanzibari, lakini nafahamu kuwa Waziri wa Fedha Saada Salum Mkuya ni Mzanzibari na sasa anatakiwa awajibike kwa kuzembea kwake kusimamia fedha za wananchi. Namuhurumia Da Saada, mwalimu mwenzangu wa muda wa ziada pale kwenye kituo cha Ruec Center, Mlandege.

La tatu, na ndilo ninalokusudia hasa, ni kuwa juu ya uwazi wa kashfa hii ambao hautugusi Wazanzibari, kuna uficho wake ambao unatuhusu sana – ambao unahusiana na siasa za Muungano kuelekea Zanzibar.

Unakumbuka kuwa Alhamisi iliyopita ya tarehe 20 Novemba, wabunge kadhaa kutoka upinzani na kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM) walisimama bungeni Alhamisi iliyopita (20 Novemba) kuhoji kile walichosema ni barua ya mahakama kuzuia mjadala wa ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG).

Moja ya hoja iliyorejewa takribani na wote, akiwamo Naibu Spika Job Ndugai, ni kwamba kumekuwa na tabia ya mahakama kutumika kwa maslahi ya kifisadi nchini Tanzania. Kwamba vita dhidi ya ufisadi vimekuwa vigumu kwa kuwa chombo kinachopaswa kusimamia utekelezwaji wa sheria zinazopitishwa na bunge, nacho kimevamiwa na mafisadi. Kwa hakika, katika orodha ya waliopokea fedha za akaunti hiyo ya Tegeta Escrow ni pamoja na majaji wa ngazi za juu.

Kama nilivyosema, suala zima la kashfa hii ni shari lakini ndani yake inaweza ikazalika kheri, hasa kwetu Wazanzibari. Kwa nini? Kwa kuwa hili linatupa hoja ya kuhoji uadilifu wa mahakama za Tanzania Bara, ambako hivi sasa Wazanzibari wenzetu wamekuwa wakipelekwa kushitakiwa kwa makosa ya ugaidi.

Ni sisi wenyewe raia wa kulisemea na kulifanyia kazi hili, na tusitegemee serikali, maana kiongozi wake mkuu, Rais Ali Mohamed Shein, ameshasema wazi kwake hilo ni sawa tu. Sisi kwetu si sawa. Halikuwa sawa tangu awali. Awali tulilipinga kwa kuhoji uhalali wa kisheria wa kuwachukuwa Wazanzibari wanaotuhumiwa kufanya makosa ndani ya ardhi ya Zanzibar yenye mamlaka yake tafauti kisheria na kuwapeleka na kuwafungulia mashitaka Bara kwenye mamlaka nyengine ya kisheria.

Sasa tuna hoja ya ziada. Hii inahusu kuhojika kwa uaminifu na uadilifu wa mahakama hizo, ambazo tayari Bunge limeambiwa kuwa ni vichaka vya mafisadi. Hoja yetu ni kuwa kamwe mahakama hizi haziwezi kuaminika kuendesha kesi inayowahusu washukiwa ambao tangu hapo kesi yao ni ya kisiasa zaidi kuliko ya kisheria. Mahakama ambazo kesi zake huendeshwa kwanza kwenye vikao vya baa, vyumba vya hoteli au ofisi za mabwana walio nje na juu ya sheria, hazina uhalali wa kusikiliza mashitaka haya.

Ndio maana kwa msingi huo wa uadilifu, sasa sisi Wazanzibari tunaoamini kuwa kesi dhidi ya Wazanzibari wenzetu waliopelekwa Bara ni ya kisiasa, tuna wajibu wa kuanzisha kampeni ya BringBackOurPeople.

Hiyo ni kheri moja miongoni mwa yatokanayo na shari za kashfa ya Tegeta Escrow Account kwa Zanzibar.

Iko kheri nyengine pia. Hivi umewahi kulisikia jina la Dokta Thomas Kashililah? Huyu ni Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Katika mkasa huu wa Escrow, ripoti za magazeti zinasema kwamba kumbe ndiye huyu aliyeiandikia Mahakama Kuu kuiomba kile alichokiita “orodha ya kesi za Escrow zilizoko mahakamani ndani na nje ya nchi.“ Wachambuzi wanasema kuwa barua hiyo ilikusudiwa kupata idhini ya Mahakama Kuu kuzuia mjadala wa ripoti ya CAG juu ya kashfa hiyo usifanyike bungeni.

Ni kuwepo kwa barua hiyo ndiko kulikotaka kutumiwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuuzuia mjadala huo. Yaliyobakia ni hadithi moja ya aibu sana kwa Mwana wa Mkulima Pinda, kwani hajawahi “kukosewa adabu“ na wabunge hata wa chama chake, kama siku aliyoonesha muelekea huo bungeni!

Lakini yalianza na Dk. Kashililah, yumkini kwa kimbelembele chake au kwa kufuata maagizo ya nguvu zisizoonekana nyuma yake.

Sasa Mzanzibari mwenzangu nikurudishe nyuma kidogo kwenye ‘ilivyopatikana‘ thuluthi mbili ya kura za Zanzibar kupitisha Katiba Iliyopendekezwa kwenye Bunge Maalum la Katiba, wakati huyu huyu Dk. Kashililah akiwa ndiye Katibu Mwenza wa Bunge hilo akishirikiana na Yahya Hamad wa Baraza la Wawakilishi.

Mimi na wewe tunajuwa kuwa bunge hilo lililoongozwa na Samuel Sitta halikuweza kupata thuluthi mbili kutokea Zanzibar kupitisha Katiba Iliyopendekezwa na iliyoandikwa chini ya uwenyekiti wa Andrew Chenge, ambaye mwenyewe anatuhumiwa kupokea shilingi bilioni 1.6 kwenye kashfa ya Akaunti ya Tegeta Escrow.

Uliofanyika ulikuwa ni udanganyifu. Udanganyifu, kwa mfano, wa kuigeuza kura ya Zakia Meghji kuwa ya Zanzibar, ilhali mwenyewe hakutokea Zanzibar (kwa nafasi yake ya ubunge wala kisiasa). Udanganyifu, kwa mfano, wa kuipiga kura ya Ambar Khamis kuwa ya ndiyo, ilhali mwenyewe hata hakupiga kura. Udanganyifu, kwa mfano, wa kura hewa za mahujaji waliokuwa Makka, ambao ushahidi wa ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, unasema wazi kwamba hawakuweza kupiga kura. Udanganyifu, kwa mfano, wa Mohamedraza Dharamsi na Mohamed Turki, ambao kura zao hazikupigwa lakini zilihisabiwa kupigwa na zikaitwa ni za NDIO.

Hili unapoliunganisha na jitihada za kuzuia mjadala bungeni juu ya kashfa ya Akaunti ya Tegeta Escrow, hapana shaka, linakupa jawabu inayohoji uadilifu wa watendaji wa bunge, akiwamo Dk. Kashililah.

Na hili nalo linatupa hoja na haja ya kuanzisha kampeni nyengine kama Wazanzibari – BringBackOurKatiba!

Halle Berry amburuta mahakamani mwenza kwa kumfanya binti awe 'mweupe'

(picha: lovebscott.com)

Halle Berry amempeleka aliyekuwa mpenzi wake Gabriel Aubry mahakamani kwa madai ya kutaka kubadilisha muonekano wa binti yao ili awe 'mweupe'.

Anadai Aubry amezinyoosha nywele za Nahla zilizojinyonganyonga na kuzipaka rangi kwa nia ya kumfanya asionekane Mmarekani mweusi.

Nyaraka za mahakamani zinamshutumu Aubry kwa kumsababishia “uharibifu wa kisaikolojia na wa mwili” kwa binti yao mwenye umri wa miaka sita na kumsababishia aanze kuwaza “kwa nini muonekano wake wa asili hautoshi ”.

“Nataka mimi na Gabriel tuchukue uamuzi pamoja juu ya binti yetu, ukuaji wake, maendeleo yake na maisha yake kwa ujumla,” alisema Berry kwenye nyaraka hizo.

Wakili wa Berry, Steve Kolodny, ndie aliyekuwepo mahakamani siku ya Jumatatu pamoja na Aubry.
Jaji alitoa uamuzi kuwa hakuna mzazi hata mmoja anayeweza kubadili muonekano wa Nahla kutoka asili yake.

Wapenzi hao waliachana mwaka 2010 baada ya kuwa pamoja kwa miaka minne.

Mdahalo wa Katiba pendekezwa (katika picha)Wananchi wakiwa katika foleni ya kuingia katika ukumbi wa mdahalo.


Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba akizungumza katika mdahalo ulioandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere kuhusu Katiba inayopendekezwa na kufanyika jijini Dar es Salaam.


Mwanaharakati wa mambo ya vijana Humphrey Polepole na aliyekuwa mjumbe wa Tume ya mabadiliko ya katiba akzungumza katika mdahalo huo.Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba akizungumza katika mdahalo ulioandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere kuhusu Katiba inayopendekezwa na kufanyika jijini Dar es Salaam.

Picha zote: Francis Dande

Kongamano la 31 la Kisayansi linaendelea Bagamoyo

Maximilian Mapunda kutoka shirika la Afya Duniani (WHO-Country Officer) akiwasilisha mada kwenye kongamano hilo.
Pichani ni baadhi ya picha za matukio ya siku ya pili, jana Novemba 25 kwenye kongamano la Kisayansi la 31, '31th Annual Scientific Conference and Annual General Meeting'.. lililoandaliwa na Tanzania Public Health Association (TPHA).

Mkutano huo unafanyika mjini hapa Bagamoyo katika Ukumbi wa Stella Maris, Bagamoyo, Pwani Tanzania.

Kongamano hilo la kisayansi la 31, limeanza Novemba 24 linatarajia kuwa la siku tano na kutarajia kumalizika Novemba 28 ambapo wataalamu wa afya na wadau watajadilina mambo mbalimbali ya afya hapa nchini.Katibu Mtendaji wa TPHA Taifa, Dk. Oberlin Kisanga akiwasilisha mada maalum kwenye kongamano hilo.Dk. Ali Mzige mshiriki wa Kongamano la Kisayansi la 31, akiwasilisha mada maalum.Mwenyekiti wa TPHA Taifa, Dk.Elihuruma Nangawe akitoa ufafanuzi kwenye mada zinazotolewa na wajumbe kwenye kongamano hilo.Wajumbe wa kongamano hilo wakichangia mada.Katibu Mtendaji wa TPHA Taifa, Dk. Oberlin Kisanga (kushoto) akifuatilia kwa makini kongamano hlo.

---
Picha habari kutoka kwa Andrew Chale, Bagamoyo (wavuti.com tumeshirikishwa na MoDewji blog)

Kanuni za Bunge zasemaje Spika kuendesha mjadala ikiwa ni mtuhumiwa?

Kama ni kweli Spika naye katajwa kwenye orodha ya/za ugawanaji wa fedha za Escrow, kanuni za kudumu za Bunge zinasemaje kuhusu mgongano wa maslahi kwenye kuendesha mjadala wa sakata hilo Jumatano?

Na kama (ikatokea kuwa) wasaidizi wake wote wa kuendesha mjadala huo (i.e. Naibu Spika, Mwenyekiti et al.) nao wametajwa katika orodha hiyo/hizo, inakuwaje tarehe 26 Novemba 2014?

Je, Bunge inabidi lipige kura kutafuta Mbunge au mtu mwingine asiye na mgongano wa maslahi (i.e. ambaye hajatajwa kwenye ripoti za CAG, PCCB na PAC) na muadilifu kuendesha mjadala huo kesho?

---

Mkosamali kortini kwa 'vurugu' kituo cha kujiandikisha wapiga kura

Mbunge wa jimbo la Muhambwe wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma Felix Mkosamali amepandishwa kizimbani katika mahakama ya wilaya hiyo akikabiliwa na shitaka la kumzuia karani kuendelea kufanya kazi yake kuandikisha wapiga kura wa uchaguzi wa serikali za mitaa.
 
Mbele ya Hakimu Mkazi wa wilaya hiyo, Erick Marley Mwendesha mashitaka wa polisi Peter Makala alisema kuwa Mkosamali alitenda kosa hilo mwanzoni mwa wiki hii katika kitongoji cha Nduta Kijiji cha Kumhasha Kata ya Murungu wilayani Kibondo. 

Mwendesha mashitaka huyo aliieleza mahakama hiyo kwamba wakati karani huyo, Hamidu Kabibiliakiendelea na shughuli zake Mkosamali alifika katika kituo hicho na kuzuia asiendelee kuwaandikisha wananchi jambo ambalo ni ukiukaji wa sheria ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa. 

Makala alisema kuwa kitendo hicho ni kuwanyima wananchi haki yao ya msingi ambao hata baada ya kuzuiwa, waliendelea kudai kujiandikisha lakini na mbunge huyo kushinikiza na kuzuia kabisa kutoendelea na kazi hiyo. 

Ilidaiwa kuwa Mbunge huyo alimnyang’nya karani huyo vitabu na madodoso yote na kuamua kuondoka nayo na kuyapeleka katika ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya kibondo kinyume cha taratibu na ndipo baadaye aliamatwa na Polisi kwa tuhuma za kufanya vurugu katika kituo cha kuandikisha wapiga kura.

via Lukwangule blog

Taarifa ya TFF ya wito wa Watanzania kupigia kura jezi ya Taifa StarsWatanzania wanatakiwa kupigia kura jezi ya timu ya Taifa ya nyumbani na ugenini kupitia mtandao wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wa www.tff.or.tz ambapo jezi hizo zimewekwa.

TFF ilipokea mapendekezo ya mwonekano mpya wa jezi ya timu ya Taifa kutoka kwa Watanzania 86. Jezi 11 za nyumbani, bukta nane za nyumbani, jezi nane za ugenini na bukta tano za ugenini ndizo zimepitishwa kwa ajili ya kupigiwa kura.

Mwisho wa kupiga kura ni Desemba 31 mwaka huu. Mpigaji kura anatakiwa kubonyeza kwenye jezi na bukta ambayo ameichagua. Anatakiwa kufanya hivyo kwa jezi ya nyumbani na jezi ya ugenini.

Tunawashukuru wote waliojitokeza kupendekeza mwonekano mpya wa jezi ya timu ya Taifa.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

Ziara ya Tume ya Mipango bandarini Mbamba Bay

Baadhi ya wajumbe wa timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakiingia kwenye gati la Bandari ya Mbaba Bay iliyopo wilayani Nyasa mkoani Ruvuma.

Timu wakaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Tume ya Mipango imetembelea Bandari ya kimkakati ya Mbaba Bay iliyopo wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na Bandari hiyo.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, kiongozi wa timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri alisema kwamba Bandari hiyo ni muhimu kwa uchumi wa nchi kwa kuzingatia eneo la kijiografia la bandari hiyo.

“Bandari hii ni muhimu kwani kijiografia inaweza kuzifikia nchini nyingi zilizo kusini mwa nchi yetu hivyo inaweza kutumika kama lango la kibiashara miongoni mwa jirani zetu licha ya uhaba wa miundombinu yake,” alisema.

Aliwasihi wafanyakazi wanaoihudumia Bandari hiyo kufanya kazi kwa bidii bila ya kuchoka ili kuweza kuvutia wafanyabiashara na watumiaji wengine kuendelea kuitumia bandari hiyo.

Kwa upande wake, afisa bandari ya Mbaba Bay, Bw. Jarome Urio aliutaarifu ugeni huo kuwa Mamlaka ya Bandari ipo katika mkakati wa kuindeleza bandari hiyo ili kuweza kuihudumia wateja wengi zaidi.

Pia, Bw. Urio aliwashukuru wajumbe wa timu hiyo ya ukaguzi kwa kwenda kuitembelea na kujionea maendeleo ya bandari hiyo.

“Tunafarijika sana kuona viongozi wa serikali wanapokuja kututembelea kwani hali hii uongeza hamasa ya utendaji kazi wetu,” alisema.

Kwa mujibu wa Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2011/2012 – 2015/2016) bandari ni mojawapo ya vipaumbele vitano vya kimkakati vyenye lengo la kufungulia fursa za ukuaji uchumi wa nchi ili kuweka misingi wa uchumi kwa watu walio wengi.

Vipaumbele vingine ni Kilimo ambapo lengo kuu likiwa ni kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao ya kilimo ili kujitosheleza kwa chakula na kuwa na ziada ya kuuza nje ya nchi; Maendeleo ya viwanda: Msisitizo umewekwa katika kuvutia, kuanzishwa na kuendeleza viwanda vinavyotumia malighafi zinazopatikana nchini (kama vile viwanda vya nguo, mbolea, saruji, makaa ya mawe, chuma na bidhaa za chuma) na pia sekta ya madini kwa lengo la kuongeza mapato ya Serikali.

Pamoja na kipaumbele cha Maendeleo ya rasilimali watu na ujuzi: Mpango unahimiza kuwekeza katika elimu (hasa katika elimu ya juu na vyuo vya ufundi) na huduma za afya (kuongeza ubora na upatikanaji wa huduma) katika kujenga nguvu kazi itakayotuletea maendeleo ya kiuchumi na kijamii; na Utalii, Biashara, na huduma za Fedha ambapo jitihada zimewekwa kwenye uendelezaji uwezo wa kuuza katika masoko ya ndani na nje, kuongeza idadi ya watalii na matumizi yao wawapo nchini, na kuongeza upatikanaji wa huduma za kifedha.


Mratibu wa shughuli za ukaguzi wa miradi ya maendeleo, Bw. Senya Tuni (Wapili kulia) akieleza jambo mara walipoingia kwenye eneo la gati la Bandari ya Mbaba Bay. Wanaomsikiliza ni Mkuu wa msafara huo, Bibi Florence Mwanri (Kulia), Afisa mazingira wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bw. Julius Edward (Watatu kulia). Na kushoto ni Bw. Jordan Matonya ambae ni Mchumi kutoka Tume ya Mipango.


Afisa bandari ya Mbaba Bay, Bw. Jarome Urio (Wapili kushoto) akitoa maelezo kwa wakaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango walipofanya ziara kwenye bandari hiyo. Timu hiyo iliongozwa na Bibi Florence Mwanri (kushoto).Habari hii imewasilishwa wavuti.com na Saidi Mkabakuli, Mbaba Bay

Taarifa ya VIP Engineering and Marketing Ltd: Umiliki wa fedha za escrow hauna utata, tatizo ni Mawakili

Kinachoitwa kwamba ni kashfa ya akaunti ya Escrow ni ngoma ambayo wanaoichezesha wanafanya hivyo kwa matumaini kwamba wakiivutia kwao basi hatimaye watafaidika ipasavyo. Miongoni mwa wanaoishangilia ngoma hii ni baadhi ya mawakili waliokuwa wakiitetea Tanesco na Benki ya Standard Chartered.

Benki ya Standard Chartered inataka kuhakikisha kwamba kunakuwapo na sintofahamu kuhusu akaunti hiyo ya Escrow na kulazimisha imilikiwe ama na Serikali ya Tanzania au Tanesco kwa sababu hiyo inaweza kuisaidia katika lengo lake kuu la kupata fedha isizostahili. Ni wazi kwamba fedha zilizohifadhiwa katika akaunti hiyo ya Escrow si za Serikali wala si za Tanesco kama ambavyo Standard Chartered na wapambe wao wanavyolazimisha iwe. Fedha hizo ni za IPTL.

Migogoro kati ya TANESCO na IPTL ilianza mwaka 1998 baada ya IPTL kukamilisha kwa kiasi kikubwa ujenzi wa mtambo wa 100MW Tegeta Mjini Dar es Salaam. IPTL walitaka Tanesco inunue umeme kwa bei kubwa kuliko ilivyo kuwa halali lakini Tanesco walikataa kwa madai kwamba gharama zilizoainishwa na IPTL zilikuwa kubwa mno kuliko gharama halisi za uwekezaji.

Tanesco katika jitihada za kujinasua iliajiri kampuni ya uwakili ya Mkono & Co. Advocates ili kutoa huduma za kisheria kwa kushirikiana na Huntons & Williams ya Marekani.

Kutokana na tofauti za mitazamo ya gharama za uwekezaji, mawakili hawa waliishauri Tanesco ifungue kesi katika Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji {ICSID} nchini Uingereza dhidi ya IPTL ili kupinga gharama hizo.

Katika uamuzi wa Julai 2001 uliotolewa na ICSID kwenye kesi iliyofunguliwa na Tanesco dhidi ya IPTL mwaka 1998, mahakama hiyo ilitoa uamuzi kwamba, gharama za uwekezaji zishuke kutoka dola za Marekani milioni 163.53 hadi milioni 121.83.

Uamuzi huo wa mwaka 2001 uliridhia mfumo wa kifedha {financial model} iliyokuwa imekubalika katika kukokotoa viwango {tariff calculation} kati ya Tanesco na IPTL ambayo inaipa IPTL marejesho ya uwekezaji {internal rate of return - IRR} ya asilimia 22.31 badala ya asilimia 23.1 iliyodaiwa na IPTL. Mawakili wa Tanesco Mkono & Co Advocates walishauri kwamba Tanesco itekeleze mfumo huo.

Mwaka 2004, mawakili hao hao wa Tanesco wakiongozwa na Mkono & Co. Advocates waliishauri Tanesco isitekeleze ulipaji wa tozo ya uwezo wa kuzalisha umeme {Capacity Charges} kwa kutumia mfumo wa kifedha uliokubalika mwaka 2001. Kutokana na ushauri huo, Tanesco kwa kuamini ushauri wa mawakili wao mwaka 2006 kwa kupinga thamani ya invoices zilizowasilishwa na IPTL kwa kutumia mfumo wa fedha {financial model} iliyotolewa na ICSID. Kitendo hicho kiliifanya IPTL kuupinga uamuzi huo wa Tanesco wa kutofuata ulipaji wa tariff kwa kutumia mfumo wa fedha wa mwaka 2001.

Baada ya Tanesco kupokea ushauri wa Mkono & Advocates iliutilia mashaka na hivyo kuamua kuomba ushauri kwa kampuni ya Huntons & Williams iliyokuwa ikiishauri Serikali katika mashauri ya nje ya nchi.

Kampuni ya Huntons & Williams ilisisitiza kuwa unaosemekana kuwa ni ugunduzi uliofanywa na kampuni ya Mkono & Co. Advocates ulikosa hoja ya msingi yakuifanya Tanesco ipinge kulipa tozo ya uzalishaji umeme {capacity charge} kama ilivyokubalika mwaka 2001.

Ni wazi kwamba ushauri wa kampuni ya Mkono & Advocates ulikuwa ni wa kuipotosha Serikali na Tanesco kwa manufaa binafsi na kwa mantiki hiyo basi kampuni ya Mkono & Co Advocates ilikusudia kesi kati ya Tanesco na IPTL iendelee ili waendelee kulipwa gharama za kuendelea na kesi.

Ushahidi wa upotoshaji ni mwaka 2012 Mkono & Co. Advocates kuitaka Tanesco kukubali usuluhishi nje ya mahakama katika shauri la Tanesco kukataa kuilipa IPTL capacity charges kwa kigezo kwamba uwezekano wa Tanesco kushinda katika kesi ya kupinga kiwango cha tozo ulikuwa mdogo na unaashiria kuendela kuuiingiza Tanesco kwenye hasara kubwa na kesi zisizokuwa na ukomo.

Aidha, moja ya kesi ambazo zinathibitisha kuwapo kwa mgongano wa kimaslahi wa mawakili ni shauri kati ya Tanesco na Benki ya Standard Chartered ya Hong Kong {SCB-HK} lililoko ICSID.

Shauri hilo linawakilishwa na mawakili wenye asili na historia ya pamoja na kampuni ya Mkono & Co. Advocates. Mkono & Co. Advocates anaiwakilisha Tanesco na kwa upande mwingine Bw. Charles Morison mwenye mahusiano makubwa na kampuni ya Mkono & Advocates kwa kuwa alikwa mwanasheria wake ndiye anaiwakilisha SCB-HK.

Mahusiano haya ya kikazi kati ya mawakili hawa yanaashiria mgongano mkubwa wa kimaslahi na kuifanya Serikali na Tanesco wasinufaike na huduma yao kwa kuwa huduma za mawakili hao zilikuwa zimegubikwa na maslahi binafsi na kuwatwisha Watanzania mzigo mkubwa.

Ukiachilia mbali kizungumkuti hicho cha mgongano wa maslahi tangu kampuni ya Mkono & Co. Advocates kwa pamoja na Huntons & Williams wapewe kazi hiyo ya uwakili na Tanesco mwaka 1998, jumla ya shilingi bilioni 62.9 zimelipwa kwa kampuni ya Mkono & Advocates.

Kadhalika kampuni hizo bado zinaidai Serikali ya Tanzania jumla ya dola za Marekani milioni 4.5.

Ni wazi kwamba gharama zingeweza kuongezeka endapo Serikali na Tanesco wangeendelea kuwatumia mawakili hao kwa kuwa mawakili hao wamekuwa wakishinikiza kujiingiza katika kesi kwa kuipa Serikali na Tanesco matumaini ya kupata ushindi jambo ambalo matokeo yake ni Serikali na Tanesco kuendelea katika kesi zisizoisha kwa hasara kubwa lakini kwa manufaa ya mawakili ambao wamegeuza hizo kesi kuwa miradi yao ya kudumu.

Aidha, kwa mujibu wa Sheria ya Kampuni za Tanzania, ni dhahiri SCB-HK haikusajili hati inayoitwa Deed of Assignment au dhamana nyingine hapa nchini ambazo zingelihalalisha madai ya madeni na dhamana inayodaiwa kuipa benki hiyo uhalali wa kutambulika kisheria kama mdai wa IPTL.

Baadhi ya mambo yanayoonesha ni jinsi gani mawakili waliipotosha Tanesco ni kwamba SCBHK ilifungua shauri kwenye Mahakama ya Usuluhishi (ICSID ARB/10/20) kimakosa na TANESCO ilipewa ushauri usio sahihi na wanasheria wake kuhusu kesi hiyo.

Jambo linaloshangaza ni kwa vipi mawakili wa TANESCO waliamua kutofuatilia masuala muhimu ambayo yalistahili yafuatiliwe na kujengewa hoja za kisheria. Kwa mfano hoja za kisheria kwamba baadhi ya mashauri mengine hayawezi kusikilizwa nje ya Mahakama za Tanzania lakini mawakili wa TANESCO na Kampuni ya Mkono & Co. Advocates haikutetea hoja hiyo.

Kampuni ya Mkono & Co. Advocates ambayo ilikuwa ni Mawakili wa TANESCO hawakuipasha ICSID kwamba mgororo kati ya TANESCO na IPTL ulimalizika Oktoba 2013. Pia inaelekea kwamba mawakili wa TANESCO walitaka mgogoro uendelee badala ya kufikia mwisho, kwani kila mara walikuwa hawatekelezi kama mteja wao alivyokuwa anataka mambo yawe.

Mawakili ni waajiriwa waaminifu wa mteja na maafisa wa mahakama. Taaluma yao, licha ya kuwa na umaalumu wake, matakwa ya kutoa ushauri ili mteja awe katika hali ya kujua kila kinachoendelea na pia kama hapana budi kupunguza gharama kama ushauri usingelikuwepo.

Hata hivyo, mawakili wanaofanya kazi wanatakiwa kuwa na uadilifu wa hali ya juu sifa ambazo inaelekea mawakili wa TANESCO wameshindwa kuthibitisha kuwa nazo katika kutimizia wajibu wao kitaaluma. Haya yatajionesha wazi wazi katika kufanya mapitio kwenye maeneo mbalimbali yanayohusu uhusiano wa kibiashara na kiutendaji kati ya TANESCO na IPTL kwa ushauri wa mawakili.

Aidha, katika muendelezo huo huo wa kuivuruga Tanesco Standard Chartered Bank imeiomba ICSID katika shauri ICSID ARB/10/20 kuiamuru TANESCO kuilipa SCB-HK USD 208.3 milioni pamoja na riba ya LIBOR + 4% katika kesi nyingine ya Novemba 14, 2014 deni ambalo uhalali wake unabishaniwa siyo tu na Tanesco bali pia na kampuni ya VIP.

Suala la umiliki wa fedha za escrow halina utata
Kumekuwapo na mchezo mchafu wa kisiasa wa kujaribu kupotosha ukweli kuhusu umiliki wa fedha zilizokuwapo katika akaunti ya escrow iliyojulikana kama Tegeta Escrow.

Ili kuelewa kwamba fedha katika akaunti hiyo zilikuwa zitaendelea kuwa ni za IPTL na kamwe hazijawahi kuwa za Tanesco wala Serikali ni muhimu kutambua ukweli tu kwamba mlipaji wa deni hawezi kuwa mmiliki wa deni analolilipa.

Akaunti ya Escrow ilifunguliwa kutokana na ushauri wa Mkono & Co. Advocates wa mwaka 2004 ambao walitoa hoja kuwa gharama za kununua umeme zilizokokotolewa kwa kutumia asilimia 22.31 ya urejeshwaji wa uwekezaji {IRR} zilikuwa hazikubaliki na hivyo Tanesco walikuwa wakitoa hati ya kupinga malipo kwa kila ankara ya malipo kupinga gharama hiyo kulingana na kifungu Na.6.8 cha mkataba wa ununuzi wa umeme {PPA}. Kifungu hicho kinaeleza kuwa ikiwa upande wowote haukubaliani na usahihi wa malipo katika ankara zilizowasilishwa kwa ajili ya malipo ya gharama za umeme wanatakiwa watoe notisi {Invoice Dispute Notice} kwa upande mwingine.

Vile vile, mawakili wa Tanesco Mkono & Co. Advocates waliishauri kwamba kutokana na pingamizi hilo, ifunguliwe akaunti maalum {Escrow Account} kwa ajili ya kuhifadhi fedha ambazo zilitokana na ankara zilizokuwa zinapingwa.

Ushauri huo ulitekelezwa na Tanesco na mnamo Julai 5, 2006 Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilisaini mkataba wa kufungua akaunti maalum kwa ajili ya kuweka fedha zote za ankara zilizopaswa kulipwa kwa IPTL.

Kwa mantiki hiyo Akaunti ya Escrow ilifunguliwa kwa ajili ya kuhifadhi fedha za malipo ya IPTL yaliyokuwa yakisubiri kuthibitishwa na Tanesco kwa pamoja na IPTL kwa pamoja kama ilivyoainishwa katika kifungu cha 6.8 cha mkataba wa ununuzi wa umeme yaani PPA.

Kwa mantiki hiyo basi ni vema ikafahamika na kueleweka kuwa fedha hizo zilikuwa za IPTL na wala siyo fedha za Serikali wala si za Tanesco.

Ni wazi pia kutambua kwamba wahusika walikuwa na uhuru wa kuweka fedha hizo katika akaunti nyingine yoyote kutegemea na makubaliano yao yaani ya IPTL na Tanesco.

Hivyo basi kitendo cha fedha hizo kuhifadhiwa katika akaunti iliyofunguliwa na kuhifadhiwa katika Benki Kuu haina maana kuwa fedha hizo zilikuwa za Serikali.

Kwa mujibu wa kifungu namba 7.7 cha mkataba wa Akaunti hiyo ya Escrow fedha zilizomo kwenye akaunti hiyo zingeendelea kuhifadhiwa na Wakala wa Escrow {Escrow Agent}, hadi muafaka utakapofikiwa kati ya Tanesco na IPTL kuhusiana na mabishano ya ankara.

Kwa mujibu wa mkataba wa escrow, Benki Kuu ndiyo iliyopewa jukumu la kusimamia na kuendesha akaunti ya Escrow hadi hapo Tanesco na IPTL watakapofikia muafaka na akaunti kufungwa.

Baada ya uamuzi wa Mahakama Kuu ya Tanzania uliotolewa na Jaji Utamwa wa kuiondoa IPTL kwenye ufilisi na kuitambua PAP kama mmiliki wa asilimia 100 wa IPTL, Tanesco ilifanya mazungumzo na IPTL na kukubaliana na kiasi ambacho Tanesco ilikuwa inadaiwa na IPTL.

Baada ya makubaliano kati ya Tanesco na IPTL serikali ilisaini makubaliano na IPTL kuruhusu fedha za akaunti ya Escrow zilipwe kwa IPTL na Benki Kuu ikaagizwa kuzilipa fedha hizo na hatimaye kuifunga akaunti hiyo.

Oktoba 21, 2013 Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini na IPTL walisaini makubaliano ya kutoa fedha zilizomo katika akaunti ya Escrow ili zilipwe kwa IPTL. Makubaliano hayo yaliyojulikana kama Agreement for Delivery of Funds to Independent Power Tanzania Limited yaliambatana na muhtasari wa kikao cha pamoja cha uhakiki wa malipo ya tozo kati ya IPTL na Tanesco pamoja na barua ya Wizara ya Nishati na Madini ikiwasilisha makubaliano hayo na kuiomba Benki Kuu iruhusu malipo hayo kwenda IPTL kama uhakiki ulivyobainisha, na kwa vile matakwa ya kifungu 7.7 cha mkataba wa Akaunti ya Escrow unavyosema yalikuwa yametekelezwa kikamilifu.

Kufuatia maombi ya Benki Kuu kwenda Wizara ya Fedha ya kufunga akaunti ya Escrow kutokana na kumalizika kwa mgogoro kuhusu mali ya uwekezaji na kwa kuzingatia uamuzi wa Mahakama Kuu, mwezi Desemba 2013 akaunti hiyo ya Escrow ilifungwa rasmi.

Wakati wa kufunga akaunti hiyo ya Escrow, Tanesco ilikuwa ikidaiwa na IPTL jumla ya dola za Marekani milioni 79.05 sawa na shilingi za Tanzania bilioni 125.04 zilizotokana na tozo ya uzalishaji {capacity charges} ambazo hazijalipwa. Kimsingi fedha zilizokuwa katika akaunti ya Escrow wakati wa kuilipa IPTL na kufunga akaunti hiyo zilikuwa kidogo kuliko madai ya IPTL.

Ikumbukwe kwamba kuanzia Septemba 2009 Tanesco iliacha kulipa fedha za tozo ya uzalishaji umeme {capacity charges} kwenye akaunti ya Escrow kwa sababu ya ukata wa TANESCO/ Serikali.

VIP ina Tax Credit kubwa na TRA

Kampuni ya VIP ilipouza hisa zake asilimia 30 kwa PAP mwaka 2013 ilideposit tax credit ya jumla ya TZS 38,186,584,322.-ambazo ni asilimia 30 (30%) ya gharama za mauzo kiasi ambacho ni kikubwa kuliko matakwa ya Sheria ya Capital Gains Tax inayotamka kuwa kiwango kinachotakiwa ni asilimia 10 (10%) kwa sababu VIP iliomba suala la kodi lijadiliwe baadaye ikiwa na washauri wa maswala ya kodi.

Tozo ya uwekezaji wa IPTL ni ya chini

Ukweli usiopingika ni kwamba tozo ya uwekezaji ya IPTL ni senti za Marekani 1.06/kWh ikilinganishwa na za Songas ambazo ni senti za Marekani 4.31/kWh, Symbion senti za Marekani 4.99kWh na Aggreko inayotoza senti za Marekani 5.77/kWh.

VIP inasimamia Maslahi ya Taifa

Wakati wote VIP imetetea maslahi ya Taifa katika IPTL na itaendelea kufanya hivyo hata baada ya kuuza hisa zake kwa PAP. Ikumbukwe kwamba VIP iliiomba Mahakama kuweka masharti katika hukumu ya kesi yake ya kutaka kumaliza mgogoro wa IPTL. Masharti ambayo VIP iliyaomba na Mahakama kuyaridhia ni kutaka wamiliki wapya wa IPTL kampuni ya PAP: Kuongeza uwezo wa uzalishaji wa IPTL mpaka MW 500, kupunguza bei ya umeme wa IPTL kuwa kati ya senti za Marekani 6/kWh na senti za Marekani 8/kWh, PAP kulipa madeni yote halali ya IPTL na kubadilisha matumizi ya mafuta mazito kuendesha mitambo na badala yake itumike gesi asilia.

Imetolewa na VIP Engineering and Marketing Limited

Jifunze kutumia "Kamera ya Simu" kupiga picha nzuriJifunze mengi kuhusu matumizi mazuri na jinsi ya kupiga picha nzuri kwa kutumia "kamera ya simu" kupitia blogu mpya ambayo jina lake ni "KAMERA YA SIMU" inayopatikana kwa anwani ya kamerayasimu.blogspot.com


TimesFM Sunrise 'waifagilia' Vodacom kwa kuwa mlipakodi wa pili mkubwa

Hali halisi ilivyo kwa Wanafunzi wa Chuo cha Elimu cha Bustani

Go Pinda! Nenda tu mzee wangu. Mpe fursa JK aunde baraza jipya!Tofauti na wengi wanavyodhani, mzee wangu Pinda ulishaonyesha dalili za wazi ikiwa kweli unamudu vyema nafasi ya uwaziri mkuu. Kuna mengi tu yaliyofanya baadhi yetu tutilie shaka umahiri wako lakini hii skandali ya Tegeta/escrow imefunga mjadala!

Unakumbuka uliposema na wapigwe tu? Liwalo na liwe!
Wakumbuka ile kauli ya tumechoka?
Wakumbuka mgomo wa madaktari?
Je wakumbuka kauli yenye utata “anayeua albino na yeye auwawe”?
Lakini wajua namna “mchwa” katika baadhi ya halmashauri wanavyotafuna fedha za wananchi?

Tegeta/Escrowni hitimisho la yote haya, mzee wangu Pinda mtoto wa kulima, let it go! Jiuzulu, mpe fursa rais Kikwete aunde baraza jipya la mawaziri, urais unaweza kutafutwa hata nje ya uwaziri mkuu!

Ukiwa mwanasheria utanielewa vizuri naposema hoja si ikiwa unahusika au la! Hili si muhimu sana, hoja hapa ni dhamana ya uongozi kusimamia shughuli za serikali ilishindwa kutumika kunusuru “skandali”hii.

Kiongozi waumma “kutuhumiwa” si jambo jema, tuhuma pekee zinatosha kukufanya ubwage manyanga “resigning does not mean you are weak, but sometimes it means you are strong enough to let it go”

Achia ofisi ya umma kwa manufaa ya walala hoi wa Tanzania, kiongozi wa umma umetuhumiwa kutosimama kidete kuzuia uozo huu kabla, kauli za “kila mtu atabeba msalaba wake” si za kulisaidia taifa, ni kauli inayoashiria hamu ya mtawala asiyependa kuwajibika, anayetaka kung’ang’ania madaraka! Haifai kabisa, busara inakutaka kuwajibika kama mtangulizi wako Edward Ngoyai Lowassa, kumbuka “Caesar’s wife must be above suspicion’’

---
Imeandikwa na Nova Kambota, 

Bilioni 2.9 zinahitajika kujenga maabara Kilolo

Shilingi bilioni 2.9 zinahitajika ili kukamilisha ujenzi wa maabara za sayansi katika shule 24 za Sekondari wilayani Kilolo. Hayo yamesemwa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmsahauri ya Kilolo Bi. Rukia Muwango alipozungumza na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake.

Bi Muwango amesema kuwa katika shule 24 za wilaya hiyo vinahitajika vyumba 72 vya maabara za sayansi lakini mpaka sasa kuna vyumba 11 tu vilizokamilika na vinamika. Changamoto iliyopo ni namna ya kukamilisha vyumba vingine 61 ili kuhakikisha kuwa kila shule inakuwa na vyumba vitatu vya maabara yaani maabara ya Fizikia, Kemia na Baiolojia.

Akizungumzia hali ilivyokuwa mpaka jana na jitihada zilizofanyika, Muwango alisema Wilaya imeanza kujenga ka kuchangisha michango kwa wadau mbalimbali wakiwemo watumishai wa halmashauri hiyo, wananchi na wadau wengine na hivyo mpaka sasa vyumba 46 katika shule 20 vipo katika hatua ya ujenzi wa nguzo za meza za ndani na vyumba 15 katika shule 9 vipo katika hatua ya ujenzi wa kuta.

Aidha Bi. Muwango amewaomba wananchi, wadau mbalimbali na wapenda maendeleo ya wilaya ya Kilolo POPOTE walipo kuchangia ujenzi wa maabara hizi kwa maendeleo ya kilolo na Taifa kwa ujumla.

Michango inaweza kuwasilishwa kupitia akauti ya benki CRDB IRINGA Na 0J71295300 (KILOLO EDUCATION TRUST FUND) au Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo na kupata stakabadhi ya Halmashauri (HW5) au kupitia simu yake ya mkononi 0788211330 / 0717194121. Vilevile wilaya inapokea michango ya vifaa vya ujenzi kama vile saruji, nondo, mabati n.k.

---
Taarifa hii imewasilishwa wavuti.com kupitia ukurasa wa "Contact"

Mwili wa Sebastian Mgimba wawasili, kuzikwa kesho Kinondoni

Ndugu pamoja na jamaa wa marehemu Sebastian Mgimba aliyefariki dunia nchini Malaysia wakibeba jeneza lenye mwili wa Marehemu mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Dar Es Salaam eneo la Mizigo ukitokea nchini Malaysia.Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Sebastian Mgimba aliyefariki nchini Malaysia likiingizwa katika gari maalumu la kubebea jeneza katika uwanja wa Ndege wa Dar Es Salaam katika eneo la kutolea na kusafirishia mizigo mara baada ya mwili huo kuwasilini Nchini Leo ukitokea Nchini Malaysia.Mchungaji akiendelea na ibada fupi iliyofanyika katika eneo la Kutolea mizigo katika uwanja wa ndege wa Dar Es Salaam mara baada ya Mwili wa Marehemu Sebastian Mgimba kuwasili nchini leo.

Habari picha kutoka kwa Josephat Lukaza/josephatlukaza.com

Msiba wa marehemu Sebastian Mgimba upo Sinza Kumekucha ambapo baada ya mwili kupokelewa leo uwanja wa ndege wa Dar es Salaam umepelekwa kwake Sinza na hatimaye kesho kutakuwa na misa ya kumuombea marehemu kala ya mwili wa marehemu kupumzishwa katika nyumba yake ya milele katika makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam. 

Mungu ailaze Roho ya Marehemu mahala pema peponi. Amina.

Bwana ametoa na Bwana Ametwaa Jina la Bwana lihimidiwe

Suzuki Escudo inauzwa


Upande wa kushoto

REGISTRATION NUMBER: T 746 AAT
MAKE: SUZUKI
MODEL: ESCUDO
MODEL NUMBER: TDIIW
BODY TYPE: STATION WAGON
COLOR: BLUE METALLIC
Year Of Manufacture:1995
ENGINE CAPACITY: 1998 cc
FUEL USED: PETROL
HALAFU NI 4WD
TRANSIMISSION: AUTOMATIC.

Gari lipo kwenye hali nzuri kabisa.

Bei ni shilingi milioni 6.5/=

Kwa mawasiliano, piga simu namba 0712 390 200
Kwa ndani inaonyoonekana

Serikali yaipongeza TPHA kwa kukuza sekta ya afya

Mkurugenzi wa Idara ya Tiba wa Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii, Dk. Margaret Mhando akifungua kongamano hilo la kisayansi.

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, imepongeza juhudi za makusudi zinazofanywa na Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (TPHA) katika kushughulikia masuala ya afya kwa jamii huku ikiahidi kushirkiana kwa ukaribu.

Hayo yalisemwa jana mjini hapa na mgeni rasmi Mkurugenzi wa Idara ya Tiba wa Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii, Dk. Margaret Mhando, aliyemwakilisha Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk.Donan Mmbando wakati wa ufunguzi wa kongamano la 31 la Kisayansi na Mkutano mkuu wa mwaka wa TPHA unaoendelea katika ukumbi wa Stella Maris, Bagamoyo.

Dk.Margaret Mmbando alisema kuwa juhudi za dhati zinazofanywa na wadau wa afya serikali inazitambua na watahakikisha wanaendelea kuungana nao kwa hali na mali ilikuisaidia jamaii kwenye mambo yote ya msingi hususani masuala ya afya.

"Tunaipongeza TPHA kwa juhudi hizi za dhati kabisa katka ukuaji na ustawi wa sekta ya afya. Hivyo pia naamini baada ya kongamano hili kwa muda wa siku tano kila atakayetoka hapa atajifunza mambo makubwa na ya msingi katika mustakaba wa sekta hii" alisema Dk.Margaret Mhando.Katibu Mtendaji wa TPHA Taifa, Dk. Oberlin Kisanga (kulia) akimkaribisha, Dk. Margaret Mhando kwenye ufunguzi huo.

Aidha aliwataka TPHA kutanuka zaidi kuwa na matawi mengi ikiwemo kufika pembezoni mwa nchini ilikuweza kutanua huduma zao hizo.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa TPHA Taifa, Dk.Elihuruma Nangawe alisema kongamano hilo la kisayansi la 31, linatarajia kuwa la siku tano na kutarajia kumalizika Novemba 28 ambapo wataalamu wa afya na wadau watajadilina mambo mbalimbali ya afya hapa nchini.

Naye Katibu Mtendaji wa TPHA Taifa, Dk. Oberlin Kisanga alisema kongamano hilo ni la kuwakutanisha wataalamu ili kubadilishana ujuzi, uzoefu na kutoa mapendekezo namna ya kuleta mabadiliko katika jamii.

“Kongamano la kisayansi na mkutano mkuu wa mwaka unahusisha wataalamu wa kisayansi wa ndani na nje ya Tanzania ambapo watajadili masuala ya jamii na maendeleo ya milenia,” alisema Dk. Kisanga na kubainisha kwamba shughuli hiyo itahitimishwa Novemba 28.

Mkutano huo leo unaingia siku ya pili ambapo wajumbe wa TPHA, wanachama na wadau wa sekt za afya na mambo ya jamii wameendelea kujadili mambo mbalimbali katika ukuaji wa sekta ya afya hapa nchini.Mwenyekiti wa TPHA Taifa, Dk. Elihuruma Nangawe akitoa lecture katika kongamano hilo.Baadhi ya washiriki wa kongamano hilo wakifuatlia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa.

Mgeni rasmi Dk. Margaret Mhando kwenye picha ya pamoja na washiriki mara baada ya kufungua kongamano hilo.


 • Habari imeandaliwa na Andrew Chale, Bagamoyo

Ajali mbaya ya gari la abiria yaua 9 papo hapoGari aina ya Toyota Hiace yenye namba za usajili T761 CKD iliyokuwa ikitoka wilayani Kahama kuelekea mjni Shinyanga ikiwa imepinduka katika eneo la Buhangija katika Manispaa ya Shinyanga na kuuwa watu tisa huku ikiwaacha tisa wakiwa majeruhi.

Gari hilo lilipinduka mara tatu baada ya kuvuka tuta na kugonga daraja na kisha kuangukia mtaroni, kutokana na mwendo kasi.

Dereva wa gari hilo Anwar Awadhi mkazi wa Lubaga Shinyanga aliruka na kukimbia.Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limesema waliofariki dunia katika ajali ya Hiace yenye namba za usajili T761 CKD mali ya Fabian Mzaya wa Shinyanga ikiendeshwa na Anuari Awadhi wa Shinyanga aliyekimbia baada ya ajali iliyotokea leo katika eneo la Buhangija mjini Shinyanga kuwa ni 9,majeruhi 9.

Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SSP Longinus Tibishubwamu amewataja waliofariki dunia kuwa ni:-

Nkingwa Kariagi (50) mkazi wa Mwamanota Kishapu, Kelvin Michael (21) utingo wa gari hilo,mkazi wa Ngokolo, mjini Shinyanga, Masanilo Jisandu (miaka 50) mkazi wa Negezi Kalitu Kishapu, Amina Abdallah, mkazi wa Mbika Kahama, Nkola Shija (20) mkazi wa Kahama, Elizabeth Ngusa (15) mkazi wa Maswa na wengine watatu hawajajulikana majina, umri, kabila wala makazi yao.

Majeruhi katika ajali hiyo ni 9, ambao ni Peter Yustasi (49) mkazi wa Sengerema, Flora Ngudungi (35) mkazi wa Ushetu Kahama, Yesaya Samwel (40) mkazi wa Singida, Kwimba Damayake (36) mkazi wa Iramba Tabora na Nyanzobe Henge (70) mkazi wa Uloa Kahama.

Majeruhi wengine ni Katumbi Nangi (36) mkazi wa Uloa Kahama, Emmanuel John (22) mkazi wa Mwakitolyo, Jimoda Kaliagi (52) mkazi wa Mwamanota Kishapu na Kalwa Mwandu (36) mkazi wa Kahama.
 • Imeandikwa na Kadama Malunde, Shinyanga

Rais Obama amtumia salam Rais Kikwete kumtakia afya njema

Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula akiwasilisha kwa Rais Kikwete salamu za kumtakia kheri na afya njema kutoka kwa Rais wa Marekani Barack Obama leo jijini Baltimore, Maryland, Marekani.
Rais Kikwete akiongea kwa furaha na ujumbe kutoka Ubalozi wa Tanzania ulioko jijini Washington DC uliomtembelea kumjulia hali na kwasilisha salamu maalumu za pole za Rais Barack Obama jijini Baltimore, Maryland.


Rais Kikwete akiongea na Balozi Liberata Mulamula na ujumbe wake wa maafisa waandamizi wa ubalozi wa Tanzania nchini Marekani baada ya kupokea salamu maalumu za kumtakia kheri na afya njema kutoka kwa Rais Barack Obama wa Marekani leo jijini Baltimore, Maryland, Marekani.


Rais Kikwete akiongea na Balozi Liberata Mulamula na ujumbe wake wa maafisa waandamizi wa ubalozi wa Tanzania nchini Marekani baada ya kupokea salamu maalumu za kumtakia kheri na afya njema kutoka kwa Rais Barack Obama wa Marekani leo jijini Baltimore, Maryland, Marekani. Rais Kikwete akiwa na maafisa waandamizi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani uliopo Washington D.C. wakati walipomtembelea mjini Baltimore Maryland ambapo balozi Liberata Mulamula aliwasilisha kwa Rais Kikwete salamu maalum za kumtakia kheri na afya njema kutoka kwa Rais Barack Obama leo jijini Baltimore, Maryland, Marekani. 

Habari picha kutoka: Freddy Maro