Ni makusudi hakuna matangazo? Kesho ni mwisho kujiandikisha kupiga kura SM

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja akiwa kijijini kwake akijiandikisha (picha: KJ blog)

Nimetoka kujiandikisha kwa ajili ya kupiga kura hivyo mimi ni mpiga kura halali!

WEWE UMEJIANDIKISHA?

Mara kadhaa nimeongea na baadhi ya watu kama wamejiandikisha, baadhi wanasema hamna haja ya kujiandikisha maana hawaoni wa kuwapigia kura na wengine wanasema hawako taayri kuwapigia kura wagombea maana ni kama tu watakuwa wamewapa njia ya kujipatia ulaji.

Nadhani hii ni dhana potofu. Tujiandikishe ili tuwachague viongozi tunaoona wanatufaa na ikitokea wanafanya madudu tuwe na nguvu ya kuwakemea. AMA HUPIGI KURA NGUVU YA KUKEMEA UTATOA WAPI? Watanzania TUJIANDIKISHE ba KESHO NDO MWISHO WA KUJIANDIKISHA KWA AJILI YA Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

KITU KIMOJA TU CHA KUSHANGAZA SANA NI KUTOKUWEPO NA ELIMU PAMOJA NA MATANGAZO YA KUWAKUMBUSHA NA KUWAHIMIZA WATANZANIA KUJIANDIKISHA. KWANI TUME YA UCHAGUZI HAPA HAIHUSIKI? FUNGU HALIPO LA KULIPIA MATANGAZO NA VIPEPERUSHI?

WAKATI MWINGINE UNAWEZA FIKIRI KUTOKUWEPO NA MATANGAZO HAYO NI MAKUSUDI!

---
Imeandikwa na Zeph Kambele via ukurasa wa wavuti.com wa Facebook.

The launch of African Health Stats website
African Health Stats

Because data is power!

MamaYe is proud to announce the launch of this innovative data site which allows you to chart, map and compare key health indicators across all 54 African Union member states.After months of careful gathering of the data, deciding the indicators, testing the codes, designing how the numbers will be translated into graphs and maps, consulting with governments across Africa, a new website - www.africanhealthstats.org is finally here.
The site is the brainchild of the African Union Commission’s Department of Social Affairs, and provides reliable data on the progress made by members towards their Maputo Plan of Action and Abuja Call commitments.What you will see when you explore African Health Stats is a site which is both informative and beautiful.

You will see an accessible, up-to-date and visually exciting website which details all the data for 33 indicators across four categories in Africa:
Reproductive, maternal, neonatal and child health
HIV and AIDS
Malaria and tuberculosis
Health finance
For the first ever time, data for indicators tracking progress of the Maputo and Abuja commitments are gathered together on one site for all 54 African Union member states, in French or English.

These indicators are populated with internationally recognised and verified data to allow for easy comparison. Find out how the data are collected, and why these indicators matter, view alternative data sources and download graphs in numerous formats.

Importantly, African Health Stats is African-led – this is a tool for Africans to learn about what is happening in their country, to use this information to hold their government's accountable for commitments made.

The site also provides vital evidence for the African Union Commission to support and motivate governments and policy makers to take action on health challenges in the continent. It is powerful way of sharing experiences, best practices and lessons learnt.The effort involved should not be underestimated and I pay tribute to all of our partners who contributed to the development of this fantastic website.

Congratulations to the African Union for supporting its member states to learn from each other, so that all nations make the progress that Africans deserve.

I encourage you to take the time to explore the site and share with colleagues - after all, the more people who have access to the latest evidence - and use it - the more lives we can save.

Partners supporting the development of African Health StatsVery best,
Louise
Dr Louise Hulton
Programme Director
 

Keep in Touch
Feel free to forward this newsletter to interested colleagues and friends.

Follow us:

Here is the number of Students from Sub-Saharan Africa at U.S. Colleges and Universities


The Institute for International Education reports that in the 2013-14 academic year, there were 31,113 students from sub-Saharan Africa enrolled at colleges and universities in the United States. They made up 3.5 percent of the 886,052 foreign students at U.S. colleges and universities that year. The number of students from sub-Saharan Africa was up 1.7 percent from the prior year. But due to an overall increase in the number of foreign students of 8.1 percent, the percentage of all foreign students that were from sub-Saharan Africa decreased from 3.7 percent to 3.5 percent.

Among sub-Saharan African nations, Nigeria in 2013-14 sent the most students to American colleges and universities. That year there were 7,921 Nigerians studying here, up by more than 8 percent from a year ago. The number of students from Nigeria is more than double the number from any other sub-Saharan African nation.

In 2013-14, Kenya ranked second, sending 3,201 students to the United States. But enrollments from Kenya have declined in recent years, including a nearly 9 percent drop this year following a nearly 10 percent drop in the previous year. Ghana ranked third with 2,914 students at U.S. colleges and universities.

South Africa, Ethiopia, Cameroon, Zimbabwe, and Cote’Ivoire each had more than 1,000 students studying in this nation. Angola, Tanzania, Uganda, and Rwanda all sent at least 700 students to study at U.S. colleges and universities.

All told, 50 nations from sub-Saharan Africa had college students studying in the U.S. during the 2013-14 academic year.

Undoubtedly, some of these students from sub-Saharan Africa nations such as Namibia, South Africa, and Zimbabwe are White, but there is no data to report on the racial or ethnic makeup of this group of African students at U.S. colleges and universities.

---
 • wavuti.com cross-posted this article from The Journal of Blacks in Higher Education - www.jbhe.com (firstly seen at the Wanazuoni Yahoo! Group)

Job opportunity at the UNCDF

Basically, professionals with this at least a Master’s Degree in Business Administration, Finance, Banking or related areas, plus preferably a Bachelor Degree in engineering, finance or economics.

Experience:
 1. Preferably a minimum of 5 years of relevant experience;
 2. Ability to build partnerships and deliver results that meet the needs and long-term interest of clients within and outside the institution;
 3. Demonstrated experience in preparation of project financial analysis and creation/evaluation of advanced and complex Ms Excel spread sheet financial models;
 4. Demonstrated experience with private equity/venture investments, credit and risk assessment, with solid financial modelling and risk assessment skills. Project financing experience in the private sector is a plus;
 5. Demonstrated experience in preliminary evaluation of project proposals for assessing their feasibility for private sector funding and/or technical support by LFI.
Here is the link with more info.: jobs.undp.org...51739

(shared to us by MoBlog)Andrew Nyerere: Kama Mwalimu angekuwepo...

Andrew Nyerere
Andrew Nyerere

Kuna maswala kadha wa kadha yanayoikabili Tanzania kwa hivi sasa, miongoni mwa mambo haya ni sakata la akaunti ya BoT Tegeta Escrow, mchakato wa upatikanaji wa Katiba Mpya na mengineyo. Mwandishi Nova Kambota amehojiana na Andrew Julius Nyerere ambaye ni mtoto wa kwanza wa baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, na hii ni sehemu ya mahojiano hayo…

1. SWALI; Kuna mambo kadhaa yaliyojitokeza siku za karibuni ambayo watu wanataka kufahamu manufaa yake kwa taifa, moja ya matukio hayo ni ziara ya Jafar Mermo Idd Amin mtoto wa rais wa zamani wa Uganda marehemu Idd Amin mwaka 2008, je ziara hiyo ambayo ilimkutanisha na
Madaraka Nyerere walipozuru Butiama ilikuwa na manufaa gani kwa taifa?

JIBU; Kwa familia ya Mwalimu Nyerere na familia ya marehemu Idd Amin nadhani ilikuwa jambo zuri kuleta upatanishi, kuhusu kama taifa lilipata faida sijui. Aliongea Jafari kuhusu kuanzisha mfuko wa hela kuwasaidia wanajeshi walioathirika na vita vya Kagera (wa Uganda na Tanzania), pia nchi hizi mbili zilihitaji kupatanishwa , Jenerali Musuguri alikuwa anaongea katika redio miezi michache iliyopita, kwamba wanajeshi wetu walikuwa na hasira sana, kabla ya kufika Kyaka walikuwa wameshawaua watu 10,000 (elfu kumi), Jenerali Musuguri yupo hapa Butiama, natamani kwenda kumuuliza kama hao wote waliouwawa walikuwa ni maadui kwasababu hii ilikuwa ni vita yetu ya kwanza, inawezekana makosa yalifanyika.

2. SWALI; Una maoni gani kuhusiana na mwenendo wa CCM iliyoasisiwa na Mwalimu Nyerere ambayo sasa baadhi ya viongozi wake wanatuhumiwa vikali kujihusisha na ufisadi? Hudhani ni sababu tosha kwa watanzania kuikataa CCM ikiwa inakiuka misingi ya kuundwa kwake?

JIBU; CCM iliamua kujiita Chama Cha Mapinduzi kwa maana ya mapinduzi yaliyofanyika Urusi au Uchina, kwa maana kwamba watu walio wengi wakiwa na njaa wataleta fujo za kuiangusha serikali kama wamechochewa au hata kama hawajachochewa. Iwapo CCM itaendeleza hayo mapinduzi wananchi wataendelea kuichagua, inategemea tu watu wangapi bado wanaamini inaendeleza mapinduzi, maoni yangu mimi siyo muhimu, watu waamue, na nadhani wanaweza kugawanyika katika maamuzi.

3.SWALI; Miaka ya karibuni kumekuwa na watu wanaohoji namna baba wa taifa Julius Nyerere alivyoaga dunia, baadhi ya wanasiasa wametilia shaka mara kadhaa kifo chake mpaka ikampelekea Madaraka Nyerere kutoa kauli, vipi mtazamo wako kuhusu hili? Kuhoji kifo cha Nyerere kuna
maslahi yoyote kwa taifa?

JIBU; Magige, mtoto wa Mwalimu anasema kuna chanjo moja ilikuwa wapewe watanzania ambayo Mwalimu alikuwa ana mashaka nayo. Mwalimu alimwambia Dr Mwakyusa kwamba yeye apewe, aijaribu halafu akiridhika ataiidhinisha wapewe Watanzania, lakini alipopewa hiyo chanjo, Mwalimuhali yake ilibadilika ghafla, amefariki. Niliposikia hiyo stori nilimweleza Magige kuhusu Global 2000 Report ya Warren Christopher, inasemekana katika miaka ya sabini viongozi wa Afrika walishauriwa na IMF wakubali wananchi wao wachanjwe chanjo za magonjwa ili watu wapungue ili iwe rahisi kuwasaidia; kwamba tatizo la kuwasaidia ni tatizo la logistics tu. Inasemekana ushauri huo ulikubaliwa na viongozi wetu. Global 2000 Report ni Top Secret ipo United Nations na hata ukiwa kule huwezi kuipata mpaka uwe na Special Clearence. No, nilimwambia Magige hatutapata faida yoyote tukianza kuuliza maswali kuhusu kifo cha Mwalimu, kama kuna mtu anabisha kwamba World Health Organization inaweza kufanya ufisadi, mtu huyo huwa anashauriwa kufanya utafiti jinsi W.H.O ilivyoanzishwa.

4.SWALI; Unazungumziaje mchakato wa kupatikana kwa katiba mpya nchini, kutokana na matukio yanayoendelea kujitokeza kama Mzee Warioba kupigwa na hali ya kutoelewana miongoni mwa watanzania, Je unaona wapi tumekosea? Nini kifanyike kunusuru mchakato huu ili tupate katiba
itakayolivusha taifa letu kutoka hapa tulipo?

JIBU; Hakuna matatizo kuhusu katiba , isipokuwa kama kuna maoni yanayoweza kuiboresha katiba , maoni mapya ambayo siyo ya UKAWA, sasa ndiyo wakati wa kuyatoa.

5. SWALI; Unazungumziaje uongozi wa baba wa taifa hayati Mwalimu Nyerere? Una lipi la kusema kwa kumlinganisha na viongozi wa zama hizi?

JIBU; Sioni sababu ya kuwalinganisha viongozi wa awamu tofauti, zama tofauti zinahitaji viongozi, kumlinganisha Nyerere na Kikwete hiyo itakuwa sawa kumlinganisha Bismark na Angela Markel.

6.SWALI; Unazungumziaje harakati za vyama vya upinzani nchini kupambana na ufisadi kama wa hivi karibuni wa Tegeta/Escrow? Unadhani vyama hivi vya upinzani vina dhamira ya dhati kupambana na madudu?Je vitafanikiwa?

JIBU; Vyama vya upinzani vina nia njema , hii kashfa inayojadiliwa sasa hivi Bungeni imeletwa na upinzani. Hii vita ya sasa hivi ya Bungeni wanaweza kushinda, lakini kushinda uchaguzi wa serikali za mitaa ni jambo lingine.

7.SWALI; Kadri ulivyomwelewa hayati Nyerere, unazungumziaje kutokuwepo kwake? Je unadhani angekuwepo angesaidia vipi kunusuru taifa kwenye kupambana na ufisadi na kunusuru mchakato wa katiba mpya? 

JIBU; Mwalimu angekuwepo angepinga ufisadi, kuhusu katiba hakuna tatizo kubwa au naweza kusema hakuna tatizo lolote zaidi ya fujo inayoletwa na UKAWA.

8.SWALI; Ukipewa nafasi ya kuwashauri vijana wa sasa wa Tanzania, ungependa wafanye nini kulisaidia taifa lao?

JIBU; Vijana wa Tanzania wafikiri sana kabla ya kuwachagua viongozi.

9.SWALI; Unapata tafsiri gani unapoona taasisi za kidini kama Kanisa Katoliki likianzisha, kusimamia na kuratibu mchakato wa kumtangaza hayati Mwalimu Nyerere kuwa Mtakatifu?

JIBU; Kanisa katoliki ndiyo linataka Mwalimu aitwe lay saint, Mwalimu aliishi maisha ya uadilifu lakini kama alikuwa mtakatifu hiyo ni kwa Vatican kuamua.

10.SWALI; Unaweza kueleza nini kuhusu siku za mwisho za uhai wa Mwalimu na namna alivyokuwa akilalamikia ubinafsishaji/uuzwaji wa mashirika ya umma kama benki ya taifa ya biashara NBC, ukizingatia hali ya ugonjwa wake na uzalendo wake kwa nchi, alikuwa mtu wa namna
gani? Alionekanaje nyakati zile?

JIBU; Uuzaji wa mashirika ya umma au ubinafsishaji siyo jambo baya wakati wote.

Swali; una lolote la kumalizia? 

JIBU; Kwa kumalizia, nataka kusema viongozi wachaguliwe kwa uadilifu, kwasababu ukiwachagua mafisadi, Mungu ataheshimu uteuzi wako, hatabadili kitu chochote!

---
Andrew Nyerere anaweza kupatikana kwa namba 0718- 536281, ikiwa unataka kuwasiliana na Nova Kambota mwandishi aliyefanya mahojiano haya piga simu namba 0712-544237, barua pepe; [email protected] au tembelea novakambota.wordpress.com

----
Mahojiano haya yamewasilishwa wavuti.com na Nova Kambota

Tigo Pesa returns 3/= billion to customers as 1st quarterly payPRESS RELEASE
 • Tigo Pesa returns TZS 3 Billion to customers as first quarterly payment
 • The first mobile money service in the world to pay profit to its users
DAR ES SALAAM, Tanzania, November 27, 2014/ — Tigo (http://www.tigo.co.tz) announced today the first of its regular quarterly payments worth 3bn/- (US $ 1.8 million) to Tigo Pesa users.

This payment comes three months after the company paid a staggering profit of TZS 14.25 billion (US $ 8.64 million) accumulated in the Tigo Pesa Trust Account to become the first mobile money service in the world to pay profit to its users. Tigo Pesa has a subscriber base of 3.6 million customers.

Tigo General Manager Diego Gutierrez said “This second round of profit disbursement shows the company’s continued commitment to benefit and improve the lives of Tanzanians. The payment goes to all Tigo Pesa users including super agents, retail agents and individual users of the service.”

“The first payment was bigger due to the fact that the profit had been accumulated over a period of three and a half years. This second payment is the profit accumulated from funds held in trust in commercial banks for three months in the quarter July to September 2014,” the General Manager said.

Mr Gutierrez explained that, as before, the average return to a customer will vary based on their average daily balance in their Tigo Pesa e-wallet. This applies to super-agents, retail agents and individual customers.

The next installment for the quarter of October to December 2014 will be paid out in February 2015.

For further information visit: www.tigo.co.tz or contact:
John Wanyancha – Corporate Communications Manager
Mobile: 0658 123 089
[email protected]

Mhe. Prof. Tibaijuka jiuzulu kulinda heshima yako

MHESHIMIWA PROF. ANNA TIBAIJUKA BORA UJIUZULU KULINDA HESHIMA YAKO NA CHAMA


Mheshimiwa Bi. Anna Tibaijuka (Mb) Waziri wa Ardhi ni moja wa viongozi wachache sana wenye ujasiri na kiongozi muwazi katika sakata zima la akaunti ya Tageta Escrow, kwani kiongozi huyu amekiri wazi kuwa amepokea fedha shilingi billion 1.6 kutoka kwa mmiliki wa kampuni ya VIP Engineering Bw. James Rugimalira.

Si jambo jema kumhukumu Mheshimiwa Anna Tibaijuka, lakini siyo vibaya kumshauri kwa kuwa amekuwa muwazi katika sakata hili, basi lingekuwa jambo la maana sana kama angejiuzulu madaraka aliyonayo katika serikali ili kulinda heshima yake na ya chama tawala.

Msomi yoyote yule anapofikia kuitwa Profesa na tena Waziri mwenye kushika dhamana ya nchi na wananchi yaani, Ardhi na Makazi, halafu akakubali kupokea fedha ya kiasi kikubwa hivyo bila ya kutia shaka yoyote kama ananuliwa kwa namna moja au nyingine kutokana na dhamana ya cheo chake, litakuwa ni jambo jema kwake kujiuzulu ili aonyeshe mfano bora kuwa yeye ni kiongozi mkweli na viongozi wengine wafuate nyao.

Msomi aliyefikia daraja la juu kabisa tunamwona kama kiongozi anayejua wazi kuwa yeye ni mojawapo wa Mawaziri wachache ambao Wizara zao zina dhamana kubwa ya nchi, leo hii akikubali kununuliwa kiurahisi au kufanya biashara akiwa katika madaraka mazito, tuna mashaka naye ikiwa atandelea kututumikia wananchi katika Wizara ambayo pia inahusika na mipaka ya ardhi ya nchi.

Watanzania tunajiuliza, hivi Mhe. Anna Tibaijuka yupo katika utumishi wa umma tena na huku akiwa Mkurugenzi wa Mashirika au Shule na miradi binafsi, ndiyo kusema cheo chake cha utumishi wa umma ndio dhamana ya biashara zake?

Hivi kuna hosptali ngapi hapa nchini hazina dawa? Je wakina mama wangapi wajawazito wanafariki wakati wa kujifungua kwa ukosefu wa vifaa vya mahosptalini? Shule ngapi za serikali hazina madawati?

Leo Mheshimiwa mabilioni ya fedha na kusema kuwa hakujua kama ni fedha chafu. Kwa vipi Watanzania tusiwe na mashaka naye?

Professor Anna Tibaijuka anafahamu wazi kuwa amevunja sheria ya maadili ya viongozi wa umma "(Sheria namba 13 ya mwaka 1995) ambayo inawataka viongozi watoe taarifa ya zawadi wanazopokea au malipo wanayolipwa."

Hivyo, sisi wananchi wenye kuiamini serikali hii hautuwezi kabisa kukubali au kuona kiongozi tena msomi anavunja dhamana ya wananchi na kumvunjia heshima mkuu wa nchi ambaye ndiye alimteua.

Litakuwa jambo la busara sana Mhe. Anna Tibaijuka ujiuzulu ili kulinda heshima yako kama msomi Professor, pia kulinda heshima serikali na Chama tawala. Huwezi kutumikia ofisi mbili, yaani utumishi wa umma na biashara.

Wanachi tunasikitika sana kuona katika sakata la fedha za umma mpaka baadhi watumishi wa Mungu ambao ni viongozi wa Kanisa nao wanahusika na bila ya woga. Wanapokea fedha bila ya hofu ya kujenga udini.

Mungu ibariki Tanzania.

---
Imewasilishwa wavuti.com via barua pepe.

Mwakilishi wa Ubalozi wa Marekani awapasha Watanzania, "Watanzania hayawezi kumalizwa na Marekani"

Wanahabari Iringa wakimhoji mwakilishi wa balozi wa Marekani Nchini Bw David Feldmann

Taasisi isiyo ya Kiserikali ya mpango wa Maendeleo Salama wa Maendeleo ya Vijana (SYDS) chini ya ufadhili wa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania imekusudia kuwainua kwa kilimo wanachama wa vikundi 43 katika tarafa ya Pawaga wilaya ya Iringa vijijini mkoani Iringa

Akizungumza na waandishi wa habari wakati sherehe ya kufunga mradi huo wa mrejesho kwa vikundi, meneja mahusiano wa SYDS, Arnold Pangani alisema SYDS imejitoa kuendeleza mapambano dhidi ya changamoto zinazowakabili wengi wa akina mama katika sekta kilimo nchini.

Pia alisema hadi sasa tayari wamekwisha toa mafunzo ya kilimo bora kwa wanachama zaidi ya 300 katika tarafa hiyo.

“SDYS kwa udhamini wa serikali ya Marekani kupitia ubalozi wake nchini Tanzania tunaungana kwa pamoja na wananchi wa Pawaga zaidi tukitambua ushiriki wa wanawake katika kilimo,” alisema Panagani.

Aidha, wanavikundi walitoa shukrani ya dhati kwa SDYS kwa kuwapatia mwongozo bora ambao umewawezesha kupata uelewa juu ya elimu ya mpango biashara na uendashaji vikundi.

Walisema kuwa kuja kwa asasi ya SDYS kumeweza kuhamasika na kuunda vikundi ambavyo vitasaidia katika shughulu za kilimo.

Walisema kwa mafunzo hayo kama vijana wametambua umuhimu wao kama vijana ni nguvu kazi na wanatakiwa kushiriki shughuli za maendeleo na kujifunza zaidi juu ya mpango salama kwa maendeleo ya vijana.

Kwa upande wake mwakilishi wa ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, David S. Feldmann alisema Tanzania itajengwa na Watazania wenyewe kama ambavyo Marekani inajengwa na Wamarekani. Akasema matatizo ya Watanzania hayawezi kumalizwa na Marekani ila katika uwezekaji lipo suluhisho la matatizo mengi.

Alisema ni jukumu la kila mwananchi kuhakikisha kuwa anashiriki kikamilifu katika kuinua na kukuza uchumi. Pia, Watanzania lazima hawana budi kulipa kodi kwa Serikali ili waweze kupatiwa huduma stahiki kutoa Serikalini kama ilivyo nchini Marekani. Alisema kuwa asilimia 90 ya serikali ya Marekani inaendeshwa kwa mapato ya ndani kwa vile wananchi wengi wanalipa kodi kwa serikali bila kutegemea misaada ya nje.


Wasanii wakionyesha igizo jinsi watakavyonufaika na asasi hiyo


Mwakilishi wa balozi wa Marekani David Feldmann wa pili kulia akifuatilia burudani mbalimbali

Baadhi ya viongozi wakimsikiliza mwakilishi wa balozi wa Marekani nchini

Wanakikundi wakiwa katika mkutano huo wakimsikiliza mwakilishi wa balozi

Baadhi ya wana kikundi watakaonufaika na taasisi hiyo

Wananchi Pawaga wakifuatilia mkutano huo

Msanii kutoka mjini Iringa akionyesha ujuzi wa kucheza na nyoka aina ya chatu kwa kujaribu kummeza

wavuti.com imeshirikishwa taarifa hii na Francis Godwin/Matukio Daima blog

StarTimes yawashushia wateja ofa kabambe msimu huu wa sikukuu • StarMedia yashusha bei ya ving’amuzi vyake msimu huu wa sikukuu kutoka sh. 79,000/- mpaka 59,000/- ambapo mteja akilipia kifurushi chochote na kufikia kiwango cha sh. 120,000/- atapatiwa simu ya bure aina ya S100 hii ni katika sharamshamra za msimu wa sikukuu za Krisimasi na Mwaka Mpya.


Dar es Salaam, Novemba 26, 2014 — Katika kuhakikisha kila mtanzania anapata fursa ya kufurahia huduma ya matangazo ya digitali nchini kampuni ya StarMedia Tanzania wameamua kushusha bei ya ving’amuzi vyao vya StarTimes kutoka shilingi 79,000/- mpaka 59,000/- katika kipindi hiki cha msimu wa sikukuu za Krisimasi na Mwaka Mpya.

Akizungumza na waandishi wa habari Meneja wa Mauzo wa kampuni hiyo, David Kisaka alibainisha kuwa bei hiyo iliyoshushwa ni kwa ving’amuzi vinavyotumia antena za nje na ndani au DTT na hii ni katika jitihada zetu kuhakikisha kila mtanzania anafikiwa na huduma zetu kwa gharama nafuu.Waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini uzinduzi wa uzinduzi wa promosheni ya krisimasi na mwaka mpya ambapo wameshusha bei ya ving’amuzi vya antenna kutoka sh. 79,000/- mpaka 59,000/- na ofa ya simu ya kisasa ya bure aina ya S100 endapo mteja atalipia kifurushi chochote kwa kiasi cha Sh. 120,000/-. Pia kampuni hiyo ilitangaza kupatikana kwa simu za kisasa aina ya P40, Solar 5, na Planet 5 zitakazopatikana katika ofisi na maduka ya mawakala na washirika wa kampuni ya StarTimes Tanzania katika kipindi hiki cha msimu wa sikukuu za Krisimasi na Mwaka Mpya.

Kisaka amesema, “StarTimes tumedhamiria kuwahakikishia watanzania kuwa huduma zetu zitaendelea kuwa nafuu kulingana na hali halisi ya maisha tuliyonayo. Kulithibitisha hilo, ninayofuraha kubwa leo kuwatangazia bei mpya ya ving’amuzi vya antena za nje na ndani itakuwa ni shiling 59,000/- na sio shilingi 79,000/- kama ilivyokuwa awali. Bei hii mpya ni dhamira yetu ya dhati kabisa ya kuwapatia wateja matangazo ya digitali ya uhakika na kwa bei nafuu ambayo kila mtu ataimudu hata yule mwenye kipato cha chini kabisa.”

“Punguzo hili la bei linakwenda sambamba na ofa kabambe ambapo endapo mteja wa StarTimes atalipia kifurushi chochote kile na kunafikia kiwango cha shilingi 120, 000/- basi atapatiwa simu ya bure na ya kisasa kabisa aina ya S100 na hapa ninamaanisha kwa watumiaji wa ving’amuzi vya kawaida na madishi. Kwa ving’amuzi vya kawaida inamaana akilipia kwa kiwango hicho ni sawa na kulipia kifurushi cha Mambo kwa mwaka mzima (10,000/-), Uhuru kwa miezi sita (20,000/-) na Kili kwa miezi minne (30,000/-). Na kwa upande wa madishi pia ni hivyo hivyo endapo akilipia vifurushi vya smart ambacho ni shilingi 32,000/- na special kwa shilingi 16,000/-,” aliendelea Bw. Kisaka.

“Mbali na ofa ya punguzo la bei na zawadi za simu pia mteja wa StarTimes akilipia kifurushi chochote kwa miezi mitatu atapatiwa ofa ya mwezi mmoja wa bure na atakayelipia mwezi mmoja na nusu au siku 45 atapatiwa nusu mwezi au siku 15 bure,” alisema na kuongezea Bw. Kisaka, “Lengo la kufanya hivi ni kuwafanya wateja wetu waendelee kufurahia zaidi chaneli na vipindi vyetu na pia kuwashawishi waendelee kulipia zaidi na chaneli zingine ili kupata uhondo zaidi kwani haitoshi tu kutazama chaneli na vipindi vya nyumbani.”

“Hivyo basi ningependa kuwasihi wateja wetu na watanzania kwa ujumla ambao mpaka sasa bado hawajaunganishwa na huduma za StarTimes basi wakati ndio huu kwani tumewashushia gharama za chini kabisa kwa lengo la kumfikia kila mtu. Ili kuweza kupatiwa huduma zetu basi ningewaomba mtembelee ofisi na maduka yetu, kwa sasa tunayo maduka sita jijini Dar es Salaam likiwemo hili la hapa mtaa wa Samora, Tegeta, Buguruni, Bamaga, Msimbazi-Kariakoo na Ukonga huku mengine kumi yakiwa mikoani zilizo huduma zetu.” Alimalizia Bw. Kisaka.

Baadhi ya simu za kisasa aina ya P40, Solar 5, na Planet 5 zitakazopatikana katika ofisi na maduka ya mawakala na washirika wa kampuni ya StarTimes Tanzania katika kipindi hiki cha msimu wa sikukuu za Krisimasi na Mwaka Mpya. Pia kampuni hiyo imetangaza kushusha bei ya ving’amuzi vya antenna kutoka sh. 79,000/- mpaka 59,000/- na ofa ya simu ya kisasa ya bure aina ya S100 endapo mteja atalipia kifurushi chochote kwa kiasi cha Sh. 120,000/-. Uzinduzi huo ulifanyika leo jijini Dar es Salaam katika duka la kampuni hiyo lilipo makutano ya mtaa wa Samora na barabara ya Morogoro.

Naye kwa upande wake Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa StarTimes Tanzania, Jack Yu alitumia fursa hiyo pia kuwapatia watanzania habari njema kuhusu simu mpya na za kisasa zitakazopatikana katika msimu huu.

“Kwa mara nyingine tena StarTimes tunawaletea simu za kisasa ambazo zitapatikana kwa bei nafuu kabisa katika maduka yetu ya Bamaga, Msimbazi na hili la Samora. Mbali na maduka hayo pia simu hizi zitapatikana kwenye maduka ya mawakala na washirika wetu kama vile Vodacom na Airtel.” Alisema Bw. Yu

“Simu hizi ambazo zitapatikana kwa bei nafuu ni zawadi yetu kwa wateja wetu na watanzania kwa ujumla watakaotembelea ofisi na maduka yetu. Aina ya simu ambazo zitakazopatikana ni P40 yenye garantii ya miezi 13, Planet 5 na Solar 5 ambayo mteja atapatiwa na power bank ya bure, zote hizi zitapatikana kwa bei ya shilingi 129,000/-, 225,000/- na 270,000/-”

“Simu hizi zina uwezo mkubwa wa kupata huduma zote ikiwemo kutumia laini mbili za simu, uwezo mkubwa wa kuhifadhi vitu (memory card ya GB 8 ya bure) kwa ajili ya kuweka kumbukumbu ya matukio mbalimbali, kamera ya mebele na nyuma kwa kupiga picha nzuri na za kuvutia, uwezo wa kupata intaneti yenye kasi (3G) itakayokuwezesha kuperuzi mitandao ya kijamii kama vile Facebook, Twitter, Whatsap, Viber, Wechat na kadhalika. Ningependa kuchukua fursa hii kuwataka watu wajitokeze na kujinunulia simu hizi kwani ni chache.” Alihitimisha bosi huyo wa StarTimes.

What happens to data deleted from your computer?

Huh? "Vampire Club" at Harvard?

(image: postsecret.com)

Uenyekiti wa EAC kuchukuliwa na Tanzania

Joyce Mapunjo, Katibu Mkuu EAC
Joyce Mapunjo, Katibu Mkuu EAC

Mkutano wa 16 wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utafanyika Tarehe 30 Novemba, 2014 Nairobi, Kenya.

Kwa mujibu wa Mkakaba Mkutano huu utatanguliwa na Mkutano wa Baraza la Mawaziri la
Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika Tarehe 20 – 27 Novemba, 2014 katika ngazi ya Wataalam, Makatibu Wakuu na Mawaziri. Aidha, katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatarajiwa kukabidhiwa uwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kipindi cha mwaka mmoja na Jamhuri ya Kenya inayomaliza kipindi chake, Ikiwa ni utekelezaji wa Ibara ya 12 (2) ya Mkataba wa Uanzishaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Akizungumzia Tanzania kuchukua Uenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Katibu Mkuu wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Joyce Mapunjo alisema, “Katika kipindi cha uenyekiti wake, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendeleza mafanikio yaliyopatikana wakati wa kipindi cha uenyekiti wa Jamhuri ya Kenya. Aidha, mkazo utawekwa katika kuhakikisha mtangamano wa Afrika Mashariki unaendelezwa kwa kuzingatia matakwa ya Mkataba wa Uanzishwaji wa Jumuiya pamoja na Kanuni na Taratibu za Jumuiya. Aidha, mkazo utawekwa katika kuhakikisha Sekta binafsi na Wadau wengine wanashirikishwa kikamilifu katika utekelezaji wa mtangamani wa Afrika Mashariki ikiwa ni pamoja na kuzitumia fursa zitokanazo na Jumuiya ya Afrika Mashariki,”

Mkutano wa 16 wa Wakuu wa Nchi utatanguliwa na Mkutano wa tatu wa Kazi wa Wakuu wa Nchi kuhusu uendelezaji wa miundombinu katika Jumuiya. Mkutano hu utapokea taarifa ya utekelezaji wa maagizo waliyoyatoa katika mkutano wa pili uliofanyika mwezi Novemba, 2012 na kuidhinisha miradi 72 ya miundombinu ya kipaumbele ya barabara, reli, nishati na bandari. Kwa upande wa utekelezaji miradi 16 imekamilika, 39 utekelezaji unaendelea na 17 ipo katika hatua za awali za kutafutiwa fedha kwa ajili ya utekelezaji wake.

Kwa upande wa Tanzania miradi nine imekamilika ambayo ni kuupatia mji wa Kibondo umeme, mradi wa barabara ya Mbezi-Shule-Tangibovu-Makutano ya Nelson Mandela na barabara ya Tabata. Barabara nyingine iliyokamilika ni Nyangunge – Musoma-Airari. Shemu ya Simiyu-Musoma inayounganisha Kenya na Tanzania ujenzi unaendelea.

Kwa mujibu wa Agenda, Wakuu wa Nchi watapokea taarifa ya Baraza la Mawaziri la Jumuiya kuhusu utekelezaji wa mtangamano wa Afrika Mashariki kwa kipindi cha Novemba, 2013 – Novemba, 2014. Aidha, Wakuu wa Nchi watajadili hatua iliyofikiwa katika majadiliano ya Sudan Kusini kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki, maombi ya Jamhuri ya Somalia kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki, suala la uchangiaji katika bajeti ya Jumuiya na mapitio ya mfumo wa Kitaasisi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Wakuu wa Nchi watajadili pia hatua iliyofikiwa katika majadiliano ya uanzishaji wa Shirikisho la Kisiasa la Afrika Mashariki Ikiwa ni pamoja na maandalizi ya Mpangokazi wa kuelekea katika Shirikisho pamoja na mchakato wa kuiongezea mamlaka Mahakama ya Afrika Mashariki ili iweze kushughulikia mashauri yanayohusu biashara, uwekezaji na utekelezaji wa Umoja wa Fedha wa Afrika Mashariki.

Kumekuwepo na mafanikio kupitia ushiriki wa Tanzani katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Tangu kuanza kwa Umoja wa Forofha wa Afrika Mashariki, mauzo ya Tanzania katika Jumuiya ya Afrika yameongezeka kutoka Dola za Marekani Milioni 142 mwaka 2005 hada kufikia Dola za Marekani Milioni 1,120 mwaka 2013. Bidhaa ambazo zimekuwa zikiuzwa kwa wingi ni pamoja na nafaka, karatasi, mbole, vifaa vya umeme, mashine, bidhaa za mafuta na vimiminika, vyandarua, bidhaa za plastiki, chai, na bidhaa za karatasi. Bidhaa nyingine ni saruji, matunda, chuma, samaki, ngano, sukari na nguo.

Kwa upande wa uwekezaji, miradi iliyowekezwa hapa Nchini kutoka nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki imeongezeka kutoka miradi 35 yenye thamani ya Dola za Marekani Milioni 39.65 mwaka 2005 na kufikia Miradi 244 yenye thamani ya Dola za Marekani milioni 676.45 mwaka 2013. Miradi hii imezalisha jumla ya ajira 15,721 katika kipindi husika.

Katika kuimarisha biashara na fursa za masoko ndani ya Jumuiya, Tanzania imeanza utekelezaji wa mfumo wa Himaya ya Forodha ulioanza 1 Julai, 2014. Katika mfumo huu, uthamini wa bidhaa na ukusanyaji wa kodi unafanyika katika Nchi mwanachama iliyoagiza bidhaa na baada ya kuthibitisha kwamba kodi imelipwa bidhaa zinaondolewa kutoka bandari ya Dar es salaam na kusafirishwa kwenda nchi husika mwanachama chini ya usimamizi wa Mamlaka ya Forodha kwa kutumia mfumo wa Kieletroniki wa Ufuatiliaji wa bidhaa. Aidha, bidhaa zilizolipiwa kodi katika Nchi husika husafirishwa hazihitaji kuwekewa dhamana na hivyo kupunguza gharama za kufanya biashara.

Kwa upande wa uendelezaji wa Miundombinu Jumuiya imeandaa Mipango Kabambe ya uendelezaji wa barabara na reli zinazounganisha Nchi Wanachama. Utekelezaji wa mipango hiyo unaendelea na kwa upande wa Tanzania umehusisha ujenzi wa barabara ya Arusha- Namanga-Athi river, Arusha-Holili-Voi-Mwatate na Malindi-Lingalinga lunga/Tanga-Bagamoyo zote zikiunganisha Tanzania na Kenya. Kwa upande wa mtandao unaounganisha Tanzania, Burundi, Rwanda na Uganda ujenzi wa barabara zinazoanzia Tunduma-Iringa/Sumbawanga na kuelekea nchi hizo jirani umekamilika.

Ibara ya 124 ya Mkataba inatambua kuwa amani na usalama ndiyo msingi wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Nchi Wanachama zimeidhinisha na kutekeleza Mkakati wa kikanda wa Amani na Usalama tangu mwaka 2006.

Katika kukabiliana na changamoto za kiusalama katika Jumuiya Mkakata huu umefanyiwa mapitio na kuongeza masuala ya Kukabiliana na Uharamia, Kupambana na uhalifu wa kimtandao, Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu, Mauaji ya Kimbari na Usafishaji wa fedha haramu ambazo ndizo zimekuwa zikitumika kufadhili uhalifu.

Aidha, ili kushirikisha wadau zaidi katika kuimarisha usalama, Jumuiya iliandaa kongamano la viongozi hao katika kuzuia kusambaza kwa waumini wa itikadi kali za kidini na pia kuwashirikisha katika kufundisha umuhimu wa imani yao ya dini na amani kwa waumini wao. Katika kuhakikisha wanachi wanashirikishwa utaratibu wa Katibu Mkuu wa Jumuiya kukutana na Sekta binafsi, Asasi za kiraia na wadau wengine kwa ajili ya mashauriano na kupata maoni yao juu ya uendeshaji wa Jumuiya.

Imetolewa na
Katibu Mkuu

The most popular (and probably best) 2014 Android phone

I am glad to say that I am a happy owner of OnePlus One! This is the most expensive new phone I've ever bought ($350) but totally worth every dime! Before it, I had an HTC One (not M8) which was overall good except for the picture quality and colors, and if I had no option but one phone to choose among the HTCs, I'd stick to my HTC One S or buy an HTC One 8.Over at LifeHacker, Alan Henry has shared this post:

There are so many great Android phones on the market right now that no list could contain them all, but when we asked you for your picks, you gave us a great selection. We looked at the five best Android phones of the year based on those picks, and after over 38,000 votes, it's time to highlight your favorite.

The poll results

The Cyanogen-powered, difficult-to-obtain OnePlus One took the top spot by a fair margin, bringing in close to 49% of the overall vote and taking first place. The team behind it still operates on invites, but they've recently opened the door to a batch pre-order system that will get you in line to get one of the affordable, high-end phones if you want one.

Second place went to the slightly old but arguably another killer bang for your buck, the Nexus 5 by LG. Many of you said it was just the right size, just the right price, and since it's a Nexus, if you have one you already have Lollipop—and Lollipop sings on an Nexus 5. It brought in close to 16% of the overall vote. In third with just under 15% of the votes cast was the successor to last year's top pick, the HTC One M8. Almost every comment about it praised its build quality, all-metal design, and improved features over the original HTC One. Fourth place went to the Moto X, a great all-around phone that brings powerful features to the table without costing you an arm and a leg to get them. It picked up close to 11% of the vote. Bringing up the rear in fifth was the Sony Xperia Z3, Sony's latest flagship, with its dustproof and waterproof chassis and high-quality camera. It earned just over 10% of the overall vote.

For more on each of these and the honorable mentions not listed here, make sure to head back to the full Hive Five feature to read more.

The Hive Five is based on reader nominations. As with most Hive Five posts, if your favorite was left out, it didn't get the nominations required in the call for contenders post to make the top five. We understand it's a bit of a popularity contest. Have a suggestion for the Hive Five? Send us an email at [email protected]!

Photo by opopododo.

Mugabe apewa madaraka zaidi


Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ameendelea kushutumiwa kuwa anashikilia chama tawala cha ZANU-PF kama chama chake biinafsi.

Ikiwa imesalia wiki moja ili mkutano mkuu wa chama hicho ufanyike, ambapo anatazamiwa kuongezwa muhula kwa kuendelea kushikilia nafasi hiyo kwenye chama, Robert Mugabe amejipa madaraka yote katika chama, ikiwa ni pamoja na kumwondosha mrithi wake katika uongozi wa nchi.

Makamu wa rais wa Zimbabwe Joice Mujuru ameondolewa katika Kamati kuu ya chama tawala ZANU-PF kwa tuhma za kupanga mbinu za kumuua rais Robert Mugabe na pia anatuhumiwa kuhusika na wizi wa fedha kutoka Kampuni za serikali.

Bi Mujuru amekuwa akishtumiwa na Mke wa Mugabe, Grace Mugabe wakati huu siasa zikiendelea ndani ya chama cha ZANU-PF kuhusu ni nani atakayemrithi Mugabe ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 90.

C Chachage: Tofauti kati ya Ripoti ya "Escrow" na ya Richmond

Tofauti kubwa kati ya ripoti ya uchunguzi wa RICHMOND na ya ESCROW ni kuwa:

Ya kwanza ilitolewa na KAMATI TEULE ya BUNGE ambayo ilikuwa na MUDA mwingi sana na RASILIMALI nyingi mno za kufanya UCHUNGUZI uliohusisha hadi ZIARA za kwenda NCHI za MBALI kufuatilia KAMPUNI hiyo ILHALI hiyo ya pili imetolewa na KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE ambayo ilikuwa na MUDA mfupi sana na RASILIMALI chache mno za kufanya UCHUNGUZI ambao ulihusisha kupitia/kuchambua/kuhakiki/kujumuisha TAARIFA za UCHUNGUZI wa CAG n.k. pamoja na kuwahoji wakuu wa TAKUKURU, TRA, CAG et al.

Kilicho muhimu sasa ni kuhakikisha haturudii makosa yaliyogusiwa hapa chini kuhusiana na MAAZIMIO ya BUNGE:

 • Tusirudie makosa kwenye maazimio ya #Escrow, tujikumbushe maazimio ya #Bunge kuhusu #Richmond ambayo hayakutekelezwa:

Taarifa ya Hoja kuhusu utekelezaji wa maazimio juu ya Richmond

Tarehe 25 Januari 2012 nimewasilisha kwa Katibu wa Bunge taarifa ya hoja kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge Toleo la 2007 Kanuni 54 (4) na 55 (1) kuhusu utekelezaji wa maazimio ya Bunge juu ya mkataba baina ya TANESCO na Kampuni ya Richmond Development Company LLC.

Hoja hiyo ikipewa nafasi ya kuwasilishwa na kujadiliwa itaongeza msukumo wa utekelezaji wa maazimio ya bunge na hivyo kuchangia katika mapitio ya mikataba yenye kuongeza bei ya umeme; kuweka mfumo wa kulihusisha bunge katika maandalizi ya mikataba yenye maslahi ya taifa ikiwemo katika mafuta, gesi asilia na ujenzi na kuwezesha uwajibikaji na hatua kamili kuchukuliwa kwa waliohusika na ufisadi na uzembe uliolisababishia hasara taifa.

Taaarifa hii ya hoja niliiwasilisha awali tarehe 13 Aprili 2011 na kupatiwa majibu; hata hivyo niliijibu ofisi ya bunge kupatiwa taarifa ya utekelezaji uliofanywa na serikali baada ya Februari 2010 bila kupatiwa majibu hivyo nimeiwasilisha tena ili hoja husika ijadiliwe.

Lengo la Hoja Binafsi nitakayoiwasilisha kufuatia taarifa hiyo ni kutaka uamuzi wa Bunge uliofanyika katika Bunge la Tisa Mkutano wa 18 mwezi Februari 2010 kuhusu utekelezaji wa maazimio ya Bunge juu ya mkataba baina ya TANESCO na kampuni ya Richmond Development Company LLC; UBADILISHWE.

Katika muktadha huo, hoja binafsi husika itawezesha mjadala kuhusu uamuzi husika kufunguliwa na kutoa fursa kwa jambo hilo kufikiriwa tena ili kuwezesha hatua kamili kuchukuliwa juu ya maazimio 23 ya Bunge yaliyopitishwa tarehe 15 Februari 2008 katika Mkutano wa 10 wa Bunge la Tisa.

Taarifa ya tatu ya Serikali Februari 2010 ilitanguliwa na Taarifa mbili zilizowasilishwa Bungeni na Waziri Mkuu, Mheshimiwa Mizengo Pinda, tarehe 28 Agosti, 2008, tarehe 11 Februari, 2009 na Taarifa moja iliyokabidhiwa na kujadiliwa na Kamati, ambazo zililitaarifu Bunge kuwa utekelezaji wa Maazimio 10 kati ya 23 yaliyotolewa na Bunge, yamefanyiwa kazi hadi mwezi Februari, 2009 na Maazimio 13 bado yalikuwa hayajakamilika. Maazimio hayo 13 ni: Nambari 1,2,3,5,7,8,9,10,11,13,14,15 na 18. Hoja binafsi itakapojadiliwa bungeni itawezesha Bunge na wananchi kwa ujumla kupata taarifa ya utekelezaji wa maazimio hayo 13.

Kati ya maazimio hayo 13, baadhi ya maazimio ambayo utekelezaji wake haujakamilika ni pamoja:

Azimio Na. 3, ambalo liliagiza kwamba “Mkataba kati ya TANESCO na Richmond Development Company LLC (uliorithiwa na Dowans Holdings S.A.) na ile kati ya TANESCO na IPTL, SONGAS, AGGREKO na Alstom Power Rentals, ipitiwe upya mapema iwezekanavyo kama ambavyo Mikataba ya Madini ilivyopitiwa upya na Serikali”. Iwapo Azimio hili lingetekelezwa kwa ukamilifu wake, gharama za uzalishaji TANESCO zingepungua na hivyo bei ya umeme isingepandishwa kwa kiwango kikubwa kama ilivyo sasa, ambapo Januari 2011 ilipandishwa kwa wastani wa 18.5% na Januari 2012 imepandishwa tena kwa wastani wa 40.29 kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo mzigo mkubwa wa ufisadi na ubovu wa mikataba.

Azimio Na. 8 na 14, maudhui ya maazimio hayo yanafanana kwa sababu yaliitaka “Serikali iwawajibishe Viongozi wenye dhamana ya kisiasa waliokuwa Mawaziri wa Wizara ya Nishati na Madini ambao wakati ule alikuwa ni Mheshimiwa Dkt. Ibrahim Msabaha na Mheshimiwa Nazir Karamagi.” Bunge lilielezwa kwamba vyombo vya Dola vimekamilisha uchunguzi wake wa ndani ya Nchi kuhusu suala hili. Hata hivyo zoezi lililoendelea toka Februari 2010 ni kufanya uchunguzi wa nje ya Nchi kwa kushirikiana na Vyombo vya Dola vya Kimataifa ambapo mwaka mmoja umemalizika bila hatua zozote kuchukuliwa kwa wahusika katika kashfa ambayo maazimio ya bunge yalipitishwa zaidi ya miaka mitatu iliyopita hali ambayo inaweza kusababisha hata mashahidi na ushahidi kupotea.

Azimio Na. 13, “Serikali izihusishe Kamati za Kudumu za Bunge kwenye hatua za awali za maandalizi ya Mikataba mikubwa ya muda mrefu ya kibiashara ili kuondokana na utaratibu uliopitwa na wakati kwamba Mikataba ya Kibiashara ni siri hata kwa walipa kodi wenyewe. Aidha, Serikali ihakikishe kuwa, Kamati zote za Bunge zinapitia Mikataba mikubwa ya muda mrefu ya kibiashara chini ya sekta zao ili kuliondolea Taifa mizigo isiyo ya lazima”. Azimio hili halijaanza kutekelezwa kwa ukamilifu wake matokeo yake ni kwamba serikali katika kipindi cha kati ya mwaka 2008 mpaka 2011 imeendelea kuwa siri katika hatua za awali za maandalizi na pia mikataba mingi haijafanyiwa mapitio. Hoja binafsi itawezesha mjadala kuhusu suala hili kufunguliwa na utaratibu thabiti kuwekwa katika kipindi hiki ambacho taifa linaingia katika mikataba mingi ya ujenzi na miundombinu na pia mikataba ya utafutaji na uchimbaji wa madini, mafuta na gesi asilia ambayo ina umuhimu wa pekee kwa uchumi na usalama wa nchi. Aidha, azimio hili lingetekelezwa kwa ukamilifu lingesaidia kuwa na mfumo mzuri zaidi wa maandalizi ya mikataba wakati huu ambapo serikali inaingia mikataba mingi ya gharama kubwa ya utekelezaji wa mpango wa dharura wa umeme hali ambayo imeongeza mzigo mwingine wa gharama za maisha kwa wananchi.

Azimio Na. 10, “Gavana wa Benki Kuu pamoja na Bodi ya Wakurugenzi, wachunguze kwa makini uhalali wa malipo ya ziada (US$ 4,865,000) yaliyofanywa kwa Dowans Holdings S.A iliyorithi majukumu ya Richmond Development Company LLC na kuwachukulia hatua waliohusika na uzembe huo.” Hoja Binafsi itawezesha mjadala kufunguliwa na mambo zaidi yaliyojiri kuhusu suala hili na mengine kuweza kujulikana na hatua kuchukuliwa kwa wote waliozembea ili kuimarisha misingi ya uwajibikaji katika taifa.

Masuala zaidi kuhusu maazimio mengine nitayaweka katika Maelezo ya Hoja na Hoja Husika ili niwasilishe katika Mkutano wa Sita wa Bunge la 10 uliopangwa kuanza tarehe 31 Januari 2011 kwa kadiri itakavyoelekezwa.

Imetolewa tarehe 27 Januari 2012 na:

John Mnyika (Mb)

Mbunge wa Ubungo


Richmond: Kufunga mjadala bungeni ni kukejeli umma

 • Tujikumbushe maazimio ya Bunge kuhusu Richmond ambayo hayakutekelezwa ili tusirudie makosa kwenye maazimio ya Escrow:
BUNGE la Jamhuri limetishwa. Spika Samwel Sitta “ameng’olewa meno” na kurejeshwa katika “dini” yake ya asili.
Viwango na kasi – Standard and Speed – alivyosema ni mwongozo katika kutenda kazi zake, vimepingwa kikumbo kabla kipindi chake cha ofisi hakijamalizika.
Wiki tatu zilizopita, Sitta alifunga mjadala wa Richmond bungeni kwa kile alichodai “serikali imetekeleza maazimo 21 kati ya 23 yaliyotolewa na bunge.”
Spika alionekana na kusikika akisema maazimio mawili yaliyosalia yamekabidhiwa kwa mamlaka zinazohusika.
Hakuishia hapo. Sitta alionya wabunge kuwa yeyote atakayeibua mjadala huo upya, atamshughulikia kwa mujibu wa kanuni za bunge. Haya yana maana gani?
Sitta amesema serikali imetekeleza maazimio ya bunge 21 kati 23. Siyo kweli. Ni azimio moja tu la bunge ambalo limetekelezwa na serikali ipasavyo.
Azimio lililotekelezwa ni lile lililotaka Wakala wa Usajili wa Leseni za Makampuni na Biashara (BRELA) kuifuta Richmond katika daftari lake la usajili. Mengine yote hayajatekelezwa.
Kwa mfano, serikali ilitakiwa kutotumia mawakala katika kufanya manunuzi ya umma na kuiondoa mamlaka ya manunuzi ya umma (PPRA) katika minyororo ya wizara ya fedha.
Katika taarifa yake bungeni, serikali inasema, “…Marekebisho ya Sheria ya PPRA (sura ya 410) na muswada husika, vitawasilishwa bungeni katika mkutano wa Aprili mwaka huu, kulingana na ratiba ya vikao vya bunge.”
Hapa serikali haijasema kama muswada umepelekwa bungeni. Inasema, “unatarajiwa” kupelekwa. Wala haijasema kwa nini imeshindwa kufanya hivyo miaka mitatu iliyopita.
Je, kule kusema kwamba inatarajia kutekeleza, kunatosha kuaminisha Sitta kuwa serikali imetekeleza? Kuna mangapi ambayo serikali hii imeahidi na ambayo hayajatekelezwa hadi leo, zikiwamo hata hukumu za mahakama.
Azimio jingine ni lile lililotaka serikali kupitia upya mikataba kati ya TANESCO na makampuni ya kuzalisha umeme ya Richmond/Dowans, IPTL, Songas, Aggreko na Alstom.
Hili nalo halijatekelezwa. Badala yake serikali imekuja na visingizio lukuki, kwamba “kuna mashauri mahakamani yaliyokwamisha utekelezwaji.”
Hapa kuna hoja mbili kubwa. Kwanza, serikali imekiri kutotekeleza kile ilichoagizwa. Pili, imeshindwa kueleza uhusiano kati ya mashauri yaliyopo mahakamani na upitiaji wa mikataba.
Kama kuwapo kwa kesi mahakamani ndiko kulikozuia kupitiwa mikataba, kwanini serikali imekubali kusitisha malipo ya Richmond/Dowans? Je, hatua hiyo haingiliani na kesi iliyopo mahakamani?
Si hivyo tu, ni serikali hiyohiyo iliyositisha uzalishaji wa umeme; iliyoagiza TANESCO kununua umeme wa IPTL – wakati nayo iko mahakamani.
Ni serikali iliyotumia mamilioni ya shilingi kununulia mafuta ya mitambo ya kampuni iliyoshitaki serikali na ambayo mkataba wake unalalamikiwa kutolewa katika mazingira ya rushwa.
Hata maazimio Na. 4, 5, 7 na 9 yaliyotaka serikali kuwajibisha watendaji wa umma waliohusika na mchakato za zabuni, hayakutekelezwa.
Ripoti ya serikali katika ukurasa wa 26 inasema, “…Baada ya serikali kupitia tena tuhuma zilizotolewa na Kamati Teule… imeridhika na maamuzi ya Mamlaka za nidhamu za kuwafutia mashtaka watuhumiwa.”
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, waliofutiwa mashtaka ni Julius Sarota (nishati na madini), Mwita Wagwe (TANESCO), Lutengano Mwakahesya (wakala wa nishati vijijini- REA) na James Mwalilimo (TANESCO).
Azimio Na 8 lililotaka serikali kuwajibisha viongozi wenye dhamana ya kisiasa na kuwachukulia hatua za kinidhamu, halikutendwa kama bunge lilivyoelekeza wala umma ulivyotaka.
Waliokuwa mawaziri wa Nishati na Madini, Dk. Ibrahim Msabaha na Nazir Karamagi, walijiuzulu hata kabla maazimio kutolewa.
Hadi leo hawajafikishwa mahakamani kwa kuisababishia serikali hasara kwa kuipa kazi kampuni isiyokuwa na sifa.
Badala yake, serikali imesema “haijaona jinai iliyotendwa na viongozi hao.” Inasisitiza kuwa vyombo vya dola vinaendelea na uchunguzi wake nje ya nchi.
Je, serikali inahitaji miongo mingapi kukamilisha kazi hii? Mbona Kamati Teule iliweza kukamilisha uchunguzi wake kwa wiki mbili kwa kwenda Marekani na kugundua kuwa Richmond ilikuwa kampuni ya mfukoni?
Je, serikali yenye vyombo vyote vya dola inashindwa nini kufanya hivyo? Kama uchunguzi unaendelea, kwanini Sitta amezimwa, kung’olewa meno na kulazimishwa kufunga mjadala?
Hata azimio Na. 10 halikutekelezwa. Katika azimio hili, bunge lilitaka serikali ichungunze uhalali wa malipo ya dola za Marekani 4,865,000 (karibu Sh. 6 bilioni) yaliyofanywa kwa Richmond/Dowans.
Kwanza serikali, kwa mara ya kwanza, imekiri kuwa kuna malipo yamefanywa kwa Dowans na dada yake Richmond. Mara kadhaa imekuwa ikisisitiza kuwa hakuna hata shilingi iliyotolewa kwa kampuni hiyo.
Pili, serikali imethibitisha kuwa hata gharama za usafirishaji wa mitambo ya kampuni binafsi, zilibebwa kwa fedha za umma.
Tatu, serikali imesema ukweli kwamba kiasi cha dola 30.9 milioni (Sh. 40 bilioni) zimechotwa kinyume cha taratibu kwa kuonyeshwa kuwa zilitumika kugharamia usafirishaji wa mitambo kwa njia ya meli, wakati mitambo imesafirishwa kwa ndege.
Katika kujitetea, serikali inasema madai hayo ya dola za 30.9 milioni yamejumuishwa katika hoja za TANESCO katika shauri lililofunguliwa na Richmond katika mahakama ya kimataifa nchini Ufaransa.
Je, hapa Sitta anapata wapi ujasiri wa kufunga mjadala wakati Bunge limechezewa na Richmond?
Inakuwaje serikali iliyosafirisha mitambo ya kampuni binafsi ifikishwe mahakamani kwa kudai mali yake na Sitta akubali kuziba wabunge midomo?
Jingine ambalo halikutekelezwa ni Azimio Na. 11 ambalo lilitaka serikali ifanyie marekebisho sheria ya maadili ya viongozi wa umma ya mwaka 1995.
Serikali imesema tayari kikundi kazi kimeandaliwa na muswada uko katika ngazi ya makatibu wakuu (IMTC).
Hata hapa haikusema muswada uko tayari mbele ya bunge; imesema “mipango ya kuuandaa imekamilika.” Ni miaka mitatu ya maendelezo ya ngonjera.
Kama hili nalo halijatekelezwa, nani anaweza kujitapa kwamba bunge limefanikiwa kuzima Richmond?
Azimio Na. 13 nalo limepigwa mweleka. Katika azimio hili, bunge lilitaka serikali kulihusisha katika maandalizi yote ya mikataba mikubwa ya kibiashara na hasa ile ya muda mrefu ili kuondokana na kile kilichoitwa “siri” katika mikataba.
Hata hivyo, serikali katika taarifa yake inasema itapeleka kila mkataba bungeni na kuuweka katika “maktaba maalum ya bunge.”
Kinachowekwa hapa ni mkataba, si rasimu ya mkataba. Je, nini faida ya bunge katika hili? Kule kujua kwamba kuna mkataba wa kinyonyaji, lakini ikiwa haina meno ya kubadilisha chochote?
Mbona hata mkataba kati ya serikali na kampuni ya reli ya India (RITES), iliyopewa kuendesha shirika la reli la taifa (TRC) unafahamika, na bunge limeshindwa kuchukua hatua?
Je, bunge lilitaka kuona mikataba inawekwa katika maktaba huku likiwa halina meno kuijadili, au ilitaka kushirikishwa katika hatua zote zikiwamo zile za maandalizi?
Kilichotakiwa na bunge, kwa manufaa ya taifa, ni kuona kila hatua ili hatimaye kuliepusha taifa na hasara inayotokana na mikataba ya kinyonyaji.
Serikali inafika mbali zaidi: Inasema imeunda “Timu ya wataalamu” walewale walioshiriki katika kuigamiza nchi, kujifunza katika mabunge mengine ya Jumuiya ya Madola katika hatua za awali za uandaaji wa mikataba.
Katika kuonyesha “ubutu wa bunge” Spika Sitta anakubali kuundwa kinachoitwa, Kamati ya Masuala ya Biashara itakayopitia mikataba “mikubwa ya kibiashara bila kuathiri taratibu za serikali na zile za mikataba husika.”
Je, bunge linaweza kujigamba kuwa azimio hilo limetekelezwa?
Azimio Na. 14 nalo limekufa kifo cha mende. Serikali ilitakiwa katika azimio hili, kuwajibisha wote waliohusika katika kupitisha mkataba wa Richmond.
Lakini aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa serikali, Johnson Mwanyika na katibu mkuu wa wizara ya nishati na madini, Arthur Mwakapugi wameachia ofisi za umma baada ya kufikisha umri wa kustaafu kwa mujibu wa sheria.
Taarifa zinasema tayari wamelipwa haki zao zote wanazostahili kazini na uwezekano wa kuwachukulia hatua hauonekani.
Hata aliyekuwa waziri mkuu, Edward Lowassa, bado anaendelea kupeta na kuchukuliwa kama mstaafu wakati yeye anajua vema kuwa hajawahi kustaafu wala kustahili mafao ya wastaafu.
Je, hapa napo Sitta anaweza kusema kuna kitu kimetekelezwa hadi kuapiza na kufunga mjadala?
Angalia Azimio Na. 15 ambalo halikuwa gumu kutekeleza; nalo serikali imegoma kulitekeleza.
Katika hili, serikali iliagizwa na bunge kuachana na utaratibu wa kuteua wakurugenzi na makamishina katika wizara kuwa wajumbe wa bodi za mashirika ya umma kwa kuwa kufanya hivyo ni kinyume cha misingi ya utawala bora.
Lakini taarifa ya serikali inasisitiza, “bado inaona utaratibu huu uendelee katika baadhi ya bodi ili kusaidia mipango ya serikali.”
Je, nani hapa anasema serikali imetekeleza yaliyoelekezwa na bunge?
Azimio Na. 18 liliagiza serikali kuchukulia hatua za kisheria wamiliki wa Richmond waliofanya udanganyifu na “ujanja wa kuibia serikali.” Hili nalo halikutekelezwa.
Mohammed Gire ambaye ameithibitishia Kamati Teule kuwa ni mmoja wa wabia katika Richmond, bado anapeta uraiani.
Naye Rostam Aziz, ambaye bunge limehusisha na Richmond, bado hajaguswa.
Aliyepelekwa mahakamani na kubebeshwa mzigo wa Richmond, si mmiliki halisi. Ni wakala aliyepewa kazi ya kutafuta waandishi wa habari na maofisa wa serikali kupoza machungu ya kukosekana kwa umeme.
Katika hili, serikali inasema imeunda kamati maalum ya uchunguzi kutafuta wamiliki wa kampuni ya Richmond; hivyo “kazi ya uchunguzi bado inaendelea.”
Je, hatua ya Sitta ya kufunga mjadala ina maanisha kuwa mmiliki wa Richmond ameshapatikana? Maazimio yameshatekelezwa?
Azimio Na. 20 lililosisitiza kuwapo kwa taarifa mbili za uchunguzi na hivyo kutaka Mkurugenzi wa TAKUKURU, Edward Hoseah awajibishwe; nalo limezimwa.
Serikali inasema, “vyombo vya dola vilivyofanya uchunguzi vimebaini kuwa hakukuwa na taarifa mbili za ripoti ya Ricmond.”
Sitta anajua kwamba wakati kinachoitwa uchunguzi kinafanyika, Hoseah hakutoka ofisini. Hivyo, haki haikutendeka.
Je, hatua ya Hoseah kubaki ofisini wakati uchunguzi unaendelea, haikutosha kughairisha ufungaji wa mjadala?
Kilichomfanya Sitta kufunga mjadala si kutekelezwa kwa maazimio ya bunge, bali ni vitisho vya chama chake. Ndani ya bunge, Sitta hakuwa Sitta wa awali.
Wiki moja kabla ya mkutano wa bunge, ni Sitta aliyekaripia Mathias Chikawe, waziri wa sheria na katiba aliyesema “Bunge halina mamlaka ya kusimamia serikali.”
Sitta alisema, tena kwa utulivu, “Chikawe azungumzie hayo bungeni.”
Lakini haikuchukua muda, serikali iliwasilisha taarifa yenye kurasa 30 kwa Kamati ya Nishati na Madini ikipinga bunge kuagiza serikali.
Serikali ilisema, “…Kwa mujibu wa Ibara ya 63 (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977 maagizo ya bunge ni ushauri kwa serikali na siyo maagizo.”
Kama bunge haliwezi kusimamia serikali, huku Sitta akikubali mjadala ufungwe, wako wapi wanaojitapa kwamba serikali imetekeleza maagizo ya bunge na hivyo bunge linahitaji kupongezwa?
Hakuna ubishi kwamba bunge limetishwa. Limezibwa mdomo. Sauti za wanaowakilishwa zitapitia wapi?
Mjadala huu utaendelea wiki ijayo: Nini kilisababisha Sitta kufunga mjadala kabla maji hayachemka?
Saed Kubenea, 03 March 2010


----
Chambi Chachage

Maelezo ya Serikali yaliyotolewa Bungeni kuhusu ripoti ya CAG ya BoT Tegeta Escrow Account

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Mhongo akizungumza, Bungeni mjini Dodoma Novemba 27, 2014.


MAELEZO YA SERIKALI KUHUSU TAARIFA YA UKAGUZI MAALUM KUHUSIANA NA MIAMALA ILIYOFANYIKA KATIKA AKAUNTI YA “ESCROW” YA TEGETA PAMOJA NA UMILIKI WA KAMPUNI YA IPTL


1.  Historia ya Mradi
Mheshimiwa SpikaKatika miaka ya tisini (1990s), Tanzania ilikuwa ikikabiliwa na tatizo la uhaba wa maji katika mabwawa ya kuzalisha umeme, hali iliyopelekea kuwepo kwa upungufu wa umeme na kuathiri shughuli za maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini. Ili kukabiliana na tatizo hilo, Serikali ilichukua hatua za dharura za kuanzisha mradi wa kufua umeme wenye uwezo wa kuzalisha Megawati (MW) 100.
2.  Upatikanaji wa IPTL
Mheshimiwa SpikaMwaka 1994 Serikali ilitoa kazi ya uwekezaji kwa Kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) iliyokuwa inamilikiwa na Kampuni za VIP Engineering and Marketing Ltd ya Tanzania iliyokuwa na Asilimia 30 na MECHMAR Corporation ya Malaysia(MECHMAR) iliyokuwa na Asilimia 70. Kampuni ya IPTL ilipewa leseni ya kujenga, kumiliki na kuendesha (Build-Own-Operate) Mtambo wenye uwezo wa kuzalisha umeme wa MW 100 kwa kutumia mafuta mazito eneo la Tegeta-Salasala, Dar es Salaam.
Katika Ukurasa wa 52 Aya ya 2 ya Taarifa ya PAC, Kamati imependekeza Mtambo huo utaifishwe.
Ufafanuzi:
Mheshimiwa Spika, Kulingana na Mkataba wa PPA kati ya TANESCO na IPTL, majukumu ya IPTL yalikuwa ni kujenga, kumiliki na kuendesha (Build, Own and Operate – BOO). Hivyo, kutaifisha Mtambo huo ni kukiuka makubaliano katika Mkataba wa PPA wa tarehe 26 Mei 1995, ukiukwaji wa aina hii ukitokea unaweza kuingiza Serikali katika mgogoro mkubwa ikiwa ni pamoja na kushtakiwa kwenye Mahakama za kibiashara za kimataifa. Aidha utaifishaji wa miradi ya uwekezaji binafsi itakuwa ni njia ya kufukuza wawekezaji binafsi.
Mheshimiwa SpikaTarehe 26 Mei, 1995, TANESCO na IPTL walisaini Mkataba wa PPA kwa muda wa miaka ishirini (20), kwa ajili ya kununua umeme utakaozalishwa na IPTL. Kwa mujibu wa Mkataba huo, IPTL ilitakiwa kuiuzia TANESCO umeme usiopungua Asilimia 85 ya uwezo wa Mtambo (minimum off take). Hata hivyo, uzalishaji wa umeme haukuanza mara moja kutokana na mgogoro uliotokea kati ya TANESCO na IPTL kuhusu gharama halisi za uwekezaji na namna ya kukokotoa Capacity Charges. Hivyo, IPTL ilianza kuzalisha umeme tarehe 15 Januari, 2002. Kutokana na hali hiyo muda wa miaka 20 ya Mkataba ulianza kuhesabiwa tarehe 15 Januari, 2002 baada ya kuanza uzalishaji (Commercial Operation Date).
Mheshimiwa SpikaPamoja na mambo mengine muhimu yaliyokuwemo katika PPA, Kifungu Na. 6 cha Mkataba huo kinaipa TANESCO wajibu wa kulipa malipo yaliyotajwa hapo juu na kwamba endapo kutakuwa na mgogoro wowote kuhusiana na malipo hayo (Disputed Amount), itafunguliwa Akaunti maalum (Escrow Account) ya kuhifadhi fedha hizo hadi pale pande mbili zitakapokubaliana juu ya uhalali wa malipo yanayobishaniwa. Aidha chini ya PPA, migogoro yote kuhusiana na masuala ya utekelezaji wa Mkataba huo ilitakiwa kuwasilishwa na kuamuliwa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji (ICSID) ya London. Hivyo, ilikuwa ni jukumu la kila mhusika katika Mkataba huu kuwasilisha malalamiko yake ICSID yanapotokea.
Katika Ukurasa wa 8 Aya ya 2 ya Taarifa ya PAC imeelezwa kuwa mwaka 2004 TANESCO ilifungua shauri la ICSID 2 kupinga kiasi kikubwa cha tozo ya Capacity Charge.
Ufafanuzi
Mheshimiwa SpikaTaarifa hiyo siyo kweli kwani TANESCO haijawahi kufungua shauri lolote ICSID ya London au Mahakama yo yote dhidi ya Standard Charterd Bank kupinga kiasi kikubwa cha Capacity Charge kama inavyoelezwa katika Taarifa ya PAC. Shauri la ICSID 2 lilifunguliwa tarehe 31 Oktoba 2010 na Standard Chatered Bank Hong Kong (SCBHK) kwa ajili ya kudai malipo ya deni ililonunua kutokana na mkopo uliotolewa na mabenki ya ushirika ya Malaysia kwa IPTL.  Wahusika katika Shauri hilo la ICSID 2 ni SCBHK na TANESCO na wala siyo TANESCO na IPTL.
Mheshimiwa Spika, Tarehe 12 Februari, 2014 ICSID ilitoa uamuzi kuhusiana na Shauri la SCBHK na TANESCO na kuwashauri wakae kukokotoa upya malipo ya Capacity Charge. Hata hivyo, ilikuwa vigumu kwa pande hizo kutekeleza uamuzi huo kutokana na pande hizo kutokuwa na Mkataba wa kibiashara baina yao. Vile vile, kupitia Shauri la Madai Na. 60/2014, lililofunguliwa Mahakama Kuu ya Tanzania na IPTL tarehe 4 Aprili, 2014 ilizuia utekelezaji wa maelekezo hayo.
3.  Mgogoro kati ya IPTL na TANESCO
Mheshimiwa SpikaMigogoro kati ya TANESCO na IPTL ilianza muda mfupi baada ya PPA kusainiwa tarehe 26 Mei 1995. IPTL waliitaka TANESCO wakubaliane bei za kununua umeme kwa kuzingatia gharama za uwekezaji. Pande hizo mbili zilishindwa kukubaliana gharama za Capacity Charge kwa vile TANESCO walidai kuwa gharama zilizoainishwa na IPTL ni kubwa kuliko gharama halisi za uwekezaji. Mwaka 1998, TANESCO iliajiri Kampuni ya Mawakili ya Mkono & Co Advocates kutoa huduma za kisheria kwa kushirikiana na Huntons & Williams ya Marekani. Kutokana na tofauti za gharama za Uwekezaji, Mawakili hawa waliishauri TANESCO ifungue Kesi ICSID nchini Uingereza dhidi ya IPTL ili kupinga gharama hizo.
Mheshimiwa SpikaKwa kuzingatia ushauri huo wa Mawakili, TANESCO ilifungua Kesi Na.ARB/98/8 ya mwezi Agosti, 1998 ikidai kuwa gharama halisi za uwekezaji ni Dola za Marekani milioni 90 na siyo milioni 163.53 kama ilivyodaiwa na IPTL. Aidha, IPTL ilidai kuwa kiwango cha marejesho ya uwekezaji (Internal Rate of Return-IRR) ni Asilimia 23.10 ambacho pia kilipingwa na TANESCO.
Mheshimiwa SpikaTarehe 12 Julai, 2001, ICSID ilitoa uamuzi wa Kesi hiyo pamoja na mambo mengine kwamba:-
i.     Gharama halisi za uwekezaji zikiwemo Mtambo na nyumba za wafanyakazi wa IPTL zilizoainishwa katika hesabu ya IPTL zilikuwa ni Dola za Marekani milioni 163.53 lakini ICSID iliona kuwa gharama halisi ni Dola za Marekani milioni 127.20;
ii.     Kiwango cha marejesho ya uwekezaji (Internal Rate of Return-IRR) ilikuwa Asilimia 22.31 badala ya Asilimia 23.10 iliyodaiwa na IPTL; na
iii.  TANESCO na IPTL wakubaliane mfumo wa malipo ya kununua umeme ukizingatia gharama halisi za uwekezaji na kiwango cha marejesho ya uwekezaji (IRR) cha Asilimia 22.31 kwa kutumia financial modeliliyokubalika na ICSID.
Katika Ukurasa wa 11 Aya ya 2 ya Taarifa ya PAC, imeelezwa kuwa mtaji wa uwekezaji katika Mtambo wa IPTL ni Shilingi 50,000/= na kwamba huo ndio ungetumika kukokotoa Capacity Charges ili kulipa tozo ndogo kuliko ilivyo sasa.
Ufafanuzi
Mheshimiwa Spika, Maelezo hayo siyo sahihi. Ukweli ni kwamba kutokana na maamuzi ya ICSID 1 ya tarehe 12 Julai, 2001, gharama za ujenzi wa Mtambo wa Tegeta ni Dola za Marekani 127.20 kama ilivyoelezwa katika Ukurasa wa 47Aya ya 4 ya Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali. Katika Taarifa hiyo, pia imeelezwa kuwa ilikubalika kuwa uwiano wa deni na mtaji utakuwa 70:30. Hii ikiwa na maana kwamba, deni ni Dola za Marekani milioni 89.04 na mtaji ni Dola za Marekani milioni 38.16. Uamuzi huo haujabadilishwa na Mahakama yo yote au mtu ye yote.
Mheshimiwa Spika, Tunakubaliana kwamba fedha iliyopokelewa kutoka Mabenki ya Ushirika ya Malaysia kama mkopo ni Dola za Marekani milioni 85.86 ambazo kati ya Dola za Marekani milioni 105 zilizokuwa zimeidhinishwa. Swali la kujiuliza, je Mtambo huo ulikamilikaje kwa gharama ya Dola za Marekani milioni 85.86, huku gharama halisi ya ujenzi wa Mtambo wa Tegeta ikawa Dola za Marekani milioni 127.20?
Mheshimiwa Spika, Ni dhahiri kwamba kuna matumizi ya zaidi ya Dola za Marekani milioni 38.16 ambazo pia zimetumika kwenye uwekezaji. Taarifa ya Kamati ya PAC haikuonesha fedha hiyo kuwa sehemu ya uwekezaji.
                                        
Mheshimiwa SpikaTarehe 30 Juni, 2004, Kampuni ya Mawakili iliyokuwa ikiiwakilisha TANESCO katika kesi ya kwanza ya usuluhishi, Kampuni ya Mkono & Co Advocates, iliishauri TANESCO iendelee kupinga kiwango cha malipo ya Capacity Charge kilichokuwa kimeafikiwa tarehe 12 Julai, 2001 na pande hizi mbili katika Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICSID) ya London. Hii ilikuwa ni miaka miwili tu baada ya usuluhishi uliochukua miaka minne kukamilika na Mtambo kuanza kuzalisha umeme tarehe 15 Januari, 2002.
Mheshimiwa SpikaHata hivyo, baada ya ushauri huu, Mawakili hawa (Mkono & Co. Advocates) hawakuishauri TANESCO ifungue kesi katika Mahakama za Tanzania wala katika Mahakama ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kimataifa (ICSID) ya London.
Mheshimiwa SpikaHadi kufikia tarehe 5 Septemba, 2013 wakati Mheshimiwa Jaji Utamwa anatoa hukumu yake juu ya mgogoro wa Wanahisa wa IPTL hapakuwepo na kesi yo yote kwenye Mahakama yo yote ya kupinga gharama za Capacity Charge kati ya TANESCO na IPTL, iwe katika Mahakama za ndani au za nje. Kwa kutokuwepo Msuluhishi (Broker) katika suala hili, madai yo yote ya TANESCO yanakuwa ni madai ya upande mmoja ambayo kisheria hayawezi kuchukuliwa kuwa ndiyo madai halisi.  Kwa sababu hiyo haikuwepoformula rasmi ya kuutatua mgogoro huozaidi ya majadiliano na maafikiano kati ya pande mbili (TANESCO na IPTL).
4.  Uuzaji wa Hisa za VIP
Mheshimiwa SpikaKutokana na VIP Engineering and Marketing Limited (VIP) kuona kuwa hainufaiki na ubia wake katika IPTL, ilikusudia kuuza Hisa zake kwa MECHMAR. Hata hivyo, MECHMAR haikuweza kununua Hisa hizo kwa sababu ilitaka thamani ya Hisa za VIP zitokane na ripoti ya ukaguzi ya mwaka (Audited Financial Report) na taratibu za kihasibu za kimataifa (International Accounting Rules), VIP haikukubaliana na utaratibu huo.
Mheshimiwa SpikaKutokana na kutokubaliana, MECHMAR iliishauri VIP ifungue Shauri la madai hayo kwenye Mahakama ya Usuluhishi ya Uingereza (LCIA) kulingana na Mkataba wa Wanahisa wa IPTL. Hata hivyo, VIP haikufungua Shauri katika Mahakama ya usuluhishi kama ilivyoshauriwa na MECHMAR badala yake tarehe 25 Februari, 2002 VIP ikafungua Shauri katika Mahakama Kuu ya Tanzania (Miscellaneous Civil Application No. 49/2002) ikiomba Kampuni ya IPTL ifilisiwe ikiwa ni mwezi mmoja tangu kuanza uzalishaji.
5.  Uamuzi kuhusu Ufilisi wa IPTL
Mheshimiwa SpikaShauri lililofunguliwa na VIP tarehe 25 Februari, 2002 liliendelea kuwa Mahakamani hadi ilipofika tarehe 16 Desemba, 2008. Mahakama Kuu ya Tanzania chini ya Jaji Oriyo, J ilitoa uamuzi wa kuiweka IPTL katika Ufilisi wa Muda (Provisional Liquidation) chini ya Kabidhi Wasii Mkuu (Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini - RITA). Mfilisi wa Muda alipewa majukumu maalum yafuatayo:
            i.      Kulinda mali zote za IPTL katika kipindi chote cha Ufilisi wa Muda; na
          ii.      Kufanya uchunguzi wa tuhuma zote zilizotolewa na VIP dhidi ya MECHMAR na kutoa ripoti za uchunguzi huo ili Mahakama iweze kutoa uamuzi.
Mheshimiwa SpikaTarehe 15 Julai, 2011, Mahakama Kuu ya Tanzania (Kaijage, J) ilitoa uamuzi kwamba, IPTL iwekwe kwenye Ufilisi Kamili (Full Liquidation) na RITA ilithibitishwa kuwa Mfilisi wa IPTL.
Mheshimiwa SpikaKutokana na uamuzi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Standard Chartered Bank Hong Kong (SCBHK) iliyokuwa imenunua deni la IPTL kutoka kwa DANHARTA, ilipinga na kuiomba Mahakama ya Rufaa ifanye mapitio ya uamuzi wa Mahakama Kuu (Application for Revision – Civil Revision No. 1/2012) ikiainisha dosari katika uamuzi wa Mahakama Kuu ulioamuru kufilisiwa kwa IPTL. SCBHK ilibainisha dosari za maombi ya kutaka IPTL kufilisiwa kwa kuwa maombi ya SCBHK ya kutaka Mahakama iteue msimamizi (Administrator) wa kuisimamia IPTL (kwa niaba ya SCBHK) yalikuwa hayajasikilizwa.
Mheshimiwa SpikaMahakama ya Rufaa ya Tanzania ilikubaliana na hoja za SCBHK na hivyo kuamuru shauri hilo lirejeshwe Mahakama Kuu ili IPTL irudi mikononi mwa Mfilisi wa Muda (Provisional Liquidator) ambaye alipewa majukumu yafuatayo:-
                      i.        Kukusanya mali na madeni yote ya IPTL;
                    ii.        Kupokea na kusajili madeni yote dhidi ya IPTL;
                  iii.        Kusuluhisha migogoro kati ya wanahisa wa IPTL; na
                   iv.        Kusimamia na kuendesha Mtambo wa kuzalisha umeme wa IPTL kwa niaba ya IPTL.
Mheshimiwa SpikaBaada ya kuteuliwa, Mfilisi wa Muda (Provisional Liquidator) alifanya juhudi ya kumaliza mgogoro huo wa IPTL nje ya Mahakama kwa kushirikisha wadau mbalimbali (Stakeholders) wa IPTL kupitia kikao chake cha tarehe 9 Novemba, 2011. (Kiambatisho Na.1). Juhudi hizo hazikufanikiwa na ikalazimu shauri liendelee Mahakamani.
6.  Uhalali wa uhamishwaji wa Asilimia 70 za
   Hisa za MECHMAR kwenda PAP
Mheshimiwa SpikaSuala la uhalali wa umiliki wa Hisa katika Kampuni hizi linahusu wanahisa wa Kampuni wenyewe. Serikali haiwajibiki kuingilia mahusiano ya kibiashara ya wanahisa katikaKampuni Binafsi. Hata hivyo, kulingana na Sheria za nchi ikiwa ni pamoja na Kifungu cha 172 cha Sheria ya Makampuni (Sura 212), mauziano ya Hisa yaliyofanyika nje ya nchi yatatambuliwa tu, endapo usajili wa Hisa hizo utafanyika hapa nchini. Kwa mujibu wa taarifa za BRELA za tarehe 31 Desemba, 2013, zinaonesha kuwa uhamishaji wa Hisa 7 za MECHMAR katika IPTL kwenda PAP ulisajiliwa hapa nchini. Kwa maana hiyo, PAP ni mmiliki wa Asilimia 70 za IPTL.
Katika ukurasa wa 44 Aya ya 1 ya Taarifa ya PAC imeelezwa kuwa PAP siyo mmiliki halali wa Hisa 7 za MECHMAR katika IPTL.
Ufafanuzi
Mheshimiwa Spika, Katika maelezo ya Kamati ukurasa wa 30, Kamati imethibitisha kwamba nyaraka za mauziano kati ya MECHMAR na Piper Link zilipokelewa na Harbinder Singh Sethi ambaye pia ndiye mmiliki wa PAP. Kwa uthibitisho huo, Kamati inakubali kuwa Hisa za MECHMAR katika IPTL zinamilikiwa na PAP. 
Katika Ukurasa wa 25 Aya ya 2 ya Taarifa ya PAC imeelezwa kuwa hakuna ushahidi wa PAP kumiliki Asilimia 70 ya Hisa zilizokuwa zikimilikiwa na MECHMAR katika IPTL.
Ufafanuzi
Mheshimiwa Spika, Napenda kulijulisha Bunge lako Tukufu kuwa umiliki wa Hisa 7 za IPTL unatambuliwa hata na SCBHK ambayo ilisaini makubaliano tarehe 25 Novemba 2011 na PAP ya kulipwa deni la mkopo wa fedha za kununua deni la ujenzi wa Mtambo wa Tegeta. Kiambatisho Na 2.
7.  Majadiliano ya mikopo ya IPTL na Wadai
Mheshimiwa SpikaKutokana na Hukumu ya Mahakama Kuu ya Tanzania iliyotolewa tarehe 5 Septemba 2013, Kampuni ya PAP ilijadiliana na wadai halali wa mikopo ya IPTL na kuingia Mkataba wa kuwalipa wadai wote wa IPTL. SCBHK inayodai kuidai IPTL mikopo katika ujenzi wa Mtambo wa Tegeta haikuwasilisha madai ya aina yo yote ili iweze kulipwa.
Mheshimiwa SpikaUkweli ni kwamba, SCBHK iliyokuwa ikiidai IPTL fedha ilizotumia kununua deni lililotokana na kufilisiwa kwa MECHMAR kule Malaysia (siyo Tanzania) haijawahi kujadiliana na IPTL kuhusu malipo ya mkopo wake kama upo. Mvutano huu unaendelea ICSID kati ya TANESCO na SCBHK, ukiitaka TANESCO ilipe gharama za kununua umeme ikijumuisha deni la IPTL. Madai ya SCBHK dhidi ya TANESCO yanatokana na madai ya kuwepo kwa Deed of Assignment ya MECHMAR kuhusiana na Mkopo wa IPTL ambapo Mtambo wa IPTL uliwekwa kama dhamana ya Mkopo.
Mheshimiwa SpikaHata hivyo Deedof Assignment hiyo haikuwahi kusajiliwa hapa nchini kama inavyotakiwa katika Kifungu Na. 172 cha Sheria za Makampuni Sura. 212 zinavyoelekeza. Kutokana na kutokusajili Assignment DeedhiyoSCBHK ilikosa sifa za kufungua madai yake hapa nchini badala yake ilifungua madai haya ICSID nchini Uingereza. Kitendo hicho kinaonesha kudharau Mahakama zetu na PAC inataka tuziamini Mahakama za nje kuliko za kwetu.
8.  Jitihada za Makampuni mbali mbali kununua Hisa za VIP
Mheshimiwa SpikaKutokana na tofauti zilizokuwepo kati ya MECHMAR na VIP kuanzia mwanzo wa mradi, VIP iliamua kuuza Hisa zake zilizoko IPTL kwa makampuni mbalimbali kwa nyakati tofauti ikiwemo MECHMAR kama mwanahisa mwenzake,  NSSF, Camel Oil, Great White Shark Opportunity Fund pamoja na SYMBION lakini haikuwezekana kutokana na kutoafikiana katika bei.
Mheshimiwa SpikaBaadaye VIP chini ya usuluhishi ya RITA, iliuza Hisa zake kwa PAP kwa thamani ya Dola za Marekani milioni sabini na tano (US$ 75,000,000/=). Ununuzi wa Hisa Asilimia 30 za VIP uliofanywa na PAP ndiyo uliyomaliza mgogoro wa Wanahisa uliyokuwa Mahakamani na kuufanya Mtambo wa IPTL kumilikiwa na PAP kwa kuwa ndiyo iliyomiliki Hisa zote Asilimia 100 za IPTL.
Taarifa ya PAC: Katika ukurasa wa 58 wa Taarifa ya PAC imeelezwa kuwa Waziri wa Nishati na Madini ndiye aliyekuwa Dalali Mkuu aliyewakutanisha Bw Harbinder Sethi na Bw James Rugemalira
Ufafanuzi
Mheshimiwa Spika, Taarifa hii siyo sahihi kwa kuwa tangu tarehe 9 Novemba, 2011, RITA aliitisha mkutano na kuwakutanisha wadau wote wa IPTL. Wakati huo, Waziri wa Nishati na Madini aliyeko sasa alikuwa bado hajateuliwa kwenye wadhifa huo.
9.  Kufungua ESCROW Akaunti
Mheshimiwa SpikaTarehe 30 Juni 2004, TANESCO kwa ushauri wa Mkono & Co Advocates walitoa hoja kuwa gharama za kununua umeme zilikokotolewa kwa kutumia IRR ya Asilimia 23.10 na makadirio ya gharama za mtaji wa Asilimia 30 ambao ni Dola za Marekani milioni 38.16, wakati mtaji halisi (equity) wa IPTL ni chini ya Dola za Marekani 100. Hivyo, TANESCO walikuwa wakitoa notisi (Dispute Notice) kwa kila Ankara ya malipo kupinga gharama hiyo kulingana na Kifungu Na. 6.8 cha Mkataba wa PPA. Kifungu hicho kinaeleza kuwa ikiwa upande wote haukubaliani na usahihi wa malipo katika Ankara zilizowasilishwa kwa ajili ya malipo ya gharama za umeme wanatakiwa watoe notisi (Invoice Dispute Notice) kwa upande mwingine. Vile vile, Mawakili wa TANESCO (Mkono & Co Advocates) walishauri kwamba kutokana na pingamizi hilo, ifunguliwe Akaunti Maalum(Escrow Account) kwa ajili ya kuhifadhi fedha ambazo zilitokana na Ankara zilizokuwa zinapingwa.
Mheshimiwa SpikaKutokana na ushauri wa Mkono Co. & Advocates tarehe 5 Julai, 2006, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ilisaini Mkataba wa kufungua Akaunti Maalum (Escrow Account) kwa ajili ya kuweka fedha zote za Ankara zilizopaswa kulipwa kwa IPTL. 
10.    Mmiliki wa Fedha za Akaunti ya Escrow:
Mheshimiwa Spika, Katika Taarifa ya Kamati ya PAC ukurasa wa 22 imeelezwa kuwa Akaunti ya Escrow ilipaswa kuwa na Shilingi bilioni 306.70 ambazo zingekuwa zimewekwa na TANESCO. Hata hivyo, katika mapendekezo ya Kamati ya PAC ukurasa wa 50, Kamati imeeleza kwamba imethibitisha bila chembe ya mashaka kwamba mchakato mzima wa kutoa fedha katika Akaunti ya Escrow umegubikwa na mchezo mchafu na kwamba Mfumo mzima wa Serikali ulipata ganzi ili kuwezesha zaidi ya Shilingi bilioni 306kuporwa kutoka Benki Kuu ya Tanzania na kutakatishwa kupitia benki mbili hapa nchini.
11.                  Tahadhari iliyochukuliwa na Serikali
        wakati wa kutoa fedha kwenye akaunti ya  
        Escrow
Mheshimiwa Spika, Kwa kuelewa kwamba kunaweza kukatokea madai kwa IPTL, na kwa kuwa Serikali ilitoa dhamana kwa TANESCO ya kununua umeme wa IPTL, Serikali ilihakikisha inachukua KINGA (Indemnity) kutoka IPTL katika maeneo yote muhimu. Kwa mujibu wa KINGA hiyo, kama kutajitokeza madai yo yote yale, IPTL yenyewe itawajibika. Ikumbukwe kuwa kabla ya kusaini, KINGA hiyo ilipitiwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali na kuthibitisha kwamba inakidhi matakwa ya kulinda maslahi ya Taifa. KINGA hii ilitolewa tarehe 27 Oktoba, 2013. Inasema, nanukuu:
“IPTL do hereby agree to INDEMNIFY and keep INDEMNIFIED the Government and the Escrow Agent (jointly and severally) against all presentand future claims, actions and legal proceedings that may arise in respect of and/or all losses, charges, costs, and expenses the Government and the Escrow Agent may suffer or incur consequent upon the release and payment of the funds in the Tegeta Escrow Account or part thereof to IPTL pursuant to the Agreement for Delivery of Funds”.
Katika Ukurasa wa 48 wa Taarifa ya PAC, imeelezwa kuwa Serikali haikuchukua tahadhari ya kutosha dhidi ya madai mengine yanayoweza kujitokeza kabla ya kutolewa kwa fedha kutoka akaunti ya Escrow.
Ufafanuzi
Mheshimiwa Spika, KINGA iliyochukuliwa inakidhi matakwa ya kisheria na imezingatia athari yo yote ambayo ingeweza kutokea baadaye kutokana na kutolewa kwa fedha katika Akaunti ya Escrow. Kwa hiyo siyo kweli kwamba Serikali haikuchukua tahadhari kama ilivyodaiwa na PAC.
12.    Dhana ya Madai ya Shilingi Bilioni 321
Mheshimiwa Spika, Madai ya kwamba TANESCO inaidai IPTL Shilingi bilioni 321 msingi wake ni dhana kwamba mtaji wa IPTL ni Dola za Marekani 100, sawa na Shilingi za Tanzania 50,000/- kwa wakati huo.Dhana hii ilipuuza ukweli kwamba Dola za Marekani milion 38.16 ziliwekezwa kwenye mradi wa Tegeta. Aidha, Bodi ya TANESCO imekana kuyatambua madai hayo ya Shilingi bilioni 321Kimsingi hata Vitabu vya Hesabu vya TANESCO ambavyo vimekuwa vikikaguliwa na CAG, havioneshi kuwepo kwa deni hilo.
Mheshimiwa SpikaMadai ya Shilingi bilioni 321 yaliyowasilishwa kwa Mfilisi na Mwanasheria wa TANESCO (Mkono & Co. Advocates) ulihitaji kuhakikiwa kabla ya kukubaliwa na Mfilisi kama madai halali. Hata hivyo, uhakiki huo haukufanyika kwa sababu ya Hukumu ya Mahakama ya Rufaa katika Civil Revision No. 1 ya Mwaka 2012, ambayo ilifuta maamuzi ya Mahakama Kuu ya kuiweka IPTL katika Ufilisi na kuirudisha kwenye Ufilisi wa Muda. Hivyo, madai hayo ya Shilingi bilioni 321 na kiapo chake ambacho hakitambuliwi na Bodi ya TANESCO hayakuwa tena na uhalali wo wote.
Kamati ya PAC: Katika ukurasa wa 47 Aya ya 2 Kamati imejiridhisha kuwa madai ya TANESCO ya Shilingi Billioni 321 yana uhalali japo usahihi wake utapatikana baada ya kutekelezwa kwa uamuzi wa ICSID 2 na TANESCO na IPTL kukubaliana kiwango sahihi cha Capacity Charge.
Ufafanuzi
Mheshimiwa Spika, Madai ya kwamba TANESCO inaidai IPTL Shilingi bilioni 321 msingi wake ni dhana kwamba mtaji wa IPTL ni Dola za Marekani 100, sawa na Shilingi za Tanzania 50,000/- kwa wakati huo. Dhana hii ilipuuza ukweli kwamba Dola za Marekani milion 38.16 ziliwekezwa kwenye mradi wa Tegeta. Aidha, Bodi ya TANESCO imekana kuyatambua madai hayo ya Shilingi bilioni 321Kimsingi hata Vitabu vya Hesabu vya TANESCO ambavyo vimekuwa vikikaguliwa na CAG, havioneshi kuwepo kwa deni hilo.
13.      TANESCO na IPTL kufanya Reconcillation ya fedha iliyokuwa kwenye Akaunti ya Escrow
Mheshimiwa SpikaTANESCO kwa kushirikiana na IPTL ilifanya uhakiki (reconciliation)tarehe 9 Oktoba, 2013 ili kujua madai halali ya IPTL kabla ya kufanya malipo. Takwimu za Mfilisi wa Muda wa IPTL (RITA) wakati akikabidhi mali na madeni ya IPTL, ilionesha kwamba deni lote alilokuwa akidaiwa TANESCO na IPTL kamaCapacity Charges ni Shilingi bilioni 370.70, sawa na Dola za Marekani milioni 224.30. Katika majadiliano kati ya TANESCO na IPTL, gharama zilizokubaliwa kama Capacity Charges zilizokuwa zinadaiwa ni Shilingi bilioni 275.20. Fedha hizi ni pungufu kwa Shilingi bilioni 95.50 ya madai ya IPTL. Hadi kufikia tarehe 25 Novemba 2013, fedha iliyokuwa katika Akaunti ya Escrow ilikuwa jumla ya Dola za Marekani milioni 22.20, sawa naShilingi bilioni 36.72 na Shilingi bilioni 161.39.
Mheshimiwa Spika, Ukaguzi maalum umeonesha pia kuwa fedha zilizokuwa kwenye Akaunti ya Escrow wakati wa kuifunga ni Shilingi bilioni 182.77 na kuwa na upungufu wa Shilingi bilioni 123.90 wa madai ya IPTL.
14.      Iwapo Serikali ilistahili kutoa fedha katika Akaunti ya Escrow wakati Shauri la ICSID, London inaendelea
Mheshimiwa SpikaKesi iliyopo ICSID, London ilihusu madai ya Benki ya Standard Chatered ya Hong Kong yaliyotokana na kununua deni lililotokana na uwekezaji katika Mtambo wa IPTL wa Tegeta. Katika Mkopo huo, Mkataba wa kuuziana umeme (PPA) na Mtambo wa kuzalisha umeme wa Tegeta viliwekwa kama dhamana.
Mheshimiwa SpikaTANESCO haikuhusishwa kwenye majadiliano ya dhamana hiyo. IPTL ilishindwa kumaliza marejesho ya Mkopo huo na hivyo Benki ya Standard Chartered ya Hong Kong kuanza kuidai TANESCO madeni yaliyotokana na Mkopo huo. Hata hivyo, fedha katika Akaunti ya Escrow ilitokana na Ankara za Capacity Charges zilizokuwa zikibishaniwa kati ya TANESCO na IPTL kuhusu viwango vilivyotumikakukokotoa malipo hayo na siyo mikopo ya IPTL.
Mheshimiwa SpikaHata hivyo, Standard Chartered Bank Hong Kong siyo mhusika (not a party)katika Mkataba wa tarehe 26 Mei, 1995 wa PPA kati ya TANESCO na IPTL. Kwa mujibu wa Sheria za Tanzania, madai yo yote yaliyotokea nje ya nchi yakihusu uwekezaji ulioko nchini ni lazima yasajiliwe hapa nchini.
Mheshimiwa SpikaKwa mantiki hiyo, Shauri lililoko ICSID, London halihusiani na fedha za Akaunti ya Escrow bali mikopo ya IPTL. Hata hivyo, wadai wa IPTL waliamriwa na Mahakama Kuu ya Tanzania tarehe 5 Septemba, 2013 kuwasilisha madai yao kwa PAP. Benki ya Standard Chatered ya Hong Kong haijafanya hivyo.
15.    Ulipwaji wa Madai na Madeni
Mheshimiwa SpikaKuhusu madai na madeni dhidi ya IPTL ikiwemo VAT, Serikali na BOT ziliitaka IPTL iweke KINGA (Indemnity)ili kuihakikishia Serikali kuwa endapo kutakuwa na madai au madeni ya aina yo yote, IPTL itawajibika kuyalipa. Tarehe 27 Oktoba, 2013, IPTL ilitoa KINGA hiyo, nanukuu:
“IPTL do hereby agree to INDEMNIFY and keep INDEMNIFIED the Government and the Escrow Agent (jointly and severally) against all present and future claims, actions and legal proceedings that may arise in respect of and/or all losses, charges, costs, and expenses the Government and the Escrow Agent may suffer or incur consequent upon the release and payment of the funds in the Tegeta Escrow Account or part thereof to IPTL pursuant to the Agreement for Delivery of Funds”.
16.        Gharama za Mawakili (Mkono & Co. Advocates na Hunton & Williams ya Marekani) Katika Kuendesha Kesi za IPTL
Mheshimiwa SpikaHadi Hukumu ya Mheshimiwa Jaji Utamwa inatolewa tarehe 5 Septemba mwaka 2013, TANESCO na Serikali zilikuwa zimewalipa Mawakili (Mkono & Co. Advocates na Hunton & Williams) jumla yaShilingi za Tanzania bilioni 62.90 na bado Mawakili hawa (Mkono & Co. Advocates na Hunton & Williams) wanaidai TANESCO Dola za Marekani milioni 4.50. Katika ushauri wao walikuwa wamependekeza kwa Serikali wapewe kazi nyingine ya kwenda kutetea Guarantee ya Serikali pamoja na kupingaHukumu ya tarehe 12 Februari, 2014 iliyotolewa katika uamuzi wa ICSID-2. Ushauri wao upo katika Memorandum yatarehe 9 Oktoba, 2013 waliyowasilisha TANESCO.
Mheshimiwa Spika,Wakati ambapo hatukujua ni kiasi gani Serikali na TANESCO ingeweza kupata kwa kuendelea kupinga Capacity Charges za IPTL, tunajua fika ni hasara gani tumepatakupitia malipo ya Mawakili (Mkono & Co. Advocates na Hunton & Williams) yaani ya Shilingi bilioni 62.9 na bado wanadai Dola za Marekani milioni 4.5.
Mheshimiwa Spikakumalizika kwa mgogoro huu wa IPTL si tu kwamba kumetuondoa kwenye hatari ya kuendelea kukamuliwa na Mawakili (Mkono & Co. Advocates na Hunton & Williams) hawa bali pia katika mazungumzo yaliyofanywa kati ya TANESCO na IPTL tumeweza kuokoa takribani Shilingi bilioni 95 katika madai ya awali ya IPTL.
17.      Ushauri wa Mawakili (Mkono & Co. Advocates na Hunton & Williams) wa TANESCO wa Tarehe 4 Oktoba, 2012
Mheshimiwa Spika, Mawakili wa TANESCO na Serikali yaani Kampuni za Mkono & Co Advocates na Hunton & Williams waliandika ushauri wa pamoja wa tarehe 4 Oktoba 2012 ambapowalifafanua kwa kina juu ya Shauri lililokuwa likiendelea katika Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICSID) ya London. Katika Ushauri wao walionyesha wazi kwamba TANESCO ilikuwa na nafasi finyu mno ya kushinda katika Kesi iliyokuwa ikiendelea kati ya TANESCO na SCBHK.
Mheshimiwa Spika, Katika ushauri wao walieleza mambo muhimu ambayo ni vema Bunge lako Tukufu likAyaelewa hasa kwa ajili ya watu wanaodhani kwamba ilikuwa ni makosa kwa TANESCO kukaa na IPTL baada ya Hukumu ya Mahakama Kuu ya tarehe 5 Septemba, 2013. Baadhi ya maeneo walioshauri TANESCO ikae na IPTL kujadiliana kwa kile kilichoelezwa na Mawakili (Mkono & Co. Advocates na Hunton & Williams) kuwa uwezekano wa kushinda kesi ni mdogo ni pamoja na:-
18.    Ushauri wa Mawakili Unaokinzana
Mheshimiwa Spika, Tarehe 4 Oktoba, 2012, Mawakili wetu (Mkono & Co. Advocates na Hunton & Williams) walitoa ushauri kwamba, kwa kuzingatia utetezi walioutoa kwa TANESCO kwenye kesi hii kule ICSID, London kiasi cha chini kabisa kinachoweza kuidhinishwa na Mahakama ya ICSID, London kama malipo ya Capacity Charges kwa IPTL ni kati ya Dola za Marekani milioni 85 hadi 90 na Mawakili wetu (Mkono & Co. Advocates na Hunton & Williams)  wakasema, nanukuu, This could be considered TANESCO’s  Best Case Scenario. Hata hivyo waliendelea kusema “This best Case Scenario is overly optimistic”.
Mheshimiwa Spika,Katika maelezo yao mengine ya tarehe 4 Oktoba 2012, Mawakili hawa (Mkono & Co. Advocates na Hunton & Williams) wanasema, “In these circumstances, SCBHK may recover 100% of itsclaimeddamages of USD 130 milion even if substantially TANESCO prevails on a portion of its equity defense”.
Kwa lugha nyingine Mheshimiwa Spika, Mawakili hawa (Mkono & Co. Advocates na Hunton & Williams) wanasema kiasi cha chini kabisa ambacho TANESCO ingedaiwa na SCBHK kingekuwaDola za Marekani milioni 130 bila kujumuisha gharama nyingine za moja kwa moja kwa IPTL.
Mheshimiwa SpikaKatika majumuisho yao ya tarehe 4 Oktoba, 2012, Mawakili (Mkono & Co. Advocates na Hunton & Williams) waliishauri TANESCO ikae na SCBHK na kukubaliana nje ya Mahakama na kumlipa Dola za Marekani kati ya milioni 75 na milioni 90 na kiasi kitakachobaki kikidaiwa kilipwekwa wadai wengine, wakiwemo IPTL, Law Associates na Kampuni ya Mafuta ya TOTAL.
Mheshimiwa Spika, Kufikia tarehe 5 Septemba, 2013 kwa mujibu wa Taarifa ya Mfilisi (RITA), ilionesha kuwa Kampuni ya IPTL ilikuwaikiidai TANESCO zaidi ya Dola za Marekani milioni 224.30, sawa naShilingi bilioni 370.70. Majadiliano yaliyofanyika kati ya TANESCO na IPTL tarehe 9 Oktoba, 2013 yaliwezesha kukubaliana kuwa malipo stahiki kwa IPTL ni jumla ya Dola za Marekani milioni 166, sawa na Shilingi bilioni 274.56. Kati ya hizo, Dola za Marekani milioni 121, sawa na Shilingi bilioni 220.13 zilikuwa kwenye Akaunti ya ESCROW na Dola za Marekani milioni 45, sawa na Shilingi bilioni 74.43 zitalipwa kwa kipindi cha muda mrefu usiozidi miaka mitano.
19.    Kama fedha zilizokuwa kwenye Akaunti ya Escrow ni za Umma
Katika ukurasa wa 58 wa Taarifa ya PAC imeelezwa kuwa fedha zilizokuwa katika Akaunti ya Escrow zilikuwa za Serikali.
Ufafanuzi:
Mheshimiwa Spika, Huu si ukweli zipo sababu kuu zinazothibitisha kuwa fedha hizo hazikuwa za Serikali.
1.  TANESCO ilikuwa inapata huduma ya umeme bila kulipa moja kwa moja IPTL, lakini ikawa inapeleka fedha hizo katika Akaunti ya Escrow.
2.  TANESCO ilisimamisha kupeleka malipo kwenye Akaunti ya Escrow na wala kulipa IPTL kuanzia tarehe 30 Oktoba, 2010.
Pamoja na kutokulipa, TANESCO iliendelea kupata huduma ya umeme kwa kadri ilivyohitaji kutoka IPTL.
Mheshimiwa Spika, Katika Ukurasa wa 36 hadi 42 wa Taarifa ya Ukaguzi Maalum ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ambayo tumekabidhiwa inaonesha kiasi ambacho TANESCO inadaiwa na IPTL.
Mheshimiwa Spika, Kulingana na Taarifa hiyo ukurasa wa 36 hadi42 imeonesha kuwa kiasi ambacho kilipaswa kuwekwa kwenye Escrow Account kwa mujibu wa Ankara za IPTL ni Shilingi bilioni 306.68. hata hivyo, kwa mujibu wa Ukaguzi huo fedha zilizokuwa kwenye Akaunti wakati wa kuifunga ni Shilingi bilioni 182.77 na kuwa na  upungufu wa Shilingi bilioni 123.90 ikiwa ni deni ambalo TANESCO bado wanadaiwa na IPTL.
Mheshimiwa Spika, Kwa msingi huo fedha zote zilizokuwa kwenye Akaunti ya Escrow ni mali ya IPTL na IPTL kama Wakala wa Kodi anastahili kudaiwa na mwisho kulipa kodi yo yote ambayo hajalipa.
Kwa msingi huo, Taarifa ya PAC haisemi ukweli kuhusu fedha zilizowekwa katika Akaunti ya Escrow kuwa ni fedha za umma.
Mheshimiwa spika, Ili kuthibitisha kwamba fedha hizi siyo za Umma, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) katika ukaguzi wake wa Hesabu za TANESCO wa tarehe 31 Desemba 2012, alielekeza kutoa fedha za Escrow kwenye Vitabu vya Hesabu vya TANESCO na kupunguza deni kwa kiasi hicho hicho kwa maelezo yafuatayo:
“As a result, the deposit balance in Escrow account does not meets the definition of an asset of the Company and therefore an adjustment has been made to de-recognize the asset and related liability to the tune of the amounts available in the Escrow account”.
20.    Iwapo kwa mujibu wa Mkataba wa PPA TANESCO na IPTL walilazimika kutumia Mtaalamu wa Upatanishi (Mediation Expert) katika utatuzi wa mgogoro kabla ya kutolewa fedha zilizopo kwenye Akaunti ya Escrow.
Mheshimiwa Spika, Taarifa ya Kamati ya PAC ukurasa wa 9, imeeleza kuwa kwa mujibu wa Mkataba wa PPA, TANESCO na IPTL walipaswa kutumia Mtaalam wa Upatanishi katika mgogoro wa Capacity Charge.
Mheshimiwa Spika, Tunapenda kulijulisha Bunge lako Tukufu kuwa kwa mujibu wa Ibara ya 18.1 ya Mkataba wa PPA, wahusika wa Mkataba huo ambao ni TANESCO na IPTL wanatakiwa kwanza kumaliza mgogoro baina yao kwa njia ya upatanishi (amicable settlement). Iwapo watashindwa kufikia makubaliano ndipo watalazimika kutumia Mtaalam wa Upatanishi kutatua mgogoro huo. TANESCO na IPTL walimaliza mgogoro baina yao kwa njia upatanishi kwa kufanya uhakiki wa kiasi ambacho kila upande ulikuwa unastahili kulipwa katika Akaunti ya ESCROW kabla ya akaunti hiyo kufungwa. Kwa msingi huo, hapakuwa na sababu ya kutumia Mtaalam wa Usuluhishi kama ilivyoelezwa katika Taarifa ya PAC.
21.    Kama muda wote wa Mkataba wa TANESCO na IPTL
hapakuwahi kuwa na Kamati ya Uendeshaji
Mheshimiwa Spika, Taarifa ya PAC inaeleza kuwa hapakuwahi kuwa na Kamati ya Uendeshaji kwa kipindi chote cha Mkataba wa PPA. Ukweli ni kwamba, Kamati ya Uendeshaji iliundwa kabla ya kuanza uzalishaji wa Mtambo hapo 2002 na imeendelea kuwepo hadi leo. Kamati hiyo ina wajumbe  sita. Wajumbe watatu kati ya hao wanatoka TANESCO. Wajumbe watatu waliobakia wanatoka IPTL. Wajumbe wa TANESCO walikuwa ni kama ifuatavyo:
1.  Mhandisi Masanyiwa Malale;
2.  Mhandisi Christian Msyani; na
3.  Mhandisi James Mtei.
Mheshimiwa Spika, Kwa msingi huo si kweli kwamba Kamati ya Uendeshaji haikuundwa kama ilivyoelezwa na Kamati ya PAC katika ukurasa wa 10.
22.    Wizara kutambua Hati za Hisa za Makampuni
Mheshimiwa Spika, Katika ukurasa wa 27 wa Taarifa ya Kamati ya PAC, Kamati hiyo imeitaka Wizara ya Nishati na Madini kutambua usajili wa Hati za Hisa za Makampuni. Tunaomba ieleweke kuwa siyo majukumu ya Wizara kutambua na wala kujishughulisha na Hati za Hisa za Makampuni Binafsi. Aidha, katika ukurasa wa 45, imeelezwa kwamba “Waziri wa Nishati na Madini ndiyo Mamlaka ya kuthibitisha uhamishaji wa umiliki wa Kampuni katika sekta yake”. Ningependa kulijulisha Bunge lako Tukufu kwamba jukumu hilo pia siyo la Wizara ya Nishati na Madini ni vizuri majukumu ya Wizara yakaangaliwa vizuri na kutoleta mkanganyiko na kuwadanganya wananchi wetu. Hii inaonesha kuwa kamati haikupitia vizuri majukumu ya Wizara.
Mheshimiwa Spika, Katika Taarifa ya PAC, ukurasa wa 30 Aya ya 2, imeelezwa nanukuu “nilishuhudia nyaraka kwamba Piper Link ilinunua Hisa za MECHMAR na katika mauziano hayo Kampuni hiyo iliwakilishwa na Bw. Harbinder Singh Sethi hivyo huyu bwana ndiye Piper Link na ndiye PAP”. Kwa maneno haya ya Kamati ya PAC, aliyekuwa na hati za Piper Link ni Bw. Sethi na aliyenunua Piper Link ni Bw. Sethi anayemiliki PAP. Kwa kuzingatia maelezo haya ya kamati ya PAC, inaonesha kwamba hakuna tatizo la uhamishaji wa Hisa Asilimia 70 kwenda kwa PAP.
Mheshimiwa Spika, Pamoja na maelezo ya Aya iliyotangulia, bado Kamati ya PAC ukurasa 44 wa taarifa yake, inaonesha kuwa Hisa hizo zinashikiwa na Martha Renju huko BVI lakini Martha Renju amefungua kesi mara mbili Mahakama Kuu ya Tanzania kwa kutumiwa na SCBHK akiwa na lengo la kutaka kujipatia fedha za Escrow bila uhalali. Hata hivyo, amekuwa akiziondoa kesi hizo mahakamani.
23.    Mikutano ya Bodi ya Wakurugenzi wa
  TANESCO
Mheshimiwa Spika,Katika ukurasa wa 29 wa Taarifa ya PAC, inasema kuwa Bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO ilifanya mikutano miwili mfulilizo kati ya tarehe 16 na tarehe 19 Septemba, 2013 na kwamba uharaka huo unatia mashaka kwamba kulikuwa na njama.
Mheshimiwa Spika, Muda wa siku 3 kwa Bodi kukutana si jambo la kutiliwa mashaka kwani Bodi haikutani kwa ajenda moja tu. Napenda kulijulisha Bunge lako Tukufu kuwa tarehe 16 Septemba, 2013 hapakuwa na kikao cha Bodi isipokuwa kikao cha Bodi kilifanyika tarehe 19 Septemba, 2013. Hivyo si sahihi kusema kuwa Bodi ya TANESCO ilikuwa ina njama katika kushughulikia na kulitolea maamuzi suala la Akaunti ya Escrow na kwamba ilikutana ndani ya siku tatu.
24.    Hoja ya Mwanasheria wa TANESCO
  Kufukuzwa Kazi
Mheshimiwa Spika, Katika ukurasa wa 30 wa Taarifa ya PAC kuna hoja kuwa Mwanasheria wa TANESCO kwa wakati huo Bw. Godwin Ngwilimi aliagizwa na TANESCO kwenda Malaysia kufanya Due Diligence ya Kampuni ya MECHMAR Corporation na kwamba taarifa hiyo ya Due Diligence ilifikishwa katika Bodi na Bodi iliipuuza na kinyume chake Mwanasheria huyo aliachishwa kazi. 
Mheshimiwa Spika, Taarifa hizi si za kweli na ni uongo uliokithiri kwa aliyekuwa Mtumishi wa Umma kuudanganya umma wa Watanzania kwa kiasi cha kutisha na Kamati inatoa taarifa ya uongo ndani ya Bunge.
Mheshimiwa Spika, Ukweli wa jambo hili ni kama ifuatavyo:
1.  Mwanasheria huyo Bw. Ngwilimi alileta ombi la kusafiri kwenda Malaysia kwa kumdanganya Mwajiri wake kwa kudai kuwa alipewa ushauri wa kwenda Malaysia na Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Katika barua ya kuomba ruhusa alisema kuwa alikuwa aende na Mwanasheria Mwandamizi kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na aliruhusiwa.  Hata hivyo, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali haikutoa Ofisa huyo na hivyo kuamua kwenda peke yake.
2.  Bw. Ngwilimi hakufukuzwa kazi na Bodi kama ilivyodaiwa katika Taarifa ya kamati ya PAC katika ukurasa wa 30, bali aliomba kuacha kazi mwenyewe kwa kutoa taarifa kwa Mkurugenzi Mtendaji kwa barua ya yenye Kumb na. SEC.215/Conf/2/2014 ya tarehe 27 Februari, 2014 iliyokuwa inasomeka “Notice to Terminate my Service with TANESCO” akitoa notisi ya siku 90 kwa mujibu wa Mkataba wake wa kazi.
3.  Katika ombi lake alidai kuwa anaacha kazi kwa hiari yake mwenyewe kwa kuwa anahitaji kufanya shughuli nyingine na akaushukuru uongozi wa TANESCO kwa ushirikiano kwa kipindi chote alichofanyakazi. Machi 10, 2014 Shirika lilimjibu Bw. Ngwilimi kwa barua yenye Kumb. Na. N.837 kuwa Uongozi na Bodi ya TANESCO wamekubali ombi lake la kuacha kazi.
Mheshimiwa Spika, Kwa maelezo hayo ni wazi kuwa Bodi haikuwahi kumfukuza na Bodi haikukataa utoaji wa fedha za IPTL katika Akaunti ya Escrow. Badala yake Bodi ilielekeza IPTL ipewe fedha zilizopo kwenye Akaunti ya Escrow tu na kwamba usuluhisho uliyofanyika unakubalika. Aidha, Bwana Ngwilimi aliamua kuacha kazi mwenyewe na kukimbia baada ya kuelewa kuwa angechukuliwa hatua kutokana kumsingizia Mtumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuwa walitumwa wote na kusafiri wote kwenda kufanya kile alichodai due diligence.