Askari wa JKT akutwa mferejini akiwa kalewa chakariKatika hali isiyotegemewa askari mmoja wa jeshi la kujenga Taifa (JKT) anayesadikika kuwa na wa kambi ya Mafinga wilaya ya Mufindi mkoani Iringa usiku wa leo amenusurika kuvuliwa nguo za jeshi hadharani baada ya kukutwa amelewa chakari na kulala katika mfereji wa maji machafu eneo la nje ya stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani mjini Iringa

Tukio hilo lilitokea muda wa saa 2 usiku baada ya wasamaria wema kumshusha askari huyo kutoka katika basi la Mgumba ambalo alikuwa amepanda kutoka Mafinga kuja mjini Iringa.

Akisimulia kisa na mkasa wa askari huyo kulewa chakali kiasi cha kushindwa kujitambua mmoja kati ya wasamaria wema aliyejitolea kumshusha katika basi hilo alisema kuwa askari huyo alipanda basi hilo Mafinga huku akiwa amelewa na wakati wote wa safari alionekana akinywa pombe kali kiasi cha kushindwa kujimudu na kuanza kutapika na kujisaidia haja ndogondani ya basi hilo.

Hata hivyo alisema baada ya kufika stendi ilikuwa ni vigumu kujitambua hivyo kupoteza fahamu na kulazimika kumpa msaada na kumzimua kwa maji kabla ya kupata fahamu kiasi na kujificha chini ya mfereji wa maji machafu .

Alisema kuwa mara baada ya kujitambua kiasi aliweza kutoa namba ya ndugu yake ambae ni askari wa FFU mjini Iringa aliyefika kumnusuru kuvuliwa nguo na kiongozi wake aliyefika eneo hilo na kumkutana akilishushia heshima jeshi kwa ulevi uliopitiliza

"Umelidhalilisha sana jeshi kwa askari kulewa hivi ukiwa katika sare, sasa nataka kukuvua sare kisha nakupeleka kulala polisi kabla ya kesho kukuchukulia hatua zaidi " alisikika akisema kiongozi huyo ambae jina wala cheo chake hakukitaja.

Maamuzi hayo ya kiongozi wake yaliwafanya mashuhuda kumuangukia na kumwomba amsamehe kwani bado ni kijana mdogo sana maombi ambayo aliyakubali na ndugu zake kumpakiza katika Taxi na kumpeleka eneo la Kihesa.

Ushauri wetu kwa askari wetu kujaribu kuheshimu nafasi hizo japo hakuna anayewakataza kunywa pombe ila watambue kuwa unywaji pombe kupita kiasi ni hatari kwa afya yako ama chonde chonde ulevi noma.

Hongera Mwl. Ishengoma kwa kuhitimu masomo ya shahada ya Udaktari


Dk Nelson Ishengoma

Dk Nelson Ishengoma ametunukiwa shahada yake ya udaktari katika Mahafali ya Tano ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) yaliyofanyika jana katika viwanja vya Chimwaga vilivyopo Chuoni hapo.

Hongera sana Mwalimu wangu na sasa mwanzo wa jina linaanza na Dk. Siyo kazi rahisi lakini Mungu ameweza kukusimamia na kukuongoza. Nakuombea kwa Mungu ufanikiwe zaidi na zaidi. 

Kutoka kwa mwanafunzi wako,  Josephat Lukaza

[video] Dakika 54 za mazungumzo na Rais Kikwete aliporudi kutoka kwenye matibabu

Polisi aliyemwua Michael Brown ajiuzulu

Michael Brown (kushoto); Darren Wilson (kulia)

Darren Wilson (28), askari polisi wa kituo cha Ferguson huko St. Louis nchini Marekani ambaye alimpiga risasi iliyomwua kijana wa asili ya Afrika, Michael Brown (18) takriban miezi minne iliyopita, ameacha kazi.

Uamuzi huo wa Wilson ulitanganzwa jana Jumamosi na mmoja wa mawakili wake, Neil Bruntrager ambaye amesema hatua hiyo inaanza mara moja. Kabla ya hapo, Wilson alikuwa katika likizo ya kikazi tangu Agosti 9.

"I, Darren Wilson, hereby resign my commission as a police officer with the City of Ferguson effective immediately. I have been told that my continued employment may put the residents and police officers of the City of Ferguson at risk, which is a circumstance that I cannot allow. For obvious reasons, I wanted to wait until the grand jury made their decision before I officially made my decision to resign. It was my hope to continue in police work, but the safety of other police officers and the community are of paramount importance to me. It is my hope that my resignation will allow the community to heal. I would like to thank all of my supporters and fellow officers throughout this process."

Hivi karibuni uamuzi uliotolewa baada ya miezi mitatu ya uchunguzi wa vielelezo vya sababu ya kifo cha Brown na kumwona Wilson hana mashitaka ya kujibu, uliamsha ghadhabu miongoni mwa wananchi na kuzua maandamano katika majimbo tofauti nchini Marekani ya kupinga uamuzi huo.

Mahakama yamfutia mashitaka ya mauaji Rais Mubarak

Mahakama Kuu nchini Misri jana Jumamosi ilimfutia mashitaka ya mauaji rais wa zamani wa nchi hiyo Hosni Mubarak, mashitaka ambayo yalikuwa yanamkabili awali yaa vifo vya waandamanaji wakati wa vuguvugu la mapinduzi ya mwaka 2011 baada ya kujaribu kutaka kusalia tena madarakani huku akiwa ameongoza nchi hiyo kwa miaka 30.

Uamuzi huo umechochea hasira ya wapinzani wa Mubarak ambapo karibu watu 1,000 walikutana katikati mwa jiji la Cairo kupinga serikali.

Wizara ya afya imesema kuwa mtu mmoja amepigwa risasi na kufariki dunia wakati Polisi wa kutuliza ghasia nchini Misri wakijaribu kuwatawanya waandamanaji waliokuwa wakiandamana kupinga uamuzi ya mahakama nchini humo.

Aidha mahakama imemwondolea rais huyo wa zamani mashataka ya rushwa, lakini ataendelea kubaki kizuizini kwa sababu anatumikia kifungo cha miaka mitatu katika kesi nyingine ya rushwa.

Maaafisa wengine saba waliohudumu kwenye serikali ya Mubarak akiwemo waziri wa zamani wa mambo ya ndani anayeogopwa Habib al Adly pia wamefutiwa mashitaka ya mauaji ya watu 800 waliouawa katika mapinduzi hayo.

via RFI Swahili