Mwl. Mndeme: Makosa na suluhisho katika kutafuta viongozi Tanzania

Baadhi ya majina yanayotawala mjadala wa uchaguzi mkuu mwaka 2015

Makosa Katika Mchakato wa Kutafuta na Kupata Viongozi wa Kisiasa Tanzania na Suluhisho Lake

SEHEMU YA TATU

Katika sehemu ya kwanza na ya pili ya makala hii, nilitoa utangulizi wa jumla kwa kuonesha shida kubwa ya uongozi tuliyonayo katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu. Nilieleza jinsi "siasa" imekua ndiyo jambo muhimu zaidi kuliko mengine yote kwenye jamii na kudhoofisha maeneo mengine. Nilieleza kwa undani kwa nini tuko tulipo na aina ya uongozi tulionao. Nilijenga hoja kuwa nchi yetu haina (na huenda haijawahi kuwa) na mfumo imara, mpana na wa kudumu wa kuandaa viongozi wenye kubeba maono makubwa ya nchi yaliyo juu ya maendeleo ya mtu binafsi, chama chake cha siasa au taasisi nyingine yoyote ile ya umma au ya kijamii. Nilionesha ni kwa jinsi gani kukosekana kwa mfumo huu imara wa uongozi kumedhoofisha hata uwezo wa kurithishana maono, mwelekeo, majukumu na madara katika nchi yetu. Naomba uendelee kusoma sehemu ya tatu:TUMERUHUSU MFUMO UTUTENGENEZEE VIONGOZI HATARI NA SASA WANATUMALIZA SISI WENYEWE

Sayansi ya asili, inatufundishwa kuwa vitu viwili haviwezi kuwa kwenye sehemu moja kwa wakati mmoja. Ni lazima kimoja kiondoke ndipo kingine kichukue ile nafasi. Unapokua na ndoo imejaa maji na ukawa unataka ndoo hiyohiyo uijaze maziwa, unalazimika kwanza kuondoa maji hayo ndipo ujaze maziwa. Wanaoamini katika Mungu wanajua pia kwamba sheria ya imani inasema huwezi kutumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja maana kwa kufanya hivyo unaweza kujikuta unamheshimu mmoja na kumpotezea mwingine. Hivyo ni ama unaamini bwana mmoja na kumpotezea mwingine lakini huwezi ambatana na wote wawili. Hali kadhalika, sheria ya asili inatuonesha kwamba hakuna mahali ambapo kuna uwazi (vacuum) na kama hakuna kabisa kitu cha kuonekana kwa macho basi kuna hewa. Na wenye imani za kidini wanaamini kwamba kila mtu kuna kitu anachoamini kwani kwa asili mwanadamu hajioni amekamilika bila nguvu ya ziada iliyo juu yake. Hata wanaosema hawaamini katika Mungu, bado kuna mambo wanayaamini katika huo upagani au kutokuamini kwao.

Kama nilivyoelezea kwenye makala zilizopita, nchi yetu haina mfumo wa kueleweka wa kuandaa na kupata viongozi wa kisiasa. Hata hivyo viongozi ni lazima wawepo katika jamii bila kujali wanafaa au hawafai; ni wazuri au ni wabaya; wameandaliwa au wamejiandaa; wamewekwa au wamajiweka. Ulazima huo na ukweli kwamba kumekua na ombwe la kutokua na mfumo wa uongozi unaotoa mwelekeo kuonesha ni wapi taifa linatakiwa kwenda, kumetoa upenyo wa mifumo mingi mingine kujitokeza na kujiimarisha hadi kufikia kiwango cha kujiendesha kitaasisi. Hata pale ambapo tumejitahidi kuonesha kwamba tuna mfumo na tuna viongozi wazuri, ombwe hili limekua wazi na dhahiri na mara nyingi waovu wameshinda wema na mfumo wa uongozi mbovu umeuzidi nguvu mfumo wa uongozi wenye malengo. Hii ni kwa sababu tumeacha mfumo hatari ukue miongoni mwetu na sasa tumejikuta katika changamoto ya kutumikia mabwana mawili na huku bwana mmoja akiwa ni katili na asiye na huruma nasi.

Nchi yoyote duniani inapofikia mahali vyombo vyake vya ulinzi na usalama vinashindwa kuonesha uwepo na mamlaka yake, cha kwanza kujidhihirisha ni uwepo wa makaundi yanayotishia amani, usalama na uimara wa nchi (stability) ambapo hupelekea kudorora kwa usalama wa raia na mali zao. Kwa kawaida hujitokeza makundi ya wezi, mafisadi, majambazi, majangili, wabakaji, vibaka, na wengine kama hao ambao wanajiimarisha katika jamii na kutekeleza matendo yao bila hofu. Kunapokua na ucheleweshaji zaidi wa serikali na vyombo vyake kujiimarisha, makundi haya hufikia kiwango cha kuwa taasisi zenye nguvu na hata kujijengea himaya za utawala rasmi. Kwa mfano:
  • Miaka kama miwili iliyopita, nchini Mexico kulikuwa na mbabe mmoja wa dawa za kulevya ambaye siyo tu alijiimarisha na kundi lake kubwa, bali alijiundia utawala na wananchi walimtambua na kumtumikia kama kiongozi katika eneo ambalo alikua ameweka mskani yake. Serikali ilipoamua kupambana naye kwa kulivamia eneo la mji alilokua anaishi, ilikua ni vita ngumu sana ya wiki kadhaa na walikufa watu wengi ikiwa ni pamoja na wanajeshi wa serikali wenye silaha nzito.
  • Kuibuka kwa makundi hatari kama Al Shabab, Al Qaida, Boko Haram, Mungiki, Mafiana mengine yanayotingisha nchi mbalimbali na dunia, kumechangiwa na nchi kukosa uongozi wenye maono na maslahi mapana ya kuhakikisha usalama wa kitaifa.
  • Kukosekana kwa mfumo imara wa uongozi kwa nchi kama Libya, Iraq, Syria, Lebanon na nchi zingine, ndio kumeibua makundi ya wapiganaji na wababe wa kivitawanaoisnyia dunia usingizi.

Tanzania kama nchi tumeshindwa kuwa na mwelekeo wa pamoja kama taifa na hivyo kukosa kuwa na utaratibu wa kuandaa viongozi wa kutuongoza huko tunakokwenda (ambako hatukujui kwa sasa). Kwa kufanya hivi, tumeruhusu mifumo mingine ijiinulie maono yao na viongozi wa kuyabeba. Jambo hili ni hatari sana na ndilo limefanya mchakato mzima wa upatikanaji wa viongozi wa kisiasa kuwa soko huria lisilokuwa na mwenyewe. Yameibuka makundi ndani na nje ya vyama vya siasa na kupandikiza maono yao ambayo wametuaminisha kuwa ni maono ya kitaifa na kisha kuweka viongozi wa kuyasimia.  Wameibuka watu binafsi kupitia makundi yanayotambulika kama vile vyama vya siasa na makundi ya kidini na kujiingiza kwenye uongozi wa kisasa kwa malengo binafsi na mara nyingine mbali sana hata na mtazamo wa makundi wanayosema wanayawakilisha.

Ombwe la kukosa mfumo wa kuandaa viongozi wenye maono ya nchi, ndilo limefanya siasa kuwa mradi wa uwekezaji kwa kila anayejisikia: kuwa uwekezaji wenye masharti nafuu sana na ulio na kila aina ya uwezeshwaji na misamaha ya kodi yasiyofuata taratibu na sheria za nchi. Ombwe hili limebinafsisha dhana nzima ya uongozi wa nchi na kupandikiza picha isiyo sahihi kwa wengi juu ni nini hasa maana ya uongozi na majukumu yake.

Tunaendeshwa na Majina
Mfumo huu, umeruhusu baadhi ya watu kwa malengo na maono yao na makundi wanayoyaongoza kututengenezea maono; kutuchongea viongozi na kutushawishi kuwa ni wema na waadilifu wenye uwezo wa kututoa Misri na kutupeleka kwenye nchi ya ahadi. Pale ambapo makundi yamekosa nguvu za kutosha kutuchagulia viongozi, hata watu binafsi wenye uwezo wa kifedha wameibuka na kufanya uongozi ni biashara. Watu hawa wanawekeza fedha na mali zao katika kuwahonga na kuwanunua wananchi ili kujitafutia uhalali wa kuwaongoza nje ya matakwa na maslahi ya wananchi husika. Tunagharimika kukuza majina badala ya uongozi:

  • Mojawapo ya viashiria vikubwa vya mfumo mbovu wa uongozi ni pale ambapo taifa linapongelea uongozi wa nchi, linajikuta linajadili na kujenga hisia zao katika kuongelea majina ya watu na makundi badala ya dhana ya uongozi na maono ya nchi. Tatizo hilo huwa kubwa zaidi tunapojikuta tunajipa kazi ya kujadili, kuyakuza na kuyatafutia heshima majina badala ya kukuza na kuyatangaza maadili, uwajibikaji, na mwelekeo wa taifa.Tunajadili ni mgombea au mtajwa gani ni maarufu kuliko mwingine; nani ana pesa kuliko mwingine; nani amewahi kufanya nini ukilinganisha na mwingine; na nani ana mke/mume mzuri kuliko mwingine; nani ana watu wengi nyuma ya harakati zake;nani ana sura nzuri zaidi; na nani anaungwa mkono na kiongozi gani mkubwa wa nchi. Tunachukua majina au jina la mtu fulani na kuliweka kuwa kiwango cha juu na kipimo cha aina na uhitaji wetu wa uongozi, sio tu ni hatari kwetu kama taifa, bali ni kiwango kikubwa cha kufilisika kimaono na mtazamo kama jamii.
  • Kuendeleza mjadala wa majina katika kuelekea uchaguzi mkuu ni kuzima na kunyamazisha jitihada na harakati za kuibua watu wenye vipawa vya uongozi na maono sahihi kwa taifa letu. Tunapoutazama mjadala wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, kwa miaka kadhaa sasa, tumejikuta katika mjadala ya majina na kuendeshwa na hisia za majina na makundi yao badala ya nini matarajio na maono yetu kama taifa.
  • Katika mazingira yaliyoko ya kujadili majina na makundi ya watafuta uongozi, ni ngumu sana kupata mwanya wa kuona watu wanaoweza kusaidia nchi nchi yetu. Hatutaweza kuwaona wala kuwasikia watu sahihi wa kutuongoza maana wameshajengewa mazingira ya kunyamazishwa.
  • Kwa kuendelea kujadili majina na makundi yao, tunakua sehemu ya kujenga ufalme na ngome zao na hivyo kujiimarisha zaidi na kujihakikishia kuongoza nchi yetu kwa mitazamo na maono yao ambayo mwisho wa siku wanakua kongwa na mzigo kwa wananchi.
  • Tunazuia nafasi kwa jamii kuweza kujadili kwa mapana matakwa ya kiuongozi na mwelekeo wa taifa wanalolitaka

Kwa kuyasema haya, sina maana kwamba hakuna viongozi wazuri na wenye maono ya kitaifa miongoni mwa majina yanayotajwa; la hasha! Ninachosema ni kwamba, ni hatari sana kuweka majina mbele ya vigezo stahiki katika kutafuta na kupata viongozi wa kisiasa kwa taifa letu. Kiuhalisia ilitakiwa sifa, vigezo, maono na uhitaji wa viongozi kwa nchi yetu ndio viibue majina ya wanaostahili kuingia kwenye vigezo hivyo na sio kinyume chake. Tukitanguliza vigezo, tusingepata changamoto ya majina kwani majina yasiyofaa yangejiengua yenyewe na yasingejitokeza, na majina ya waliobeba vigezo yangejitokeza au kutafutwa na wanachi.

Kwa kuwa tumekosa mwelekeo wa pamoja kama taifa, moja kwa kwa moja tumejikuta tumeingia katika changamoto ya kuruhusu mifumo hatari ya kutuangamiza kutuongoza. Pamoja na kwamba hatujaingia katika mapambano ya vita kwa maana ya silaha, lakini ukweli ni kwamba tuna mifumo na watu binafsi hatari sana ambao wamechomoza na kupata uhalali wa kutuongoza kwenye taifa letu. Watu hawa hawana huruma na watanzania; hawana huruma na rasilimali zetu; hawana huruma na mjane; hawana huruma na watoto maskini; hawana huruma na usalama wetu. Wanatuaminisha usiku na mchana kwamba wako kwa ajili yetu, lakini hali halisi tunayopitia kama taifa katika ngazi mbalimbali, inawakana na kuonesha ni nini hasa wanachokisimamia.

Katika mijadala kadhaa ya kitaifa ambayo imekua ikiendelea kwa miaka kadhaa hasa katika eneo la maslahi ya taifa, rushwa, ufisadi na kukosa maadili, utaona ni kwa jini gani wale wanaojiitga viongozi wetu wanavyotofautiana katika kuutafsiri ukweli. Viongozi wetu hawana maana zinazofafa za ufisadi; hawana maana inayofanana ya uongozi mbovu; hawama maana inayofanana ya rushwa; na wata tafsi zinazokinzana kuhusu utumishi wa umma na uhifadhi wa rasilimali za nchi. Watu hawa, wana tafsiri zinazobishana kuhusu usalama na amani ya nchi.

Tumenyamaza na tumekataa kujishughulisha kama taifa kuwa na mwelekeo; madhara yake ni  tumeruhusu kuibuka kwa viongozi wa kututafuna na kutungamiza kabisa; na sasa tunavuna tunachoendelea kupanda.

Katika sehemu ya nne ya makala hii, nitaanza kutoa baadhi ya mapendekezo ya nini cha kufanya kama taifa ili kukabiliana na changamoto zinazotukabili. Nitajaribu kuweka mapendekezo yanayohitaji utekelezaji wa muda mfupi na yale ambayo ni muda mrefu kwani utekelezaji wake ni mtambuka na kuhitaji muda wa utekelezaji wake.

Nitapenda kusikia maoni yako na unaweza kuniandikia kupitia barua pepe yangu ambayo ni [email protected].

Mwalimu MM


Bensouda apewa wiki moja kuamua kuhusu kesi ya Rais Kenyatta

Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu ICC imekataa ombi la Mwendeska mashitaka mkuu, Fatou Bensouda, kuahirisha kesi dhidi rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta. 

Bensouda amepewa wiki moja kutupilia mbali kesi hiyo au aiarifu Mahakama kwamba amepata ushahidi wa kutosha kuendelea na kesi.

Uamuzi huo umekua unasubiriwa kwa hamu na gamu, baada ya rais wa Kenya kujielekeza Hague mwezi Oktoba. Kenyatta alitakiwa kuripoti mbele ya majaji wa Mahakama hiyo ili upande wa mashitaka na upande wa utetezi mbili waisikilizwe, na Mahakama iamuwe iwapo kesi hiyo iendelee au isitishwe.

Mahakama imechukua uamzi huo Jumatano Desemba 3. Awali Fatou Bensouda alikiri mwenyewe kwamba hana ushahidi wa kutosha, lakini aliomba apewe muda ili aendelee kutafuta ushahidi, akibaini kwamba mashahidi aliokua nao waliamua kujiondoa katika kesi hiyo. Bensouda aliituhumu serikali ya Kenya kwamba ilikataa kutoa ushirikiano.

Bensouda alikusudia kupata ushahidi kutoka upande wa serikali ya Kenya, akiitaka serikali kutoa nyaraka muhimu zinazo muhusu Kenyatta ambazo zingelionyesha kuwa alihusika katika ghazia za baada ya uchaguzi katika mwaka wa 2007 hadi 2008. Hata hivyo Mahakama ilitupilia mbali kwamba serikali ya Kenya ilikataa kutoa ushirikiano.

Rekodi zinasema kiasi cha watu 1200 waliuawa katika ghasia hizo.

Above the law in Tanzania? Hand cuffed for an offence I did not commit.

The role of the police in any community is to execute and implement the law and to make sure the law is abided by the habitants within the country, but have you noticed how Tanzanian law changes depending on the person involved or even the time of the day?!

Three weeks ago on a Monday morning I was heading towards Kenyatta Drive from Toure Drive. It was 7am and every commuter was hastening towards what earns them their bread and butter. During rush hour, two lanes of cars head towards Ali Hassan Mwinyi Road (on Kenyatta Drive) which is initiated by the traffic police stationed at the junction of Kenyatta Drive and Toure Drive and Kaunda Drive. Also, vehicles are not permitted to turn into Kenyatta Drive from Ali Hassan Mwinyi Road. To allow for this route, as I was driving, the police at that junction ordered me to take the second lane to get vehicles moving towards Ali Hassan Mwinyi Road. As I got close to the traffic lights, another police man stops me at the junction where Laibon Road meets Kenyatta Drive and starts shouting at me for driving on the wrong lane. As an individual who knows my rights and responsibilities, I asked him how I was breaking the law while there are so many vehicles ahead and behind me in the same situation and that this lane was started by the police who was at the previous junction. Apparently, asking was my mistake.

The police officer started writing a fine of Tshs 30,000 for driving on the wrong side of the road. I was not ready to accept the fine at that time because I only abided to the enforcers of the law. So I started collecting evidence on my phone by taking photos of how other cars were using the same road I was in but I was subject to a fine and they were not. This was another mistake I made according to the “police” – the same police officer then physically pushed me aside and started snatching my phone. I guarded my phone in my pocket firmly. That’s when another police officer came and forced the phone out of my hands and a third police officer cuffed my hands (who also racially discriminated against me)!

So here I was, at 7:30am on a Monday morning during rush hour, hand cuffed for an offence I did not commit. The options laid to me were: Pay the fine right there and then (with no receipt), or leave the car on the side of the road with the keys in custody of the “police” and go to the police station to make a statement and then head to court to fight the case. I was already getting late for work, so now I HAD TO accept that I indeed “broke the law” and should pay the fine, which I did out of harassment. As if by miracle, the handcuffs opened, my phone was returned to me, and I was on my way as if nothing had happened.

A few days later, the same police officer who wrote the fine stops me on the same road at the same time and hands me my receipt for the fine I paid. On that day I was on the same second lane and was not fined!!

Most of the offenders of the traffic law are vehicles with specific pattern of number plates; they may be red plates, they may be black plates, they may be yellow plates beginning with ST.. or SU.. and very few are actually private cars (with non-influential people in them). Of course, the vehicles with the white plates are exempt from all common sense and logic!

Just today it was raining and at the onset of rain, all traffic police controlling movement of vehicles at the Selander Bridge and Kinondoni junction walked into shade while they were dressed for the rain, letting all hell loose withbodabodas and bajajs scrambling like ants escaping a massacre.

So when is the law applicable? To whom is it applicable? What are we as citizens doing about it? Because as it stands, there are some who are above the law.

By Irfan Walji, Dar-es-Salaam: Above the law?
This is a cross-post from VijanaFM

Mafuriko mkoani Mwanza

Hali halisi katika maeneo ya Ilemela na Mabatini jijini Mwanza. Suluhisho ni kubuni miundombinu wezeshi kwa wale waliojenga milimani dhidi ya wale walio chini tambarare.
Picha: Daniel Ngosha.
(wavuti.com imenukuu kutoka Mtwara Kumekucha blog)
NBC Press Release: Fire threat at the NBC Head Office

Wafanyakazi wa NBC Sokoine Drive wakiwa kwenye viwanja vya Samora baada ya kutokea hitilafu ya umeme kwenye jengo la benki hiyo, jana. Hakuna aliyejeruhiwa.


Dar es Salaam, December 3rd, 2014 Today at 09:30am on 3rdDecember 2014, there was a fire threat at NBC Head Office building situated along Azikiwe and Sokoine Drive in the city center. All staff and customers were safely evacuated and accounted for. The NBC technicians and safety officers established an electrical fault at one of the cargo lifts that resulted in the triggering of the fire alarms. The fire brigade and police force responded to the scene.

“The threat was contained and there was no damage to the people and property. And we assure our customers and the general public that everything is calm and we are back to our normal operations”, said Jimmy Myalize the Acting Chief Operating Officer of NBC.

Due to the evacuation procedures at NBC, and the arrival of the fire brigade and police, may have caused some traffic congestion and anxiety of pedestrians within Dar es Salaam CBD. NBC sincerely apologizes for the inconvenience caused, and at the same assures customers and the general public that business resumed as usual immediately after the fire threat was contained.

We would like to assure our customers that everything is safe and we are committed to serving our customers in the most convenient and innovative manner to help our customers achieve their ambitions – in the right way.

NBC has introduced exciting and innovative products into the market in the quest to make banking easier for customers in their journey to become the leading bank in Tanzania and to support their ambition of helping customers achieve their ambitions – in the right way. Among other banking services, NBC customers can also send money to their loved ones who do not have banking account through the bank’s Cash Popote product. Recipients are able to withdraw funds from any NBC ATM.

Editors Note;NBC is one of the most represented retail bank in the country with over 45 years experience in providing financial services. Apart from offering traditional banking services, NBC also prides itself with an expanded branch network of 52 branches and over 280 Visa enabled ATMs. The bank also services over 250 Points of Sales strategically located throughout the country. NBC has employed over 1,300 staff.
Watoa huduma ya kwanza wakiandaaa vifaa kwa ajli ya kazi hiyo.
Ofisa wa benki hiyo, Rukia MTingwa akizungumza na waanahabari baada ya hali kutengemaa

Uandikishaji raia wa kigeni wazinduliwa Kigoma

Kamishina wa Uhamiaji, Usimamizi na udhibiti wa Mipaka nchini Tanzania, Abdullah Khamis, akiongea na Waandishi wa Habari kabla kuzindua rasmi zoezi la uandikishaji raia wa kigeni. Pembeni kushoto kwake ni Deputy Chief of Mission kutoka Shirika la Kimataifa la Uhamaji (OIM), Tamara KEATING na kulia kwake ni Naibu Kamishina wa Uhamiaji, ambaye pia ni Afisa Uhamiaji Mkoa wa Kigoma, Ebrosy Kingdom Mwanguku.

SERIKALI ya Tanzania kupitia Idara ya Uhamiaji leo imezindua rasmi zoezi la uandikishaji raia wa kigeni waishio nchini na kuwapatia vitambulisho maalum vya nchi zao ili waweze kupata hadhi ya kuishi kihalali hapa nchini.

Akiongea wakati wa kuzindua zoezi hilo kwenye uwanja wa Lake Tanganyika, Mjini Kigoma, Kamishina wa Uhamiaji, Usimamizi na udhibiti wa Mipaka nchini Tanzania, Abdullah Khamis, amesema nia ya zoezi hilo ni kuwatambua wasio raia wa Tanzania na kuwapa hadhi inayostahili.

Amesema zoezi hilo litasaidia kuondoa utata ambao umekuwepo kwa muda mrefu wa kujua nani raia wa Tanzania na nani asiye raia hasa linapokuja suala la haki za raia ikiwemo uchaguzi wa viongozi wa nafasi mbali mbali.

Amesema walengwa katika zoezi hilo ni pamoja na walowezi walioingia na kuishi nchini na kujishughulisha na kilimo, biashara, ufugaji nk. Wengine ni wanaoishi nchini kwa vile wameolewa au kuoa watanzania, watoto wa vizazi vya waliopewa uraia ambao ni watoto wa waliokuwa wakimbizi ambao wazazi wao walipewa uraia lakini wao hawakupewa pamoja nao na walizaliwa kabla ya wazazi wao kupewa uraia.

Kundi lingine ni wakimbizi waliopewa uraia miaka ya 1980 ambao wanatakiwa kujiandikisha ili kupata taarifa zao ziingizwe kwanye kanzi data (database).

“tulifanya kwanza kuwatambua maeneo na kukadiria idadi yao ili tuweze kujua tutajipanga vipi katika kuwasajili,”alisema Kamishina wa Uhamiaji.

Aidha alisema kuwa wameanza zoezi la kusajili tangu tarehe mosi Disemba na kwamba mwitikio ni mzuri ambapo takribani watu 1050 wameshajitokeza na kusajiliwa rasmi.

Kamishina wa Uhamiaji, Usimamizi na udhibiti wa Mipaka nchini Tanzania, Abdullah Khamis, akipata maelezo kutoka kwa maafisa wa uhamiaji kuhusiana na namna ambavyo zoezi la usajili linavyofanyika.Kamishina wa Uhamiaji, Usimamizi na udhibiti wa Mipaka nchini Tanzania, Abdullah Khamis, akizindua rasmi zoezi la uandikshaji raia wa kigeni waishiio nchini kwa kukabidhi kadi au kitambulisho maalum cha ukaazi.

Wizara ya Mambo ya Ndani yapokea pikipiki 10 toka Dalbit Petroleum


Kamishina wa oporesheni na mafunzo wa jeshi la polisi, Paulo Chagonja akisisitiza jambo wakati wa hafla ya kupokea msaada wa pikipiki 10 aina ya boxes kutoka kwa Kampuni ya mafuta ya Dalbit Petroleum ya nchini kwa ajilia ya kusaidia kikosi cha usalama barabarani kupambana na swala zima la usalama barabarani.Katikati ni Mwenyekiti wa kampuni Hum Dalbit Petrolium Humprey Kariuki na Kushoto ni Mkurugenzi wa maswala ya Uhusiano wa Kampuni hiyo Magaret Mbaka.


Baadhi ya askari wa kikosi cha usalama barabarani wakiangalia pikipiki aina ya Boxes kati ya 10 zilizotolewa msaada na kampuni ya mafuta ya Dalbit Petroleum nchini kwa ajilia ya kusaidia kikosi cha usalama barabarani kupambana na swala zima la usalama barabarani.Hafla hiyo ilifanyika makao makuu ya jeshi jijini Dar es Salaam


Kamishina wa oporesheni na mafunzo wa jeshi la polisi Paulo Chagonja akijaribu kuendesha moja ya pikipiki aina ya boxes kati ya 10 zilizotolewa msaada na kampuni ya mafuta ya Dalbit Petroleum nchini kwa ajilia ya kusaidia kikosi cha usalama barabarani kwa kupambana na waalifu wa makosa mbalimbali. Kulia aliyevaa koti ni Mwenyekiti wa kampuni hiyo Humprey Kariuki.

#GoldenExperience: Imebaki nafasi moja tu


ICC yapigilia msumari hukumu ya Lubanga ya miaka 14 jela

Thomas Lubanga wakati wa hukumu yake ya mwanzo na baadae alikata rufaa, lakini Mahakama ya kimataifa ICC imethibitisha hukumu ya miaka 14 jela, Jumatatu Desemba 1 mwaka 2014.
REUTERS/Michael Kooren
Standard
Mahakama ya kimataifa ICC imethibitisha Jumatatu, Desemba 1 hukumu ya miaka 14 jela kwa Thomas Lubanga, kiongozi wa zamani wa wanamgambo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Katika hukumu iliyochukuliwa Hague, mahakama ya kimataifa imefutilia mbali rufaa ya hukumu kwa kiongozi huyo wa kivita iliyotangazwa mwaka 2012.

Lubanga alipatikana na hatia ya kusajili askari watoto katika jimbo la Ituri, kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mwaka 2002 na 2003. Thomas Lubanga yuko gerezani mjini Hague kwa miaka nane sasa.

Kwa upande wa majaji, Thomas Lubanga, mwenye umri wa miak 53, alipatikana na hatia ya kusajili askari watoto wakati alikua akiongoza kundi la waasi la UPC katika jimbo la Ituri, kaskazini mashariki mwa Congo. Watoto hao walisajiliwa katika katika tawi la kijeshi la kundi hilo la waasi. Watoto hao walipewa mafunzi ya kuua na kubaka.

Watoto hao walilazimishwa pia kushiriki katika mapigano, hasa dhidi ya kundi jingine la waasi. Mapigano yalifanyika wakati wa vita vya pili viliyotokea Congo kati ya serikali ya rais wa zamani Congo laurent Desire Kabila na waasi wa RCD, ambao walikua walikua waliliteka eneo nzima la mashariki mwa Congo.

Kitengo cha rufaa cha Mahakama ya kimataifa ICC kimethibitisha hukumu ya Thomas Lubanga kwa makosa ya uhalifu wa kivita na kimethibitisha pia kifungo cha miaka 14 jela.

Thomas Lubanga bado ana miaka 6 ya kutumikia kifungo chake kwa vile ameshatumikia miaka nane katika kituo cha Umoja wa Mataifa katika kitongoji cha Scheveningen nje kidogo ya mji wa Hague. Atabaki huko mpaka nchi nyingine kukubali kumchukua atumikie miaka inayosalia ili akamilishe hukumu yake.

Kikwete alijua kuhusu akaunti ya escrow? Lini?

TUSIPOANGALIA mwisho wa kashfa ya Akaunti ya Dhamana ya Tegeta tutamsikia Rais Jakaya Kikwete akizungumza na kutuambia kuwa alikuwa hajui nini kimetokea na kuwa na yeye, kama sisi wengine, atakuwa ameshangazwa na kushtushwa. Atakapozungumza bila ya shaka atajaribu kutuonesha kuwa jambo hili limemshangaza sana kwani alitarajia baada ya kujiuzulu kwa Edward Lowassa na kuvunjika kwa Baraza la Mawaziri kufuatia kujiuzulu huko alitarajia watendaji wake wangekuwa wamejifunza kitu. Hawakujifunza.

Hata ikitokea mawaziri na Mwanasheria Mkuu pamoja na watajwa wengine kujiuzulu kuna uwezekano Watanzania watajaribu kuaminishwa kuwa kashfa hii inahusu watu wenyewe tu na si serikali na wala isihusishwe na chama. Tayari jaribio hili limeanza kusikika na siku zinavyozidi kuja ndivyo tutalisikia sana bungeni kuhusu wote waliochukua fedha za akaunti ya Tegeta ambayo ilikuwa inashikilia fedha kwa niaba ya Tanesco na IPTL huko Benki Kuu. Tumekwishasikia baadhi ya viongozi wa CCM na wale wa ndani ya serikali wakijitahidi kuwabebesha mizigo watu ambao wanatajwa kukatiwa fedha nyingi na mmojawapo wa wafanyabiashara maarufu nchini, fedha ambazo zinadaiwa ni kutokana na akaunti hiyo ambazo zilichukuliwa baada ya muda mrefu wa migongano ya kisheria kati ya Tanesco, ITPL na kampuni zingine ambazo zilidai kuchukua nafasi ya IPTL. Siyo kusudio langu kuelezea hili sana.

Hata hivyo, hadi hivi sasa hatujasikia kauli yoyote kutoka Ikulu hususan juu ya nafasi ya Rais Kikwete katika suala hili zima hasa kwa vile viongozi wake waandamizi wakiwemo Waziri Mkuu, Mwanasheria Mkuu, Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi na wengine wametajwa kuwa ni sehemu ya watu waliochukua mgao huo kutoka kwa Rugemalila (mfanyabiashara na ofisa wa mojawapo ya kampuni zilizochukua IPTL). Ni wazi kuwa yawezekana ukimya wa Rais Kikwete kwa sasa unatokana na kuwa yuko anapata nafuu baada ya upasuaji wa tezi dume wiki mbili tu hizi zilizopita.

Uzito wa kashfa hii na jinsi ambavyo inaonekana imegusa watu mbalimbali maarufu nchini na kiasi kinachotajwa kuchotwa na kugawiwa kunalazimisha kujiuliza kama Rais Kikwete alikuwa hajui chochote juu ya jambo hili na kama alikuwa hajui inawezekana vipi na kama alikuwa anajua basi alijua nini na lini? Haya ni maswali muhimu sana kujiuliza kama kweli tunataka kupata kina cha kashfa hii kwani Rais Kikwete inaonekana haiwezekani akatenganishwa na IPTL.

Wakati Horace Kolimba – aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM na Waziri wa Mipango – ameenda Malaysia na akiwa huko kuanza mazungumzo ya kutafuta suluhisho la tatizo la umeme Waziri wa Maji, Nishati na Madini kwa wakati huo alikuwa Jakaya Kikwete. Hiyo ilikuwa Julai 1994. Mwezi Agosti mwaka huo huo ofisa wa juu wa kampuni ya Mechmar, Datuk Majid alifanya ziara nchini na kufanya mazungumzo na Kikwete juu ya jinsi Mechmar ingeweza kusaidia kuondoa tatizo la nishati. Mwezi Septemba makubaliano ya awali (Memorandum of Understanding) yalitiwa saini.

Kwa hiyo tunajua kwa uhakika wa historia kuwa Kikwete anajua kuhusiana na mktaba wa IPTL na licha ya mapingamizi mengi yaliyotolewa na taasisi mbalimbali na nchi wahisani miaka ile ya tisini, CCM na serikali yake waliendelea na mchakato huo. Baadhi ya maofisa ambao walihusika na kuileta IPTL nchini wengi tayari majina yao yanajulikana; Andrew Chenge – aliyekuwa Mwanasheria Mkuu, Abdallah Kigoda ambaye aliingia na kushikilia Wizara ya Nishati na Madini Februari 1997 ni wachache tu kuwataja.

Kwa muda wote ambao Kikwete alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje ndiyo IPTL nayo imekuwa ikishindana na Tanesco na serikali na hivyo uhakika mwingine wa wazi kabisa ni kuwa Kikwete alikuwa na nafasi ya kujua mambo mengi yanayofanyika kutokana na kuwa waziri mwandamizi kwa miaka kumi, muda ambao pia ulitumiwa kutafuta usuluhishi katika mahakama ya kimataifa ya biashara. Hawezi kudai kuwa alikuwa hajui.

Baadhi yetu tunakumbuka kuwa wakati wa kashfa ya rada, Kikwete alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje aliyejitokeza na kutetea ununuzi ule akidai kuwa tulikuwa tunaihitaji licha ya bei ghali na teknolojia ambayo kwa kweli hatukuwa tunaihitaji. Kwenye hili la IPTL ni hivi hivi, karibu watendaji wote waliokuwa wanaipigia debe IPTL inaonekana wazi kabisa walikuwa wanapata makato fulani kutoka kwa wadau wa IPTL. Kuna ripoti nyingi ambazo zilikuwa zinaonesha jinsi James Rumegalila alivyokuwa akisogea karibu na wanasiasa na watu wa karibu wenye kugusa maslahi ya IPTL na kuwalainisha.

Mmojawapo wa watu waliokuwa wamepinga mradi huu tangu mwanzo na labda angeweza kuwa shujaa mkubwa ni Patrick Rutabanzibwa. Ruta – kama wengi walivyozoea kumuita alikuwa amejaribiwa kulainishwa sana na “kakake” Ruge (Rugemalila). Inadaiwa Ruge alishawahi kujaribu kumpa hongo ya dola laki mbili ili abadili msimamo wake wa kupinga ujio wa IPTL; Ruta alikataa na hata zawadi ya X’mass ya shilingi laki tano (mwaka 1994) ambayo Ruge alimwachia nyumbani kwake aliirudisha.

Madai ambayo yametolewa na baadhi ya walioshikishwa hela na Ruge kuwa ni za kirafiki wanawachukulia Watanzania wote kuwa ni watu wasio na kumbukumbu na hili pia inabidi lije kuhoji nia ya kweli ya Rais Kikwete kupambana na ufisadi. Wakati sakata la IPTL linaanza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ilishafanya vikao na kukusanya ushahidi mbalimbali ambao ungeweza kusababisha Rugemalila kukamatwa. Inadaiwa Dk. Edward Hosea wakati huo akiwa Mkurugenzi tu ndani ya Idara chini ya Generali Kamazima alitaka kumtia pingu Rugemalila lakini alijikuta anazidiwa na bosi wake pamoja na Mwanasheria Mkuu, Andrew Chenge.

Katika ushahidi mbalimbali uliokusanywa dhidi ya Ruge na ambao bila ya shaka Rais Kikwete atakuwa anaujua kwani Hosea amekuwa mpambanaji wake mkuu dhidi ya rushwa na majina yanaonesha baadhi ya watu mashuhuri na wasio mashuhuri sana wakishikishwa hela ili waunge mkono IPTL. Na ni mtindo ule ule ambao ulitumika miaka ya tisini unaonekana kurudia tena kutumika safari hii kulainisha wanasiasa na watendaji mbalimbali. Miongoni mwa watu waliodaiwa kushikishwa fedha ni: Prosper Victus aliyekuwa ofisa katika Waziri ya Nishati na Madini alipewa ofa na Ruge kuzuia baadhi ya taarifa zisimfikie Rutabanzibwa; huyu anadaiwa kupewa ofa ya dola laki mbili vile vile.

Esther Mzunzu naye alikuwa ofisa chini ya Ruta, yeye anadaiwa kupewa kiasi cha shilingi laki moja.

Lakini zaidi tukumbuke kuwa sakata zima hili halijafichika tangu Kikwete mwenyewe aingie madarakani. Aliingia madarakani tatizo la nishati likiwepo na chini yake tumeshuhudia kashfa za Richmond/Dowans na vile vile hii ya IPTL ikijirudia – ukiondoa kashfa nyingine. Mawasiliano yote ambayo yamepatikana kuhusiana na kesi hii inaonekana bila ya shaka hadi Ikulu walikuwa wanajua kwani kuna barua zimetumwa kwa Katibu Mkuu Kiongozi – msaidizi mkuu wa Rais na Mkuu wa watumishi wa umma. Kama Katibu Mkuu kiongozi amejua hili dili la kuchukua fedha za escrow ni wazi bila ya shaka hadi Kikwete atakuwa anajua kwani mojawapo ya nakala za barua yenye kuelekeza Benki Kuu kutoa fedha za IPTL ilitumwa kwenda kwa Katibu Mkuu Kiongozi.

Watanzania tutafanya makosa makubwa sana kama tutaangalia kashfa hii na watu wanaohusika kama ni kashfa ya mtu mmoja mmoja tu. Na tutafanya makosa makubwa sana tukidhani kuwa Rais Kikwete hana hatia katika hili. Tutafanya makosa makubwa zaidi kama tutaamini kuwa CCM na serikali siyo wadau katika hili – zipo kumbukumbu za muda mrefu tu za madai ya jinsi CCM yenyewe ilivyoshikishwa fedha ili kuhakikisha IPTL kuingia nchini. Na hata hizi fedha ambazo watu wanafikiria zimechotwa na mtu mmoja mmoja kuna uwezekano mkubwa sana wakati tunaendelea kupiga soga fedha hizi zinazungushwa na kusafishwa (money laundering) hasa tukiangalia baadhi ya watu ambao wanadaiwa kukatiwa mamilioni ya hizo fedha. Akaunti ambazo fedha hizo ziliingizwa tutakapokuja kushtuka hatutakuta akaunti hata moja yenye fedha; tutakuwa tumeliwa na wale wanaosema “Turudishieni Fedha Zetu” itakuwa imekula kwao.

Lakini kwanza, tuanze kumuuliza Kikwete, ulijua nini kuhusiana na uporaji huu na ulijua lini?

Serikali yapiga marufuku ujenzi wa majengo yasiyo rafiki na wenye ulemavu

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na Uratibu wa Bunge,Mhe. William Lukuvi akimkabidhi cheti cha ushiriki Tumain Mdegella kwa niaba ya ofisi za Neema Crafti mjini Iringa wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya walemavu duniani iliyofanyika kitaifa mjini Iringa

Waziri Lukuvi akimkabidhi mwanafunzi wa shule ya Msingi Kipera Rahel Mwikonzi cheti cha ushiriki mzuri wa siku ya walemavu
 SERIKALI imeziagiza mamlaka za usafiri wa majini na nchi kavu (SUMATRA ) nchini kuanza mchakato wa kukaa na wamiliki wa vyombo hivyo ili kuanza uangizaji wa vyombo vya usafiri yakiwemo mabasi ambayo ni rafiki na walemavu nchini huku ikipiga marufuku majengo ya serikali kujengwa bila kuwepo kwa mchoro unaoonyesha mazingira yanayozingatia makundi yote ya jamii likiwemo la walemavu wa viungo .

Agizo hilo limetolewa na waziri mkuu Mizengo Pinda wakati wa maadhimisho ya siku ya walemavu duniani yaliyofanyika kitaifa katika viwanja vya kichangani mkoani Iringa jana.

Akiwahutubia walemavu hao na wananchi waliofika katika viwanja hivyo Waziri Mkuu, aliyewakilishwa na waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu (sera na uratibu wa bunge),Wiliam Lukuvi ambae ni mbunge wa jimbo la Isimani mkoani Iringa alisema kuwa kimekuwepo kilio cha muda mwingi kutoka kwa walemavu juu ya kusaulika katika ujenzi wa majengo mbali mbali ambayo yamekuwa yakijengwa bila kuzingatia kundi la watu wenye ulemavu jambo ambalo ni sawa na kuwabagua watu hao.

Hivyo alisema katika kuona kilio hicho cha walemavu kinafanyiwa kazi kuanzia sasa majengo yote ya serikali zikiwemo shule na taasisi nyingine kabla ya kuanza ujenzi wake lazima wasimamizi wa ujenzi huo kujiridhisha kwa mchoro ambao utaonyesha mazingira yatakayomuwezesha mlemavu kutumia jingo hilo bila usumbufu tofauti na ilivyo sasa ambapo idadi kubwa ya majengo mazingira yake si lafiki kwa walemavu.

" Ni siku nyingi watu wenye ulemavu wamekuwa wakilalamika juu ya mazingira yasiyo rafiki katika majengo mbali mbali .....sasa leo naomba kuagiza kuwa michoro yote inayochorwa katika majengo ya huduma za kijamii ni marufuku kupitishwa ama wasimamizi wa ujenzi husika kuruhusu ujenzi iwapo mchoro hauonyeshi kama utayajali makundi yote wakiwemo walemavu.....wasimamizi wote msikubali kusimamia wala kutangaza tenda ya ujenzi kama ramani yake si rafiki kwa walemavu.....lakini pia hata kwenye mabasi hivi unamtegemea mtu mwenye ulemavu wa miguu ataingia vipi na baiskeli yake katika gari iwapo hakuna mazingira yanayomwezesha kuingia .... hivi sasa teknlojia imezidi kukua na baadhi ya nchi wameanza muda mrefu kuwajali walemavu kwa kuwa na mabasi ambayo mlemavu anaingia na baiskeli yake na kushuka nayo bila usumbufu ni vema hata Sumatra kuangalia uwezekano wa kuwajali walemavu hao . pia ni vizuri hata nyumba za ibada nazo ningeshauri baba askofu kuangalia kuweka mazingira " alisema Lukuvi.

Kuhusu ombi la walemavu hao hasa wale wasio sikia kuomba serikali kuwa na wakalimani katika kituo cha Televisheni ya Taifa (TBC) na vituo vingine vya luninga ili kuwawezesha walemavu hao nao kuweza kufuatilia hotuba ya Rais mwisho wa mwezi na mambo mengine badala ya kutengwa ,alisema kuwa suala hilo ni wajibu wa serikali kuwajali watu wake hivyo tayari imeuagiza uongozi wa TBC na mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) kulitafutia ufumbuzi suala hilo la mkalimani hasa katika TBC .

Katika hatua nyingine Lukuvi aliwataka walemavu hao ili ombi lao la kutazamwa katika nafasi za uongozi liweze kuzingatiwa ni vema wao wenyewe kujitokeza kwa wingi kuipigia kura katiba iliyopendekezwa pindi itakapokuja kwa wananchi kwa madai kuwa katika katiba hiyo imezingatia mambo mengi ya kijamii likiwemo la kuwajali watu wenye ulemavu kwa kuwatengea nafasi nyingi zaidi na iwapo katiba hiyo itapitishwa kazi ya msuguano wa rushwa unaweza kuhamia kwa walemavu kwa kila mmoja kutaka kupewa nafasi.

" Hadi hivi sasa ni chama cha mapinduzi (CCM) pekee ambacho kina wabunge wa viti maalum wa kuteuliwa kutoka kundi la walemavu huku vyama vingine vyote havijawakumbuka kabisa watu wenye ulemavu ukiacha mbunge wa jimbo la Lindi mjini pekee ambae hakupendelewa katika ubunge wake bali alishindwa kihalali kwa kuchaguliwa na wananchi wake..nafikiri tushirikiane kuhakikisha katiba hii iliyopendekezwa inapita ili tuungane pamoja katika kujenga nchi yetu "

Katika salam za walemavu waziri wa Afya na ustawi wa jamii Dkt Seil S. Rashid zilizotolewa kwa niaba yake na mwenyekiti wa baraza la watu wenye ulemavu nchini na Dunford Makala alisema kuwa wizara inaendelea kuimarisha ushirikiano na vyama vya watu wenye ulemavu na shirikiasho la vyama vya watu wenye ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) katika kuhakikisha utekelezaji wa uwekaji wa fursa na haki sawa kwa watu wenye ulemavu nchini .

Alisema katika kuhakikisha ushirikiano unakuwepo wizara yake imezindua baraza la ushauri la Taifa la watu wenye ulemavu toka mnamo 1 Novemba 2014 na katika hilo kamwe hawataacha kumpongeza Rais Dkt Jakaya Kikwete kwa kumteua mwenyekiti wa baraza hilo

Aidha alisema kuwa ni ukweli usiopingika kuwa nchi hii chini ya Rais Dkt Kikwete imefanya mambo mengi zaidi ya kuwajali watu wenye ulemavu katika Nyanja za kiuchumi ,kiutamaduni na kisiasa ambavyo vyote hivyo kumwezesha mlemavu kujikwamua kimaisha

Hata hivyo alisema ushahidi wa yote hayo ni pamoja na kuridhia mikataba ya kimataifa juu ya haki za watu wenye ulemavu , kutungwa kwa sharia Na.9 ya mwaka 2010 ya watu wenye ulemavu na kanuni zake ,kuwashirikisha watu wenye ulemavu katika tume ya mabadiliko ya katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania pamoja na kuteuliwa kwa wajumbe 20 wenye ulemavu katika bunge maalumu la mabadiliko ya katiba la mwaka 2014.

Awali walemavu hao katika risala yao iliyosomwa na makamu mwenyekiti wa SHIVYAWATA Amina Mollel pamoja na kuishukuru serikali kwa jinsi kwa kuendelea kuwa karibu zaidi na watu wenye ulemavu kwa kushiriki shughuli mbali mbali za walemavu ,bado waliweza kuishukuru serikali kwa kuandaa sera ya maendeleo ya watu wenye ulemavu ya mwaka 2004, kutambuliwa kwa watu wenye ulemavu katika MKUKUTA, kuwezesha kuongezeka kwa idadi ya watu wenye ulemavu wanaopata elimu kuanzia shule za msingi hadi elimu ya juu na mambo mengine mengi ambayo wao kama walemavu wamekuwa wakiona serikali yao ipo pamoja nao.

Sanjari na mema hayo bado waliiomba serikali kuzingatia kuwapatia walemavu mambo muhimu katika maisha ya kila siku ikiwa ni pamoja na kuwa na vyombo vya usafiri rafiki kama magari moshi.vyombo vya usafiri majini ,angani ,miundo mbinu katika majengo na viwanja vya ndege ambavyo vitamwezesha mlemavu pia kuwa huru .

Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza alisema kuwa maadhimisho hayo yaliyofanyika chini ya kauli mbiu isemayo " Maendeleo endelevu ;Ahadi ya Teknolojia huku mkoa wa Iringa ukiendelea kuwa bega kwa bega na walemavu ikiwa ni pamoja na kufanya kazi karibu na vyama hivyo vya watu wenye ulemavu na kuwa mkoa huo kwa sasa una jumla ya walemavu zaidi ya 179 ,000 na wote serikali imeendelea kuwalinda na kuwa nao pamoja. 

mwenyekiti wa baraza la watu wenye ulemavu Prof Edward Bagandashwa

Kamishina wa ustawi wa jamii Bw Dunford Makala akitoa salam zake

Viongozi mbali mbali wakiwa pamoja na kamati ya ulinzi mkoaMwenyekiti wa CCM mkoa Jesca Msambatavangu akiwa na viongozi wa chama cha walemavu Tanzania kushoto ni makamu mwenyekiti Bi Amina Mollel na katikati ni mwenyekiti wa baraza la watu wenye ulemavu Prof Edward Bagandashwa

Waziri Lukuvi akihutubia


Ndumbalo akipokea cheti toka kwa waziri LukuviWaziri Lukuvi akiteta jambo na mkuu wa mkoa wa Iringa Bi Amina Masenza (kulia)Waziri Lukuvi akimakabidhi cheti mwanafunzi mlemavu wa shule ya sekondari ya wasichana IringaKatibu wa chama cha Viziwi Tanzania Bw Shaibu Juma akiwa katika ulingo wa wasanii wa ngoma 
kutoka kikundi cha ViziwiWalemavu nchini wakiwa katika maandamano leo wakati wa kilele cha siku ya walemavu duniani kwa Tanzania maadhimisho hayo yamefanyika mkoa wa Iringa,kushoto ni mkalimani wa kujitolea ambae ni Mtangazaji wa radio Nuru Fm Bw Clement akisaidia kuwaelekeza walemavu haoHiki ndicho cheti ambacho kampuni ya Asas imepewa kutokana na ushiriki mzuri wa uchangiaji katika maadhimisho hayoWaandamanaji wakiwa katika maandamano hayo leo

Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu (sera na uratibu wa bunge) Wiliam Lukuvi akihutubia katika kilele  cha siku ya walemavu duniani ,maadhimisho yaliyofanyika katika viwanja vya kichangani mjini Iringa Kitaifa na Lukuvi kumwakilisha waziri mkuu Mizengo PindaWalemavu wakiwa katika maadhimisho hayo kitaifa mjini IringaMwenyekiti wa mkoa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu na mwenyekiti wa UWT wilaya ya  Iringa mjini wakipongezwa na waziri Lukuvi kwa kuunga mkono maadhimisho ya siku ya walemavu nchiniMakamu mwenyekiti wa Shivyawata Bi Amina Mollel akipongezwa na waziri Lukuvi kwa maandalizi mazuri.Walemavu wakiwa katika maandamano yao leoAskari wa usalama barabara Iringa aliyefahamika kwa jina la Sarehe Mollel akiongoza maandamano ya  watu wenye ulemavu leo wakati wa maadhimisho ya siku ya walemavu duniani yaliyofanyika kitaifa katika viwanja vya kichangani mjini Iringa na kuhudhuriwa na waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera na uratibu wa bunge Bw Wiliam Lukuvi kwa niaba ya waziri mkuu Mizengo Pinda
Taarifa ya Francis Godwin/MatukiodaimaBlog


Mazishi ya Mrakibu wa polisi Capt. Kidai SenzalaMaafisa wa Polisi wakiwa wamebeba sanduku lililohifadhi mwili wa Marehemu Capt. Kidai Senzala Kalise aliyefariki Novemba 29 mwaka huu katika ajali ya Helkopta iliyotokea Kipunguni B-Moshi Bar Dar es Salaam wakielekea katika makaburi ya familia huko Gonja Maore Wilaya ya Same mkoa wa Kilimanjaro Desemba 1, 2014.

Marehemu Kidai alikuwa Mrakibu wa Polisi na alizikwa kwa heshima zote za Kipolisi ikiwa ni kupigiwa mizinga na saluti mbalimbali za kipolisi kabla na baada ya maziko yake.

Helkopta aina ya Robertson R44 iliyo tolewa msaada kutoka kwa Taasisi ya Howard G. Foundation inayomilikiwa na mfanyabiashara mashuhuri nchini Marekani Bw. Warren Buffet ililetwa nchini kwa lengo la kukabiliana na vitendo vya ujangili na kupokelewa nchini na Waziri wa Maliasili na Utalii June 14, 2014 jijini Dar es Salaam na kuikabidhi kwa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) ilipata ajali majira ya saa nne asubuhi baada ya kupata hitlafu katika injili yake na kupoteza maisha ya Mrakibu wa Polisi Capt. Kidai Senzala Kaluse, Mkaguzi wa Polisi Capt. Simba Musa Simba, Konstebo wa Polisi, Josso Selestine na Capt. Joseph Khalfan wa Malisasili aliyezikwa Arusha.


Maofisa wa Polisi wakijiandaa kulibeba jeneza la Marehemu Capt Kidai.

 Wanafamilia wakiwa katika gari lililobeba mwili wa mpendwa wao Capt. Kidai Senzala.

 Maofisa wa Polisi wakiwa wamebeba sanduku la Mrakibu wa Polisi-Capt. Kidai.

 Heshima za Kihjeshi zikitolewa kabla ya jeneza kushushwa kaburini na kupigiwa mizinga.

 Heshima zikiendelea...Ndugu wa marehemu akiwepo mkewe, mama yake mzazi marehemu, dada zake na ndugu wengine wakitafakari kazi ya Mungu baada ya kufanyika kwa mazishi ya Capt. Kidai Senzala.

Picha taarifa kutoka kwa Mroki Mroki/Father Kidevu Blog

Castle Lite ilivyoufunga mwaka katika Just Got Paid

Party ya Just Got Paid ilifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita ikiwa ni ya mwisho kwa mwaka huu na kuwakutanisha wakazi mbalimbali wa jiji la Dar waliokutana kufurahia wikiendi ya mwisho wa mwezi. Paty hiyo inayodhaminiwa na bia ya Castle Lite ilitawaliwa na burudani ya muziki na vinywaji huku waliohudhuria wakipata nafasi ya kujumuika kutakiana mwisho mzuri wa mwaka.

Hizi ni baadhi ya picha kutoka party hiyo