Picha za Mbowe akiwanadi wagombea uongozi SM wa UKAWA

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe akihutubia katika mkutano wa Kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika katika viwanja Kata ya Vijibweni Kigamboni jijini Dar es Salaam. 


Mbowe akiwanadi wagombea

Umati wa watu wakimsikiliza Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe wakati wa mkutano wa kuwanadi wagombea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kupitia UKAWA katika Kata ya Vijibweni Kigamboni jijini Dar es Salaam.Habari picha: Francis Dande

Sheria Ngowi na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda

Mbunifu wa Kimataifa wa mavazi, Sheria Ngowi akimuonesha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda baadhi ya vitambaa vya kisasa vya suti ambavyo vitatuka kumtengenezea Waziri Mkuu juzi jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiangalia na kuchagua aina ya vitambaa vya suti amabvyo vitatumika kutengenza baadhi ya suti zake alipotembelewa na mbunifu wa Kimataifa wa mavazi, Sheria Ngowi juzi jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Mbunifu wa kimataifa wa Mavazi, Sheria Ngowi alipotembelewa juzi nyumbani kwake Masaki jijini Dar es Salaam.

Picha na: Atuza Nkurlu wa Sheria Ngowi Brand
Tumeshirikishwa na: Haki Ngowi

Tanzanians: Country will become middle-income by 2025

  • Tanzanians are optimistic about their future
  • Citizens think the country will become middle-income by 2025

4 December 2014, Dar es Salaam: More than half of citizens (54%) think their lives will be better in 2025. This is true among young and old, men and women, and rural and urban residents. This is in stark contrast to the United States and Europe where almost seven out of ten (65%) think that their children will be financially worse off than they are.

These findings were released by Twaweza and the Society for International Development (SID) in a research brief titled Tanzania in 2025: are Tanzanians optimistic about their future? The brief is based on data from Sauti za Wananchi, Africa’s first nationally representative high-frequency mobile phone survey that interviews households across Tanzania Mainland (Zanzibar is not covered in these results). The main findings are based on data collected from 1,408 respondents in August 2014.

Looking at the country in general, two out of three citizens believe that Tanzania will be a good place to live in 2025. This holds true regardless of levels of wealth; 64% of the wealthiest citizens and 68% of the poorest citizens see the future positively. Both personally and nationally, citizens are deeply optimistic about what is in store for the country.

However, some citizens are worried. Almost one out of five citizens (18%) fear that their lives will be worse in 2025 than today, and there are those who think the country will be a bad place to live in 2025. Here there are some differences between rich and poor; one out of four wealthy citizens (25%) and one out of five poor citizens (18%) are pessimistic about the future.

Whichever view citizens hold, they are certain that the outcome will be in Tanzanian hands. Nine out of ten citizens believe that Tanzanian leaders (54%) or citizens (37%) will have the most control over important decisions in the country. When it comes to their own lives, citizens are even more confident about their own agency; six out of ten think they themselves will have the most influence over their own future However, while one out of five rural citizens believe that the Government will have the strongest influence over their future welfare, no urban citizens mention the Government as an important incfluence. Aside from themselves, urban respondents mention their family (20%) and friends or peers (19%) as having influence over their future.

Looking more specifically, almost three out of four citizens (72%) are confident that Tanzania will be a middle-income country by 2025. Seven out of ten (68%) also think that there will be a female president by 2025 and six out of ten (64%) foresee a growth in manufacturing and reduction in agriculture. On the other hand, many citizens predict religious conflict (62%) and half (51%) expect a split of the United Republic of Tanzania. Whatever the future holds, citizens see big changes, with six out of ten predicting that the opposition will win the presidency and that elephants will disappear by 2025. Interestingly the two least likely scenarios are thought to be Tanzania qualifying for the World Cup (38%) and the formation of the East African Federation with one president (34%).

Citizens’ main concerns for the future are improvements in the quality of social services (28% see this as the main future priority) and economic growth (16% prioritise this).

Aidan Eyakuze, Associate Director of the Society for International Development, commented on the findings “Tanzanians are largely optimistic about their personal future, especially when compared with their peers in developed economies in the United States and Europe. This resilience and positivity is a huge asset. It enhances the country’s potential to move forward with confidence, It also places a burden on each one of us to ensure that we realize this positive vision for our country.”

Rakesh Rajani, Head of Twaweza, said “In a time of significant global and national change, citizens of all wealth classes, locations and gender, are optimistic about what the future holds for them in Tanzania. The challenge, for the Tanzanian Government, local elites and citizens themselves, is to ensure that this optimism is harnessed through good policy making and implementation, to promote equitable development and building social cohesion, so that citizens’ aspirations for a brighter future are met.”

Kuitwa kwenye usaili - Jeshi la Magereza04 Desemba 2014


KUITWA KWENYE USAILI

Jeshi la Magereza linawatangazia wafuatao kufika kwenye usaili kwa nafasi walizoomba. Usaili huo utafanyika kuanzia tarehe 10/12/2014 mpaka tarehe 17/12/2014 katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Magereza Ukonga Jijini Dar es salaam kuanzia 2:00 asubuhi kwa mujibu wa tarehe za makundi kama yalivyoainishwa. Kwa wale wa kidato cha Nne na Sita waliosailiwa kupitia Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wasubiri maelekezo mengineyo. Aidha wale ambao hawakuona majina yao hapa wahesabu kuwa hawakufanikiwa.

Waombaji wanatakiwa kuzingatia yafuatavyo;-

i. Kuja na Vyeti halisi (Original Certificates) vya elimu na ujuzi

ii. Kuja naCheti halisi cha kuzaliwa,

iii. Hati za matokeo ya mitihani (Result Slip/Statements) hazitakubaliwa isipokuwa kwa wahitimu ambao vyeti vyao halisi havijatolewa na vyuo husika wakiwa na barua Maalum ya kuthibitisha kwamba vyeti halisi havijatolewa,

iv. Wahusika watajitegemea kwa nauli za kuja na kurudi, chakula na malazi kwa kipindi chote cha usaili

Tangazo hili pia linapatikana kwenye Mbao za Matangazo zilizopo Bwalo Kuu la Magereza, tovuti ya magereza kwa anwani ya www.magereza.go.tz sanjari na blog ya magereza kwa anwani ya www.magereza.blogspot.com

Imetolewa na Kamishna Jenerali wa Magereza

J.C.Minja

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA

  • Bofya HAPA kupata orodha ya wanaotakiwa kufika kwenye usaili

Jaji Warioba na Zitto wateta pamoja kuhusu 'escrow'

Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba (kushoto), akizungumza na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe. Masaki Dar es Salaam jana.


Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba juzi alifanya mazungumzo ya saa mbili ya Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe kuhusu masuala ya uongozi na uwajibikaji baada ya mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini kumtembelea nyumbani kwake, Masaki, Dar es Salaam.

Katika mazungumzo hayo, Zitto pia alimweleza Waziri Mkuu huyo mstaafu maazimio ya Bunge kuhusu uchotwaji wa Sh306 bilioni katika Akaunti ya Tegeta Escrow.

Katika ujumbe wake mfupi alioutuma katika mtandao wa Facebook, Zitto alisema: “Nimekuwa na mkutano wa zaidi ya masaa mawili (saa mbili) na Mzee Warioba kuhusu masuala mbalimbali ya nchi yetu kama uongozi na uwajibikaji. Pia nimemweleza kwa ufupi kuhusu maazimio ya Bunge kuhusu Akaunti ya Tegeta Escrow.”

Kukutana kwa viongozi hao kumekuja ikiwa zimepita siku mbili tangu Jaji Warioba kuzungumza na gazeti hili kuhusu sakata la escrow na maazimio manane ya Bunge.

Zitto alimtembelea Jaji Warioba siku habari hiyo ilipochapishwa, kitendo ambacho kimetafsiriwa kama ni mbunge huyo kutolea ufafanuzi maoni ya Jaji Warioba ambaye pia amewahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali hasa kuhusu maeneo yaliyoachwa katika ripoti hiyo licha ya kuwa yanaonekana kuhusika katika kashfa hiyo.
Bunge lilihitimisha mjadala wa kashfa hiyo, kwa kupitisha maazimio manane, ikiwa ni pamoja na kuwawajibisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) Jaji Frederick Werema, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo; Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka na Katibu Mkuu wa Nishati na Madini, Eliakim Maswi.

Bunge hilo pia liliazimia kuwajibishwa kwa wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Tanesco pamoja na wenyeviti watatu wa kamati za kudumu za Bunge; Victor Mwambalaswa (Nishati na Madini), William Ngeleja (Katiba, Sheria na Utawala) na William Ngeleja (Bajeti).

Katika maoni yake juu ya kashfa hiyo, Jaji Warioba alisema Bunge limefanya makosa ya kutozijumuisha Wizara ya Fedha na ile ya Viwanda na Biashara katika uchunguzi huo kwa kuwa nazo zinahusika.

Alisema katika Ripoti ya CAG na PAC, wametaja ukiukwaji wa malipo ya kodi ya ongezeko la mtaji (capital gain) na ushuru wa stempu (stamp duty) na kuwa wanaohusika katika hilo ni Wizara ya Fedha na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na upande mwingine ni Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) ambao uko chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara.

Alisema hata kampuni iliyotajwa kuwa imesajiliwa Brela inaonyesha katika ripoti kuwa wahusika walioisajili hawakuweka majina yao, bali saini tu.

Alifafanua kuwa uamuzi wa Bunge uliilenga Wizara ya Nishati na Madini lakini hasara iliyotajwa kuonekana inazihusu zaidi Wizara ya Fedha na ile ya Viwanda na kusisitiza kuwa uamuzi wa Bunge ulitawaliwa na mchezo wa siasa, kwamba baadhi walindwe na wengine waachwe.

Jaji Warioba alisema kasoro nyingine ni kitendo cha watu wanaodaiwa kupewa fedha na James Rugemalira kutajwa majina yao sambamba na akaunti ya aliyewapa, lakini wale waliodaiwa kuchota fedha hizo katika magunia hawakutajwa.

Pia, alisema haamini kama fedha za escrow ni za Serikali na kuhoji kama zingekuwa za umma zingewekwa katika akaunti hiyo kwa misingi ipi?

Katika maazimo yake Kamati ya PAC ilieleza kuwa uchunguzi kuhusu sakata hilo uliofanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ulieleza kuwa fedha za umma zinaweza kuwamo katika akaunti hiyo.

Aua mtoto, mama mkwe na kujiua; Mke anusurika

MKAZI wa kitongoji cha Ng’anandi kijiji cha Mpinga, Kata ya Kigwe, Wilayani Bahi, Jumanne Ichirile (23) amefanya mauaji ya kinyama kwa kuwaua mama mkwe wake, mtoto wake mwenye umri wa miaka miwili kwa kuwachoma visu.

Pia katika tukio hilo alimjeruhi mkewe, kabla ya kujiua kwa kujichoma na kisu tumboni kutokana na wivu wa kimapenzi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) David Misime amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo Jumamosi iliyopita.

Waliouawa wametajwa kuwa ni Sarah Mango anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka kati ya 60 na 70 na mtoto Amina Jumanne mwenye umri wa miaka miwili ambao waliuawa kwa kucharangwa kwa visu sehemu mbalimbali za miili yao.

Akisimulia mkasa huo, mke wa marehemu ambaye alijeruhiwa katika tukio hilo Elizabeth Kulwa (21) , alisema akiwa nyumbani kwa mama yake mzazi Sarah Mango ilipofika majira ya saa 11 jioni akivamiwa na mume wake Jumanne Icherile huku akiwa amekishika kisu mkononi.

Alisema ghafla alianza kumshambulia na kisha kumchoma kisu tumboni mara mbili na katika sehemu mbalimbali za mwili wake.

“Kabla hajaanza kunishambilia alikuwa akisema ananitaka mimi na mtoto ili tuondoke wote jambo ambalo mama alilipinga ndipo akaanza kumshambulia mama yangu mzazi kwa kumchoma visu sehemu mbalimbali za mwili wake, kisha akamgeukia mtoto na kuanza kumchoma visu” alisema
Alisema hii si mara ya kwanza kwa mwanaume huyo kumshambulia kwani hata mwaka jana alifanya hivyo kwa kumkatakata kwa mapanga yeye na mama yake.

Alisema katika shambulio hilo walifanikiwa kuripoti kwenye vyombo vya sheria na kisha kesi ikafunguliwa mahakamani ambapo mumewe alihukumiwa kifungo cha miezi minane gerezani.
Hata hivyo mama huyo hana kumbukumbu mumewe huyo alitoka gerezani lini lakini anachokumbuka ni miezi ya hivi karibuni.

Alisema mara baada ya kutoka gerezani alifika nyumbani kwa mama mkwe wake ili kumshawishi arudiane na mkewe jambo ambalo mama huyo hakukubaliana nalo.

“Kitendo cha mama kumkatalia kilikuwa cha busara kwani alikuwa akinishambulia mara kwa mara , kitendo cha mama kumkatalia kumtia hasira” alisema.

Kulwa sasa amelazwa katika hospitali ya mkoa wa Dodoma kwa matibabu amejeruhiwa vibaya kwenye ziwa la kushoto, mbavuni , tumboni na mkononi.

Diwani wa Kata ya Kigwe, Gaitani Mwinga, amelaani mauaji ya watu kujichukulia sheria mkononi.
Kwa upande wake Kamanda Misime akizungumzia matukio ya mauaji kwa kutumia silaha za jadi, alisema Jeshi la Polisi limewaagiza Polisi Kata kutoa elimu kwa wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi ili kuepuka uvunjaji wa sheria.

Alisema tayari amewaagiza Polisi kata wote mkoani Dodoma kuhakikisha wanatoa elimu kwa wananchi kuacha mara moja kutembea na silaha za jadi kwa sababu kufanya hivyo ni kosa la jinai.
Aliwataka watu wenye malalamiko kuyafikisha kwenye vyombo vya sheria ili hatua ziweze kuchukuliwa kwa mujibu wa sheria.

---
  • Taarifa ya Sifa Lubasi wa Habarileo, Dodoma

Usikose! The night of Kings @DarLive

Anza kuzichanga sasa, jiji zima kuhamia Mbagala Dar Live!Hofu ya kutumia condoms kwa madai zinachangia maambukizi ya VVU

MATUMIZI ya kondomu bado ni ya kiwango cha chini mkoani Njombe jambo linaloelezwa na shirika la TMarc Tanzania kwamba linachangia kuyafanya maambukizi ya virusi vya UKIMWI (VVU) yawe juu.

Moja ya sababu ni uzushi kwamba kondomu zimepandikizwa magonjwa hazifai kutumika.

Kwa mujibu wa Meneja Mahusiano na Mawasiliano wa TMarc Tanzania, Maurice Chirimi shirika hilo linafanya kazi ya uraghibishi wa mambo ya afya kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo Wizara ya Afya na washirika mbalimbali wanochangia sekta hiyo.

Takwimu za Tume ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS) za mwaka 2012 zinaonesha mkoa wa Njombe unaongoza kitaifa kwa kuwa na asilimia 14.8 ya maambukizi.

Chirimi alisema mbali na kutoa elimu, shirika lao limekuwa likisambaza kondomu za kiume aina ya dume, za kike aina ya red pepeta pamoja na vidonge vya uzazi wa mpango.

“Tunafanya yote hii katika jitihada zetu za kuunga mkono juhudi za serikali na washirika wake katika kukabiliana na janga la UKIMWI,” alisema.

Katika usambazaji wa kondomu hizo, Chirima alisema baadhi ya watu wamekuwa wakipuuza matumizi yake kwa madai kwamba zimepandikizwa magonjwa.

Alisema kwa mkoa wa Njombe muitikio wa matumizi yake ni mdogo hali inayochochea maambukizi ya VVU tofauti na mikoa mingine nchini.

Alisema mwaka uliopita TMarc ilisambaza kondomu dume milioni moja ambazo hata hivyo hazikwisha kwasababu ya mwitikio huo mdogo.

“Shida tunayoiiona katika mazingira haya ni kwamba watu hawaziamini kondomu lakini wanaamini sana katika matumizi ya dawa za kufubasha VVU” alisema.

Alisema ni muhimu kwa mtu anayeshindwa kuwa mwaminifu kwa mpenzi wake aliyepima akatumia kondomu ili kujinusuru na maambukizi mapya.

Akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani, Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Dk Rehema Nchimbi alisema wanaompango wa miaka mitatu wa kukabiliana na janga hilo.

Kwa kupitia mpango huo ulioanza kutekelezwa Julai mwaka jana, Dk Nchimbi alisema mbali ya kuhimiza matumizi ya kondomu, mpango huo unaendelea kuboresha huduma za tohara.

“Mkoa una vituo 13 vya kutolea huduma ya tohara na lengo letu ni kuona ifikapo mwaka 2017 jumla ya wanaume 163,495 mkoani hapa ambao hawajatahiriwa wawe wametahiriwa,” alisema.

Basic Principles in Occupational Hygiene Course

The short course "Basic Principles in Occupational Hygiene Course" focuses on how to anticipate, evaluate, prevent, and control a wide range of hazards in the workplaces. 

This course is designed for participants with direct responsibility for industrial hygiene, employees’ health and safety, and prevention of work-related injuries and diseases. 

Participants will learn the concepts critical to creating a safe work environment and sharpen their technical expertise in protecting employees from workplace hazards. 

Tumeingizwa tena mkenge katika kashfa ya 'Tegeta escrow account'?


Waingereza wana msemo ambao unatafsirika kwa Kiswahili kama "chuki ya pamoja ni mwanzo wa urafiki mkubwa." Kimahesabu kama A hapatani na B, na A anamchukia C kama ambavyo B anamchukia pia C, basi chuki ya A na B kwa C yaweza kuwa mwanzo wa wawili hao A na B kuwa marafiki wenye lengo la kumwangamiza C.

Binafsi, naomba kukiri kuwa kwa muda sasa nimekuwa siafikiani na mitizamo na mwenendo wa mwanasiasa mahiri wa upinzani, Zitto Kabwe. Siwezi kusema nina chuki dhidi yake bali mie sio miongoni mwa supporters wake.Pamoja na sababu nyingine, kubwa ni kile ninachokitafsiri kama mwanasiasa huyo kutanguliza mbele maslahi yake binafsi badala ya chama chake yaani Chadema. Kwa mtizamo wangu, mgogoro uliopelekea hatua ya Chadema kumvua madaraka Zitto ni matokeo ya 'imani potofu' kuwa kuna mwanasiasa anayeweza kuwa maarufu kuliko chama chake, Si kwamba haiwezekani kabisa kwa hilo kutokea lakini si kwa hatua waliyofikia Chadema hivi sasa.

Lakini lengo la makala hii si kumjadili Zitto wala ugomvi kati yake na Chadema. Ila nimegusia suala hilo kwa sababu nililazimika 'kurejesha urafiki' na mwanasiasa huyo, angalau kinadharia, wakati akifanya jitihada kubwa binafsi na kama mwenyekiti wa PAC kushughulikia ufisadi wa Tegeta Escrow. Kwa kutumia mfano huo hapo juu wa chuki za A kwa C na za B kwa C, na A ni Zitto, na B ni mie, huko C wakiwa mafisadi wa Escrow, basi 'urafiki' usingeepukika.

Hakuna Mtanzania atakayeshindwa kumpongeza Zitto na Kafulila pamoja na PAC kwa ujumla walivyofanya kazi kubwa na nzuri katika kushughulikia skandali hiyo. Nina imani hata wahusika wa ufisadi huo wa Escrow wanamkubali kwa jinsi alivyowakalia kooni...ALMOST.

Hata hivyo, mara baada ya kumalizika kwa 'timbwili' hilo la Escrow bungeni, nilitumiwa meseji na 'mjuzi mmoja wa mambo ya huko nyumbani' ambaye alidai kuwa pamoja na kazi nzuri iliyofanywa na PAC, kuna 'mchezo mchafu' uliofanyika katika kufikia mwafaka miongoni mwa wajumbe, hususan wale wa kutoka CCM. Alidai kuwa kilichowezesha mwafaka huo kufikiwa ni pamoja na 'kumnusuru' Rais Jakaya Kikwete, ambaye kama Mbunge Tundu Lissu alivyobainisha bungeni, anatajwa kuhusika katika skandali hiyo. Kimsingi, hoja ya Lissu, ambaye pia aliilaumu Idara ya Usalama wa Taifa kwa kutowajibika ipasavyo katika mlolongo wa skandali mbalimbali zinazougubika utawala wa Rais Kikwet, iliuawa kimyakimya licha ya umuhimu wake mkubwa.

Hata hivyo, kwa uelewa wangu, jaribio lolote la kumhusisha Rais Kikwete na skandali hiyo hata kama ushahidi upo lingepelekea mparaganyiko mkubwa katika kamati hiyo ya Zitto. Na kama tulivyoshuhudia 'makada' wa CCM huko bungeni walivyopigana kufa na kupona hadi Waziri Mkuu Mizengo Pinda akanusuriwa, kwa hakika ishu ya Kikwete kuhusishwa na Escrow ingepelekea bunge hilo kuvunjika pasi kufikia hitimisho.

Lakini what if mkakati huo wa 'kumnusuru Rais Kikwete' unabeba mengi zaidi ya tunavyodhani?

Kwa kifupi, tume-settle for less. Na Waingereza wana msemo unaotahadharisha kuhusu ku-settle for less, ambapo wanasema 'pindi ukikubali kupokea pungufu ya unachostahilki basi hatimaye utaishia kupokea pungufu zaidi ya kile ulichostahili awali.' Japo ni mapema kuhitimisha kwamba 'tumeingizwa mkenge,' lakini ukimya wa Rais Kikwete katika kutekeleza maazimio ya Bunge kuhusu Escrow umeanza kuzua wasiwasi.

Na 'kigugugmizi' kinachomkabili Rais Kikwete kina sababu kadhaa za wazi. Kwa mfano, kumtimua Mwanasheria Mkuu Jaji Werema kunaweza kupelekea kuzuka kwa skandali nyingine iwapo Jaji huyo ataamua 'mmemwaga mboga, na mie namwaga ugali' kwa maana anajua mengi yaliyojiri na yanayojiri katika utawala wa Rais Kikwete. Japo si kwamba haiwezekani kumtimua na kisha kumfunga mdomo, lakini historia ya wanasheria wakuu huko nyuma inapaswa kutukumbusha jinsi 'wanavyobebwa' kwa minajili ya 'kutotengeneza uadui na mtu anayejua siri nyingi.'

Kwa upande wmingine, ni muhimu kukumbuka kuwa kimsingi Rais Kikwete ndo aliyemleta Profesa Muhongo katika frontline politics. Hawa ni marafiki wa karibu. Na hadi sasa Muhongo ameendeleza jeuri yake ya kisomi na kusisitiza kuwa fedha za Escrow si za umma. Msimamo huo pia washikiliwa na Waziri Mkuu Pinda. Je kuna anayefahamu msimamo wa Rais Kikwete? Maelezo yanaonyesha kuwa yeye aliridhia malipo ya Escrow kufanyika. Je amebadili mawazo na kutambua kuwa hilo lilikuwa kosa?

Lakini wakati tayari tunafahamu majina mengi ya walionufaika na mgao wa Escrow kupitia Benki ya Mkombozi, inadaiwa kuwa mgao mkubwa zaidi uliopitia Benki ya Stanbic ulihusisha vigogo kadhaa lakini hadi muda huu hakuna jina hata moja lililowekwa hadharani. So far, gazeti la Raia Mwema limeripoti kuwa mke wa kigogo momja mwandamizi huko Ikulu alikatiwa shilingi bilioni 5. Sasa huhitaji kujua hesabati vizuri kubashiri kwamba kama mke wa kigogo alikatiwa mbilioni tano, mumewe alipewa kiasi gani?


Hayo yote tisa, kumi ni kauli niliyokumbana nayo muda mfupi uliopita, na ambayo kwa hakika ndio iliyonisukuma kuandika makala hii. Kauli hiyo ni ya Jaji Mkuu Chande ambayo kimsingi inaharibu mwenendo wa kesi yoyote itakayofunguliwa dhidi ya wahusika wa ufisadi wa Escrow. Nimeinukuu kwa picha hapa chini.


Je Jaji Mkuu alikuwa anatoa tu tahadhari au alikuwa akifikisha ujumbe mahsusi kwamba hata tukiwapeleka mahakamani wahusika wa Escrow, utetezi wao upo bayana...kwamba walishahukumiwa bungeni. Na kama Jaji Mkuu 'hakutumwa' basi kwa hakika amewapatiwa washtakiwa-watarajiwa ushauri mzuri wa bure kisheria kuhusu jinsi ya kupambana na kesi yoyote watakayofunguliwa kuhusisna na suala hilo: wajitetee kuwa walishahukumiwa na bunge, na mawakili waoa waweza kutumia kauli hiyo ya Jaji Mkuu kama supporting evidence.

Anyway, pengine ni mapema mno kuhukumu lakini kama ambavyo Mzee Warioba alivyoonyesha mapungufu ya taarifa ya PAC na maazimio ya bunge kuhusu skandali ya Escrow, sintomshangaa mtu yeyote atakayeanza kupatwa na wasiwasi kuwa tumeingizwa mkenge...TENA.

Sijui msomaji mependwa unaonaje.

---

Viongozi wa CHADEMA katika ziara nchini Ubelgiji


Makamu wa Rais wa Bunge la Ulaya (EP), Rainer Wieland akizungumza jambo na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Zanzibar, Salum Mwalimu na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana (BAVICHA), Patrobas Katambi. Ujumbe wa CHADEMA ukiongozwa na mwanadiplomasia mahiri Profesa Abdalla Safari, uko nchini Ubelgiji kwa ziara ya kikazi kufuatia mwaliko wa bunge hilo.


Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, Profesa Safari Abdalla akisalimiana na Makamu wa Rais wa Bunge la Ulaya (EP) Rainer Wieland wakati ujumbe wa CHADEMA ulioko nchini Ubelgiji, ulipofika ofisi za bunge hilo mjini Brussels kwa ajili ya ziara ya kikazi. Wengine kutoka kulia ni Mwenyekiti wa BAVICHA, Patrobas Katambi, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu, Katibu Mkuu wa BAWACHA, Grace Tendega na Mkurugenzi wa Bunge na Halmashauri John Mrema.


Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demoikrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, Profesa Abdalla Safari na Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Zanzibar, Salum Mwalimu wakiwa kwenye mazungumzo na Makamu wa Rais wa Bunge la Ulaya (EP), Rainer Wieland, wakati ujumbe wa CHADEMA ulipofika Ofisi za EP kuanza ziara ya kikazi kufuatia mwaliko wa bunge hilo.


Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, Profesa Abdalla Jumbe Safari akiwa na Makamu wa Rais wa Bunge la Ulaya (EP), Rainer Wieland, walipokutana jana mjini Brussels, Ubelgiji kwa mazungumzo, ikiwa ni sehemu ya ziara ya kikazi ya ujumbe wa CHADEMA kufuatia mwaliko wa bunge hilo.

Tahadhari ya SUMATRA kwa wasafirio msimu huu wa sikukuu


Katibu Mtendaji wa Baraza la Ushauri la Watumiaji Huduma za Usafi wa nchi kavu na Majini, Dk Oscar Kikoyo akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es salaam jana juu ya hali ya usafiri kipindi cha siku kuu za Krismas na mwaka mpya ambapo ametahadharishja abiria kuto kukubali kutozwa nauri za juu na pindi ikitokea hivyo Sumatra ipewe taarifa haraka. Soma taarifa kamili hapa chini. Source Father Kidevu Blog.  • JEDWALI LA NAULI HALALI ZA MABASI YA MIKOANI


Kauli ya NBC kuhusu taarifa za wizi wa fedha za wateja

Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Rukia Mtingwa (kulia) akitoa ufafanuzi kuhusu tatizo lililojitokeza jana katika huduma zao za kibenki kupitia mtandao wa simu za mkononi (Mobile Banking) ambapo alisema licha ya wateja kutoona salio katika akaunti zao hakuna hata senti moja iliyopotea. Kushoto ni Kaimu Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa NBC, Jimmy Myalize.

Uongozi wa NBC umebaini kuwepo kwa ujumbe kupitia mitandao ya jamii unayohusisha NBC na wizi wa fedha za wateja kwa kupita mashine za kutolea fedha (ATM). Ujumbe huo huo unahamasisha wateja kutoa fedha kwenye akaunti zao.

NBC tunapenda kuwafahamisha wateja wetu na umma kwa ujumla kwamba ujumbe huo hauna ukweli wowote. Papo hapo, matukio ya miamala ya wizi ni tatizo ambalo linaendelea kutafutiwa utatuzi na mabenki yote yaliyo chini ya Chama cha Mabenki Tanzania (TBA).

Tunapenda kuwahakishia wateja wetu na umma kwamba NBC inaendelea kudhamiria kuwapatia wateja wetu huduma bora na ya kisasa.

Imetolewa na uongozi

Kaimu Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Jimmy Myalize (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo akitoa ufafanuzi wa tatizo la huduma za kibenki kupitia mtandao wa simu za mkononi (Mobile Banking) ambapo alisema licha ya tatizo hilo hakuna hata senti moja ya mteja wao iliyopotea. Kulia ni Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano, Rukia Mtingwa.


NBC management has of recent come across messages that are circulating within the social media channels carrying stories that NBC has become a victim of mass fraud ATM transactions in customers’ accounts, and urging customers to withdraw their balances.

NBC would like to inform our esteemed customers and the general public that the stories circulating in the social media are unfounded. However, ATM fraud transactions, also known as Card Skimming, are an industry wide concern that is jointly being resolved by all commercial banks under the auspices of Tanzania Bankers Association (TBA).

NBC wishes to once again reassure our customers and the general public that the messages circulating in the social media channels are unfounded. NBC remains committed to serving our customers in the most convenient and innovative manner.

Issued by Management

Tanzania na Saudia zatia saini mkopo wa zaidi ya bilioni 45/=

Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum (kushoto) akisaini mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu kwa serikali ya Tanzania kwa niaba ya Serikali ya Tanzania leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Saudia Mhandisi Hassan Al-Attas.

Serikali ya Tanzania imesainiana mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wa zaidi ya shilingi bilioni 45.2 na Shirika la Maendeleo la Saudia kwa lengo la kuboresha miradi wa maji kwa wilaya ya Same, Mwanga na ujenzi na ukarabati wa barabara Visiwani Zanzibar.

Mkataba huo umesainiwa leo jijini Dar es salaam na Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Saudia Mhandisi Hassan Al-Attas.

Akiongea na waandishi wa habari katika hafla hiyo, Waziri Saada alisema kuwa kati ya mkopo huo shilingi bilioni 41.25 ambazo ni sawa na Dola za Kimarekani milioni 25 zitagharimia mradi wa maji katika wilaya za Same na Mwanga na shilingi bilioni 3.96 kwa ajili ya maradi wa barabara Pemba, visiwani Zanzibar.

Waziri Saada alilishukuru Shirika la Maendeleo la Saudia kwa jitihada zao za kuisaidia Serikali ya Tanzania katika kautatua tatizo la maji wilaya za Same na Mwanga pamoja na uboreshaji wa barabara katika visiwa vya Pemba.

Aidha, mradi wa maji wa Same- Mwanga utagharimu Dola za Kimarekani milioni 110.34 ambazo benki ya BADEA, Shirika la Maendeleo Kuweit, OPEC na mashirika mengine wamekubali kukamilisha sehemu ya fedha iliyobakia.

Mradi wa maji wa Same- Mwanga baada ya kukamilika utasaidia kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji vijijini amabapo utasaida kuboresha hali ya maisha wa wananchi wa maeneo hayo, upatikanaji nwa maji safi na salama kwa maendeleo ya afya za wakazi hao na kuboresha uchumi wao kwa kutumia muda mwingi kwa shuighuli za uzalishaji mali badala ya kutumia muda mwingi kutafuta maji.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Saudia Mhandisi Hassan Al-Attas amesema kuwa makataba waliosaini leo unaonesha kuwa Saudi Arabia iko mstari wa mbele katika kuendelea kuiunga mkono Serikali ya Tanzania katika kukuza uchumi wake kwa kuzingatia mahusiano mazuri yaliyopo kati ya nchi hizo.

Hafla hiyo ilihudhuriwa waandishi wa habari na baadhi ya watumishi wa wizara ya Fedha na wawakilishi wa Serikali ya Saudi Arabia.

 Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum (kushoto) akibadilishana hati ya mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu kwa serikali ya Tanzania waliosaini kwa niaba ya Serikali ya Tanzania leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Saudia Mhandisi Hassan Al-Attas.


Baadhi ya waandishi wa habari na watumishi wa wizara ya Fedha pamoja na wawakilishi wa Serikali ya Saudi Arabia wakiwashuhudia Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum na Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Saudia Mhandisi Hassan Al-Attas wakisaini mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu kwa serikali ya Tanzania leo jijini Dar es salaam.

Picha na Taarifa kutoka kwa Eleuteri Mangi / Maelezo

Taarifa ya DAWASCO kuhusu hitilafu ya mtambo wake wa maji

Shirika la Maji Safi na Majitaka Dar-es-salaam (DAWASCO), linawatangazia wakazi wa KIMARA na TABATA; Miji ya Kibaha na Mlandizi mkoani Pwani kuwa, Mtambo wa kuzalisha Maji wa Ruvu Juu umepata hitilafu kuanza siku ya Jumatano ya tarehe 03.12.2014 baada ya kuharibika kwa pampu moja ya kusukuma Maji (Pre-lift pump).

Hali hii imelazimisha kupungua kwa uzalishaji Maji.

Mafundi wa DAWASCO wanaendelea na matengenezo na kuhakikisha Pampu hii inafanya kazi na Huduma ya Maji itarejea katika hali ya kawaida ifikapo siku ya Jumapili tarehe 07/12/2014
Wakazi wa maeneo yafuatayo wataathirika; MLANDIZI, KIBAHA, KIBAMBA, MBEZI, KIMARA, UBUNGO, MSEWE, KIBANGU, RIVERSIDE, BARABARA YA MANDELA, TABATA, NA SEGEREA.

PIGA SIMU KITUO CHA HUDUMA KWA WATEJA NAMBA 022- 2194800/ 0659-574012
DAWASCO INAWAOMBA RADHI KWA USUMBUFU AMBAO NI WA DHARULA.

IMETOLEWA NA OFISI YA UHUSIANO
DAWASCO-MAKAO MAKUU
“DAWASCO TUTAKUFIKIA”

Mbunge wa Chalinze atoa wito kwa makampuni ya mawasiliano

Mkuu wa Idara ya Uuzaji na usambazaji bidhaa wa Vodacom Tanzania Upendo Richard (kulia) akimfafanulia jambo kuhusiana na simu aina ya Vodafone Smart Kicka, Mbunge wa jimbo la Chalinze, Pwani Mhe. Ridhiwani Kikwete (katikati) mara baada ya kuzindua duka jipya la Vodacom Tanzania lililopo Chalinze mjini Mkoa humo, Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Umma wa kampuni hiyo Matina Nkurlu.

Mbunge wa jimbo la Chalinze mkoani Pwani Mh. Ridhiwani Kikwete,ametoa ushauri kwa Makampuni ya Mawasiliano kufungua zaidi vituo vya kutoa huduma kwa wateja mkoani Pwani na maeneo mengine ya miji midogo inayokua kwa kasi ili kuwawezesha wateja wake kupata huduma kwa karibu badala ya kuzifuata mbali na kupoteza muda mwingi ambao wangeutumia kufanya shughuli za uzalishaji.Alitoa ushauri huo wakati akifungua duka la Vodacom Tanzania lililopo Chalinze mjini ambapo pia alitoa pongezi kwa hatua hiyo.

Katika kuhakikisha wakazi wa vitongoji vya Chalinze na maeneo jirani ya Ruvu,Miono,Gwata wanapata huduma kwa karibu,Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania leo imefungua duka jipya katika eneo la Chalinze.

Chalinze ni moja ya kituo maarufu katika mkoa wa Pwani ambacho wanapitia wasafiri wengi wanaotumia barabara ya Morogoro pia ni makutano ya barabara ya kuelekea mikoa ya Kaskazini ya Moshi,Tanga na Arusha.Vilevile mji huu unakuwa kwa kasi kutokana na kuongezeka kwa wafanyabiashara wanaowekeza eneo hili.

Duka hili jipya lenye mazingira rafiki kwa wateja litakuwa linatoa huduma mbalimbali kwa wateja wa Vodacom ikiwemo huduma kwa mawakala wa M Pesa na uuzaji wa bidhaa za Vodacom na litawawezesha wateja wa Chalinze na vitongoji vyake wakiwemo wasafiri wanaoelekea mikoa mballimbali na nje ya nchi kupata huduma bora.Mtandao wa Vodacom unaongoza kwa kupatikana vizuri na umeenea sehemu zote katika mkoa wa Pwani.

Mkuu wa Idara ya Uuzaji na usambazaji bidhaa wa Vodacom Tanzania Upendo Richard wa Vodacom Tanzania, alisema ufunguzi wa duka hili la kisasa ni mwendelezo wa malengo ya Vodacom kuendeleza kuboresha maisha murua kwa kila mtanzania kwa kupata huduma za kampuni hiyo zenye ubora na kuwafikia wateja kwa urahisi zaidi popote pale walipo ikiwemo huduma mpya ya kilimo klabu inayolenga kuwawezesha wakulima nchini.

“Uzoefu na utafiti umetuonyesha kuwa wananchi wanataka ubora,kama mtandao unaoongoza nchini tumejizatiti kuhakikisha tunafanya ubunifu wa hali ya juu wa kiteknolojia ili kutumia mtandao wa simu kuboresha maisha ya wananchi ikiwemo kutoa huduma bora na ndio maana tunazidi kufungua maduka kama haya kwa ajili ya kuwasogezea karibu wananchi huduma bora,na ninawahakikishia kuwa popote wateja wetu walipo tutawafikia na tunawashukuru sana wateja wetu kwa kutuunga mkono na tunawakaribisha ambao hawajajiunga na familia ya Vodacom kujiunga na kupata huduma bora kwa gharama nafuu.”Anasema Richard

Vodacom ina mtandao wa maduka 85 na wakala mbalimbali wakuuza bidhaa zake nchini na duka lililofunguliwa leo ni la 3 kufunguliwa katika mkoa wa Pwani.


Mbunge wa jimbo la Chalinze mkoani Pwani Mh. Ridhiwani Kikwete(kushoto) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa duka jipya la Vodacom Tanzania lililopo Chalinze mjini Mkoa humo. Katikati ni Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu,(kulia)Mkuu wa Idara ya Uuzaji na usambazaji bidhaa wa kampuni hiyo Upendo Richard. Hafla hiyo imefanyika leo mkoani humo.


Mbunge wa jimbo la Chalinze mkoani Pwani Mh. Ridhiwani Kikwete wapili kutoka kulia ,akigonganisha glasi za mvinyo na baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania ikiwa ni ishara ya kusherehekea uzinduzi wa duka jipya la kampuni hiyo alilolizindua lililopo Chalinze mjini Mkoa humo. Hafla hiyo imefanyika leo mkoani humo.


Mkuu wa Idara ya Uuzaji na usambazaji bidhaa wa Vodacom Tanzania Upendo Richard(kushoto)akimfafanulia jambo Mbunge wa jimbo la Chalinze mkoani Pwani Mh. Ridhiwani Kikwete (kulia) alipofika kuzindua duka jipya la Vodacom Tanzania lililopo Chalinze mjini Mkoa humo,Kulia kwa Mheshimiwa ni Meneja Uhusiano wa Umma wa kampuni hiyo Matina Nkurlu.


Duka jipya la Vodacom Tanzania lililopo Chalinze mjini Mkoa wa Pwani.


Mbunge wa jimbo la Chalinze mkoani Pwani Mh. Ridhiwani Kikwete wanne toka kulia akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania,baada ya kuzindua duka jipya la kampuni hiyo lililopo Chalinze mjini Mkoani humo.

Msimu wa pili Siri ya Mtungi kuanza kuonyeshwa


Baadhi ya waigizaji wa tamtilia ya Siri ya Mtungi katika picha ya pamoja

Tamthilia ya Siri ya Mtungi imezinduliwa rasmi na kutarajiwa kuanza kuonyeshwa kupitia TBC1. Akizungumza katika uzinduzi huo muongozaji wa tamthilia hiyo ndugu Jordan Riber amesema msimu hu unatarajiwa kufungua vitendawili vingi ambavyo havikukamilika katika msimu wa kwanza na kuwahakikishia mashabiki watarajie kuona msisimko wa kipekee.