Mabati-Cornell Kiswahili Prize for African LiteratureCORNELL UNIVERSITY COLLEGE OF ARTS AND SCIENCES

FOR IMMEDIATE RELEASE

November 21, 2014

Contact: Linda Glaser

Phone: (607) 255-8942

E-Mail: [email protected]

Major New Prize for African Literature Announced

ITHACA, N.Y. – A major new award, the Mabati-Cornell Kiswahili Prize for African Literature, was announced today in Nigeria at the Ake Art & Books Festival in Abeokuta, Nigeria. The prize recognizes excellent writing in African languages and encourages translation from, between and into African languages.

Renowned author Ngugi Wa Thiong’o, a Board member, said that the Mabati-Cornell prize is a “major intervention in the struggle for writing in African languages, for their place and visibility in the global sun of literary imagination. Prizes have generally been used to drown African Literature in African languages under a Europhone flood. With the Mabati-Cornell prize the dreams of Diop, A.C. Jordan, Obi Wali and others are very much alive. I hope that this prize becomes an invitation for other African languages to do the same and much more.”

Over 140 million people speak Kiswahili in Eastern and Southern Africa; Kiswahili is also one of the official languages in Kenya and Tanzania. The Prize will be awarded to the best unpublished manuscripts or books in Kiswahili published within two years of the award year across the categories of fiction, poetry and memoir, and graphic novels. First prize winners receive $5,000 in the categories of prose and poetry; second prize in any genre is $3,000 and third prize is $2,000.

The winning entry will be published in Kiswahili by East African Educational Publishers (EAEP) and the best poetry book will be translated and published by the Africa Poetry Book Fund. Award ceremonies will be held at Cornell University, and in Kenya and Tanzania. The four prize winning writers will spend a week in residence at Cornell and a week at an additional partner institution.

Cornell English professor Mukoma Wa Ngugi, prize co-founder, said the prize recognizes that all languages are created equal and no one language should thrive at the expense of others. “But beyond that recognition, the Prize sets an historical precedent for African philanthropy by Africans and shows that African philanthropy can and should be at the center of African cultural production.”

Sarit Shah, director of Prize sponsor Mabati Rolling Mills, Kenya, said that “supporting literature and literacy is crucial to the development of a thriving culture, and Mabati Rolling Mills is proud to provide financial support for the foundation of a new venture in African language publishing. The new prize for Kiswahili Literature seeks to reward East African writers, artists and thinkers who, through their work, encourage literacy at all levels of East African society. We believe it is vital to reconnect the world of ideas with the practical world of business and commerce.”

Literary critic Lizzy Attree, who co-founded the Prize with Wa Ngugi, noted that while there exist international literary prizes for African writing such as the Caine Prize and the recently established Etisalat Prize, there are no major international and Pan-African literary prizes awarded to works produced in an African language. “The Mabati-Cornell Kiswahili Prize makes an important contribution to the body of world literature; the establishment of this new literary prize sets a precedent for other literature in African languages to follow.”

Laurie Damiani, Director of International Initiatives at Cornell University’s Office of the Vice Provost for International Affairs said they are pleased to co-sponsor this exciting new initiative, as part of Cornell’s commitment to diverse global society. “It is an honor to be part of an effort that promotes vibrant literary traditions and encourages meaningful interaction between the peoples of East Africa,” he said.

The Prize is primarily supported byMabati Rolling Mills of Kenya (a subsidiary of the Safal Group), the Office of the Vice Provost for International Affairs at Cornell University and the Africana Studies Center at Cornell University.

For more information: http://kiswahiliprize.cornell.edu

Twitter handle: @KiswahiliPrize

Facebook: Mabati-Cornell Kiswahili Prize for African Literature

Contact information:

Prof. Mukoma Wa Ngugi, [email protected]

Dr Lizzy Attree, [email protected]

Jinsi mtandao wa Al Shabab unavyofanya kazi

MWISHO wa mwezi uliopita, kikundi cha Al Shabaab (Harakat al-Shabaab al-Mujahideen au Harakati ya Vijana Mujahidina) kutoka Somalia waliliteka nyara basi lililokuwa likitoka Mandera, Kaskazini mwa Kenya karibu na mpaka wa Somalia, likielekea Nairobi.

Kati ya abiria 60, waliwatenga abiria 28 wasio Waislamu na kisha kuwaua.

Kitendo hiki cha kigaidi kiliifanya serikali ya Kenya kulipiza kisasi bila ya kuchelewa. Ndipo majeshi ya Kenya yalikivamia kituo cha Al Shabaab nchini Somalia na kuwaua waasi wapatao 115.

Makamu wa Rais, William Ruto, alisema majeshi yalifanya mashambulio mawili na kuteketeza kambi na vifaa vya Al Shabaab zikiwemo lori nne zenye silaha. Hata hivyo waasi hao walikataa madai hayo ya Ruto na kusema wapiganaji wao wako salama

Al Shabaab walitangaza kuwa mauaji ya Mandera yalikuwa ni kisasi kwa majeshi ya Kenya kuivamia misikiti minne katika jiji la Mombasa. Ruto alisema misikiti hiyo ilikuwa ikitumiwa na mujahidina kuficha silaha zao

“Tunawasihi viongozi wa dini wahakikishe kuwa misikiti yao haitumiwi na Mujahidina. Kwa upande wetu tukigundua tutachukua hatua kali,” alisema Ruto

Mauaji ya Mandera hayakuwa ya kwanza. Mnamo Juni na Julai mwaka huu Al Shabaab waliendesha mashambulizi kadha mkoa wa Lamu na watu takriban 100 walipoteza maisha yao. Kati yao 49 waliuliwa katika ushambulizi mmoja tu huko Mpeketoni

Halafu kuna mauaji makubwa ya Septemba mwaka jana wakati watu 67 walipopoteza maisha yao katika kituo cha biashara jijini Nairobi. Mauaji kama haya yamekuwa yakifanyika tangu 2011 wakati majeshi ya Kenya yalipoingia Somalia kwa wingi, kama sehemu ya kikosi cha umoja wa Afrika (AU)

Mjini Mombasa majeshi yaliuvamia msikiti wa Sakina. Watu kadha walikamatwa na wakachukuliwa. Baada ya siku mbili walivamia misikiti ya Swafaa na Musa na kuifunga. Hii ikapelekea maandamano kufanyika na watu wasiopungua watatu kuuawa, akiwemo askari mmoja

Hali iliharibika tangu Agosti 2012 wakati Sheikh Aboud Rogo alipouliwa. Huyu alikuwa Imamu wa Msikiti wa Musa ambao ulivamiwa na polisi.

Ni vizuri tukaelewa mujahidina hawa wanapata wapi nguvu zao, na kwa nini imekuwa vigumu kwa majeshi ya AU na Marekani kuwang’oa

Mwaka jana, mwandishi mmoja wa BBC aitwae Peter Taylor alifanya uchunguzi ili kujua jinsi Al Shabaab wanavyopata misaada kutoka nje na jinsi vijana wanavyojiunga na kikundi hicho, wengi wao wakitoka nje ya Somalia

Mjini Mombasa alikutana na bwana mmoja maarufu kama Makaburi aliyekuwa akiishi katika chumba kidogo. Jina lake halisi ni Abubaker Shariff Ahmed. Mwaka 2012, Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa (UN) lilimuweka katika orodha ya watu waliopigwa marufuku kusafiri nje ya nchi. Mali zake zote zikakamatwa

Baraza lilimueleza kuwa alikuwa akiwasajili vijana wa Kenya na kuwapeleka kwa mafunzo kabla ya kujiunga na Al Shabaab nchini Somalia. Katika mahubiri yake huwahamasisha vijana kuachana na Uislamu poa na kujiunga na ‘Jihad dhidi ya Wamarekani’

“Maadui wetu wanataka tuwe Waislamu poa ili watukandamize,” Makaburi alimwambia mwandishi Taylor ambaye aliandamana naye hadi vijijini ambako aliendesha mahubiri yake misikitini

Alipoulizwa, Makaburi alikataa kuwa anatuma fedha kwa Al Shabaab, ila alisisitiza kuwa Mujahidina hao wana haki ya kuzuia nchi yao isiingiliwe na wageni. Alisema Wasomali wana haki ya kuiendesha nchi yao watakavyo bila kuingiliwa na majeshi kutoka nje

Taylor aliona madrasa iliyokuwa ikiendeshwa na Makaburi. Ilianzishwa na Sheikh Aboud Rogo Mohammed ambaye alielezwa na UN kuwa ni mshiriki wa Makaburi.

Mnamo Agosti 2012, Rogo aliuawa mjini Mombasa. Wafuasi wake wanadai hiyo ni kazi ya polisi

Taylor alitumia wiki mbili akichunguza mtandao wa Al Shabaab, jinsi wanavyowachukua vijana na kuwapeleka katika kambi zao huko Somalia. Anasema mchakato huo unaanzia na Makaburi na wenzake ambao wanawahubiria vijana wa Kiislamu. Wengine ni vijana kutoka nchi mbali mbali, waliosilimu

Baada ya kutayarishwa mjini Mombasa, vijana hao husafirishwa na jahazi hadi kisiwa cha Pate kabla ya kuelekea Somalia

Taylor aliwahoji vijana wawili ambao hawakutaka watajwe. Wao walisema katika mahubiri walifundishwa kuwa anayejitolea katika jihad basi roho yake inakwenda peponi. Pia wanaahidiwa fidia kwa familia zao.

Baada ya kuuawa kwa Sheikh Rogo, Makaburi akakamatwa na kufunguliwa mashtaka ya kuchochea vurugu. Akaachiliwa kwa dhamana. Polisi walimwambia Taylor kuwa ni vigumu sana kupata ushahidi wa kuwafunga watu kama hao kwa vile sheria inawalinda.

“Hata nyie huko Uingereza mna matatizo kama haya ya kuwafunga wahubiri kama Makaburi,” alisema Msemaji wa Polisi. Hata hivyo alikuwa na hakika kuwa wangevunja mtandao wao

Taylor anasema majeshi ya Kenya yanasaidiwa na Marekani, Uingereza na Ulaya ili kuzuia vijana kujiunga na Al Shabaab. Mnamo Septemba 2012 majeshi hayo yalishambulia kambi iliyoko Kismayu, Kusini mwa Somalia. Hii ni bandari inayowasaidia sana Al Shabaab kujipatia mapato, hasa kutokana na waharamia wanaoteka nyara meli za kimataifa .

Al Shabaab ilianzishwa mwaka 2006. Baada ya hapo kwa muda wa miaka minne ilikuwa ikipigana ndani ya Somalia. Mnamo 2008, Kiongozi wake, Ahmed Abdi Aw-Mohamed "Godane, alitangaza kuwa kikundi hicho ni sehemu ya mtandao wa al Qaida

Ndipo Serikali ya Mpito ya Somalia (Transitional Federal Government - TFG) ikaungana na Umoja wa Afrika (AU) wakisaidiwa na Marekani wakashambulia kijeshi Al Shabaab

Al Shabaab nao wakaonesha uwezo wa mtandao wao waliposhambulia Uganda tarehe 11 Julai 2010. Baada ya hapo majeshi ya AU (African Union Mission in Somalia – AMISOM) yakaongeza nguvu na mnamo Mei 2011 yakafanikiwa kuteka maeneo ya Bakara mjini Mogadishu na Afogye yaliyokuwa yakishikiliwa na Al Shabaab

Wengi walifikiria kuwa huo ulikuwa mwisho wa Mujahidina hawa kwa vile walikuwa wakikusanya ‘kodi’ kutoka maeneo haya. Lakini haikuwa hivyo, kwani wangali walikuwa wakipata mapato kutoka vyanzo mbali mbali

Chanzo kimoja ni wafuasi wao walio nje ya Somalia, hususan Wasomali wanaoshi kote duniani. Wengi wao wamekuwa wakituma pesa za msaada kwa familia na ndugu zao kwa njia inayoitwa ‘hawala’ pamoja na kutumia benki. Baadhi ya fedha hizi huwa zinawafikia Al Shabaab na zinatumika katika mafunzo, usafiri na kununulia silaha.

Kwa mujibu wa ripoti ya UN inasemekana Eritrea imekuwa ikisaidia. Ripoti inasema kwa muda wa miaka kumi nchi hiyo imekuwa ikituma dola 80,000 kila mwezi kwa kupitia ubalozi wake Nairobi. Eritrea imekanusha

Kumekuweko na shutuma pia kuwa Yemen na Qatar zimekuwa zikituma fedha na silaha kwa Al Shabaab. Kwa mfano waasi wa Yemen inasemekana walituma shehena mbili za silaha kama gruneti na bunduki za Kalashnikov zilizowasili bandari ya Kismayo

Mnamo Machi 2010, wachunguzi wa UN walidai kuwa kamanda wa Al Shabaab aliyekuweko Puntland, Muhammad Sa'iid Atom amekuwa akipokea shehena za silaha kutoka Yemen na Eritrea. Pia inasemekana Saudia na tawala zingine za Guba zimekuwa zikituma fedha

Ripoti pia imetaja asasi kama ‘World Assembly for Muslim Youth’ na ‘International Islamic Relief Organization’ pamoja na wafanya biashara wa Kisomali wanaoishi Uarabunu, Australia, New Zealand, Malaysia, Singapore, Ulaya, Marekani na kadhalika

Shutuma pia zimetupiwa asasi kama African Muslims Agency nchini Kuwait, Mwezi Mwekundu nchini UAE, al Islah Charity, Harakat al-Islah nchini Saudia, Muslim World League (Rabitat al-Islam al-‘âlamiyya), International Islamic Relief Organization, nchini Saudia, Dawa al-Islamiyya na al Wafa Charitable Society

Inakisiwa kuwa kuna Wasomali takriban milioni moja wanaoishi nchi za nje kama Uarabuni, Ulaya na Marekani. Inasemekana badhi yao wanasaidia Al Shabaab

Ndio maana mwishoni mwa 2010, kwa mfano, Wasomali wanne, mmoja akiwa mwanamke, walikamatwa mjini San Diego (Marekani) na kushtakiwa kwa makosa ya kutuma fedha kwa Al Shabaab

Halafu mwaka huohuo Msomali mmoja, Mohamud Abdi Yusuf, aliyekuwa dereva wa teksi mjini St Louis (Marekani) alikubali makosa ya kukusanya dola karibu 6,000 kwa ajili ya Al Shabaab.

Pia kuna ripoti ya tajiri kutoka Saudia, Sheikh Mohamed Abu Faid pamoja na Omar Hammami ambao inasemekana wamekuwa wakisaidia vijana kutoka Marekani ambao wanasaifi hadi Somalia kujiunga na Al Shabaab

Almuradi, Wasomali wanaoishi nje wanakisiwa kuwa wanatuma nyumbani kati ya dola milioni 500 hadi 800 kila mwaka ili kusaidia wazee na ndugu zao. Hata kama fedha hizi zinatumwa kihalali fungu kubwa linatumika kuwasaidia Al Shabaab.

Waasi hawa pia wanafaidika kutoka Wasomali wanaoishi Nairobi, hasa maeneo ya Pumwani na Eastleigh, na katika kambi ya wakimbizi ya Dadaab iliyo Kenya kaskazini. Fedha hukusanywa kwa kisingizio cha kukarabati msikiti kumbe zinawasaidia wapiganaji

Nchini Somalia, wafanya biashara katika maeneo ya Al Shabaab hulazimishwa kulipa ‘kodi’ kwa wapiganaji. Kila mmoja hutozwa thamani ya bunduki moja ya Kalashnikov. Benki hulazimishwa kulipa ‘kodi’ kutokana na fedha za hawala zinazotumwa kutoka nje

Mwaka 2008, al Shabaab waliichukua bandari ya Kismayo, baada ya mapigano makali ya siku tatu na majeshi ya Somalia. Baada ya hapo wakaanza kutoza ushuru kima cha asilimia 30 kwa mali inayoingia na kutoka hapo.

Mali inayotoka ni kama samaki, mbuzi, ngamia, mirungi na mkaa kwenda Uarabuni, na inayoingia ni vyakula kama mchele kutoka Pakistan. Kwa ujumla inakisiwa kuwa Al Shabaab wamekuwa wakikusanya ushuru wa bandari ya Kismayo zaidi ya dola milioni moja kila robo mwaka. Inakisiwa mkaa wenye thamani ya dola 500,000 yanapelekwa Uarabuni kila mwezi kupitia bandari hiyo

Hata hivyo baada ya majeshi ya Kenya kuuchukua mji wa Kismayo mwezi Septemba 2011, Al Shabaab waliamua kujitoa “kwa muda”

Mnamo Oktoba 2011, majeshi ya Kenya yaliipokonya Al Shabaab miji ya Ras Kamboni na Bur Gaboby, maarufu kwa uvuaji wa samaki. Hapa ndipo waasi walikuwa wakikusanya ushuru. Kutoka Ras Kamboni samaki husafirishwa hadi Lamu, Kenya, ambako huuzwa kwa mahoteli ya kitalii. Baada ya kupoteza miji hii Al Shabaab wakapoteza pia mapato

Mpaka sasa mkakati wa majeshi ya AMISOM umekuwa ni kutumia silaha. Wakati huhuo huwanyima Al Shabaab vyanzo vyao vya mapato kutokana na kodi na ushuru. Wamefanikiwa kuwafukuza kutoka mji mkuu wa Mogadishu. Matokeo yake wanakimbilia miji midogo ambako wanajiimarisha na kuendelea na operesheni zao

Kuhusu mapato, kama tulivyoona wanaendelea kutegemea vyanzo vingine vya ndani na nje ya nchi. Fedha zinaendelea kuingia kutoka nje. Wakati huohuo wapiganaji wanajiunga kutoka nchi za nje kama tulivyoona

Al Shabaab ni sehemu ya mtandao wa Al Qaida. Ni mtandao uliopo Afghanistan, Yemen, Libya, Iraq, Syria na hata Nigeria.

Ziara ya Malcolm X nchini Tanzania

Malcom X kushoto akiwa na Abdulrahman Babu kulia
Malcom X (kushoto) akiwa na Abdulrahman Babu (kulia)

Hii leo, Desemba 3, imetimia miaka 50 kamili tangu Malcolm X, mwanaharakati wa Kimarekani mwenye asili ya Kiafrika, alipokuwa mgeni wa Chuo Kikuu cha Oxford, Uingereza. Alialikwa kushiriki katika mdahalo ulioandaliwa na Oxford Union, Jumuiya ya Midahalo ya Chuo Kikuu hicho.

Jumuiya hiyo ni medani ya midahalo yenye sifa ya “babu kubwa” nchini Uingereza. Wengi wa wasemaji wazuri wa Uingereza wenye kusifika kwa ufasaha walianzia huko. Baadhi yao baadaye walikuwa Mawaziri Wakuu, mawaziri, wanasiasa, waandishi mahiri au watu walioshikilia vyeo vikuu katika jamii.

Miongoni mwa watu mashuhuri kutoka nje ya Uingereza waliowahi kushiriki katika midahalo ya Oxford Union ni Askofu Mkuu Desmond Tutu wa Afrika ya Kusini, Dalai Lama wa Tibet, kiongozi wa Wapalestina Yasser Arafat, Mama Teresa, Rais wa zamani wa Pakistan Pervez Musharaf, Waziri Mkuu wa Bangladesh Sheikh Hasina na Marais wa Marekani Richard Nixon, Jimmy Carter na Ronald Reagan.

Muhimu kwa Uingereza, taifa lililogawika vibaya kitabaka, jumuiya hiyoya mijadala imekuwa ikitumiwa tangu ilipoasisiwa 1823 kama jukwaa la kuwapa mazoezi ya kujadiliana chipukizi wa kibwanyenye wenye shauku ya kujitosa katika bahari ya siasa.

Malcolm X na hao “watoto wa watu” walikuwa kama mbingu na ardhi. Wengi wakimuona kuwa ni mtu hatari. Wakimuona kuwa yeye ni tashihisi ya mapinduzi, yaani nafsi yake yote ilikuwa ni hatari kwa jamii.

Mdahalo alioshiriki Malcolm X Desemba 3, 1964ni moja ya midahalo ya Oxford Union iliyosisimua sana kiasi cha kuitwa mdahalo wa kihistoria. Wakati huo Malcolm X alikuwa na umri wa miaka 39 na alikuwa amezongwa na mengi.

Idara za kijasusi za Marekani na za nchi nyingine zilikuwa zikimuandama. Hali yake ya afya haikuwa nzuri.Kina Elijah Muhammad wa‘Nation of Islam’ walikuwa nao wakimuandama.

Hata hivyo, hakutishika. Aliendelea kuwapigania Wamarekani wenzake wenye asili ya Kiafrika.

Hoja ambayo akiitetea kwenye mjadala huwa Oxford ilikuwa: “Kutumia siasa kali kutetea uhuru si upotofu; kutumia siasa wastani kupigania haki si uadilifu.”

Umbuji na ufasaha wa Malcolm X wa kuweza kuitetea hoja hiyo katika mazingira ya Oxford Union hauelezeki.Kwa ufupi, usiku huo Malcolm X alicheza na shingo alitoa.

Waliokwenda kumsikiliza usiku ule wa Desemba 3, 1964 wakitaraji kwamba Malcolm X atatumia lugha kali na msamiati wa vitisho kuitetea hoja yake.

Walikosea. Walimkuta akiwa na silaha nyingine kabisa: ucheshi. Aliwabwaga kwahaiba, bashasha na mvuto wake uliowafanya mara kwa mara waangue kicheko.


Juu ya umahiri wake Malcolm X alishindwa katika mdahalo huo. Alipata kura 137 na mpinzani wake, Humphrey Berkeley, mwanasiasa wa chama cha Conservative,alipata kura 228.

Hata hivyo, Malcolm X alionekana kuwa ni mtu shujaa, aliyejiamini na aliyekuwa akitafahari kwa asili yake ya Kiafrika. Muhimu zaidi akijulikana kuwa ni mtu aliyejitolea kupigania usawa na haki kwa watu wake.

Stephen Tuck, mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Oxford, ameandika kitabu kizima kuhusu mdahalo huo. Kitabu hicho,‘The Night Malcolm X Spoke At The Oxford Union,’kinaeleza mengi.

Miongoni mwa yanayoelezwa humo ni kwa nini jumuiya ya Oxford Union ilimwalika Malcolm X na kwa nini alikubali kwenda. Kadhalika kitabu hicho, kilichochapishwa mwezi huu, kinaeleza jinsi Malcolm X alivyoathiriwa na ziara yake ya Oxford na jinsi yeye alivyowaathiri wanafunzi waliokuwa wakimsikiliza.

Miezi miwili kabla Malcolm X alikuwa ziarani nchini Tanzania.Kabla ya kuwasili Tanzania alikuwa amekwishazizuru nchi mbalimbali za Afrika ya Magharibi, ya Kaskazini na Mashariki ya Kati.

Ghana, ambako alizungumza na Rais Kwame Nkrumah, alikuwa akikaa kwa Cameroon Duodu, mwandishi ambaye mara nyingi mimi hushirikiana naye katika vipindi vya BBC World Service hasa kile cha kila mwaka cha mashindano cha “the African Quiz.”

Mwaka huo wa 1964 ulikuwa ni mwaka wa safari nyingi za Malcolm X, safari zilizompeleka kwingi na zilizomkutanisha na wengi — viongozi pamoja na wananchi wa kawaida. Kote alikokwenda akieleza madhila yaliyokuwa yakiwafika Wamarekani wenye asili ya Kiafrika na akiutaka ulimwengu uyaunge mkono mapambano yao.

Yote hayo yamo kwenye shajara yake ya 1964, kitabu cha kumbukumbu zake za kila siku.Kitabu hicho, ‘The Diary of Malcolm X – El-Hajj Malik El-Shabazz 1964’ kimehaririwa na Herb Boyd pamoja na Ilyasah Al-Shabazz, ambaye ni binti wa tatu wa Malcolm X.

Boyd ni mtu ninayejuwana naye kwa miaka mingi na amewahi kabla kuhariri kitabu kingine kumhusu Malcolm X. Hiki cha shajara yake ya 1964, kilichochapishwa na Third World Press, kinambainisha Malcolm X aliyepevuka na aliyekuwa na dira maalum aliyoamini kuwa itasaidia kuwakomboa Wamarekani wenye asili ya Kiafrika.

Alipokuwa Ethiopia alikutana na Otini Kambona, mdogo wake Oscar Kambona.Pia huko Addis alionana na Watanganyika wengine kadhaa ambao hakuwataja kwa majina.

Oktoba 3 alikwenda uwanja wa ndege wa Addis kuonana na Abdulrahman Babu aliyekuwa njiani kuelekea Cairo.

Babu na Malcolm X walitoka mbali. Aliyewakutanisha alikuwa Mohamed Ali Foum, mfuasi mkubwa wa Babu katika chama cha Umma Party huko Zanzibar na aliyekuwa katika Ubalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa.

Usuhuba wa Foum na Malcolm X ulikuwa mkubwa kiasi cha kuwafanya wawe wanatembeleana majumbani mwao. Mwingine aliyekuwa akimtembelea Foum kwake alikuwa Che Guevara, mwanamapinduzi wa Cuba.

Majuzi tu, Ashura Hilal (maarufu Ashura Babu), aliyekuwa mke wa Babu, alinikumbusha kuhusu karamu ya chakula cha usiku aliyoiandaa Foum nyumbani kwake New York. Che alikuwa amealikwa.

Baada ya chakula, Babu, Ashura na Foum wakenda Harlem kwenye ukumbi wa Audubon Ballroom ambako Malcolm X alikuwa akihutubia. Babu na Che walikuwa pia wauhutubie mkutano huo lakini Fidel Castro alimzuia Che asiende akichelea kwamba angeweza kudhuriwa na Wamarekani. Che akamuomba Babu amtolee salamu zake.

Wakati huo Tanzania ikijulikana kwa jina la‘Jamhuri ya Muungano ya Tanganyika na Zanzibar’ na ndio maana Malcolm X karibu miezi sita baada ya kuzaliwa Tanzania ameandika kwenye shajara yake kuhusu “Watanganyika” aliokutana nao wakiwa pamoja na “wanafunzi kutoka Tanganyika” aliozungumza nao Addis Ababa hadi saa nne na nusu za usiku.

Malcolm X aliwasili kwanza Zanzibar Oktoba 9. Kwa bahati mbaya alipata usumbufu kidogo kwa vile hakuwa na viza ya kuingilia Visiwani humo.

Oktoba 12 alikwenda nyumbani kwa Babu Dar es Salaam. Ameandika kuwa “Babu hakuwa na mbwembwe hata kidogo na alikuwa na mkabala wa kirafiki. Ni mtu aliye macho saa zote na aliyejitolea kwa anayoyaamini.”

Inavyoonyesha ni kwamba alikuwa akiingia na kutoka nyumbani kwa Babu na hata ofisini mwake. Chakula cha mchana akila kwa Babu. Kwa mujibu wa Ashura Malcolm X akivipenda sana vyakula vya Kiswahili hasa samaki wa kupaka.

Oktoba 13 baada ya kuchukuwa viza ya kuingia Nigeria kutoka Ubalozi wa nchi hiyo alitembea kwa mguu hadi ofisini kwa Babu.

Alipokuwa akimsubiri Babu amalize shughuli zake alipiga soga na katibu wake. “Alitoka Zanzibar, mcheshi na mzuri (wa sura).” Huyo, bila ya shaka, ni Shirin Hassanali ambaye kwa muda wa miaka mingi tangu Babu alipokuwa waziri Zanzibar hadi alipokuwa waziri Dar es Salaam ndiye aliyekuwa katibu wake.

Halafu Babu akamchukuwa Malcolm X nyumbani kwake kwa chakula cha mchana. Aliwakuta watu wengine wapatao wanne. Malcolm ameandika kwamba akijuwa ya kwamba walikuwa “wakinipima na nilisisimkwa nilipoambiwa kwamba nitakutana na Rais saa 12 za magharibi (hasa kwa vile niliambiwa mapema asubuhi ya leo kwamba haitowezekana).”

Malcolm X akaendelea kuandika kwamba alikutana na watoto wawili wa Babu, “mmojawao (msichana wa miaka minne) alifuatana na dereva kunirejesha hotelini kwangu.”

Huyo binti wa Babu alikuwa ni Salma ambaye siku hizi anaishi Uingereza na mumewe, mwananchi wa Ghana, na watoto wao. Alipokuwa na umri wa miaka mitatu, Salma aliletewa zawadi ya mtoto wa sanamu mweusi na mrefu na mkewe Malcolm X, Betty Shabazz. Zawadi hiyo alikabidhiwa mamake amchukulie.

Ilipotimu saa 12 kasorobo, Malcolm X alirudi nyumbani kwa Babu na wakafuatana kwenda Ikulu. Huko walimkuta Oscar Kambona na Mwalimu Julius Nyerere aliingia saa 12 na robo.

“Ni mtu mwerevu sana, mwenye akili, mwenye kukupoza, ni mtu mwenye kucheka na mwenye kufanya dhihaka sana (lakini kwa uzito kabisa),” ndivyo Malcolm X alivyomuelezea Mwalimu.

Kama miezi sita baada ya kuizuru Tanzania na haikutimu hata miezi mitatu baada ya ule mdahalo wa Oxford Union Malcolm X alipigwa risasi na kuuliwa mjini New York Februari 21, 1965. Aliuliwa katika ukumbi uleule wa Audubon Ballroom ambako yeye na Babu walihutubia 1964.

Kenya arrests 77 Chinese living near US Embassy, UN Headquaters for cybercrime

Kenyan police have arrested 77 Chinese nationals and are consulting experts to see if they used advanced communications equipment in several houses in an upscale Nairobi neighbourhood to commit espionage.

Kenya's foreign ministry has also summoned China's top diplomat in the capital Nairobi as it seeks to establish if Beijing was in anyway linked to the affair.

Police said they believed the gang was "preparing to raid the country's communication systems".

The Daily Nation newspaper said a series of police raids had turned up equipment capable of infiltrating bank accounts and government servers, Kenya's M-Pesa mobile banking system and ATM machines.

"The suspects are being interrogated to establish their mission in the country and what they wanted to do with the communication gadgets. They have been charged in court," said the director of Kenya's Criminal Investigation Department, Ndegwa Muhoro.

"We have roped in experts to tell us if they were committing crimes of espionage,'' he told the Associated Press news agency.

Police said many of those detained appeared to have been in the country illegally.

The arrests began on Sunday, when computer equipment in one of the upscale houses the Chinese nationals had rented near the US Embassy and UN headquarters caught fire, killing one person.

Kenyan foreign minister Amina Mohamed "made it clear that the Chinese government should fully cooperate on this matter," Kenya's communications minister Fred Matiang'i said, adding that China has promised to send investigators to Kenya to work on the case.

Police said it appeared the group was also manufacturing ATM cards, and that the suspects may have been involved in money laundering and Internet fraud.

Mpya kuhusu kesi ya Lwakatare

Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilfred Lwakatare (wa tatu kushoto) akiongozana na familia yake wakati akitoka katika Mahakama ya Rufaa Tanzania, baada ya mahakama hiyo kuyatupilia mbali maombi ya serikali ya kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu wa kumfutia mashitaka ya ugaidi.

Picha: Francis Dande
Mahakama ya Rufani imetupilia mbali maombi ya marejeo kuhusu uhalali wa uamuzi wa Mahakama Kuu Dar es Salaam kuwafutia mashtaka ya ugaidi Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilfred Lwakatare na mwenzake Joseph Ludovick Rwezahura.

Hatua hiyo ya mahakama imefanya kiongozi huyo wa CHADEMA na mwenzake kuibwaga Serikali kwa mara ya pili mahakamani katika mashitaka dhidi yao.

Maombi hayo namba 5 ya mwaka 2014, yalifunguliwa na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) katika Mahakama ya Rufani akipinga uamuzi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kufumfutia mashtaka ya ugaidi yaliyokuwa yakimkabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Uamuzi wa kutupilia mbali maombi hayo ulisomwa jana na Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufani, Zahra Maruma kwa niaba ya Jopo la Majaji watatu wa mahakama hiyo lililokuwa limepangwa kusikiliza maombi hayo.

Majaji hao ni Nathalia Kimaro (kiongozi wa jopo), William Mandia na Profesa Ibrahimu Juma.
Mahakama hiyo ilifikia uamuzi huo baada ya kujiridhisha kuwa maombi hayo yalikuwa na dosari za kisheria kutokana na DPP kutoambatanisha mwenendo wa uamuzi wa Mahakama Kuu aliokuwa akiupinga.

Dosari hiyo iliibuliwa na Jaji Prosefa Juma katika tarehe ambayo maombi hayo yalikuwa yamepangwa kusikilizwa ambapo alihoji iwapo ni halali kusikiliza maombi hayo bila kuwepo kwa mwenendo huo.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Angaza Mwipopo akisaidiana na Wakili Serikali Mwandamizi, Hashim Ngole, alijibu kuwa wanachopinga ni uamuzi wa mahakama kufuta mashtaka katika kesi ambayo haikuwa mbele yake.

Wakili Angaza alidai kwamba kutokuwepo kwa mwenendo huo hakuathiri na kwamba mahakama ina uwezo wa kuyasikiliza maombi hayo hata bila kuwepo kwa mwenendo huo.

Akijibu hoja hizo, Wakili wa Lwakatare, Peter Kibatala alisema kuwa suala la mwenendo wa uamuzi unaopingwa ni miongoni mwa hoja za pingamizi lake la awali dhidi ya maombi hayo.

Wakili Kibatala alidai kuwa kutokuwepo kwa mwenendo huo ni dosari ambayo ina athari kubwa kiasi kwamba mahakama haitakuwa na uwezo wa kutoa kile kinachoombwa.

Alisisitiza kuwa kutokuwepo kwa kumbukumbu za mwenendo huo ni athari ambayo tiba yake ni mahakama kuyatupilia mbali maombi hayo.

Kamati ya Wanablogu wa Tanzania yaanza kuijadili rasimu yao

Katibu Msaidizi wa Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania , Shamim Mwasha (kushoto),akizungumza na wajumbe wa kamati hiyo wakati wa mapitio ya rasimu hiyo. Kulia ni Mjumbe wa Kamati, Henry Mdimu.

WAJUMBE wa Kamati ya Muda ya Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania (Bloggers) wameanza vikao vyao kujadili rasimu ya katiba ya umoja huo kabla ya kufanya usajili wa chama chao kitakacho waunganisha wamiliki na waendeshaji wa mitandao hiyo Tanzania.

Akizungumza jana katika vikao hivyo vinavyofanyika jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Muda wa Kamati ya Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania, Joachim Mushi amesema wajumbe waliokutana ni wawakilishi wa wamiliki wa mitandao hiyo kutoka makundi mbalimbali ya waendeshaji hao wa mitandao ya jamii nchini.

Alisema pamoja na mambo mengine wajumbe hao wanatarajia kufanya majadiliano baada ya kuipitia rasimu ya Katiba ikiwa ni kuelekea mchakato wa kupata Katiba ya Chama cha Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania. Alisema masuala mengine ambayo yataongoza mjadala huo ni pamoja na kuangalia muundo wa chama, uendeshaji wake, maadili ya chama kwa wanachama katika utekelezaji kazi zao.

"Kikao hiki kinashirikisha wajumbe wa kamati ambao ni wawakilishi wa makundi mbalimbali ya wamiliki na waendeshaji wa mitandao ya jamii Tanzania na kazi kubwa ambayo wataifanya jana kwa pamoja ni kupitia rasimu ya uumoja wetu. Wajumbe wote walikabidhiwa rasimu hii wiki mbili zilizopita kuipitia wenyewe kabla ya kukutaka katika majadiliano ya leo," alisema Mwenyekiti wa Muda, Mushi.

Aidha aliishukuru Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa mchango wake wa dhati wa kuwaunga mkono Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania hasa katika kipindi hiki cha mchakato kuelekea uundwaji wa chama chao.

Miongoni mwa wajumbe wa kamati hiyo ya muda waliokutana ni pamoja Shamim Mwasha (Katibu Msaidizi) Khadija Kalili (Katibu), Joachim Mushi (Mwenyekiti), Henry Mdimu (Mjumbe), Mariam Ndabaganga (Mjumbe), William Malecela (Mjumbe), Othman Maulid (Mjumbe-Zanzibar) na Francis Godwin (Makamu Mwenyekiti - Iringa).

Mkutano wa mafunzo wa idadi kubwa ya wawakilishi wa wamiliki wa mitandao ya kijamii nchini (Bloggers) uliofanyika Novemba 11, 2014 jijini Dar es Salaam ulioitishwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania uliibua uundwaji wa Kamati ya Muda ya Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania chini, ambapo kamati hiyo ilipewa jukumu la kupitia rasimu kabla ya kushughulikia usajili wa chama cha jumuia hiyo.

Mwenyekiti wa muda wa Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania (Bloggers), Joachim Mushi (wa pili kushoto), akizungumza wakati akifungua majadiliano kwa wajumbe wa kamati ya muda ya wamiliki wa mitandao ya jamii Tanzania ya kujadili Rasimu ya Katiba ya umoja huo Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mjumbe wa Kamati hiyo ya muda kutoka Zanzibar, Othman Maulid.

Wajumbe wa kamati wakipitia rasimu hiyo. Kulia ni William Malecela na Marion Ndabaganga.
Mwenyekiti wa Muda wa Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania (Bloggers), Joachim Mushi (wa pili kushoto), akizungumza wakati akifungua majadiliano kwa wajumbe wa kamati ya muda ya wamiliki wa mitandao ya jamii Tanzania ya kujadili rasimu ya Katiba ya umoja huo Dar es Salaam jana. Majadiliano hayo yameanza jana kujadili rasimu ya katiba kabla ya kuipitisha kwa hatua za usajili wa Chama cha Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania (Bloggers). Kutoka kushoto ni Mjumbe, Othman Maulid, Katibu Msaidizi wa Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania , Shamim Mwasha, Henry Mdimu (Mjumbe), Mariam Ndabaganga (Mjumbe) na William Malecela (Mjumbe).
Wajumbe wa kamati hiyo wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mkutano wao uliofanyika katika Mgahawa wa MOG Longue, jijini Dar es Salaam  jana asubuhi.

Kuhusu taarifa kuwa Lowasa kalazwa Ujerumani

Ofisi ya mbunge na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, jana ilikanusha vikali uvumi uliozagaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kuwa mbunge huyo wa Monduli amelazwa nchini Ujerumani.

Taarifa zilizoenea zinaeleza kuwa Lowassa, ambaye wakati wote wa Mkutano wa 15/16 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano uliofanyika kwa wiki tatu, hakuwepo bungeni, amekuwa Ujerumani ambako amelazwa kwa matibabu.

Hata hivyo, jana msemaji wake, Aboubakary Liongo aliliambia gazeti hili kuwa taarifa hizo ni za uzushi lakini akaeleza ni kweli yuko nchini humo kwa ajili uangalizi wa afya yake. 

“Aliondoka kwenda India kumuona (mbunge wa Kilindi) Beatrice Shelukindo ambaye amelazwa huko na baada ya hapo alimpeleka mke wake Ujerumani kwa ajili ya kutibiwa matatizo ya miguu,”
“Alipofika huko na yeye akaamua kuangalia afya yake kwa kuwa daktari wake yuko nchini humo.”
alisema Liongo.

Alisema Lowassa atarejea nchini wiki ijayo kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za sikuku ya Uhuru itakayofanyika Desemba 9 na baadaye ataelekea Monduli kwa ajili ya kampeni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Desemba 14.

“Atakwenda kuhakikisha chama kinashinda nafasi zote katika uchaguzi huo,” 
alisema Liongo.

UDSM appointments: Prof. Luoga, Prof. Mfinanga, Prof. Kimambo

Kauli ya Wizara kuhusu taarifa kuwa "Waziri Muhongo 'atimkia' Norway"

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA 

WIZARA YA NISHATI NA MADINI

TAARIFA KWA UMMA

KANUSHO LA WAZIRI WA NISHATI NA MADINI PROFESA SOSPETER MUHONGO KWENDA NCHINI NORWAY.


Mnamo tarehe 4 Desemba 2014, Gazeti la Raia Tanzania, Toleo Na.0259 liliandika habari iliyokuwa na kichwa cha habari “Waziri Muhongo ‘atimkia’ Norway”.

Gazeti hilo lilieleza kwamba Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ambaye anapaswa kuwajibishwa kwa mujibu wa ushauri wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, yuko kikazi nchini Norway ambako ameongozana na viongozi waandamizi wa Wizara yake.

Wizara inatoa taarifa kwa Watanzania kwamba habari hiyo haina ukweli wowote kwani Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo yupo hapa nchini na tarehe ambayo gazeti husika lilichapisha habari hiyo, Mhe. Muhongo alikuwa wilayani Musoma, mkoani Mara kuhudhuria hafla ya kuwapongeza wanafunzi waliofanya vizuri kwenye masomo katika shule ya Msingi ya Mwisenge A na B.

Waziri Muhongo alihudhuria hafla hiyo baada ya kualikwa na Ubalozi wa China hapa nchini, ambao umetoa ufadhili wa masomo na zawadi kwa wanafunzi walemavu wapatao 108 waliofanya vizuri katika masomo yao. Aidha, Ubalozi wa China umetoa ufadhili wa kuwapeleka baadhi ya wanafunzi kutoka katika shule hizo kwenda nchini China kwa lengo la kujifunza utamaduni wa nchi hiyo.

Ufadhili huo wa masomo umetolewa na Ubalozi wa China kwa ajili ya kumuenzi Baba wa Taifa Mwl. Julius. K. Nyerere ambaye alisoma katika shule hiyo.

Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na Balozi Mdogo wa Ubalozi wa China Bw. Li Xuhang, Meya wa Mji wa Musoma Mhe. Alex Kisulura, Mhe. Madaraka Nyerere, Bw. Joseph Kahama pamoja na walimu na wanafunzi wa shule hizo.

Tunapenda kuwakumbusha waandishi wa habari kuzingatia maadili ya taaluma na uzalendo ikiwa ni pamoja na kuandika habari zilizofanyiwa uhakiki na zenye ukweli, zisipotoshe Umma ili kuondoa usumbufu kwa wananchi.

Imetolewa na,

WIZARA YA NISHATI NA MADINI

5 Desemba 2014

Picha za 'mashujaa' waliookoa wengine kwenye mafuriko Mwanza
MVUA kubwa iliyonyeesha juzi (Jumanne) asubuhi imeleta mafuriko katika maeneo mbalimbali Jijini Mwanza huku eneo la Mabatini likiathirika zaidi na mafuriko hayo yaliyoambatana na mvua kubwa iliyonyeesha takribani kwa muda usipoungua saa mbili mfululizo.

Mafuriko hayo yalisababisha maji kujaa katika nyumba za wakazi wa maeneo ya Mabatini, pia mafuriko hayo yalisababisha magari kutopita eneo la daraja hilo linalotumiwa na waenda kwa miguu baada ya maji hayo ya mafuriko kuigawa barabara hiyo, hali iliyosababisha kukatika kwa mawasiliano.

Juhudi za jeshi la Zimamoto na uokoaji ambao walifika mapema eneo la tukio zilisaidia kuokoa baadhi ya wakazi wa nyumba zilizokumbwa na mafuriko yaliyosababisha nyumba hizo kujaa maji ndani.

Katika zoezi hilo la uokoaji watu mbalimbali waliokolewa wakiwepo watoto wadogo na akina mama huku mali mbalimbali zikiwemo runinga, vitanda, magari yakisombwa na mafuriko hayo.

Akizungumzia tathimini ya zoezi nzima la uokoaji Kamanda wa Jeshi la zimamoto na uokoaji Jijini Mwanza, Andrew James Mbate amesema zoezi la uokoaji lilienda vizuri na walifanikiwa kuokoa maisha ya watu waliokowepo ndani ya nyumba huku akitanabaisha changamoto mbalimbali walizokutana nazo katika zoezi zima.


Wanajeshi wa Kikosi cha zimamoto Mwanza wakimvusha mama huyu kutoka juu ya paa la nyumba moja hadi upande wa pili penye usalama kupisha maji yaliyokuwa yamefurika hata kuzifunika nyumba za wananchi eneo la Mabatini jijini Mwanza.

“Zoezi la uokoaji lilienda limeenda salama na linaendelea vizuri tunashukuru wenzetu wa shirika la umeme waliwahi kukata umeme mapema hali iliyopelekea sisi kama Jeshi kuanza kazi mara moja tulivyofika eneo la tukio”. Aliongeza Gadafi ambaye ni msemaji wa jeshi la Zimamoto


Akizungumza juu ya mafuriko hayo mkazi wa mabatini, Charles Samson alisema wamepoteza vitu vyao vya thamani huku wakioomba serikali iwasaidie kuhama mabondeni kwani madhara yaliyowakuta ni makubwa.


TANESCO walizima umeme kwaajili ya tahadhali.


Kivuko asilia ni ajira kwa wengine.

Tamasha la Mitikisiko ya Pwani, Desemba 13 @DarLive


Kauli ya Serikali kuhusu wawekezaji wanaobadili majina

Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha, Mwigulu Nchemba katika mahojiano na Redio One kwenye kipindi cha Kumepambazuka amesema Serikali imegundua kuhusu mbinu zinazotumiwa na baadhi ya wawekezaji kukwepa kulipa kodi kwa kubadili majina ya kampuni.

Mwigulu alisema serikali ilishachukua hatua kwa kubadilisha sheria ambayo sasa haitoi fursa kwa wawekezaji kupata unafuu wa kodi anapobadili jina la kampuni.
“Kubadili jina haihusiani na badiliko lolote la jina la kampuni, akibadili jina kodi ipo pale pale, kwa hiyo wanaobadili majina ya kampuni wanajidanganya watatakiwa kilipa kodi kama kawaida kwa mujibu wa sheria,” 
alisema.

Mwigulu alisema kutokana na mabadiliko hayo ya sheria mwekezaji au mtu yeyote akibadili jina la kampuni mmliki wa kwanza ndiye anakuwa bado anatambuliwa na akiuza hisa bado taifa itanufaika kwa kodi.

Alisema serikali imejipanga kuhakikisha kila mtu analipa kodi kwa mujibu wa sheria na kwamba serikali haitakubali kuona baadhi ya wawekezaji wanakwepa kulipa kodi na kuikosesha nchi mapato.

Tahadhari kutoka Michuzi Media GroupKauli kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Michuzi Media Group (MMG) inahadharisha wadau kuhusiana na ujumbe (pichani) ambao upo kwenye ukurasa Facebook na hata kwenye Twitter kwamba, ujumbe huo hauhusiani kwa namna yoyote na 'Ankal' Muhidin Issa Michuzi wala MMM ama Wakala wake.

"Hivyo, tunawasihi tusihusishwe nayo na pia tunawaomba kuwa macho na mambo kama haya maana ulaghai na utapeli mitandaoni ni mwingi mno.

AHSANTENI SANA 

ANKAL"

Scandal in Tanzania: Corruption charges show need for reform in oil and gas sector

The following has been cross-posted from OxfamAmerica.org 'as is'.

I was in Tanzania last month as what may turn out to be a major corruption scandal in the country’s history was coming to light. Contained in these events and international headlines are lessons about the importance of a broad good governance agenda in managing the oil and gas industries.

Two senior members of Tanzania’s Petroleum Development Corporation were arrested for failing to meet a deadline imposed by Parliament for releasing the details of all 26 of the contracts, or Production Sharing Agreements, that Tanzania has signed with oil and gas companies, including: ExxonMobil, Shell, Norway’s Statoil and the UK’s BG Group and Ophir. While the arrests made international headlines, the two were released hours later on grounds that their arrests were not suitably authorized.

How about a little context?

With policies and laws still being formulated, Tanzania’s emerging oil and gas industry is largely governed by the 26 Production Sharing Agreements, signed by a range of companies that, to date, have not been released to the public.

Public concern over the fairness of these agreements was ignited in July this year when a 2012 addendum to a 2007 Production Sharing Agreement between Statoil and the Tanzanian government was leaked to the public. Its revelations included the fact that the split of “profit gas” between the Tanzanian government and Statoil was between 20% and 30% lower than what was described in model contracts.

Parliament didn’t respond to the leak, but public interest ballooned when a blogger translated the implications of the addendum into understandable terms for citizens in Tanzania: This 20-30% difference could result in Tanzania losing hundreds of millions of dollars. Put another way, the increased revenue to the Norwegian government from this deal could be more than twice the total of Norwegian aid given to Tanzanian since independence. (The Natural Resource Governance Institute’s analysis of the leaked contract concluded that the contract was “not out of line with international standards for a country that had no proven offshore reserves of natural gas at the time when the original contract was signed” but acknowledged that there were limitations to their review, including “continued secrecy around the full PSA itself.” NRGI also did not disclose its own economic model.)

Momentum around this issue built quickly. With the public raising questions about both the fairness of the other 25 agreements, and about the capacity of the Tanzania Petroleum Development Corporation (TPDC) to negotiate such deals. Lurking in the background were concerns about political will and the possibility of corruption.

Public outcry finally sparked a political reaction. The National Assembly’s Clerk ordered that TPDC disclose all 26 contracts to the Parliamentary Oversight Panel by November 3. TPDC resisted this directive, saying that the contracts could not be made public as they were governed by confidentiality clauses. When the November 3 deadline came and went, the Parliamentary Committee on Public Accounts ordered the arrest of both the acting Director General and the board chairman of TPDC.

While many people may feel outraged at the ongoing lack of transparency and the impunity of TPDC officials, this entire process has ignited calls from politicians, the general public and civil society , for increased transparency in Tanzania’s oil and gas sector.
The drama contains 3 important lessons

The following lessons pertain to the importance of a broader approach to good governance, including the maintenance of space for civil society.

Transparency is fundamental: A clear message from Tanzania’s recent experience is that transparency is fundamental to ensuring that natural resources are managed in the public interest. At the moment it remains unclear whether the deal between Statoil and the Tanzanian government is a fair one. Without access to the original profit sharing agreement, the economic modeling on which the oil contract is based, as well as documentation detailing the bidding process, we simply cannot answer that question. But without transparent access to similar information for the other 25 contracts, there can be no public discussion at all on whether those deals are fair. There growing international momentum for “open contracting”. Many countries, such as Peru, disclose all of their oil and gas agreements, and the World Bank’s private sector lending arm, the IFC, requires contract disclosure for extractive projects it finances. One oil company, Kosmos Energy, has disclosed its contracts wherever it operates, while Tullow has disclosed its agreements in Ghana and has stated its preference to disclose wherever it does business. Many mining companies also support contract disclosure. Finally, Oxfam, the World Bank, Transparency International and others back the new Open Contracting Partnership.

The public is interested: Despite the complexity and large amounts of technical content in the debates on managing oil and gas revenues, the Tanzanian public is hungry for information on the topic. Arguments that there is no need to publish these technical documents because the public is not interested are clearly wrong. Tanzania remains one of the poorest countries in the world, ranking 159th out of 187 countries in the Human Development Index. If managed well and invested in pro-poor growth related to agriculture, education and health, people certainly understand that future gas revenues could support inclusive development and poverty reduction.

Space for civil society is crucial: Despite the fact that parliamentary actors in Tanzania eventually acted to demand access to the profit sharing agreements, the initial leak generated almost no political response. It was only after an active member of civil society published a story that public attention flared up. It was after this that politicians decided to respond, and the global media picked up the story. Space for civil society groups is therefore fundamental for ensuring that issues of natural resource management are effectively policed and for enabling the public to engage around this topic. This process cannot be left solely to elected politicians, appointed officials and the established media.

These events in Tanzania illustrate the importance of civil society, transparency, and active citizenship and the need for companies, such as Statoil, to take public and proactive steps to encourage contract disclosure. Countries like Tanzania, as well as neighbors Kenya, Uganda and Mozambique, have the potential to become major energy producers, but also face poverty and inequality, need these structures in place even more – millions of people are depending on governments, activists and institutions to get it right.
  • James Morrissey is a researcher on extractive industries and governance at Oxfam America.
  • OxfamAmerica.org Editor’s Note: Two of the hyperlinks originally included in this blog post referred to another case in Tanzania. These have been corrected.

Kauli ya Lady Jaydee kuhusu kuingia kwenye siasa

Mhariri Msaidizi wa Gazeti la Jambo Leo, Frank Balile (kulia), akimuelekeza jambo Lady Jaydee wakati akimuonesha gazeti hilo.

MWANADADA anayefanya vizuri katika muziki wa kizazi kipya nchini, Judith Wambura 'Lady Jaydee' amesema kamwe hatarajii kujiingiza katika masula ya siasa kama wanavyofanya wanamuziki wenzake.

Kauli hiyo aliitoa wakati akizungumza na waandishi wa habari wa gazeti la Jambo Leo, Dar es Salaam jana, baada ya kutembelea chumba cha habari cha gazeti hilo katika Jengo la Hifadhi House katika makutano ya Barabara za Azikiwe na Samora.
"Binafsi sitarajii kuingia katika masula ya siasa mimi nitaendelea na muziki na hao wenzangu waliojiingiza katika siasa ni utashi wao," 
alisema Jaydee.

Alisema anafurahi kufanya mziki na wala hajuti kwa kuwa unamuongezea kipato kikubwa ni kutunga nyimbo zenye maudhui na mvuto na kwa wakati husika.

Baadhi ya wanamuziki waliojiingiza katika siasa ni Joseph Mbilinyi 'Sugu' ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Joseph Haule 'Profesa J, Khadija Shabani 'Keisha', Ummy Wenceslaus 'Dokii', Mwanacotide na wengine.

  • Imenukuliwa kutoka kwenye blogu ya Habari za Kijamii

Kilimanjaro imekuwaje siku hizi? Aliyeongoza STD VII aozeshwa kwa kilo ya sukari?

Mmoja wa wanafunzi walioongoza mtihani wa Taifa wa darasa la saba mwaka huu mwenye umri wa miaka 16 kutoka wilayani Siha Mkoani Kilimanjaro anadaiwa kuozwa kwa mwanaume mwenye umri wa miaka 50 baada ya wazazi wake kupewa sukari kilo mbili kama mahari.

Kutokana na hali hiyo, Mtandao wa Kuelimisha Jamii kuhusu Ukeketaji mkoani Kilimanjaro (NAFGEM), umefanya jitihada za kumuokoa pamoja na wanafunzi wa kike wengine 15 waliotaka kufanyiwa vitendo vya ukeketaji kwa ngariba.

Msichana huyo wa miaka 16 wa kabila la kimasai kutoka kata ya Orkolili (jina limehifadhiwa) baada ya kufaulu mtihani huo, aliozeshwa kwa mmoja wa wanaume ambaye ni wafugaji wa kabila hilo.

Meneja Mipango wa Mtandao wa Kuelimisha Jamii kuhusu Ukeketeaji mkoani Kilimanjaro (NAFGEM), Honoratha Nasua, alitoa taarifa za kuokolewa kwa wanafunzi hao katika kijiji cha Naibili wilayani hapa.

“Wanafunzi 15 walikuwa wameandaliwa kwa ajili ya kukeketwa wakati wa mapumziko ya mwezi Desemba, mwaka huu na waliamriwa kuacha shule ili waozeshwe baada ya kukeketwa,” alisema.

Nasua alisema katika utafiti huo wamefanikiwa kupata orodha ya Mangariba wanaohusika katika mtandao wa ukeketaji.Alisema suala la mwanafunzi huyo aliyeozeshwa limefikishwa katika Dawati la Jinsia la Polisi Wilaya ya Siha mkoani humo kwa ajili ya kuchukua hatua zaidi za kisheria.

Kwa upande wake, Mkuu wa Dawati la Ukatili wa Kijinsia mkoa wa Kilimanjaro, Grace Lyimo, alisema mwanafunzi huyo aliyeozeshwa aliokolewa baada ya polisi na maofisa wa NAFGEM kuingilia kati.

Alisema wazazi wa wanafunzi huyo wameshiriki kudidimiza maendeleo ya mtoto wao kwa kukubali aolewe na kubuni mbinu mpya ya kukeketa watoto wachanga ili kukwepa vyombo vya dola na mkono wa wanaharakati.

Lyimo alisema utafiti uliofanywa na NAFGEM, umebaini kuwa kata zilizoathirika zaidi kwa ukeketezaji ni Orkolili, Makiwaru, Karansi, Gararagua na Biriri.

Hata hivyo, alisema inakuwa ngumu kudhibiti vitendo hivyo kutokana na kuingiliwa na masuala ya kisiasa kwa baadhi ya wagombea kuogopa kuchukua hatua kwa sababu ya kuogopa kukosa kura.

Awali, wanafunzi walionusurika kukeketwa walimweleza Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, Batilda Mhando aliyemwakilisha Mkuu wa wilaya ya Siha,kuwa hawapo tayari kuolewa wala kufanyiwa tohara.

Mtandao huo wa kupinga ukeketaji unaendesha shughuli zake katika wilaya hiyo ikishirikiana na Shirika la World Education kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la Kimataifa Marekani (USAID) kupitia mpango wa Pamoja Tuwalee.


Siha. Licha ya Serikali na mashirika yasiyoyakiserikali kupinga mila potofu zinazofanywa na jamii ya wafugaji kwa watoto wa kike, mila hizo zimeendelea kuwaathiri watoto hao wilayani Siha mkoani Kilimanjaro.

Inadai zaidi ya watoto wa kike 30 wamekimbia makwao baada ya kutakiwa kukeketwa na kuozeshwa wakiwa katika umri mdogo.

Mabinti hao walitoa kilio chao kwa uongozi wa Wilaya ya Siha wakati wa maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili iliyoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Nafgem.

Akisoma risala kwa niaba ya watoto wenzake, Rogathe Daniel (15) anayesoma darasa la sita katika Shule ya Msingi Donyomurwa, Kata ya Orkolili, alisema watoto 15 wako hatarini kukatishwa masomo baada ya wazazi wao kuwatafutia wachumba wa kuwaoa.

Mtoto huyo alisema yeye na wenzake 14 walikimbia baada ya kutakiwa kuozeshwa na wenzao 15 wanatakiwa kukeketwa mwezi huu.

meonyeshwa wachumba na kutakiwa kuozeshwa hata hivyo walifanikiwa kukimbia na kwenda kutoa taarifa kwa walimu waliowasiliana na polisi na shirika la Nafgem ambao waliwanasua kwenye kitanzi hicho. Alisema watoto wengine 15 wanatarajiwa kukeketwa mwezi huu.

baada ya shuke kufungwa, ukatili huu hufanywa na wazazi kwa kushirikiana na wanafamilia.

“Mkuu wa wilaya, mara nyingi sisi watoto hujiuliza mlinzi wetu yuko wapi? je viongozi wa Serikali wako wapi kutusaidia? tunaomba sana uwakumbushe viongozi hawa wajibu wao” alisema.

Mtoto huyo alisema licha ya wanafunzi wa maeneo mengine kufurahia kipindi cha likizo kifikapo, hali hiyo ni kinyume kwa watoto wa jamii ya wafugaji ambao ni muda wa kufanyia tohara.

Ofisa program kutoka Nafgem, Honoratha Nasua alisema pamoja na jitihada zinazofanywa na shirika hilo bado wanakabilina na changamoto kubwa kutoka kwa viongozi wa vijiji kutotoa ushirikiano pindi wanapopelekewa malalamiko na watoto juu ya ukeketaji na wanaoozeshwa wakiwa shuleni.

Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Siha, Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, Batilda Muhando alimtaka mkurugenzi wa Halmashauri hiyo pamoja na watendaji wa kata za jamii ya wafugaji kuhakikisha majina yaliyoripotiwa yanafuatiliwa na wahusika kuchukuliwa hatua za kisheria.
-------


Moshi. Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Utabibu cha Kilimanjaro Christian Medical (KCMU), amejifungua mtoto katika choo cha Hospitali ya Rufani ya KCMC na kisha kumtupa kwenye kasha la takataka.

Kcmu ni chuo kikuu kishiriki cha chuo kikuu cha Tumaini.

Tukio hilo ambalo limezua gumzo kubwa mjini hapa, lilitokea juzi asubuhi katika choo kilichoko eneo la mapokezi ya wagonjwa waliozidiwa (Casualty).

Habari kutoka KCMU na KCMC zimedai kuwa mwanafunzi huyo (jina limehifadhiwa) ni wa mwaka wa kwanza, anasomea masomo ya matibabu ya mazoezi ya viungo (Physiotherapy).

Kwa mujibu wa habari hizo, juzi mwanafunzi huyo alifika eneo hilo la mapokezi akiwa na mwanafunzi mwenzake na akaingia chooni kwa lengo la kujisaidia.

“Baadaye alitoka akionekana kama anachechemea na yule mwenzake akampokea mkoba aliokuwa ameubeba na kisha wakaondoka eneo hilo,” alidai mmoja wa wauguzi wa hospitali hiyo.

Ilidaiwa baada ya muda mfupi kupita, mhudumu wa usafi aliingia katika choo hicho na kukuta kuna damu iliyokuwa imetapaa sakafuni na mara alisikia sauti ya mtoto akilia kutoka kwenye kasha la taka lililokuwa ndani ya choo hicho.

“Alipoangalia ndania alimkuta mtoto mchanga ambaye alikuwa hajakatwa hata kitovu,” alisimulia muuguzi huyo.

Ofisa Uhusiano wa KCMC, Gabriel Chisseo alipohojiwa na gazeti hili, alikiri kuwapo kwa tukio hilo na kuthibitisha kuwa uchunguzi wa awali umeonyesha aliyemtupa mtoto huyo ni yule mwanafunzi.

“Ni kweli hilo tukio lipo na tumebaini ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza na alikwenda hapo Casualty kwa ajili ya kupata matibabu baada ya kuhisi kuumwa na tumbo,” alisema Chisseo.

Alisema mwanafunzi huyo amelazwa hospitalini hapo akichunguzwa afya yake.

Mtoto anaendelea vizuri na yeye anaendelea na matibabu na madaktari wanamchunguza Kisaikolojia ili kujua alipatwa na nini hadi akaamua kuchukua uamuzi huo,” alisema Chisseo.