Kongamano la Tafakuri ya UhuruJUMUIYA YA WANATAALUMA YA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM (UDASA) KWA KUSHIRIKIANA NA JUMUIYA ZA WANATAALUMA WA VYUO VIKUU VYA UMMA TANZANIA (ASAS)

inawaletea:

KONGAMANO LA TAFAKURI YA HATIMA YA UHURU 

MADA KUU: Miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara: Tumetoka Wapi, Tuko Wapi na Tunakwenda Wapi


MCHOKOZAJI WA MADA: Mama Getrude Mongela

Wazungumzaji wakuu

  1. Dkt. Alexander Makulilo
  2. Dkt. Ayoub Ryoba
  3. Dkt. John Jingu

TAREHE: JUMANNE, 9 DESEMBA 2014

UKUMBI: NKRUMAH, CHUO KIKUU CHA DSM

MUDA: SAA 8:00 MCHANA HADI SAA 12:00 JIONI

NYOTE MNAKARIBISHWA

Katibu wa CCM auawa kwa kukatwa shingo

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi kata ya Mwalugulu wilayani Kahama mkoani Shinyanga Daudi Lusalula anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya 55-56 ameuawa kikatili kwa kwa kuchinjwa shingo na watu wasiofahamika katika eneo la Malenge kata ya Mwaluguru wilayani humo wakati akitokea kwenye mkutano wa Chama cha Mapinduzi uliofanyika wilayani Kahama.

Tukio hilo limetokea jana saa mbili usiku wakati katibu huyo wa CCM kata ambaye pia ni Katibu wa Elimu, Malezi na Mazingira wa Baraza la Wazazi wa CCM wilaya ya Kahama akitokea Kata ya Kagongwa kwenda nyumbani kwake Sungamile baada ya kutoka kwenye mkutano wa chama chake uliokuwa unafanyika mjini Kahama.

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kahama Mabala Mlolwa ameiambia Malunde1 blog kuwa katibu huyo amechinjwa shingoni na watu wasiofahamika wakati akitoka eneo la Kagongwa akielekea nyumbani kwake.

“Siku ya tukio tulikuwa na mkutano na makatibu kata na madiwani wote wa CCM wilaya ya Kahama,tukijadili mikakati mbalimbali ikiwemo suala la uchaguzi wa serikali za mitaa,tulimaliza kikao saa nane mchana,majira ya saa mbili usiku tukapata taarifa katibu wetu ameuawa kwa kuchinjwa,”
ameongeza Mlolwa.

"Tunaomboleza msiba wa mwenzetu,amechinjwa shingo kama mfugo,inauma sana,tumepoteza mtu muhimu katika chama,wakati wa kikao chetu, mbali na veo vyake hivyo viwili pia wakati wa mkutano wetu alitangazwa kukaimu nafasi ya mwenyekiti wa wazazi wilaya ya Kahama,tunashukuru jeshi la polisi liko eneo la tukio kuchunguza juu ya kifo hiki,"
aliiambia Malunde1 blog.

Katibu wa siasa na uenezi mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Mlimandago alisema CCM inalaani kitendo hicho CCM na kwamba wamepata pigo kubwa kwani alikuwa na mchango mkubwa katika kujenga chama.

Hata hivyo Mlimandago alisema siyo vyema kuhusisha kifo hicho na moja kwa moja na mambo ya kisiasa bali vyombo vya dola viachwe vifanye kazi yake ili kubaini chanzo cha tukio hilo.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa bado wanafanya uchunguzi juu ya tukio hilo na kwamba taarifa kamili watatoa baada ya uchunguzi kukamilika.

LAPD to investigate abuse claim against Bill Cosby

Entertainer Bill Cosby gestures during a Nov. 6 interview about an upcoming Smithsonian exhibit featuring his family's extensive African-American art collection. Later in the interview, and in a subsequent NPR interview, Cosby refused to comment on the recently renewed attention given to rape allegations against him.Evan Vucci/AP

Los Angeles police say they will investigate a woman's claims that in the mid-1970s at the age of 15, she was molested by comedian Bill Cosby.

The Associated Press says:

"The investigation was opened Friday after Judy Huth, who is suing Cosby for sexual battery, met with detectives for 90 minutes, Officer Jane Kim said.
"Huth's civil suit claims Cosby forced her to perform a sex act on him in a bedroom of the Playboy Mansion around 1974 when she was underage."

The AP says Cosby's attorney, Martin Singer, filed a response on Thursday to the lawsuit by Huth, now 55, calling her claims "absolutely false" and alleging they are part of an extortion effort.

Although the LAPD did not give any details of the investigation, Police Chief Charlie Beck on Thursday urged potential victims of sex abuse by Cosby to speak with detectives, the AP says.

The latest troubles for Cosby, 77, come as more than 15 have come forward to accuse the comic actor of sexual misconduct including several claims of rape.

Cosby, in an interview with NPR last month, declined to comment on allegations by Barbara Bowman, who recently published a column in The Washington Post saying that in 1985, when she was 17, the comedian drugged and raped her. In a separate videotaped interview with the AP last month, Cosby replied "no comment" to a question about Bowman's charges.

Similar claims were made a decade earlier by another woman, Andrea Constand, who settled with Cosby out of court in 2006.

Sherehe za waliopata mgao wa 'escrow' zife! Ni lini Watajiuzulu?

Prof.Anna Tibaijuka na Mfanyibiashara Rugemarila wakisakata dansi ( ?kusherekea mgao wa fedha za escrow? )

  • Vigogo waliopata mgao ni lini Watajiuzulu?
  • Watanzania tunaomba haraka mkondo wa sheria ufanye kazi zake
  • Watanzania tunaomba sherehe za vigogo watuhumiwa zifikike mwisho

Ni mategemeo yetu Watanzania wengi kuwa vigogo waliohusika kwa namna moja au nyingine katika sakata la fedha za Tegeta Escrow Account kuwa wanajiuzulu nafasi zao na mkondo wa sheria uwashughulikie haraka kwani hakuna aliye juu ya sheria.

Vigogo hawa wazito wanahusika kupokea mgao wa fedha za wavujajasho wa nchi hii lazima washughulikiwe na vyombo vya dola ili wawe mfano kwa wengine kuwa mvunja sheria lazima mkondo wa sheria umshughulikie.

Kwa kuwa kila kitu kiko wazi katika sakata zima Tageta Escrow Account na wahusika wametajwa, basi hakuna haja ya kesho au keshokutwa, bali wao wenyewe watuhumiwa wangeachia ngazi kwa kujiuzulu ili kuonesha uzalendo wao kuwa wanaziheshimu sheria za nchi na Katiba ambayo ndiyo mama wa sheria zote.

Lingekuwa jambo la kiungwana sana kama wangejiuzulu wenyewe kabla ya kuenguliwa na mamlaka iliyowateua.

Baadhi ya vigogo hawa wapo Maprofesa, sasa hawa viongozi wetu Maprofesa ndiyo ingekuwa wa mwanzo kuonesha mfano wa kujiuzulu. Mfano Waziri wa Ardhi, Prof.Anna Tibaijuka. Yeye kakubali kwa namna moja kuwa kapokea mgao Tsh. bilioni 1.6 akidai kuwa ni za shule zake, wakati shule zenyewe kuna baadhi ya walimu kutoka nje ya nchi mabo wanalipwa mishaara kwa dola za Marekani!

Ni vema Waziri, Anna Tibaijuka akaonyesha mfano kwanza wa kujiuzulu.

Pia tungeshauri hati zao za kusafiria au pasipoti za vigogo hawa zichukuliwe na idara husika za usalama hadi pale itakapothibitika kuwa hawana hatia.

SHERA MSUMENO UKATE HUKU NA HUKU

Sijui tena kama patakuwa na kuchekeana kama hivi

  • "Rant" hii imewasilishwa hapa wavuti.com kupitia anwani pepe.

Picha za maonesho ya keki Dar na Washindi

Baadhi ya wananchi waliotembelea Maonesho ya 'Azam World of Cakes Exhibition' wakipita kuangalia keki.

Majaji wa Maonesho ya 'Azam World of Cakes Exhibition' watipita kukagua, kupata maelezo ya watengenezaji wa keki hizo kabla ya kuwapata washindi.

Baadhi ya wananchi waliotembelea Maonesho ya 'Azam World of Cakes Exhibition' wakipita kuangalia keki.

Marion Elias Mkurugenzi wa Kampuni ya Insights Productions Limited, ambaye pia Mratibu wa Maonesho ya 'Azam World of Cakes Exhibition' akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) katika maonesho hayo.

Majaji wa Maonesho ya 'Azam World of Cakes Exhibition' watipita kukagua, kupata maelezo ya watengenezaji wa keki hizo kabla ya kuwapata washindi.

Majaji wa Maonesho ya 'Azam World of Cakes Exhibition' watipita kukagua, kupata maelezo ya watengenezaji wa keki hizo kabla ya kuwapata washindi.

Keki mbalimbali zilizoshiriki katika Maonesho ya 'Azam World of Cakes Exhibition' yaliofanyika katika Hoteli ya Serena ya jijini Dar es Salaam.

Keki mbalimbali zilizoshiriki katika Maonesho ya 'Azam World of Cakes Exhibition' yaliofanyika katika Hoteli ya Serena ya jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya washiriki wa Maonesho ya 'Azam World of Cakes Exhibition' katika picha ya pamoja.

Baadhi ya washiriki wa Maonesho ya 'Azam World of Cakes Exhibition' katika picha ya pamoja.

Baadhi ya washiriki wa Maonesho ya 'Azam World of Cakes Exhibition' katika picha ya pamoja.

Keki mbalimbali zilizoshiriki katika Maonesho ya 'Azam World of Cakes Exhibition' yaliofanyika katika Hoteli ya Serena ya jijini Dar es Salaam.

Majaji wa Maonesho ya 'Azam World of Cakes Exhibition' wakijumuisha alama kabla ya kuwapata washindi.

Baadhi ya wananchi waliotembelea Maonesho ya 'Azam World of Cakes Exhibition' wakipita kuangalia keki.
JOPO la Majaji watatu na mabingwa wa fani za mapishi leo wamewatangaza mabingwa wa utengenezaji keki waliojitokeza katika Maonesho ya bidhaa za keki 'Azam World of Cakes Exhibition' yaliofanyika katika Hoteli ya Serena ya jijini Dar es Salaam.
Jumla ya makampuni na watengenezaji keki wapatao 39 wameshiriki katika maonesho hayo ya keki yalioandaliwa na kampuni ya Insights Productions Limited kwa udhamini wa Kampuni ya Azam Tanzania.

Akitangaza washindi katika maonesho hayo ya keki, mmoja wa majaji ambaye pia ni Mpishi Mkuu, toka Ramada Encore ya jijini Dar es Salaam, Edward Mukabana alisema timu ya majaji hao imewapata washindi wa kwanza watatu katika makundi matatu; yaani mshindi wa Keki yenye Radha Bora, Mbunifu Bora wa Keki na Mshindi wa Keki yenye Mvuto Kimuonekano.

Jaji huyo wa 'Azam World of Cakes Exhibition' aliwataja Amina Salim kuwa ndiye aliyeibuka mshindi wa keki yenye radha bora zaidi, huku kampuni ya Beta Bakery ikitwaa taji la mbunifu Bora wa Maonesho hayo ya keki. Pia alimtangaza Janeth Muawiriro kuwa ndiye mshindi wa keki yenye Mvuto kimuonekano katika washiriki wote.

Jopo hilo la majaji wa 'Azam World of Cakes Exhibition' pia lilimtangaza Leila Dhiyebi kuwa ni mshindi wa kwanza aliyepigiwa kura na wananchi waliotembelea maonesho hayo makubwa ya keki Tanzania. Kundi lingine la washindi ambao keki zao ziliwavutia majaji ni pamoja na Haika Shao na Caroline Gul pamoja na wanae wawili ambao walishiriki kubuni umbo la keki kwa mchoro iliyotengenezwa na mamayao.

Akizungumza awali kabla ya kuwatangaza washindi, Jaji Mkuu wa Mashindano hayo ya 'Azam World of Cakes Exhibition', Tom Owino (Executive Chef) alisema walisema wamezipitia keki zote za washiriki kuangalia vigezo mbalimbali vya upishi, muonekano na kuonja radha ya kila keki kabla ya kukaa chini na kuanza kufanya maamuzi ya pamoja ya majaji kwa kuzingatia vigenzo vya msingi katika utengenezaji keki.

Aidha kwa upande wake, Marion Elias Mkurugenzi wa Kampuni ya Insights Productions Limited, ambaye pia ni Mratibu wa maonesho hayo alisema maonesho hayo yamekuwa na mvuto baada ya kushirikisha makampuni na watu binafsi huku yakilenga kutangaza bidhaa nzima ya keki na ubunifu katika utengenezaji.

Alisema washiriki wote wamepata fursa ya kubadilishana uzoefu na kujifunza ubunifu zaidi wa shughuli hizo toka kwa wataalam wengine jambo ambalo litawabadili kwa namna fulani, ikiwa ni pamoja na kupata zawadi toka kampuni ya Azam na vyeti maalum vya kutambua mchango wao kiushiriki.

Kwa upande wake Mratibu wa Matangazo na Uhusiano wa Umma toka Kampuni ya SSB, Mohammed Ramadhan alisema Azam ikiwa ni kampuni inayotengeneza unga bora wa kutengenezea keki imeamua kudhamini ikiwa ni ishara ya kutambua taaluma hiyo ya utengenezaji wa keki nje na ndani ya Tanzania. Wananchi walipata fursa ya kuangalia keki mbalimbali pamoja na kuonja radha zake jambo ambalo lilileta mvuto zaidi kwa washiriki.

Kafulila apokelewa, ahutubia; Adai uchaguzi SM utapima ridhiko la Watanzania baada ya kuijua 'escrow'

Kafulila

MBUNGE wa Jimbo la Kigoma Kusini David Kafulila, amesema uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni, ni kipimo halisi cha kuona kama Watanzania wameridhika na serikali ya CCM kutochukua hatua dhidi ya watuhumiwa wa ufisadi wa  akaunti ya Tegeta escrow.

Kafulila amesema hayo muda mfupi mara baada ya kuwasili mkoani Kigoma, ambapo amepata mapokezi makubwa kutoka kwa wakazi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, kama shujaa wa sakata la akaunti ya Tegeta Escrow, na baadaye kusisitiza kauli hiyo alipohutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Mwanga Center, mjini Kigoma.

Amesema kukipigia kura Chama cha Mapinduzi CCM, katika uchaguzi ujao wa serikali za mitaa katika mazingira ambayo serikali yake imeshindwa kuchukua hatua katika ufisadi uliowekwa wazi na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzo Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG, ni kuonyesha kwamba wanaunga mkono ufisadi.

“nitoe wito kwa watanzania kwamba wanapaswa kuonesha hasira zao na uchaguzi huu wa serikali za mitaa ni kipimo kama watanzania tumekasirika ama hatujakasirika kutokana na ufisadi huu,”alisema Kafulila.

“uchaguzi huu ni kipimo kwamba haturidhishwi na jinsi mambo yanavyokwenda. Wanafunzi wamekosa mikopo kwa sababu serikali haina pesa, leo hii wananchi wanachangishwa fedha kwa ajili ya maabara wakati kuna watu wamepora zaidi bilioni 300!
Katika mazingira kama hayo wananchi wanapaswa kuonesha hasira zao, na moja ya njia za kistaarabu za kuonesha hasira ni kukataa kuchagua chama ambacho kinafanya maovu haya.”

Kauli hiyo ya Kafulila imekuja kufuatia baadhi ya vyombo vya habari kumnukuu Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Nape Nauye, akisema kuwa CCM haina mpango wa kuchukua hatua zozote dhidi ya wote waliotajwa kuhusika na kashfa hiyo.

Katika maelezo yake Nape alikaririwa akisema kuwa:
“Suala hili lipo chini ya Bunge na hivyo chama hakijaingilia kati na kuchukua hatua wabunge wake waliotajw. “Hatujawachukulia hatua (waliotajwa), wala hatuna mpango wa kuwachukulia hatua kwa sababu suala hili haliko ndani ya CCM… liko ndani ya bunge, labda kama litaingia ndani ya chama ndiyo tutalitolea maamuzi.”

Nape alikuwa akijibu swali kwamba suala la akaunti ya escrow litaathiri vipi chama chake kwenye uchaguzi kama rais Jakaya Kikwete atachelewa kuwawajibisha waliohusika na suala hilo kwa mujibu wa maazimio ya bunge ambapo Nape alijibu kuwa wao kama chama halitawaathiri chochote.

Kufuatia kauli hiyo David Kafulila amesema tafsiri ya kauli hiyo ni kwamba CCM inawatazama raia wa Tanzania kama watu ambao hawana ufahamu wa kutosha.

“unaposema kwamba hatutachukua hatua kwa watu ambao wanalalamikiwa na nchi nzima na kwamba hilo halituathiri kwenye uchaguzi, tafsiri yake ni kwamba pengine wana namna nyingine ya kushinda uchaguzi zaidi ya utaratibu wa kawaida ambao watu wanapigia kutokana na hisia zao, kutokana nay ale ambayo wanayaona,”aliongeza Kafulila.

Akisisitiza kauli yake Kafulila amesema nchi inapita katika kipindi kigumu ambacho kinahitaji mshikamano wa wanyonge kuweza kusimama kuhakikisha kwamba taifa linarudi kwenye mstari.

“tushikamane bila kujali itikadi za vyama tukijua kabisa kwamba tunachokifanya ndio njia pekee ya kuhakikisha taifa hili linabaki kuwa nchi moja; msipofanya hivyo nchi hii itasambaratika.”

Kauli ya Nape imekuja siku chache baada ya chama hicho kutoa msimamo wake dhidi ya wabunge wa chama hicho waliohusika katika sakata hilo kuwa bunge lichukue hatua stahiki. Nape, akiwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, katika ziara ya kukagua, kuhimiza na kusukuma utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2010/15 mkoani Mtwara, walisema kila aliyehusika katika kashfa hiyo, abebe msalaba wake.

Nape alisema chama hakiwezi kulea maovu yanayofanywa kinyume na kanuni na taratibu za chama hicho, hivyo kama bunge limebaini waliokiuka maadili wachukuliwe hatua stahiki dhidi yao. Kwa upande wake Kinana alisema muda wa kulindana na kubebana ndani ya chama umeisha na anayekiuka taratibu na kanuni za chama hicho awajibishwe na akishindikana achie ngazi.

Msafara wa mapokezi ya Kafulila umefunga barabara ya Lumumba Mjini Kigoma.

Msafara wa magari uliopmpokea Kafulila Airport Kigoma, ukimsindikiza hadi Hoteli ya Tanganyika Beach

Bango, "Mwigulu, Je wewe ni yule anayekuja 2015..."Mwigulu Nchemba akiwasili Uwanja wa MKutano Geita mjini.

Kiongozi wa ACT Kanda ya Ziwa (Mratibu) akitoa shukurani zake za dhati kwa Mwigulu Nchemba kwa namna alivyokuwa mfano kwa kuwatetea masikini na wanyonge ndani na nje ya Bunge.Comrade Mwigulu Nchemba wakiwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita hiyo jana wakati wa mkutano."Uchaguzi wa Serikali za Mitaa hatujazi nafasi, tunatafuta viongozi wenye uwezo wa kusimamia Halmashauri zetu za Vijiji, Mitaa na Vitongoji ili ziweze kufanya kazi za aendeleo kwa uadilifu na ufanisi wa hali ya kuridhisha"

Mwigulu Nchemba aliwasisitiza Wananchi kuchagua wagombea wa Chama Cha Mapinduzi kwa sababu ndiyo wenye sera inayotekelezwa, hivyo wanajua mahitaji ya Wananchi wao.

"Kuna Wananchi wanatamani sana kubadilisha vyama kama nguo. Kubadilisha vyama siyo suluhisho la kutatua kero za maendeleo. Tujitahidi kufanya maamuzi yenye tija wakati wa uchaguzi, tuchague viongozi imara na wenye nia ya kuwaongoza. Achaneni na kubadilisha vyama vya siasa."Nchemba alisisitiza kuwa, 

"hakuna atakayeichafua Tanzania na abaki salama. Hakuna atakayeiba mali ya umma akatembea kifua mbele. Wahujumu uchumi wote wa nchi hii waanze kujiandaa kisaikolojia."

Mkutano ulimalizika na wananchi kuanza kurejea makwao.

Awali Mkutano huu ulipaswa Kurushwa Live na Star Tv, ila kwa bahati mbaya mitambo yao ilikwama. Tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.

wavuti.com imeshirikishwa habari picha hii na Sanga Festo / Habari Kwanza

Rais Kikwete katika mazoezi

Rais Jakaya Kikwete akifanya mazoezi jana katika viwanja vya Ikulu ikiwa ni kufuata ushauri wa madaktari waliomtaka afanye hivyo mara tatu kwa siku ili kuendelea kuimarisha afya yake baada ya kufanyiwa upasuaji mwezi uliopita katika hospitali ya Johns Hopkins nchini Marekani. 
(picha: Freddy Maro/Ikulu)

Diamond awasili Marekani tayari kwa sherehe ya UhuruDiamond akiwasili kwenye uwanja wa kimataifa wa Dulles muda huu tayari kwa makamuzi ya sharehe ya Uhuru itayofanyika muda si mrefu Sheraton, ya Downtown Silver Spring, Maryland.Diamond akimsalimia mwenyeji wake hayupo pichani mara tu alipowasili Dulles.Kutoka kushoto ni Dj Romy Jones, Diamond na mmoja wa waratibu wa sherehe ya Uhuru Bwn. Phanuel Ligate

MOSES IYOBO, RAMA TONSA NA DJ ROMY JONES WALIPOWASILI WASHINGTON, DC
Kutoka kushoto ni Dj Romy Jones, Moses Iyobo na Rama Tonsa wakisubili usafiri na huku wakijaribu kupata mawasiliano mara tu baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dulles uliopo Sterling, Virginia tayari kwa kuwasha moto leo kwenye sherehe ya Uhuru itakayofanyika Sheraton ya Downtown Silver Spring.Moses Iyobo, Dj Romy Jones wakiwa uwanja wa ndege wa kimataifa mara tu baada ya kuwasili siku ya Ijumaa Desemba 5, 2014 kwa ajili ya sherehe ya Uhuru itakayofanyika leo Jumamosi Sheraton ya Downtown Silver Spring, Maryland.Moses Iyobo na Rama Tonsa wakiwasili hotelini mara tu baada ya kutoka uwanja wa ndege.Dj Romy Jones (Dj wa Diamond) akiendelea na mawasiliano akiwa hotelini.

 Kushoto ni Inno na watatu toka kushoto ni Phanuel ambao ni waratibu na waliomleta Diamond wakishirikiana na DMK (hayupo pichani wakiwa katika picha ya pamoja na Dj Romy Jones, Moses IyoboSaada Wadau kutoka Michigan wakiwasili tayari kwa show ya Diamond. Picha na Vijimambo.


  • Picha taarifa hii tumeshirikishwa wavuti.com kutoka kwa Luke Joe/Vijimambo Blog (shukurani)

Kigoma, mwisho wa reli!Picha kutoka kwa Dk B. Lelo

Tanzania's Azam Media launches in KenyaTanzania-based media company Azam Media has launched a new pay television service in Kenya to get a slice of the country's growing market. 
The move comes at a time when Kenya is expecting to finally shift from analogue to digital broadcasting beginning next month, a move expected to greatly facilitate growth of the local entertainment industry. 

Azam TV joins a growing list of media content providers recently licensed by the Communication Authority of Kenya, in the build-up of the digital migration switch whose global deadline is June 2015. On Wednesday, the government through CAK stated that the scheduled phase off of analogue signals will start with Nairobi at the end of this month with the second phase covering major towns including Mombasa, Malindi, Nyeri, Meru, Kisumu, Webuye and Kakamega. 

Other areas like Garissa, Kitui, Lodwar, Lokichogio, Kapenguria, Kabarnet and Migori will be covered in the second phase and by the end of march next year, television viewers from all over the country are expected to experience digital broadcasting. 

The pay TV market has traditionally been a hard nut to crack for players trying to break the dominance of South African company Multichoice which holds a majority share of the market. Azam media states that Azam TV will offer 60 local and international channels and will cost Sh870 per month, a pricing model which will drive volumes and boost revenue. 

"We know that there are other companies in the pay TV industry whose model is exclusive packages for a higher premium but we have one bouquet for all our subscribers which costs the same across the markets," 
said Mr Rhys Torrington, Azam TV CEO. 

The fully installed AZAM TV setup is retailing at an introductory price of Sh6,300 or Sh2,905 for a decoder and smartcard only for viewers who already have satellite dishes. The normal price for a decoder, dish and installation after the introductory offer will be Sh9,000. 

Azam Tv is on an ambitious African-wide expansion plan which has seen the company venture into Uganda, Kenya, Zaire and is currently eying Zambia and Rwanda. 

"We believe that there is a huge market particularly television viewers who are having their first pay TV experience and since launching in Tanzania exactly a year ago and in just under a year we have sold over 150,000 full decoder kits," 
said Torrington.

Polisi barabarani na Vodacom waelimisha na kupima vilevi madereva

Afisa wa Jeshi la Polisi – Kikosi cha Usalama Barabarani akimpima kiwango cha pombe mwilini dereva wa basi la kwenda mikoani, Steven Mwakibolo kwa kutumia kifaa maalum wakati wa upimaji madereva ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa kampeni ya Usalama Barabarani inayodhaminiwa na Vodacom Tanzania. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa kampuni hiyo Rosalynn Mworia, akifuatilia kwa karibu zoezi hilo lililofanyika leo katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani cha Ubungo jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia, akimuelimisha dereva wa basi liendalo mkoani Elias Samu kuhusiana na pete ya kidoleni inayotolewa na Vodacom Tanzania kwa ushirikiano na jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani yenye ujumbe “Wait To Send” unaohamasisha madereva wa vyombo vya moto kutokutumia simu za mkononi wakati wakiwa wanaendesha vyombo hivyo. Zoezi hili lilifanyika leo katika kituo cha mabasi yaendayo mkoani cha Ubungo jijini Dar es Salaam katika mwendelezo wa kampeni ya Usalama Barabarani inayodhaminiwa na kampuni hiyo.

Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Kamanda Mohammed Mpinga akiwafafanulia jambo Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia (kushoto) wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani Hamza Kassongo na Henry M. Bantu wakati wa zoezi la upimaji wa kiwango cha pombe mwilini kwa madereva wa mabasi yaendayo mikoani lililofanyika leo katika kituo cha mabasi cha Ubungo jijini Dar es Salaam. Zoezi hilo ni mwendelezo wa kampeni ya Usalama Barabarani inayodhaminiwa Vodacom Tanzania.

Maafisa wa Kikosi cha Usalama Barabarani wakimsomea dereva wa basi la kwenda mikoani matokeo yake ya vipimo vya kilevi mwilini wakati wa zoezi la upimaji wa kiwango cha pombe mwilini kwa madereva wa mabasi lililofanyika leo katika kituo cha mabasi yaendayo mkoani cha Ubungo jijini Dar es Salaam,anaeshuhudia kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia ambapo kampuni yake ni wadhamini wa kampeni ya Usalama Barabarani.

 Afisa wa Jeshi la Polisi – Kikosi cha Usalama Barabarani akimpima kiwango cha pombe mwilini dereva wa basi la mkoani, Elias Samu kwa kutumia kifaa maalum wakati wa zoezi la upimaji wa kiwango cha pombe mwilini kwa madereva wa mabasi yaendayo mikoani katika mwendelezo wa kampeni ya Usalama Barabarani inayodhaminiwa na Vodacom Tanzania. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia, akifuatilia kwa karibu zoezi hilo liliofanyika leo katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani cha Ubungo jijini Dar es Salaam.

Mjumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani Hamza Kassongo pamoja na maafisa wa Vodacom Tanzania wakionyesha pete zenye ujumbe wa “Wait to Send” wakati wa zoezi la upimaji wa kiwango cha pombe mwilini kwa madereva wa mabasi yaendayo mikoani lililofanyika leo katika kituo cha mabasi cha Ubungo jijini Dar es Salaam ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya Usalama Barabarani inayodhaminiwa na Vodacom Tanzania. Pete hizo ziligawiwa kwa madereva wa mabasi yaendayo mkoani zikiwa na ujumbe huo unaowakumbusha kusubiri hadi wakiwa wamesimamisha vyombo hivyo ndipo watumie simu zao za mkononi.