Kanisa Anglikana waanzishia waajiriwa wake mfuko wa mafao ya uzeeni

KANISA la Anglicana Dayosisi ya Tanga limeanzisha mfuko wa kulipa malipo ya uzeeni (Pensheni), watumishi wake kama mafao yatakayowasidia baada ya kustaafu utumishi katika kanisa hilo.

Hayo yalisemwa na Askofu wa kanisa hilo MahimboMndolwa wakati alipokuwa akizungumza kuhusu sherehe ya kumuaga mchungaji wa kigango cha Mashewa Thomas Ngereza, iliofanyika katika Kanisa ST. Andrews Manundu wilayani Korogwe Mwishoni mwa wiki.

Askofu Mndolwa, alisema kuanzishwa kwa mafao hayo ya uzeeni kutasaidia mhusika wakati atakapostaafu aepukane na maisha magumu yatakayowafanya wageuke kuwa ombaomba.

“Leo kwa pamoja tukiongozwa na Mwenyekiti wetu DominicSingano tumemzawadia mstaafu mabati 59, mbao, misumali kilo 10 pia alikabidhiwa cheti,”alisema Mndolwa.

Askofu Mndolwa, aliyataja baadhi ya mafao ambayo atayopatiwa mstaafu ni kama vile nyumba, gari na fedha, ambayo anaamini kuwa yatamsaidia mstaafu huyo katika kupambana na changamoto mbalimbali za maisha.

Licha ya kumuaga mchungaji Ngereza pia walikuwepo watumishi wengine wanne waliostaafu kutoka katika Taasisi ya Afya naSayansi Shirikishi ya St. Agustino ya wilayani Muheza ambao ni Mery Dismasi,Charles Juma, Peter Rajabu na Itikija Mbaga.

Askofu mstaafu wa Aglicana Dayosisi ya Tanga Philip Baji, alikemea tabia za baadhi ya wachungaji ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya wizi wa sadaka.

Sherehe hiyo ilihudhuriwa na Askofu mkuu mstaafu Anglicana Verentino Mokiwa kutoka jijini Dar, Askofu wa Anglikana Dayosisi ya Zanzibar Michael Afizi na Padri Joseph Mhina.


Serikali yapokea mabehewa 22 ya abiria na 50 ya mizigoSerikali imepokea mabehewa 50 ya mizigo na mabehewa 22 ya kisasa ya abiria ikiwa ni sehemu ya mabehewa 274 yanayotawarajiwa kuwasili nchini ili kuboresha huduma za usafiri wa mizigo na abiria.

Akizungumza na waandishi wa habari, Waziri wa Uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe amesema kuingia kwa mabehewa hayo ni ishara ya jitihada za serikali katika kuimarisha huduma ya usafiri wa reli ambapo amesema serikali imetumia zaidi ya bilioni 200 katika kuboresha sekta ya reli nchini.

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la reli nchini, Kipalo Kisamfu amesema mabehewa hayo ya abiria ni kwa ajili ya safari katika mikoa ya Mwanza na Kigoma, na kusisitiza shirika hilo kwa kushirikiana na wakala wa usafiri wa majini na nchi kavu wako katika mchakato wa kuanzisha usafiri wa haraka wa abiria ambao utasimama katika vituo vikubwa pekee.Picha: Ernest Nyambo

Sababu za operesheni "Ondoa CCM"


Chenge asema, "Nene nale nzoka ihenge" Achangia maabara milioni 116/=Mbunge wa Bariadi Magharibi Andrew Chenge juzi ameongoza harambee ya kuchangia ujenzi wa maabara katika halmashauri ya Mji wa Bariadi, ambapo alichangia kiasi cha shilingi milioni 116/= kati ya shilingi milioni 174.06/= zilizopatikana katika harambee hiyo.

Mbunge huyo ambaye alitajwa kupewa fedha kiasi cha shilingi bilioni 1.6 katika kashfa ya uchotwaji wa fedha akaunti ya Tegeta Escrow, alichangia kiasi hicho huku akikwepa kuongelea kashfa hiyo inayomkabili.

Hrambee hiyo ambayo ilikuwa imeandaliwa na Halmashauri ya Mji wa Bariadi, ilikuwa na lengo la kukusanya fedha kiasi cha shilingi milioni 400, fedha kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa maabara wilayani hapa.

Hata hivyo mbunge huyo alisema kuwa katika mchango wake, milioni 115 zitatumika kununua mabati 500 ambazo alisema ameamua kuezeka maabara zote za wilaya.

Kuhusu kupokea fedha Bilioni 1.6, kutoka katika akaunti ya Tegeta Escrow, mbunge huyo hakuweza kuzumgumzia kashfa hiyo na kubaki akitoa misemo kwa lugha ya Kisukuma.

“…suala la Escrow tuachane nalo kuna sehemu husika katika majukwaa nitaliongelea na wananchi wangu…hapa tuzumgumzie elimu na harambee hiii…hilo tuliache huko Dodoma na siyo la hapa Bariadi” 

“tuache hayo ya Dodoma mimi ndiye nyoka mwenye makengeza” neno aliloliongea kwa lugha ya Kisukuma “Nene nale nzoka ihenge” na kuongezeka kuwa yeye ni tumbili “ Nene nale nhombele.”

Baadhi ya washiriki katika arambee hiyo walieleza kuwa mbunge huyo alikuwa akimaanisha kuwa yeye anajua mengi sana kuliko wengine wanavyodhani na amepata bahati ambayo wengine hawawezi kuipata.

Wengine walieleza kuwa maneno ya mbunge huyo yalikuwa na maana kubwa, ambapo walibainisha kuwa alieleza kuwa kuna watu wengine wanajifanya wao wanafahamu kila kitu hapa nchini, wakiwa hawajui kuwa kuna watu waliwatangulia kujua.


Rais Kikwete amshukuru Mungu
Rais .Jakaya Mrisho Kikwete akiongea katika hafla ya kisomo maalum cha Kumshukuru Mwenyezi Mungu baada ya kufanyiwa upasuaji na kurejea nyumbani salama kilichofanyika katika viwanja vya ikulu jijini Dar es Salaam jana.


Rais Kikwete akiwasalimia Mashekhe na wageni waliohudhuria hafla ya kisomo maalum cha kumshukuru Mwenyezi Mungu baada ya kufanyiwa upasuaji na kurejea nyumbani salama kilichofanyika katika viwanja vya ikulu jijini Dar es Salaam jana.


Mjukuu wa Rais, Ayman Ridhiwani Kikwete akicheza kwa furaha wakati Babu yake Rais Kikwete akiwashukuru wageni na Mashekhe waliohudhuria hafla ya kisomo maalum kilichofanyika katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam jana.


Rais Kikwete akiwa na mjukuu wake Ayman Ridhiwani Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam muda mfupi baada ya kumalizika kisomo cha shukran kwa Mwenyezi Mungu kilichofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam jana. 

Picha zote: Freddy Maro/Ikulu

Watoto wa kituo cha "Mwandaliwa" waazimia kutimiza ndoto zao

Mwandaliwa

Tunu Jamal (17) hivi sasa anasoma kozi ya kutimiza ndoto yake ya kuwa Ofisa Ugavi katika Chuo cha Kilimanjaro Institute of Technology na ameanzia ngazi ya cheti ili akifanya vizuri aweze kujiendeleza zaidi.
Mbali na kozi hiyo anaungana na wenzake wanne wanaolelewa pamoja katika kituo cha Mwandaliwa kusoma kozi ya ushonaji ili ndoto yake isipotimia awe na ujuzi mbadala wa kuendesha biashara ya ushonaji.

“Nachukua mafunzo ya ushonaji wa nguo ili nisipofanikiwa katika fani ya ndoto yangu au nisipopata kazi haraka inayohusiana na kazi ninayoisomea niwe na kazi nyingine itakayoniwezesha kujipatia kipato cha kuendesha maisha yangu na kuweza kujitegemea”Anasema Tunu.

Kituo cha Kulea watoto yatima na wenye mazingira magumu cha Mwandaliwa mwaka huu kilipata msaada wa mashine za kushona nguo kutoka taasisi ya Vodacom Foundation ili kuwezesha kituo hicho kujitegemea badala ya kuendeshwa kwa kutegemea misaada.Darasa la ushonaji la kituo hicho hivi sasa lina cherahani ambazo zinawawezesha wanafunzi kujifunza fani ya ushonaji nguo.

“Tumeona mpango wa Mwandaliwa kujiendesha na tumetoa msaada utakaobadilisha maisha wanaolelewa katika kituo hiki,tumeona tuanze kusaidia mradi wa kufundisha watoto ushonaji kwa kuwa ni rahisi kutekelezwa na una uhakika wa kuwapatia kipato cha kuendesha maisha yao wakishapata ujuzi wa kutosha”.Anasema Reenu Verma,Mkuu wa kitengo cha Vodacom Foundation na kuongeza kuwa lengo kuu na kusaidia mradi huu ni kuona kituo cha Mwandaliwa kinapata uwezo wa kujiendesha.

Lengo la kituo kuanzisha mradi wa ushonaji ni kupata fedha za kulisha watoto,pia watoto kwa upande wao wameonekana kuufurahia mradi huu unaowawezesha kupata ujuzi utakaowawezesha kujitegemea siku za usoni na kukabiliana na changamoto za dunia ya sasa hivi yenye ushindani mkubwa.

Msimamizi wa kituo hicho Omar Kyaruzi ameishukuru taasisi ya Vodaom Foundation kwa kufadhili mradi huu wa ushonaji na kuongeza kuwa kwa muda mfupi umeonekana kuleta mafanikio kwa kuwa watoto wengi wamepata ujuzi na kituo kimeanza kupokea kazi za ushonaji wa sare za shule zilizopo jirani na kituo.

“Kupitia uwezeshwaji kama huu uliofanywa na taasisi ya Vodacom Foundation tumeanza kupata mafanikio ya kuelekea katika kujitegemea na tutaendelea kubuni miradi mbalimbali ya kusaidia kituo na watoto tunaowalea.Hivi sasa tuko mbioni kuanzisha kozi za kingereza,hesabu na mbinu za biashara ili kuwawezesha watoto kupata ujuzi utakaowawezesha kutimiza ndoto zao”.Anasema Kyaruzi.

Vodacom Foundation kupitia kampeni yake ya kuwawezesha wasichana ijulikanayo kama Girl Pawa inaendelea kusaidia miradi mbalimbali ya kuwajengea uwezo wasichana na wanawake ili waweze kutimiza ndoto zao.

Picha za Diamond aliponogesha sherehe ya Uhuru

Prezida wa Wasafi, Diamond Platnumz akiwa pamoja na wacheza show wake Roma Tonsa na Moses Iyobo wakitoa burudani katika kunogesha sherehe ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara iliyofanyika Sheraton Hotel ya Silver Spring, Maryland nchini Marekani na kuhudhuriwa na mashabiki wake kutoka kila pembe ya Marekani huku mashabiki wengine wakitokea Tanzania. (Picha zote: Vijimabo Blog)

Mzuka unazidi kupanda Diamond Platnumz asaula koti lake.

Balozi akimshukuru Diamond kwa kuwezesha kunogesha usiku wa Uhuru wa Tanzania na pia aliwashukuru wadhamini wa sherehe hiyo ya moaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara.

Diamond akizidi kuwapa burudani mashabiki wake

Shabiki akicheza wimbo wa mdogo mdogo

Shabiki akijumuika na Diamond kwenye jukwaa.


Picha zote tumeshirikishwa wavuti.com na Luke Joe/VIJIMAMBO blog (Shukurani)