Viongozi wamkabidhi Balozi Mulamula ripoti ya DICOTA Convention 2014


Viongozi wa DICOTA Lunda Asmani (kushoto)na Dr. Kurwa Nyigu wakitia saini kitabu cha wageni mara tu walipofika Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani uliopo Washington, DC kuonana na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamuala (hayupo pichani) na kumkabidhi ripoti ya mkutano wa kongamano wa DICOTA uliofanyika mapema mwezi wa Oktoba kwenye tarehe 2 mpaka 5 2014.


Viongozi wa DICOTA Lunda Asmani na Dr. Kurwa Nyigu walifika jioni ya Desemba 8, 2014 ofisi ya Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani uliopo Washington DC kumkabidhi Mhe. Liberata Mulamula ripoti ya mkutano wa kongamano wa DICOTA wa 2014 uliofanyika mapema mwezi Oktoka kati ya tarehe 2 mpaka 5.

Katika makabidhiano hayo yaliyo ambayo yalikua ni maelezo ya viongozi wa DICOTA na maoni ya wahudhuriaji wa mkutano huo wa kongamono wa ndani na nje ya Marekani ikiwemo DVD 2 ya mkutano huo.

Viongozi hao walimweleza Mhe. Balozi Liberata Mulamula kwamba mkutano wa DICOTA COnvention 2014 ulikua wa mafanikio na kutokana na swala la uchaguzi mkuu mwaka 2015 mkutano wa kongamano wa DICOTA hautafanyika na matarajio yao ni kuufanya mwaka 2016 mji na jimbo bado haijajulikana. Pia bwn. Lunda Asmani alielezea DICOTA inavyojihusisha kwa karibu na viongozi wa Jumuiya za Watanzania wa majimbo nchini Marekani huku wakijaribu kuboresha mahusiano na baadhi ya viongozi wa Jumuiya ambao hapo nyuma ulilegalega.

Mhe. Balozi Liberata Mulamula alianza kwa kuwashukuru viongozi hao kwa kupata wasaa wa kufika Ubalozini na kukabidhi ripoti na DVD na kusema alifurahi sana na mkutano wa DICOTA uliofanyika Durham, North Carolina kwani ulikua wa mafanikio  makubwa na ulitoa fulsa nyingi kwa wahudhuriaji wa mkutano huo mwaka huu. Mhe. Balozi Liberata Mulamula aliwaasa viongozi wa DICOTA kuendelea kuwasiliana na wadhamini wa mkutano huo hasa walioweza kufika na kunadi bidhaa zao ili waweze kujua maendeleo ya bidhaa walizonadi kwenye mkutano huo akitolea mfano wa Azania Bank, NHC, PPF na wengine ambao wangependa kujua ni Watanzania wangapi nchini Marekani walionufaika na ujio wao kwenye mkutano huo. Kwa kufanya hivyo kunaleta mahusiano mazuri na wadhamini ili wasiishie hapo wazidi kuwatangza na wao kujitangaza kupitia mikutano ya DICOTA.

Mhe. Balozi Liberata Mulamula aliendelea kwa kusisitizia viongozi hao kuendeleza mahusiano na Jumuiya za Watanzania nchini Marekani hususani viongozi wa Jumuiya hizo na kutafuta uwezekano wa kukutana nao mara kwa mara na akashauri Jumuiya zinapofanya mijumuiko yao na vyema na wao wakatuma mwakilishi kuhudhuria mijumuiko hiyo huku akitoa mfano wa sherehe za Uhuru zinafanyika kwenye majimbo toafauti ni vizuri DICOTA kutuma mwakilishi ili kuwa karibu na Jumuiya hizo pia kutajenga mshikamano wa karibu na Viongozi wa Jumuiya hizo.

Mwisho viongozi wa DICOTA waliuomba Ubalozi wasisite kuwaita mara wanapohitaji msaada wao kwani wanapotoa msaada kwa Ubalozi hujisikia kufarijika kwani ni furaha ni kutumia utaalamu na uzowefu wao katika kusaidia kusukuma kurudumu la maendeleo kwa kwa pamoja tunaweza.

 Viongozi wa DICOTA Dr. Kurwa Nyigu (kushoto na Lunda Asmani(wapili toka kushoto) wakifanya mkutano wa makabidhiano ya ripoti ya mkutano wa kongamano wa DICOTA wa 2014 na Mhe. Liberata Mulamula akiwemo Afisa Ubalozi Switebert Mkama(kulia) jioni ya Jumatatu Desemba 8, 2014 katika Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani uliopo barabara ya 22 NW, Washington, DC.
 Mkutano wa makabidhiano ukiendelea
 Kiongozi wa DICOOTA Lunda Asmani akimkabidhi Mhe. Balozi Liberata Mulamula Ripoti ya mkutano wa kongamano wa DICOTA wa 2014 uliofanyika mapama mwezi wa Oktoba Durham, North Carolina nchini Marekani.
 Kiongozi wa DICOTA Lunda Asmani akitoa maelezo kwa Mhe. Balozi Liberata Mulamula kuhusiana na ripoti hiyo.
 Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiipitia kwa haraka haraka ripoti hiyo
 Kiongozi wa DICOTA Lunda Asmani akimkbidhi Mhe. Balozi Liberata Mulamula DVD za mkutano wa kongamano wa DICOTA wa 2014 uliofanyika mapema mwezi Oktoba Durham North Carolina nchini Marekani.
 Kiongozi wa DICOTA Lunda Asmani akiemwelezea jambo mhe. Balozi Liberata Mulamula.
 Kiongozi Lunda Asmani akiendelea kuelezea jambo huku kiongozi mwenzake Dr. Kurwa Nyigu akimsikiliza.
Afisa Ubalozi Switebert Mkama akifuatilia mkutano wa makabidhiano wa ripoti ya DICOTA Convention 2014 uliofanyika Durham, North Carolina mapema mwezi wa Oktoba 2014.

Salamu za Balozi Mulamula za Miaka 53 ya Uhuru

[audio] DMV All Stars - Najivunia

Desemba 9, 2014 ni siku ya uhuru wa Tanganyika. Wakati taifa la Tanzania linaadhiminisha miaka 53 ya uhuru, tunapenda kuwasilisha rasmi wimbo “Najivunia”. Wimbo “Najivunia” umetungwa na kurekodiwa Maryland, USA na kundi la wasanii wa Kitanzania waishia Marekani kwa ushirikiano na DMK Global Promotions kuadhimisha miaka 53 ya uhuru wa Tanzania.
Wasanii wenyewe ni:

DMV All Stars:

Mr.Tz aka SanTized
Prince Herry
Dominic
E-Breezy (Ibra. Max)
AJ Ubao

Jamaa kaulizwa na Rais nikusaidieni? Akajibu 'pombe'; Akapewa!

RAIS Uhuru Kenyatta ameombwa pombe na mlevi na gesi what? Amempatia.

Imeelezwa na mtandao wa Maisha kwamba rais huyo ambaye ana katabia ka kutembea bila ulinzi mkali, Jumapili hii alienda kuhani kifo cha mfanyabiashara mmoja huko Githunguri. Katika safari yake hiyo alikuwa na gari moja na walinzi wachache kweli kweli.

Akiwa kwenye maduka ya Gathaje kiasi cha kilomita 2.5 kutoka Githunguri alikutana na mlevi mmoja ambaye alipomuona alikuwa kama kjapigwa shoti na Rais akamuuliza kikwao yaani kumeki wish.

“Ukuenda nguikire atia? (naweza kukusaidia nini?).” aliuliza.
“Ngurira kanuthu.. (ninunulie nusu)” alisema jamaa.

Na hiyo nusu unajua ni ghali kiasi gani?
Inagharimu bob 60 tu.

Zitto Kabwe: Mhanga wa mafanikio yake

ZITTO Zuberi Kabwe ni mwanasiasa mdogo kiumri lakini mwenye mafanikio na changamoto nyingi kiuongozi na kisiasa kuliko umri wake. Katika makala haya tunajadili wasifu wa mwanasiasa huyu katika maeneo mbalimbali yanayohusu sifa muhimu za Rais ajaye.

Zitto alizaliwa tarehe 24 Septemba 1976 katika Kijiji cha Mwandiga, Wilaya ya Kigoma. Alisoma katika Shule ya Msingi Kigoma kutoka mwaka 1984 hadi mwaka 1990. Alisoma katika Shule ya Sekondari Kigoma (1991-1994) na kumalizia katika Shule ya Sekondari Kibohehe (Moshi) kati ya mwaka 1994 na 1995, akiwa amepata daraja la kwanza (Division 1:8).

Alisoma katika Shule ya Juu ya Sekondari Galanos (Tanga) mwaka 1996 na kumalizia katika Shule ya Sekondari Tosamaganga (Iringa) mwaka 1998, akiwa amepata daraja la pili huku akiibuka mwanafunzi bora katika somo la uchumi katika Mkoa wa Iringa.

Zitto ana shahada ya uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam aliyoisomea kati ya mwaka 1999 na 2003, akiwa amepata alama 3.5 (second upper class). Zitto ana Diploma ya Juu katika Masoko ya Kimataifa kutoka Chuo cha Inwent-IHK kilichopo mjini Bonn nchini Ujerumani aliyehitimu mwaka 2004, na ana shahada ya umahiri katika sheria na biashara kutoka Chuo cha Sheria cha Bucerius nchini Ujerumani aliyohitimu mwaka 2010.

Mambo mawili yanajitokeza kuhusu elimu ya Zitto

Mosi, amesoma vizuri; hii ni sifa muhimu kwa kiongozi wa kisiasa katika nyakati za sasa kwa sababu elimu ni msingi wa fikra na falsafa unaohitajika kwa kiongozi kuweza kutoa dira na ushawishi.

Aidha, tafiti nyingi zinaonyesha kwamba elimu ni sifa ya kwanza ya kiongozi miongoni mwa wapiga kura walio wengi nchini Tanzania.

Pili, ukichunguza miaka aliyosoma Zitto utaona kwamba amesoma miaka mingi zaidi kwa elimu ya sekondari na Chuo Kikuu kuliko ilivyo kawaida.

Hii ni kwa sababu alipokuwa akisoma Shule ya Sekondari Kigoma alifukuzwa shule kwa kudaiwa kuwa alianzisha, kuendesha na kufanikisha mgomo yeye akiwa Kiranja Mkuu. Ndipo akalazimika kuhamia Shule ya Sekondari Kibohehe mkoani Kilimanjaro.

Aidha alipokuwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Zitto alilazimika kurudia mwaka baada ya kusimamishwa masomo kutokana na kuhusishwa na mgomo wa kupinga sera ya uchangiaji wa gharama za elimu ya juu.

Alikuwa ametuhumiwa kuwa alikuwa miongoni mwa viongozi waliochochea mgomo huo yeye akiwa Mwenyekiti wa wanafunzi waliokuwa wanakaa Hosteli ya Kijitonyama.

Hii maana yake ni kwamba ‘ukorofi’ wa Zitto tunaouona leo ulianza siku nyingi.

Zitto amefanya kazi katika maeneo kadhaa kabla ya kuwa mbunge. Alipata kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Wanafunzi nchini (TSNP) kati ya mwaka 2001 na 2003.

Na kabla hajagombea ubunge na kushinda, Zitto alipata kuajiriwa na Shirika la Ujerumani (FES) kama Meneja wa Miradi kati ya mwaka 2004 na 2005.

Kiuongozi, Zitto alikuwa Kiranja Mkuu wakati akisoma Shule ya Sekondari Kigoma na baadaye kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanafunzi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (DARUSO) kati ya mwaka 2001 na 2003.

Ndani ya CHADEMA, Zitto alishika nafasi kadhaa za uongozi kabla ‘hajakorofishana’ na viongozi wenzake. Kwanza, alikuwa Mkurugenzi wa Mambo ya Nje mwaka 2004 na wakati huo huo akiwa pia Mkurugenzi wa Uchaguzi na kampeni wa chama hicho.

Mara baada ya kuchaguliwa kuwa mbunge mwaka 2005, Zitto alichaguliwa kuwa Katibu wa wabunge wa CHADEMA. Mwaka 2007 alichaguliwa na Baraza Kuu la CHADEMA kuwa Naibu Katibu Mkuu Bara, nafasi ambayo aliishikilia hadi mwaka jana baada ya kuondolewa na Kamati Kuu ya chama hicho.

Ndani ya Bunge, Zitto alipata kuwa Mwenyekiti wa iliyokuwa Kamati ya Mashirika ya Umma (POAC) na baadaye kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC). Ni katika kipindi cha uenyekiti wa Zitto, ndipo ambapo kamati hizi zilijulikana sana kwa jamii.

Kihaiba, Zitto ana sifa mbili muhimu ambazo ni taswira chanya ya uongozi lakini wakati huo huo ikiwa ni taswira tata ya kiuongozi katika mazingira ya kitanzania.

Sifa ya kwanza ni tamaa na ujasiri wa kupenda kufanya makubwa ambayo hugeuka kuwa kero kwa baadhi ya viongozi wenzake anaofanya nao kazi.

Kwa mfano, akiwa anamaliza muda wake kama Katibu Mkuu wa DARUSO ‘alilazimisha’ hesabu za taasisi hiyo zikaguliwe na wakaguzi wa hesabu (auditors) kabla hawajakabidhi ripoti kwa uongozi mpya.

Hii haikuwa kawaida ya DARUSO na baadhi ya viongozi wenzake hawakulipenda jambo hili na wakamnunia.

Zitto amekuwa kinara wa kuibua ‘madudu’ mengi serikalini kuanzia kashfa ya Buzwagi, mabilioni ya Uswisi na sasa sakata la kashfa ya akaunti ya Escrow.

Pengine, taswira ya Zitto kuhusu tamaa na ujasiri wa kupenda kufanya mambo makubwa ni kitendo cha kamati anayoiongoza ya PAC kuwasweka ndani viongozi wa juu wa TPDC kwa kushindwa kutekeleza amri ya kamati hiyo.

Bila kuingia ndani ya sakata hili, ni wazi kwamba hili ni jambo ambalo lilikuwa halijawahi kutokea huko nyuma na linaweza likawa limefungua ukurasa mpya katika mahusiano kati ya Kamati za Bunge na uongozi wa taasisi za umma.

Sifa ya pili kihaiba kuhusu Zitto ni uvumilivu. Katika maisha yake ya kisiasa, Zitto amekumbana na misukosuko mingi hasa kuhusu kashfa mbalimbali zinazomlenga.

Tangu azozane na viongozi wenzake ndani ya CHADEMA kufuatia uamuzi wake wa kugombea uenyekiti mwaka 2009, Zitto amekuwa akirushiwa kashfa mbalimbali zenye lengo la kuchafua taswira yake kisiasa katika jamii.

Pamoja na kwamba hakuna hata kashfa moja ambayo imepata kuthibitishwa kimantiki na kisheria, kashfa hizo zimefanikiwa kutikisa taswira yake kiuadilifu.

Kifamilia, Zitto Kabwe hajaoa lakini ana mtoto mmoja wa kiume maarufu kwa jina la Chachage.

Hili ni jina alilompa mtoto wake kutokana na mapenzi makubwa aliyokuwa nayo kwa mhadhiri maarufu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, marehemu Profesa Chachage Seithy Chachage.

Kikazi, Zitto ana sifa tatu zinazomtenga kwa mbali na wanasiasa wengi hapa Tanzania. Mosi, Zitto anaamini kikamilifu katika itikadi, falsafa na sera kama msingi wa uongozi wa kisiasa.

Katika kipindi ambacho ujamaa umepoteza mashiko katika Bara la Afrika, yeye anajipambanua waziwazi kwamba ni mjamaa akiamini katika falsafa ya Unyerere.

Zitto anaamini kwamba kijiji ndiyo kitovu cha maendeleo ya Mtanzania na ni muhimu kuwekeza katika kilimo. Ndiyo mwanasiasa pekee nchini na pengine katika bara la Afrika aliyeweza kuisimamia kwa vitendo dhana ya hifadhi ya jamii kwa mwananchi wa kawaida hadi katika ngazi ya kijiji.

Ni kwa sababu hii, amekuwa mwanasiasa wa kwanza barani Afrika kushinda tuzo ya hifadhi ya jamii. Zitto pia anaamini katika demokrasia rasilimali kama msingi wa kuwapa wananchi fursa ya kumiliki na kufaidika na rasilimali za taifa.

Pili, Zitto anajipambanua kifikra. Hili linajitokeza katika ukweli kwamba Zitto ni miongoni mwa wananasiasa wachache hapa nchini wanaosoma sana. Mimi na yeye kila mwisho wa mwaka huwa tunapeana hesabu kuhusu idadi ya vitabu ambavyo kila moja wetu amevisoma kwa mwaka huo.

Aidha, Zitto ni mwandishi mzuri akiwa ni miongoni mwa wanasiasa wachache kabisa hapa nchini wenye uwezo na utayari wa kuandika makala. Kwa sababu hii sio kazi ngumu kujua anachofikiri na kukiamini Zitto kwani fikra zake zipo wazi kupitia maandishi yake.

Sifa ya tatu kikazi inayomtenga na wanasiasa wenzake wa upinzani hapa nchini ni mtandao mpana alionao ndani na nje ya nchi.

Kwa hapa nchini, Zitto ni mwanasiasa pekee wa upinzani aliyeonyesha uwezo wa kufanya kazi na kushirikiana na wanasiasa wa vyama vingine bila kujali tofauti zao za kisiasa.

Zitto ana uhusiano mzuri na viongozi mbalimbali nchini, wakiwemo viongozi wastaafu wanaoheshimika nchini.

Zitto ana mahusiano mema ya kikazi na viongozi wa vyombo vya dola ndani ya Jeshi la Wananchi, Polisi na Usalama. Hii ni sifa muhimu kwa kiongozi anayejiandaa kuwa mkuu wa nchi na dola.

Aidha, Zitto ana mahusiano mema ya kikazi na viongozi mbalimbali katika bara la Afrika, Amerika, Ulaya na Asia, pamoja na taasisi za kimataifa.

Hii nayo ni sifa muhimu kwa kiongozi anayejiandaa kushika uongozi wa juu wa nchi kwa sababu mafanikio ya kiongozi wa juu hutokana kwa kiasi kikubwa na mahusiano yake na Jumuiya ya Kimataifa.

Mafanikio ya Zitto Kabwe ndiyo pia udhaifu wake, hasa katika mazingira ya siasa za Tanzania. Kikazi, Zitto anaponzwa na tabia yake ya kutokuendana na utamaduni wa kimaisha na kisiasa wa Tanzania.

Kwa mfano, katika jamii yetu watu wanaofanya kazi kwa bidii sana hutazamwa kwa jicho lisilo chanya sana. Tangu tukiwa shuleni, mwanafunzi anayesoma sana hupachikwa majina ya ajabu ajabu kama vile ‘mnoko’, ametumwa na kijiji, ‘msongo’, n.k.

Tukiwa kazini, watu wanaofanya kazi sana kwa kuzingatia taratibu si miongoni mwa watu wanaopendwa.

Watu wa namna hii huonekana kama wanajipendekeza na ‘kujifanya wajuaji’ na hivyo hupachikwa majina mbalimbali na hata kupakaziwa.

Utamaduni huu pia upo katika siasa na kwa kiasi umemponza sana Zitto kwani anaonekana kama ni mwanasiasa mwenye kimbelembele kwa tabia yake ya ‘kung’ang’ania’ hoja mbalimbali zenye maslahi mapana kwa jamii na nchi.

Pili, ukaribu wa Zitto na viongozi wa serikali umefifisha taswira yake kisiasa kama mpinzani.

Tangu mfumo wa vyama vingi uanze katika nchi yetu viongozi wa upinzani wamejitahidi kujenga taswira kwamba wapinzani ni wakombozi na CCM ni wakoloni weusi.

Kwa hiyo siasa za upinzani ni siasa za harakati mithili ya wapigania uhuru enzi za ukoloni.

Kwa sababu ya taswira hii, kiongozi yeyote wa upinzani anayekuwa karibu na viongozi wa CCM na serikali kwa uwazi huonekana kwamba ni msaliti wa harakati za ukombozi.

Kwa utamaduni wetu wa kisiasa upinzani si ushindani wa hoja kati ya chama cha upinzani dhidi ya CCM, bali ni harakati za kumtoa ‘mkoloni’ mweusi kwa kile kinachoelezwa kwamba ni ukombozi wa pili.

Eneo la tatu la udhaifu wa Zitto katika maziingira ya siasa za upinzani Tanzania lipo katika aina ya siasa anazofanya.

Wakati yeye huamini kwamba kazi ya upinzani ni kujenga hoja mbadala, viongozi wenzake wa upinzani wanaamini kwamba kazi ya msingi ya upinzani ni kushambulia haiba na matendo ya viongozi wa chama tawala.

Kwa sababu ya tofauti hizi za kimtazamo, Zitto amejikuta yupo mbali kabisa na viongozi wenzake wa upinzani na hivyo kujikuta kama mtoto yatima akilelewa na walezi wasio mpenda.

Nilipomuuliza yeye anaamini ni kwa nini aligombana na viongozi wenzake ndani ya CHADEMA, Zitto alikuwa wazi kabisa kwamba ilikuwa ni mapema mno kwa yeye kugombea uenyekiti wa CHADEMA mwaka 2009.

Kwamba tangu agombee uenyekiti mwaka 2009, wenzake walimuona ni msaliti na mahusiano yao hayajawahi kurudi katika hali ya kawaida.

Ni wazi kuwa Zitto ameshindwa kuenea katika utamaduni wetu wa kisiasa, ambao hauruhusu ushindani wa kisiasa hasa ndani ya vyama vya upinzani.

Kiongozi wa upinzani huongoza hadi pale atakapochoka au kuchokwa sana na hata pengine atakapoitwa na mola.

Kwa hiyo Zitto alikuwa ‘mjinga’ kwa kuamini kwamba angeweza kupata uenyekiti wa CHADEMA kwa kujaza fomu na hatimaye kupigiwa kura.

Nami lazima nikiri kwamba nilikuwa ‘mjinga’ kwa kumshawishi na hatimaye kumtia moyo kugombea nikiamini kwamba ushindani wa kisiasa ndani na baina ya vyama ndiyo msingi na kiashiria cha kukua kwa demokrasia katika nchi.

Pengine udhaifu mkubwa wa Zitto kama kiongozi upo katika maeneo makubwa mawili.

Kwanza, ni kushindwa kupima maana na matokeo mapana ya kauli zake kabla hajazitoa. Mara kadhaa Zitto amekuwa akitoa kauli ambazo huacha ukakasi mkubwa katika jamii.

Kwa mfano, akiwa katika kampeni za ubunge mwaka 2010 alitangaza kwamba katika awamu ijayo angerudi kugombea urais na siyo ubunge tena.

Zitto alitoa tangazo hili huku akijua kwamba chama chake kilikuwa na mgombea urais na kwamba kauli kama ile ingeweza kupunguza imani ya wapiga kura kwa mgombea wa chama chake kwa kuonyesha kwamba asingeshinda na pengine alikuwa hafai.

Pili, baadhi ya kauli za Zitto huonyesha kwamba ni kiongozi anayechokozeka kirahisi.

Kwa mfano, alipomwagiwa ‘upupu’ na Tundu Lissu mapema mwaka huu kwamba alikuwa amehongwa magari na Nimrod Mkono, Zitto alitoa kauli ya haraka tata kwamba, yeye asingekufa kama alivyokufa Chacha Wangwe (“Chacha died, I won’t”).

Hii ni kauli tata kwa sababu inatoa taswira kwamba pengine Chacha Wangwe hakufa kwa ajali kama inavyojulikana bali aliuawa na watu ndani ya chama chake.

Pili, kwamba yeye asingekufa kama Wangwe inaweza kutoa taswira kwamba Zitto ana nguvu za ziada za kumkinga na kifo.

Eneo la pili la udhaifu wa Zitto lipo katika mahusiano ya kimapenzi yasiyoeleweka kwa mtu mwenye dhamana ya uongozi. Zitto amekuwa akihusishwa na wasichana kadhaa maarufu hapa nchini ambao maadili yao kindoa yanatia shaka katika mazingira ya Kitanzania.

Inapokuja katika mahusiano ya kimapenzi, Zitto hujisahau kabisa kwamba yeye ni kiongozi mkubwa katika jamii pamoja na kwamba ana haki zake kama binadamu.

Pengine hili ndilo eneo ambalo Zitto ameshindwa kujitofautisha na wanasiasa wenzake hapa nchini, ambao wengi wao nao uadilifu wao katika eneo hili ni wa mashaka.

Hitimisho

Zitto Kabwe ni kiongozi aliyejipambanua kiitikadi, kifalsafa, kisera na kimsimamo. Husimamia anachokiamini bila kujali wengine wanaamini nini na watamwonaje.

Ni miongoni mwa viongozi wachache kabisa hapa nchini wanaoheshimu kazi za kitafiti na kitaalamu.

Ni kiongozi mwenye bidii, umakini na weledi katika kazi. Katika umri wake wa miaka 38, Zitto Kabwe amefanya mambo makubwa kisiasa na kijamii.

Hoja zake kuhusu mikataba ya madini zilifanikisha kubadilishwa kwa sheria ya madini na kwa mara ya kwanza kuifanya nchi yetu ianze kuambulia angalau mapato kidogo katika sekta hii.

Pamoja na sifa alizonazo za kuweza kuwa kiongozi mkuu wa nchi, Zitto Kabwe hatagombea mwakani kwa sababu za kikatiba. Pengine hii ni fursa kwa Zitto kuendelea kujipanga zaidi na kurekebisha baadhi ya maeneo yanayotia doa taswira yake kiuongozi.

Hata hivyo, mafanikio ya Zitto kisiasa huko mbele yatategemea zaidi na aina ya taasisi ya kisiasa atakayofanya nayo kazi.

Kama Zitto ataendelea kufanya siasa ndani ya chama chake cha sasa na viongozi hawa waliopo, hakuna shaka kwamba taswira ya usaliti itaendelea kushamiri kwa sababu siasa zake haziendani na utamaduni wa kisiasa wa viongozi wa sasa wa chama hicho.

Kwa sababu hii, Zitto Zuberi Kabwe anahitaji kuchukua hatua nyingine moja kubwa ya kijasiri katika maisha yake ya kisiasa, ambayo ni kujiunga na chama ambacho ana nafasi na fursa ya kujenga utamaduni mpya wa kisiasa hapa nchini.

Yaya aliyemkatili mtoto Uganda apanda kizimbani

...akimkanyaga mtoto

Yaya ambaye ametuhumiwa kumpiga mtoto wa miezi 18 nchini Uganda kiasi cha kuleta kizaazaa katika mitandao ya kijamii, jana kwenye mahakama ya Uganda amekiri kosa hilo na kuomba wazazi wa mtoto, taifa la Uganda na mahakama kumsamehe.

Mdada huyo wa kazi alinaswa na kamera maalumu za usalama akimwadhibu kikatili kabisa mtoto wa miezi 18 ambaye alikuwa mgonjwa baada ya kutapika wakati akilimlisha.

Jolly Tumuhirwe, 22, ambaye alifikishwa mahakamani kwa tuhuma za kumtesa binti wa miezi 18 amekiri kufanya vitendo hivyo.

Baba wa mtoto, Eric Kamanzi, ambaye aliweka kamera hizo sebuleni baada ya kubaini binti yake alikuwa ana michirizi na huku anashindwa kutembea vyema.

Video ilinyochukuliwa iliioneshwa inamuonesha Tumuhirwe akimpiga mtoto wakati alipokataa kuendelea kula kabla ya kumtupa chini, kumpiga na tochi na kumkanyaga.
Video hiyo ambayo haikuoneshwa mahakamani leo imeshaonwa na maelfu ya watu katika mtandao wa kijamii.

Shauri hilo lilifika katika mikono ya polisi Novemba 13 mwaka huu.

Tumuhirwe, ambaye hakuna na uwakilishi wa wakili katika shauri hilo anakabiliwa na kifungo cha miaka 15 jela au faini ya dola za Marekani 400 au vifungo vyote viwili.

Mmoja wa wanasheria mashuhuri nchini Uganda alijitolea kumtetea mdada huyo wa kazi lakini mahakama ilimweleza kwamba hakufuata taratibu katika shauri hilo kwa hiyo alikataliwa kumtetea.

Baba wa binti huyo alidodndosha amchozi wakati mdada huyo wa kazi akiuomba kuosamehewa kwa matendo yake.

Kesi hiyo itafikishwa mahakamani Jumatano kwa ajili ya kutolewa hukumu.

Baada ya watu kulalamika awali polisi walisema kwamba wanataka kubadili mashtaka yawe jaribio la kuua.
Hata hivyo Mwendesha mashtaka mkuu wa serikali amesema kwamba wakati uchunguzi unaendelea mashtaka dhidi ya binti huyo yatakuwa ya kutesa mtoto.

baba mtoto mahakamani Jumatatu

Yaya mwenyewe mahakamani jana

Mtoto aliyebamizwa

Taarifa ya Ikulu ya Rais Kikwete kuanza kazi rasmi

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumatatu, Desemba 8, 2010, ameanza kazi rasmi baada ya afya yake kuimarika kufuatia upasuaji aliofanyiwa mwezi uliopita.

Mhe. Rais ameanza kazi rasmi kwa kumwapisha Mkuu mpya wa Mkoa wa Arusha, Mheshimiwa Daudi Felix Ntibenda katika shughuli fupi iliyofanyika Ikulu, Dar Es Salaam.

Kwa kuanzia Mhe. Rais atakuwa anafanya kazi za ofisini na kwa muda mchache. Muda na kasi ya kufanya kazi ya Mhe. Rais vitaongezeka kwa kadri afya yake inavyozidi kuimarika.

Na kwa sababu sasa ameanza kazi, Mhe. Rais ataanza kushughulikia mambo yale ambayo yamekuwa yanasubiri maamuzi yake.

Rais Kikwete alifanyiwa upasuaji wa tezi dume katika Hospitali ya Johns Hopkins ya Baltimore, Maryland, Marekani Novemba 8, mwaka huu na alirejea nyumbani Novemba 29, mwaka huu.

Tokea awasili nyumbani, Mhe. Rais amekuwa anafanya mazoezi asubuhi na jioni kuimarisha afya yake kama alivyoshauriwa na madaktari.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
8 Desemba,2014

A major reorganisation of the ICC Registry

The Registrar of the International Criminal Court, Herman Von Hebel spoke to Rosemary Tollo about proposed change for the better

NAIROBI, Kenya, December 8, 2014-- ReVision project is also looking into areas such as assistance and support to the defence, field operations and field presence, outreach, state co-operation and external relations, information management, and internal communication.

The Registrar of the International Criminal Court, Herman Von Hebel spoke to Rosemary Tollo about proposed change for the better.

Q: You are undertaking a major reorganisation of the ICC Registry. Explain the need for change.

A: Change is desperately needed in order to make a more effective and efficient Registry, especially in dealing with victims.

Over the past 12 years of the court’s existence, we have learned many lessons and we need to ask ourselves whether the current organisational design, policies and practices of the Registry meet the needs of those that we serve.

And the feedback from Registry staff, clients and partners indicates that things could be organised in a better way. There is just too much fragmentation and overlaps in some areas while we need to reinforce the Registry’s operations in others.

One of the main things we are looking at is the assistance and support to victims and their representatives. Victims are often confused and frustrated by the numerous actors from different parts of the court who contact them or seek to represent them — VPRS, OPCV, CSS, PIDS (Outreach), TFV.

Even as ICC Registrar, I am sometimes completely lost as to who does what, when and where. How can we then expect the victims to understand this complex system? Clearly, we must create a more coherent, consolidated and effective structure to support victims and facilitate their legal representation.

The ReVision project is also looking into areas such as assistance and support to the defence, field operations and field presence, outreach, state co-operation and external relations, information management, and internal communication. The goal is to make the Registry more dynamic, effective and efficient in order to service our clients to the best of our ability.

Q: How will the changes you are contemplating affect the victims?

A: The changes will strengthen the support that the Registry provides to victims and provide a better support structure for their participation in the proceedings.

As a first step, I am proposing to consolidate functions performed in several Registry offices into a Victims Office. There are just too many different parts of the court that often work independently in their contact with the victims.

This has to change, and we have received support from a number of parties, including common legal representatives who have direct substantive experience in representing victims before the court. Victims are confused and frustrated with the multiple actors. We need to organise these actors. A single Victims Office is the best way to achieve that.

This office will handle the entire victim participation — from the collection of applications to the provision of information and updates on the cases in the field to the actual representation in court.

There will be a pool of independent lawyers within the office available for assignment to groups of victims at all times, much like a Public Defender’s Office.

There will also be a second counsel assigned to every case for the duration of that case. That counsel would typically be based in the situation country to ensure closer ties and communication with the victims but will be an integral part of the team.

We also foresee a reinforcement of our field offices, which will play a central role in the provision of assistance and support to victims and their legal representatives.

We are addressing reorganisation from a number of important angles. I am convinced that this system, if adopted, would enable a more robust and better support structure for the participation of victims.

Q: Concerns are being raised about the proposed changes, including the possibility that they could leave defendants and victims insufficiently represented given the budget cuts. Are the concerns valid?

A: The proposal to establish a single Victims Office is not intended to save money.

Indeed, victims are the primary beneficiary of the proposed changes. The consolidation of functions will simply enable us to pool existing resources in support of victims, thereby rendering their participation in proceedings more effective and meaningful.

It is my responsibility to ensure the Registry supports victim participation, as well as the defence and other functions, in the best possible way.

If we do not create such an office, the problems being created now will only accumulate and make this an even more pressing issue.

Q: What can be done to increase field autonomy for the common legal representatives, given the budget cuts challenges? For instance, a legal representative’s complaints point to micromanagement by the Registry.

A: The structure that I am proposing will address this.

The perception of micromanagement is due to the fact that common legal representatives are often assigned under the court’s legal aid scheme. This means all their fees and expenses are vetted by the Registry to ensure that they are reasonable and necessary, including the approval of field missions and other activities. This is rather frustrating to counsel.

Counsel would become more independent operationally as they would no longer be remunerated under the legal aid scheme, which requires an hourly accounting of work. The pool of in-house counsel, functioning as a Public Defender’s Office, will be joined by “external” counsel for each new case.

The external counsel would be retained either as a temporary staff member or a consultant for the duration of the case. That way, counsel’s remuneration would not depend on the approval by the Registry of counsel’s activities. Counsel would be fully independent and their performance subject only to the Code of Professional Conduct.

All the support that counsel requires in the performance of their representation duties will be available within the Registry. There will be a coherent support structure — including legal assistants, case managers, field assistants and other support staff — who will be at the disposal of counsel, including field staff to support counsel’s activities on the ground.

Q: When will the proposed changes come into effect and what effect are they likely to have on the ongoing cases?

A: We have started implementing some of the structural changes. However, the changes in the areas of victims and defence, in particular the creation of a Victims Office and a Defence Office, require an amendment of the Regulations of the Court and, therefore, the approval of the court’s judges. This, inevitably, takes some time.

I have already briefed the judges on the proposals and I am preparing a proposal for amendments to the regulations of the court.

Q: How does the Registry respond to the political onslaught against the Kenyan cases that might affect the victims?

A: The ICC is a court of law and cannot get involved in politics.


Distributed by APO (African Press Organization) on behalf of The EastAfrican.

Maendeleo na mageuzi ya ukaguzi na kazi za PAC

KAMATI YA HESABU ZA SERIKALI (PAC) NA JAMII

Zitto Kabwe, Mb
Mwenyekiti wa PAC, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Utangulizi

Baraza la Wawakilishi kama chombo cha kikatiba cha Kuisimamia na Kuishauri Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar limepewa haki na Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984 ya kujiunda katika Kamati mbalimbali (Ibara ya 85 ya Katiba ya Zanzibar). Kamati ya PAC ndio haswa Kamati ya Usimamizi (oversight) wa
Serikali na hivyo kuifanya kuwa Kamati muhimu kuliko Kamati nyingine zote za Baraza. Wakati Kamati nyingine za Baraza na Baraza kwa ujumla wake hutimiza wajibu wake kwa mujibu wa Ibara ya 88 ya Katiba ya Zanzibar, Kamati ya Hesabu za Serikali husimamia matumizi yote ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyoidhinishwa na Baraza na kutoa Taarifa yake kwa Umma. Kwa hiyo Kamati hii inapaswa kuwezeshwa na kujipambanua vilivyo katika kutekeleza majukumu yake. Ni muhimu kusisitiza kuwa Kamati nyingine za Baraza ni muhimu pia katika kusimamia utekelezaji wa Sheria zilizotungwa na Baraza la Wawakilishi (oversight over execution of laws by ministries and agencies).

Ukaguzi na Kamati

Baraza la Wawakilishi katika mkutano wake wa kila mwaka wa Bajeti hupitisha mpango wa mapato na matumizi ya Serikali ya Zanzibar. Baada ya makusanyo ya Mapato hayo na kugawanywa kwa kila Wizara hutumiwa kwa malipo ya Mjadala katika Semina ya Kamati ya PAC Zanzibar iliyofanyika katika Hotel ya
SeaCliff tarehe 6 Disemba 2014. huduma, mishahara na miradi ya maendeleo. Mara baada ya kufungwa kwa mahesabu, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali hukagua na kuwasilisha Taarifa yake kwa Baraza la Wawakilishi. Kamati ya PAC sasa huchukua Taarifa hiyo na kuwahoji kila Katibu Mkuu wa Wizara kuhusu hoja za ukaguzi. Baada ya kukamilisha Taarifa yake PAC huwasilisha Taarifa hiyo
kwenye Baraza kwa mjadala na kupitisha Maazimio.

Hivyo Ripoti ya CAG ndio nyenzo kuu ya Baraza katika kusimamia fedha za Umma. Hata hivyo pale ambapo PAC huona inafaa, huweza kuagiza ukaguzi maalumu kwenye maeneo mahususi. Siku zilizopita nyenzo hii ya ukaguzi maalumu ilikuwa haitumiki sana. Kutumika kwake hivi sasa ni moja ya maendeleo ya kiusimamizi katika PAC. Huko Tanzania bara njia hii imekuwa ikitumika sana hivi sasa na kupitia njia hiyo mambo mengi yameibuliwa kuhusu matumizi ya fedha za umma.

CAG anatazama mambo mengi kwa wakati mmoja na ndani ya mwaka mmoja. Hivyo kuna nyakati mkaguzi anakuwa haoni masuala Fulani Fulani mpaka anapoombwa na vyombo vingine na hata wananchi. Ni vema Kamati ya PAC Zanzibar kutumia pia njia hii ili kuimarisha usimamizi bora wa fedha za Umma katika Nchi ya Zanzibar kama ilivyo sasa katika Jamhuri ya Muungano.

Ni muhimu sana kuzingatia kwamba Wawakilishi ndio chombo za mwisho cha maamuzi kuhusu masuala ya wananchi wa Zanzibar ikiwemo matumizi ya fedha za umma. Kwa hiyo ni wajibu wa PAC kuhakikisha kuwa Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali inafikishwa Barazani, inajadiliwa na kuamuliwa. Muhimu zaidi kuhakikisha kuwa Wizara ya Fedha ya Zanzibar inajibu hoja za PAC ( treasury notes) na hapo ndipo mzunguko wa uwajibikaji unakuwa umekamilika (accountability loop). Hata katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wakati mwingine ‘treasury notes’ hazipewi msukumo wa kutosha na Wabunge na hivyo kujikuta masuala mengi yanabaki yanaelea bila kumalizwa na kufanya mfumo wa Uwajibikaji kuwa dhaifu.

Mageuzi muhimu kufanyika Wakaguzi wa Mahesabu wana chombo chao cha Kimataifa ambacho kinatoa
miongozo ya mara kwa mara kuhusu masuala ya ukaguzi ( International Accounting Standards). Hii huwafanya kuleta mabadiliko ya mara kwa mara katika taaluma yao na kuboresha utendaji wa kazi zao. Siku hizi ukaguzi wa thamani ya fedha (value for money) hufanywa ili kugundua kama kweli fedha iliyotumika inaendana na huduma iliyotolewa. Kwa mfano, kama barabara imejengwa kwa tshs 50 bilioni, wakaguzi sasa wanaweza kuona kama kweli barabara hiyo ina thamani tajwa.

Kamati ya PAC pia huweza kutembelea miradi kujiridhisha kama taarifa ya mkaguzi inakubaliana na mradi uliopo. Hata hivyo, Wawakilishi kama ilivyo Wabunge wanaweza wasiwe na taaluma husika katika jambo linalofanyiwa ufuatiliaji wa thamani ya fedha. Ni muhimu basi kuwa na mahusiano ya karibu kati ya CAG na PAC ili lugha ya kikaguzi kuwa ni lugha inayoeleweka kwa Wawakilishi.

Wawakilishi wanapaswa kuendana na mageuzi ya mara kwa mara katika ukaguzi na usimamizi wa fedha. Kwa mfano, badala ya kusubiri Taarifa ya mwaka ya CAG ndio wafanye kazi, PAC yaweza kuona ni jambo gani katika jamii ambalo linalalamikiwa na wananchi kwamba kuna matumizi mabaya na kuagiza ukaguzi maalumu katika eneo hilo. Katika Bunge la Jamhuri ya Muungano mijadala mingi Bungeni yenye hoja kali kali zenye kuleta mabadiliko makubwa imetokana na ukaguzi maalumu. Hii hoja iliyomalizika katika Mkutano wa Bunge wa 16 na 17 ( Tegeta Escrow ) ilitokana na habari ya Gazeti la kila siku la The Citizen. Kutokana na uzito wa hoja hiyo PAC iliagiza ukaguzi maalumu na hatimaye kuwasilishwa Bungeni.

Mwezi Februari katika Taarifa ya mwaka ya PAC moja ya taarifa itakayowasilishwa inahusu ukaguzi maalumu kuhusu mchakato wa ubinafsishaji wa Benki ya Taifa ya Biashara mwaka 2000 na mapitio ya mkataba wa uendeshaji wa Benki hiyo kati ya mwekazaji kama mwanahisa mmoja na Serikali
kama mwanahisa mwingine.

Mageuzi muhimu sana kufanyika ni hayo, PAC Zanzibar itoke katika kutegemea tu Taarifa ya mwaka ya CAG na ijielekeze pia katika masuala yanayozungumzwa na Jamii kuhusu matumizi ya Fedha za Umma.

Eneo lingine la kusisitiza katika mageuzi ni eneo la itikadi za vyama. Iwapo PAC ikifanya kazi kwa kuegemea itikadi za vyama za wajumbe, kazi ya usimamizi wa Serikali haitafanyika. Ni vigumu kwa wajumbe kusahau vyama vilivyowaingiza barazani, lakini ni muhimu wajumbe kufahamu kuwa utendaji mbovu wa Serikali
unaathiri wananchi wote bila kujali itikadi. Kazi za PAC zinakuwa na ufanisi mkubwa pale ambapo wajumbe wake wanaweka mbele maslahi ya Taifa.

Kwenye Nchi za Jumuiya ya Madola PAC hufanya ‘postmorterm’. Kwamba jambo limekwisha fanywa ndio ukaguzi unafanyika na mjadala kufuata. Kuna haja ya kutazama upya mfumo huu kwani mara nyingi hausaidii. Ni wakati wa kufikiria namna ambavyo CAG na PAC wanaweza kutimiza wajibu katika kuzuia matumizi
yanayoelekea kutokuwa na ufanisi. Nchini Ujerumani PAC ni sehemu ya Kamati ya Bunge ya Bajeti, hivyo inashiriki katika kupitisha Bajeti na kusimamia utekelezaji wa Bajeti. Pale ambapo PAC inaona kuwa Wizara Fulani katika mwaka uliotangulia imepata hoja ya ukaguzi katika eneo Fulani, inaweza kuzuia Bajeti ya ‘item’ hiyo mpaka CAG aridhie majibu ya hoja ya ukaguzi. Iwapo Zanzibar itaridhia mfumo kama huu fedha nyingi za Umma zaweza kuokolewa na Jamhuri ya Muungano yaweza kujifunza baada ya kuona matunda yake Zanzibar.

Hitimisho

Usimamizi ya Fedha za Umma ni jukumu endelevu. Kamati ya PAC inapaswa kukua kwa kujifunza ukuaji wa sekta ya ukaguzi na vile vile kuangalia malalamiko ya wananchi. Mageuzi yaliyoainishwa hapo juu ni sehemu tu ya maeneo ambayo PAC inaweza kutafakari na kufanyia kazi ili kuboresha wajibu
wake.

Taarifa ya Jeshi la Polisi kwa umma

Tunapoelekea kipindi hiki cha uchaguzi wa Serikali za Mitaa, ambao unatarajiwa kufanyika tarehe 14 Disemba, 2014, kwa taarifa tulizonazo, katika baadhi ya maeneo hapa nchini, kumejitokeza makundi ya vijana wanaopita katika baadhi ya maeneo na kuwatishia watu waliojiandikisha kupiga kura hususani wazee na wanawake kuwa, siku ya kupiga kura wasijitokeze na endapo watajitokeza watafanyiwa vurugu.

Jeshi la Polisi nchini, linatoa onyo kali kwa mtu yeyote au kikundi chochote cha watu kutokujihusisha na vitendo vya vurugu, fujo ama vitisho vinavyoweza kusababisha uvunjifu wa amani wakati wa zoezi zima la uchaguzi wa viongozi wa Serikali za Mitaa.Hata hivyo, Jeshi la Polisi katika mikoa yote limejipanga vizuri kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama kuhakikisha kwamba hakuna vitendo vyovyote vya uvunjifu wa amani vitakavyojitokeza wakati wa kampeni na hata siku ya kupiga kura na pale ambapo vitajitokeza vitadhibitiwa kwa haraka, na wahusika kukamatwa.

Aidha, Jeshi la Polisi nchini, linawatoa hofu wananchi wote kwamba, ulinzi umeimarishwa katika maeneo yote kipindi hiki chote cha kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa na hata siku ya upigaji kura. Waliojiandikisha kupiga kura wote wajitokeze siku ya kupiga kura bila hofu ya aina yoyote.
Jeshi la Polisi linaendelea kuomba ushirikiano wa jamii kutoa taarifa za mtu ama vikundi vya aina yoyote vinavyojihusisha na vitendo vya vitisho, vurugu na fujo dhidi ya wananchi waliojiandikisha kupiga kura ili hatua kali za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yao mapema.

Imetolewa na:-
Advera John Bulimba – SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.