Ndoto za Kipanya kuhusu Tanzania ifikapo mwaka 2037


Rais Kikwete afungua jengo la vyumba 53 la Ikulu

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete jana, Jumatatu, Desemba 8, 2014, amefungua rasmi Jengo la Shughuli Nyingi (Multipurpose Hall) la Ikulu katika moja ya shughuli zake za kwanza baada ya kuanza rasmi kazi kufuatia upasuaji mwezi uliopita.

Sherehe hiyo ya ufunguzi wa Jengo hilo lililoko upande wa kushoto wa Bustani za Ikulu upande wa Lango Kuu la Ikulu, zimehudhuriwa na Mawaziri, Makatibu Wakuu na viongozi waandamizi wa Serikali wakiongozwa na Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo Pinda na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Mheshimiwa Anne Makinda.

Mara baada ya kufungua rasmi Jengo hilo lenye vyumba 53, Rais Kikwete ametembezwa kuona shughuli zitakazofanyika kwenye Jengo hilo ambalo ukumbi wake mkubwa una uwezo wa kubeba watu kati ya 500 na 1,000 kwa wakati mmoja.

Akimkaribisha Rais Kikwete kufungua Jengo hilo, Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Balozi Ombeni Sefue ambaye ndiye alikuwa msimamizi mkuu wa Mradi wa Ujenzi huo, alisema kuwa ukumbi huo mkubwa unaweza pia kugawanyika na kuwa na kumbi tatu kubwa na kutumika kwa wakati mmoja.

Balozi Sefue amesema kuwa Jengo hilo pia lina vyumba viwili vya mikutano vya kuweza kubeba watu 30 na 60, chumba cha Wageni Mashuhuri na jiko lake dogo, chumba cha utawala, chumba cha habari na mikutano ya waandishi wa habari, chumba cha usalama, mgahawa, jiko kubwa lenye chumba cha kuokea na chumba cha kuwashia mitambo itakayotumika katika Jengo hilo.

Kufunguliwa kwa Jengo hilo ni matokeo ya maelekezo ambayo Rais Kikwete aliyatoa mjini Dodoma Agosti 21, 2009, wakati alipoelekeza kujengwa kwa Jengo hilo kwa nia ya kuongeza nafasi ya kufanyia shughuli mbali mbali Ikulu kwa kutilia maanani kuwa nafasi imekuwa finyu kwenye Jengo la sasa la Ikulu lililojengwa mwaka 1902. Aidha, alitaka uwepo ukumbi mkubwa wa mikutano ili kuondokana na gharama za kukodi kumbi wakati wa mikutano ya Ikulu ikiwemo mikutano ya viongozi wa nchi za nje.

Maandalizi ya ujenzi yalianza mwaka wa fedha wa 2010/2011 na kazi ya maandalizi ya kumpata mkandarasi ilichukua miaka miwili na hatimaye ujenzi wenyewe ulianza Agosti 22, mwaka 2012.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
9 Desemba,2014

Kamanda wa Polisi Mkoa alazimika kuingilia vurugu za wakulima vs wafugaji Dumila zilizofunga barabara ya Dar-Moro  • Magari 200 yakwama polisi walazimika kutumia mabomu ya machozi
  • Kamanda wa Polisi wa mkoa aongoza polisi kutuliza ghasia

POLISI mkoani Morogoro wakiongozwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Leonard Paulo walilazimika kutumia nguvu za ziada kutawanya wakulima waliofunga barabara kuu Moro- Dodoma eneo la dumila kwa makusudi wakitaka kilio chao dhidi ya wafugaji kushughulikiwa.

Wakulima hao waliokuwa na hasira wamesema kwamba serikali imewacha njia ya panda kwa kutoshughulikia tatizo la wafugaji ambao wametawanya mifugo yao katika mashamba na wao wanashindwa kuyaandaa.

Wakulima hao katika makundi makubwa kutoka Kijiji cha Mabwegele, Kata ya Msowero, Tarafa ya Magole, wilayani Kilosa walifunga barabara kuu ya Morogoro - Dodoma na kuchoma moto matairi kwa muda wa saa sita na kusababisha adha kubwa ya usafiri.

Kijiji hicho hakiko barabarani kwani kipo kilometa kadhaa kutoka Dumila walikoamua kutolea sauti yao wakijua kwamba barabara kuu ya Morogoro - Dodoma itaupeleka mbio uongozi.

Vurugu za wakulima hao zilianza saa tatu na kwa saa sita walikabiliana na polisi na kusababisha zaidi ya magari 200 ya abiria na malori kutoka pande zote mbili kukwama.

Kwa mujibu wa mmoja wa wandishi wa habari waliokuwa eneo hilo magari yalianza kuondoka jana alasiri.

Vurugu hizo zinaonesha kwamba mgogoro kati ya wakulima na wafugaji wa Kijiji cha Mabwegele wilayani Kilosa uliokuwa umepoa umeibuka tena.

Wakulima walisema pamoja na kutoa taarifa mara kadhaa kwa viongozi wa serikali za Kata na wilaya ya Kilosa, hakuna hatua zilizochukuliwa hadi sasa na walipoona muda unakwenda kwa ajili ya kilimo wameamua kushinikiza hatua ziweze kuchuliwa dhidi ya wafugaji hao ambao ni wa jamii ya kimasai.

Mwaka jana, walifunga barabara hiyo kwa muda wa saa kadhaa , kuvunja baadhi ya nyumba zilizojengwa wafugaji eneo la Dumila na kuharibu magari yao hali iliyowalazimu Polisi kutumia nguvu kuwatawanya.Ikulu: Viongozi wa dini wamjulia hali Rais KikweteTAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete usiku wa jana, Jumatatu, Desemba 8, 2014 amepokea ujumbe wa viongozi wa dini wa Mkoa wa Dar Es salaam, ukiongozwa kwa pamoja na Askofu Valentino Mokiwa wa Kanisa la Anglikana na Sheikh wa Mkoa wa DSM, Alhaj Alhad Mussa Salum.

Viongozi hao walifika Ikulu, Dar Es Salaam kumjulia hali Rais Kikwete kufuatia upasuaji ambao alifanyiwa mwezi uliopita kwenye Hospitali ya Johns Hopkins, Baltimore, Maryland, Marekani.

Mbali na kumjulia hali, viongozi hao pia walimwombea dua na sala wakiomba Mwenyezi Mungu amjalie kasi ya kurejesha afya yake kamili na kuweza kuendelea na kazi ya kuwahudumia Watanzania.

Rais Kikwete pia alitumia muda huo kuwaelezea viongozi hao kuhusu ugonjwa uliokuwa unamsibu na kusisitiza kuwa anakusudia kuchukua hatua zaidi za kuwahamasisha Watanzania kupima afya zao mapema ili kujua fika hali za afya zao.

“Mimi Mwenyezi Mungu aliniongoza kuweza kupima mapema na kugundua kuwa ilibidi nipatiwe matibabu ya haraka kuhusu saratani ya tezi dume (prostrate). Vinginevyo nisingejua. Nawashukuru kwa maombi yenu, nawashukuru kwa dua zenu. Daktari mkubwa ni Mungu na ndiye aliniongoza kufanya vipimo mapema,” amesema Rais Kikwete na kuongeza:

“Kwa hakika, saratani inatibika lakini ni lazima igundulike mapema na inaweza kugundulika mapema kama tukifanya uchunguzi wa mara kwa mara wa afya zetu. Mimi nimenusurika kwa sababu nilipima mapema. Nataka tuanze kuwasaidia watu wengi zaidi wapime afya zao mapema.”

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
9 Desemba,2014

Katuni za siku ya 'Uhuru Tanzania'
Aliyepigwa sururu kichwani na picha kusambaa kuwa 'alifumaniwa' apona na kuzungumza

Kovu la sululu kama linavyoonekana kichwani mwa Bw. Oka Kaombe. 

HAKUNA neno jingine la kutumia zaidi ya kusema; KWELI MUNGU MKUBWA! Ni miezi mitano sasa imekatika tangu kusambaa kwa picha mitandaoni zilizomwonesha mwanaume mmoja akiwa ameshindiliwa sululu kichwani huku kisa kikiwa hakijulikani.

Mbali na mitandao ya kijamii, Gazeti la Risasi Jumamosi nalo lilijitoa kufuatilia tukio hilo na kuandika habari katika toleo lake la Julai 26, mwaka huu ikiwa na kichwa cha habari;

Baadhi ya mitandao iliandika kuwa, jamaa huyo apigwa sululu baada ya kufumaniwa na mke wa mtu gesti, mingine ikasema hapana, alipigwa sululu katika kugombea madini machimboni, wengine wakasema kwanza tukio lile halikuwa Tanzania. 

Ni kawaida kwa Magazeti Pendwa ya Global Publishers kufuatilia mambo kwa kina, hata ikipita miaka. Hivi karibuni, timu ya waandishi wa Global jijini Mwanza ilimchimba mwanaume huyo mpaka ikampata na kubaini kwamba anaitwa Oka Kaombe.

Oka ni mkazi wa Mtaa wa Nyakazuzu, Kata ya Nyamatogo wilayani Sengerema, Mwanza ambapo waandishi wetu walimtembelea nyumbani anakoishi na baba yake mzazi (mzee Kaombe) na kuzungumza naye ‘ei tu zedi’ kuhusu mkasa wake huo wa kuzamishwa sululu kichwani.

“Kwanza kabisa napenda kusema kweli Mungu ni mkubwa, nimepona! Ingawa mwili bado hauna nguvu sawasawa lakini naendelea vizuri. “Ilikuwa tarehe 19, Julai mwaka 2013 katika machimbo ya Mgodi wa Miombo- Rwamgasa wilayani Geita, mimi ni fundi wa kuchimba maduara yanayotumika kuchimbia dhahabu.

“Baada ya kumaliza kazi zangu majira ya jioni, nikaenda kupumzika ili kujiandaa kwa siku iliyofuata. “Nilikuwa nimepumzika na wenzangu zaidi ya mia moja, unajua tena migodini. Kufika saa 3 hivi usiku nikiwa nimeanza kusinziasinzia, nilishtukia kitu kizito kinaingia kichwani mwangu upande wa kushoto.”

“Hii sululu kule machimbo ni maarufu kwa jina la Moko, hutumika kuchimbia madini katika migodi. Nilichukuliwa na sululu yangu kichwani na kukimbizwa Hospitali ya Rufaa ya Bugando, Mwanza kwa ajili ya matibabu ya haraka.” SIKU NNE BILA FAHAMU Oka anazidi kusimulia: “Mengine ninayosimulia niliambiwa kwani nilipoteza fahamu kwa siku nne.

“Nilishindwa kupiga kelele nadhani kwa sababu ya kule kusinzia. Wenzangu ambao nao walianza kulala walishtuka kwa kusikia harufu ya damu, wakaamka na kuja wakanikuta sululu ikiwa imezama kichwani.

Nilianza kujitambua baada ya siku nne nikiwa palepale Bugando na kujikuta nipo hospitali lakini nilikuwa siwezi kuzungumza wala kusikia vizuri. Maumivu yalikuwa makali sana kutokana na sululu kuzama kichwani maana ilipoingia ilikwenda kutokea upande wa pili wa kichwa. “Nikiwa nimeshafanyiwa upasuaji kwa kuchomolewa sululu, niliendelea kukaa Bugando kwa siku 52.”

Oka alisema kuwa, hiyo siku ya 52 aliamua kutoroka hospitalini hapo kwa sababu alishindwa kulipia gharama za matibabu ambazo ni shilingi laki tisa (900,000). “Kiasi hicho cha pesa kwangu kilikuwa kikubwa na hata sasa bado ni kikubwa ndiyo maana niliamua kutoroka,’’ alisema Oka.
Oka anaendelea kusimulia:Sululu iliyotolewa kichwani mwa Bw. Oka Kaombe

“Nilipotoka hospitalini kitu cha kwanza nilianza kumtafuta mtu aliyenifanyia kitendo kile cha kinyama, marafiki zangu wakanipa ushirikiano na kuniambia unyama ule ulifanywa na jamaa mmoja anayeitwa Masha. “Huyu Masha ni mchimbaji wa madini kwenye ule mgodi lakini alikimbia baada ya kufanya tukio na mpaka sasa hajulikani alipo.

Oka alisema taarifa alizopata baadaye kutoka kwa wachimbaji mgodini hapo ni kwamba, lengo la Masha kumpiga na sululu lilikuwa ni kumtoa kafara (ndagu) ili aweze kupata dhahabu nyingi na awe bilionea kwa siku za usoni. “Ila Mungu ni mkubwa alitupilia mbali wazo hilo mpaka sasa niko hai,” alisema Oka.

Oka alisema kwa sasa anaamini amepona kabisa kidonda chake kichwani ila hawezi kufanya kazi yoyote kutokana na mwili kukosa nguvu za kutosha.

Bw. Oka Kaombe akiwa na baba yake mzazi mzee Kaombe.

Aliendelea kusema kuwa, akiwa Bugando aliambiwa na madaktari kuwa anatakiwa kufanyiwa upasuaji kwa mara nyingine na kuwekewa vyuma kichwani baada ya kuwekewa vyuma hivyo itabidi akae miaka mitatu bila kufanya kazi yoyote ndipo atapata nguvu za kufanya kazi kama zamani.

Oka alisema maisha yake kwa sasa ni magumu kwani ana watoto 5, lakini pia alitengana na mke wake hivyo yeye ndiye baba na mama wa familia kwani hata wazazi wake wamezeeka, hivyo wanamtegemea yeye.

Alisema kwa sababu bado ana safari ya kujitibu na pia kutunza familia, amewaomba Watanzania wenye kuguswa na mkasa wake wamsaidie pesa kwa kiasi chochote atakachojaliwa mtu kwa kutumia simu yake ya mkononi ambayo ni 0682 013479.

Zimamoto yaambia wananchi waibane Serikali na siyo kuilalamikia

Kamishna Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji akizungumza na wana habari wa mkoani Shinyanga.

JESHI la Zimamoto na Uokoaji nchini limewaomba wananchi kuacha kutoa lawama dhidi yake kila pale panapotokea janga la moto na badala yake walisaidie kwa kuishinikiza serikali itatue changamoto kadhaa zinazolikabili ili liweze kufanya kazi zake kwa ufanisi mzuri.

Ombi hilo limetolewa na Kamishna Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini, Pius Nyambacha alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini Shinyanga muda mfupi baada ya kuwasili mkoani humo kukagua shughuli za jeshi hilo.

Nyambacha alisema kwa kipindi kirefu Jeshi la Zimamoto limekuwa likilaumiwa kwa uzembe kutokana na kushindwa kukabiliana na majanga ya moto katika maeneo mengi nchini ambapo hata hivyo jamii haichunguzi kwa kina chanzo chake na badala yake hubaki wakilalamika kulaumu.

Alisema zipo changamoto nyingi zinazolikabili Jeshi lake na hivyo kushindwa kufanya kazi zake kwa ufanisi ikiwemo suala la uhaba wa maeneo ya kuongezea maji mijini pale linapotokea tatizo la nyumba kuungua moto kutokana na kuhitajika kwa maji mengi ili kuweza kukabiliana na moto.

“Yapo mambo mengi ambayo tunaamini wenzetu wananchi hawayaelewi na hivyo kila mara kutushushia lawama kwamba sisi ni wazembe, ukweli tunajitahidi sana, sasa tuwaombe wenzetu wana habari mtusaidie kuielimisha jamii ili iweze kuwa na uelewa wa kutosha jinsi tunavyofanya hii kazi hasa upande wa uzimaji wa moto,”

“Zipo changamoto nyingi zinazotukabili hasa tatizo la uhaba wa maeneo ya kuongezea maji katika sehemu nyingi za miji yetu, wananchi wanapaswa waelewe kuwa magari yetu hutumia lita 2000 za maji ndani ya dakika mbili yanapozima moto, hivyo yanapomalizika lazima tuongeze mengine,” alieleza Nyambacha.

Akifafanua magari mengi yaliyopo nchini hayana uwezo wa kuchukua maji mengi zaidi hivyo yanapomalizika hulazimika kurudi katika eneo la kujazia maji na mara nyingi maeneo hayo yanakuwa mbali na eneo la tukio la moto na kwamba ndiyo sababu ya wananchi kulalamika kwamba zimamoto walikwenda bila maji.

“Hili ni tatizo kubwa sana, sisi wenyewe hatupendi iwe hivyo, laiti miji yetu ingekuwa na utaratibu wa kujenga 'viosk' vingi mitaani kwa ajili ya magari yetu kujazia maji tungeweza kukabiliana vizuri na majanga ya moto yanayotokea katika maeneo yetu, lakini pia lipo tatizo la uchakavu wa magari, hili linafanyiwa kazi na serikali,” alieleza.

Kwa upande wake Kamanda wa Jeshi la Zimamoto mkoani Shinyanga, Elias Mugisha aliiomba serikali iuongezee mkoa wake askari wa kutosha ili kuweza kufanya kazi zao kwa ufanisi ambapo alisema mpaka sasa mkoa huo una askari 41 katika wilaya zote ikiwemo na viwanja vya ndege vya Ibadakuli na Kahama.

Viongozi wa CHADEMA watekwa

Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Kahama, Juma Protas

Msafara wa viongozi na wanachama wa chama Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wa Kanda ya ziwa Magharibi wametekwa na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wakati wakitoka kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni za serikali za Mitaa kata ya Bulyanhulu wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Kahama, Juma Protas alisema tukio hilo lilitokea juzi katikati ya Kijiji cha Kalagwe kata ya Ntobo na Kijiji cha Nyambula Kata ya Ngongwa majira ya Saa 3:30 Usiku wakati wakitoka kwenye Kampeni Kijiji cha Kakola.

Akizungumzia tukio hilo Protas alisema walipofika eneo la Daraja walikuta magari matatu yamesimama pembeni ambayo ni Basi la Jordan ambalo lilikuwa linatoka mkoani Geita kuelekea Kahama, lori aina ya Fuso na gari ndogo inayomilikiwa na Kampuni ya TBL kupitia bia ya Balimi ambayo nayo yalikuwa yametekwa.

Alisema wakati wanajaribu kuyapita magari hayo ghafla waliona mawe na miti ambayo ilikuwa imetandazwa barabarani na ndipo majambazi hao waliamuru msafara huo ambao ulikuwa na magari mawili wenye watu 10 wasimame na watoe simu na fedha walizokuwa nazo.

“Tulisikia sauti wakisema zimeni taa za gari na muziki na hatuwezi kuwadhuru nyinyi Makamanda ila tunataka fedha na simu, na tupo kazini mnatakiwa kuwalaumu viongozi waliokula pesa za Escrow bila hiyo tusingefanya haya mnayoyaona,”
alifafanua Protas.

Aliwataja waliokuwemo kwenye msafara huo kuwa ni mratibu wa Kanda ya ziwa mashariki Renatus Mzemo, Mwenyekiti wa Kamati ya Rasilimali Kanda ya ziwa Magharibi, Emmanuel Mbise na Mwenyekiti wa Kamati ya Uenezi wa chama hicho Kanda hiyo Juma Protas ambaye ndiye Mwenyekiti wa CHADEMA.

Viongozi hao wa CHADEMA walikuwa wamepanda gari aina ya Toyota Prado yenye na. T707 BBP ambayo hata hivyo ilivunjwa baadhi ya vioo.

“Tuliibiwa fedha tathimini zaidi ya shilingi laki tisa pamoja na simu 11 ambazo hazikufahamika mara moja thamani yake na gari yetu moja ambayo ni ya mdau alyejitolea kutusaidia ilivunjwa vioo na ile ya M4C yenyewe walisema hawawezi kuivunja maana ni wananchi walichanga kuinunua”,
aliongeza Protas

“Kulikuwa na magari mengi tuliyoyakuta yametekwa na abiria walinyang’anywa simu na fedha zao, pia kulikuwa na Mwalimu mmoja wa Shule ya Msingi Lunguya ambaye alitekwa akiwa na pikipiki na wakamfunga Kwenye mti pamoja na ddugu yake na baada ya kuchukua fedha walitoweka kusikujulikana,”
aliongozea Mwenyekiti huyo.

Jeshi la Polisi wilayani Kahama lilifika eneo hilo baada ya kupewa taarifa na abiria waliokuwa kwenye basi ambalo lilitekwa na kukuta majambazi hayo yakiwa yametokomea kusikojulikana na kutoa msaada wa kiusalama kwa magari yote na abiria waliotekwa.

Waziri Mkuu akagua mabehewa mapya 22 ya treni


Waziri Mkuu, Mh. Mizengo Pinda akiongozwa na Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia kwake) na Naibu Waziri wake, Dkt. Charles Tizeba (kulia) kukagua baadhi ya mabehewa mapya ya Shirika la Reli nchini (TRL) yaliyonunuliwa na kwa fedha za serikali wakati alipokwenda kwenye bandari ya jijini Dar es salaam Desemba 8,2014.


Waziri Mkuu, Mh. Mizengo Pinda na Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe wakikagua moja ya mabehewa mapya ya TRL yaliyonunuliwa kwa fedha ya serikali wakati alipokwenda kwenye Bandari ya Jijini Dar es salaam Desemba 8, 2014 kupokea mabehewa hayo.


Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda na Waziri wa Uchukuzi Dr Mwakyembe wakiangalia jiko ambalo liko ndani ya behewa la daraja la pili kwenye moja ya mabehewa 22 yaliwasili nchini mwisho wa wiki, katika bandari ya jijini Dar es Salaam, Desemba 8,2014.


Waziri Mkuu, Mh. Mizengo Pinda na Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe wakikagua moja ya mabehewa mapya ya TRL yaliyonunuliwa kwa fedha ya serikali wakati alipokwenda kwenye Bandari ya Jijini Dar es salaam Desemba 8, 2014 kupokea mabehewa hayo.


Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda akishuka kwenye moja ya mabehewa 22 yakiyowasili nchini mwisho wa wiki, katika bandari ya Dar es Salaam.Mh. Pinda alifika Bandarini hapo kukagua mabehewa hayo. Waziri Mkuu amempongeza Waziri wa Uchukuzi pamoja na watendaji wake kwa kazi nzuri wanayoifanya katika Kuimarisha usafiri wa Reli nchini. Utekelezaji wa mradi huu ni mojawapo wa Miradi inayotekelezwa chini ya mpango wa "Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now - BRN).

Kafulila aapa kufa na 'Singasinga' hata akilindwa na Ikulu

Kafulila akihutubia wakazi wa mji mdogo wa Nguruka, jimbo la Kigoma Kusini.

MAELFU ya wakazi wa Mji mdogo wa Nguruka Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma, wamejitokeza kumpokea Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kusini, David Kafulila, mara baada ya kuwasili jimboni humo kwa ziara ya kikazi na kufanya mikutano kadhaa na wananchi wa jimbo lake.

Akihutubia wananchi kwenye mikutano ya hadhara katika vijiji vya Mpeta, Malagarasi na Tarafa ya Nguruka, kwa nyakati tofauti, Kafulila amesema yuko tayari kupambana na Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya IPTL na PAP, Harbinder Singh Sethi, ili kutetea maslahi ya umma wa watanzania kuhusu ufisadi wa zaidi ya shilingi bilioni 300 kwenye akaunti ya Tegeta Escrow.

Kafulila alisisitiza kuwa Harbinder Singh Sethi ni mwizi na kwamba hata kama Ikulu itamlinda atapambana nae kwani kwamba haiwezekani mtu mmoja aiweke serikali yote na watanzania mfukoni.

“juzi nimemsikia anasema sasa anatafakari upya kuangalia uwezekano wa kuendelea kuwekeza tanzania, na kwamba eti atang’oa mitambo yake apeleke sehemu nyingine; nimemwambia na nawaambia waandishi wa habari wawambie watanzania kwamba Kafulila anasema Singh Seth ni mwizi ni tapeli ntapambana nae hata alindwe na Ikulu,”
alisema Kafulila.

Aidha Kafulila aliwataka wananchi jimboni kwake kutochangia ujenzi wa maabara zinazojengwa kwa agizo la rais Jakaya Kikwete, mpaka hapo hatua zitakapochukuliwa dhidi ya waliohusika na ufisadi wa akaunti ya Escrow.

“mheshimiwa rais anakuja anaonyesha yeye ni muungwana, anawajali masikini, anapenda watu masikini, anashika watoto wa kimasikini, kwanini hakamati wezi? Ndo maana tunasema Ikulu inahusika,” “mimi ninao ushahidi kwamba Ikulu ya Kikwete inahusika kwenye wizi huu.”
aliongeza.
Kwa upande wake mjumbe wa mkutano mkuu wa CHADEMA, moja ya chama ambacho kinaunda UKAWA, Jessica Kishoe, amewataka wananchi kutokichagua Chama cha Mapinduzi CCM, kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, badala yake wachague viongozi watakaokuwa na uwezo wa kuinyooshea kidole serikali ya CCM.

“serikali ya chama cha mapinduzi imeshawaona watanzania ni mbumbumbu na ndio maana inaiba na bado inakuja kuomba kura kwenu ikiamini kuwa mtaipigia. hawaibi fedha zenu wakiamini hamtajua, wanaiba kwa sababu wanajua hata wakiiba mtawachaguaivyo fanyeni chaguo sahihi ili msije mkajutia,”

Mama na Mwana...

A Dar es Salaam city resident walks along with her toddler in a furrow to avoid being knocked by motor vehicles at a narrow Chanika road as depicted by our roving photographer.
photo: Robert Okanda/DAILY NEWS

Taarifa mpya kuhusu mwekezaji wa treni, Robert Shumake
Nadhani mnakumbuka jinsi kikundi cha WANAHARAKATI kilivyoshikilia bango kuhusu kilichoitwa mradi wa treni za kisasa kati ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere na Mjini Kati Dar, ambapo aliyeitwa 'mwekezaji, ROBERT SHUMAKE, alidai yupo tayari kuuanza hata siku hiyohiyo uliposainiwa mkataba wa awali. Bonyeza HAPA kusoma zaidi kuhusu suala hilo na ufuatiliaji wetu.

Hata hivyo, nadhani haitoshi tu kumtilia mashaka SHUMAKE Pasi kuchukua hatua dhidi ya wahusika. Ikumbukwe SHUMAKE bado ni Balozi wetu wa heshimu huko Marekani. Je kama anatiliwa mashaka katika suala hili haitoshi kumvua wadhifa huo aliopewa katika mazingira yasiyoeleweka? Kadhalika, je kwanini waliokurupuka kusaini mkataba wa awali na mbabaishaji huyo wasiwajibishwe?

Tusipokuwa makini, mtu huyo 'mjanja mjanja' anaweza kuzua IPTL nyingine kwa kusaini mkataba kwa huduma isiyopatikana kisha kudai malipo asiyostahili.
  • Imeandikwa na Evarist Chahali via blog yake

DC Korogwe atoa wito kampuni za mawasiliano zisambaze zaidi mawasiliano Wilayani humo

Mkuu wa Idara ya Uuzaji na usambazaji bidhaa wa Vodacom Tanzania Upendo Richard (kulia) akimfafanulia jambo Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mrisho Gambo (kushoto) kuhusiana na kifaa cha Router chenye uwezo wa kuunganisha zaidi ya watu nane kutumia huduma ya intaneti wakati wa uzindua duka jipya la Vodacom Tanzania lililopo mtaa wa manundu wilaya ya Korogwe mjini.Katikati ni Meneja Uhusiano wa Umma wa kampuni hiyo Matina Nkurlu na anaeshuhudia kulia ni Abubakary Lubuva.

Mkuu wa wilaya ya Korogwe Mrisho Gambo,ametoa ushauri kwa Makampuni ya Mawasiliano kufungua zaidi vituo vya kutoa huduma kwa wateja mkoani Tanga na maeneo mengine ya miji midogo inayokua kwa kasi ili kuwawezesha wateja wake kupata huduma kwa karibu badala ya kuzifuata mbali na kupoteza muda mwingi ambao wangeutumia kufanya shughuli za uzalishaji.Alitoa ushauri huo wakati akifungua duka la Vodacom Tanzania lililopo Korogwe mjini ambapo pia alitoa pongezi kwa hatua hiyo.

Katika kuhakikisha wakazi wa Korogwe na maeneo jirani wanapata huduma kwa karibu,Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania mwishoni mwa wiki iliyopita imefungua duka jipya katika eneo la Korogwe mjini.

Korogwe ni moja ya kituo maarufu katika mkoa Tanga ambacho wanapitia wasafiri wengi wanaotumia barabara ya kuelekea mikoa ya Kaskazini ya Moshi,Tanga na Arusha.Vilevile mji huu unakuwa kwa kasi kutokana na kuongezeka kwa wafanyabiashara wanaowekeza eneo hili.

Duka hili jipya lenye mazingira rafiki kwa wateja litakuwa linatoa huduma mbalimbali kwa wateja wa Vodacom ikiwemo huduma kwa mawakala wa M Pesa na uuzaji wa bidhaa za Vodacom na litawawezesha wateja wa eneo hilo na vitongoji vyake wakiwemo wasafiri wanaoelekea mikoa ya Kaskazini na nchi jirani kupata huduma bora.Mtandao wa Vodacom unaongoza kwa kupatikana vizuri na umeenea sehemu zote katika mkoa wa Tanga.

Mkuu wa Idara ya Uuzaji na usambazaji bidhaa wa Vodacom Tanzania Upendo Richard , alisema ufunguzi wa duka hili la kisasa ni mwendelezo wa malengo ya Vodacom kuendeleza kuboresha maisha murua kwa kila mtanzania kwa kupata huduma za kampuni hiyo zenye ubora na kuwafikia wateja kwa urahisi zaidi popote pale walipo ikiwemo huduma mpya ya kilimo klabu inayolenga kuwawezesha wakulima nchini.

“Uzoefu na utafiti umetuonyesha kuwa wananchi wanataka ubora,kama mtandao unaoongoza nchini tumejizatiti kuhakikisha tunafanya ubunifu wa hali ya juu wa kiteknolojia ili kutumia mtandao wa simu kuboresha maisha ya wananchi ikiwemo kutoa huduma bora na ndio maana tunazidi kufungua maduka kama haya kwa ajili ya kuwasogezea karibu wananchi huduma bora,na ninawahakikishia kuwa popote wateja wetu walipo tutawafikia na tunawashukuru sana wateja wetu kwa kutuunga mkono na tunawakaribisha ambao hawajajiunga na familia ya Vodacom kujiunga na kupata huduma bora kwa gharama nafuu.”Anasema Richard

Vodacom ina mtandao wa maduka 86 na wakala mbalimbali wa kuuza bidhaa zake nchini na duka lililofunguliwa leo ni la pili kufunguliwa katika mkoa wa Tanga.


Mfanyakazi wa duka jipya la Vodacom Tanzania lililopo mtaa wa manundu Korogwe mjini,Maudy Mbaga(kulia)akitoa huduma kwa wateja wa kwanza waliofika katika duka hilo baada ya kuzinduliwa rasmi na Mkuu wa Wilaya hiyo Mrisho Gambo (hayupo pichani)


Baadhi ya wateja wakipatiwa huduma mbalimbali na mfanyakazi wa duka jipya la Vodacom Tanzania lililopo mtaa wa manundu Korogwe mjini, Abubakary Lubuva(kushoto)duka hilo lilizinduliwa rasmi na Mkuu wa wilaya hiyo Mrisho Gambo (hayupo pichani)


Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mrisho Gambo wa kwanza (kulia) akikata utepe kuzinduzua duka jipya la Vodacom Tanzania lililopo mtaa wa manundu Korogwe mjini, katikati ni Mkuu wa Idara ya Uuzaji na usambazaji bidhaa wa Vodacom Tanzania Upendo Richard na Meneja Uhusiano wa Umma wa kampuni hiyo Matina Nkurlu.Hafla hiyo imefanyika hivi karibuni.

Government commited to send capitation grant directly to schools

  • Government affirms commitment to send capitation grant directly to schools
  • Twaweza program shows how to improve quality of basic education

8 December 2014, Dar es Salaam: Government officials have confirmed the government’s intention to send capitation grant money directly to primary and secondary schools, in order to boost quality of learning.

This was said by the Minister of Education and Vocational Training (MOEVT) and the Minister of Prime Minister’s Office – Regional Administration and Local Government (PMO-RALG) at an event on 5 December releasing preliminary results for KiuFunza (thirst to learn), Tanzania’s largest randomized control trial in education.KiuFunza, run by Twaweza and Innovations for Poverty Action (IPA) with support from the Commission for Science and Technology (COSTECH), has demonstrated that when funds are sent directly to schools they reach there in full and on time, and in a predictable manner, increasing the ability of schools to plan better and purchase essential learning materials.

The Minister of Prime Minister’s Office – Regional Administration and Local Government (PMO-RALG) said 
“…the process of sending money directly to schools is being reviewed to plan for effective implementation. The government will work with stakeholders , including Twaweza, to see how best to implement the program successfully.”

Sara Mlaki, speaking on behalf of the Minister of Education and Vocational Training (MOEVT) and Kassim Majaliwa (MP), Deputy Minister PMO-RALG responsible for education, both emphasized how the Twaweza project had shown how the capitation grant could be administered more effectively. Congratulating Twaweza, the ministers noted that the civil society organization’s approach increased reliability, transparency and accountability. They assured the participants that the government is open to ideas and evidence, and that these measures will be taken up without further delay, including strengthening auditing of use of funds at school level.

Twaweza presented its first year preliminary results at a special event held in Mbweni and Kiumbageni Primary Schools in Dar es Salaam Region the presence of a number of key government personnel and members of parliament. KiuFunza tests the impact on learning outcomes of two ideas – sending capitation grant directly to schools and providing teachers bonuses based on how many of their students pass basic literacy and numeracy tests. The two are also being tested in combination. The project operates in 156 schools in 11 districts of the country.

Initial findings show that after one year, children in schools where the interventions were tested together show significantly better learning outcomes than schools in which no interventions were carried out. In addition, the capitation grant was received in full by all the schools and this has led to reports of fewer shortages of essential materials. However, the capitation grant alone did not lead to improved learning results, at least in the first year.

The bonus only scheme has had some result evidenced by teachers spending more time teaching (extra classes and additional test taking) but has not yet shown significant impact on learning outcomes. However, in early 2014 teachers have responded positively to receiving the bonus for 2013. Many teachers confirmed that in 2013 they lacked trust in the bonus offer, but, having seen Twaweza deliver the bonus as promised, they have expressed belief in the incentive offer in the second year of the project.

During the event, there was broad support for the Twaweza initiative with government officials expressing interest in implementing the local cash on delivery (bonuses for teachers whose children learn) intervention. On behalf of the Chief Executive Officer Of the President's Delivery Bureau (PDB), Omari Issa, Dr Linda Ezekiel stressed discipline and accountability, as well as teamwork in implementing Initiatives, in conjunction with KiuFunza’s incentive payments experiments, which is also a BRN initiative that PDB oversees. Dr Hassan Mshinda, Director General of COSTECH, emphasized the need for policy to be informed by this type of rigorous scientific research and called for similar initiatives in other sectors.

All participants at the event, which included MPs and donors, were able to observe school premises and KiuFunza testing methodology. The tests determine teachers’ bonus payments and are based on the national curriculum and developed in collaboration with experts from the Tanzania Institute of Education (TIE) and endorsed by the Tanzania’s Teachers’ Union (TTU). The tests are for Grades 1, 2, and 3 in Kiswahili, English and Mathematics.

All schools and districts in the trial were chosen randomly and the methodology for KiuFunza conforms to the highest scientific standards. The work of the research team is overseen by Professor Isaac Mbiti of the University of Virginia and Professor Karthik Muralidharan of the University of California in San Diego, international leaders in education research. The entire trial takes place over two years and final results are due mid-2015.

Rakesh Rajani, Head of Twaweza, said 
“Everyone agrees that we have a quality of education problem in our country. The challenge now is how to improve learning. A lot of things are done with good intentions, but they are not as effective. The fact that the budget for education has tripled in the last decade while quality has gone down shows we need to do something different. KiuFunza employs scientifically rigorous research methods to generate new ideas and evidence for what works. Although we are only half-way through the trial, we are already seeing positive results in the combination schools. We are pleased that the government is following developments closely and has already acted swiftly to change the way in which capitation grants are disbursed. In mid-2015 we will have new data on what works, and in particular whether the bonus scheme increases teacher motivation and accountability. In the 21st century, the government needs to use evidence and thoughtful ideas to improve education.”

TRA kuchambua ripoti ya ICTD

Wataalamu wa kimataifa wa masuala ya kodi wakiendesha mjadala katika mkutano wa mwaka wa kituo cha kimataifa cha utafiti wa masuala ya kodi,mkutano uliofanyika jana jijini Arusha ,Kamishna Msaidizi wa Mamlaka ya Mapato Uganda (URA), Milly Nalukwago (kushoto), Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Rished Bade (katikati) na Mtaalam wa Kodi wa Uingereza, Rhiannon Mc Cluskey.

Mamlaka ya mapato nchini TRA imeanza kuchambua ripoti ya utafiti uliofanywa na kituo cha kimataifa cha utafiti wa masuala ya kodi na maendeleo inayobainisha changamoto mbalimbali za ulipaji kodi katika
maendeo mbalimbali nchini.

Zoezi la uchambuzi wa ripoti hizo linatajwa kuwa na shabaha ya kuangalia mapungufu yaliyopo na kuboresha mifumo ya sheria na ulipaji kodi kwa hiari.

Sehemu ya Taarifa ya utafiti uliofanwa katika kipindi cha mwaka uliopita na kituo cha kimataifa cha kodi na maendeleo katika mikoa mbalimbali nchini, inabainisha mazingira tofauti ya ulipaji wa kodi ambapo baaadhi ya maeneo yameonekana kuwa katika changamoto kubwa za ukwepaji kodi.

Kamishana wa TRA Rished Bade kizungumza Jijini Arusha wakati wa Mkutano wa kimataifa baina yao na kundi la wataalamu, wanaofanya utafiti kuhusu masuala ya kodi duniani amesema pamoja na mapitio ya ripoti za utafiti wa taasisi hiyo,fursa hiyo inatoa mwanya kwa wataalamu wa ndani kujifunza mbinu za kushughulikia changamoto za walipa kodi wanaofanya biashara za kimataifa.

Awali Afisa Mtendaji Mkuu wa kituo cha kimataifa cha kodi na maendeleo Profesa Mick Moore ameeleza kusudio la tafiti zao katika nchi mbalimbali za Afrika kuwa unalenga kuimarisha mifumo ya kodi hususani katika sekta za maliasili zikiwemo Madini,Gas na Mafuta.

Katika hatua nyingine Mamlaka ya mapato nchini TRA imeibuka kinara kwa kuwa na hesabu bora miongoni mwa taasisi za serikali kwa mwaka 2013-2014 zinazotolewa na bodi ya wahasibu na wakaguzi wa hesabu nchini NBAA ambapo kamishna wa mamlaka hiyo akizungumza Jijini hapa katika hafla ya kukabidhiwa ushindi huo amesema hatua hiyo inazidi kuwajengea imani walipa kodi juu ya utendaji wa chombo hicho.

Raha tele tabu ya nini?: zinaonyesha ongezeko la idadi ya walipa kodi chini,idadi iliyopo sasa inatajwa kuwa ndogo kulinganisha na mataifa mengine kutokana na mfumo wa kibiashara usio rasmi unaopelekea kupunguza idadi ya walipa kodi wanaofikia milioni moja nukta nane hivi sasa.

Kamishna mkuu wa mamlaka ya mapato Tanzania TRA RISHED BADE kushoto akiwa na afisa mtendaji mkuu wa kituo cha kimataifa cha kodi na maendeleo Prof MICK MOORE wakiongoza majadiliano juu ya mada mbalimbali zilizowasilishwa katika mkutano mkuu wa mwaka wa kituo cha kimataifa cha kodi na maendeleo, mkutano uliofanyika jana jijini Arusha
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Rished Bade, kushoto akiwa na afisa mtendaji mkuu wa kituo cha kimataifa cha kodi na maendeleo, Prof Mick Moore, wakiongoza majadiliano juu ya mada mbalimbali zilizowasilishwa katika mkutano mkuu wa mwaka wa kituo cha kimataifa cha kodi na maendeleo,mkutano uliofanyika jana jijini Arusha
Mwakilishi wa Channel Ten Arusha, Jamila Omar (katikati) , Mwakilishi wa kituo cha Star TV Arusha, Ramadhani Mvungi ,Iddy Uwesu wa Azam tv Arusha wakifanya mahojiano maalumu na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) Rished Bade jijini Arusha wakati wa mkutano mkuu wa mwaka wa kituo cha kimataifa cha kodi na maendeleo.

  • Tumeshirikishwa taarifa hii na Mroki Mroki/Father Kidevu blog

Dar Live yafurika katika kilele cha EFM bar-kwa-bar muziki mneneUMATI wa wapenzi wa burudani jana ulifurika katika Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live uliopo Mbagala, Zakheem jijini Dar katika kilele cha matamasha yaliyoandaliwa na EFM Radio yajulikanayo kama Bar kwa Bar Muziki Mnene.

Burudani kutoka kwa Inspector Haroun zilikonga vilivyo nyonyo za mashabiki huku DJ Makey, watangazaji wa EFM Maulid Kitenge na mwenzake Omary Katanga wakiwapa raha tosha mashabiki waliofurika katika ukumbi huo.

Picha taarifa tumeshirikishwa na PATRICK BUZOHELA / GP

Inspector Haroun 'Babu' akifanya makamuzi wakati wa kilele cha EFM Bar kwa Bar Muziki Mnene ndani ya Dar Lve jana.Nyomi iliyohudhuria sherehe za kilele hicho.

Burudani mwanzo mwisho.

DJ mkongwe nchini, Majay Majizzo akifanya yake stejini na kupagawisha mashabiki vilivyo.Babu aliamua kuvua viatu na kubaki peku baada ya burudani kukolea.Ma DJ kutoka EFM wakitoa burudani.

Mtangazaji wa Michezo wa EFM Radio, Maulid Kitenge akiwaburudisha mashabiki.Omary Katanga wa EFM naye akifanya yake stejini.
Wafanyakazi wa EFM Radio wakiwa katika pozi wakati wa kilele cha EFM Bar kwa Bar Muziki Mnene.Kitenge katika pozi na mdau.Mtangazaji wa EFM, Ssebo katika picha ya pamoja na Meneja Uhusiano wa EFM, Kanky Mwaigomole.Watangazaji na Ma DJ wa EFM wakifanya yao ndani ya Dar Live.

Idris, Feza Kessy, Diamond wametoa 'gundu' kwa wasanii Tz - La Veda

La Veda akipozi na baadhi ya wadau waliofika kumpokea.

MWANADADA, aliyeiwakilisha Tanzania katika shindano la Big Brother Hotshots, Irene Neema Vedastous ‘LA VEDA' amefunguka kuwa Diamond, Fezza na Idris wameondoa gundu kwa ushindi wao.

Akizungumza na GPL leo jioni katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, wakati akiwasili kutoka Afrika ya Kusini alipokwenda kuungana na washiriki wengine wa BBA katika fainali, La Veda alisema, “Binafsi nimefurahi sana kwa Idris kushinda Dola za Kimarekani 300,000, ni furaha kubwa sana kwangu na kwa Watanzania kwani naamini pia Diamond kuchukua tuzo tatu za Channel O na nyingine aliyopata juzi kutoka Nigeria, Fezza kuingia tena mjengoni wote watakuwa wameondoa gundu kwa wasanii wa Kitanzania’, alisema.

Aidha La veda amewaomba Watanzani kujitokeza kwa wingi kumpokea Idris siku atakapowasili maana ushindi wake unazidi kuiweka Tanzania katika ramani nzuri kimataifa.

Kujua zaidi Mahojiano aliyofanya La Veda baada ya kuwasili, usikose kutembelea www.globaltvtz.com


La Veda baada ya kuwasili jijini Dar akitokea nchini Afrika Kusini alipokwenda kushiriki fainali za BBA.

La Veda akipokelewa baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.


PICHA / HABARI: Gabriel Ng’osha/GPL