Overloaded motorbike. Children without helmets.

A motorbike rider violates safety regulations by overloading his bike along Mandela Expressway in Dar
es Salaam.
photo: Robert Okanda/DAILY NEWS

Chumvi yatumika kuombea kura (?)

Chumvi iliyozua kizaa zaa huko Geita-Picha na Valence Robert-Malunde1 blog Geita

Watu 10 wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),wakiwemo mabalozi wa nyumba kumi wakazi wa mtaa wa Mkoani kata ya Kalangalala Wilayani Geita Mkoa wa Geita wamenusurika kuuawa kwa kuchomwa moto na wananchi wenye hasira kali baada ya kuwakuta wakigawa chumvi kwa wananchi kama njia ya kuwashawishi kuchagua viongozi wa chama chao katika uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Desemba 14 mwaka huu.

Katika tukio hilo,vigogo wa CCM mkoa wa Geita akiwemo mbunge wa viti maalumu Vicky Kamata walichafua hali ya hewa baada ya kufika eneo hilo la tukio kwa lengo la kuwakingia kifua watuhumiwa na kusababisha upepo kuchafuka zaidi hali iliyopelekea polisi kutishia kuondoka eneo hilo ili wananchi wajitawale.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Desemba 10 mwaka huu majira ya saa 3:30 usiku ambapo jeshi la polisi lilifika eneo hilo na kutumia nguvu ya ziada kuwashawishi wananchi wasijichukulie sheria mkononi kwa kuwapiga na kuwachoma watu hao mbele ya vyombo vya dola.

Mwandishi wa malunde1 blog mkoani Geita Valence Robert alipigiwa simu majira ya saa 2:30 usiku na baadhi ya wananchi mwandishi wa wakimtaka afike eneo la tukio kushuhudia tukio hilo na bila kuchelewa mwandishi wetu alifika eneo hilo na kukuta wananchi hao wakiwa wamefura hasira.

Mwandishi wetu alishuhudia wananchi wakiwa wamewafungia kwa nje watuhumiwa hao waliokuwa ndani ya nyumba ya balozi wa chama hicho tawala.

‘’Bora mwandishi umekuja hii ni nyumba ya balozi wa CCM na ndani ya nyumba hii tumewafungia mabalozi wake na wananchi mbalimbali ambao tumewakuta wakigawa chumvi kwa wananchi",walieleza.

"Na hapa unapotuona tumekupigia simu uje uchukue picha ya majivu ya hawa watu maana tunataka kuiteketeza kwa moto nyumba hii tumechoka na hawa watu kutugeuza kuku wa kienyeji’’alisikika mkazi mmoja wa eneo hilo akizungumza kwa jazba na mkononi akiwa na kidumu cha mafuta ya petrol.

Kufuatia hali hiyo,mwandishi wa habari hizi aliwasihi wananchi hao kuacha kuchukua hatua hiyo ya kinyama na badala yake aliwataka waite polisi iwachukue na kuwafikisha kwenye vyombo vya dola ambapo walikubali na kuamua kuita polisi waliofika bila kuchelewa.

Hata hivyo muda mfupi baada ya polisi kuwasili eneo hilo,baadhi ya vigogo wa chama hicho mkoa wa Geita akiwemo mbunge wa viti maalumu mkoa wa Geita Vicky Kamata,mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM Taifa Leonald Bugomola, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Geita Muhoja Mapande, Katibu mwenezi wa CCM Wilaya ya Geita aliyejulikana kwa jina moja la Masele waliwasili eneo hilo.

Viongozi hao walianza kuwakingia kifua watuhumiwa hao wasipelekwe polisi hali iliyosababisha upepo uliokuwa umetulia eneo hilo kuvuma tena na wananchi kutishia kupiga yowe ili wananchi wakusanyike na kuwachoma moto watu hao.

Aidha polisi waliamua kutumia lugha za ukali wakiwataka vigogo hao wa CCM kuwa wapole huku wakitishia kuondoka eneo hilo ili wananchi wafanye watakavyo kutokana na vigogo hao kutaka kutumia vyeo vyao na jina la chama tawala kuwafundisha kazi poliusi.

‘’Mmekuja hapa mmekuta wananchi wametulia lakini nyinyi mnataka kuleta fujo na kutuona sisi hatufai,sasa kama ni hivyo tutaondoka hapa tuwaache wananchi watimize adhima yao na tuone kama mtaweza kukabiliana na nguvu ya umma".

"Hebu kuweni wasitaarabu tuwachukue hawa watu kwa amani tuwapeleke kituoni na kama kuna mtu anashida na hawa watuhumiwa aje kituoni’’,alisikika askari mmoja aliyefahamika kwa jina la Dani akipiga mkwara vigogo hao ambao waliamua kuwa wapole.

Baadaye wanachama hao walifikishwa kituo cha polisi Wilaya ya Geita wakiwa na pakiti zao za chumvi kama kidhibiti.

Kwa mjibu wa mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai wilaya ya Geita John Maro aliyekuwa eneo la tukio hilo alisema watuhumiwa wanashikiliwa na jeshi hilo kwa mahojiano zaidi na upelelezi ukikamilika watafikishwa mbele ya sheria kujibu tuhuma zinazowakabili. 

Wananchi wakiwa nje ya nyumba waliwafungia wafuasi wa CCM -Picha na Valence Robert-Malunde1 blog Geita

Valence Robert,
Geita

Kafulila akamatwa

JESHI la Polisi linamshikilia Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kusini, David Kafulila kwa tuhuma za uchochezi, akiwataka wananchi wasichangie ujenzi wa maabara katika shule za sekondari nchini.

Kafulila alikamatwa mapema jana asubuhi katika mji mdogo wa Nguruka wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma, ambako alikuwa akifanya mikutano ya hadhara, kuelezea sakata la uchotwaji wa fedha katika akaunti ya Escrow na kampeni kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Jafari Mohammed amethibitisha kukamatwa kwa mbunge huyo, ambaye anahojiwa katika Kituo Kikuu cha Polisi mjini Kigoma.

Kamanda huyo alisema Kafulila alikamatwa jana asubuhi na askari polisi na kusafirishwa hadi mjini Kigoma, ambako anahojiwa kuhusu matamko ya uchochezi aliyokuwa akitoa kwenye mikutano yake ya hadhara.

Alisema katika mikutano yake, Kafulila aliwataka wananchi kutochangia kwa namna yOyote ujenzi wa maabara katika shule za sekondari na kwamba viongozi watakaokuwa wakifika kwenye maeneo yao kuhamasisha michango na ujenzi wa maabara hizo, wawapige mawe.

“Alichokuwa akifanya Mbunge Kafulila kwa kweli tumeona ni uchochezi na kinaweza kusababisha kuvurugika kwa amani na hivyo tumemkamata tunamshikilia hapa kituo kikuu mjini Kigoma, anahojiwa na maafisa wa juu wa upelelezi wa mkoa,” alisema Kamanda huyo.

Katika mazungumzo yake na waandishi wa habari, Kamanda Mohammed alisema kwa leo (jana) hawakuwa na maelezo ya ziada ya hatua gani watachukua na kwamba baada ya mahojiano jana, leo wanatarajia kutoa taarifa ni hatua gani zitachukuliwa dhidi yake.

Kafulila aliwasili mkoani Kigoma Jumamosi Desemba 6 mwaka huu, ambapo alihutubia mkutano wake wa kwanza katika uwanja wa Community Centre Mwanga mjini Kigoma kabla ya kuendelea na ziara katika vijiji mbalimbali vya wilaya ya Uvinza.

Katika mikutano yake, Mbunge huyo alikuwa akitumia muda wake mwingi kuelezea sakata la uchotwaji wa fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow, huku akitoa shinikizo kwa serikali kutekeleza maazimio manane yaliyotolewa na bunge kuhusu sakata hilo.

BASATA kutathmini shindano la ulimbwende Tanzania 2014

TATHMINI YA SHINDANO LA UREMBO LA MISS TANZANIA 2014

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kama msimamizi na mratibu wa sekta ya Sanaa nchini linanatarajia kufanya tathmini ya Shindano la Urembo la Miss Tanzania la mwaka 2014 tarehe 12/12/2014 saa 3 asubuhi katika ofisi zake Ilala Sharif Shamba.

Waandishi wa Habari na wadau wa Sanaa mnakaribishwa kutoa maoni yenu ili kuboresha shindano hili.
Ni imani ya Baraza kwamba, mahudhurio yenu katika tathmini hii yatasaidia kwa kiwango kikubwa kuboresha mashindano haya ya urembo na kuwezesha Tanzania kupeperusha bendera yake vizuri katika mashindano ya kimataifa. 

Ni matumaini ya Baraza kwamba waandaaji wa shughuli za sanaa wataendelea kutambua umuhimu wa kufuata sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa.

Sanaa ni kazi, tuipende na kuithamini

Godfrey Mngereza
KAIMU KATIBU MTENDAJI

Taarifa ya teuzi mbalimbali za Rais: Mafuru ateuliwa kuwa Msajili wa Hazina

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Laurence Nyasebwa Mafuru kuwa Msajili wa Hazina kuanzia tarehe 5 Novemba, 2014.

Taarifa iliyotolewa leo Desemba 11, 2014 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue inasema kuwa kabla ya uteuzi wake, Bwana Mafuru alikuwa Mkuu wa Idara ya Rasilimali Fedha katika Ofisi ya Rais inayohusika na ufuatiliaji Miradi ya Matokeo Makubwa Sasa (PDB). Aidha Bwana Mafuru pia alikuwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Benki ya FBME iliyowekwa chini ya uangalizi wa muda wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Wakati huohuo, Taarifa ya Balozi Sefue inasema Rais Kikwete amemteua Bibi Beng’i Mazana Issa kuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kuanzia tarehe 4 Desemba, 2014. Kabla ya uteuzi wake, Bibi Mazana Issa alikuwa Mkurugenzi wa Utawala wa Fedha katika Tume ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS).

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Profesa Dominic M. Kambarage kuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Kipya cha Kilimo cha Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kuanzia tarehe 5 Desemba, 2014.

Taarifa iliyotolewa leo Desemba 11, 2014 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue imesema kabla ya kuteuliwa kwake kuwa Makamu Mkuu wa Chuo, Profesa Kambarage alikuwa Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Sokoine, Morogoro.

Taarifa ya Balozi Ombeni Sefue imesema kufuatia kuanzishwa kwa Chuo hicho kingine cha Umma, Rais Kikwete pia amemteua Profesa Lesakit S. Mellau kuwa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo hicho upande wa Taaluma kuanzia tarehe 5 Desemba, 2014, na kabla ya uteuzi wake, Profesa Mellau pia alikuwa Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Sokoine, Morogoro.

Aidha Taarifa ya Balozi Sefue imesema Rais Kikwete amemteua Profesa Msafiri M. Jackson kuwa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo cha Kilimo cha Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (Utawala) kuanzia tarehe 5 Desemba, 2014. Kabla ya uteuzi huo, Profesa Jackson alikuwa Mratibu wa Masomo ya Taaluma za Shahada za Juu katika Chuo Kikuu cha Ardhi, Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bi. Katarina Tengia Revocati kuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani kuanzia tarehe 5 Desemba, 2014. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Desemba 11, 2014 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue, imesema kabla ya uteuzi huo, Bi. Revocati alikuwa Msajili wa Mahakama Kuu, Divisheni ya Biashara.

Vilevile katika Taarifa hiyo, Rais Kikwete pia amemteua Bwana Rugalema J. Kahyoza kuwa Msajili wa Mahakama Kuu kuanzia tarehe 5 Desemba, 2014. Kabla ya uteuzi wake, Bwana Kahyoza alikuwa Hakimu Mwandamizi Msaidizi, Mahakama Kuu, Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Menejimenti na Mashauri.

Katika hatua nyingine, Rais Kikwete amemteua Dkt. Fidelice Mafumiko kuwa Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) kuanzia tarehe 4 Desemba, 2014. Kabla ya uteuzi huo, Dkt. Mafumiko alikuwa Naibu Mkuu TEWW.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
11 Desemba,2014

Statement by The Palestine Embassy in Tanzania on assassination of Ziad Abu Ein

PRESS STATEMENT

11 December 2014

Abu Ein, who was among the peaceful and unarmed protesters along with foreign activists, lost consciousness after being directly shot in the chest with a gas canister by an Israeli soldier and was transferred to hospital where he was pronounced dead shortly afterwards.

Prior to that, three soldiers had grabbed Abu Ein and hit him in the chest, an AFP photographer confirmed.

The assassination by Israeli occupying forces of Abu Ein while leading a peaceful demonstration near Ramallah yesterday is another example of Israel's vicious and arrogant actions committed against the Palestinians. It clearly demonstrates that Israel is responding to Palestinian non-violent resistance with acts of violence, terror and crimes against humanity.

Israel’s actions are nothing short of state-sponsored terrorism, war crime in all the meaning of the word. It is barbarism and savagery of the Israeli occupation

Israel’s use of excessive and indiscriminate violence against Palestinians constitutes war crimes under international law. Israel habitually uses extreme violence, especially against non-violent resistence.

Abu Ein was guilty of nothing more than planting olive trees on Palestinian land that Israel is attempting to steal. The assault on Abu Ein is intolerable and barbaric act that cannot be tolerated nor accepted.

Abu Ein was born in 1959, and was first arrested at the age of 18 in November 1977. In August 1979, he was rearrested by the American CIA and was ‘extradited’ to Israel two years later, where he received a life sentence.

He was released in a prisoner swap in May 1985 and rearrested in July 1985 and held several times later under administrative detention, which means imprisonment without trial.

The UN General Assembly passed several resolutions, including Resolution 36/171, in favor of Abu Ein. The UN General Assembly said Abu Ein was ‘illegally detained’ in a US prison for over two years and that “the sole basis for probable cause against Mr. Ziad Abu Ein was a statement in Hebrew extracted from a person who had no knowledge of the Hebrew language and who was in Israeli custody, whose statement was later withdrawn.”

He assumed several key Fatah positions, including a member of the Fatah Revolutionary Council while previously he served as deputy minister for prisoner affairs.

He was member of Fatah Mobilization and Organization Commission from 2003 to 2007, Deputy Minister of Prisoners’ Affairs in 2006, and his current position is Minister in the President’s Office and Head of the Anti-Wall and Settlement Commission.

With the murder of Minister Abu Ain, Israeli occupiers would fabricate stories in order to clear itself, as they always do. However they bear full responsibility for the killing of Minster Abu Ein and the systematic crimes committed against the Palestinian people.

This new assassination will have severe consequences, for we are determined to continue popular resistance until the Zionist occupation and settlements in the land of Palestine are removed.

The people of Palestine are sure to succeed as did the people of South Africa. This is evident from the movement of boycott, divestment and sanction against Israel (BDS) that is gaining momentum by the day, as well the global solidarity and recognition of the State of Palestine

Embassy of the State of Palestine
612 United nations Road
Dar es Salaam
[email protected]

Mercedes Benz ML320 for saleMercedes Benz ML320CDI 4-Matic, Diesel, 2998cc, 2008
Duty fully paid and registered
Full service at CFAO after computer diagnosis
Fitted with brand new michelin tyres

Call 0715-210113 or write to [email protected]

Miundombinu ya bandari ya Kigoma kuboreshwa

Mkuu wa Bandari ya Kigoma, Bw. Athuman Malibamba (katikati, mbele) akifafanua jambo kwa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango mara walipofika kujionea shughuli za maendeleo kiwanjani hapo.

Na Saidi Mkabakuli, Kigoma

Serikali imeazimia kuendelea kuboresha miundombinu ya bandari hususan miradi iliyoibuliwa katika Programu ya Matokeo Makubwa Sasa ikiwemo kuanza kufanya upanuzi wa Bandari ya Kigoma na kuendelea kuboresha miundombinu na ununuzi wa vifaa mbalimbali vya kuhudumia shehena katika Bandari ya Kigoma ili kuweza kukidhi mahitaji yanaongeza siku baada ya siku katika bandari hiyo.

Ahadi hiyo imetolewa na Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri wakati walipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya miundombinu katika Bandari ya Kigoma.

Bibi Mwanri alisema kuwa serikali kupitia Mamlaka ya Bandari nchini nchini ipo kwenye mkakati wa kuiendeleza bandari hiyo ili iwe ya kiwango kizuri kwa kuhudumia watumiaji wa wa bandari hiyo.

“Kama munavyokumbuka Serikali katika mwaka huu wa fedha ilipanga kuiendeleza na kuboresha miundombinu ya usafiri wa majini na anga ili kuongeza ufanisi wa sekta hizi, ambapo Bandari ya Kigoma ni mojawapo ya bandari zilizopewa kipaumbele kwa ajili ya uendelezaji,” alisema Bibi Mwanri.

Kwa mujibu wa Bibi Mwanri, upanuzi wa bandari hiyo upo kwenye hatua za upembuzi yakinifu kwa ajili ya kuboresha bandari ya Kigoma na kutwaa maeneo zaidi kwa ajili ya upanuzi wa bandari hiyo.

Akitoa taarifa ya maendeleo ya Bandari hiyo, Mkuu wa Bandari hiyo Bw. Athuman Malibamba alisema kuwa mpaka kufikia Juni 2014 hatua ya utekelezaji iliyofikiwa ni kukamilika kwa kazi ya uthamini wa mali eneo la Kibirizi lenye hekta 10 kwa ajili ya upanuzi wa bandari hiyo. “Pia, Mamlaka imempata Mtaalam Mshauri (M/S Royal Haskoning H.D.V Nederland, B.V) atakaefanya kazi ya Upembuzi Yakinifu. Aidha, kazi ya uthamini wa mali imekamilika kwa eneo la Katosho lenye hekta 69 kwa ajili ya kujenga bandari kavu,” alisema.

Kuongezeka kwa shughuli za kiuchumi katika nchi za jirani kunatoa fursa ya kuimarisha miundombinu ya bandari ya Kigoma ili kuwa na uwezo wa kuhudumia shehena inayoongezeka na kukuza uchumi katika mkoa na Taifa kwa ujumla. Aidha kuanzishwa kwa Eneo Maalum la Kiuchumi, katika mkoa wa Kigoma ni kichocheo muhimu kwa Mamlaka ya Bandari (TPA) kuimarisha huduma katika bandari ya Kigoma na hivyo kuweza kuzitumia fursa zitakazojitokeza mara baada ya shughuli mbalimbali za kiuchumi kuanzishwa. 


Sehemu ya chelezo zinazotumika kwa ajili ya matengenezo ya meli na boti katika Bandari ya Kigoma.


Mratibu wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bw. Senya Tuni (Wapili kushoto) akiuliza jambo kwa Mkuu wa Bandari ya Kigoma, Bw. Athuman Malibamba (Wapili kulia) walipofanya ziara bandarini hapo.

Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Aliyenyanyua mkono) akionesha kufurahia jambo wakati walipofanya ziara katika Bandari ya Kigoma.

Mkuu wa Bandari ya Kigoma, Bw. Athuman Malibamba (Wapili kulia) akifafanua jambo kwa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango mara walipofika kujionea shughuli za maendeleo kiwanjani hapo

Afisa utekelezaji wa Bandari Kigoma, Bw. Teophil Luoga (Kulia aliyechuchumaa) akiwaonesha eneo la upanuzi wajumbe wa timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango mara walipofika kujionea shughuli za maendeleo kiwanjani hapo.


Mkuu wa Bandari ya Kigoma, Bw. Athuman Malibamba (Kulia) akimkaribisha Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Kushoto) mara alipofika kujionea maendeleo ya bandari hiyo.Boti na meli zikipandisha shehena kwenye Bandari ya Kigoma.

United against Ebola / Tokomeza EbolaMikopo ya Elimu kwa Vijana yazinduliwa

Waziri Kabaka akizungumza katika uzinduzi wa huduma ya mikopo ya elimu na kuanzia maisha kwa wanachama wa Mfuko wa PSPF jijini Dar es Salaam.
 
WAZIRI wa Kazi na Ajira nchini Tanzania, Gaudensia Kabaka ameipongeza Benki ya Posta Tanzania (TPB) pamoja na Mfuko wa PSPF kwa kushirikiana na kuanzisha mpango wa utoaji wa mikopo ya elimu kwa vijana pamoja na mkopo wa kuanzia maisha kwa wafanyakazi. Waziri Kabaka ametoa pongezi hizo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizinduwa huduma ya mkopo wa elimu kwa wanachama wa mfuko wa PSPF iliyofanyika katika Ukumbi wa Golden Jubelee Tower.

Alisema huduma za mikopo ya elimu na kuanzia maisha ni huduma muhimu sana kwa vijana kwani upataji wa fedha za kujiendeleza kwa kundi hili imekuwa changamoto kubwa hivyo kupatikana kwake itafungua milango kwa vijana kujiendeleza kielimu bila vikwazo.

Akizungumzia huduma ya mkopo wa wa kuanzia maisha alisema huduma hiyo imekuja wakati muafaka kwani mtu anapoanza kazi anakuwa akihitaji vitu muhimu na vya msingi katika maisha lakini wamekuwa wakikwamishwa na hali ya kipato. Hivyo mkopo huu utakuwa mkombozi wa wengi wanaoanza maisha kazini.

"...Kitu kilichonifurahisha zaidi ni jinsi PSPF mlivyoshirikiana na Benki ya Posta Tanzania katika kubuni, kupanga, kuandaa na hatimaye kutekeleza utaratibu huu, hili ni jambo sahihi na muafaka kwani kwa mujibu wa taratibu za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii duniani kote kazi za mifuko hii sio kutoa mikopo bali ni kuwawezesha wanachama wake kupata mafao yao stahili pale wanapostaafu," alisema Waziri Kabaka.

Benki ya Posta Tanzania (TPB) kwa kushirikiana na Mfuko wa PSPF imezinduwa aina mpya ya mikopo kwa wanachama wake ambapo watapata fursa ya kupewa mikopo ya elimu pamoja na ya kuanzia maisha kwa wale wafanyakazi wanaoanza maisha.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mpango huo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, Sabasaba Moshingi alisema TPB inatambua mzigo mkubwa uliobebwa na Serikali katika kuwasomesha vijana hivyo imeamua kubeba jukumu la kuwasaidia vijana kukopa kwa lengo la kujiendelea kielimu.

"Benki ya Posta inatambua mzigo mkubwa uliobebwa na Serikali katika kuwasomesha vijana wetu katika vyuo vikuu mbalimbali hapa nchini, na tukiwa kama Benki halisi ya Kitanzania tumeamua kwa dhati kabisa kuisaidia Serikali katika nyanja hii, tukishirikiana na wenzetu wa PSPF," alisema Moshingi.

Alisema hata hivyo Benki ya Posta imeendelea kubuni huduma za kibenki mbalimbali kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya wananchi wa kila kada hapa nchini. Alisema Mwezi Machi 2014 benki hiyo iliingiza huduma mpya ya mikopo kwa kundi la wastaafu nchini jambo ambalo limekuwa faraja kubwa kwa wastaafu nchini.

"...Adhma yetu ni kuhakikisha kuwa tunamkomboa kiuchumi mwananchi, hususan mwenye kipato cha chini kwa kumpatia mkopo wenye riba nafuu. Mkopo huu wa elimu uliozinduliwa leo una lengo la kumsaidia mwanachama wa PSPF kutimiza ndoto zake kwa kujiendeleza kielimu katika ngazi yoyote, stashahada, shahada, shahada ya uzamili na nyinginezo," alisema.

"Mwanachama wa PSPF anayetaka kukopa aina hii ya mkopo atadhaminiwa na mwajiri wake, pia mkopo huu unabima, hivyo endapo mkopaji atafariki familia yake haitaendelea kudaiwa na riba inayotozwa kwa mkopo huu ni nafuu yaani asilimia 14 tu kwa mwaka," alisisitiza Moshingi.

 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, Sabasaba Moshingi akizungumzia katika hafla ya uzinduzi wa huduma ya mkopo wa elimu kwa wanachama wa mfuko wa PSPF leo jiji ni Dar es Salaam.

 Waziri wa Kazi na Ajira nchini Tanzania, Gaudensia Kabaka akizinduwa huduma ya mikopo ya elimu na kuanzia maisha kwa wanachama wa Mfuko wa PSPF jijini Dar es Salaam.

 Ofisa Mtendaji Mkuu, PSPF Adam Mayingu akizungumza katika uzinduzi huo.

 
Waziri wa Kazi na Ajira nchini Tanzania, Gaudensia Kabaka akiwasili katika Ukumbi wa Golden Jubelee Tower pamoja na viongozi wakuu wa Benki ya Posta Tanzania na Mfuko wa PSPF tayari kwa uzinduzi wa huduma ya mikopo ya elimu na kuanzia maisha kwa wanachama wa Mfuko wa PSPF jijini Dar es Salaam.

 
Waziri wa Kazi na Ajira nchini Tanzania, Gaudensia Kabaka akizinduwa huduma ya mikopo ya elimu na kuanzia maisha kwa wanachama wa Mfuko wa PSPF jijini Dar es Salaam.

 Waziri wa Kazi na Ajira nchini Tanzania, Gaudensia Kabaka akiwa amewanyanyua juu mikono Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, Sabasaba Moshingi (kushoto) na Ofisa Mtendaji Mkuu, PSPF Adam Mayingu (wa pili kulia) mara baada ya uzinduzi wa huduma ya mikopo ya elimu na kuanzia maisha kwa wanachama wa Mfuko wa PSPF jijini Dar es Salaam.

 Kutoka kushoto ni Waziri wa Kazi na Ajira nchini Tanzania, Gaudensia Kabaka, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, Sabasaba Moshingi na viongozi wengine wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa huduma ya mikopo ya elimu ya juu kwa vijana.

 Balozi wa Mfuko wa PSPF, Mrisho Mpoto (mjomba) akiwa katika hafla hiyo ya uzinduzi.

 Uzinduzi wa huduma ya mikopo ya elimu na kuanzia maisha kwa wanachama wa Mfuko wa PSPF jijini Dar es Salaam.

 Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Posta Tanzania na PSPF wakiwa katika uzinduzi huo.

 Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Posta Tanzania na PSPF wakiwa katika uzinduzi huo.

*Imeandaliwa na www.thehabari.com

Wanavyuo Iringa waambiwa waachane na siasa

Hassan Mtenga kiwahutubia wananchi wa mtaa wa Semtema, Iringa

Na Fredy Mgunda, Iringa

Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM mkoani Iringa Hassan Mtenga, amefungua rasmi kampeni za uchaguzi wa Serikali za mitaa katika mtaa wa Semtema mkoani iringa.

Akiwahutubia mamia ya wananchi wa mtaa wa Semtema, Mtenga aliwataka wananchi wa eneo hilo kuwa makini wakati wa kuchagua kiongozi katika uchaguzi utakao fanyika tarehe 14/12/2014.

Mtenga alisema kuwa uchaguzi wa serikali za mitaa ni muhimu sana kwa maendeleo ya nchi na watu binafsi kwa kuwa kila maendeleo yanaanzia chini ndiyo yanaenda juu, hivyo wananchi wanatakiwa kuwa makini sana na kumchagua kiongozi anayefaa.

Aidha, Mtenga aliwataka wanafunzi wa vyuo vikuu mkoani Iringa kuacha kuiga siasa chafu ambazo huiga kutoka kwa wapinzani wao kwa kuwa wanaiga wasichokijua ambacho kitawaletea madhara baadae.

Alisema kuwa Iringa ni ya watu wa Iringa hivyo kuwaambia wanafunzi wa vyuo vyote mkoani Iringa kuwaachia siasa Wanairinga na wao waendelee na walichokifuata hapa.

Wanafunzi waliohudhuria mkutano huo walimsifu Katibu huyo kwa kuwa na sera zinazotekeleza na kuwaambia ukweli vijana waliopo vyuoni kwa kuwa wananfunzi wengi wamekuwa wakiiga mambo mengi bila kujua nini kipo mbele yao.

Wananchi waliojitokeza eneo hilo walimuita katibu huyo kwa jina dawa ya muarobaini kwa maneno aliyoyatoa katika mkutano huo na kumsifu kiongozi huyo kuwa ni kiongozi anayefaa kuigwa hapa mkoani Iringa.

Baadhi ya wananchi walisikika wakisema kwa sera za Mtenga, basi Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini atake asitake ataondoka tu, na kumwomba aanze kukusanya kilicho chake.


Wananchi wa mtaa wa Semtema
HC Melrose hand-over Fire, Police and Medical Equipment to Chikawe

HC Dianna Melrose from The British High Commission-Dar, Minister Mathias Chikawe from Ministry of Home Affairs and Representatives from Police Force
  
            


PRESS STATEMENT


Thursday 11th December, 2014


British charity, UK Police Aid Conveys, gifts Tanzania vital fire fighting and police equipment


British High Commissioner, Dianna Melrose, handed over a variety of fire fighting and police equipment on 11th December on behalf of the UK charity ‘UK Police Aid Conveys’, to Minister Mathias Chikawe, Ministry of Home Affairs and Minister Dr Seif Rashid, Ministry of Health and Social Welfare.


Speaking at the event, Ms Melrose said:


“The donation of these materials demonstrates the collaborative nature of the United Kingdom’s partnership with Tanzania. Today we are handing over a large quantity of different items – from fire fighting and medical items, to police uniforms and protective clothing, and furniture. These goods have been provided by numerous different donors in the UK – by the National Crime Agency, a number of UK Police Forces, the Fire Service, the Ambulance Service, and by hospitals across the United Kingdom. They will benefit Tanzania’s Fire and Police Services and medical centres across the country”.


The goods were organised by UK charity National Police Aid Convoys. The UK Police Aid Convoys is a volunteer charity based in the UK that collects, sorts and then dispatches this sort of development aid to communities all over the world.


Wanda Adams, the secretary of the UK Police Aid Convoys charity said:


“I am delighted to see everything delivered safely in Tanzania and look forward to news of its reception and utilisation.  We would like to express our thanks to the National Crime Agency in the UK and to Songas Ltd in Dar es Salaam for supporting the costs of importing the containers to Tanzania  Thanks also to the  National Police Aid Convoys in the UK for selecting Tanzania and Zanzibar to be the benefactors of this equipment.”


Speaking on behalf of Songas Ltd Nicodemus Chipakapaka said:


“Songas is proud to play a part in supporting this strong collaborative partnership between the United Kingdom and United Republic of Tanzania. These contributions will be of immediate benefit to the Police, Fire and Medical services and hence to people of Tanzania”.


A further 42 foot container of emergency services equipment is in the process of being prepared for handover to authorities in Zanzibar shortly.


The donation represents a small part of the wider programme of partnership working that is achieved on a daily basis between the UK and Tanzanian institutions, but is demonstrative of the collaborative approach that we believe provides the most benefit to both nations’.


HC Dianna Melrose, The British High Commission Dar hand-over equipment to Police Force

HC Dianna Melrose shake hands with Minister Mathias Chikawe after handling over of equipments

Angela Akilimali atunukiwa Shahada ya Mawasiliano ya UmmaKaimu Mukurugeni wa Uhuru FM, Angela Akilimali (katikati) akiwa na wahitimu wenzake wa Shahada ya Mawasiliano ya Umma ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) katika mahafali yaliyofanyika hivi karibuni mkoani Kibaha mkoani Pwani. Kushoto ni Hemed Mbaraka na Mganwa Nzota.Wanahabari wa morogoro nao walikula nondo zao katika mahafali hayo.Angela Akilimali akiwa na mumewe Hassan Hemedi Chamshama baada ya kumkabidhi shada la maua wakati akimpongeza.Toka kushoto ni Idda Mushi wa ITV/Redio One - Morogoro, Angela Akilimali wa Uhuru FM na Hana Mayige wa TBC wakipozi kwa picha wenye furaha baada ya kula nondo zao. 

  • Tumeshirikiishwa habari picha hii na Mroki Mroki. Picha zaidi, tizama KIDEVU BLOG.

Katibu Mkuu UVCCM aanza ziara ya siku 14 Kanda ya Ziwa


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Katibu Mkuu wa jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) Ndugu Sixtus Mapunda anategemea kufanya ziara ya siku na nne (14) katika mikoa minne ya Kanda ya Ziwa, ambayo ni Tabora, Shinyanga, Geita na Kagera kuanzia kesho tarehe 12st Dec 2014.

Ziara hii ya kikazi ya Katibu Mkuu inalenga kukagua na kuhimiza ujenzi na uimara wa jumuia ya Vijana katika maeneo husika lakini pia kushiriki kampeni zinazoendelea za uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mnamo tarehe 14th Dec 2014.

Pia, Katibu Mkuu anatarajia kufanya mikutano ya ndani na viongozi wa Jumuiya na Chama, pia kufanya mikutano ya hadhara inayolenga kuingiza wanachama wapya ndani ya jumuiya na chama kwa ujumla.

Kuhimiza wanachama wa chama cha mapinduzi na viongozi kuwaandaa wananchi katika kuipigia kura katiba mpya iliyopendekezwa wakati ukifika.

Ziara hiyo ya Katibu Mkuu inategemea kumalizika tarehe 25th Dec 2014.

Kidumu Chama Cha Mapinduzi.

Mikoa ihamasishe uwekezaji wa viwanda

Afisa fedha wa Kiwanda cha nguo Dahong Bw. Luke Li akiwaonyesha Bw. Erasmus Masumbuko na Bi. Angela Shayo (wachumi kutoka Tume ya Mipango) ubora wa nyuzi za pamba zinazotengenezwa na kiwanda chake.

Na Oyuke Phostine - Shinyanga

Serikali imetoa wito kwa Ofisi za wakuu wa mikoa kuhamasisha uwekezaji katika sekta ya viwanda kwenye mikoa yao ili kuweza kukuza uchumi wa mikoa husika na taifa kwa ujumla.

Wito huo umetolewa na Bw. Paul Sangawe, Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, anayeshughulikia Biashara za Kimataifa wakati akiongoza timu ya wataalam kutoka ofisi hiyo iliyokuwa ikifanya ukaguzi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali na sekta binafsi katika mikoa ya Shinyanga, Mara, Simiyu, na Mwanza.

Bw. Sangawe, alisema kuwa Wajibu wa Serikali ni kuweka mazingira wezeshi kwa sekta binafsi kuwekeza. Alifafanua kuwa, moja ya vipaumbele katika Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano ambao utekelezaji wake unaishia 2015/16, ni miundombinu ili kufungulia fursa za ukuaji wa uchumi.

Aidha, Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano unaofuata kuanzia 2016/17 utalenga katika kuendeleza viwanda. Hivyo, alitoa rai kwa viongozi katika ngazi za mikoa kuratibu masuala ya uwekezaji hususan katika viwanda ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa uwekezaji huo unawanufaisha wananchi wa maeneo husika kwa kuongeza fursa za ajira na masoko ya bidhaa za kilimo.

“Uwepo wa viwanda hivi unaonyesha mwenendo na mwelekeo mzuri wa taifa katika kufungua fursa za maendeleo na kiuchumi kupitia sekta ya viwanda, hivyo basi iwapo jitihada za kuhamasisha uwekezaji wa viwanda katika kila mkoa zitatiliwa maanani ni dhahiri kuwa fursa za ajira zitaongezeka na kasi ya ukuaji uchumi itaongezeka” alisema Bw. Sangawe.

Akizungumza na timu hiyo ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo ilipotembelea na kukagua kiwanda cha kusindika mafuta kwa kutumia alizeti na mbegu za pamba cha Jielong Holdings Mkoani Shinyanga, Kaimu Meneja Utawala Bw. Atanas William alisema kuwa mpaka sasa kiwanda hicho kinaweza kusindika na kuhifadhi lita milioni 2.4 kwa mwezi.

“Kwa sasa upatikanaji wa mali ghafi ni wakuridhisha kwa sababu bado tunanunua alizeti kutoka kwa wakulima, na mbegu za pamba katika vinu vya kuchambua pamba (Ginneries). Tuna mpango wa kuhamasisha na kuwafundisha wakulima njia bora za kilimo na utunzaji wa mazao ili kujihakikishia upatikanaji wa mali ghafi yenye ubora zaidi” alisema Bw. Atanas.

Viwanda vingine vilivyotembelewa ni kiwanda cha Dahong kinachotengeneza nyuzi za pamba na kiwanda cha Xinghua cha kusindika ngozi mkoani Shinyanga na kiwanda cha nguo cha Mwatex Mkoani Mwanza. Kiwanda cha Dahong kina uwezo wa kununua tani 12,000 za pamba kwa mwaka na kuzalisha tani 7 za nyuzi za pamba kwa siku. Kiwanda hiki kimeanza uzalishaji mwezi Septemba 2014, na nyuzi zote zinazozalishwa zitauzwa nchini China.

Kwa mujibu wa bwana Luke Li, ambaye ni afisa fedha wa kiwanda hicho, mipango ya baadae ya kiwanda hicho ni kutengeneza nguo. Bwana Li pia alisema kuwa kuna mpango wa kujenga kinu cha kuchambua pamba na kutoa mafunzo kwa wakulima ili kuwezesha upatikanaji wa pamba yenye ubora unaotakiwa.

Kwa upande wake, Meneja wa kiwanda cha Xinghua, Bw. Wang, alisema kuwa usindikaji wa ngozi unasuasua kutokana na upatikanaji hafifu wa malighafi. Wafugaji wanapowekea alama mifugo na kutoboa ngozi wakati wa kuchinja, wanaathiri sana ubora wa ngozi alisema meneja huyo. Katika kukabiliana na changamoto hii, mwekezaji huyo ana mpango wa kujenga machinjio ya kisasa ambayo pia itahusisha usindikaji wa nyama.

Aidha Bw. Sangawe alitoa rai kwa viongozi wa mikoa inayotoa ngozi kwa wingi kuongeza jitihada za kutoa elimu kwa wafugaji kuhusu umuhimu wa ubora wa ngozi ili kuhakikisha ngozi inayopatikana Tanzania inakuwa na thamani ya hali ya juu.

Kaimu Meneja Utawala Bw. Atanas William wa Kiwanda Cha Mafuta (Jielong Holdings) akimwonyesha Bw. Paul Sangawe, Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, shehena ya mbegu za pamba zinazotumika na kiwanda katika usindikaji wa mafuta.

Kaimu Meneja Utawala Bw. Atanas William wa Kiwanda Cha Mafuta (Jielong Holdings) akitoa maelezo kwa timu ya ukaguzi jinsi mafuta yanavyofungashwa katika ndoo tayari kwa kwenda sokoni. Kiwanda hiki kina uwezo wa kuzalisha lita za mafuta milioni 2.4 kwa mwezi.

Wakaguzi wa Miradi kutoka Ofisi ya Raisi, Tume ya Mipango wakiwa na Kaimu Meneja Utawala Bw. Atanas William wa Kiwanda Cha Mafuta (Jielong Holdings) wakiangalia jinsi mitambo inavyomimina mafuta katika ndoo tayari kwa kwenda sokoni.

Meneja wa Kiwanda Cha Ngozi Bw. Wang (aliyeinama) akiwaonyesha wakaguzi wa miradi kutoka Ofisi ya Rais Tume ya Mipango ngozi za mbuzi zilizochakatwa . Kiwanda hiki kina uwezo wa kuchakata ngozi 10,000 za mbuzi na 2,000 za ng’ombe kwa siku.

Meneja wa Kiwanda Cha Ngozi Bw. Wang (Kulia) akitoa maelezo kuhusu uandaaji ngozi kabla ya kwenda sokoni. Kiwanda hiki kina uwezo wa kuchakata ngozi 10,000 za mbuzi na 2,000 za ng’ombe kwa siku. Wengine katika picha kutoka kulia ni Bw. Paul Sangawe, Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango anayeshughulikia Biashara za Kimataifa na Bw. Erasmus Masumbuko, Mchumi Tume ya Mipango.