Waichoma moto Toyota VX baada ya kugonga na kuua 3

Gari aina ya Toyota VX likiwaka moto baada ya kuchomwa na wananchi mchana jana, Ijumaa huko Bunju B jijini Dar es Salaam kwa kusababisha ajali na kuua madereva watatu wa bodaboda. (picha: Michuzi blog)

Imeelezwa kuwa ajali imetokea Bunju B.  Dereva wa Toyota VX alitoka mzima ila gari lake lilichomwa moto na wananchi. Miili ya maiti ilipelekwa Kituo cha Polisi Bunju A. (picha: Malunde1 blog)

Singasinga wa 'escrow' anasakwa na vyombo vya usalama

MMILIKI wa kampuni ya IPTL, Harbinder Sethi Singh, ametoweka na vyombo vya usalama vimejiandaa kumkamata endapo atarejea nchini, Raia Mwema limeelezwa.

Singh ambaye kampuni yake ya Pan African Power Solutions (PAP) inadaiwa kununua umiliki wa kampuni ya kufua umeme ya IPTL katika mazingira yaliyozua utata, anadaiwa kuwa yupo nchini Kenya au Afrika ya Kusini.

Gazeti hili lilielezwa kwamba Singh aliondoka nchini siku chache kabla ya Bunge la Tanzania kutoa maazimio yaliyotaka wahusika wote wa makosa ya kijinai katika suala hilo wakamatwe na hatua za kisheria dhidi yao zichukuliwe.

Azimio namba moja la Bunge lilisema;….. 
“TAKUKURU, Jeshi la Polisi na vyombo vingine husika vya Ulinzi na Usalama viwachukulie hatua stahiki za kisheria, kwa mujibu wa sheria za nchi yetu, watu wote waliotajwa na Taarifa Maalumu ya Kamati kuhusika na vitendo vyote vya kijinai kuhusiana na miamala ya Akaunti ya Escrow, na watu wengine watakaogundulika kuhusika katika vitendo hivyo vya jinai kufuatia uchunguzi mbalimbali unaoendelea”.

Raia Mwema limeelezwa kwamba Singh ambaye katika siku za nyuma alikuwa akipenda kufikia katika hoteli tofauti ikiwamo Sea Cliff ya jijini Dar es Salaam, sasa hayupo Dar es Salaam lakini anafuatilia kwa karibu yanayoendelea.

“Naweza kukuthibitishia kwamba Sethi hayupo nchini hivi sasa. Kwenye hili suala sitaki kuwa mzungumzaji wake lakini nafahamu kwamba aliondoka kabla ya Bunge kuazimia wahusike wakamatwe.
“Sasa kama alifanya hivyo kwa kujua hayo yanaweza kutokea mimi sijui. Siwezi pia kujibu swali lako la atakuja lini kwa sababu sijaambiwa. Hata hili la kukwambia kwamba hayupo nimekwambia kwa sababu tunafahamiana na sitaki kukudanganya,” 
alisema mmoja wa watu wafanyakazi wa Seth ambaye hata hivyo gazeti hili (Raia Mwema) haliwezi kumtaka jina.

Mwanasheria wa IPTL, Joseph Makandege, ambaye pia ndiye msemaji wa kampuni hiyo, hakupokea simu wala kujibu ujumbe mfupi wa maneno kupitia njia ya simu aliyoandikiwa na gazeti hili  (Raia Mwema) tangu juzi.

Hata hivyo, gazeti hili (Raia Mwema) limeambiwa kwamba vyombo vya usalama vinafahamu Seth hayupo na vimejipanga kumkamata endapo atarejea nchini ili ajibu tuhuma zinazomkabili.

Msemaji wa TAKUKURU, Doreen Kapwani, hakutaka kuthibitisha wala kukana kuhusu mpango wa taasisi hiyo kumkamata Singh, kwa maelezo kwamba kwa sasa yuko likizo na hana taarifa rasmi.

“Ningeshauri umtafute Mkurugenzi Mkuu, Dk. Edward Hoseah, ili akupe taarifa rasmi. Mimi niko likizo na hivyo sina taarifa zozote. Mkurugenzi anaweza kuwa na taarifa mpya zaidi,” 
alisema Kapwani.

Ingawa Seth ni mzaliwa wa Iringa, Tanzania, anaishi nchini Afrika Kusini ambako inaelezwa anafanya biashara; akitajwa kuwa mshirika muhimu wa kibiashara wa mtoto wa Rais mstaafu wa Kenya, Daniel Moi, aitwaye Gideon Moi.

“Hatuwezi kutangaza kwamba tutamkamata Singh. Hii itamfanya ajifiche huko aliko na asije. Wewe subiri arudi uone. Wengine waliopo hapa nchini ambao tutahitaji kuwakama tutawakamata tu. Ngoja kwanza tuanze naye huyo,” 
alisema mmoja wa maofisa wa ngazi za juu wa Jeshi la Polisi aliyezungumza na gazeti hili (Raia Mwema) kwa masharti ya kutotajwa majina.

Nchini Kenya, Singh anafahamika kama mmoja wa wahusika katika ufisadi wa Goldenberg ambako yeye na baadhi ya wafanyabiashara kama Kamlesh Pattni na familia ya Moi walihusishwa nayo.

Katika kipindi cha wiki iliyopita, Singh amezungumza na baadhi ya vyombo vya habari vya hapa nchini ambapo katika mahojiano yake yote, amekataa kueleza alipo.

Baadhi ya tuhuma ambazo zinamkabili Singh moja kwa moja kutokana na maazimio ya Bunge ni madai ya kukwepa kulipa kodi, kughushi nyaraka na kutakatisha fedha haramu.

Chanzo cha habari cha gazeti hili (Raia Mwema) kimeeleza kwamba Singh hana pa kukimbilia zaidi ya Kenya au Afrika Kusini ambako kimsingi ndiko kwenye biashara zake na makazi yake.

Singh alikwenda nchini Kenya kwenye miaka ya 1980 ambako alifanikiwa kujiingiza kwenye familia ya Moi na kutengeneza urafiki na baadhi ya wanasiasa wenye nguvu na ushawishi nchini humo kama Nicholas Biwott.

Mbali na IPTL, Singh tayari ameingia katika biashara ya kutafuta mafuta katika Visiwa vya Songosongo, eneo la Mnazi Bay, ambako yeye ni mmoja wa wakurugenzi wa kampuni ya Hydrotanz ambayo inaendeshwa kwa ubia na kampuni ya Adhunik.

Suala la Singh limefika hapa kutokana na kazi ya uchunguzi iliyofanywa na Takukuru pamoja na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ambayo iliwasilishwa kwa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ambayo ilichambua taarifa hizo na kisha kuzipeleka bungeni.

PAC ilipendekeza Sethi akamatwe na kuhojiwa kutokana na tuhuma mbalimbali kama vile utakatishaji wa fedha, kukwepa kulipa kodi na udanganyifu lakini maazimio ya Bunge ndiyo yaliyojumuisha na wahusika wengine katika suala hilo.

Katika gazeti hili (Raia Mwema) wiki iliyopita, iliripotiwa kwamba mtu wa karibu zaidi na Sethi hapa Tanzania kwa sasa anafahamika kwa jina la Rajiv Bhesania, ambaye jina lake limeonekana katika miamala iliyofanywa kupitia akaunti ya PAP ya Benki ya Stanbic ya hapa nchini ambayo inafanyiwa uchunguzi kwa sasa.

“Kama Serikali inataka kupata chochote kutoka kwa Sethi inabidi wambane huyuhuyu Rajiv Bhesania. Yeye ndiye kila kitu kwa Sethi hapa Tanzania. Hata akitaka mambo yake yanyooke mahali huwa anamtumia huyu.
“Nafahamu si rahisi kusema kila kitu lakini nafahamu kwamba kama vyombo vya ulinzi vitambana kisawasawa, anaweza kutoa siri zote za Sethi na hatimaye Watanzania wakapata wanachokitaka,” 
alisema mfanyakazi huyo wa IPTL.

Mmoja wa maofisa wa Takukuru aliyezungumza na gazeti hili (Raia Mwema) kwa masharti ya kutotajwa jina kwa maelezo kwamba uchunguzi unaendelea, alisema wamepata ushirikiano mzuri kutoka Stanbic na kuna uwezekano kwamba 
“ watu watakula Krismasi wakati tayari TAKUKURU ikiwa imemaliza kazi”.
via Raia Mwema: Singh wa Escrow atoweka

[updated] Taarifa ya MjengwaBlog kutokuwa hewani


Ndugu zangu,
Ni saa kadhaa zilizopita. Tunawashukuru wote mliotutumia jumbe na kutupigia simu kuulizia kulikoni. Mmeonyesha kujali. Tunaamini, kuna wengi pia ambao hawakupata nafasi ya kuulizia tatizo, lakini, kuwa wapo pamoja nasi,tunawashukuru sana. Unaweza sasa kutembelea mjengwablog.com
Ndugu zangu,

Kutokana na sababu za kiufundi ikiwamo marekebisho muhimu, blogu yako ya kijamii, Mjengwablog.com haiko hewani kuanzia jana jioni. Wataalam wanalishughuIikia tatizo na Mjengwablog itarudi tena hewani kabla ya saa sita mchana kwa saa za Afrika Mashariki. Hata hivyo, KwanzaJamii Radio iko hewani kama kawaida, sikiliza live... ustream.tv/channel/kwanzajamii-radio

Poleni kwa usumbufu.

Maggid Mjengwa,
Mwenyekiti Mtendaji
IkoloMedia
Iringa.

CCM yazoa viti bila kupingwa katika uchaguzi wa SM

Wana CCM wakimshangilia Nape alipowasili kwenye mkutano huo


Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana na baadhi ya viongozi wa CCM baada ya kuwasili katika mkutano wa kufunga kampeni za Uchaguzi wa serikali za Mitaa za Jimbo la Ilala, Dar es Salaam, leo jioniWananchi wakimshangilia Nape alipowasili kwenye mkutano huoNape akiwa Jukwaa Kuu pamoja na viongozi wa CCM baada ya kuwasili kwenye mkutano huoLwiza Mbutu akiongoza bendi ya Twanga Pepeta kutumbuiza baada ya kuwasili Nape kwe ye mkutano huoTwanga akionyesha uhodari wa kuchezambele ya meza kuuKatibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Abilahi Mihewa akisalimia wananchi wa Jimbo la Ilala waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano huo wa kufunga kampeni za serikali za mitaaKada wa CCM Haji Manara akiwasalimu wakazi wa Jimbo la Ilala wakati wa mkutano huo. wa kufunga kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika kwenye makutano ya mtaa wa Kongo na Faru ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa jimbo la Ilala ni sehemu salama sana kwa CCM kwa kuwa jimbo hilo lina historia ya CCMMwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Ramadhani Madabida akisalimia wananchi wa Jimbo la Ilala wakati wa mkutano huo wa kufunga kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa jimbo la ilala uliofanyika kwenye makutano ya mtaa wa Kongo na Faru.Mbunge wa Jimbo la Ilala Azani Zungu akilonga jukwaani, ambapo aliwataka watendaji wa serikali kuacha kuwabunghudhi mamalishe wa jimbo hilo kwa kuwa ni eneo la biashara tu, hivyo watendaji hao watengeneze mazingira mazuri badala ya timua timua ya mara kwa maraNape akihutubia kwenye mkutano huoNape akihutubia wananchi kwenye mkutano huo na ifuatayo ni habari kamili ya alichosema

Na Bashir Nkoromo
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaingia katika uchaguzi wa serikali za mitaa kesho, kikiwa kimeshajizolea maelfu ya nafasi ambazo wagombea wake wamepita bila kupingwa.

Akihutubia kwenye mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi huo, katika Mtaa wa Mtambani B, Kata ya Jangwani, jimbo la Ilala jijini Dar es Salaam, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye alisema, kulingana na takwimu CCM imepita bila kupingwa katika vijiji 2708, mitaa 644, na vitongoji zaidi ya 26,300.

Alisema, CCM imeweza kupita bila kupigwa baada ya vyama vya upinzani kushindwa kusimamisha kabisa wagombea na maeneo mengine kuweka wagombea ambao walionekana kukosa sifa za kugombea baada ya kuwekewa pingamizi.

Nape alisema, hatua hiyo ya CCM kuingia kwenye uchaguzi huo ikiwa na mtaji mkubwa wa nafasi ambazo wagombea wake amepita bila kupingwa ni dalili tosha kwamba chama kitavibwaga vibaya vyama vya upinzani kuliko uchaguzi uliopita mwaka 2009.

"Uchaguzi uliopita wa serikali za mitaa CCM iliibuka na ushindi wa asilimia 96, sasa kutokana na dalili za mapema, uchaguzi wa safari hii sina shaka kabisa kwamba wapinzani tutawapiga kwa ushindi wa asilimia mia moja", alisema Nape.

Nape aliupongeza uongozi wa CCM katika jimbo la Ilala, baada ya kumthibitibishia kwamba katika kipindi chote cha kampeni jimbo hilo
wamekuwa wakifanya kampeni za kistaarabu na wanao uhakika wa
kuibuka na ushindi kwa asilimia mia moja baada ya uchaguzi.

"Sina shaka kabisa kwamba hapa Ilala tutashinda kwa kishindo, mnastahili kupata pongezi kutoka makao makuu kutokana na mlivyoendesha kampeni, hongereni sana.". alisema Nape.

Alisema, pamoja na CCM kuwa na uhakika wa kushinda lakini itafanya kazi ya ziada ya kuhakikisha wapigakura waliojiandikisha wanapata fursa ya kwenda kupiga kura bila kubughudhiwa na watu ambao huandaliwa na vyama vya upinzani kufanya fujo ili kuzuia watu wasijitokeze kupiga kura.

"Nasema bila kificho, vijana wa CCM kama mtamuona mtu yeyote anajaribu kufanya fujo wakati wa upigaji kura mshughulikieni kidogo kabla ya kumpeleka polisi, maana watu wa aina hii wanabaka demokrasia, lazima waadabishwe". alisema Nape na kuongeza.

"Vijana wa CCM lazima tuwe shupavu, maana kujifanya wanyonge unyonge huu hautatusaidia chochote, na hili mimi sihamasishi fujo na si wa kwanza kulisema hata Mwenyekiti wetu wa CCM alishasema kwamba unyonge basi. Sasa mimi hapa napigilia msumari tu".

Nape aliwataka wananchi wa Ilala na Watanzania kwa jumla kuchagua wagombea wa CCM, kwa kuwa ana uhakika ndio watakao watumikia vizuri.

Aliwataka viongozi watakaochaguliwa katika uchaguzi huo wa serikali za mitaa kuhakikisha wanawatumikia wananchi, hasa kwa kusimamia kuondoa kero zao na kusimamia misingi ya kuboresha mazingira ya shughuli mbalimbali zikiwemo za biashara kama za mamalishe na machinga.

Nape alisema, CCM, itaendelea kusimamia na kutetea haki za wananchi hasa walio wanyonge na si kwa sababu ya kutaka kura ila kwa sababu ni wajibu wake kama chama kilichopewa ridhaa ya kutawala nchi.

Katika mkutano huo, Nape aliwanadi wagombea wa nafasi mbalimbali katika Mtaa huo wa Mtambani B, akiwemo mgombea wa nafsi ya Ueneyekiti wa mtaa huo, Gungu Tambaza.
...Sasa endelea na picha zaidi za mkutano huoNape akimkaribisha jukwaani Gungu Mohamed Tambaza, mgombea wa Uenyekiti mtaa wa Mtambani B ili kuomba kura kwa niaba ya wagombea wenzake wa jimbo la Ilala wakati wa mkutano huo wa kufunga kampeni za serikali za mitaa uliofanyika leo kwenye makutano ya mtaa wa Kongo na Faru.Nape akimsikiliza Gungu Mohamed Tambaza akiomba kuraKada wa CCM Khamis Mkotya akimpongeza Nape wakati wa mkutano huoNape akimpongeza Haji ManaraMkotya na ZunguMkotya na makada wengine wa CCM wakifuatiliaShamrashamra uwanjani baada ya mkutano.


  • Tumeshirikishwa taarifa hii na  Bashir Nkoromo / TheNkoromo Blog

Study says: Men are idiots who do stupid things

Abstract

Sex differences in risk seeking behaviour, emergency hospital admissions, and mortality are well documented. However, little is known about sex differences in idiotic risk taking behaviour. This paper reviews the data on winners of the Darwin Award over a 20 year period (1995-2014). Winners of the Darwin Award must eliminate themselves from the gene pool in such an idiotic manner that their action ensures one less idiot will survive. This paper reports a marked sex difference in Darwin Award winners: males are significantly more likely to receive the award than females (P<0.0001). We discuss some of the reasons for this difference.
Figure1
Male and female Darwin Award winners. Line H0 indicates expected percentages under the null hypothesis that males and females are equally idiotic


Vodacom wins "Employer Of the Year Award" again!

2014 Employer Of the Year


Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakifurahia ushindi wa tuzo ya mwajiri bora 2014 iliyotolewa na chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) baada ya kuyashinda makampuni mbalimbali yaliyoshindanishwa kuwania tuzo hizo katika hafla ilifanyika jijini Dar es Salaam, kampuni hiyo ilishinda tuzo mbalimbali katika Nyanja tofauti kwa mwaka wa pili mfululizo

Dar es Salaam December 12, 2014: The Association of Tanzania Employers (ATE) has declared Vodacom Tanzania Limited the Employer of the Year for the second year in a row.

The Right Honourable Prime Minister Mizengo Pinda was the Guest of Honour at this year’s ATE Employer Of the Year Award Presentation ceremony which was held at the Mlimani City Conference Centre in Dar es Salaam on December 11, 2014.

“This is the second time in a row that we have won this accolade and is a clear indication of the work that we continue to put in to make Vodacom a great place to work, ” 
says Vodacom Tanzania’s Managing Director Rene Meza.

Vodacom Tanzania also emerged top in the following categories: Performance Management Process, Leadership and Governance, Human Resource Policy and Practice, Workforce Focus and Quality and Productivity of Employees.

Meza goes on to say that Vodacom was truly honoured by the ATE recognition and that Vodacom Tanzania's win this year was a clear demonstration of his company’s commitment to ensuring that it remained at the forefront of furthering best business practices in the country.

“These awards serve as an incentive to us to continue to invest in our people, our systems, the community and our network because what we do has a tremendous impact within and without Vodacom. The mobile phone has transcended the traditional use of just making and receiving calls. Today, you can access your finances from your palm, watch TV, listen to the radio and so much more because of the services that we offer,” 
he says.

Our employees who are the key drivers of all our initiatives remain central to all that we do and that is why we continue to go from strength to strength, says Meza.

Last month Vodacom was also declared the second largest contributor to government revenue and the top taxpayer in the telecoms sector at the 2014 National Compliant Tax Payer Award ceremony that was held at the Julius Nyerere International Conference Centre.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda (wapili toka kulia)akimkabidhi kombe la Mwajiri bora 2014 Ofisa Mkuu wa Idara ya rasilimali watu wa Vodacom Tanzania Dr.Fredy Mwita(watatu toka kushoto) waliloshinda toka chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) baada ya kuyashinda makampuni mbalimbali yaliyoshindanishwa kuwania tuzo hizo katika hafla ilifanyika jijini Dar es Salaam.Kampuni hiyo ilishinda tuzo mbalimbali katika Nyanja tofauti,Wengine katika picha kulia ni Mwenyekiti wa chama hicho Almasi Maige na wafanyakazi wa kampuni hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakifurahia ushindi wa tuzo ya mwajiri bora 2014 iliyotolewa na chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) baada ya kuyashinda makampuni mbalimbali yaliyoshindanishwa kuwania tuzo hizo katika hafla ilifanyika jijini Dar es Salaam, kampuni hiyo ilishinda tuzo mbalimbali katika Nyanja tofauti kwa mwaka wa pili mfululizo

Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(katikati)akijadili jambo na wafanyakazi wenzake Simon Martin(kushoto)na Gloria Mtui(kulia)wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo za mwajiri bora 2014 zinazotolewa na chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) ambapo kampuni hiyo iliyashinda makampuni mbalimbali yaliyoshindanishwa kuwania tuzo hizo, kampuni hiyo ilishinda tuzo mbalimbali katika Nyanja tofauti kwa mwaka wa pili mfululizo.Hafla hiyo ilifanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakipata picha ya kumbukumbu na kombe lao baada ya kutwaa ushindi wa tuzo ya mwajiri bora 2014 iliyotolewa na chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) baada ya kuyashinda makampuni mbalimbali yaliyoshindanishwa kuwania tuzo hizo katika hafla ilifanyika jijini Dar es Salaam, kampuni hiyo ilishinda tuzo mbalimbali katika Nyanja tofauti kwa mwaka wa pili mfululizo


Wateja wa TTCL kununua salio kupitia ‘Mobile Banking’

Kutoka kulia ni Meneja Mipango na Mauzo wa TTCL, Benjamin Bizere, Mkuu wa Mauzo wa TTCL, William Chamla, Ofisa Habari wa TTCL, Edwin Mashasi wakizungumza na wanahabari (hawapo pichani) juu ya uzinduzi wa huduma ya kuongeza salio kwa wateja wa TTCL kupitia simu za mkononi 'Mobile Banking'.

KAMPUNI ya Simu nchini Tanzania (TTCL) sasa imerahisisha upatikanaji wa vocha zake baada ya kuingia makubaliano kuishirikiano na benki 13 nchini zinazotoa huduma zake pia kwa kupitia simu za mkononi (Mobile Banking) ambapo sasa mteja wa TTCL ataweza kuongeza salio kupitia simu yake ya mkononi (TTCL top-up).

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Meneja Mipango na Mauzo wa TTCL, Benjamin Bizere alisema huduma hiyo ya kununua salio kwa njia ya simu kupitia mabenki 13 imeanza kufanya kazi hivi sasa hivyo mteja wa TTCL anaweza kununua salio lake popote alipo kwa kutumia simu yake.

Alisema TTCL imeingia makubaliano ya kiushirikiano katika uuzaji wa muda wa maongezi kwa benki za Standard Chartered, Akiba Commercial (ACB), Tanzania Postal Bank (TPB), Exim Bank, Dar Es Salaam Community Bank (DCB), Mkombozi Bank, KCB Bank pamoja na Bank of Africa ambazo wateja wa beki hizo wanaweza kununua salio kupitia simu zao popote walipo kwenye akaunti zao.

“…Jumla ya benki 13 zimeingia ubia wa kibiashara na TTCL kwa ajili ya kuuza vocha za TTCL kupitia benki zao…hapo juu nimetaja majina ya benki zote ambazo zinatumika kwa ajili ya kufanya miamala mbalimbali ikiwemo TTCL TOP-UP,” alisema Bw. Bizere.

Akifafanua zaidi juu ya huduma hiyo Mkuu wa Mauzo wa TTCL, William Chamla alisema huduma ya TTCL TOP-UP na Mobile banking ni njia ambayo TTCL imeanzisha kwa wateja wake kwa ajili ya kuongeza salio la muda wa maongezi kwa simu za mezani, mkononi na kununua vifurushi vya intaneti hivyo mteja ataweza kununua salio lake muda wowote na popote.

“…Mteja atakayenufaika na huduma hii ni yule mwenye akaunti ya benki, na amejisajili katika huduma ya kibenki kupitia simu ya mkononi yaani 'mobile banking'”.

 Hata hivyo alisema ili kuwarahisishia upatikanaji wa huduma kwa wateja wa wao vocha za TTCL pia zinapatikana katika vituo vya Maxmalipo na Selcom ‘wireless Point’ na kwenye Ofisi za TTCL, pamoja na vituo vya huduma kwa wateja ambako viko katika kila mkoa na wilaya.

Tabasamu la kupata maji kwa juhudi za Mbunge

Furaha ya kupata maji 
Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe akinywa maji kwa majani ya miti baada ya kuzindua mradi wa maji na kukabidhi vifaa vya kuvuta maji vyenye thamani ya zaidi ya Tsh milioni 14.5 kwa wakazi wa kitongoji cha Dodoma kijiji cha Amani Ludewa 

WANANCHI wa kitongoji cha Dodoma kijiji cha Amani wilaya ya Ludewa mkoani Njombe kuondokana na kero ya maji safi na salama baada ya mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe kuwatimizia ahadi yake ya vifaa vyenye thamani ya zaidi ya Tsh milioni 14. 5 kwa ajili ya kuvuta na kusambaza maji safi na salama ya bomba katika kitongoji hicho .

Akishukuru kwa niaba ya wananchi wengine wakati wa hafla ya kukabidhiwa vifaa hivyo jana Bi Belinada Mwenda alisema kuwa awali wananchi wapatoa zaidi ya 600 wa kitongoji hicho ambacho kimeanzishwa na jamii ya wachimbaji wa madini ya dhahabu ,walikuwa wakitumia maji machafu yanayotumika kuoshea madini na kunyweshea mifuko .

Hivyo alisema kuwa msaada huo wa maji safi na salama utasaidia kuwaepusha na magonjwa na milipuko kama kuhara na mengine ambayo walikuwa wakiyapata kutokana na matumizi ya maji yasiyo salama kwa afya ya binadamu kwa kipindi chote cha zaidi ya miaka 10 sasa toka kitongoji hicho kilipoanzishwa mwaka 1992.

" Hakika tunakushukuru sana mbunge wetu kwa kutusaidia msaada wa vifaa hivi kwa ajili ya maji .....toka mwaka 1992 hadi leo tumekuwa tukiteseka kwa magonjwa mbali mbali na hata baadhi yetu kupoteza maisha kutokana na matumizi ya maji machafu ambayo tulikuwa tukitumia maji ambacho kimsingi yalikuwa ni mabaki ya maji yanayobaki katika kunyweshea mifugo na kuoshea madini"

Bi Mwenda alisema wananchi hao mbali ya kero kubwa ya maji ambayo walikuwa wakiipata ila bado walionyesha uaminifu kwa mbunge wao kwa kuendelea kubaki ndani ya CCM hadi sasa wanapotimiziwa ahadi yao hiyo kwa kitongoji hicho kuwa ni moja kati ya vitongoji vyenye msimamo na mbunge wao kwa kutoviunga mkono vyama vya upinzani .


" Kwa shida tuliyokuwa tukiipata kama maeneo mengine leo wote tungekuwa tumejiunga na upinzani ila tuliamini chama pekee ambacho kinaweza kutusaidia na CCM na ndio sababu hatukuona sababu ya kujiunga na vyama vya upinzani .....mheshimiwa mbunge wetu tunakuhakikishia kuwa kitongoji hiki hakuna hata mwananchi mmoja ambae ni upinzani na wala hatuna mpango wa kuhangaika na vyama sisi tutabanana hapa hapa CCM"

Akizungumza na wananchi hao mbunge Bw Filikunjombe pamoja na kuwapongeza kwa kutojiunga na vyama vya upinzani bado alisema kuwa ameguswa kutimiza ahadi yake kwa wakati kutokana na mateso makubwa ambayo wananchi hao walikuwa wakiyapata kwa kukosa huduma ya maji safi na salama.

Kwani alisema kuwa lengo la serikali ya CCM iliyopo madakarani chini ya Rais Dr Jakaya Kikwete ni kuona watanzania wanaendelea kuboreshewa mazingira ya maisha yao na hata kupunguza baadhi ya kero zinazoweza kupunguzw kwa wakati uliopo na ndio sababu ya yeye kama mbunge pia kuendelea kukimbiza kasi ya maendeleo ya jimbo hilo la Ludewa na kamwe hatakubali kuona wananchi wake wakiendelea kuteseka.

"Ndungu zangu wananchi wa kitongoji hiki cha Dodoma katika kijiji hiki cha Amani nimewapenda sana na ninyi wenyewe mnatambua kuwa mimi mbunge wenu nawapenda ..... hivyo msaada huo leo ni utekelezaji wa ahadi yangu niliyoitoka miezi michache iliyopita nikiwa kama mbunge wenu japo siku nilipotoa ahadi hii baadhi yenu hamkuweza kuamini kama leo ingetekelezwa ...nawaombeni sasa tunzeni vema vifaa hivi na kutunza zaidi mazingira ili kufanya chanzo cha maji kuendelea kuwa hai zaidi "

Mbunge Filikunjombe alivitaja vifaa ambavyo amevitoa ni pamoja na bomba za maji ambazo zitasambazwa katika kitongoji chote kutoka kwenye chanzo cha maji zaidi ya kilometa 20 hadi kwenye kitongoji hicho .

Kuhusu wafugaji wanaochungia mifugo katika chanzo cha maji mbunge huyo aliwataka wananchi na viongozi hao kuweka sheria ya kulinda chanzo hicho cha maji vinginevyo hakutakuwa na maana ya kuwa na bomba za maji safi ambazo zitaingiliwa na mifugo.


Mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe akisoma maandishi mara baada ya kuzindua mradi wa maji kitongoji cha Dodoma kijiji cha Amani
Mbunge Filikunjombea akifurahia utamu wa maji


Mbunge Filikunjombe kushoto akifurahia utamu wa majiFilikunjombe akitengeneza matawi ya miti kuwa chombo cha asili cha kuchotea maji


Mbunge wa Filikunjombe na viongozi wa kitongoji cha Dodoma kijiji cha Amani wakipanda mlima mkali pindi walipotoka kutazama chanzo cha maji


Upandaji wa mlima kutoka kwenye chanzo cha maji ulivyomtesa mbunge Filikunjombe


Mbunge Filikunjombe akijiandaa kuruka korongo


Wananchi wa kitongoji cha Dodoma wakifurahia majiWanawake wa kitongoji cha Dodoma kijiji cha Amani wakiwa wamemkumbatia mbunge wao Filikunjombe kwa furaha baada ya kutimiza ahadi ya maji


Mbunge Filikunjombe (mwenye shati la kijani, kulia) akikabidhi baadhi ya vifaa vya maji kwa wananchi wa kitongoji cha Dodoma Ludewa

Wananchi akifurahia vifaa hivyo


Baadhi ya vifaa hivyo


Mbunge Filikunjombe akiwahutubia wananchi hao kwa furaha.Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe akiwahutubia wananchi wa kitongoji cha Dodoma kijiji cha Amani wilayani Ludewa baada ya kukabidhi vifaa vya maji vyenye thamani ya zaidi ya Tsh milioni 14.5 jana huku mmoja kati ya wanawake wa kijiji hicho akiwa amelala miguuni mwake kama sehemu ya kushukuru kwa msaada huoWananchi wakifurahia wakati mbunge Filikunjombe akiwahutubia


Mkazi wa kitongoji cha Dodoma Bi Belinada Mwenda akimshukuru mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe kwa msaada wa maji 


Wananchi wa kitongoji cha Dodoma kijiji cha Amani Ludewa wakimzawadia zawadi ya mkungu wa ndizi mbunge wao Deo Filikunjombe baada ya kuwasaidia msaada wa vifaa vya maji vyenye thamani ya Tsh milioni 14.5

  • Taarifa hii tumeshirikishwa na Francis Godwin/Matukio Daima blog (shukurani)