Another prominent trader in Moshi shoots himself to death

A prominent Moshi businessman, Mr Augustino Felex Mallya (40), a resident of Katanini Karanga in Moshi Municipality, Kilimanjaro Region has reportedly committed suicide at his home, his family has said.

Mr Mallya shot himself by using his personal gun of Browning make with registration numbers T 96,682 which was found with four bullets in the living room of his home on Tuesday evening.

Describing the incident, the wife of the deceased, Mrs Elizabeth Augustino (32), said that she found her husband dead after hearing a gunshot from the living room of their house while she was in the bedroom and when she rushed to the living she found her husband dead with a gunshot wound to the chest.

She said that the late Mallya was suffering from stomach pains for a long time and was sent to India for further treatment after being treated in different hospitals in the country without any success.

"A few days before the incident he was complaining of severe abdominal pains that he was tired of and he could no longer take it.

I did not think then that he would take his own life because he was expected to go back to India on December 12," she said.

Kilimanjaro Regional Police Commander, Mr Godfrey Kamwela confirmed the incident, adding that the deceased was living with his wife and four children at the same house.

It should also be noted that on May 27, a prominent businessman Werasimba Lema (74), resident of Msasani Mailisita in Moshi Municipality shot himself after being diagnosed with throat cancer.

Haya! Baada ya maelfu kuitwa Uwanja wa Taifa, safari hii maelfu tena waitwa Diamond Jubilee kwenye usaili TRA


Vijana takriban elfu kumi kutoka kila pembe ya nchi juzi walimiminika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam kusailiwa katika nafasi mbalimbali za ajira katika Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Vijana hao ambao wengi ni wale waliomaliza vyuo mwaka huu na miaka ya hivi karibuni, walifika ukumbini hapo tangu saa kumi na mbili asubuhi na hadi muda wa saa 9:00 mchana bado walikuwa hawajaingia ndani kufanya usaili huo kutokana na wingi wao.

Usaili huo ulisimamiwa na watumishi wa Chuo Kikuu cha Tumaini kampasi ya Mwenge jijini Dar es Salaam.Baadhi ya wasailiwa walilalamikia utaratibu unaotumika kwani ni wa mateso dhidi yao kwa kuwa walikalishwa kwa muda mrefu:

"Ukweli hapa ni mateso. Ndiyo tupo wengi tunaoatafuta ajira lakini kinachofanyika hapa ni kutesana na njaa na jua kali maana kila upande watu wamejaa na hata matumaini hadi sasa ya kufanya usaili huo ni mdogo," alisema mmoja wa vijana.


Hivi ndivyo ilivyokuwa hali halisi katika ukumbi wa Diamond Jubilee ambapo vijana wengi wasaka ajira walijazana kusaka nafasi za ajira za TRA.


[video] Jinsi ya kufunga zawadi bila kutumia boksi / How to wrap a gift without using a box

Mahitaji/What you will need
  • Zawadi /A gift
  • Karatasi ya kufungia zawadi / A wrapping paper
  • A tape
Kisha fuata maelekezo yaliyomo kwenye video iliyopachikwa hapo chini / Then follow instructions in the video embedded below...

Ufafanuzi kuhusu Wanajeshi kushiriki kuboresha Daftari la Kupiga Kura

TUME ya Taifa ya Uchaguzi-NEC, imetoa ufafanuzi zaidi kuhusu ushiriki wa Wanajeshi katika uboreshaji wa zoezi la Uandikishaji wa Daftari la Kudumu la Kupiga Kura, linalotarajiwa kuanza kwa majaribio Jumatatu ijayo, katika Majimbo Matatu nchini.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Tume, kutakuwepo na Wanajeshi Sita wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania, JWTZ, ambao kazi yao itakuwa ni kusaidia shughuli za Lojistiki kama vile kuhamisha Vifaa kutoka Kata Moja kwenda nyingine.

Pia Wanajeshi hao watasaidia katika shughuli za kufanya matengenezo Madogo Madogo ya Vifaa yanayoweza kujitokeza wakati wa zoezi la uandikishaji.

Taarifa inasisitiza kuwa Wanajeshi hao hawatakuwepo kwenye vituo vya Uboreshaji wala hawatahusika na zoezi la uandikishaji kama baadhi ya vyombo vya habari vilivyoripoiti hivi karibuni.

Aidha, katika mkutano na Vyama vya Siasa uliofanyika juzi jijini Dar es Salaam ulifafanua kuwa watendaji watakaohusika katika zoezi hilo ni maafisa Waandikishaji na wasaidizi wao, Waandishi Wasaidizi, Wataalamu wa fani ya TEHAMA na wataalamu kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Picha za arusi ya Meshack Maganga na Rose AmbaliKashfa, Uchaguzi Mkuu vyachochea thamani ya TZS kuendelea kushuka

Picha via ZanziNews blog

Hatua ya wahisani kuzuia Sh1 trilioni za misaada ya kibajeti kwa Serikali kutokana na kashfa ya IPTL na wasiwasi wa Uchaguzi Mkuu mwakani, ni miongoni mwa sababu za kuporomoka kwa kasi thamani ya Shilingi nchini, imefahamika.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wiki iliyopita, wasomi na wadau wa biashara nchini walisema sababu nyingine ni uagizaji na uuzaji bidhaa nje ya nchi.

Kwa mujibu wa takwimu za Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Januari 2, mwaka huu, Dola moja ya Marekani ilikuwa ikiuzwa kwa Sh1,586 lakini sasa imepanda hadi Sh1,745. Ikumbukwe kuwa katikati ya mwaka huu, Dola moja ilikuwa ikinunuliwa kwa hadi Sh1,800 katika baadhi ya benki na maduka ya kubadilishia fedha, jambo lililoongeza gharama za ufanyaji biashara na kuongeza bei ya bidhaa.

"Escrow"

Hivi karibuni, wahisani walitangaza kusimamisha misaada hadi Serikali itakapopitia ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuhusu sakata la Akaunti ya Tegeta Escrow na kuchukua hatua.

Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Dk Prosper Ngowi alisema hatua iliyochukuliwa na nchi wahisani ya kuzuia fedha za misaada hiyo ambazo zingeingia katika mzunguko wa fedha, imesababisha upungufu wa Dola katika soko la fedha, hivyo kuongezeka thamani.

Alisema iwapo fedha hizo zingekuwa kwenye mzunguko, zingesaidia kupunguza uhaba wa Dola uliopo ambao umesababisha kuuzwa kwa bei kubwa na hivyo kuchangia kupandisha thamani ya Shilingi.

“Hata kitendo cha Tanzania kuuza bidhaa chache nje ya nchi kimechangia mahitaji ya Dola kuongezeka kutokana na uhaba wa fedha hizo hapa nchini,” alisema Dk Ngowi akitaja sababu nyingine ya kuporomoka kwa Shilingi.

Hoja ya Dk Ngowi iliungwa mkono na Meneja wa Fedha wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Mshindo Ibrahim akisema kuzuiwa kwa fedha hizo za hisani, kumechangia kupaisha thamani ya Dola, licha ya kuwapo tatizo la kuuza bidhaa kidogo nje ya nchi.

“Sisi ni waagizaji wakubwa wa bidhaa kuliko kuuza nje, tunajikuta tunapata Dola kidogo kuliko mahitaji jambo linaloiongeza thamani yake, lakini hili la wahisani kushikilia fedha za bajeti kutokana na sakata la IPTL ni moja ya sababu kubwa kwa sasa,” alisema Ibrahim.

Iwapo wahisani ambao hutoa fedha zao kwa sarafu za kigeni wataziachia, mtaalamu huyo alisema zitasaidia kupunguza wingi wa Shilingi kwa kuwa Dola hizo zinatakiwa kubadilishwa kwa sarafu ya ndani ili zianze kutumika.

Alisema kuna wakati hali hiyo ni kawaida kibiashara.

Uchaguzi Mkuu


Katika hatua nyingine, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Dhamana na Uwekezaji ya Zan Securities, Raphael Masumbuko alisema safari hii Shilingi imeshuka thamani kwa kasi isiyo ya kawaida tofauti na miaka ya nyuma, jambo ambalo linaweza kuchangiwa na homa ya uchaguzi.

“Huenda imetokea kwa sababu tunaelekea katika kipindi cha uchaguzi. Katika kipindi kama hiki, wawekezaji wengi kutoka nje huwa wanahifadhi fedha zao katika Dola ili kujiokoa na hasara iwapo utatokea mfumuko wa bei wakati wa mchakato wa uchaguzi,” alisema Masumbuko.


Alisema Shilingi pia imeshuka thamani kutokana na Dola kutumika mno katika sekta ya nyumba na msimu huu ni wa kulipa kodi, hivyo Dola inahitajika zaidi kuliko Shilingi.

“Nyumba nyingi siku hizi zinakodishwa kwa Dola wanaita ‘mita ya mraba kwa Dola’ hadi majumba yanayomilikiwa na mifuko ya hifadhi za jamii… sasa kwa hali hii usitegemee Shilingi itapanda thamani,” alisema Masumbuko.

Hata hivyo, alisema hali hii haitakiwi kutia hofu Watanzania kwa kuwa inaweza kutengamaa baada ya msimu wa baridi kuanza Ulaya ambako watalii wengi watakuja na kuleta fedha za kigeni, pia juzi, BoT imeuza dhamana zitakazoipunguza Shilingi sokoni.

Mkuu wa Kitivo cha Biashara cha Chuo Kikuu cha Tumaini Dar es Salaam, Deogratius Massawe alisema kuongezeka kwa bidhaa mbalimbali nchini zinazonunuliwa kwa Dola pia kumechangia thamani ya fedha hiyo kuongezeka huku Shilingi ikishuka.

Massawe alisema mfumo huo unawalazimisha Watanzania kununua bidhaa hizo kwa bei ya juu zaidi tofauti na ile inayouzwa kwa Shilingi.

“Hata hivyo, ipo sheria inayomzuia mtu kumlazimisha mwingine kununua kitu chochote kwa Dola, ila mteja anaweza kununua bidhaa kwa Dola iwapo wamekubaliana na muuzaji.”

Profesa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Benjamin Mutagwaba alisema sera makini ndizo zinazoweza kuinusuru thamani ya Shilingi ya nchi hii.

“Kama kutakuwa na usimamizi mzuri, kilimo pekee kinaweza kuleta mapinduzi katika biashara na kubadili thamani ya kubadili fedha. Kama mazao yote yataongezwa thamani kabla hayajauzwa nje, nchi itapata fedha nyingi… unaweza ukaona hata madini tunayasafirisha yakiwa hayajaongezwa thamani, jambo ambalo si zuri kwa mustakabali wetu kiuchumi kama nchi,” alisema Profesa Mutagwaba.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya ukaguzi wa hesabu ya KPMG, David Gachewa alisema hakuna njia ya mkato wa kuifanya Shilingi iwe na thamani kama si kuongeza uuzaji wa bidhaa nje ya nchi.

“Miaka 10 iliyopita thamani ya Dola moja ya Marekani ilikuwa Sh800 lakini leo hii ni Sh1,700 na bado tunaagiza bidhaa zilezile kwa sarafu hiyo. Hii inamaanisha kuwa gharama za bidhaa hizo zimeongezeka na mwananchi ndiye anayelipia. Hali hii itaendelea kama hakutakuwa na mabadiliko ya kiuchumi ili kuongeza uuzaji wa bidhaa nje ya nchi,” alisema Gachewa na kuongeza:

“Nadhani mafuta na gesi yatakapoanza kuzalishwa hapa nchini na kusafirishwa kwenda nje itasaidia kwa kiasi kwa kuwa Serikali itaokoa fedha zilizokuwa zinatumika kuagiza nishati hizo, pia kuna fedha zitakazoingia kutokana na mauzo ya bidhaa hizo.”

Kauli ya Waziri

Akijibu swali la Cecilia Pareso (CHADEMA - Viti Maalumu) wiki iliyopita bungeni, kuhusu kuongezeka kwa matumizi ya fedha za kigeni nchini, Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima alisema linapunguza ufanisi wa sera za fedha na uwezo wa BoT kutimiza wajibu wake kuwa mkopeshaji wa mwisho katika uchumi.

Malima aliongeza kuwa endapo wananchi watalazimika kutumia fedha za kigeni, jambo hilo pia linaweza kuwa kero kwao kwa kuwasababishia usumbufu.

Hata hivyo, Malima alisema kiwango cha matumizi ya Dola nchini hakijafikia kiasi cha kuwa na madhara hayo.

Alisema uwiano wa amana za fedha za kigeni na ujazo wa fedha, ambao uliwahi kupanda hadi kufikia asilimia 34 mwaka 2003, kwa sasa umeshuka mpaka kufikia asilimia 27.2 mwaka 2013.

Alisema mwaka 2007, Serikali ilitoa tamko rasmi kuhusu matumizi ya fedha za kigeni katika kulipia huduma na bidhaa katika soko la ndani kuwa Mtanzania yeyote asilazimishwe kulipia huduma au bidhaa yoyote kwa fedha za kigeni.

Baada ya agizo hilo, Malima alisema fedha za kigeni zinazotunzwa na BoT ziliongezeka kutoka Dola 228.3 milioni mwaka 1993 sawa na asilimia sita ya Pato la Taifa hadi Dola 4 bilioni sawa na asilimia 14 ya Pato la Taifa mwaka 2012.

Kafulila atambulisha kuwa Anna ni mchumba wa Zitto

Ndnai ya Kanisa siku ya arusi ya Kafulila

HATIMAYE kitendawili cha nani atakuwa mwandani wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto kabwe kimeteguliwa kufuatia mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila kuutangazia umma juu ya jambo hilo.

Kafulila alitumbua jipu hilo wakati akitoa utambulisho wa wageni waliofika kwenye tafrija ya harusi yake iliyofanyika kwenye ukumbi wa Annex mji Mdogo wa Uvinza wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma.

Katika utambulisho huo Kafulila alimtambulisha Anna kuwa ni mchumba wa Zitto na muda si mrefu mambo yatakuwa hadharani.

Kafulila alisema kuwa licha ya kuwa mchumba wa ZITTO pia ni mtumishi wa Ubalozi wa Ireland hapa nchini.

Harusi hiyo pia ilihudhuriwa na Mbunge David Silinde na Deo Filikunjombe na mkewe (wapambe wa maharusi) na Dk. Kitila Mkumbo.

Utambulisho huo wa mchumba wa Zitto unavunja ukimya wa Mbunge huyo kuwa na mahusiano na Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA) Mkoa wa Kigoma, Muhonga Ruhwanya na Mtangazaji wa Clouds FM, Loveness Malinzi (Diva The Boss).

Kwenye burudani wakati wa arusiMstaafu CAG kutuzwa; Aagwa rasmi na Ikulu

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Mstaafu, Bw. Ludovick Utouh (kulia), na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu mpya wa Hesabu za Serikali, Profesa Mussa Juma Assad (kushoto), katika hafla ya kumpongeza na kumuaga Bw. Utouh iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro jijini Dar es Salaam,11 Desemba, 2014.

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue, juzi tarehe 11 Desemba 2014, alimuaga rasmi Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Mstaafu Bw. Ludovick Utouh, katika hafla maalum iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jijini Dar es Salaam.

Hafla hiyo ambayo ilihudhuriwa na baadhi ya Watendaji Wakuu na Waandamizi kutoka Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali ilikuwa mahsusi pia kumkaribisha Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu mpya wa Hesabu za Serikali, Profesa Mussa Juma Assad.

Katika hotuba yake ya kumpongeza Bw. Utouh, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Sefue, alielezea historia ya Utumishi uliotukuka ya Bw. Utouh ambayo imeleta sifa kubwa Ofisi hiyo ndani na nje ya nchi na katika medani za kimataifa. Kwa ujumla, hotuba ya Katibu Mkuu Kiongozi ilijikita kuelezea mchango binafsi wa Bwana Utouh kwa taifa ndani ya miaka zaidi ya arobaini (40) ya Utumishi wake Serikalini.

Aidha, Katibu Mkuu Kiongozi alielezea mafanikio ya Serikali kwenye eneo la utawala bora, uwajibikaji na uzingatiaji wa sheria, kanuni na taratibu za fedha za umma ambayo yamechangiwa na Bw. Utouh. Balozi Sefue aliwasihi watumishi wa umma kuiga weledi, uaminifu, msimamo, bidii na maarifa ambayo Bw. Utouh alivionyesha kwa vitendo katika utumishi wake.

Katibu Mkuu Kiongozi alitumia fursa hiyo pia, kumtakia kila la kheri, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali mpya, Profesa Juma Assad, katika kufanikisha majukumu aliyopewa.
Bwana Utouh alistaafu rasmi nafasi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, tarehe 19 Septemba, 2014 baada ya kuitumikia nafasi hiyo kwa miaka saba na miezi kumi tangu alipoteuliwa na Rais, tarehe 19 Agosti, 2006

Nayo taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya “Dream Success Enterprises” imeandaa dhifa ya kumtunuku tuzo maluum aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Bw. Ludovick Utouh.

Hayo yasemwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo Bw. Charles Makoba katika taarifa yake aliyoitoa jana kwa vyombo vya habari, ambapo alisema dhifa hiyo inatarajia kufanyika Desemba 22, mwaka 2014 kwenye ukumbi wa Nyumba ya Utamaduni, Makumbusho ya Taifa kuanzia saa 8:00 mchana hadi saa 12:00 jioni.

Alisema lengo kuu la dhifa ni kumpongeza Bw. Utouh kwa kulitumikia taifa kwa uadilifu mkubwa na kuweza kufichua watu wanaotumia madaraka yao kufanya matumizi mabaya ya pesa za umma.

Makoba alisema mgeni rasmi katika dhifa hiyo aliyekuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Makampuni (BRELA) Bw.Eusteriano Mahingila.

“Utendaji mzuri wa Bw.Utouh umeliletea taifa heshima kubwa duniani na hata kupelekea kuteuliwa kwake kuwa Mjumbe wa Bodi ya Ukaguzi wa Umoja wa Mataifa(United Nations Board of Audit(UNBoA) nafasi hii ilikuwa ikishindaniwa na nchi zote duniani hivyo ushindani wake ulikuwa mkubwa,”alisema Bw. Makoba.

Aidha Makoba aliongeza kuwa uteuzi wa Bw.Utouh kuwa mmoja wa wajumbe wa bodi ya UNBoA kuna pelekea Tanzania kuweka historia ya kimataifa,ya kuwa ya tatu kutoka Afrika kwa kuwa na mjumbe wa bodi hiyo tangu ilipoanzishwa,nchi nyingine kutoka Afrika ambazo zimeshawahi kuwa na wajumbe katika bodi hiyo ni Ghana na Afrika kusini.

“Bw.Utouh ni miongoni mwa viongozi wa kitaifa waliotunukiwa Nishani ya Utumishi wa Umma uliotukuka na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Jakaya Kikwete mwaka 2012 katika sherehe za miaka 51 ya Uhuru.Nishani hiyo ilikuwa ni matokeo ya kazi nzuri alikuwa akifanya kama Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali”, alisema.

Bodi ya UNBoA ina majukumu mbalimbali ikiwemo Ukaguzi wa Hesabu za Makao Makuu ya Umoja wa Kimataifa (UN),Mashirika Asasi zote zilizo chini ya UN ambazo ni Misheni za Ulizi Amani za Umoja wa Mataifa,Miradi mbalimbali inayosimamiwa na UN ,hesabu za Mahakama ya Kimataifa ya makosa ya Jinai zikiwamo za mauaji ya kimbari za Rwanda na Yugoslavia.

Chikawe azindua “Wait to Send” ya Vodacom

Waziri Chikawe (watatu kutoka kulia) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kampeni ya usalama barabarani uliofanyika eneo la Mwenge makutano ya barabara ya Sam Nujoma na Ali Hassan Mwinyi jijini Dar es Salaam, uzinduzi huo uliambatana na upimaji wa kiwango cha pombe mwilini kwa madereva na ugawaji wa pete maalumu za kuwakumbusha madereva kuacha kutumia simu za mkononi wanapokuwa wanaendesha vyombo vya moto, wanaoshuhudia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Kamanda Mohammed Mpinga, Mwenyekiti wa usalama barabarani wilaya ya Kinondoni Hua Tluway (wa pili kushoto) na Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani Hamza Kassongo na Henry Bantu.
Waziri Chikawe (watatu kutoka kulia) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kampeni ya usalama barabarani uliofanyika eneo la Mwenge makutano ya barabara ya Sam Nujoma na Ali Hassan Mwinyi jijini Dar es Salaam, uzinduzi huo uliambatana na upimaji wa kiwango cha pombe mwilini kwa madereva na ugawaji wa pete maalumu za kuwakumbusha madereva kuacha kutumia simu za mkononi wanapokuwa wanaendesha vyombo vya moto, wanaoshuhudia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Kamanda Mohammed Mpinga, Mwenyekiti wa usalama barabarani wilaya ya Kinondoni Hua Tluway (wa pili kushoto) na Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani Hamza Kassongo na Henry Bantu.

Madereva nchini wametakiwa kuzingatia sheria za barabarani,kutotumia vinywaji vyenye ulevi na kuacha tabia ya kuongea na simu au kutuma na kupokea ujumbe wa maneno (sms) wanapokuwa wanaendesha vyombo vya moto.

Wito huo umetolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani,Mheshimiwa Mathias Chikawe, katika kampeni ya uhamasishaji wa usalama barabarani iliyozinduliwa leo na serikali kupitia Jeshi la polisi,Baraza la Taifa la Usalama barabarani na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania eneo la Mwenge jijini Dar es Salaam ambapo pia alishiriki katika zoezi la kuwagawia madereva pete maalum za kuwakumbusha kutotumia simu za mkononi wanapokuwa wanaendesha magari na pikipiki.

Alisema madereva wakizingatia sheria za barabarani kwa kiasi kikubwa ajali zinazoendelea kutokea kila siku zitapungua hususani katika kipindi hiki kuelekea sikukuu ya Krismas na mwaka mpya na aliipongeza Vodacom Tanzania kwa kuunga mkono jitihada za serikali katika kupambana na tatizo hili ambalo limekuwa sugu .

Naye Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani cha Jeshi la Polisi,Kamanda Mohamed Mpinga amesema kampeni hii ni muhimu katika kupunguza matukio ya ajali “Watumiaji wa barabara hususani madereva wa vyombo vya moto hawana budi kuzingatia maelekezo ambayo tumekuwa tukiwapa katika kampeni hizi ili tupate matokeo mazuri kwa kupunguza ajali kama ilivyokusudiwa”Alisema

Kwa upande wake,Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na uhusiano wa Umma wa Vodacom,Rosalynn Mworia, alisema Vodacom itaendelea kushirikiana na serikali kuunga mkono jitihada za kuondoa matatizo kwenye jamii kama lilivyo tatizo hili la ajali ili kuhakikisha wananchi wanaishi maisha murua na marefu.”Tunaomba madereva kufuata sheria za barabarani kwa usalama wenu,usalama wa abiria mnaowabeba na watumiaji wengine wa barabara".

Aliongeza kuwa Vodacom itakuwa mstari wa mbele kuelimisha jamii athari za kuendesha gari wakati huo huo unatumia simu ya mkononi kupitia kampeni ya "Wait to Send" pia itaendelea kuhamasisha madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani.Mbali na kampeni hii alisema kwa mwaka huu kampuni ilidhamini Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani.

Alisema kabla ya uzinduzi wa kampeni ya leo tayari umefanyika uhamasishaji wa madereva kuzingatia sheria za barabarani katika miji ya Dar es Salaam,Mwanza na kampeni itaendelea kufanyika sehemu mbalimbali nchini.

Katika uzinduzi huu wafanyakazi wa Vodacom kwa kushirikiana na askari wa usalama barabarani walitoa uhamasishaji wa madereva kuacha kuongea na simu wanapoendesha vyombo vya moto pia zoezi la kupima madereva kubaini kama wanatumia vilevi lilifanyika.

Ufafanuzi wa Wizara kuhusu habari ya Raia Mwema ya kuuzwa hisa za TanzaniteOne


Walionunua hisa za TanzaniteOne wafahamika


via Raia Mwema

MMOJA wa wafanyabiashara maarufu mjini Arusha, mtoto wa kiongozi wa juu wa serikali na vigogo wa Wizara ya Nishati na Madini wanadaiwa kuwa nyuma ya ununuzi wa asilimia 50 za hisa za kampuni ya Richland Resources katika kampuni ya TanzaniteOne inayochimba madini ya Tanzanite katika machimbo ya Mererani wilayani Simanjiro.

Katika toleo la wiki iliyopita, gazeti hili liliripoti kuwa kampuni ya Richland Resources imeuza “kinyemela” asilimia 50 za hisa zake katika kampuni ya TanzaniteOne ambayo inachimba madini hayo huko Mererani.

Kampuni ya TanzaniteOne inamiliki kwa ubia na Shirika la Madini la Taifa (Stamico) migodi ya madini hayo tangu mwaka 2012 katika eneo la kitalu C kama sehemu ya kutekeleza sheria ya madini ya mwaka 2010 inayoelekeza kuwa madini yote ya vito yatachimbwa na wazawa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, imeuza hisa zake asilimia 50 Oktoba 31 mwaka huu kwa kampuni inayotajwa kuwa ni Sky Associates kwa dola za Kimarekani 5,100,000 sawa shilingi bilioni 8.8 za Kitanzania.

Ushiriki wa vigogo:

Taarifa zilizopatikana wiki hii kutoka miji ya Arusha na Dar es Salaam zimebainisha kuwa pamoja na kutajwa kwa kampuni ya Sky Associetes kama mnunuzi wa hisa hizo, mpango wa kuzinunua ulisukwa mjini Arusha na moja wafanyabiashara maarufu wa Kitanzania (jina linahifadhiwa kwa sasa).

Mfanyabiashara huyo anatajwa kuwa na uhusiano wa karibu sana na mmoja wa watoto wa vigogo wa serikali nchini (jina linahifadhiwa) ambaye anaelezwa kuwa atakuwa mshirika kibiashara kuendesha migodi hiyo pale serikali itakaporidhia uuzwaji wa hisa hizo.

“Kimsingi huyo mfanyabiashara na mtoto wa kiongozi wa juu wa serikali ni watu wa kati (madalali) katika biashara hiyo, na wamepewa asilimia kati ya 5-10 ya hisa katika kampuni ya Sky Associetes ili kutumia nafasi zao kulinda maslahi ya kampuni hiyo hapa nchini”alieleza mtoa taarifa wetu ambaye ni mtumishi katika Wizara ya Nishati na Madini.

Kwa mujibu chanzo chetu, hisa hizo zimenunuliwa kwa mamilioni ya Dola za Kimarekani tofauti na kiwango kinachotajwa na kampuni ya Richland ya dola milioni 5.1 (sawa na bilioni 8.8 za Kitanzania) kwa lengo la kukwepa tozo za kodi za serikali.

Anaongeza:”Kwa mujibu wa vyanzo vyetu hapa wizarani, biashara tayari imefanyika na katika makubaliano hayo Sky Assocites ndiyo watakaoshughulikia mchakato wa serikali na Stamico kuridhia uuzwaji wa hisa za TanzanieOne”.

Alieleza kuwa hatua hiyo ya serikali kuridhia ndiyo “ngumu” katika mchakato huo na hapo Richland na Sky wameonelea kumtumia mtoto huyo wa kigogo pamoja na mfanyabiashara na maofisa wengine wa wizara (ambao kwasasa majina yao yanahifadhiwa).

Kwa mujibu wa taarifa hizo, kampuni Sky inamilikiwa na mfanyabiashara maarufu wa madini ya vito nchini India aliyefahamika kwa jina la Rizwan Ullah.

Hata hivyo taarifa binafsi za mfanyabiashara huyo na kampuni yake hazikuweza kupatikana mara moja.

Wadau wapinga:

Mwenyekiti wa Chama Cha Wachimbaji Madini Mkoa wa Manyara (MAREMA) Sadick Mneney alieleza kusikitishwakwake na hatua ya kuuzwa kwa hisa hizo kwa kampuni ya nje.

“Kama TanzaniteOne wamefanya hivyo basi hawajawatendea haki Watanzania fedha wanazodai kuuza hisa ni fedha ambazo Watanzania wengi wanazimiliki na ingekuwa fursa nzuri ya madini hayo kuchimbwa na wazawa kama sheria inavyoelekeza”alisema.

Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa hali hiyo pia inachangiwa zaidi na “ukiritimba” uliokithiri katika Wizara ya Nishati na Madini ambayo viongozi wake hatoi fursa za kiuwezeshaji kwa wazawa katika sekta hiyo.

“Hivi karibu Waziri anayesimamia Wizara hiyo alitoa kauli kuwa Watanzania hawana fedha za kuwekeza katika gesi na mafuta, fedha zao ni za Juisi (maji ya matunda) labda TanzaniteOne wamezingatia kauli ya Waziri kuwa hakuna Mtanzania mwenye Dola za Kimarekani milioni tano,”alisema.

Akizungumza na Raia Mwema wiki hii Mwenyekiti wa Chama Cha Wauzaji Madini (Master Dealers- TAMIDA) Sammy Mollel alisema uuzwaji huo wa hisa za TanzaniteOne ni muendelezo wa kuwachezea “akili” Watanzania kuhusu uwekezaji wa kampuni hiyo.

“TanzaniteOne kwa zaidi ya miaka 15 imekuwa katika mgogoro mkubwa na wachimbaji wadogo, katika kipindi cha mwaka huu wachimbaji wamepeleka malalamiko yao kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini na malalamiko hayo bado hajapatiwa ufumbuzi,”alisema.

Mollel aliongeza:”Sasa jiulize kwanza wameingia ubia na Stamico katika kipindi cha miaka miwili wameuza hisa, tena kabla hata mgogoro uliopo haujamuliwa na serikali, ni wazi kuwa hapa Watanzania tunaendelea kuchezewa akili tu”.

Aliongeza kuwa kama kulikuwa na nia njema ya kuuza hisa hizo, Richland wangetangaza kwa uwazi na Watanzania wangejitokeza kuzinunua kwa kuwa hata bei ya kuuzwa si fedha ambazo wachimbaji wengi wanazimiliki au wana mali zenye thamani hiyo.

Mollel alitahadharisha kuwa uuzwaji wa hisa hizo unaweza kugeuka kuwa moja kashfa kubwa nchini katika sekta ya madini na kutoa wito kwa viongozi wa Wizara ya Nishati na Madini kuchunguza kwanza suala hilo kabla ya kutoa idhini ya kuendelea na uchimbaji.

Kati ya malalamiko yaliyowasilishwa kwa Pinda na Wachimbaji wadogo katika barua yao ya Mei 19 mwaka huu ni kulalamikia uhalali wa leseni ya uchimbaji ya TanzaniteOne.

Katika barua hiyo kwa Pinda, wachimbaji hao walilalamika kuwa TanzaniteOne walipewa leseni mpya Julai 6 mwaka 2012 ikiwa ni siku tatu kabla ya leseni ya awali kuisha muda wake jambo ambalo ni uvunjaji wa sheria za nchi.

“Leseni ya awali ya TanzaniteOne ilikuwa inamaliza muda wake tarehe 9/7/2012 leseni ikatolewa 6/7/2012 siku tatu kabla ya muda wa leseni ya awali kuisha jambo ambalo ni kosa kisheria,”ilisomeka barua hiyo.

Aidha wachimbaji hao wanafafanua kuwa kwa mujibu wa Sheria ya Madini ya mwaka 2010 kifungu cha 8 (3) leseni ya madini ya vito inatakiwa kutolewa kwa Watanzania tu lakini kama kuna ulazima wa kushirikiana na wageni kwa lengo la kutumia teknolojia utaalamu na uwekezaji mkubwa, waziri mhusika na anaweza kuruhusu ubia kati ya Mtanzania na mwekezaji wa nje.

Wanaeleza kuwa kwa maana hiyo , kuna utata wa kisheria kwa suala la TanzaniteOne kuingia ubia na shirika la madini la Taifa (STAMICO), ambalo ni shirika la serikali linaloendeshwa kwa fedha za umma kupitia bajeti ya serikali.

“Kwa maana hiyo, fedha za umma zinaweza kuingizwa kwenye uwekezaji wa kibiashara je nani atafanya maamuzi kuhusu fedha hizi? Nani atazikagua? Kimsingi serikali haipaswi kulipa kodi na mrabaha, je mkataba huu unasemaje kuhusu wajibu wa STAMICO juu hili?” wanahoji.

Pia wanahoji TanzaniteOne kumegewa eneo kubwa la uchimbaji kinyume na Sheria ya Madini ya mwaka 2010 kifungu cha 5 (1) kinachoeleza kuwa leseni ya madini ya ujenzi au vito ukubwa wa eneo unatakiwa usizidi eneo la kilomita za mraba moja ambapo TanzaniteOne wanamiliki eneo la kilomita za mraba 7.6.

Taarifa zinaeleza kuwa wakati mgogoro huo ukiendelea, Mbunge wa Simanjiro, Christopher ole Sendeka, alikuwa anaandaa hoja binafsi ya kuipeleka bungeni kuhusu matatizo ya muda mrefu katika machimbo hayo ya Mererani.

Sendeka mwishoni mwa wiki aliimbia Raia Mwema kwa njia ya simu amechoshwa sana na migogoro isiyoisha katika eneo hilo na asingeweza kuzungumzia suala la kuuzwa kwa hisa za TanzaniteOne bila kupata taarifa sahihi za kiserikali.

“Ndugu yangu mambo ya Mererani yanachosha sana, migogoro baina ya huyo mwekezaji na wachimbaji wazawa imezorotesha shughuli za uchimbaji, naomba nisubiri taarifa rasmi za kimaandishi kuuhusu uuzwaji wa hisa hizo ndipo niweze kutoa maoni yangu”alisema.

Madini ya Tanzanite yanapatikana katika eneo hilo pekee duniani na pamoja na kuwa kati ya vito vyenye thamani kubwa, Tanzania kama nchi haijanufaika ipasavyo na takwimu zinaoonyesha kuwa nchi za Kenya na India ndiyo zinaongoza kwa kusafirisha na kuuza katika soko la dunia.

Kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Nishati na Madini mwaka jana, Tanzania haikufikia hata nusu ya Kenya kwa mauzo ya madini hayo ya vito.

Kenya ilisafirisha na kuuza nje ya nchi Tanzanite yenye thamani ya zaidi ya Dola 100 milioni za Marekani (Sh173 bilioni) dhidi ya Dola 38 milioni (Sh45.5 bilioni) zilizouzwa na Tanzania.

Katika kipindi hicho cha mwaka jana, India iliuza tanzanite zenye thamani ya zaidi ya Dola za Marekani 300 milioni (Sh509 bilioni) kiasi cha baadhi ya wanunuzi wakubwa, hasa kutoka Marekani kujiuliza iwapo madini hayo yanachimbwa nchini humo.

Juhudi za Raia Mwema kuwapata Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo na Naibu wake Steven Maselle kuzungumzia suala hilo hazikuweza kufanikiwa mwishoni mwa wiki.


----------------


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA 

WIZARA YA NISHATI NA MADINI

TAARIFA KWA UMMA

Ufafanuzi Kuhusu Kuuzwa kwa Hisa za Kampuni ya TanzaniteOne.

Gazeti la Raia Mwema la Desemba 10, 2014 liliandika habari iliyodai kwamba mmoja wa Wafanyabishara maarufu wa mjini Arusha alishirikiana na mtoto wa kiongozi wa juu wa Serikali na vigogo wa Wizara ya Nishati na Madini kufanikisha uuzwaji wa asilimia 50 ya hisa za Kampuni ya Richland Resources katika Kampuni ya TanzaniteOne inayochimba madini ya Tanzanite katika eneo la Merelani Wilayani Simanjiro.

Aidha, taarifa hiyo ilidai kuwa licha ya hisa hizo kuuzwa kwa mamilioni ya Dola, Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya TanzaniteOne ametoa taarifa kuwa hisa hizo zimeuzwa kwa kiwango cha Dola za Kimarekani 5.1milioni (sawa na shilingi bilioni 8.8 za Kitanzania) ili kukwepa kodi. Vilevile, taarifa hiyo imeeleza kuwa Wizara ina ukiritimba wa kuwawezesha watanzania kumiliki rasilimali na kwamba leseni ya TanzaniteOne ilitolewa kimakosa na hivyo si halali.

Wizara inapenda kutoa maelezo yafuatayo kuhusu hoja zilizotolewa:

Suala la Uuzaji wa Hisa za TanzaniteOne

Kampuni ya TanzaniteOne imeijulisha Wizara kuhusu kusudio la kuuza hisa zake asilimia 50 kwa Kampuni ya Sky Associate Group Limited. Kampuni ya TanzaniteOne haijaomba rasmi Wizara iridhie uuzaji wa hisa zinazokusudiwa kuuzwa. Mara Kampuni hiyo itakapowasilisha taarifa kamili za kuuza hisa zake ikiambatana na maombi ya kupata ridhaa ya kuhamisha umiliki wa hisa hizo kwa Kampuni ya Sky Associates Group Limited, Wizara itafanya uchunguzi wa kina na kuona kama utaratibu umefuatwa wakati wa kuuza hisa hizo.

Uhalali wa Leseni ya TanzaniteOne/STAMICO
Kampuni ya TanzaniteOne imekuwa ikimiliki leseni ya uchimbaji mkubwa wa madini-Special Mining Licence (SML 8/92) kwa asilimia 100 katika eneo la Kitalu C Merelani iliyotolewa mwaka 1992. Leseni hiyo ilikuwa inafikia ukomo wake tarehe 9 Julai, 2012. Tarehe 25 Januari, 2011 Kampuni ya TanzaniteOne iliwasilisha ombi la kuhuisha leseni hiyo kwa lengo la kuendelea kuchimba madini katika eneo hilo la Kitalu C.

Wizara ilielekeza Kampuni ya TanzaniteOne irekebishe ombi la tarehe 25 Januari 2011 kwa mujibu wa Kifungu cha 116 cha Sheria ya Madini ya Mwaka 2010. Kifungu hicho kinaruhusu kufanyika marekebisho mbalimbali kwa ajili ya kuwezesha leseni zilizotolewa chini ya Sheria ya Madini ya Mwaka 1998 kuhamia kwenye Sheria ya Madini ya Mwaka 2010. Marekebisho kama hayo yamefanywa kwa maombi ya leseni za utafutaji mkubwa wa awali wa madini (PLR) na leseni za uchimbaji madini ya vito (GML) ambazo hazitolewi tena chini ya Sheria ya Madini ya Mwaka 2010.

kwa kuwa Kampuni ya TanzaniteOne ilikwishamilikishwa leseni katika eneo hilo kwa mujibu wa Sheria ya Madini ya Mwaka 1998, uhuishaji wa leseni Na. SML/8/92 na marekebisho yaliyofanyika haukufanywa kwa mujibu wa Kifungu cha 8 cha Sheria ya Madini ya Mwaka 2010, bali chini ya kifungu cha 116 kama ilivyoelezwa awali.

Kwa kuwa maombi ya Kampuni ya TanzaniteOne yalishughulikiwa katika mazingira ya kufanya marekebisho (modification) ya leseni kutoka Sheria ya Madini ya Mwaka 1998 kwenda katika Sheria ya Madini ya Mwaka 2010, leseni mpya (ML 490/2013 )ilitolewa kwa ajili ya uchimbaji wa madini ya Tanzanite, tsavorite, graphite na madini mengine yanayoweza kupatikana. Leseni hiyo ina ukubwa wa kilomita za mraba 7.6. Kihistoria uchimbaji katika kitalu C umekuwa ukihusisha madini hayo yaliyoainishwa katika leseni hiyo.

Katika miaka ya 1970, TGI walijihusisha zaidi na uchimbaji wa madini ya vito. Baadaye miaka ya 1990, Kampuni ya Graphtan Ltd ilijihusisha zaidi na uchimbaji wa graphite katika eneo la kitalu C, huku madini ya vito (Tanzanite) yakiwa ni by-product.

Kwa kuzingatia matakwa ya Sera ya Madini ya Mwaka 2009 yanayohusu ushiriki wa Serikali kimkakati katika miradi ya madini, Serikali ilifanya majadiliano na Kampuni ya TanzaniteOne yaliyowezesha STAMICO kumiliki asilimia 50 ya hisa katika mgodi huo wa Tanzanite. Kutokana na makubaliano hayo Kampuni ya TanzaniteOne ilifanyia marekebisho ombi lake la leseni ya uchimbaji madini na kuingiza STAMICO ambayo inamiliki asilimia 50 katika leseni ya uchimbaji madini eneo la Kitalu C.

Uwezeshaji wa Wazawa katika Sekta ya Madini

Katika taarifa ya gazeti hilo la Raia Mwema ilidaiwa kuwa Wizara ya Nishati na Madini ina ukiritimba uliokithiri na viongozi wake hawatoi fursa kiuwezeshaji kwa wazawa katika sekta ya madini.

Madai hayo ni kupotosha ukweli kwamba Wizara imepiga hatua kubwa katika urasimishaji leseni kwa watanzania na katika uwezeshaji wa wachimbaji wadogo. Hadi sasa kati ya leseni za madini zipatazo 45,000, Watanzania wanamiliki asilimia 75 ya leseni zote, na wageni wanamiliki asilimia 25. Aidha, katika kipindi cha kuanzia mwaka 2011/12 hadi sasa Wizara imetenga maeneo 33 kwa ajili ya uchimbaji mdogo; pamoja na kutenga takriban shilingi bilioni 8 kwa ajili ya uwezeshaji wa wachimbaji wadogo kupitia Benki ya Maendeleo ya TIB.

Imetolewa na,

WIZARA YA NISHATI NA MADINI

11 Desemba, 2014

Tanzania yasaini mkataba wa bil 15.5/- za ADB kwa ajili ya MUHAS

anzania yasaini mkataba wa Sh. bilioni 15.5 kutoka benki ya ADB kuboresha kituo cha utafiti MUHAS.
Katibu Mkuu Wizara ya fedha Bw. Servacius Likwelile (kushoto) akikisaini Mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) kwa ajili ya kuboresha kituo cha utafiti wa magonjwa ya moyo kinachosimamiwa na Chuo Kuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Muwakilishi wa Benki ya ADB nchini Tonia Kandiero akisaini mkataba huo kwa niaba ya Rais wa benki hiyo Dkt. Donald Kaberuka.
Katibu Mkuu Wizara ya fedha Bw. Servacius Likwelile (kushoto) akikisaini Mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) kwa ajili ya kuboresha kituo cha utafiti wa magonjwa ya moyo kinachosimamiwa na Chuo Kuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Muwakilishi wa Benki ya ADB nchini Tonia Kandiero akisaini mkataba huo kwa niaba ya Rais wa benki hiyo Dkt. Donald Kaberuka.

Eleuteri Mangi

Serikali ya Tanzania imetiliana saini mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 9.4 ambazo ni sawa na Sh. Bilioni 15.5 kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) kwa ajili ya kuboresha kituo cha utafiti wa magonjwa ya moyo kinachosimamiwa na Chuo Kuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).

Mkataba huo wa makubaliano umesainiwa leo jijini Dara es salaam na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Muwakilishi wa Benki ya ADB nchini Tonia Kandiero kwa niaba ya Rais wa benki hiyo Dkt. Donald Kaberuka.

Dkt. Likwelile alisema kuwa kituo hicho kitasaidia kupunguza tatizo la wataalam wa afya nchini na nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na hivyo kupunguza idadi kubwa ya wagonjwa wanaotibiwa nje ya nchi.

Kwa upande wake Muwakilishi wa Benki ya ADB nchini Tonia Kandiero ameipongeza Tanzania kuwa nchi ya kwanza kusaini mkataba huo kati ya nchi nne za jumuiya ya EAC zinazokusudiwa kujenga kituo kama hicho.

Bi Tonia alisema kuwa benki ya ADB imejiwekea lengo kuboresha rasilimali watu katika fani ya afya ambapo mradi wa ujenzi wa kituo kinachojengwa MUHAS upo katika mkakati wa benki hiyo ambao uulianza 2011 hadi 2015, mpango mkakati wa benki wa 2013 hadi 2017 na mfumo mpya wa elimu katka nchi za Afrika.

Mfumo huo unalenga kutatua tatizo la utaalaam katika soko la ajira kwa kupitia vituo bora vya kanda vya afya ili kuendana na dira ya maendeleo ya Taifa na mkakati wa kupunguza umasikini ifikapo mwaka 2025.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Donan Mbando ameushukuru uongozi wa benki ya ADB kwa kuendelea kushirikiana na Tanzania na kuahidi fedha hizo zitatumiwa kwa malengo yaliyokusudiwa.

Hadi kukamilika kwa kituo hicho cha afya kinachojengwa katika chuo cha MUHAS kitagharimiwa na benki ya ADB kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania.

Gari la Malocha lavunjwa viooGari la mbunge wa jimbo la Kwela, Ignas Malocha ambalo limevunjwa vioo na wafuasi wanaosadikiwa kuwa wa vyama vya upinzani katika kijiji cha Kapenta jioni ya tarehe 12 /12/2014.

Mbunge huyo alikuwa akitokea kijiji cha Kaoze aliposhiriki mkutano wa kampeni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa za CCM kabla ya kundi la vijana kutanda barabarani kisha kuanza kutoa lugha chafu. Baada ya kuona hivyo, dereva aligeuza gari huku mawe yakirushwa ambayo alivunja vioo hivyo.

Badala ya 'chopa' CHADEMA watumia 'mkokoteni'

Wananchi wakiwa wamembeba kwenye toroli Mgombea wa Uwenyekiti wa Mtaa wa Tambuka Reli Mabula Ndoshi mara baada ya kumaliza Mkutano wake wa kampeni kwenye viwanja vya mtaahuo jana.
(picha: Valence Robert via Malunde1 blog)

Gari la Lema lavunjwa kioo; Afyatua risasi 3

Gari la Godbless Lema lililovunjwa kioo huko Clock Tower, Arusha (picha: wazalendo25)


Wi-Fi ya bure kwenye kituo cha 'daladala' Sinza yazinduliwaManispaa ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam, imedhihirisha jitihada zake za kwenda na wakati katika huduma zake, baada ya kuamua kutoa huduma ya bure ya mtandao wa intrenet wa WiFi kwenye Kituo kipya cha Mabasi cha Sinza, jijini Dar es Salaam.

Akizindua huduma hiyo, jana, Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yussuf Mwenda alisema, mtandao wa WiFi umeunganishwa kwenye kituo hicho kupitia mkongo wa mawasiliano kupitia Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL).

Mwenda alisema, mtandao huo utakuwepo usiku na mchana na kila mwenye kompyuta au simu zenye uwezo wa kunasa Wi-Fi ataona katika simu au kompyuta yake akitaarifiwa kuwepo mtandao wa bure wa KMC_FREE WiFi.

Alisema, mdau atakachofanya ni kujinga bure na kuendelea kupata taarifa mbalimbali zikiwemo za tovuti ya serikali na ya Manispaa hiyo ya Kinondoni na nyingine zote atakazotaka.

Mwenda alisema, baada ya kuweka mtandao kwenye Kituo hicho, mwakani Manispaa hiyo itaweka mtandao huo wa WiFi kwenye Kata zote 34 za Manispaa hiyo.

Alisema, mradi huo wa WiFi umegharimu sh. milioni 21, na Manispaa hiyo itakuwa ikiendelea kulipia huduma hiyo sh. milioni 2 kila mwezi ambazo itakuwa inalipa kwa mkupuo kwa mwaka.

Kuzinduliwa kwa huduma hiyo, kumeifanya Manispaa ya Kinondoni kuwa ya kwanza nchini kote, na pengine hata Afrika Mashiriki, kutoa huduma hiyo bure tena bila kutumia namba ya siri.

Mwandishi wa habari hii alishuhudia huduma ya aina hii kwa mara ya kwanza alipotembelea nchini China, ambapo WiFi inapatikana bure kwenye simu hata ukiwa barabarani.Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yussuf Mwenda akibofya kompyuta kuzindua huduma ya WiFi ya bure kwenye Kituo cha Mabasi cha Sinza, wilayani humo, Ijumaa, Desemba 12, 2014Mwenda akikata utepe kwenye chumba ilimo mitambo ya kuendesha mtandao huo wa huduma ya WiFi kwenye Ofisi za Kituo hicho cha mabasi
Kweli: "WiFi ya Manispaa ya Kinondoni inapatikana bure!" vijana wakisema baada ya kuipata WiFi iliyozinduliwa kwenye Kituo hicho cha Mabasi Vibao vinavyoonyesha Mabasi yaendeko kutoka kwenye Kituo hicho

  • wavuti.com imeshirikishwa taarifa hii na Bashir Nkoromo / Nkoromo Blog

C. Chachage "Mtwara or Lindi: Oil and Gas in Rival Port Cities"

Mtwara is booming and buzzing. It was not like this seven years ago when I first saw the town. Why such a dramatic change? The answer seemed to be crystal clear: oil and gas.

Even the richest man in Africa, hailing from an oil producing country, is also frequently visiting Mtwara. He is constructing a cement plant named after him – Dangote Industries (Tanzania) Limited. No wonder roads are being paved and hotels are getting upgraded.

As my childhood friend, who moved there, has aptly put it in the title of his blog, Mtwara Kumekucha. But, surprisingly, I hardly saw any significant change at the old port. Why?

Sitting at the famous Bandari Club, itself a far cry from the glory of its good olden days, I lazily watched its workers play Baoand wondered what is happening. I then asked one of them if Mtwara has already started to benefit from gas discovery and oil prospecting.

His answer was brief: “No, not yet.” What about all the changes that we are seeing, I kept enquiring. He didn’t seem amused. Then, disturbingly, he suddenly gave me an elaborate explanation: “We cannot really tell until oil is found!” And constructing a port, I quipped.

For him my question deserved a contextual analysis. He started explaining how far the place where they were prospecting for oil is – somewhere near Mozambique and the Comoros. By way of triangulating, I vaguely recalled, in my mental map coupled with its faulty memory, an exploration activity map from the Tanzania Petroleum Development Corporation (TPDC) that I had seen before and found his premise sound. “So,” he argued, “they may find it reasonable to locate a port somewhere closer, i.e., not Mtwara!”

Lindi came up as a potential port. I mentioned Kilwa. But he affirmed that even that is in Lindi. Another worker mentioned another site in Mtwara yet no one knew where exactly the new port would be constructed. Interestingly, later on someone who had encountered some oil prospectors alleged that there is an agreement among them on where to build it.

Two months down the line that conversation lingers in my head. Then I stumble on the writings of a visitor who observed these places on the eve and dawn of independence in 1961. In her colonial travelogue on Tanganyika: Sail in the Wilderness, with a foreword by none other than Mwalimu Julius Nyerere, Kathleen Stahl tells a tale of two rival ports.

The tale is so telling that it needs to be cited in length: “The whole artificiality of the situation began when the decision was taken in London by the British Government in 1947 to make Mtwara the groundnut port instead of Lindi. Ten years later the Tanganyika government was still enmeshed in the consequences of that decision, and the two ports were like rival characters in a little drama not yet played out...As for the choice of the port, Lindi offered many advantages. It was already an established seaport; it was the provincial headquarters with all administrative services, and it had the main road through the province starting in the port”. After all what was to be shipped grew therein.

Stahl expounded: “The conflict between Lindi and Mtwara was not at once apparent for the simple reason that while Mtwara was the designated port, Lindi did the actual traffic. The only road running out Mtwara was the 70 miles of bad winding coastal road to Lindi. Thus, even supposing that it had been practicable to import through Mtwara all the vast tonnage of equipment needed for the Nachingwea scheme all that could have then been done was to send it up by road to Lindi and then 100 miles inland to the groundnut area.”

“Moreover,” she noted, “owing to the nature of the ground the new railway from Mtwara to Nachingwea could not be built as quickly, by a margin of two years, as a railway from the head of Lindi creek to Nachingwea. All the vast quantities of equipment and stores imported for the groundnut scheme then went to Lindi…. It was a boom town as never before in its history.” Karim Hirji who grew up there during that time also attests to this.

In his recent memoir on Growing Up with Tanzania: Memories, Musings and Maths, he thus recalls and analyzes what Aga Khan III, who had visited Lindi in 1946, had advised Ismailis: “The advice to set up shop in the south likely had the nod of the British rulers who were instituting a massive groundnuts production scheme in central and southern Tanzania. It came with an influx of colonial officials, company employees and their families. The Asians were to be the middlemen for the European firms, and were as well expected to establish the service infrastructure for colonial rule, thereby enabling the European way of life to operate without too many glitches.” By 1957 they totaled 1,800.

Hirji concludes: “The poorly conceived schemed failed in a matter of years. The bulk of the European left, but the Asians stayed behind. Groundnuts or not, their presence was vital for the import-export structure to take root, expand geographically and flourish financially.” As such they experienced the rivalry between Lindi and Mtwara port towns.

When the schemed failed by 1951 what it left, as Stahl noted, were “the port of Lindi and the new railways from it, both in actual working, and at Mtwara half a port and half a railway.” Hence “a decision had to be made whether to carry on with Mtwara or to give it up and leave Lindi as the port for the Southern Province.” Interestingly, “Mtwara won and it was resolved to complete the port and railway on their original scale as planned.”

For Stahl, what followed after “was a case of killing Lindi to give life to Mtwara. Every device was used to induce the trade of Lindi to go over to Mtwara.” According to her, the “search” had “been for ways and means to persuade the old-established thriving Asian commercial community at Lindi to transplant itself and forsake the bright lights of the town, the only bright lights in the province, and all its civil amenities, schools, hospitals, cinema, sports club and telephone system, for the [then] virgin marshy bush of Mtwara.”

To that end, she noted, in “1953 provincial headquarters were removed from Lindi to Mtwara where a large new building had been put up to house them.” The “failure of this gesture to arouse any response”, Stahl conjectured, “may be regarded as disproving the old adage that trade follows the flag.” Nevertheless, in “1954 the railway from Lindi to Nachingwea was pulled up.” That “same year”, as Stahl noted, “saw a grand opening of Mtwara port and the railway connecting it with Nachingwea…. By the end of the year it became apparent that losses would be greater than expected on both the railway and the port since the actual tonnages available were far less than had been imagined. The railway services were [then] cut down to achieve economies and differential port rates were introduced in order to make it cheaper for ships to use Mtwara rather than Lindi.”

Then, Stahl thus concluded: “Finally in 1955 it was decided that it was unnecessary to have two ports for the Southern Province and that Lindi must go. As the coup de grace, the drastic decision was taken to remove all lighterage and port facilities from Lindi.” It is a decision that made her curious mind wonder whether it “would give life to Mtwara.”

Her ‘iffy’ take on what might have happen thus remains relevant to us today, notwithstanding their colonial clouding: “Had Mtwara never been invented, Lindi would still be a booming port and the provincial headquarters might be moving, not to Mtwara, but inland to Masasi, poised to push the development of the [then] province farther west.”

The Southern Question in Tanzania that tends to pit Dar es Salaam against Mtwara when it comes to oil and gas remains unresolved. However, in our quest to resolve it let us not forget what we can term ‘the Southern Question within the Southern Question’, i.e., that of the role of Lindi vis-à-vis Mtwara port city in relation to oil and gas.

  • Article by Chambi Chachage via his blog, Udadisi