Tanzania, Zambia, Kenya sign $1.2 billion MOU for power

THE Governments of Zambia, Kenya and Tanzania yesterday signed a power inter connector memorandum of understanding (MOU) project worth USD 1.2 Billion.

Mines, Energy and Water development Minister Christopher Yaluma said the agreement signed yesterday would set out principles that underlined the relationship amongst the three governments of Zambia, Kenya and Tanzania.

Speaking in Livingstone yesterday during the signing ceremony, Mr Yaluma re affirmed the commitment of the Zambian government to the realization of the Zambia-Kenya-Tanzania power interconnector project which would link the Eastern African Power Pool (EAPP) to the Southern African Power Pool (SAPP).

Mr Yaluma said once completed, the project would promote electricity trade, enhance security of electricity supply and foster regional trade.

He further noted that the project which is expected to start in December next year and expected to be completed in December 2018, would also stimulate investment in power generation to meet the increased demand from the large market that would be created by interconnecting the two sub regions.

My Yaluma however said the three countries could not fully realize the project in the absence of financial support from development partners and asked for more support.

“However, the three countries cannot fully realize the project in the absence of financial support from the development partners and other financing institutions. Therefore, I wish to appeal to our development partners to support the project by providing the required financial support,” Mr Yaluma said.

And Tanzania Minister of Energy and Minerals Professor Sospeter Muhongo said what was happening now in Africa was a fulfillment of what the continents forefathers wanted.

Professor Muhongo said Africa was still faced with a number of challenges in the education sector, infrastructure development andfinances among others.

He said one key challenge was electricity which was a major factor to development.

Professor Muhongo said 50 percent of Africa’s population lived in rural areas and had no access to electricity.

“We need an investment of between 300 to 500 billion dollars as a region to meet some of these challenges. We want by 2030, both rural and urban Africa must have access to electricity,” Professor Muhongo said.

Some of the developing partners to the project which witnessed the signing ceremony included the European Union (EU), COMESA, the Norwegian Fund and World Bank.

Others were African Development Bank and China Developmentbank including some other financial institutions.

Boti yazama ziwa Tanganyika na kuua watu 129

At least 129 people have drowned after a boat capsized on Thursday night on Lake Tanganyika in the southeast of Democratic Republic of Congo, according to a new official death toll, the AFP news agency said.

"Rescue workers recovered a total of 129 bodies," an official told AFP.

On Saturday, the provincial government said at least 26 people had died after the boat packed with passengers and goods capsized.

The vessel, which was travelling north from Kalemie in Katanga province to Uvira in South Kivu province, sank in the early hours of Friday, survivors speaking by telephone from Katanga's capital Lubumbashi said.

Deadly shipwrecks are frequent on the lakes and rivers of DRC, where boats are often overloaded, life jackets frequently missing and many people cannot swim.

Lake Tanganyika is the longest freshwater lake in the world and also borders Tanzania, as well as Burundi and Zambia.

CECAFA yafutilia mbali michuano ya mwaka 2014


Baraza la soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) limetangaza kuwa, michuano ya mwaka huu baina ya timu za taifa imefutiliwa mbali.

Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicholas Musonye amesema kuwa michuano ya mwaka huu imefutuliwa mbali baada ya kukosekana na mwenyeji wa michuano hiyo kuchukua nafasi ya Ethiopia iliyojiondoa katika dakika za lala salama.

Uaumuzi huo ulifikiwa mwishoni mwa juma lililopita baada ya kikao cha viongozi wa soka kutoka eneo la Afrika Mashariki na Kati uliofanyika jijini Nairobi nchini Kenya.

Musonye ameongeza kuwa, mipango itafanyika ili kubadilisha mfumo wa michuano hiyo ili kuvutia zaidi katika siku zijazo.

Rwanda itakuwa mwenyeji wa michuano hiyo mwaka ujao wa 2015. Mabingwa watetezi ni Kenya walionyakua taji hilo mwaka uliopita wakati michuano hiyo ilipoandaliwa jijini Nairobi.

Mbali na hilo, viongozi wa CECAFA wameamua kwa kauli moja kuwa watamuunga mkono rais wa sasa wa FIFA Sepp Blatter mwenye umri wa miaka 78 kuwania tena urais wa Shirikisho hilo kwa muhula wa Tano mwaka ujao.

Mvutano wa Winnie na wasimamizi wa mali za Mandela

Winnie Mandela (picha: DailyMail.co.uk)

Winnie Mandela, aliye kuwa mke wa rais wa zamani wa Afrika Kusini, hayati Nelson Mandela "Madiba", amekataliwa kurithi mali ya aliyekuwa mumewe huyo, kama walivyobainisha wanaohusika na kugawa mirathi wa rais huyo wa zamani wa Afrika Kusini.

Kwa kipindi cha miezi miwili, Winnie Mandela, amekuwa akijaribu kupata miliki ya makazi ya Nelson Mandela katika kijiji kidogo cha Qunu, bila mafanikio.

Watu hao wanaohusika na kugawa mirathi ya Nelson Mandela, wamebaini kwamba watapinga kwa vyovyote vile ombi la Winnie Mandela la kutaka apate umiliki wa makazi hayo.

Winnie Mandela, aliishi na Mandela katika ndoa kwa kipindi cha miaka 38, lakini hakuwekwa kwenye orodha ya watu wanaopaswa kupewa mirathi ya rais huyo. Winnie Mandela, anadhani kuwa makazi ya Qunu ni milki yake, kwani Mandela aliipata wakiwa pamoja katika ndoa.

Hata hivyo wanaohusika na kugawa mirathi ya Nelson Mandela wamesisitiza kuwa makazi ya Qunu ni milki ya mke wa tatu wa Madiba, Graça Machel na kwamba jaribio lolote la marekebisho ya maandiko ya Madiba ni kinyume na kauli yake. Licha ya kukosolewa, Winnie Mandela ameendelea kuonesha kuwa yeye ndiye mwenye haki ya kumiliki mali ya Mandela, hususan makazi yake ya Qunu.

Winnie amefungua mashitaka kwenye Mahakama Kuu ya Mthatha, nchini Afrika Kusini. Amekosoa vikali ni kwa nini Mandela alimpa Graça makazi ya Qunu wakati ambapo ana nusu ya uraia wa Msumbiji.


Wanafunzi 130 wauawa na wanamgambo wa Taliban

Kundi la wapiganaji wa Taliban wakiwa na zana nzito nzito wameendesha shambulio mapema Jumanne Desemba 16 asubuhi katika shule ya watoto wa askari katika mji wa Peshawar kaskazini magharibi mwa Pakistan.

Kulingana na idadi iliyotolewa na viongozi, shambulio hilo limegharimu maisha ya watu 130, wengi wao wakiwa ni wanafunzi, na wengine wengi wamejeruhiwa.

Polisi imetangaza kuwa imewaua wauaji wote ambao wamekua wameshambulia shule hilo. Waziri mkuu Nawaz Sharif ameyaita mauwaji hayo kuwa ni janga la kitafa.


Jeshi la Pakistan limetangaza kuwa limerejesha hali ya utulivu katika mji wa Peshawar. Operesheni ya jeshi imetamatika baada ya kumuua mshambuliaji wa sita ambaye alikua wa mwisho. Operesheni hiyo imedumu saa 7. Hata hivyo operesheni hiyo imecheleweshwa kutokana na milipuko iliyokua ikisikika katika majengo ya shule hilo, afisa mmoja wa ngazi ya juu jeshini ameelezea kwenye akaunti yake ya Twitter.

Kundi la TTP ( le Tehreek-e-Taliban Pakistan), limekiri kuendesha shambulio hilo. Msemaji wa kundi hilo, amebaini kwamba shambulio hilo ni ulipizaji kisase kwa operesheni inayoendeshwa na jeshi katika ngome za kundi la Taliban katika eneo linalokabiliwa na mizozo ya kikabila la Waziristan ya Kaskazini, na amri ilitolewa ya kuwapiga risasi watu wa kubwa, baada ya kuwatenganisha na watoto.

Hili ni shambulio la pili baada ya miezi ya hivi karibuni kutokea shambulio jingine lililosababisha maafa makubwa nchini Pakistan, jeshi limekua likilengwa na mashambulizi hayo.


CChachage: PAC, CAG na MEM - Nani Muongo?


"Mheshimiwa Spika, Kamati imepitia Mkataba wa mauzo ya Hisa kati ya Kampuni ya PAP na VIP na kuthibitisha kuwa Waziri wa Nishati na Madini Mheshimiwa Prof. Sospeter Muhongo (Mb) ndiye alikuwa kiungo kati ya Bw. Harbinder Singh Sethi wa IPTL na Ndg. Rugemalira wa VIP (Kiambatisho Na. 16). Katika mkataba huo wa tarehe 19 Agosti, 2013. Ndg. James Rugemalila alithibitisha kuwa Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Prof. Sospeter Muhongo alimwomba kuwasilisha kiasi cha fedha ambacho angependa kulipwa na IPTL ili kumaliza Shauri lililokuwepo mahakamani. Aidha, Bw. Sethi aliwasilisha kwa Bw. Rugemalira ushahidi kwamba PAP imenunua Hisa 7 za Mechmar katika IPTL. “On 11th July 2013, the Minister of Energy and Minerals, Hon. Dr. Prof. Sospeter Muhongo invited VIP to submit to him the amount of money if paid VIP would conclusively settle VIP claims against IPTL”Mheshimiwa Spika, mchakato wote wa kutoa fedha katika Akaunti ya Tegeta ESCROW ndipo ulipoanza na mauzo ya hisa za VIP kwenda PAP na baadaye kuhitimishwa na maamuzi ya Mahakama Kuu ya tarehe 5 Septemba, 2013 ambayo ndiyo yaliyotumika kuhalalisha utoaji wa fedha katika Akaunti ya Tegeta ESCROW tarehe 28 Novemba hadi 5 Desemba, 2013" - UKURASA WA 58 WA 'TAARIFA YA KAMATI [YA KUDUMU YA BUNGE YA HESABU ZA SERIKALI (PAC)] KUFUATIA MATOKEO YA UKAGUZI MAALUM WA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI KATIKA AKAUNTI YA TEGETA ESCROW ILIYOKUWA KATIKA BENKI KUU YA TANZANIA'

"Mheshimiwa SpikaKutokana na tofauti zilizokuwepo kati ya MECHMAR na VIP kuanzia mwanzo wa mradi, VIP iliamua kuuza Hisa zake zilizoko IPTL kwa makampuni mbalimbali kwa nyakati tofauti ikiwemo MECHMAR kama mwanahisa mwenzake, NSSF, Camel Oil, Great White Shark Opportunity Fund pamoja na SYMBION lakini haikuwezekana kutokana na kutoafikiana katika bei. Mheshimiwa SpikaBaadaye VIP chini ya usuluhishi ya RITA, iliuza Hisa zake kwa PAP kwa thamani ya Dola za Marekani milioni sabini na tano (US$ 75,000,000/=). Ununuzi wa Hisa Asilimia 30 za VIP uliofanywa na PAP ndiyo uliyomaliza mgogoro wa Wanahisa uliyokuwa Mahakamani na kuufanya Mtambo wa IPTL kumilikiwa na PAP kwa kuwa ndiyo iliyomiliki Hisa zote Asilimia 100 za IPTL. Taarifa ya PAC: Katika ukurasa wa 58 wa Taarifa ya PAC imeelezwa kuwa Waziri wa Nishati na Madini ndiye aliyekuwa Dalali Mkuu aliyewakutanisha Bw Harbinder Sethi na Bw James Rugemalira     Ufafanuzi Mheshimiwa Spika, Taarifa hii siyo sahihi kwa kuwa tangu tarehe 9 Novemba, 2011, RITA aliitisha mkutano na kuwakutanisha wadau wote wa IPTL. Wakati huo, Waziri wa Nishati na Madini aliyeko sasa alikuwa bado hajateuliwa kwenye wadhifa huo"  - UKURASA WA 11-12 WA 'UTETEZI WA SERIKALI' KUPITIA WIZARA YA NISHATI NA MADINI

"Tarehe 15 Agosti 2013 kampuni ya VIP iliingia makubaliano na PAP ya kuuza hisa tatu (3) katika IPTL, ambapo utekelezaji wa makubaliano hayo ulianza rasmi tarehe 19 Agosti 2013 kulingana na Kipengele Na. 1.26 cha Makubaliano ya Uuzaji na Ununuzi wa Hisa hizo (Kielelezo 65 ). Wakati wa makubalino hayo yanafanyika kampuni ya IPTL ilikuwa katika ufilisi. Mahakama Kuu ya Tanzania iliridhia (taking judicial notice) makubaliano haya katika hukumu ya tarehe 5 Septemba 2013" - UKURASA WA 29 WA 'TAARIFA YA UKAGUZI MAALUM [WA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI (CAG) KUHUSIANA NA MIAMALA ILIYOFANYIKA KATIKA KAUNTI YA 'ESCROW' YA TEGETA, PAMOJA NA UMILIKI WA KAMPUNI YA IPTL ILIYOWASILISHWA NA CAG KWA KATIBU WA BUNGE.'

----

Katuni ya 'Wakudata' kuhusu 'uchafuzi' wa Serikali za Mitaa


Mikataba ya Kimataifa yaisaidia Tanzania katika Hifadhi ya Jamii

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk Pindi Chana (kulia) akizungumza katika mkutano wa siku tatu wa kimataifa unaohusu Hifadhi ya Jamii uliotarajiwa kumalizika jana jijini Arusha. Katikati ni Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mhe. Dkt. Kebwe Stephen Kebwe na kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima.

UTIAJI saini wa mikataba ya kimataifa, inayohusu hifadhi ya jamii kumeiwezesha Tanzania kuwa katika hatua nzuri ya kutekeleza ajenda yake ya kuhakikisha kwamba wananchi wake wanakuwa na haki sawa katika kujipatia maendeleo na ustawi.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk Pindi Chana katika mkutano wa siku tatu wa kimataifa unaohusu hifadhi ya jamii mjini hapa.

Alisema mikataba mikubwa ya kimataifa ambayo Bunge la Tanzania limeridhia na iliyoleta mabadiliko makubwa katika sera na sheria nchini ni pamoja na Mkataba wa Kufuta Aina zote za Ubaguzi na Unyanyasaji kwa Wanawake (CEDAW) wa mwaka 1979, Mkataba wa Haki za Watoto (CRC) wa mwaka 1989 na Mkataba wa Afrika wa Haki za Watoto.
Mkurugenzi mshiriki anayeshughulikia masuala ya program kutoka makao makuu ya UNICEF, Bi. Alexander Yuster, akiibua hoja kwenye mkutano mkubwa wa kimataifa wa hifadhi ya jamii ulioandaliwa na serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Fedha na wadau wengine kwa lengo la kubadilishana uzoefu juu ya nini cha kufanya kusaidia makundi maalumu katika jamii uliomalizika jana jijini Arusha. Kushoto ni Naibu Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano na Maendeleo kwenye Ubalozi wa Sweden nchini, Maria Van Berlekom.

Mikataba mingine ni Mpango wa Maendeleo wa Milenia (MDGs), Azimio la Umoja wa Mataifa Namba 1325 la mwaka 2000 na Azimio Namba 1820 la 2006, ambayo inazungumzia ushiriki na uwezeshaji wa wanawake katika kutanzua migogoro na ujenzi wa taifa.

Alisema kitendo cha kuridhia kwa mikataba na maazimio hayo, kinaonesha ni kwa namna gani serikali ina utashi wa utekelezaji wa maazimio hayo kwa lengo la kuhakikisha watoto na wanawake, wanalindwa dhidi ya vurugu za aina zozote na kuwanyima haki zao za msingi.

Dk.Chana alisema kwa kuzingatia ushiriki kuleta katika maendeleo ya nchi, Tanzania imetayarishwa Dira ya Maendeleo ya 2025 ikiwa na vipengele vyote vya haki vyenye lengo la kuongeza wigo wa ushiriki wa wanawake.

Aidha, ili kuhakikisha makundi maalumu yanalindwa, serikali pia imetengeneza Sera ya Maendeleo ya Watoto ya mwaka 2008, ambayo kwa sasa inapitiwa ili kuingiza mambo mengine yanayohusu haki za mtoto.

Aidha, ikiwa imejikita kuondoa masuala ya kuondoa udhalilishaji wa kijinsia, serikali imefanya maamuzi mengi yenye manufaa pamoja na kushirikiana na wadau binafsi kuboresha maisha ya watanzania.

Alisema kwamba suala la wanawake na maendeleo, limeingizwa katika mkakati wa taifa wa kupunguza umaskini. Alisema mwaka jana serikali ilitengeneza programu ya taifa inayohusu wadau wengi ya miaka mitatu ya kuondokana na ukatili kwa watoto.

Mkutano huo unaozungumzia hifadhi, ulifunguliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Iddi ambaye alisema misingi imara imeshawekwa kusaidia hifadhi ya jamii kuelekea dira ya taifa ya kuwa na kipato cha kati ifikapo mwaka 2025.Picha juu na chini baadhi ya washiriki wa mkutano mkubwa wa Kimataifa wa Hifadhi ya Jamii wakiwemo watengeneza sera, watafiti na waendeshaji wa mifuko ya hifadhi kutoka mataifa ya Kenya, Uganda, Bangladesh, Mozambique, Lesotho, Malawi, Afrika Kusini, Ghana, Ethiopia, Zambia, Sudan Kusini na wenyeji Tanzania, jijini Arusha.


Taarifa tumeshirikishwa na Zainul Mzige / modewjiblog

Waliovuruga uchaguzi wa SM waadhibiwe

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari, leo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, kutoa tathmini ya matokeo ya awali uchaguzi wa Serikali za mitaa uliofanyika juzi nchini kote.

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimetaka watendaji wote waliosababisha kuharibika kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika baadhi ya maeneo nchini wachukuliwe hatua kali.

Kimesema, watendaji hao wanastahili kuchukuliwa hatua kali kwa sababu kilichotokea ni uzembe wa hali ya juu uliofanyika huku ikifahamika wazi kwamba tukio la uchaguzi huo ni kubwa na muhimu sana kwa taifa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (pichani) amesema, kulingana na kosa lililojitokeza kuwa la wazi hakuna haja ya kupoteza fedha na muda kufanya uchunguzi kabla ya kuwachukulia hatua waliohusika.

"Kwa mfano, Mkurugenzi wa Halmashauri ana kila kitu na alijua mapema kuwa uchaguzi utafanyika lini kwa kuwa halikuwa jambo la dharura, inakuwaje anaruhusu karatasi ziende kwenye vituo zikiwa zimechapishwa hovyo au mahali pengine vifaa viwe vicheche?" alihoji Nape na kuongeza "Sasa hapa unahitajika uchunguzi gani tena kubaini aliyevurunda?"

"Mahali pengine zimefika karatasi za kupigia kura jina la mgombea wa CCM nembo ya CUF, au mgombea wa CUF nembo ya CCM! huu ni uzembe wa hali ya juu sana na adhabu yake haistahili kusubiri uchunguzi", alisema Nape.

Akizungumzia matokeo ya awali ya Uchaguzi huo, Nape alisema licha ya vyama vya upinzani kuwa na umri wa miaka 22 sasa, huku vikifanya harakati za kujaribu kuungana katika umoja wanaouita Ukawa, bado CCM imewagaragaraza vibaya.

Nape amesema, katika uchaguzi huo, CCM imepata zaidi ya asilimia 80 ya ushindi kwa nchi nzima, huku Dar es Salaam, ikiwa na asilimia zaidi ya 70 licha ya kwamba Chadema wanao wabunge wawili katika mkoa huo.

"Katika mazingira ya sasa ambayo vyama vya upinzani vina miaka 22, na vinafanya hata harakati za kujaribu kuungana, asilimia 80 si ndogo kwa CCM, na tunaamini huu ni mwanzo mzuri, na hatuoni namna ambavyo asilimia hii itabadilika katika uchaguzi mkuu mwakani, maana uchaguzi huu ni kama kura za maoni", alisema Nape.

"Wanaosema, asilimia ya CCM imeshuka, wajue kwamba tuliposema tunataka mfumo wa vyama vingi maana yake tulitaka ushindani katika demokrasia, katika demokrasia ya ushindani ni vema kuruhusu vyama vya upinzani vikakua ili ushindani huo uonekane", alisema Nape nakuongeza.

"Hata hivyo inasikitisha kwamba licha ya vyama vya upinzani kuwa na umri wa miakaa 22 sasa, bado havijaweza kujenga imani ya kutosha kwa Watanzania kuwa vinaweza kuongoza, lazima wapinzania wazidi kujijenga ili Watanzania wawaamini, asilimia hii 14 waliyopata karika uchaguzi huu wa serikali za mitaa bado ni ndogo sana kwa uhai wa miaka hiyo".

Amesema, asilimia iliyopata CCM wakati matokeo mengine yakisubiriwa ambako uchaguzi uliahirishwa, ni dalili za wazi kwamba, Ukawa bado ni muungano wa mashaka kwa sababu kama wangeungana na kuachiana maeneo ni kweli wangeweza kufika mbali.

"Hebu jiulizeni na ninyi, kama kweli UKawa ulitumika vema, ni kwa nini kwenye karatasi za matokeo ya uchaguzi huu, kila chama kina mtu wake na idadi ya kura alizopata? Kwa nini zisiwe za mgombea mmoja wapo wa Ukawa?... Hii inamaanisha ndoa hii ya ukawa bado sana", alisema Nape.

Nape aliwashukuru wananchi nchini kote kwa kuendelea kuiamini CCM, na kuchagua wagombea wake, huku akivipongeza vyama vya upinzani kwa maeneo waliyochaguliwa, akiwataka kuchapa kazi vinginevyo siku za baadaye wananchi watawahukumu kwa kuwatosa.Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari, leo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, kutoa tathmini ya matokeo ya awali uchaguzi wa Serikali za mitaa uliofanyika juzi nchini kote. 

Taarifa hii tumeshirikishwa na Bashir Nkoromo

Kagera kujivunia uwanja wa ndege wa kisasa

Ujenzi unaendelea! Mafundi wakiendelea na ujenzi wa jengo la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kagera.

Pichani ni muonekano mpya wa Kiwanja cha Ndege cha Bukoba.

Mkoa wa Kagera na maeneo ya jirani wataanza kujivunia uwanja wa ndege wa kisasa kufuatia kukamilika kwa Kiwanja cha Ndege cha Bukoba.

Akizungumza na Wakaguzi wa Miradi ya Maendeleo toka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Meneja Mradi wa Upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kagera, Mhandisi Suleiman Athuman, amesema kwamba maendeleo ya ujenzi wa jengo la abiria la kiwanja hicho upo kwenye hali nzuri na mkandarasi atabidhi kazi hiyo mapema mwakani.

“Katika mwaka wa fedha wa 2013/14 kazi zilizopangwa ni ukarabati na upanuzi wa miundombinu ya kiwanja, ikijumuisha barabara ya kuruka na kutua ndege, maegesho ya ndege, barabara ya kiungio, kwa sasa ujenzi unaendelea vizuri na Mkandarasi atatukabidhi kazi mapema mwakani,” alisema Mhandisi Athuman.

Akitoa taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa Kiwanja cha Bukoba, Mhandisi Mshauri wa ujenzi wa kiwanja hiko, Mhandisi Pius Gobolo amesema kuwa kazi za usimikaji wa mfumo wa taa za kuongozea ndege, ujenzi wa jengo jipya la abiria na uzio wa usalama zimeshakamilika kwa asilimia 80.

“Kama unavyojionea, sehemu kubwa ya kazi imekamilika, kwa makadirio ni zaidi ya asilimia 80 ya ujenzi wa kiwanja hiki imeshakamilika,” aliongeza Mhandisi Gobolo.

Kwa mujibu wa mpangokazi wa ujenzi wa kiwanja hicho hadi kufikia mwezi Juni 2014, hatua iliyofikiwa ni pamoja na kukamilika kwa ukarabati wa barabara ya kuruka na kutua ndege, barabara ya kiungio na maegesho ya ndege kwa kiwango cha lami; na ujenzi wa jingo jipya la abiria kufikia hatua ya usimikaji wa paa na mifumo ya maji safi, maji taka na umeme; na kuendelea kwa ujenzi wa jengo la abiria na kituo cha umeme.

Naye, Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri amesema kuwa Serikali imeazimia kuendelea kuboresha miundombinu ya viwanja vya ndege hususan miradi iliyoibuliwa katika Programu ya Matokeo Makubwa Sasa.

“Kwa mujibu Programu ya Matokeo Makubwa Sasa, serikali kupitia Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini ipo kwenye mkakati wa kuuendeleza viwanja vya ndege vyote ili viwe na kiwango kizuri kwa watumiaji wa viwanja hivyo,” alisema Bibi Mwanri.


Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipangoimu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ikiendelea na kazi ya ukaguzi wa Kiwanja cha Ndege cha Bukoba.


Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakiwasili kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kagera kujionea maendeleo ya Mradi wa Upanuzi wa Kiwanja hicho. Waliotangulia mbele ni Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Kushoto), Meneja Mradi wa Upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Bukoba, Mhandisi Suleiman Athuman (Katikati) na Meneja wa kiwanja hicho, Bw. Julius Mulungwana (Kulia).


Wahandisi Pius Gobolo (kushoto), (Mhandisi Mshauri wa ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Bukoba) na Suleiman Athuman (watatu kulia), Meneja Mradi wa Upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Bukoba wakitoa maelezo mara walipoingia kwenye sehemu ya abiria ya jengo jipya la kiwanja hicho.


Meneja wa kiwanja hicho, Bw. Julius Mulungwana (Kulia) akifafanua jambo kwa Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Wapili kulia). Wanaoshuhudia ni Meneja Mradi wa Upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Bukoba, Mhandisi Suleiman Athuman (Wapili kushoto) na Mhandisi Mshauri wa ujenzi wa kiwanja hiko, Mhandisi Pius Gobolo (Kushoto).


Hadi kuleeee.. Meneja wa kiwanja hicho, Bw. Julius Mulungwana (Mbele) akimuonesha Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Kulia) sehemu inayopendekezwa kwa ajili ya upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Bukoba. Picha na Saidi Mkabakuli-Ofisi ya Rais,Tume ya Mipango.

Taarifa ya Saidi Mkabakuli, Kagera.

[video] Masaburi akizungumzia 'kashfa ya escrow'WATANZANIA wameombwa kumuonea huruma na kumpongeza Rais Jakaya Kikwete, kutokana na kufanya kazi kubwa ya kuiletea Tanzania maendeleo katika kipindi cha miaka 9 ya uongozi wake, na si kumkatisha tamaa kwa kumtwisha mizigo mizito.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (ALAT), Dk Didas Massaburi aliyasema hayo wakati alipokuwa anazungumzia mzigo mkubwa aliokabidhiwa Rais Kikwete wa kutekeleza maazimio manane ya Bunge kuhusu sakata la madai ya kuchotwa kwa fedha zinazodaiwa kuwa ni za umma katika Akaunti ya Tegeta Escrow.

Dk Massaburi alisema hivi sasa suala la Escrow limeleta mtafaruku na madhara makubwa ndani ya nchi kutokana na kupotoshwa na kikundi cha watu wachache wenye maslahi binafsi, hatua ambayo sasa inamfanya Rais kuacha kushughulikia maendeleo ya nchi na kulishughulikia suala hilo.

“Tufike mahala tuache kumbebesha Rais wetu mizigo mizito na isiyo na sababu kwani amefanya mambo mengi na makubwa na yanayogharimu matrilioni ya shilingi katika ujenzi wa barababara, umeme, maji na elimu.

“Leo hii kutokana na sakata la Escrow ambalo fedha zinazodaiwa kuwa ni za serikali haziwezi hata kujenga barabara mbili za lami, nchi inapita katika wakati mgumu sana,” alisema Dk Massaburi.

Alisema ALAT kama mdau mkubwa wa maendeleo katika serikali za mitaa na hasa vijijini inaguswa na sakata hilo kwa vile sasa serikali inaendelea na kazi kubwa ya kupeleka umeme vijijini na hakuna maendeleo yanayoweza kufikiwa vijijini bila nishati ya umeme.

Alisema suala la Akaunti ya Tegeta Escrow limepotoshwa na watu wenye maslahi binafsi yakiwemo ya kutaka kukubalika kwenye nafasi za Ubunge, Umeya na hata Urais na kwa bahati mbaya wananchi wameingiwa na imani kali kuhusu upotoshaji huo na kujenga chuki kubwa kwa serikali yao.

“Hali imekuwa mbaya sana bila sababu ya msingi, watu wanashindwa kufanya shughuli muhimu za maendeleo kwa suala la Escrow. Imefika mahala tunaweka shinikizo la kutaka kuwajibishwa kwa viongozi wachapa kazi na walioliletea maendeleo makubwa Taifa letu kwa masuala yanayopotoshwa tu, jambo ambalo ni la hatari sana kwa mustakabali wa Taifa letu,” alisema Dk Massaburi.

Alisema mbali ya wanasiasa, taasisi za kifedha za kigeni pia zinalishabikia suala hilo kutokana na ulafi wa kutaka kuzichukua fedha hizo na wala si kuwapa wananchi na pia kampuni za kigeni za umeme ambazo zinaathirika na bei ndogo ya umeme inayouzwa na IPTL ukilinganisha na wao, zinahusika.

“Kwa bahati nzuri mimi nimeisoma vizuri sana taarifa ya CAG, hakuna mahala anaposema fedha ni za umma. Fedha ya umma inajitokeza katika ulipaji wa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) na ambayo kwa kawaida kodi hii hulipwa na aliyelipwa.

“Mimi nikilipwa fedha leo, napokea kwanza hundi yangu halafu baada ya kuchukua fedha na kuwa mikononi mwangu ndio mwisho wa mwezi nakwenda kulipa kodi ya VAT, hawakati fedha hiyo moja kwa moja kutoka kwenye akaunti yangu. TRA wanapaswa kuifuatilia kodi yao maana hapa ni suala la sheria ya Kodi kukiukwa hakuna Sheria ya Escrow,” alisema Dk Massaburi.

Alisema kwa namna taarifa ya CAG ilivyofafanua hakuna ubishi kwamba IPTL sasa inamilikiwa kihalali na Kampuni ya PAP, na hivyo ni lazima kama Taifa kuipa ushirikiano kampuni hiyo kuendelea kuzalisha umeme na kuuza kwa bei nafuu na si kushinikiza kutaifishwa kwa mitambo hatua ambayo italiingiza Taifa kwenye matatizo makubwa ikiwemo kurejea kwenye bei kubwa ya umeme.

“Mazungumzo kuhusu Escrow ni ya miaka mingi sana, yalianza tangu enzi za Ngeleja (William- aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini. Watu hawa wamezungumza suala hili kwa zaidi ya miaka minane.Leo hii mtu anapotosha kwamba makubaliano ya kuondoa fedha kwenye akaunti ya Escrow yalifanywa siku moja tu pale Kunduchi Beach.

“Tuwasaidie viongozi wetu wanaofanya kazi nzuri ili kulikoa Taifa letu. Rais anafanya kazi nzuri, Waziri Mkuu (Mizengo Pinda ) anafanya kazi nzuri, Waziri Muhongo anafanya kazi kubwa na nzuri. Hawa ni watu muhimu sana kwetu,” alisema Dk Massaburi ambaye alitangaza kutokuwa na mgongano wa kimaslahi kwa sakata hilo.

NANI WA KULAUMIWA

Mwenyekiti huyo alisema kuwa kutokana na uzoefu wake katika masuala ya hisa za kampuni, amegundua kuwa sakata ta escrow linachochewa na makundi mawili.

“Kundi la kwanza ni wapotoshaji wakiwamo wabunge, wachumi ambao walikuwa wakisambaza upotoshaji huo kwa masilahi yao binafsi...mtu mwingine anaweza kusema ninatetea labda nimepata mgao, hapana...ila ukweli unatakiwa uelezwe wazi.”

Dk Massaburi alitaja kundi lingine aliloliita la fisi ambalo lina idadi kubwa ya wapambe waliokuwa na njaa ya kupata mgao huo.

Alisema hakuna kiongozi anayetakiwa kuwajibishwa kutokana na ukweli kwamba, Kampuni ya Mechmar ndiyo iliyosababisha kuwapo kwa tatizo hilo.

Mwaka 2010, kampuni ilikabidhi umiliki wake wa asilimia 70 ya hisa za IPTL kwenda kwa Kampuni ya Piper Link.

Kongamano la kujadili makabila ya asili lafunguliwa


Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi , Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Kamani (Mb) akitoa hotuba yake wakati akifungua kongamano la siku mbili la bara la Afrika la kujadili masuala ya jamii za kiasili (indigenous people) lililofanyika katika Hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam.

(picha: Philemon Solomon)

Kongamano hilo linajadili changamoto zinazowakabili watu wa jamii za asili na namna ya kuboresha maisha ya jamii hizo bila kupoteza uasilia wao huku mada kuu ikiwa ni suala la mifumo ya upatikanaji wa chakula chao na maisha endelevu. Mapendekezo ya kongamano hilo yatawasilishwa katika mkutano wa dunia wa kujadili masuala ya jamii za kiasili utakaofanyika mjini Roma Italia, februari mwaka 2015.

Katika hotuba yake Waziri Kamani amelipongeza Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Kilimo (IFAD) kwa kuandaa sera mahsusi inayotambua uwepo wa jamii hizo, utamaduni na desturi za jamii za kiasili kama nyenzo ya kuzisaidia jamii hizo kujiletea maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Kilimo (IFAD), Bw.Francisco Pichon akieleza namna shirika lake linavyotoa kipaumbele katika kushughulikia masuala yanayohusu jamii za asili na hivyo kuitaka serikali na wadau kufanya kazi kwa pamoja katika kushughulikia masuala hayo ili kupata matokeo yanayokusudiwa.

Waziri Kamani pia ameipongeza IFAD kwa kuanzisha mfuko maalum wa miradi ya jamii za asili unaosimamiwa na watu wa jamii za asili wenyewe. mpaka sasa mfuko huo umeshafadhili miradi midogo midogo 100. IFAD pia imeanzisha jukwaa mahsusi la mijadala kuhusu haki na nafasi za watu wa jamii ya kiasili kwa kuzingatia azimio la Umoja wa Mataifa la haki za watu wa jamii ya kiasili.

Waziri Kamani alisema zerikali ya Tanzania inazitambua jamii za asili ikiwamo wahadzabe, wasandawi na masai na kusema serikali itashirikiana na wadau katika kuzilinda jamii hizo na kuzikabili changamoto wanazokumbana nazo ili kuboresha maisha yao.Wadau mbalimbali kutoka Nchi za afrika wakiwa kwenye kongamano hilo ambalo pamoja na mambo mengine linajadili namna ya kuzisaidia jamii za asili kuwa na maisha endelevu bila kuharibu mazingira yao.Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi , Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Kamani (Mb) akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa kongamano hilo.

Taarifa ya Ikulu kuhusu Jaji Werema kujiiuzulu

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema amejiuzulu nafasi yake hiyo kuanzia leo, Jumanne, Desemba 16, 2014 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amekubali ombi hilo la kujiuzulu.

Katika barua yake kwa Mhe. Rais Kikwete, Jaji Werema amesema kuwa ameomba kujiuzulu kwa sababu ushauri wake kuhusiana na suala ya Akaunti ya Tegeta Escrow haukueleweka na umechafua hali ya hewa. Mhe. Rais Kikwete amemshukuru Jaji Werema kwa utumishi wake ulioongozwa na uaminifu na uadilifu.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu, DAR ES SALAAM.
16 Desemba, 2014

NMB yatoa vifaa vya hospitali na madawati Nanyumbu

Meneja wa kitengo cha biashara za Serikali wa NMB Kanda ya Kusini, Mr. Haji Msigwa akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Mhe. Festo Kiswaga sehemu ya madawati yaliyotolewa kwa ajili ya Shule ya Msingi Likokona.

Benki ya NMB kwa kuelewa uhitaji wa vifaa vya hospitali na madawati katika jamii inayoizunguka, imetoa vifaa vya hospitali vyenye thamani ya shilingi milioni tano kwa ajili ya Hospitali ya Wilaya ya Nanyumbu pamoja na madawati sabini yenye thamani ya shilingi millioni tano kwa Shule ya Msingi Likokona iliyoko Wilayani Nanyumbu, Mkoani Mtwara.

Msaada huo uliopokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Mhe. Festo Kiswaga, ni mwendelezo wa sera ya NMB ya kuchangia huduma za jamii ili kukabiliana na changamoto zinazokabili sekta ya elimu na Afya.

Akitoa shukrani kwa niaba ya wakazi wa Nanyumbu.Mhe Kiswaga alisema “Msaada huu ambao tumeupokea leo kutoka NMB, utasaidia kupunguza uhaba mkubwa tuliokua nao kwa kipindi kirefu. Vifaa tiba vimekua havitoshelezi katika hospitali yetu lakini pia madawati nayo imekua ni kilio kikubwa katika shule za hapa Nanyumbu. Lakini leo NMB wamekua sehemu ya maisha yetu na hivyo wameweza kujua hitaji letu na kutusaidia. Naomba kutoa shukrani za pekee kwa uongozi mzima wa NMB.Meneja wa kitengo cha biashara za Serikali wa NMB Kanda ya Kusini, Mr.Haji Msigwa akimkabidhi vifaa vya Hospitali Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Mhe. Festo Kiswaga kwa ajili ya Hospitali ya Wilaya ya Nanyumbu.

Wanafunzi wa shule ya msingi Likokona walioshiriki hafla ya makabidhiano.