Color of the Year 2015 - Marsala - Rangi ya Mwaka 2015


Why you should not microwave breast milk & Tips for clever microwave uses

Below is an infographic of food items that should not be microwaved as well as tips on how to make clever use of the microwave for some microwaveable foods.


Source: PartSelect.com

Alai matatani tena, adaiwa kumtusi Rais Kenyatta mtandaoni

Robert Alai


Tweets zilizonukuliwa hapo juu na chini ndizo zilizomfikisha kortini mwanablogu maarufu na mwenye utata wa Kenya kwa madai kuwa amemdhalilisha rais.


Siku hiyo aliyomwita rais jina hilo, pia akaweka namba za simu za rais na baadhi ya maafisa waandamizi.


Robert Alai, mkosoaji mkali wa serikali, alikana mashtaka hayo na kuachiwa kwa dhamana kwa dola za Kimarekani $2,000 na kuamriwa kutokuweka ujumbe unaofanana na huo wakati uchunguzi ukiendelea.


Bw Alai ni miongoni mwa wanablogu maarufu na wenye ushawishi mkubwa Kenya akiwa na wafuasi 140,000 kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Bw Alai tayari ana wengi wanaomwuunga mkono kwenye mtandao wa kijami wa Twitter kutoka kwa Wakenya wanaoona mashtaka hayo kama mbinu ya serikali ya kuzuia uhuru wa vyombo vya habari.Alipotolewa tu kwa dhamana, aliandika kwenye Twitter kuwa itakuwa ngumu kumnyamazisha.

Miaka miwili ilyopita, alikamatwa na kuhojiwa baada ya kudai kuwa msemaji wa serikali ya wakati huo alikuwa akipanga kumwuua.

Taarifa ya uteuzi wa Kitima kuwa Msaidizi wa Rais

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Ateuliwa Msaidizi wa Rais

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Willy Kitima kuwa Msaidizi wa Rais – Nyaraka(Documentation) kuanzia Alhamisi iliyopita, Desemba 11, 2014.

Kabla ya uteuzi wake, Bwana Kitima alikuwa Mratibu wa Taasisi ya Kupambana na Rushwa ya Biashara nchini ya Business Action Against Corruption (BAAC)Tanzania.
Taasisi hiyo inaendeshwa kwa ushirikiano kati ya Jumuiya ya Madola na Serikali ya Tanzania kupitia Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (PCCB)na Taasisi ya Uendelezaji Sekta Binafsi nchini ya PPSF.

Bwana Kitima pia amewahi kuwa Mkrugenzi Mtendaji wa Shirika la Kufutilia Nyendo za Rushwa Kimataifa la Transparency International (TI) nchini. Aidha, ana ujuzi wa shughuli za benki na vyombo vya habari.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.


17 Desemba, 2014

Ni ndoto Yanga kuishinda Simba; Kwa heri Maximo, hukuwa na jipya

Kikosi cha Yanga kilicholambishwa shubiri na Simba, Uwanja wa Taifa Dar es Salaam katika mechi ya "Nani Mtani Jembe" Desemba 2014

“Ni ndoto ya mchana Yanga kuwafunga mahasimu wao Simba”, Ndivyo unaweza kusema, itabaki kuwa historia kwani wapinzani wao wanajuwa mbinu za kuwafunga, wakati ushindi wa Yanga ni sare.

Kasumba iliyojengwa na viongozi wa Yanga kukimbilia kusajili kila mchezaji anayetakiwa na Simba itaendelea kuwafanya wafungwe kila watakapokutana, hali hiyo ikichagizwa pia na Kocha Mkuu wa Klabu hiyo, Mbrazil, Marcio Maximo.

Hivi karibuni Simba ilitangaza kumsajili mshambuliaji mkongwe wa Polisi Morogoro, Danny Mrwanda, baada ya Yanga kupata tetesi, viongozi wa klabu hiyo walifanya mipango ya haraka kumsajili kana kwamba wanawakomoa Simba, kumbe wanaongeza mamluki ndani ya klabu.

Hakuna asiyefahamu kuwa Mrwada ni mchezaji na mwanachama hai wa Simba, na uongozi wa Simba kutaka kumsajili ni mkakati mojawapo wa kumrejesha kundini kada huyo aliyekuwa akicheza soka la kulipwa nje ya Tanzania kwa muda mrefu.

Waswahili wanasema kikulacho ki nguoni mwako, kwa kiasi Fulani Simba imewekeza wachezaji wao ndani ya Yanga, wakati Yanga wenyewe hawajawekeza ndani ya Simba, kwa hali hiyo, Yanga isitegemee miujiza kuwafunga Simba.

Mtoto wa nyoka ni nyoka, Ndani ya Yanga wapo nyoka kama, makipa Ali Mstafa, Deogratius Munis na Juma Kaseja (anayeondolewa msimu huu, mlinzi kisiki Kelvin Yondan aliyesajiliwa Yanga mwaka jana na sasa wamemchukua kada mwingine mwandamizi wa klabu hiyo ya Msimbazi Danny Mrwanda na Amis Tambwe ambaye Simba wameona kiwango chake kimeshuka.

Kuhusu Kocha Maximo, ataendelea kuwaudhi mashabiki wa Yanga kwa kuwaleta wachezaji wenye uwezo mdogo ili wachezaji wenye wazawa wenye uwezo mkubwa wa kusakata soka wasipate namba. Kitendo cha Maximo kuwaleta ndugu zake Emerson Oliveira na Andrey Coutinho na kuwaacha Jerryson Tegete, Hussein Javu, Nizar Khalfan na Salim Telela wenye uwezo mkubwa ni kuiangamiza Yanga.

Wakati umefika Yanga watambue kuwa si kila Kocha kutoka Brazil ana uwezo, hebu tuwapatie kazi makoche wetu wazalendo, wenye mapenzi makubwa na Yanga kama Boniface Mkwasa, Fred Minziro na Juma Pondamali. Hakika Yanga itafanya vizuri, poleni wana Yanga wote.

KWAHERI MAXIMO, HUKUWA NA JIPYA YANGA

Marcio Maximo

MCHEZO wa Nani Mtani Jembe, unaozikutanisha timu mbili kongwe zenye upinzani wa jadi nchini, Yanga na Simba imegeuka kuwa machinjio kwa makocha wa Yanga baada ya Kocha Mkuu, Marcio Maximo kutimuliwa rasmi jana.

Huu ni msimu wa pili mfululizo, kwa Yanga kuwafukuza makocha wake baada ya kufungwa na Simba, kwa kupoteza mchezo wa nani mtani jembe. Mchezo wa kwanza uliofanyika mwaka jana, 2013, Yanga ilifungwa 3-1 na kusababisha aliyekuwa kocha wake Ernie Brandts kutimuliwa pamoja na benchi lake la ufundi.

Mwaka huu Kocha Marcio Maximo nae amefungashiwa virago baada ya kungwa 2-0 Jumamosi iliyopita Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, ukiwa mchezo wa nane wa ushindani baada ya michezo saba ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Maximo aliepokelewa na mashabiki wa Yanga kwa vifijo na nderemo Juni mwaka huu baada ya kutangazwa kuwa kocha mpya wa timu hiyo, amewaaga rasmi wachezaji wakati wa mazoezi uwanja wa Sekondari ya Loyola Dar es Salaam jana.

Mazoezi hayo ya Jumanne asubuhi yaligeuka simanzi baada ya Maximo kuwakusanya wachezaji wake na kuwatakia maisha mema ndani ya klabu hiyo ya Jangwani.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wachezaji wa walielezea kutoridhishwa na uamuzi wa uongozi wa kumuacha kocha wao na mshambuliaji Hamis Kiiza kutoka Uganda. Mmoja wa wachezaji hao alisema "Ni kweli kocha ametuaga!

Viroja vya uchaguzi SM: Uchawi wahusishwa na upepo uliopeperusha kura

Imeelezwa kuwa sababu kubwa ya kurudiwa kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika kijiji cha Bubale kata ya Masengwa wilaya ya Shinyanga Vijijini uliokuwa unafanyika Desemba 14, 2014 na badala yake kufanyika Desemba 16 ni kutokana na upepo wa ajabu uliobeba boksi la kura za wagombea wakati zoezi la kupiga kura linaendelea.

Boksi la kura zilizopeperushwa na upepo ni lile la wagombea wa Uenyekiti wa kijiji cha Bubale.

Mashuhuda wakiwemo wasimamizi wa uchaguzi huo wamesema kuwa wakati zoezi la uchaguzi ghafla ulitokea upepo na kubeba boksi la kura kisha boksi hilo kujibamiza kwenye ukuta huku Mawakala wakijaribu kulizuia japo hawakufanikiwa na kura zikapeperushwa na upepo.

Kufuatia hali hiyo uchaguzi katika ngazi ya Uenyekiti uliahirishwa na kurudiwa jana, Jumanne huku mgombea kwa tiketi ya CCM, Bala Nundo aliibuka mshindi dhidi ya mgombea kwa tiketi ya CHADEMA.

Tukio la kura kupeperushwa na upepo limewaacha wakazi wa kijiji hicho midomo wazi huku wengine wakilihusisha na ushirikina.

Taarifa ya Mkurugenzi kuhusu Uchaguzi wa SM 2014

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Taifa, Kharist Michael Luanda akitoa taarifa ya matokeo ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika nchini kote kitaifa leo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) mjini Dodoma.

(picha: Sifa Lubasi /HabariLeo)

MAGAZETI kiushabiki kabisa yaliandika mtikisiko, yakaandika CCM yagalagazwa kila kona, lakini kwa taarifa hii ya ushindi wa asilimia 80.58 inadhihirisha kushindwa kwa ajenda ya magazeti kutengeneza njia ya kuing’oa CCM madarakani.
Aidha kwa takwimu hizo inaonesha ndoa ya ukawa inahitaji maboresho zaidi ili ngome za vyama zisiliwe na kuacha msambaratiko.

Lakini la msingi ipo haja ya wananchi kufahamu siasa, uwongo na ukweli, na pia kuangalia kama wanatazama kazi za watu au fikira wanazopandikizwa.

Kwa vyovyote vile ushindi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wa asilimia 80.58 katika matokeo ya awali ya uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika Desemba 14, mwaka huu , unaonesha, ikiondoa laana inayojitakia, CCM inaweza kuendelea kuwepo kwa miaka kadhaa huku upinzani ukipanda chati kukubalika kama vitababadili staili na kuwa vyama vya siasa badala ya kuwa vyama vya auanaharakati, japo ni kweli nia ya vyama vya siasa ni kukamata dola.

Hii inatokana na ukweli kuwa hata baada ya miaka 20 ya vyama vya upinzani bado Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) uchaguzi huu kimepata asilimia 13.79 ikifuatiwa na Chama cha Wananchi (CUF) asilimia 3.6 Chama cha NCCR Mageuzi asilimia 0.19 TLP asilimia 0.03 NLD asilimia 0.00 na Chama cha ACT asilimia 0.04.

Matokeo haya yaliyotangazwa na Mkurugenzi wa Serikali za Mitaa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Calist Luanda katika mkutano wake na waandishi wa habari leo yanaweza kutoa tafakari mpya ya siasa nchini, hasa siza zetu uchwara zinazonyima viongozi wa kweli nafasi kutokana na mivutano ya ndani ya chama na pia matumizi mabaya ya taarifa zilizopo kusambaza chuki.

Hata ukitazama mtawanyiko wa viongozi wachaguliwa kuna maeneo unaona matumizi mabaya ya taarifa kwa kuzipika na kuzibadili, kuacha kuonesha weledi wa kuchambua mambo na kugeuza wapiga kura mbumbu na wanazuoni hawajui kufikiri.

Kwani upande wa wenyeviti wa vitongoji CCM imeshinda kwa asilimia 83.05 ikifuatiwa na Chadema asilimia 13.9 CUF asilimia 36 NCCR asilimia 0.09 TLP asilimia 0.03 NLD asilimia 0.00 ACT asilimia 0.02

Na kwenye vijiji 9,047 CCM imepata vijiji 7,290 , Chadema vijiji 1,248, TLP vijiji viwili, NLD vijiji viwili na UDP vijiji vinne.

Kwa upande wa mitaa 3,078 iliyofanya uchaguzi, CCM imeshinda katika mitaa 2,116, CHADEMA mitaa 735, CUF mitaa 235, NCCR mitaa nane ,TLP mtaa moja, ACT mitaa tisa, UND mtaa moja, UDP mtaa moja na NRA mtaa moja.

Kwa upande wa vitongoji 42,824 CCM imepata vitongoji 35,564, Chadema 5670, CUF 1555, NCCR 80, TLP 11, NLD kitongoji kimoja ACT vitongoji 10.

Pamoja na ukweli kuwa kwenye matokeo yaliyobaki hayataiondoa CCM kirahisi kileleni kitu kimoja kipo wazi kabisa , wanasiasa wanatakiw akufanyakazi yao ya siasa kwa kujiepusha na uwongo, kusema ukweli ili wananchi wachuje nani atawaondoa kweli katika dhiki kwa vyama na utashi wa utekelezaji wa sera hizo.

Na kama wanasiasa hawatafanya siasa kitu mbaya itatokea katika nchi hii. Litakuwa taifa linaloamini uwongo na lisilojua pumba na mchele na mbaya zaidi halitajua tafakari ya kifalsafa kwa miaka mingi ijayo kwamba hatuendeshi kwa mauungu na kubabatizana makosa yasiyokuwapo bali haja ya kuangalia sheria zetu kuzifanya ziwe kali na watuj wawajibike katika nafasiu zao.

Nassari akamatwa na kupandishwa kizimbani

MBUNGE wa Jimbo la Arumeru Mashariki mkoani Arusha Mhe. Joshua Nassari alikamatwa na kushikiliwa na jeshi la polisi kwa kutuhumiwa na tukio la kumteka mtendaji wa kata ya Makiba.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Lebaratus Sabas alisema Nassari alikamatwa majira ya saa moja usiku wa Desemba 16 katika eneo la Doli lililopo katika kijiji cha UsaRiver kwenye gari aina ya Land cruiser lenye namba za usajili T 753 AQR.

Alisema Nassari anatuhumiwa kumteka Mtendaji  Kata aliyefahamika kwa jina la Nemani Ndundu wa Kata ya Makiba tarafa ya Mbuguni wilayani Arumeru mkoani Arusha Desemba 15 majira ya saa mbili asubuhi katika eneo la Maji ya Chai.

Mtendaji huyo alikumbwa na hayo alipokuwa katika pikipiki yake akielekea kwenye Kata ambapo ndipo inatuhumiwa kuwa Mhe. Nassari alimkamata na kumpiga na kumjeruhi katika sehemu mbalimbali za mwili wake huku akimtaka amuonyeshe majina ya wanachama waliopiga kura katika kituo cha huduma na maendeleo kilichopo katika Kata yake .

Mhe. Nassari alifikishwa mahakamani katika wilaya ya Arumeru leo Desemba 17, 2014 kujibu tuhuma zinazomkabili.

Hakimu David Mwita wa Mahakama ya mwanzo ya Maji ya Chai mkoani Arusha aliahirisha kesi dhidi ya Nassari hadi Desemba 24, 2014.

Madai ya tuhuma katika hiyo ni ya kuharibu mali ya umma yenye thamani ya shilingi laki mbili, kumteka mtu na kumtishia kwa bunduki.

Hata hivyo, Mahakama hiyo imemuachia Mbunge huyo baada ya kutimiza masharti ya dhamana, ikiwa ni pamoja na kuwa na wadhamini watatu ambao wana mali zisizohamishika zenye thamani ya shilingi milioni moja na nusu kila mmoja. 

Akiongea mara baada ya kuahirishwa kesi hiyo, wakili wa Mbunge huyo, Bw. James Ole Milya alisema amesikitishwa sana na tukio la mahakama hiyo kumpa masharti makubwa mteja wake kwani kesi yake ilikuwa haihitaji mashariti makubwa hivyo.
 
Aidha, alisema kuwa angependa kesi hiyo ipelekwe katika mahakama ya Wilaya ili yeye kama Wakili wa Mbunge aweze kumtetea kwa kuwa Mahakama ya Mwanzo hairuhusu kuweka Wakili.


  • Taarifa ya Woinde Shizza

EALA Speaker Zziwa impeached / Spika wa EALA atimuliwa

Hon Mukasa Mbidde casts his vote on the Motion.  

THE East African Legislative Assembly (EALA) has impeached Speaker Margaret Zziwa over misconduct, abuse of Office and disrespect to members.

Her impeachment follows a report by EALA’s Committee on Legal, Rules and Privileges which recommended that the house impeaches Zziwa with immediate effect.

In a session chaired by Uganda’s representative Chris Opoka, the interim EALA speaker, 36 out of the 39 members present in the house voted in support of the motion for a resolution to remove Zziwa while 2 voted against while there was one abstention.  (NewVision: EALA Speaker Zziwa impeached)

----------------

Spika wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) Margret Zziwa ameng’olewa na baadhi ya Wabunge wa Bunge hilo ambao wamepiga kura leo huku Ofisi ya Bunge hilo ikitoa saa 48 kwa wabunge wa Bunge la Uganda kupeleka majina yao ili uchaguzi wa Spika mwingine kutoka nchi hiyo uweze kufanyika.

Kura hizo zilipigwa leo mchana na kutangazwa na Kaimu Spika kutoka Nchini Uganda , Chris Ukomu ambaye ndiye alikuwa akiendesha kikao hicho cha Bunge.
Idadi ya wabunge waliokuwepo ndani ya Bunge hilo ilikuwa ni 39 waliopiga kura za ndio kwa ajili ya kumng’oa Spika huyo ni 36 huku kura mbili zikisema hapana kura moja ikiwa imeharibika.

Awali kabla ya zoezi hilo wabunge hao wakiongozwa na Kaimu Spika, Okumu Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria, Kanuni na Tarartibu, Frederic Ngenzebuhora alisoma mambo mbalimbali yanayomhusu Spika huyo ikiwemo suala la kutoendesha ofisi hiyo kwa mujibu wa kanuni,taratibu na sheria.

Hata hivyo awali wakili wa Zziwa, Jet Tumwebaze kutoka Kampuni ya uwakili ya Kampala Associated Advocate akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari alisema kikao hicho cha Bunge kilichofanyikaleo pamoja na maamuzi yake ni batili kwani kesi ipo mahakamani na watakata rufaa endapo kutatokea maamuzi ya kumng’oa Spika huyo.

Alisema yeye kama wakili alimshauri Zziwa kuingia ukumbini na kuendesha kikao hicho lakini Spika aliona ni busara kusubiri uamuzi wa mahakama.

“Nimemwambia aende kuendesha Bunge ili tuone watamfanya nini maana kesi ipo mahakamani na tunasubiri uamuzi ,sasa kama yatatokea maamuzi mengine ya wabunge sie tutakata rufaa’’.

Aidha wabunge kadha kutoka Tanzania hawakuwepo katika kura hizo.
Wabunge hao ni Shyrose Banji, Adam Kimbisa, Makongoro Nyerere pamoja na Mariam Ussi. (Lukwangule: Margaret Zziwa ang'olewa uspika EALA).

Taarifa ya Waziri kuwatimua kazi Wakurugenzi na kukana kujiuzulu kwa kuvurunda uchaguzi SM

Waziri Ghasia
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Hawa Ghasia, amesema leo Jumatano Desemba 17, 2014, kuwa hatajiuzulu ng’o kutoka wadhifa wake kwa sababu ya kashfa ya kuvurugika kwa uchaguzi wa serikali za mitaa kwenye baadhi ya maeneo hapa nchini Jumapili iliyopita.

Badala yake, waziri Ghasia amesema Wakurugenzi sita wa Halmashauri wamefutwa kazi, watano kusimamishwa huku wengine kushushwa vyeo baada ya kubainika kuwa walichangia kuvurugika kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa, uliofanyika tarehe 14, Desemba 2014.

Akitangaza hatua hiyo inayotokana na ripoti iliyoibua madudu yaliyofanyika katika uchaguzi huo Ghasia amesema uamuzi huo umeridhiwa na Rais Jakaya Kikwete.

Amewataja Wakurugenzi waliotenguliwa uteuzi wao kuwa ni wa Halmashauri za Mkuranga, Kaliuwa, Kasulu, Serengeti, Sengerema na Bunda. Waliosimamishwa kazi ni Wakurugenzi wa Hanang', Mbulu, Ulanga, Kwimba pamoja na Manispaa ya Sumbawanga.

Watatu waliopewa onyo kali ni wa Rombo, Busega na Muheza. Wengine watatu waliopewa onyo la kawaida ni Wakurugenzi hao wa Manispaa za Ilala, Hai na Mvomero.

Soma zaidi vipande vifuatavyo vya taarifa hiyo...